Ndugu zangu wana JF kwa heshima ya watu wote humu ndani naomba kuisotisha hii story iishie hapa sitoimaliza maana inaonekana ni chai. Na mimi siwezi kupoteza muda kuandika kitu ambacho watu wanasema ni uongo.
Nina mambo na majukumu mengi ya kufanya na hakuna anayenilipa kwenye hii story, napoteza muda wangu kuwapa watu story kilichonitokea na mpaka nikaamua kuandika lakini inaonekana ni 0,
Nafikiri kila mtu aendelee na mambo yake kwa stage iliyofikia kumaliza story itakua ngumu, nafikiri tuishie hapa. Kama mtu ameshasema story ni chai kuna haja gani ya kuendelea kuandika?.
Kwa wale tuliokuwa pamoja ahsanteni kwa muda tulionza pamoja ila mimi binafsi nimeshindwa kuendelea kuandika, maana watu wanakatisha sana tamaa.
Story haijaisha hapo niko na matukio ya March, lakini mtu kashaaanza kutukana, haters wamekua wengi, lakini hii ni JF kila mtu anahaki ya kuongea. Ustaarabu mngesubiri story iishe hapo ndo muanze kujudge, maana hivi vyote nilivyoandika na ushahidi navyo kwa picha, Contracts nilizoingia nawateja zangu zote ninazo mpaka Iryn.
Story haijaisha mtu watu wameanza kukosoa anyway ndo wabongo walivyo, sinaga muda na JF ila haya matukio yalinitokea ni kweli na nilikua ndo nimeanza kuingia kwenye kiini cha story na nilikua nimepanga kuandika Epsodes 30 tu.
Wabongo tunakosa kitu kinaitwa patient hapa ndo tunafeli sana, story haijaisha hata mjue lengo la kichwa cha story lakini watu wameanza kushout. Siwezi endelea kuandika kwa style hii inakatisha tamaa, ndomana story nyingi za JF zinaishia njiani.
Wale ambao tunawasiliana PM na tumebadlishana namba tutaendelea kuwasiliana tuko pamoja, ila niseme biashara ya Uber ilinipa mafanikio sana na mpaka sasa naendelea kunufaika.
ALL THE BEST