dr namugari
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 10,466
- 18,206
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
maua ya dunia kaka yapo meeeemgii saaana..Endelea na storyEPSODE 07:
A TRUE STORY
Baada ya Mwaka mpya kupita Mama Junior “Mama J” alirudi home tuendelee na maisha alikua kashapata dada wa kazi. Toka arudi sikutaka kumwambia lolote kama nimeanza biashara ya uber, nilijua kitendo cha kumwambia angeleta shida maana ni mwanamke ambaye ana wivu sana hivyo angenisumbua sana.
Niliamua kubadilisha ratiba zangu za kazi na kuwa Unpredictable nikaplan kuacha kukesha kwa weekend niwe naanza kazi mapema na kumaliza mapema lakini nihakikishe silali nje na home.
Mama J baada ya kurudi home alirudi ameimarika sana sijui mama mkwe alikua anamfanya nini huko kwao maana hata mikiki ya kitandani alikua anahimili sana, toka ajifungue ilikua ni miez 6 tayari.
Kwa upande mwingine Prisca aliendelea kunitafuta sana na mimi sikupenda kabisa kumpotezea maana niliona ni mteja tayari anaweza pia kunipa connection za kazi nyingi, mimi nilikua nawaza hela tu.
Kazi yangu ya kuwachukua Maggy na Mama wawili ilikua ikiendelea vizuri kabisa na mimi niliendelea kupambana na kazi huku nikiwa na mipango yangu mingi kichwani.
Prisca alinitafuta jumamosi ilikua ni week ya pili kabisa ya mwaka mpya toka uanze so akaomba tuonane jioni if possible, nilimkubalia.
Jumamosi mimi nilishinda home siku nzima sababu nilikua na wageni kutoka kwa wafanyakazi wa Taasisi X ambayo nilikua nafanyia kazi kipindi kile, walikua ni kama ndugu kwangu kwenye ile department. Kwa mara ya kwanza walikuja kunitembelea kwangu pamoja na kuijulia hali familia yangu.
Ile jioni tuliwasiliana na Prisca kumwuliza tunakutana wapi, tukakubaliana kukutane kidimbwi. Wakati nawasindikiza wageni mimi nikaenda na uelekeo wa Kidimbwi, muda huo Prisca alikua kashafika so alitext kunipa taarifa kuwa kafika. Niliamua kwenda kuonana naye sababu niliona kumkwepa sio solution sababu nilikua tayari najua nia yake hivyo nilisema nitatafuta njia ya kudeal naye lakini niendelee kumweka close.
Wakati nafika kidimbwi ilikua saa 1 usiku tayari, Kidimbwi kwa siku za kawaida panakuaga pametulia sana “very romantic place”. Baada ya kucheki nilimwona alikua na mtu mwingine so nilihisi atakua ni dada yake tu.
Nilifika pale nikawasalimia, “bila shaka utakua ni dada yake na Prisca” akatabasamu dada yake huku akitikisa kichwa.
Prisca akanitambulisha huyo ndo dada yangu Insider anaitwa Mary (code). Ukweli Mary alikua ni pini kushinda Prisca na walikua wamefanana sana.
Na muda huo mhudumu alikua kafika tayari, ajabu mhudumu alokuja ndo yule ambaye alikua akituhudumia ile siku niko na kina Manuel.
“Kaka mambo za siku?” Mhudumu alinisalimia huku akitabasamu, ofcourse na mimi nilikua nimemtambua yule dada, nikamjibu afu nikamwagiza Bucket ya Heineken, hii siku nilikua najiskia kulewa sana maana toka nianze mikiki ya Uber sikuwai kutoka nika enjoy life, sio kwamba nilikua sina hela hapana bali niliamua kuweka kipaumbele kwenye kutafuta Pesa.
Sasa bwana akina Prisca wakawa wananiangalia hawakutegemea kama mimi nitakua najulikana maeneo yale baada ya dada kutusikiliza wote, wakaniuliza dada kanijuaje??, nikawaambia dada akirudi wamwuulize atawapa jibu lao.
Story zikaendelea pale sasa Mary akadakia…“nimeamua kuja kumwona Mwanaume ambaye anampagawisha mdogo wangu ambaye anafanya asilale.”
MIMI: “Mimi nafikiri angeanza kutupa mkasa kwa kile kilochotokea mpaka akaamua kwenda kulewa maana alinambia alikua na stress”
PRISCA: “Unajua Insider ile siku nilikua na stress sana na yote sababu ya mwanaume, niliamua ile siku niende kwa boyfriend wangu sikumpa taarifa kama nakwenda nilitaka kumfanyia saprise, you can’t imagine nikamkuta na gal mwingine so nilipata hasira nikaamua kwenda kunywa pombe na best yangu”
MARY: “Yule mwanaume alikua bitch tu, nilikuambiaga mapema ukawa hunielewi, shida mdogo wangu unapenda mpaka unaoza”
MIMI: “Aisee pole sana siwezi kukutetea wala kumtetea ila nikwambie pole sana, usipende kunywa pombe ukiwa na stress za kuachwa utakuja kuliwa kimasihara afu yakawa majuto”
Tulikatisha maongezi yetu wakati dada akiwa amefika na vinywaji pale akiwa ameweka kwenye dishi la karai na ice za kutosha, kwa upande wa kina Prisca walikua wameagiza wine “4 cousins”
Palepale Prisca akamwuuliza yule dada, eti huyu kaka umemjuaje?
Dada alitabasamu akawa ananiangalia nikamwambia “go on”
“Ni mteja wetu muhimu” dada akatabasamu akaondoka.
MIMI: Mary unajishughulisha na nini?
MARY: Nasoma bado, nasomea Mastaz ya Business Administration.
MARY: Ukweli baada ya Prisca kunipa mkasa mzima na kutomfanya chochote then kumrudishia simu yale niliamini wewe ni mwanaume wa kipekee sana kwa dunia ya leo.
MIMI: Kama leo hii hata nikisema naenda kumla ni halali maana tushajuana tayari au nasema uongo Prisca?
Wakati naongea na Mary, Prisca alikua busy sana na simu yake.
PRISCA: Sorry, ulikua unasema?
MIMI: kama hujaskia bhasi.. Mary tuendelee na story zetu.
Mary baada yakuona Prisca hajaskia nilichokua naongea aliamua kunyamaza huku akicheka licha ya Prisca kuomba amwambie.
Tulikaa pale mpaka saa 5 lakini tulikua tumepiga sana story ila Mary alinifungukia kuwa mdogo wake ametokea kunielewa sana, kwa upande wangu sikumwambia chochote kile.
Niliwarudisha kwao Prisca akanambia anataka kuja kunisalimia kwangu, nikamwambia na mimi nakaa kwa wazazi kama wewe, niliamua kumdanganya tu.
*********
Kuna mteja nilimpakia Kariakoo mitaa ya Lindi/Congo huyu alikua ni dada pia alikua na mizigo ya ream paper, alikua anaelekea Masaki-Olive sasa ukiendelea kushuka kwa chini kuna shule, yule dada nilimshusha pale.
Baada ya mazungumzo kadhaa akaniuliza huwa napaki wapi gari yangu?
Nikamwambia mimi sinaga eneo maalumu lolote la kupaki hii ni Uber popote kambi tu, ila kama unakazi mimi sina shida tunafanya.
“Ok nina watoto hapa kila siku huwa nawakodia uber tofauti mmoja anakaa Mikocheni, wawili wanakaa Kunduchi kwanini usiwe unawachukua? na kwa kila mtoto ukipata pesa sio mbaya. Natamani kupata mtu ambaye nitamwamini niwe nampa hawa watoto hata usalama wao utakua wa uhakika, kuliko kila siku kupanda uber tofauti”
“Dada haina shida wewe ongea na wazazi wao sidhani kama watakupinga wewe madam, pia hili jambo ni kwaajili ya usalama wa watoto wao”
Tukabadilishana namba za simu huku akiahidi kunitafuta tufanye kazi.
*******
Ilikua jumatano “Mapinduzi day” hii siku nilikua zangu home nikicheza na Junior. Sikuingia mzigoni sababu ya sikukuu kazi zinakua chache hivyo niliamua kupumzika tu.
Hiyo siku niliamua kufanya usafi wa gari mwenyewe home na kuikagua gari kwa ujumla, mara moja moja huwa nafanya usafi wa gari pale home. Ilikua kama saa 9 mchana wakati nimetoka kuoga simu ilianza kuita kucheki ilikua ni namba ngeni kwangu ya tigo 0715*******, nikapokea ile simu.
ANONYMOUS: Kaka mambo mimi ni Iryn ulinishusha pale kijitonyama, “baada ya kuona bado mimi simkumbuki akaendelea”… ulinichukua pale Marina Towers, nakaa hapa karibu na Grand villa hotel.
MIMI: Dada nimekukumbuka, uko salama?
IRYN : Niko poa, sasa upo wapi?
MIMI: Niko home tu, leo sijatoka
IRYN: Nahitaji tuonane Mlimani city jioni by 18:00
MIMI: Sawa haina shida dada [emoji3513]
Ukweli sikutegemea kama yule dada angenicheki licha ya kuchukua namba yangu, sikuamini kama alikua binadamu wa kawaida maana sio kwa ule uzuri aliobarikiwa.
Ile jioni nikatoka home 17:30 maana kutoka mbezi shule mpaka Mlimani city haikua mbali hivyo niliona nitawai tu na siku ile sikukuu hakuna foleni.
Ile natoka namkuta Mama J yuko seblen na dada wakiangalia tamthilia zao.
“Nilijua tu lazima unatoka jion, nilikua nakuangalia unavyoosha gari mwenyewe upo busy kumbe una appointment zako”
“Mama J unawazaga mbali sana, hata hivyo kuna mtu nakwenda muona hapo Mlimani city sichelew narudi soon, nikuletee nini ?”
“Ni nani huyo?, mwanaume gani huwezi hata kutulia na mwanao ukacheza naye, niletee mafuta ya nazi Ya Alinda (mafuta ya nazi ya kupakaa kwa watoto)”
“Sichelewi mke wangu soon niko hapa”
******
Wakati nimefika pale mataa ya Mwenge Iryn alikua kasha piga simu kuwa kafika amekaa “Samaki samaki” pale nje.
Hesabu zangu zilikua kamili kwani 18:00 ndo nilikua napark gari kwenye parking ambayo inatizamana na Samaki samaki.
Nilishuka pale huku nikielekea Samaki samaki sikutaka kupiga simu maana dada alikua kashaniambia alikokaa na mimi sio mgeni na maeneo ya pale hivyo nilikwenda direct huku nikitizama zile meza za nje.
Nilimwona Iryn akiwa peke yake huku akiwa mbele yangu akinitizama so akanipa ishara lakini
nilikua nishamtambua mapema kabla hajaniona.
Alikua ni mrembo ambaye namwona kwa macho yangu huku watu wakiniangalia baada ya kunipungia mkono, dizaini kama hawakuamini kama ndo mimi naenda kuonana naye pale.
Tulisalimiana pale ghafla niliona kama naanza kupoteza confidence taratibu lakini nilionyesha uanaume wangu pale.
IRYN: Kaka nimekupigia karibu mara 2 leo lakini hukupokea simu zangu, nilihisi utakua kazini.
MIMI: Hapana leo nimeshinda home nafanya usafi wangu binafsi na gari. Vipi lakini za toka ile siku?
IRYN: Safi, nilichukua namba yako nikasema nitakutafuta ili tuongee biashara kama utakua tayari.
MIMI: Kama ni biashara halali mimi sina shida nakusikiliza bossy wangu.
IRYN: Ok, nina biashara zangu ambazo huwa nafanya usiku mara nyingi ni weekend from Ijumaa- sunday lakini kwa sunday huwa inadepend na wateja, na mara chache siku za kawaida. Nataka tuongee deal la weeknd tu hizi siku za kawaida kama inatokea nitakua nakupigia kama utakua tayari sawa. Na pia nina saloon yangu Sinza huwa naagiza mizigo mbalimbali utakua unakwenda kuchukua.
MIMI : Sawa dada nimekuelewa labda ungenielezea vizuri hilo deal la weekend muda wa kuanza na kumaliza.
IRYN: Muda wa kuanza ni saa mbili usiku muda wa kumaliza ni complicated tunaweza wahi maliza au tukachelewa lakini haiwezi kuzidi sa10 usiku. Nilichopenda gari yako ina private plate No., then-you’re so gentle.
MIMI: Ok nimekuelewa sasa nasikiliza offa yako maana hiyo itakua kazi ya kukesha ni ngumu sana, kama una offa nzuri nitaconsider proposal yako.
IRYN: Mimi siwezi kupanga bei inatakiwa wewe useme bei ili nione kama nitaweza au laah, au mwisho wa siku tubargain ili iwe “mutual benefit “
MIMI: utanipa 150 per night (niliamua kujilipua tu nione kama atakubali au laah).
IRYN: mhh kaka that is huge amount, naomba upunguze kama nililivyosema kuwe na Mutual benefit
Tuliongea pale mwisho wa siku tukakubaliana 300k kwa 3 nights na akasema kazi tunaanza weekend hii jumamosi.
Dada akaomba nimpeleke kwake kijitonyama, sasa wakati tunatoka pale aisee watu walikua wananiangalia balaa, labda walidhani natoka na mrembo IRYN. Kwanza hata mimi nilijiona kidume kuweza kuongozana na yule mrembo, nilimdrop IRYN pale kwake nikamwambia leo sitaki nauli yako nimekupa offa.
“Katika maisha yangu sijawai kukutana na mrembo mzuri kama IRYN, nimeona wanawake wengi hapa dsm lakini Iryn alikua ni mwanamke mzuri sana ambaye amekamilika kila idara, nyie Mungu ni fundi sana, sio shepu, matiti, sura, lips, mguu, mweupe, sauti na mguu mzuri. Ningekua na uwezo ningetuma picha yake ila ndo hivyo sitoweza.
Ni mwanamke ambaye akipita lazima ugeuke umtizame nyie, kiukweli sikuijutia kazi yangu ya uber ni moja ya kazi ambayo ilinikutanisha na warembo wengi sana.
Pole mkuu, hizi changamoto huwa zinatufanya tuwe wakomavu kutafuta chakwakoNimekah kwa kak angu akaniamsha usku nikakioshe kikombe Cha chai na sahani vzr kwani sijatakatisha
Yaani we acha tu!![emoji23][emoji23][emoji23]Asee pole mkuu sasa ulienda kuiuza au
Huyu ni wale tax force walio pigwa chini na majaliwa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]Kuwasapoti madogo sioni shida hata mimi home mzee anahela ila sometimes napigiwa simu nilipe ada ya dogo, wazazi pia wanaishiwa pia.
Jamaa nahisi alikua TRA kwa 100% maana kwa tasisi TANZANIA inayo deal na wafanya biashara ni TRA na hizo connection za Kariakoo nahisi alikua TRA.
CoolEPISODE 5
Kutokana na lile tukio la kukutana na Angel, ndugu yetu Manuel kumbe alikua akilitizama kwa makini sana, aliniuliza ili apate ubuyu, nikampa story kuhusu mimi na Angel. Manuel akanambia uyo dada the way nimemwona ni anakutaka, cha kukushauri achana naye kabisa,
EX’s are toxic my brother especially in a relationships, mara 100 utembee na mtu mwingine lakini sio Ex.
“Vipi ulimpa namba yako” Manuel aliuliza, nikamwambia hapana, akanambia bro you’re genius.
Niliamua kufuta namba ya Angel na sikutaka kuweka ukaribu naye kabisa, mtu aliyekuacha unapata wapi nguvu ya kumtafuta??, bora ningemwacha mimi hapo sawa, nilikua nikijiambia moyoni.
Wakati bado niko parking pale ghafla simu ikaanxa kuita, kucheki ni Maggy nikapokea alikua anasisitiza na kukumbushia suala letu tulilokubaliana, nikamwakikishia hakuna jambo litakalo haribika.
Kumbuka hapo nina wateja wawili na wote wanaelelea Posta, nikajiambia hakuna shida nitawapanga mapema kila mtu ajue atakua na mwenzie.
*****
Nikawasili pale kwa wakwe nikamkuta Mama mkwe, dada zake, wadogo zake, tukasalimiana, akanikaribisha ndani. Nikamsalimia mtoto, ukweli hakuna raha ambayo wanaume huwa tunapata kama ukiwa na mtoto ambaye mnafanana, kuna kafeeling huwa tunakapata sana (Nikimwangalia Junior na mimi ni copyright). Sikukaa sana pale maana mimi ni mtu ambaye huwa sipendelei kwenda mara kwa mara ukweni au kukaa sana.
Nikaaga pale, mama J tulikua tumeongozana mpaka kwenye gari, nikampa cash 300k hii ni ile pesa ya Manuel, baada ya kununua mazaga hio ndo ilibaki, nikaona nimpe mama yake. Nikamwambia pesa ilikotoka, maana nilijua wazungu huwa hawasahau na wanapenda uaminifu sana, ipo siku atauliza tu.
Baada ya pale nikasema acha nirudi home nikalale niweke mambo sawa kwaajili ya kesho.
Nikampigia simu Maggy na Mama ( tumwite mama wawili(2)) nikawapa mpango mzima kuhusu mkataba na kila mmoja nikamtumia soft copy. Sasa pale home nilikua na jamaa yangu mwanasheria nikampa hardcopy anipigie mhuri.
*****
Ilikua jumatatu njema kabisa nikaamka mapema sana, nikajiandaa vizuri kabisa nikapulizia na unyunyu wangu huyo nikawasha chombo kuingia mzigoni, ilikua 06:25 asubuhi nilikua tayari kwa mama wawili. Mimi nilikua nakaa mbezi beach shule so haikua mbali lakini huyu mama sikumwambia nakokaa.
Nimefika pale nikampigia uzuri na yeye alikua tayari na mtoto wake, Nikamsalimia, akanambia uko sharp sana. Nikamdrop mwanaye pale shuleni, nikamwambia kuna mtu pia tunamchukua pale Alpha uzuri Maggy alikua yuko pale barabarani nikamchukua akaja akaa mbele, Mama wawili siku hiyo alikaa nyuma na mwanae.
Nikawadrop pale Posta, nilianza na Mama wawili pale Azikiwe nikampa mkataba wake nikamwambia utausoma afu utajaza, nikasogea mpaka pale Golden nikamdrop Maggy naye nikampa mkataba akanambia ntakucheki kaka, nikamwambia sawa bossy wangu.
Kukamilika kwa deal la Maggy & Mama wawili nikawa na uhakika wa kuingiza 484,000/= kwa mwezi, nikajisemea mwanzo mzuri.
Nikapark gari yangu palepale ambapo nilimiti na Maggy nikiwa nasubiri request, saa yangu ilikua inaonesha ni saa 2 mbili tayari na madakika yamekata. Nilikua nimeshuka kwenye gari baada ya kumwona dada wa TARURA na kimashine chake akisogea upande wa gari yangu, nikawa namzingua , “Dada mapema hivi unataka kuchora subiri kidogo kukuche” kwanza Kaka gari yako inadaiwa 5,000 inabdi ulipe.
Hawa dada wa TARURA walikua wananikera sana yaani usipark gari pembeni chap kashakuja kuchora, sasa mimi nilikuaga nazinguana nao sana.
Muda uleule nikapata request ilikua location inaonesha customer yuko pale Serena Hotel, akanitext via App, gari yako ina AC? Nikamjibu ndiyo, akanambia njoo chap hapa Serena. Kufika pale namwona mfanyakazi wa pale anatoka, ndo yeye alikuwa karequest akaniuliza wewe ndo INSIDER?, nikamwambia ndo mimi, Ok subir anakuja, Park vizuri na wengine waweze kupita.
Ndani ya dakika 5 akafika mzee, tuseme ni mzee kijana, “kijana wangu hujambo?”…sijambo mzee pole na majukumu “salama sana” si umeona tunakwenda Ununio, nikamwambia sawa mzee wangu.
Nikampeleka mpaka Ununio nikamshusha nikamsaidia kutoa bag lake, sasa kijana itabid unipe namba yako ntakupigia, sawa mzee haina shida huyo nikaondoka.
Nikadrive mpaka pale Ununio shuleni nilikua najua pale lazima nikutane na wahuni na pale huwa ndo kijiwe cha Uber. Nikawa nimechili pale huku nikicheza draft na masela, kila nilikokua natega au kila kijiwe bhasi nilikua najitahidi sana niwe na ukaribu na watu wa eneo hilo.
Nikacheki whatsapp chats nikakuta Manuel kanitext “Hey bro! Good morning, we arrived safely, I’ll call you later”,.
Hii siku biashara kwangu haikuniendea vizuri nakumbuka nilikaa pale mpaka saa 6 mchana ndo nikaja kupata request mteja alikua anakwenda mwenge.
*********
Kazi ya kuwachukua akina Maggy ilikua ikiendelea vizuri na wote walikua washarudisha mikataba yangu ile jumanne wakati mama anarudisha mkataba alinambia wewe kaka upo serious asee, mpaka umegonga mhuri wa mwanasheria nimekuvulia kofia…” nikamwambia mama hii ni ofisi lazima niwe serious kama nimeandaa mkataba wa kijinga ukanikimbia itakuaje??”. Upande wa Maggy yeye alifurahi jinsi navyofanya kazi serious, Maggy ni dada ambaye nilikua nikimwona yuko serious sana na maisha.
Licha ya kuwapa mkataba tu pia niliomba copy za vitambulisho vyao, na kwenye mkataba wangu vipengele muhimu nilivyoweka ni pamoja na, mkataba ulikua wa siku 22 kwa mwezi toa jumamosi na jumapili
*****
Hii tulikua tumeanza week ya Christmas ukweli ni kwamba kipindi hiki kazi zilikua nyingi sana na pesa ilikua inaonekana, sasa nakumbuka kuna tukio lilinitokea siwezi kulisahau kwakweli.
Ilikua ni jumatano usiku nilikua nimemchukua dada mmoja hivi kutoka pale Slipway Masaki ilikua ni saa 3 usiku alikua anaelekea Sinza, sasa wakati nimefika anapokaa nika end trip na nauli ilikuja 10,000 tu. Dada akanambia kaka mimi sina hela tumegombana na boyfriend wangu hajanipa hela, nikamwambia sasa mbona hukusema mapema kama huna?, umenyamaza kimya mpaka tunafika hapa.
Nikamwambia dada wewe sema leo biashara imekua ngumu ila usianze kudanganya hapa mimi mzoefu naelewa, nikamwambia sasa naipataje hela yangu?, nikupeleke lodge au humuhumu kwenye gari??…. Kwanza lodge mbali ntapoteza pesa zangu namalizana na wewe hapahapa, mvua nguo chap (huku nimemkazia macho)…. Eeh dada si kweli akaanza kufungua kifungo cha pant yake. Dada stop! mimi sio kama wanaume wengine hii kwangu ni ofisi naomba nitumie hiyo pesa kwenye nmba yangu kama utanidhulumu ni wewe.
Kaka ahsante ntakutumia una roho nzuri sana, nisave nani jina lako nikamwambia wewe utavyoona sawa, huyo nikasepa. Kesho yake dada kweli akatuma pesa, akanipigia simu kaka nimetuma, nikamwambia hapo umetisha sasa tuongee biashara wewe nakupataje?? anytime wewe ukiwa tayari [emoji3][emoji3], nikajisemea kwa hali hii madereva wa Uber tutakufa kwa ngoma, hata maendeleo tutasahau.
*******
Ilikua imeshakata week yule mzee ambaye nilimchukua pale serena hotel kumpeleka Ununio alinipigia simu, ilikua ni 24/12 usiku,
[emoji338]….
Mzee: kijana naomba kesho uje pale nyumbani, si unapakumbuka??,
Mimi: ndio mzee napakumbuka,
Mzee: bhasi kesho uje saa 3 asubuhi, tutakwenda Mbweni na Kigamboni, gharama zako zikoje?
Mimi: Mzee inategemea na root zako ila gharama zangu kwa siku kutoka asubuhi- Jion 18:00 ni 150,000/= na kuendelea ila maongezi yapo.
Mzee: kijana gharama zako ziko juu sana, punguza kidogo
Mimi: mzee kipindi hiki cha sikukuu rate za nauli zimeongezeka sana na pia kumbuka nakua na wewe siku nzima, top kabisa 120,000/=
Mzee: Haina shida bhasi kesho mapema uwai kijana, nakusisitiza
Mimi: haina shida mzee wangu, [emoji3513]
Ilikua ni Christmas afu sasa ilikua ni jumamosi sasa hii ni siku ambayo nilikua na miadi na Mzee. Nilifika mapema sana pale Ununio kama tulivyokubaliana, mlinzi akanifungulia geti nikawa namsubiri pale parking. Mzee parking yake ilikua na VX na BMW X5, nikasema Kuna watu wana hela asee, kwanza nyumba yenyewe ni ya kibabe.
Baada ya nusu saa mzee akaja pale na bag dogo la kuvuta, nikaliweka kwenye buti, safari yetu ilikua inaanzia kwenda Mbweni. Mzee mbweni alikua anakagua nyumba yake pale, tulikaa kama saa 2 hivi tukatoka kuelekekea Kigamboni.
Saa 7 tulikua kigamboni sikumbuki panaitwaje ila ni mbele ya Pweza beach, kufika pale ilikua ni apartment ya nyumba 3 ndani. Mzee akanambia Kigamboni tunakwenda kwa mchepuko wake atakaa mpaka jioni afu tutarudi Ununio ana wageni badae.
Baada ya kufika akatoka dada pale kumpokea mzee (mchepuko wake), baada ya kuuchunguza kwa makini mchepuko wa Mzee, nikajisemea Mzee anajua kuchagua. Mzee akanipa 30k, akanambia niende nakojua mimi ila 17:00 ontime niwe pale, kumchukua, nikasema acha niende Pweza Beach nikapoteze muda tu.
Mnajua hizi kazi za Uber sometimes ni za ki**nge sana, naonaga hazinaga utofauti na utumwa, ndomana mimi nilikua sibembelezi sana customer wa kufanya naye kazi kama hafikii rate zangu namwacha. Nilikua najiamini course nilikua napata kazi nyingi so sikua na shida na tamaa za kijinga.
Nikachili pale Pweza beach nikasema simpigii Mzee simu mpaka anicheki mwenyewe, kucheki muda ilikua saa 11 na madakika kadhaa tayari hapo mzee hajanicheki, nikasema acha nisubiri mpaka ifike 17:30 nimpandie hewan, japo alisisitiza sana muda huo niwe pale.
Muda ukawa umefika 17:30 nikaona bado kimya nikasema nimpigie au niache?? Lakini nikawa najiuliza mwenyewe kama nayeye anasubiri nimpigie??. Nikampigia simu lakini cha ajabu naambiwa namba haipatikani, nikarudia tena namba haipatikani, nikaamua kwenda tu kumfuata.
Nafika pale lakini gate likikua limefungwa na hakuna mtu around wa kunifungulia, nikaanza kujiuliza kwamba mzee kapelekewa moto sana?, nikashuka kwa gari, nikagonga geti lakini hollaa! hakuna anayekuja kufungua.
Hii siku ilikua jumamosi afu Christmas demand ya usafiri ilikua juu sana na nauli pia zilikua juu sana licha ya kumaliza kazi ya mzee nilitamani sana niingie barabarani niendelee na mzigo. Dullah before alikua kanicheki whatsapp afu kanitumia ubao wake, yaani mpaka sa10 mchana alikua kashakusanya 120k, niliingiwa na roho ya wivu.
“Kipindi kama hichi cha sikukuu Uber huwa tunaringa sana sehemu ambayo haina manufaa huwa hatuendi maana request zinakua nyingi sana.”
Wakati nikiendelea kutafakari pale nje getini, Mama J akaanza kunipigia simu, nikakumbuka aliniambia niende kwao kuna chakula cha pamoja kama mimi moja ya familia natakiwa niende na baba yake (baba mkwe) atakuwepo, “nilikumbaliaga kuwa nitakwenda”. Nikapokea simu yake akanambia mbona mpaka sasa hujaja?, sikutaka ugomvi nikamwambia ntakuja badae wewe usiwe na wasiwasi.
******
Ilikua ishafika 12 na madakika tayari ndo kuna dada alikua anatoka, nikamwuliza kama ana mazoea na yule mchepuko wa mzee, akanambia sina. Nikaingiza gari ndani ikabidi nigonge mlango kama dk 3 dada akatoka, nikamwambia mzee hapatikani na alinambia 17:00 niwe hapa ontime. Dada akanambia mzee kalala toka saa 10, nikajikuta nataka kucheka, nikamwambia dada amwamshe tuondoke maana tushachelewa tayari.
Baada ya dk 15 mzee alikua tayari katoka kwaajili ya safari, nikamwambia mzee nilikua nasubiri unipigie lakini nikaona kimya, kukupigia hupatikani akanmbia bhs dada alizima simu yangu, kucheki kweli simu ilikua imezimwa. Mzee akaniomba tuondoke chap maana saa 1 anawageni muda huo ilikua sa1 kasoro tayari.
Tukatoka pale Kigamboni lakini barabarani kulikuwa na foleni sana tukajikuta tunafika Ununio saa 3 kasoro, mzee akanipa pesa zangu akanambia atakuwa ananicheki, nikamwambia haina shida.
Muda huo nilikua nishawasha App yangu muda sana nasubiri request, haikuchukua muda niakapata request ya kwenda Airpot, ile nime accept tu, ni kama dada alikua anashida sana ya usafiri palepale akapiga simu, “kaka naona haupo mbali na mimi,please njoo haraka nachelewa”. Ofcourse alikua mtaa wa pili unaofuata, nikamkuta yuko nje getini tayari, ile nashuka dada anambia yaani kaka kama bahati leo usafiri wa shida sana, nikamwambia dada hujui leo ni sikukuu??
Tukatoka hapo chap kuelekea JNIA so dada alikua na haraka sana, alikua anaomba nikimbize gari, ni kwamba dada alikua anaondoka na ndege ya 22:30 afu alikua anatakiwa kuchek in 20:30 na muda huo tunaondoka ilikua ni 21:45. Nikamwambia dada mimi huwa siendeshagi zaidi ya 60km/hr kwa mjini humu, kutokana na kusema Uber zilikua za shida na mimi natambua hili nitakuwaisha ili uwai ndege, dada akashukuru.
Sikutaka kutumia Bagamoyo road maana nilijua kutakua na foleni tu watu wanakwenda mjini kula bata. Nilikua nazijua shortcuts baadhi ya njia so nilipita chini kwa chini nikaja kutokea Ununio, hii barabara niliyopita kipindi kile ilikua inatengenezwa lakni sahivi ina lami. Nikatembea chinichini kwa chini kufika kunduchi nikaingia na barabara inayopita cota za Police hao tukatokea kwa “Mwamnyange” nikaunga na Mwaikibaki road, hao Mikocheni nikaingia na barabara ya ubalozini ghafla tunajikuta tushafika namanga huyo nikaunga na “Alli Hassan Road”. Dada muda wote macho kwenye simu akiangalia muda huku aniangalia mimi starring navyopambana na Road.
Ilinichukua dk 40 kuingia JNIA terminal 3, dada alifurahi sana hakuamini kama angewai lakni bado alikua na wasiwasi kama kachelewa.
Vipi unaondoka na ndege gani?, KLM nikamwambia usiwe na wasiwasi umewai sana, nauli ilikuja 32,000 dada akanipa 40,000 nikataka mpa change akanambia keep it. Nikamsindikiza dada mpaka anaingia ndani mimi nikakaa pale nje kwenye vile vibaraza, “ Sheria za Airpot hauruhusiwi kukaa ndani ya gari”, haikuchukua dk 5 dada akanipigia simu kaka ahsante nimefanikiwa, namba yako nimesave ntakucheki nikirudi, nikamwambia sawa, safari njema.
Wakati nimekaa pale nje nikisubiri request nilikua napiga story na moja ya mlinzi wa pale, nilikua najaribu kila nakokwenda niwe na watu naowajua hata kama kuna jambo au msalaa nakuwa ba backup. Nilikua namuuliza jamaa kwanini Uber tunazinguliwa sana mle ndani, jamaa akanifungukia akanambia zile gari/tax za Airpot ni mradi wao na pia ni gari za wakubwa humu ndani, uwepo wenu nyie Uber umepelekea biashara zao kuwa mbaya. Hapo ndo nikajua kumbe ni biashara za wakubwa mle ndani ndomana kuna vita na madereva wa Uber.
Wakati story zikiendelea na jamaa nikapata request, kuwasiliana na mteja akanambia yuko Airpot pale Puma filling station, nikamwambia mteja mimi niko terminal 3 kutoka hapa si unajua lazima nilipie getin pale akasema hiyo 2,000 mimi ntakupa fanya chap mimi nachelewa.
“Huyu mlinzi alikua mshikaji wangu sana alikua ananipa ratiba za ndege kutua nknk, alikua ni asset kwangu”, huko mbele mtaona.
Nikamwaga jamaa tukaexchange number nikampa buku 5 ya soda huyo nikapotea, kufika kwa jamaa pale Puma nikampakia alikua na demu wake, safari yetu ilikua ni kuwapeleka pale Whitesand hotel. Wakati nakaribia Whitesand nikiwa pale Ramada hotel nikapata request juu kwa juu “hii mara nyingi inatokea kama upo karibu na mteja au kama usafiri wa shida”, muda uleule customer akapiga simu, dereva njoo hapa “The wave” nikamwambia ASAP.
Nikamdrop jamaa na demu wake nikapitia kumchukua mteja pale “The wave”, hao ulekeo ulikua ni Tips Mikocheni, Pale sikukaa hata nikapata mteja alikua anakwenda Samaki samaki, Masaki. Mpaka muda huo ilikua ishafika Saa 7 usiku na madakika kadhaa, nikasema acha nitafute sehem nipark na pia nipunguze mafuta yangu ya mwilini.
Ile mitaa ilikua imejaaa sana magari sana yaani kulikua kumefurika kumbuka ilikua ni Christmas, kuanzia kule Elements yaani mpaka unakuja Samaki samaki, kumefura hatari, parking za shida afu Masai wakiona IST wanajuaga ni Uber wanazinguaga hatari [emoji23][emoji23][emoji23].
“Masai huwa hawatupendi kwasababu huwa hatuwapi hela, mimi kutokana na gari yangu nilikua natumia vibao vya njano, nilikua hawanisumbui kabisa, kama ukipark usiposhuka anakugongea anauliza wewe ni Uber au laah”
Nikasema ngoja nisogee mpaka kule chin kama unakwenda Village supermarket, sasa nikaamua kupark pale kwenye corner inayokwenda UN pale kuna ka uwazi mitaa , Ile napark gari tu aisee si nikavamiwa na wale “DADA POA” sikujua kama ni chimbo lao lile, ila walikua mapini hatari.
Sikupenda ule usumbufu nikaamua kutoka pale wakaanza kusonya huku wananitukana, nikasema leo nimevamia mtumbwi wa vibwengo.
Nikapata request pale Samaki samaki nikamfuata mteja alikua ni dada lina mahips hatari afu lizuri, akanambia kaka mimi naelekea bwawani ila map iko sawa, wewe twende. “Bwawani ni mtaa ambao unaingilia pale Kinondoni kanisani sijui kwa Selebonge ni maarufu sana kwa mapishi, sasa unakunjia corner pale au njia nyingine unaingilia pale mbele baada ya jengo la Vodacom kuna mataa pale, barabara za kule ni za nzege”.
Nikamsusha yule dada pale, kucheki muda saa 9 na madakika yake nikasema ngoja nikatege pale Tips then nikalale, kutoka pale Bwawani mpaka Tips sio mbali. Nikasogea pale Tips napo palikua pamejaa hatari si unajua sikukuu imeangukia jumamosi kila mtu katoka out.
Mida kama ya sa10 ilikua imefika nikapata request ya kwenda Maison club, hii club ipo karibu na Sea cliff mitaa ileile. Wakati nimemdrop pale mteja nikasema acha niset destination ya mbezi beach mimi pia nikalale ili kesho niendelee na mzigo mapema. Kipindi cha sikukuu ndo kipindi ambacho Uber wanaingiza sana Pesa ni kipindi cha kuwa serious na kazi.
Palepale Maison nikapata request na mteja alikua anakwenda Mbezi beach kwa Zena, nikafurahi sana maana destination mpaka uipate ni bahati sana. Huyu alikua ni demu ana uchotara flani hivi aisee ni pini hatari akaingia akakaa mbele, akakilaza kiti ili alale vizuri mimi namwangalia tu, akanambia kaka fata ramani “alitoa sauti ya kudeka”. Ilikua ni pini balaa, kama wewe ni mwanaume rijali lazima utingishike, kwanza dem toka anaingia kwenye gari wahuni walikua wanamtolea macho balaa.
Alivyonambia fata ramani mimi sikua na swali tena kwani ramani ilikua inanionesha uelekeo ni mbezi beach, tukaanza safari pale nilipita ile barabara inayokuja tokea pale Tanesco Mikocheni, tukaunga wakati tunafika pale round about ya Kawe, dizaini kama dada akaanza mitego, mara atanue miguu, kama mtu ambaye anahangaika hivi.
Tulivyofika pale Rainbow kwa mbele si kuna filling station ya GBP, nikazama pale ili kuweka wese, nikashuka pale ili nipate na kaupepo kidogo huku jamaa akiweka mafuta, so ile naingia kwenye gari nakuta kile kigauni kimepanda mpaka saizi ya kiuno yaani naona kila kitu live, naiona chupi hii hapa live, paja hilo huku kwangu frequency zishachange muda, afu namuda sijapata ile kitu si unajua wife alikua hayupo.
Kwa muda ule nilikua sielew nini cha kufanya maana tamaa ilinijia haraka sana ya kumla yule dada, nikamgusa chupi pale katikati nikaona dada anaanza kuhangaika, huku akitoa ushirikiano, nikasema leo Mbuzi kafia kwa Muuza soup, naiachaje pisi kali kama hii….
Tutaendelea,
Tukiwa pale Mlimani city juzi kati hapo Iryn alipitaDr hakuna sehem ambayo nimeandika kuna dada niliempeleka Airpot ni pisi kali/Mrembo
Prisca kwa mara ya kwanza nilimwona mzur ila nilivyokuja kumwona dada yake ndo nilijua dada yake ni mzuri zaidi sababu alikua na tyako.
Hakuna sehem ambayo nimeongelea uzuri wa mke wangu
Hakuna sehem ambayo nimesema Mzee alikua ni kigogo wa serikali, kuhusu mchepuko wake hakuna nilikosema ni pisi kali ila nilissema baada ya kumkagua niliona mzee anajua kuchagua (siku sema ni pisi kali), unafikir kwa mzee mwenye pesa kama yule angekua na mchepuko wa kawaida??
Sijataka kuandika mambo mengi sana maana nimekutana na wanawake wa kila aina ila mostly ni pisi kali, wanawake wa kawaida nilikua nakutana nao kwenye Bolt sana. Tambua kwanza watu waliokua wanatumia uber ni wale wenye Pesa, wanawake wazuri, uber rate za nauli ziko juu sana tofauti na bolt, pia Uber ilikua inapendwa sana na warembo sababu ya security.
Nimekutana na warembo mpaka nilikua najiuliza mbona hawa wanawake sikutani nao mitaani??, kuna wanawake nimemit nao uyo Prisca mbona cha mtoto na dada yake.
Nimeamua kuandika story na wanawake ambao walikua na impact kwenye maisha yangu, ningesema niandike kila kitu hapa zingefika Epsode 500,
Katika wanawake wote IRYN alikua ni funga kazi aseee, narudia sijawai kukutana na mwanamke mzuri kama Iryn kwa Tanzania hii huyu dada alikua ni pini, kisu, pisi kali, mrembo, cute, beautiful nknk, Mungu ni fundi.
Dr unafikir hapa Tanzania hakuna warembo? waulize madereva wa Uber watakwambia aseee,
grizzman Prince Mhando
Yote Maisha Home BoyKuishi kwa ndugu
Hichi ndio kipengele pekee nimelipenda , nimekumbuka kipindi nimemaliza form six nilienda kwa ndugu (baba yangu mdogo) mkoa fulani nyanda za juu kusini
Sasa kulikuwa na dogo mwingine ambaye si mwanae ni mtoto wa dada yake alikuwa akilalamika kuhusu mke wa jamaa kuwa anakauli za kibaguzi na ni kweli nilikuwa naona the way anawatreat wanae na huyo mwingine ni tofauti hivyo ilikuwa mumewe akiwepo ndio tunakuwa na ahueni ,
Kauli yake moja ilinifanya nipange safari ya kuondoka pale , alimwagiza mwanae majani ya chai dukani akampa elfu5 sasa watoto wakawa wanagombania kila mmoja anataka aende , huyu aliyepewa hela akakimbia nayo kufika getini kajikwaa kaanguka nakuanza kulia
Mama mtu kufika akasema kuna mijitu mikubwa imekaa tu haina kazi imerelax ,mtoto anaenda dukani akirudishwa chenji tsh 200 atajua?
Sikumaliza week 2 nikaondoka[emoji23]
kama kawaida ya jf, ule muda wa msimuliaji kuanza kusua sua ushafika..Tulale ama?
Yeye aendelee na Irene mi nataka nithibitishe tu urembo wake na si vinginevyo mkuu. Maana amemsifia sana😃😃Ilo pia ni jambo jema ila najua insider hawezi kuuza code ya uyo mrembo ye mwenyewe nahisi analitaka ilo colony
Acha tuukama kawaida ya jf, ule muda wa msimuliaji kuanza kusua sua ushafika..
Naimani ataleta muendelezo maana kuna watu wameibukia katikati ya story na tunahamu ya kujua HATMA zao na dogo INSIDER MAN 😃😃Acha tuu
Moderator wamezingua sana.[emoji23] [emoji1787] nishatoboa maisha na sijali
Walimerge ule uzi asa nikashindwa muendelezo na kejeli za watu hapo nikachoka
naishia hapaTulipoishia, Kama unawazazi jitahidi uwapende wazazi wako wakiwa hai, wazazi wanatuombea sana. Itoshe kusema baada ya kurudi home milango ikafunguka sikukaa muda nikapata kazi.
INAENDELEA… EPISODE 02:
Ghafla simu yangu ikaanza kuita prirrr[emoji338] priirrr[emoji338][emoji338]ilikua namba ngeni, nikapokea, halooo
SIMU: Kwa majina naitwa “Rose Mutesi” napiga simu kutoka taasisi “X” nitakua naongea na INSIDER MAN?, nikamwambia yes ni mimi karibu. Dada akanambia hongera kwa kufaulu interview umechaguliwa kupata mafunzo kazi (Internship) kwenye taasisi yetu, jiandae mwanzoni October tutakupigia simu kwaajili ya kuanza kazi. Baada ya kuongea nae akakata simu [emoji3513].
Kiukweli sikuamini kama nikweli maana niliona kama ndoto hivi, nikasema hawa wanaweza kuwa matapeli, inshort sikuwa interested na ile simu. Sikumwambia mtu yoyote juu ya hili jambo hata mama sikumwambia maana niliogopa wasije wakawa matapeli. Hapo nilikua tayari nina miezi 2 niko home, wakati nimefika mzee wangu alikaa siku 3 akarudi Zambia.
Mzee wangu ni engineer kule kuna kampuni anafanyia kazi na pia mzee wangu kurudi home ni nadra sana anaweza kukaa hata miezi 3 na zaidi bila kurudi nyumbani. Nilikua naongea na mama mambo mengi sana hasa alikua anataka kujua pale kwa Uncle kama ninaishi vizuri. Ni kwamba mama yangu anamjua vizuri sana Aunt ni mtu wa namna gani, sikutaka kumwambia mama lolote kuhusu pale kwa Uncle niliamua kuyaweka moyoni. Japo mama alihisi kuna jambo halipo sawa,lakini alinisistiza sana kuwa na adabu na heshima. “Kila siku usiku tulikua tunapiga maombi na mama” mama yangu ni mtu wa dini sana.
Mwezi wa 9 mwishoni 2019, nikaamua kurudi Dar ili kuwa karibu endapo ningepigiwa simu na ile taasisi. Nikamwaga mama, akanifungia mchele wa kutosha, unga, mafuta ya kupikia gallon, maharage akanambia mpelekee Uncle. Niliamua kurudi palepale kwa Uncle lakini this time nilikua naplan zangu kichwani tayari. Baada ya kurudi Dar haikupita week nikapigiwa simu nikareport kazini nianze training.
Uncle nilimwambia kwamba kuna sehem nimepata part time, kazi ya muda nitakua natoka asubuhi, lengo langu nipate mkataba niwe na uhakika wa kumwambia. Lakini alisisitiza niwe nahakikisha mbwa wake wanakula ontime pamoja na kumwagilia maua yake. Kutoka na kurudi jion Aunt hakupenda siku nimerudi jion akanambia wewe sikuhizi umepata kazi na husemi?… nikamwambia hapana ningekua nimepata kazi mbona ningeliwaambia ila Uncle nilimwambia nimepata kazi ya muda. Dizaini hakupenda akanambia kwahiyo ukamwambia Uncle wako tu?, nikamwambia Aunt kwan kuna shida?. Akanambia sikuhizi hata kazi hufanyi… daah! . Nikamwambia huoni napikia mbwa chakula kila nikirudi jion? bado namwagilia miti namaua au unataka nifanye kazi gani??.
Aunt yangu alikua mtu wa gubu sana alikua na roho mbaya sana kama mtu wa hasira unaweza mtukana kabisa. Alikua ananichongea maneno sana kwa Uncle mpaka nikaona dizaini mzee baba kama anakua mbali na mimi.Kuna siku niliondoka na gari ya uncle kwenda kumchukua dogo shule, Uncle mara nyingi alikua anapenda kutumia gari ya ofisi ile yake inakaa home tu.
Sasa Uncle alivyorudi Aunt akamjaza maneno kuwa niliendesha gari yake eti siku nzima na nimeichibua gari. Uncle aliongea sana ile siku usiku “Sitaki uendeshe gari yangu kwanza hujui kuendesha gari, umenichubulia gari yangu. Gari ikiharibika unahela ya kulipa?? “. Ukweli ni kwamba ile michubuko ilikua vilevile, yale maeneo yalinichoma sana nikahapa kutokuja gusa ile gari hata aombe nimpelekee wapi.
Baada ya kumaliza training hatimaye nikapangiwa kituo cha kazi na nikaambiwa kesho niripoti pale ofisini. Sikuamini nilovyopewa ule mkataba kweli kesho yake nikaanza kazi nikapangiwa moja ya Idara kwenye ile ofisi. Hii ni moja ya taasisi kubwa sana hapa nchini na inategemewa sana sana.
Nilianza hii kazi bila malipo then nilikua niko vibaya sana kiuchumi ndugu zangu, mama Junior ndo alikua ananipiga tafu za nauli sometimes. Ilibidi nimwambie Aunt kwamba nimepata kazi kwenye taasisi X that day Uncle alikua safari nikaplan ntamwambia Uncle officially akirudi kwamba nimepata kazi face to face, Ukweli hizi taarifa Aunt hakuzifurahia ni kama nilimpiga na kitu kizito sana akaanza kuulizia mambo ya salary sikutaka kumwambia lolote.
Uncle akarudi toka safari nikaongea naye kuhusu kupata kazi na taasisi “X” japo hakuonesha ile furaha halisi niliona kuna unafiki hapa hajapenda. Akaniuliza nani kakutafutia nikamwambia nilifanya interview nikapigiwa simu, akauliza mambo ya mshahara nikamwambia hili suala bado ila ni kama nafanya kujitolea, kama kuna malipo nitakuambia. Huwezi amini Uncle hata hakusema neno “hongera”, nikaanza pata picha ninaishi na ndugu wa aina gani, hata mama alinambia niwe makini sana.
Pale ofisini baada ya mwezi nilikua nimeshazoeana na maofisa wa pale hasa idara yangu kama incharge/supervisor wetu alikua na roho nzuri sana. Alitokea kunikubali sana hizi ten ten nilikua nakula sana kila siku, yaani nilikua nafanya kazi kwa bidii sana na kujituma nikaweka urafiki na watu wa idara.
Pale kwenye kile kitengo chetu interns tulikua wawili mimi na dada mmoja hivi. Kadri siku zilivyokuwa zinakwenda nikawa nimezoeana na maofisa wa idara zingine wakawa wananipa kazi zao nafanya wananipa hela sikuwa nakataa kazi. Ikafika muda nikajikuta kwasiku sikosi 20,000 kuna kipindi napata mpaka 50,000/= au zaidi, hizi hela nikawa naziweka maana nilikua na mipango yangu kichwani ya kwenda kupanga.
Hii Taasisi niliyokuwa nafanyia kazi ina deal sana na wafanyabiashara hivyo nikaanza kupata connection na wafanyabiashara mbalimbali hasa pale Kariakoo.
Baada ya miezi 2 taasisi ikasema itaanza kutulipa 450,000 kwa mwezi zitusaidie bhasi kwangu ikawa sherehe. Nikaanza kununua vitu taratibu naacha madukani kwaajili ya kuanzia maisha. Nikawa nawaza njia ya kutokea pale kwa Uncle maana wangeanza maneno kapata kazi ameondoka sikutaka hizi kelele. Nikawaza hapa nitawaambia naenda safari ya kikazi Dodoma ndo itakua gia yangu ya kusepa pale.
Baada ya hapo sikuchelewa nilikua na iphone 7 plus nikaiuza 740,000 nikawa kidogo napesa ya kuanzia maisha. Nikamtafuta dalali tukapata chumba sebule na jiko kodi ilikua 180,000 kwa mwezi, nikalipa kodi ya miezi 4 kwanza. Eneo nililopata ilikua ni salasala (Mabanda mengi) pale Mbuyuni mataa ya kwenda tegeta na kunduchi, sasa kwa mbele kama unakwenda Tegeta kuna kibarabara kinakata kushoto kwenda salasala, kule ndo nilikoanzia maisha.
Nikaweka godoro langu chini, nikaweka jiko langu la gas, nikanunua gas mtungi mkubwa, sufuria na baadhi ya vyombo vya kuanzia maisha bila kusahau subwoofer “Sea piano” [emoji3], raha ya geto mziki uwe unasikika.
Baada ya hapo nikaanza kuamisha vitu vyangu bila kushtukiwa mpango wangu. Baada ya hapo nikawaaga nitakwenda kikazi Dodoma sijui nitarudi lini wakaniambia safari njema, maisha ya geto niliyaanza March 2020.
Nimeingia pale sasa akili ya maisha ikaanza kuja kichwani, kwanza nimelala pale kuna baridi hatari sina hata shuka la kujifunika, madirisha hayana mapazia[emoji2][emoji1]. Week ileile niliyohamia kwangu nikapambana nikanunua mapazia mazuri nikayaweka. Bad news haikupita hata week nikaibiwa yale mapazia na laptop [emoji22].
Pale palikua na wapangaji watatu na wote tulikua tunatoka afu fense ilikua fupi mtu rahis kujua kama hakuna mtu, na pia geti lilikua tunarudishia si unajua tena maisha ya kupanga geti huwa halifungwi. Uzembe ulikua wangu maana sikufunga madirisha ilikua rahsi kuibiwa jama alichomoa mapazia yote mpaka seblen. Nilihisi aliyeniibia ni mzoa taka wala sio mtu mwingine maana ndo alikua na mazoea ya kuja pale home.
Mungu akaendelea kufungua milango, kutokana na kuwa na changamoto nikipika chakula kikibaki kinachacha nikaona kuna umuhimu wa kununua fridge. Nikafanya research yangu pale Kariakoo nikaona bora ninunue fridge la size ya kati bei ilikua ni 720,000 kwa kipindi kile.
Nikapambana sana pamoja na kukopa nikaweza kununua fridge, mama Junior naye hakua mbali akaniletea Micro wave ya kupashia chakula na mazaga mengine kama mashuka nknk. Ndani ya muda mfupi nikawa nimekamilika na kila kitu ndani kiasi kwamba ukiingiza pisi ndani lazima ipagawe. Baada ya hayo niakaanza kusave hela kila senti nayopata nikawa nasave kupitia vicoba na kucheza michezo.
November 2020, mama junior akaja kwangu akanambia ana mimba yangu hivyo kwao amekimbia hawezi kurudi anamwogopa baba yake. Hapo alikua anasoma chuo na mzee wake katoka kulipa ada afu sasa mzee wake ni mkorofi hatari ndomana akakimbilia kwangu hakutaka kutoa ile mimba.
Zile habari hazikunishtua niliona mtoto ni jambo la kheri then hata yeye nampenda nikamwambia kama mtoto ni wangu bhasi utakaa hapa huko kwenu tutaweka mambo sawa, si unajua wazee wa kichaga.
Nikampigia simu mama yake kumwambia bint yake yupo kwangu asihangaike kumtafuta mimi naandaa utaratibu nitakuja, mama yake alikua anajua natoka na bint yake hakua nashida na mimi. Akanambia kama yuko kwako mimi sina shida najua yuko sehem salama ila sasa baba yake ndo shida.
Tulikwenda hospital kuchek mimba ilikua na week 6, ikabd nichukue hatua zingine za haraka ili kukamilisha hili jambo, hatimaye tukalipa mahari.
Baada ya kuanza kukaa na mama Junior hapo ni mjamzito mambo yangu yakazidi kunyooka sana, nikawa mtu wa bahati sana. Kuna mwanamke ukiwa naye mambo yananyooka yenyewe. Nikaanza kutengeneza connections na wafanyabiashara wakubwa, stakeholders na watu mbalimbali maana sikuwa naona future ya kuajiriwa na hii taasisi.
Nikaanza kujiongeza mlemle Kariakoo na kufanya deals zingine nyingi, nikafungua biashara “workshop” ya kupaka rangi magari, services, lubricants, polishing nknk pale gerezani. Kwa kufupisha hii story baada ya kumaliza mkataba tukastopishwa kwenda kazini na mimi sikutaka kuhangaika na kuomba na kutafuta kazi. Hapo ilikua ni September 2021.
Sikushtuka sana, mimi binafsi nilikua nishajipanga tayari na nilishaona dalili mapema, savings binafsi nilizokuwa nazo za haraka cash in hand ni 24 million. Nikaagiza Toyota IST kutoka Japan iwe inanisaidia mishe zangu za hapa napale. Baada ya kununua gari, kukamilisha kila kitu nilitumia 14 million, nikalipa deni la kiwanja full 5,600,000/=nikamwekea wife 3 million kwa account maana mwakani 2022 alikua inabidi arudi chuo kuendelea na masomo alikua kashajifungua tayari. Nakumbuka sikubaki na kitu katika ile saving lakini nilikua na shares zangu kwa watu hivyo hata bila kazi ningesurvive.
Maendeleo ya Biashara yalikua mazuri sana nilikua na wateja wengi sana na pesa nilikua naiona kama faida. Ile September mwisho wa mwezi mwenye eneo/Landlord akanipigia simu.
LANDLORD: Kijana wangu hujambo? sasa nina habari mbaya nataka kukupa maana ipo chini ya uwezo wangu. Kutokana na ujenzi unaoendelea na upanuzi wa barabara nimepewa order ya kwamba nyumba zetu zitaweza bomolewa muda wowote. Na wewe kodi yako inaisha mwezi ujao, itabidi utafute eneo lingine mambo yatakapo kamilika nitakutaarifu kijana wangu.
Ukweli taarifa za Mzee zilinipa stress sana maana biashara ilikua imechanganya sana na kwa ile location ilikua nzuri sana. Niwaambie biashara ya workshops inalipa sana faida inaonekana sana. Mchawi ni location tu maana pale nilikua nakamata magari yanayotoka bandarini nknk.
Ofisi yangu ilikua Gerezani karibu na Round about [emoji3534] ya kwenda Kurasini. Kama unatokea central before hujafika kwenye ile Round about kuna yard ya magari bhs mitaa ileile. Baada ya kuongea na mzee nikawa sijui niende wapi maana nilikua dilemma, pia watu wakanishauri ujenzi wa barabara unaondelea biashara itakua ngumu sana maeneo yale hivyo nisubiri niangalie upepo. Ikabidi nistop kwenye hii biashara kwanza,nikaplan nitarudi barabara ikikamilika. Ilikua kama mkosi naacha kazi na biashara nafunga niliona kama mtu ananichezea hivi.
Nikafunga biashara katikati ya October kodi ndo iliisha tarehe hizo, baada ya hapo nikawa sina hela maana hakuna nilichokua naingiza. Ile ile october kuna mhindi alikua jamaa yangu sana niliweka kiasi cha pesa kwenye biashara yake ni muda. Jamaa alinicheki akanambia anakwenda India na pale watasimamia ndugu zake itaweza sumbua kupata gawio zangu hivyo akanipa pesa magawiwo yote 6,000,000. Nikakusanya na madeni yangu na pesa zingine nikapata 3,400,000 jumla nikawa na 9,400,000/=.
Ikabidi nikae na wife chini tupange mipango maana alikua anajua kinachoendelea. Nikalipa kodi ya nyumba 1,800,000/= kwa miezi sita. Nikampa wife 2,500,000/= kwaajili ya matumizi ya mtoto, mshahara wa dada, bill za umeme na maji na mahitaji ya nyumbani yote (Miezi 6). Nikamlipia mtoto bima pamoja na mama yake kama 245,000/=.
Ilibaki kama 4,800,000 tukaplan hii amount tufungue biashara ya vinywaji. Lakini kuna dogo langu anayenifuatia yeye alikataa shule alisema anapoteza pesa za wazazi na muda. Toka muda alikua ameniomba nimkopeshe million 3, “alipataga hasara walimtapeli” dogo anaduka la vifaa vya simu na Huduma za kifedha. Dogo pia alinisave sana kipindi kile nakosa nauli za kwenda kazini, so nikampa dogo million 2 kama kaka yake. Nikamlipia dogo ada “yule ambaye mama alisema anataka sayansi ila math haipandi” nililipa million 1. Hapo unaona jinsi ambavyo pesa haikai kabsa.
Nilibakiwa na 1,500,000/= hivi nikasema hizo nilizotoa nitajazia. Ukitaka kuona mambo yanabadilika acha kazi ndo utaona kila rangi. Bhasi nikaanza kuwaza namna ya kutafuta pesa nikisema nisubiri pesa iishe nitakuja aibika huko mbeleni. Nikafikiri kuingia kwenye uber maana gari nilikuwa nayo tena yangu, kumpa mtu hapana bora nikomae mwenyewe tu. Kuna jamaa yangu wa uber alikua mshikaji sana nikamcheki…[emoji338]
DULLAH: oya tajiri vipi hatutafutani sikuhizi umenitenga hunipi kazi kama zamani hali ni mbaya.
MIMI: Tajiri sijakutenga sema pale nimetoka ndomana unaona kimya mwenyewe sina maisha ndomana nimekucheki unipe ramani.
DULLAH: Sasa tajiri mimi nakupa mchongo gani hapa nakomaa na uber tu hapa, siku za kati ya wiki tunafanya kuokoteza, cha muhimu mkono uende kinywani.
MIMI: Tajiri nahitaji tuonane nina jambo langu muhimu sana unipe code nianzie wapi ili kufanikisha.
DULLAH: Jambo gani tajiri unanitisha, kesho nitakua home siku nzima, leo nitakudanganya boss wangu. Wewe kesho njoo muda wowote tutayajenga.
MIMI: haina noma kesho asubuhi nitakucheki unipe code.
DULLAH: Imeisha hio tajiri [emoji3513]
Asubuhi nikamcheki Dullah ilikua kama saa 2 asubuhi hivi akapokea akanielekeza anakaa Sinza madukani unakunja pale kwa vunja bei. Bila kupoteza muda nikaenda chap nikafanikiwa kufika kwa jamaa, tukaanza story…
DULLAH: Tajiri karibu sana naona upo na chombo mpya kabsa hii hata week haina. Hii chombo umechukua yard au umeagiza?
MIMI: [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3], Tajir huoni kabisa hadi alama za bandarini hizo chuma imetoka Japani. Sikia ndugu yangu mchongo wenyewe naotaka tuongee ndo huo unaoushangaa.
DULLAH: Sijaelewa Tajiri unauza hii IST?? au
MIMI: Nataka kusajili Uber tajiri unanisaidiaje? Nataka maelekezo kutoka kwako wewe una experince ya muda mrefu.
DULLAH: Unataka kuendesha wewe au nikutafutie dereva?
MIMI: camon mimi bro!
DULLAH: Kama wewe sikushauri hii gari ubadilishe vibao tumia hivyohivyo vya njano, akaifungua ndani akaona gari nimetia seat cover, full unyunyu, Android Tv nch 10 imekaa pale, chini carpet. Mzee hii gari utapiga sana hela niamini mimi kama hawa mademu watakutafuta sana, utapata root privates nyingi, kama nilivyokwambia usiweke vibao vyeupe.
MIMI: kwanini nisiweke vibao vyeupe?
DULLAH: Vibao vyeupe miyeyusho ndugu yangu traffic mikono mingi, bado TRA yaani tunapata shida wahuni sikuhizi wanatumia vya njano.
MIMI: Basi poa nimekuelewa sasa najisajilije?
DULLAH: Kuna jamaa namjua ila sijawai kumwona kwa sura ni kama “Ghost” anakusaidia chap wewe andaa 100k. Kama unayo hata leo anaanza kazi baada ya siku 3 kila kitu kinakua sawa. Hapa anza na Bolt hii haichelewi huku unasubiri uber hii kidogo utasubiri.
MIMI: ongea na jamaa then nipe namba yake mwambie huyu ni ndugu yangu wa damu. Afu unaongeaje na mtu usiyemjua?? Kama tapeli?
DULLAH: [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], Tajiri nishafungua account nyingi sana na yeye hana noma usiwe na wasiwasi.
Dullah akaongea na jamaa walitumia muda kidogo baada ya hapo akanirudia akanambia nimeongea naye Freshy utampa 90,000 atafanya hiyo kazi. Nikamshukuru nikampa 10,000 ya Ahsante.
Nikampigia simu Ghost tukaongea maana alikua anajua tayari kuhusu mimi. Akanambia nimtumie baadhi ya documents kama kadi ya gari, ID, bima na picha ya gari na taktaka zingine. Akanambia ndani ya siku 3 itakua tayari.
Baada ya siku 3 akanicheki ghost akanambia account yako ipo tayari, akanipa password akanambia download bolt driver app kwa simu then anza kazi. Kweli nikafanya nikaona mambo yako supa nikaona sehem ya kwenda online kama unataka request, nika touch pale nikaona inasearch nikazima data nikalala, nikaplan kuingia mzigoni jioni.
ITAENDELEA…..
Nimeshapata account ya bolt tayari nini kitaendelea? Mama Junior hajui kama nimeamua kufanya hii kazi atakubali?? Usikose mwendelezo story tamu ndo zinaanza sasa, usikose bando tu.
Domhome
Watu8
Missy Gf
Chakula Kibaya
Copa Cabana
Cute Wife
kama uchawi vile nilipofika hapo request ikapiga kenke kenkeee na mm huku uber yangu imelia dididih dididih dididihEPISODE 03
Baada ya siku 3 akanicheki ghost akanambia account yako ipo tayari, akanipa password akanambia download bolt driver app kwa istore then anza kazi. Kweli nikafanya nikaona mambo yako supa nikaona sehem ya kwenda online kama unataka request, nika touch pale nikaona inasearch nikazima data nikalala, nikaplan kuingia mzigoni jioni.
Inaendelea
“Unajua biashara ya Uber ni nzuri sana kwa kijana ambaye anataka kujiajiri, inalipa sana kama utakua makini. Niko kwenye hii biashara toka 2017 nina uzoefu wa kutosha sana, nimepitia mishale mingi sana. Mdogo wangu nakuomba sana zingatia haya, 1. Focus na malengo yako, 2. Acha tamaa, 3. Fanya kazi kwa bidii chukulia kama ni kazi nyingine. Acha tamaa na wanawake, utakutana na mademu wengi sana kuna ambao watataka uwale sababu hana nauli, kuna wamama watu wazima “mashangazi” watakutaka nakuona so HB mdogo wangu wamama wengi watavutiwa sana wewe. Kuwa mkarimu kwa wateja, Ipende ofisi yako “gari yako” hakikisha unafanya usafi muda wote liko safi, kuwa makini sana wakati wa usiku sio kila sehemu ya kwenda. Utakutana na watu wa kila aina chamsingi wewe kuwa humble usipende kugombana na wateja kabisa. Ukizingatia haya utafika mbali na pia gari yako utaiona pesa trust me. “Hayo yalikua maneno ya Dullah akinipa changamoto za biashara hii ya Tax mtandao.”
Niliamka saa 11 jioni nikaingia bafuni nikajiandaa chap nikaweka mazingira mazuri ya gari. Nilianza hii kazi ya Uber mwishoni October 2021, bhasi nikapitia filling station nikajaza mafuta full tank huyo nikaenda kupark gari pale mbezi Beach kwa zena. Hapo nilikua nimeswitch online so dizaini kama App ilikua inasearch requests.
Nimekaa kama nusu saa hollaaa hakuna hata request nikaanza pata wasiwasi au sababu mimi mpya??. Nikampigia simu Dullah kumwambia sipati request, Dullah akanambia vumilia tu zitaita usiwe na wasiwasi.
Baada ya dk 10 hivi nikaskia kitu kinaita “nke nke nkee nkeeke nkeee” uyo chap ni accept, ukweli nilikua bado na kaushamba wa kutumia hii App lakini Dullah alinielekeza namna ya kutumia map na vitu vingine muhimu akanambia vingine utamasta taratibu.
Baada ya kuaccept mteja akapiga simu akanambia fata ramani, nikamjibu sawa, (“kwa mara ya kwanza App lazima itakuchanganya”). Nikaanza kwenda uelekeo wa kawe akapiga simu nakuona unapotea “Oasisi” unakujua?… nikamjibu ndio, mteja akanambia sasa huko unakwenda wapi??. Oasisi nilikua najua kabla hujafika round about [emoji3534] ya kwenda whitesand kuna kibarabara cha lami kinakunja kushoto, chap nikageuka nikafika mpaka kwa mteja nikamchukua alikua anakwenda mbweni.
Baada ya kumshusha mteja Mbweni sikukaa sana nikapata request nyingine nika accept mteja alikua anakwenda mbezi beach- shamo tower. Nilipiga kazi mpaka saa 6 usiku nikaingiza 59,000, nikapitia sheli nikajazia mafuta tena yaliyotumika nikabaki na 39,000, nikaona pesa nzuri kwa muda wa masaa 6 tu niliyofanya ikanipa morare sana.
Asubuhi nikaamka 06:00 am nikaanza kazi kama kawaida siku hiyo nilipiga kazi mpaka muda wangu wa kudrive ukaisha. So nilirud home kama 23:00 pm, pesa nilizoingiza sio haba kwenye App ubao ulikua unasoma 153,000/= bado zile pesa nilizokua naingiza nje na App. Ukitoa gharama za wese na cost nyingine faida yangu ilikua kama 80,000 hivi.( “Uber/Bolt kuna driving limit, hutakiwi kudrive zaidi ya masaa 12 kwa siku, ukidrive masaa 12 wanakufungia App ukapumzike kwa masaa 6 then urudi mzigoni tena, kwa mtu anayetafuta pesa hii ni changamoto sana, hapo ndo utaona umuhimu wa kuwa na App zote mbili Uber/Bolt”)
Niseme ukweli kwa muda mfupi ndani ya week nilitengeneza pesa ndefu sana. Mpaka nikaona hakuna haja ya kuajiriwa kama Bolt tu inaniingizia pesa hivi kuna haja gani ya kutafuta kazi??.
Baada ya week 2 kukata “ghost”akanicheki akanambia account yangu ya Uber ipo tayari. Nikaanza kuitumia Uber aisee huku ndo nilianza kupata deals nyingi sana na pesa upande wa nauli zilikua juu tofauti na bolt, huku nikaanza pata connections nyingi na kukutana na foreigners.
*******
Nataka kidogo niwape utofauti wa Uber na Bolt. Uber wako vizuri sana upande wa fares na usalama, kwanza wanaotumia Uber wengi ni foreigners pia ni watu wenye pesa au matajiri. Abiria wa uber akirequest wanajua kwenda na muda itoshe kusema abiria wa Uber ni smart sana. Ukija kwa ndugu zetu wa Bolt abiria wao ni pasua kichwa sana, wateja wa bolt wengi ni wanachuo, wale low income earners ndo unawakuta huku sasa. Abiria wa Bolt ni wanamaneno balaa, ana request usafir anakuweka hata nusu sometimes mpaka one hour afu akija anakupa majibi rahisi nilijua upo mbali. Nauli ikiongezeka kidgo atalalamika balaa, madereva wa Tax mtandao wanakwambia bolt ni kwa maskini na Uber ni kwa matajiri. Pia raha ya Uber hata kama mteja atakuweka baada ya dk 5 inaanza kucharge waiting fee, tofauti na Bolt.
Baada ya kuanza kutumia Uber nikaona nitaendana sana na wateja wa Uber kuliko Bolt hata kimaslahi yapo Uber nikaamua kuachana na Bolt, japo nilikua naitumia kwa nadra sana na baadhi ya mazingira.
“Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya uber na wateja wake kama nilivyosema huko juu. “
Nilivyoanza kutumia Uber nilianza kupata sana hela sio hivyo tu bali niliweza kupata dili nyingi sana. Niliweza kukutana na foreigners wengi sana wa nchi mbalimbali pamoja na matajiri, viongozi wakubwa wa serikali, na celebrities mbalimbali. Niliweza kujuana na watu wengi sana mpaka leo kuna foreigners nachat nao sana hata wakija bongo lazima wanicheki.
Siwezi kusimulia matukio yote maana ni mengi kwakweli nitagusia baadhi. Muda wangu wa kazi ulikua naamka 06:00 am mpaka usiku, kama biashara siku iyo mbaya bhasi mapema niko home kucheza na Junior. Siku za weekend nilikua nakesha siku zingine narudi late night. Nilikua nazingatia sana usafi wa gari, usafi wangu binafsi, yaani siku za kazi nilikua nachomekea kama officer nakwenda kazini kumbe ni Uber tu, hii kitu ilepelekea kupendwa sana na watu na wateja wangu wengi walikua wanawake.
*******
Nikiwa barabarani kama kawaida nilikua Posta nimepaki gari yangu pale, mida ya saa10 jion nikapata request ya kwenda Airport. Nikampeleka yule mteja alikua ni dada, akanambia ameipenda gari yangu atakua ananicheki, baada ya kumdrop pale tukabadilishana namba.
Nilikua pale Terminal 2 nimechili nasubiri request ilikua nishakaa almost dk 45, nikakumbuka Dullah alinambia kwakua unatumia vibao vya njano make sure uko makini sana maana pale Airpot wakijua wewe ni Uber then gari yako haina vibao vyeupe watakupiga fine, hata wale madereva wa tax mle Airpot ni wanaa sana.
Mnajua kwanini madereva wa Tax mle Airpot hawawapendi Uber? Ujio wa Tax mtandao umewaharibia sana biashara afu Tax nyingi mle ndani ni za wafanyakazi wa mle ndani. Mfano kutumia tax ya Airport mpaka Masaki utalipia 50,000-70,000 wakati kwa Uber haizidi 25,000, hapo utaona kama Tax mtandao ikawa msaada sana.
Baada ya 1 hr hivi nikapata request mteja alikua anakwenda Sea cliff hotel, chap aka nitext kupitia App “Are you coming”, nikamjibu ASAP. Yaani “As soon as possible”
Ofcourse nilikua mgeni na Airpot na kwa mara ya kwanza lazima uchanganye kama sio mzoefu wa zile barabara za mle ndani, na pia hakuna barabara ya kutoka Terminal 2 kwenda Terminal 3 ya shortcut “sio kwamba shortcut haipo ila wameiziba tu makusudi”, so pale unavyotoka lazima ulipie then uwe kama unatoka ndo uzunguke ile round about [emoji3534] kama unatoka ndo uelekee Terminal 3.
Kama ulikua Terminal 2 unataka kwenda terminal 3 lazima ulipie 2,000 utoke pale terminal 2 then kuingia terminal 3 lazima uchukue card inamaana lazima ulipie tena utakavyotoka terminal 3 (lazima ulipie mara 2). “Hapo jamaa alikua ananielekeza pale terminal 2 maana nilikua sijui na ukichanganya hata barabara tu unalimwa fine, nilisikiliza maelezo vizurii sana nikamasta.”
Message ikaingia kwenye App “I am near the Arrival door” huyu alikuwa mteja.
Nikahisi huyu atakua foreigner tu, nikafika pale wakati nasogea akawa kashasogea barabarani akanipa ishara, nikampakia hao tukasepa. “Wazungu wako chap sana huwa hawapotezi muda kabisa, akirequest labda wewe uzingue, ila wabongo wanaringa sana”. Safari yetu ilikua ni kuelekea Sea cliff hotel kule Masaki, bhasi tukiwa njiani tukaanza story…..
MZUNGU: Bro your Car is very clean
MIMI: Thanks bro! It’s my office, how was the journey??
MZUNGU: Wow was amazing bro and I’m very happy being here in Tanzania [emoji1241] [emoji4].
MIMI: So it’s your first time being here?
MZUNGU: [emoji23][emoji23][emoji23], no bro!, it’s my second time.
MIMI: Welcome bro! so your nationality?
MZUNGU: I’m Swiss bro! [emoji1237]
MIMI: Wow nice bro! So What do you do for a living?.
MZUNGU: I am working for WORLD VISION.
Tuliongea mengi sana na Mzungu akanambia kule hotelini ana workmates hivyo atanicheki niwapeleke Morogoro na watakua Tanzania kwa week 2. Tukafika pale Sea cliff hotel nikamdrop tuka exchange contacts.
Jumatano nikiwa mzigoni kama kawaida yangu, alinipigia simu kama nitakua around maeneo ya Sea cliff nimcheki tuongee, jioni nikamcheki akanambia tukutane pale Karambezi cafe.
Tutakutana pale tukaanza story so ishu mezani ilikua ni alikua anatarajia kwenda Morogoro Ijumaa na ndugu zake( jumla watakua 4). Akaniambia tutarudi jumapili hivyo nimpe gharama zangu, nikamwambia badae nitamcheki nikiwa na cost zote. Tuliongea mambo mengi sana ya kimaisha inshort ndani ya muda alikua ametokea kunikubali sana. Bhasi tukaagana pale, katika story zetu nilimwambia na mke na mtoto mmoja hata yeye pia alinambia kaoa ana watoto 2, akanambia Msalimie Junior, before sijaondoka nitakuja kumwona.
Ile night nikamcheki huyu mzungu alikua anaitwa “MANUEL” ni jina lake halisi, nikampa mchanganuo wa gharama zangu nikamwambia hesabu ya jumla kila kitu kitakua chini yangu tukakubaliana $500 kwa zile siku tutakazokua kule Moro. Akanipa kazi nifanye booking ya hotel nzuri kwa ajili ya watu 4 kwa siku 2, that time Morena Hotel ndo ilikua imefunguliwa nika book hotel pale.
Ijumaa asubuhi na mapema nikaenda pale kuwabeba tukaenda Morogoro, nikawadrop pale Morena Hotel, tulifika Morogoro saa5 na dakika kadhaa, siku ileile tukaenda Mzumbe University sijui walikua na Agenda gani pale tukarudi hotelini jion saa11. Manuel akasema “Lets have dinner together” tukaingia hotelini tukaenjoy pale story zilikua nyingi sana, tukapiga na wine za kutosha sana.
Ilikua ishafika saa3 nikawaaga,
“So where are you going to sleep??, hilo lilikua ni swali kutoka kwa Manuel.
Wote wakawa wananitizama wakisubiri jibu. Kuna dada mmoja mzungu akasema , “he doesn’t want to sleep with us here”.
MIMI: No I have my friend here so don’t worry about me guys.
Mimi nilikwenda kwa jamaa yangu anakaa paleple around kihonda stand, nilimpanga mapema. Nilikua nakwepa gharama za hotel,
Asubuhi mapema nikapanda hotelini kuwabeba walikua wanakwenda SUA chuoni sijui walikua na agenda gani, Pale SUA tulitoka mchana ikabidi turudi tena Mzumbe jioni tukarudi hotelin. Kama kawaida have dinner, tukaplan tukirudi dar niwapeleke moja ya viwanja maarufu vya bata.
Jumapili mida ya saa6 mchana tukaanza safari ya kurudi Dar kitu kama kumi kasoro tukawa tumefika. Nikawarudisha pale Sea cliff hotel,
So bro badae tutakwenda wapi? Aliuliza Manuel,
Nikamjibu “Saprise”[emoji3]. Akanambia Ok bro I trust you!!, nikamwambia by 07:00 PM ntakua around kuwachukua, Na mimi nikarudi zangu home. Palepale akanilipa Pesa zangu ambayo tulikubaliana nikapokea, kuja kuhesabu ilikua jumla $550. Nikatabasamu.
Tukiwa parking nilitamani kumwuliza kuhusu wale dada 3 ni nani kwake? lakini nikapotezea nikapanga kumwuliza siku nyingine.” Kweli wale dada walikua ni visu sana kuna mmoja alikua mdogo mdogo hivi nilimwelewa sana.
Nilivyoingia home nikawaza hawa nawapeleka wapi ukicheki leo Jumapili, kwa jumapili sehemu yenye vibe ni Kidimbwi tu ndo watavibe na wale wote pombe wanatumia, so sikupata ukakasi sana.
“Kwa jumapili kidimbwi huwa inajaa sana tuseme ndo kiwanja pekee kwa Jumapili huwa kina vibe hapa mjini”.
Nikapata wazo nifanye booking kabisa “reservation”, maana tukichelewa tutakosa space then niko na hawa wazungu tutaanza hangaika kupata nafasi, sikutaka kupoteza point 3 kwenye vitu vidogo kama hivi.
Nikaingia Instagram nikachukua namba zao nikawapigia simu chap, dada akapokea nikamwambia dhumuni langu akanambia table bado zipo ila I have to make payment before. Nikamwambia dada sikia tuko 5 hawa wengine ni foreigners, sisi tunakuja by 08:00 PM tutakua hapo on time. Dada akawa haelewi hivi akanambia wengi huwa wanapiga simu hawatokei na hii ni biashara huu ndo utaratibu wetu, nikamwambia nakurudia ASAP.
Nika mcall Manuel kumpanga akaniambia good bro! you can proceed. Nikamrudia Dada tena akanambia cost za table kwa VIP inaanzia 500,000 na kuendelea pia akanambia kuna table zingine ili ukae lazima uwe unatumia 200k na kuendelea. Nikaona option 2 ndo nzuri zaidi, akanambia ana reserve ila ikifka muda huo bila taarifa yoyote atawapa watu wengine.
“Bro! tunatoka out, tunakwenda kunywa na kulewa, acha gari tu home kwa usalama zaidi sisi, tunakuja na Uber, nitumie location” ilikua mesage ya Manuel. Nikaona ni jambo jema sana.
By 07:00 PM ontime nikawa nimefika pale Kidimbwi ili kuweka mambo sawa na kuchagua location nzuri. Nikiwa njian nilikua nishampanga dada niko njiani, nilivyofika pale dada Ofcourse akanipeleka moja kwa moja upande wa chini kwa mbele unaona mandhari ya bahari.
Kwenye mbili kasoro Manuel na ndugu zake nao walikua wamefika pale Kidimbwi, ofcourse walikuwa wamependeza sana, niliona jinsi wabongo wakiwatolea macho wale dada waswiss. Walifurahi sana na walipapenda sana pale na yale mazingira walipagawa sana.
Hawa dada 3 wa kizungu ngoja niwape majina yao
“Dada 1, Jina lake Alex, huyu alikua ndo mkubwa age yake ni around 30’s+ hivi”
“Dada 2, jina lake Olivia, huyu alikua around 25-28s”
“Dada 3, jina lake Sophie, huyu alikua mdogo kwa wote age yake 22”. Huyu nilipata muda wa kuzungumza naye vizuri tukiwa Moro,alinitamkia mwenyewe age yake, alikua anasoma bado. Ukweli alikua mzuri sana “kisu”.
*********
Baada ya kuingia ndani wahudumu walikua wanatukimbilia sana, all Eyes on US.
Kila mtu akaagiza anachojua yeye kwa waiter pale, wakati dada anatoka kwenda kufata, Manuel akamnong’eza dada japo alionekana kuelewa alichoongea Manuel.
Baada ya dakika kadhaa dada akaja na Vodka chupa kubwa, mimi niliagiza heineken ila zikaja bucket 2, ikaja backet ya desperados na Corona beer. “Nikajua Manuel alimwambia dada kwa kila order alete backet. Tuka agiza na mishikaki 50 “ yaani kila mtu mishikaki 10”.
*********
Tulianza gambe mapema sana so kadri muda unavyokwenda na watu walizidi kumininika kwa wingi na kufanya mandhari ile izidi kupendeza.
Kuna kitu ambacho nili kinotice kutoka kwa Manuel, nikahisi uwepo wa wale ndugu zake 3 ni kama kuna uhuru anakosa, huko mbele mtakuja kufahamu ni mtu wa namna gani.
Kadri muda unavyozidi kwenda na pombe zilizidi kukolea japo kwa yale mazingira ya upepo wa bahari mwanana wa Kidimbwi ulifanya pombe kuchelewa sana kuchanganya mwilini.
Zikashuka backets zingine tukaendelea kupiga pombe, ukweli wazungu wapo vizuri sana kwenye masuala ya pombe wanakimbiza balaa. Manuel alimaliza ile chupa ya Vodka na alikua ngangari akaagiza nyingine, this time alikua anakunywa na Alex kama wanashare.
Mida ya Saa 9 usiku tukaondoka pale Manuel aka request Uber kurudi Sea cliff na mimi nikarequest kurudi home mbezi beach.
ITAENDELEA KESHO.