Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 03

Baada ya siku 3 akanicheki ghost akanambia account yako ipo tayari, akanipa password akanambia download bolt driver app kwa istore then anza kazi. Kweli nikafanya nikaona mambo yako supa nikaona sehem ya kwenda online kama unataka request, nika touch pale nikaona inasearch nikazima data nikalala, nikaplan kuingia mzigoni jioni.

Inaendelea

“Unajua biashara ya Uber ni nzuri sana kwa kijana ambaye anataka kujiajiri, inalipa sana kama utakua makini. Niko kwenye hii biashara toka 2017 nina uzoefu wa kutosha sana, nimepitia mishale mingi sana. Mdogo wangu nakuomba sana zingatia haya, 1. Focus na malengo yako, 2. Acha tamaa, 3. Fanya kazi kwa bidii chukulia kama ni kazi nyingine. Acha tamaa na wanawake, utakutana na mademu wengi sana kuna ambao watataka uwale sababu hana nauli, kuna wamama watu wazima “mashangazi” watakutaka nakuona so HB mdogo wangu wamama wengi watavutiwa sana wewe. Kuwa mkarimu kwa wateja, Ipende ofisi yako “gari yako” hakikisha unafanya usafi muda wote liko safi, kuwa makini sana wakati wa usiku sio kila sehemu ya kwenda. Utakutana na watu wa kila aina chamsingi wewe kuwa humble usipende kugombana na wateja kabisa. Ukizingatia haya utafika mbali na pia gari yako utaiona pesa trust me. “Hayo yalikua maneno ya Dullah akinipa changamoto za biashara hii ya Tax mtandao.”

Niliamka saa 11 jioni nikaingia bafuni nikajiandaa chap nikaweka mazingira mazuri ya gari. Nilianza hii kazi ya Uber mwishoni October 2021, bhasi nikapitia filling station nikajaza mafuta full tank huyo nikaenda kupark gari pale mbezi Beach kwa zena. Hapo nilikua nimeswitch online so dizaini kama App ilikua inasearch requests.

Nimekaa kama nusu saa hollaaa hakuna hata request nikaanza pata wasiwasi au sababu mimi mpya??. Nikampigia simu Dullah kumwambia sipati request, Dullah akanambia vumilia tu zitaita usiwe na wasiwasi.

Baada ya dk 10 hivi nikaskia kitu kinaita “nke nke nkee nkeeke nkeee” uyo chap ni accept, ukweli nilikua bado na kaushamba wa kutumia hii App lakini Dullah alinielekeza namna ya kutumia map na vitu vingine muhimu akanambia vingine utamasta taratibu.

Baada ya kuaccept mteja akapiga simu akanambia fata ramani, nikamjibu sawa, (“kwa mara ya kwanza App lazima itakuchanganya”). Nikaanza kwenda uelekeo wa kawe akapiga simu nakuona unapotea “Oasisi” unakujua?… nikamjibu ndio, mteja akanambia sasa huko unakwenda wapi??. Oasisi nilikua najua kabla hujafika round about [emoji3534] ya kwenda whitesand kuna kibarabara cha lami kinakunja kushoto, chap nikageuka nikafika mpaka kwa mteja nikamchukua alikua anakwenda mbweni.

Baada ya kumshusha mteja Mbweni sikukaa sana nikapata request nyingine nika accept mteja alikua anakwenda mbezi beach- shamo tower. Nilipiga kazi mpaka saa 6 usiku nikaingiza 59,000, nikapitia sheli nikajazia mafuta tena yaliyotumika nikabaki na 39,000, nikaona pesa nzuri kwa muda wa masaa 6 tu niliyofanya ikanipa morare sana.

Asubuhi nikaamka 06:00 am nikaanza kazi kama kawaida siku hiyo nilipiga kazi mpaka muda wangu wa kudrive ukaisha. So nilirud home kama 23:00 pm, pesa nilizoingiza sio haba kwenye App ubao ulikua unasoma 153,000/= bado zile pesa nilizokua naingiza nje na App. Ukitoa gharama za wese na cost nyingine faida yangu ilikua kama 80,000 hivi.( “Uber/Bolt kuna driving limit, hutakiwi kudrive zaidi ya masaa 12 kwa siku, ukidrive masaa 12 wanakufungia App ukapumzike kwa masaa 6 then urudi mzigoni tena, kwa mtu anayetafuta pesa hii ni changamoto sana, hapo ndo utaona umuhimu wa kuwa na App zote mbili Uber/Bolt”)

Niseme ukweli kwa muda mfupi ndani ya week nilitengeneza pesa ndefu sana. Mpaka nikaona hakuna haja ya kuajiriwa kama Bolt tu inaniingizia pesa hivi kuna haja gani ya kutafuta kazi??.

Baada ya week 2 kukata “ghost”akanicheki akanambia account yangu ya Uber ipo tayari. Nikaanza kuitumia Uber aisee huku ndo nilianza kupata deals nyingi sana na pesa upande wa nauli zilikua juu tofauti na bolt, huku nikaanza pata connections nyingi na kukutana na foreigners.

*******
Nataka kidogo niwape utofauti wa Uber na Bolt. Uber wako vizuri sana upande wa fares na usalama, kwanza wanaotumia Uber wengi ni foreigners pia ni watu wenye pesa au matajiri. Abiria wa uber akirequest wanajua kwenda na muda itoshe kusema abiria wa Uber ni smart sana. Ukija kwa ndugu zetu wa Bolt abiria wao ni pasua kichwa sana, wateja wa bolt wengi ni wanachuo, wale low income earners ndo unawakuta huku sasa. Abiria wa Bolt ni wanamaneno balaa, ana request usafir anakuweka hata nusu sometimes mpaka one hour afu akija anakupa majibi rahisi nilijua upo mbali. Nauli ikiongezeka kidgo atalalamika balaa, madereva wa Tax mtandao wanakwambia bolt ni kwa maskini na Uber ni kwa matajiri. Pia raha ya Uber hata kama mteja atakuweka baada ya dk 5 inaanza kucharge waiting fee, tofauti na Bolt.

Baada ya kuanza kutumia Uber nikaona nitaendana sana na wateja wa Uber kuliko Bolt hata kimaslahi yapo Uber nikaamua kuachana na Bolt, japo nilikua naitumia kwa nadra sana na baadhi ya mazingira.

“Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya uber na wateja wake kama nilivyosema huko juu. “

Nilivyoanza kutumia Uber nilianza kupata sana hela sio hivyo tu bali niliweza kupata dili nyingi sana. Niliweza kukutana na foreigners wengi sana wa nchi mbalimbali pamoja na matajiri, viongozi wakubwa wa serikali, na celebrities mbalimbali. Niliweza kujuana na watu wengi sana mpaka leo kuna foreigners nachat nao sana hata wakija bongo lazima wanicheki.

Siwezi kusimulia matukio yote maana ni mengi kwakweli nitagusia baadhi. Muda wangu wa kazi ulikua naamka 06:00 am mpaka usiku, kama biashara siku iyo mbaya bhasi mapema niko home kucheza na Junior. Siku za weekend nilikua nakesha siku zingine narudi late night. Nilikua nazingatia sana usafi wa gari, usafi wangu binafsi, yaani siku za kazi nilikua nachomekea kama officer nakwenda kazini kumbe ni Uber tu, hii kitu ilepelekea kupendwa sana na watu na wateja wangu wengi walikua wanawake.

*******

Nikiwa barabarani kama kawaida nilikua Posta nimepaki gari yangu pale, mida ya saa10 jion nikapata request ya kwenda Airport. Nikampeleka yule mteja alikua ni dada, akanambia ameipenda gari yangu atakua ananicheki, baada ya kumdrop pale tukabadilishana namba.

Nilikua pale Terminal 2 nimechili nasubiri request ilikua nishakaa almost dk 45, nikakumbuka Dullah alinambia kwakua unatumia vibao vya njano make sure uko makini sana maana pale Airpot wakijua wewe ni Uber then gari yako haina vibao vyeupe watakupiga fine, hata wale madereva wa tax mle Airpot ni wanaa sana.

Mnajua kwanini madereva wa Tax mle Airpot hawawapendi Uber? Ujio wa Tax mtandao umewaharibia sana biashara afu Tax nyingi mle ndani ni za wafanyakazi wa mle ndani. Mfano kutumia tax ya Airport mpaka Masaki utalipia 50,000-70,000 wakati kwa Uber haizidi 25,000, hapo utaona kama Tax mtandao ikawa msaada sana.

Baada ya 1 hr hivi nikapata request mteja alikua anakwenda Sea cliff hotel, chap aka nitext kupitia App “Are you coming”, nikamjibu ASAP. Yaani “As soon as possible”

Ofcourse nilikua mgeni na Airpot na kwa mara ya kwanza lazima uchanganye kama sio mzoefu wa zile barabara za mle ndani, na pia hakuna barabara ya kutoka Terminal 2 kwenda Terminal 3 ya shortcut “sio kwamba shortcut haipo ila wameiziba tu makusudi”, so pale unavyotoka lazima ulipie then uwe kama unatoka ndo uzunguke ile round about [emoji3534] kama unatoka ndo uelekee Terminal 3.

Kama ulikua Terminal 2 unataka kwenda terminal 3 lazima ulipie 2,000 utoke pale terminal 2 then kuingia terminal 3 lazima uchukue card inamaana lazima ulipie tena utakavyotoka terminal 3 (lazima ulipie mara 2). “Hapo jamaa alikua ananielekeza pale terminal 2 maana nilikua sijui na ukichanganya hata barabara tu unalimwa fine, nilisikiliza maelezo vizurii sana nikamasta.”

Message ikaingia kwenye App “I am near the Arrival door” huyu alikuwa mteja.

Nikahisi huyu atakua foreigner tu, nikafika pale wakati nasogea akawa kashasogea barabarani akanipa ishara, nikampakia hao tukasepa. “Wazungu wako chap sana huwa hawapotezi muda kabisa, akirequest labda wewe uzingue, ila wabongo wanaringa sana”. Safari yetu ilikua ni kuelekea Sea cliff hotel kule Masaki, bhasi tukiwa njiani tukaanza story…..

MZUNGU: Bro your Car is very clean

MIMI: Thanks bro! It’s my office, how was the journey??

MZUNGU: Wow was amazing bro and I’m very happy being here in Tanzania [emoji1241] [emoji4].

MIMI: So it’s your first time being here?

MZUNGU: [emoji23][emoji23][emoji23], no bro!, it’s my second time.

MIMI: Welcome bro! so your nationality?

MZUNGU: I’m Swiss bro! [emoji1237]

MIMI: Wow nice bro! So What do you do for a living?.

MZUNGU: I am working for WORLD VISION.

Tuliongea mengi sana na Mzungu akanambia kule hotelini ana workmates hivyo atanicheki niwapeleke Morogoro na watakua Tanzania kwa week 2. Tukafika pale Sea cliff hotel nikamdrop tuka exchange contacts.

Jumatano nikiwa mzigoni kama kawaida yangu, alinipigia simu kama nitakua around maeneo ya Sea cliff nimcheki tuongee, jioni nikamcheki akanambia tukutane pale Karambezi cafe.

Tutakutana pale tukaanza story so ishu mezani ilikua ni alikua anatarajia kwenda Morogoro Ijumaa na ndugu zake( jumla watakua 4). Akaniambia tutarudi jumapili hivyo nimpe gharama zangu, nikamwambia badae nitamcheki nikiwa na cost zote. Tuliongea mambo mengi sana ya kimaisha inshort ndani ya muda alikua ametokea kunikubali sana. Bhasi tukaagana pale, katika story zetu nilimwambia na mke na mtoto mmoja hata yeye pia alinambia kaoa ana watoto 2, akanambia Msalimie Junior, before sijaondoka nitakuja kumwona.

Ile night nikamcheki huyu mzungu alikua anaitwa “MANUEL” ni jina lake halisi, nikampa mchanganuo wa gharama zangu nikamwambia hesabu ya jumla kila kitu kitakua chini yangu tukakubaliana $500 kwa zile siku tutakazokua kule Moro. Akanipa kazi nifanye booking ya hotel nzuri kwa ajili ya watu 4 kwa siku 2, that time Morena Hotel ndo ilikua imefunguliwa nika book hotel pale.

Ijumaa asubuhi na mapema nikaenda pale kuwabeba tukaenda Morogoro, nikawadrop pale Morena Hotel, tulifika Morogoro saa5 na dakika kadhaa, siku ileile tukaenda Mzumbe University sijui walikua na Agenda gani pale tukarudi hotelini jion saa11. Manuel akasema “Lets have dinner together” tukaingia hotelini tukaenjoy pale story zilikua nyingi sana, tukapiga na wine za kutosha sana.

Ilikua ishafika saa3 nikawaaga,

“So where are you going to sleep??, hilo lilikua ni swali kutoka kwa Manuel.

Wote wakawa wananitizama wakisubiri jibu. Kuna dada mmoja mzungu akasema , “he doesn’t want to sleep with us here”.

MIMI: No I have my friend here so don’t worry about me guys.

Mimi nilikwenda kwa jamaa yangu anakaa paleple around kihonda stand, nilimpanga mapema. Nilikua nakwepa gharama za hotel,

Asubuhi mapema nikapanda hotelini kuwabeba walikua wanakwenda SUA chuoni sijui walikua na agenda gani, Pale SUA tulitoka mchana ikabidi turudi tena Mzumbe jioni tukarudi hotelin. Kama kawaida have dinner, tukaplan tukirudi dar niwapeleke moja ya viwanja maarufu vya bata.

Jumapili mida ya saa6 mchana tukaanza safari ya kurudi Dar kitu kama kumi kasoro tukawa tumefika. Nikawarudisha pale Sea cliff hotel,

So bro badae tutakwenda wapi? Aliuliza Manuel,

Nikamjibu “Saprise”[emoji3]. Akanambia Ok bro I trust you!!, nikamwambia by 07:00 PM ntakua around kuwachukua, Na mimi nikarudi zangu home. Palepale akanilipa Pesa zangu ambayo tulikubaliana nikapokea, kuja kuhesabu ilikua jumla $550. Nikatabasamu.

Tukiwa parking nilitamani kumwuliza kuhusu wale dada 3 ni nani kwake? lakini nikapotezea nikapanga kumwuliza siku nyingine.” Kweli wale dada walikua ni visu sana kuna mmoja alikua mdogo mdogo hivi nilimwelewa sana.

Nilivyoingia home nikawaza hawa nawapeleka wapi ukicheki leo Jumapili, kwa jumapili sehemu yenye vibe ni Kidimbwi tu ndo watavibe na wale wote pombe wanatumia, so sikupata ukakasi sana.

“Kwa jumapili kidimbwi huwa inajaa sana tuseme ndo kiwanja pekee kwa Jumapili huwa kina vibe hapa mjini”.

Nikapata wazo nifanye booking kabisa “reservation”, maana tukichelewa tutakosa space then niko na hawa wazungu tutaanza hangaika kupata nafasi, sikutaka kupoteza point 3 kwenye vitu vidogo kama hivi.

Nikaingia Instagram nikachukua namba zao nikawapigia simu chap, dada akapokea nikamwambia dhumuni langu akanambia table bado zipo ila I have to make payment before. Nikamwambia dada sikia tuko 5 hawa wengine ni foreigners, sisi tunakuja by 08:00 PM tutakua hapo on time. Dada akawa haelewi hivi akanambia wengi huwa wanapiga simu hawatokei na hii ni biashara huu ndo utaratibu wetu, nikamwambia nakurudia ASAP.

Nika mcall Manuel kumpanga akaniambia good bro! you can proceed. Nikamrudia Dada tena akanambia cost za table kwa VIP inaanzia 500,000 na kuendelea pia akanambia kuna table zingine ili ukae lazima uwe unatumia 200k na kuendelea. Nikaona option 2 ndo nzuri zaidi, akanambia ana reserve ila ikifka muda huo bila taarifa yoyote atawapa watu wengine.

“Bro! tunatoka out, tunakwenda kunywa na kulewa, acha gari tu home kwa usalama zaidi sisi, tunakuja na Uber, nitumie location” ilikua mesage ya Manuel. Nikaona ni jambo jema sana.

By 07:00 PM ontime nikawa nimefika pale Kidimbwi ili kuweka mambo sawa na kuchagua location nzuri. Nikiwa njian nilikua nishampanga dada niko njiani, nilivyofika pale dada Ofcourse akanipeleka moja kwa moja upande wa chini kwa mbele unaona mandhari ya bahari.

Kwenye mbili kasoro Manuel na ndugu zake nao walikua wamefika pale Kidimbwi, ofcourse walikuwa wamependeza sana, niliona jinsi wabongo wakiwatolea macho wale dada waswiss. Walifurahi sana na walipapenda sana pale na yale mazingira walipagawa sana.

Hawa dada 3 wa kizungu ngoja niwape majina yao
“Dada 1, Jina lake Alex, huyu alikua ndo mkubwa age yake ni around 30’s+ hivi”

“Dada 2, jina lake Olivia, huyu alikua around 25-28s”

“Dada 3, jina lake Sophie, huyu alikua mdogo kwa wote age yake 22”. Huyu nilipata muda wa kuzungumza naye vizuri tukiwa Moro,alinitamkia mwenyewe age yake, alikua anasoma bado. Ukweli alikua mzuri sana “kisu”.

*********
Baada ya kuingia ndani wahudumu walikua wanatukimbilia sana, all Eyes on US.

Kila mtu akaagiza anachojua yeye kwa waiter pale, wakati dada anatoka kwenda kufata, Manuel akamnong’eza dada japo alionekana kuelewa alichoongea Manuel.

Baada ya dakika kadhaa dada akaja na Vodka chupa kubwa, mimi niliagiza heineken ila zikaja bucket 2, ikaja backet ya desperados na Corona beer. “Nikajua Manuel alimwambia dada kwa kila order alete backet. Tuka agiza na mishikaki 50 “ yaani kila mtu mishikaki 10”.

*********
Tulianza gambe mapema sana so kadri muda unavyokwenda na watu walizidi kumininika kwa wingi na kufanya mandhari ile izidi kupendeza.

Kuna kitu ambacho nili kinotice kutoka kwa Manuel, nikahisi uwepo wa wale ndugu zake 3 ni kama kuna uhuru anakosa, huko mbele mtakuja kufahamu ni mtu wa namna gani.

Kadri muda unavyozidi kwenda na pombe zilizidi kukolea japo kwa yale mazingira ya upepo wa bahari mwanana wa Kidimbwi ulifanya pombe kuchelewa sana kuchanganya mwilini.

Zikashuka backets zingine tukaendelea kupiga pombe, ukweli wazungu wapo vizuri sana kwenye masuala ya pombe wanakimbiza balaa. Manuel alimaliza ile chupa ya Vodka na alikua ngangari akaagiza nyingine, this time alikua anakunywa na Alex kama wanashare.

Mida ya Saa 9 usiku tukaondoka pale Manuel aka request Uber kurudi Sea cliff na mimi nikarequest kurudi home mbezi beach.

ITAENDELEA KESHO.
yan kila dereva wa tax mtandao hili linajulikana abiria wa uber na bolt ya ni tofaut kitabia bolt baadh wamejawa na majibu ya ovyo kukalish muda sana alaf wengi ni waswahili[emoji28] ila uber mtu anarequest unafika unamkuta
 
EPISODE 4

Wakati naanza hii kazi Mama Junior alikua hayupo home, alikua kwao ni mimi ambaye nilimpa ruhusa aende akapumzishe akili baada ya dada wa kazi kwenda kwao. Niliona mazingira ya kubaki peke yake na mtoto bila mtu wa kumsaidia mke wangu angeteseka, uzuri kwao ni hapahapa dar. Mama Junior ni mwanamke ambaye ana wivu sana na mimi kiasi kwamba huwa anahisi mimi nachepuka, inshort niseme ni mwanamke ambaye ananipenda sana.

***
Naam! ilikua ni jumatatu tulivu sana, nikakurupuka kitandani kucheki muda saa 5 asubuhi. Wakati naangalia muda nakutana na mcd calls za kutosha, nikakutana na messages,

“Bro! Good morning, how you doing??” -Manuel
“I’m worried about you..”- Manuel

“Kaka habari yako, ni mimi maggy uliyenipeleka Airpot last week, nahitaji tuonane leo if possible”- 0712*********

“Bae! Kwanini hupokei simu zangu? Upo na nani?”- Mama Junior

Kabla sijajibu hizo message nikacheki missd calls

“Mama Junior, 6 “
“Manuel, 2”
“New number, 1”

Akili yangu ikawa inawaza nianze na nani kati ya hao, nikaanza kupigia Manuel kwanza akapokea nikamshukuru kwa kampani ya pale Kidimbwi akanambia kama ntapata nafasi nipitie pale Sea cliff kuna kazi nyingine ya kufanya.

Nikampigia simu Maggy tukaongea akanambia anytime ukifika Posta utanicheki nikamwambia “sawa”.

Nikapiga simu namba ngeni, kupokea alikua ni mama mmoja hivi nilishawai mpakia, na yeye anafanyia kazi moja ya bank pale Posta, Azikiwe.

Nikampigia simu Mama Junior niliamua awe wa mwisho sababu namfahamu vzr, na kwa kitendo cha kutopokea simu zake na kujibu messages nilijua lazima atakua kafura.

Nikampigia simu … [emoji338]

Mama Junior: “Umeshaagana na wanawake zako ndo umeona sasa unitafute kwa muda wako…, Unaweza kunambia jana ulikua wapi? na umelala wapi?”

Mimi: “ Jamani… ndo salamu hiyo?”

Mama Junior: “ Baba Junior tafadhali naomba maelezo…, mwezi umepita hata kuja kutuona na mwanao hutaki, una mambo yako wewe”

Mimi: “ Mke wangu usifike huko… jana nilikua na washikaji walinipa mwaliko, nikaingia night sana, hapa ndo naamka…, hata hvo nimekupigia nikupe habari njema”

Mama J: “Habari zipi..?”

Mimi: “Mwezi wa 12 huu Christmas nataka wewe na Junior mpendeze, piga hesabu na gharama zote then Nitumie”. Hapa nilikua nimemmaliza hata hasira zikaisha kabisa.

Mama J: “Sawa haina shida, I love you. Takecare”


Nikaamka kitandani kwenda kuoga, kwanza nilikua na mahangover ya pombe, nilipeleka backet 2 za heineken sio mchezo, na ukicheki mpaka muda huo sijapata hata soup, kwa wanywaji nadhani huwa mnajua. Dizaini kama nikawa na kauvivu ka kwenda mzigoni, lakini nikasema hapana lazima niende nipige hata kidogo then nionane na hawa watu.

Nilikua napambana sana kutafuta wateja wa private ili niwe na uhakika wa kazi na kupata pesa nyingi. “Nakumbuka Dullah alinisisitiza sana nijitahid sana kuwa na wateja wa private maana hawa ndo kila kitu, App sometimes zinazingua kuna siku kazi zinakua ngumu”. Mfano kwa kila trip kamisheni ya Uber/bolt ni 25% yaani kama ubao unasoma 100,000/= hapo 25,000 ni yao yako 75,000, kwenye hio 75 hujatoa cost za mafuta, parking fee nknk. Ili uweze kupata faida ya angalau 30,000 kwa siku inabidi uingize kuanzia 70,000.

Kuna wale ambao wanaendesha kwa mikataba unakuta kwa bossy anapeleka 25,000-30,000, inabdi apambane kwa siku apate kuanzia 100,000/=, hapo unaona inabdi akili ya ziada sana.

********
Nikaingia mzigoni kama kawaida nikapiga mzigo nikapata mteja wa kwenda pale Aga khan, baada ya kumshusha mteja nikawaza kuonana na Maggy nijue anaishu gani na pia nikakumbuka na yule mama wa azikiwe. Nikasema leo ni “Two birds one stone” napiga ndege wa2 kwa jiwe moja.

Nikamvutia waya Maggy, akanilekeza ofisi yake ni pale Golden Jubilee tower, bhasi mimi nikasogea mpaka pale mtaa wa Ohio nikapark gari oppositie na Golden jubilee. Nikamtext [emoji187] ilikua saa inasoma 9 kasoro mchana.

MIMI: “hey boss niko around”

Maggy: “Umepark wapi?”

Mimi: “Opposite hapa na jubilee, near kibanda cha Mpesa”

Maggy: “Ok nakuja soon, bossy!”

Haikuchukua dakika 10 Maggy akawa amefika kwenye eneo la tukio tayari, nikamsalimia na nikamsifia “you look great”, akatabamu akanambia “nawe pia”.

“So tunafanyia haya maongezi hapahapa, au ndani ya gari??”. Nilimwuliza

Akanambia sijala kwanini tusiende cafe? nikakumbuka hata mimi nilikua sijala chakula cha maana toka niamke, lakini nilikua sisikii njaa.

Nilikokuwa nimepark gari kwa nyuma yake au tusema opposite na “IT plaza” kulikuwa na cafe pale, bhs ndo tuliingia pale, mimi nikaagiza “dona choma” yeye akaagiza “kiepe yai, kuku”. Hiki kicafe ndo niliingia kwa mara ya kwanza, ofcourse nilikipenda wanachakula kitamu afu ni cheap, so kila nikija Posta hapa ndo nilikua nakula msosi.

Tukaanza pale kupiga story sana, Maggy alikuwa anaongea “mimi usafiri wangu ni Uber kila siku asbh pamoja na kurudi so kama upo tayari uwe unakuja asubuhi kunichukua unanipeleka ofisn then jion sa12 unanirudisha home. Pia ninakazi nyingi sana huwa zinatokea hata za siku nzima, Uber wengi gari zao sio safi na wateja wetu wengi ni foreigners, jinsi ulivyo smart na gari yako safi ntakua na amani na wateja wangu.

Nikamwuliza before mimi ulikua unafanyaje? Akanambia nilikua namtu nafanya naye kazi ila hazingatii usafi wa gari. Mimi nikatabasamu pale,

Mimi nikamwambia suala la kuja kukuchukua niachie nilifanyie kazi ntakucheki badae tuyajenge kama tutaafikiana tutafanya kazi lakini suala la wateja wako mimi sina shida hili naweza kupa jibu la direct hapahapa, nikamwambia hao muda wowote nipigie simu hata Arusha tunakwenda, hata kama unasafari nje ya mkoa mim sina tatizo.

Tukaagana pale huku nikimwahidi badae nitamtafuta, palepale nikamcheki mama yangu wa azikiwe, Palepale nikampigia simu lakini hakupokea ghafla ikaingia text “Call you letter”, nikamtext back chap “niko Posta”, akanijibu “Na kikao nitakupigia nikitoka”. Nikamjibu “Ok”.

Kucheki muda ilikua saa 10 kasoro tayari nikasema acha nimsubiri huyu mama then nielekee Masaki kuonana na Manuel. Ukweli nilikuwa natamani sana kupiga story na Manuel maana ni mtu ambaye alitokea kunikubali sana afu hakuwa na roho ya kinyongo ni mtu poa sana. Nilitamani kuongea naye mengi kuhusu Siwtzerland ( “Switzerland ni moja ya nchi nzuri sana kwa foreigners, kusoma, hata upatikanaji kazi”). Plan zangu kubwa ni kutengeneza connection nijue namna kufika kule na masuala mengine.

Wakati narudi kwenye gari yangu nikaona kuna Uber kibao wametega around na mimi, nikaona kikundi cha washikaji wakipiga story nikajua wale ni Uber, bhs nikasogea pale kujumuika na mimi.


Matajiri kwema? za kazi?, wote wakajibu nikawaambia bila shaka nyinyi ni Uber, ndomana namimi nimesogea hapa nimevutiwa na story. Kwa muda mfupi tukawa kama watu ambao tunajuana kitambo.

Unajua story za madereva wa Uber nyingi ni kuhusu madem tu[emoji3][emoji3], ukiona Uber wamekaa kwenye vijiwe vyao hizo ndo story zo kubwa huji kuta wakipiga story za maendeleo hata siku moja. Inshort madem wanaliwa sana na madereva wa Uber.

Pale Posta najuana sana na maderva wa Uber wengi wananiitaga “Wakishua” sababu mimi muda wote niko smart na gari nayo ipo smart, hii ilipelekea kupendwa sana wa abiria.

********
Tulikua watu 6 pale lakini kadri muda ulivyokua ukienda na wahuni walizidi kupungua ikafika stage tukabaki wawili,, “Request ndo zilikua zinatupunguza maana kuanzia saa 11 jion ni muda ambao request zinakua nyingi sana Posta, demand ya ya Uber inakua juu sana hata rate ya nauli inakua juu sana.

Mpaka saa 11 naona kimya yule mama wa Azikiwe hajanitafuta, sikutaka kumtafuta kwanza nitaonekana kama mimi ndo nashida, then ataniona cheap sana, kwanza kitendo cha kumsubiri mpaka saa11 nilijiona fala sana.

Nika switch online App yangu nikaset destination ya kwenda Sea cliff, “ipo hivi kama unataka mteja wa kwenda Masaki au Posta, bhs kwenye App unaset destination, hivyo utapata request zinazoelekea usawa huo inaweza isiwe exactly point ila atlist inasaidia”. So kitendo cha kuweka destinationa haikuchukua muda nikapata request ya mteja alikua anaelekea Coral beach.

Nikamshusha customer pale Coral beach nikachukua uelekeo wa Sea cliff, kutoka Coral mpaka Seacliff sio mbali sana, ilikua chap tu niko pale tayari. “Wakati nakaribia Coral nilikua nishampanga tayari Manuel so akanambia nitamkuta pale Karambezi”.

Nikafika pale Karambezi nikamzoom Manuel kwa mbali ofcourse hapakua na watu wengi sana palikua kawaida tu. Tukasalimiana pale story zikaanza, story kubwa nilikua namwuliza namna ya kufika Switzerland na ishu za kazi especially unskilled jobs. “Njia rahisi ya kuingia chap ni scholarship au kusoma, hapo ni rahisi sana ila kama unakua umepata kazi bhasi mwajiri wako akupambanie visa japo huwa inachukua muda sana na gharama yake kubwa. Kama unataka kuingia wewe apply chuo, I recommend you to use this way, ukishafika ukaanza masomo kama mastars ni mwaka mmoja tu umemaliza, ukiwa unasoma kuna mishe nyingi sana za kufanya kule kama viwandani, mashambani, migahawani nknk” Manuel alikua akiongea.

Manuel mbinu nyingine ya kutumia ya haraka bhasi uoe mswiss hapo unapewa na uraia kabisa, “Nigerians wanatumia sana hii mbinu, wanaoa sana wamama watu wazima” nilicheka sana.

Ishu nyingine kubwa pia jumatano na alhamis nitakua na ratiba ya kutembelea vituo vya watoto yatima kwa Dar, ijumaa tutakwenda kibaha na Bagamoyo, ila kwa Jumamosi utaangalia wapi unatupeleka, then J2 tutaondoka kurudi Switzerland. Manuel alikua akiongea.

Akanionesha vituo tutakavyotembelea nikaona kuna sinza, tegeta, bunju, Kunduchi, Kimara, Kigamboni. Tukakubaliana 600,000/= ( 200,000/= per day) kuhusu jumamosi nikamwambia ntawapa offa, muda ule tulikua tunaikimbiza “pearly bay wine”. Nikamwambia bro jana dizaini kama haukuwa free kule Kidimbwi, alicheka sana akanambia “bro! next time gonna be lit,”. Tukaagana pale.

“The way nilivyomwona Manuel nilihisi kama mtu wa madem sana” huko mbele mtaona.

Before sijatoka pale Karambezi mama yetu alikua kanipigia simu ila sikupokea, so wakati natoka ilikua ishapita saa tayari, na saa yangu ilikua inaonesha ni saa 19:05. Nikampigia simu akanambia karudi home kama vipi niende kwake haina shida, “nikaona mama anaongea ujinga, yaani mimi niende kwake??”. Nikamwambia mama haiwezekani kama muhimu sana tuonane pale Raibow , huyu mama alikua anakaa kule chini Mbezi Beach karibu na Rainbow. “So hakukataa akakubali tuonane pale tuongee”.

Nikawa nawaza huyu mama anataka nini kwangu? Nikachoma mafuta mpaka pale Rainbow mbili kasoro dakika nikawa pale, wakati niko Kawe alikua kanijulisha kafika tayari.

Kufika pale nikaingia ndani nikamkuta amekaa anakunywa savannah, duu! nilijisemea huyu mama hatari au ndo anaongeza nyege!??.

Mimi: Habari yako bossy

Mama: Salama tu, ndo unatoka mishemishe?

Mimi: kama unavyoona, umeniweka sana pale Posta

Mama: jamani pole, kwani ulikua unanisubiri?!

Mimi: Ndio, maana hukusema niondoke! anyway nimeitikia wito bossy wangu, nakusikiliza, what’s a deal?

Mama! Ninataka asubuhi uwe unanichukua na mwanangu, lakini mtoto unamwacha pale mikocheni Warioba( hii shule ipo karibu na msikiti wa mwinyi).

Mimi: Sawa mama, sasa mbona hili lilikuwa lakuongea kwenye simu tu na tukamaliza, au ulitaka kuniona??( nilikua nimekazia macho)

Mama: Huku akicheka, unaonekana mpole sana ila ni mwongeaji sana, unavituko sana.

Mimi: Una watoto wangapi?

Mama: Wawili tu, wakwanza wa kike yuko form 5, wapili yuko standard 3, wote wa kike.

Mimi: wow! am luckiest man, huyo wa form 5 nitunzie ntakua mkwe wako.

Mama: utanibakia mwanangu bure!!

Mimi: So unakunywa beer usiku huu, baba watoto akirudi inakuaje??

Mama: Mume namtolea wapi mimi?, naishi na wanangu tu. Unajua wewe haunywi kama unanichora hapa!

Mimi: Hilo tu usijali, siku ntakupeleka Kidimbwi tukanywe wote.

Mama: Huku akicheka, unavituko sana mimi nishachuja tayari huko wanaenda damu mbichi.

Mimi: unaweza kujiona umechuja ila mimi bado nakuona upo hot sana.

“Huyu ni mama wa kichaga mweupe anashepu nzuri, ni mama kijana afu anajipenda sana huyu age yake anavyoonekana ni 40s ni mama kijana.

Mama: huku akicheka, we kaka unavitukoa sana,

Kwa muda tulio kaa na mama nilikua nishamcontol kwa maongezi na kila kitu kama ningetupia voko angeingia king.

Tukakubaliana pale atanilipa 12,000 kwa trip ila nikamwambia nitaanza jumatatu ya week inayokuja, mama hakuwa na shida kabisa.

“Unajua hawa wateja sometimes nilikua nawapa utani ili kuendelea kuwasogeza karibu na awe huru, haipendezi muda wote kuwa kauzu.”(Kanuni ni kwamba kama mteja ni mwongeaji na wewe kuwa mwongeaji, kama kauzu na wewe kuwa kauzu, hii ndo iliku principle yangu).

*****
Nikatoka pale na furaha sana, hesabu kichwani ni kumalizana ma Maggy hapo tayari na vichwa 2 na vyote vinakwenda Posta. Ilikua saa 3 usiku tayari nikamtext Maggy, palepale akani text back ni kama alikua anasubiri text yangu. Nikampandia hewani nikamwuliza anakaa Mikocheni gani akanambia karibu na shule ya Alpha. Nikamwambia nitakuwa nampeleka tu ila kurudi kama nitakua around nitakuwa namcheki, hakuwa na noma akakubali, tukakubaliana 10,000.

Mnajua kwanini sikutaka kazi ya kumpeleka na kumrudisha? niliwaza nitakua mtumwa, kwanza utakua na stress upo zako mbweni huko afu sa11 umfuate mteja Posta unakua mtumwa, sikutaka hii kitu kabisa, au jambo lingine muda wa kwenda kazini unaeleweka wakati wa kurudi hauleweki, sikutaka kuchoma mahindi bila sababu ya msingi.

Palepale nikapata idea ya kutengeneza mkataba wa kazi, nikachukua laptop nikadizaini mkataba wangu vizuri kabisa, nikaweka mpaka sehem ya kusaini mwanasheria, sikutaka masikhara na kazi kabisa, na pia nilitaka wateja wanione niko serious.

******
Jumatano ilifika huyo nikaenda Seacliff pale kumchukua Manuel lakini this time alikua yeye na Alex tu, tukasalimiana pale. Tulielekea kwenye hivyo vituo walikua wanafanya research zao na kupiga picha. Tulitembelea vituo vyote tukamaliza kwenye sa11 jioni, nikawarudisha mimi nikaendelea na kazi yangu. Kesho yake tukatembelea vituo vingine ile kazi tuliimaliza jioni pia.

Ijumaa ndo siku ya kwenda kibaha na Bagamoyo, kama kawaida tukaenda huko wakafanya mambo yao hii siku tulirudi usiku sana, nikawadrop pale Seacliff lakini Manuel akaomba tukapate dinner then niondoke, sikukataa tukaelekea Karambezi pale.

Ile tunaingia mlango mkubwa wa kwenda Karambezi nakutana na Ex wangu, Tangu nimemaliza chuo sikuwai onana naye ilikua ishapita miaka 3 na yeye alikua 2nd yr that time, nilikua nimemwacha mwaka 1 mbele.

Yeye ndo aliyeniona akaniita jina langu “INSIDER”, Manuel ndo aliyeskia wakati akiniita. Bro somebody is calling you, kucheki namwona Angel (code), wow akaja akanihug kwa nguvu, mpaka Manuel akashangaa!!!

Nilishangaa sana kukutana naye pale ofcourse alikua na rafiki yake afu walikua wakitoka, huyu alikua dem wangu wa chuo enzi hizo baada ya kumaliza chuo aliniacha asee!!, this time tunakutana nimebadilika, nimenawiri,afu niko na wazungu.

Akaomba namba yangu sikutaka kumpa, nikamwambia anipe yake ntamcheki…..

Angel ni mwanamke ambaye nilianza naye mahusiano wakati niko chuo, so wakati wao wanaanza first year mimi ndo nilikutana naye na kuweka ukaribu hatimae tukaanza mahusiano. Tulidumu kwa kipindi chote cha miaka 2, tulipendana sana mpaka masela zangu wa chuo walikua wanaamini huyu mrembo namwoa. Kilichotokea baada ya kumaliza chuo zilianza sababu, mara hapokei simu, ubusy mwingi, nikaanza pata report kutoka kwa masela anaonekana na mwanaume uyo moja kila maeneo, mimi kama mwanaume nikajua hapa sina mtu, nika move on.

********
Tuliagana ma Manuel pale Seacliff ili asubuhi niwai kuwabeba twende misele, ile jumamosi asubuhi by saa 3 nilikua pale. Wakatoka wote hao tukaanza safari plan yetu tuanze na “Ununio beach”, Manuel akaomba twende na “Haile Selasie Road” kuna vitu akanunue vya asili. Sehemu yenyewe tuliyokwenda ni karibu na filling station ya Puma au kama unatokea “Samaki samaki” kuna barabara inakunja kulia kama unakwenda CCBRT, sasa kwenye ile kona kushoto kuna supermarket inaitwa “Shrijee”, sasa pembeni ya supermarket kuna jamaa wanauzaga vitu vya asili kama, picha, vinyago, kacha nknk.

Manuel aliingia na ndugu zake wakanunua picha, vinyago, kacha kuna vingine waliweka kwenye mfuko vingi. Wakati tunatoka pale akanambia tupitie pale Puma, akamwambia dada ajaze full tank, “nilivyosikia full tank, nilihisi moyo wangu kupasuka kwa furaha”, huyu Manuel anaroho nzuri sana, ni moja wa wazungu wenye roho nzuri sana.

Kwenye saa 5 tulikua tuko pale Ununio Beach Ofcoz walipapenda sana na ile mandhari walienjoy sana, mimi ndo nilikua kama director pale. Nakumbuka tulikwenda “Mahaba Beach” kule kulikua kuna samaki wengi sana wabichi, wavuvi ndo kama centre yao, bhs tulichoma sana samaki pale.

Tulitoka pale mchana tunaenda “Coco beach” tukala sana mihogo pale na mishikaki, usiku ilikua imefika muda unagonga kwenye moja kasoro, Manuel akasema twende tukapate dinner moja ya cafe nzuri pale Masaki afu tukamalize bata letu Samaki Samaki. “Wakati tunapita pale samaki samaki asubuhi Manuel alipaona akanambia badae tunakuja hapa”.

Nikawadrop wajiandae then tukaenda pale “The tribe” tukapata dinner hao tukamalizia pale Samaki samaki. Kama mnavyojua vibe la Samaki samaki tulienjoy sana lakini hawakukaa sana maana jumapili ndo walikua wanatakiwa kuondoka. Nikawarudisha Seacliff na mimi nikarudi kulala ili asubuhi mapema niwe pale kuwachukua kuwapeleka Airpot.

Naam asubuhi mapema saa 2 na madakika nilikua pale, wao walikua wanatakiwa “kuchek in “ pale Airpot 10:00 AM. Nikaingiza gari mle ndani Seacliff karibu na mlango wa kuingilia tukapark vitu hao safari ya Airpot, ndani ya nusu saa tulikua tumefika Termninal 3, hakukua na foleni kabisa.

Tulipiga picha za pamoja pale kama ukumbusho, wale wazungu walifurahi sana, nilipata nafasi ya kuongea na Sophie lakini sikuchukua namba nikaopotezea.

Nikawa escot mpaka ndani pale tunaongea sana na Manuel akanambia “You are my brother here in Tanzania, I’ll never stop calling you bro!”, alitoa noti 2 za Dolla 100 akanipa, nilimkatalia akanambia “bro hizi pesa sio zako nampa Junior, mfikishie”. Pale nikaishiwa pozi ikabidi nipokeee tukapeana hug na mimi nikatoka zangu kurudi parking ili niondoke.

Niseme kwamba kukutana kwangu na Manuel ilikua baraka sana kwani ndani ya week 2 niliingiza pesa nyingi sana na pia niliishi maisha mazuri sana. Nikapiga hesabu ndani ya siku ambazo nimefanya nao kazi nilikua nimeingiza $1,050 na bado alikua ananipa offa za lunch, dinner nknk.

Nikawaza hapa leo niende kwa Mama J nikamsalimie na Junior maana ilikua inakwenda mwezi wa 2 hatujaonana live zaidi ya video call tu. Nikasema hizi pesa nimepewa kwaajili ya junior acha nikanunue baadhi ya mazaga niwapelekee itakayobaki ntampa mama J.

Nikaingia Mlimani city nikanunua baadhi ya vitu nikaelekea boko kwenda kuiona familia yangu, ile nimeingia kwenye gari nikamkumbuka Angel, nikasema ngoja nimpigie maana alionesha anahamu sana ya kuongea na mimi, nikachukua simu ili nimpigie..

ITAENDELEA
ila hii stor yako inatia moyo sana katka mambo ya upambanaji
 
EPISODE 6
A TRUE STORY BY INSIDER MAN

Muda huo dada naye dizaini kama alikua yuko dunia nyingine ameshapagawa tayari, nikimtazama na ule uzuri na lile paja lilivyokua jeupe huku kwangu mnara unasoma 10G. Mara dada akaanza kutafuta nzipu ya jeans yangu kitendo cha kuweka mkono pale ni kama akili ilianza kurudi, nikasema hivi nafanya nini? Who’s this girl? palepale nikashuka kwenye gari nikanawa uso, nilikaa pale nje nikijifikiria maana kuna roho inanambia nimle nyingine inanambia nisimle, lakini roho ya kumla ilikua ikishinda.

Nikaingia kwenye gari kuchek map ni kama kidogo namaliza trip, dada alikua anakaa Shoppers kwa nyuma huku, dada akawa anaendelea kutaka kuingiza mkono kwenye jeans yangu nikawa namzuia, ndani ya muda mfupi tukawa tumefika, nika end trip akanipa pesa yangu. Dada hakutaka kushuka akawa ananambia tuondoke wote na yuko serious kabisa.

“Please bro! I’m horny”, dada ntakucheki kesho now nipo kazini, “bhs ntakulipa muda wako” huku akilalamika, ghafla geti lilifunguliwa alikua ni mlinzi , nikashusha kioo “kaka naona umepaki muda sana sikuelewi “ alivyomwona dada akanyamaza, “kaka unamjua huyu dada?”, ndio namjua anaishi humu, “bhasi msaidie aende ndani hayuko sawa” kabla hajashuka akanibusu shavuni “I have your number, ntakupigia”.

Nyie yule dem alikua mzuri sana kwakweli tuache utani “@riki boy atanisamehe kwakweli”
Na kwa mazingira ya pale nilompeleka nilijua dem ni mtoto wa kishua.

Sikuamini kama nimeushinda ule mtihani maana ulikua ni mgumu balaa yaani mpaka nafika home nilikua nikimwazia yule dada, huku roho ikinambia kesho mtafute.

Kutokana na lile tukio palepale baada ya kurudi home ilibidi niripoti kwa uber chap maana niliogopa dem nimemkazia asije akaniripoti vibaya kama “nimemharras”, Uber wako serious sana maana hawachelewi kukutia bann.

Unajua madereva wengi wa Uber hapa ndo wanakofeli yaani ukiendekeza mapenzi na kazi ni kama unajichimbia kaburi mwenyewe. Hakuna kazi ngumu kama ya uber yaani ni kunavishawishi vingi sana haya matukio ya kutakwa kimapenzi ni mengi mno, hawa wanawake ambao hawajitambui ni wengi mno yaani kama huna self control utaishia kuwala tu. Na kwa upumbavu unalala nao humohumo kwenye gari unazidi kujiweke nuski, balaa na mikosi.

Hakuna watu wenye siri kama maderva wa Uber kama hapa Dsm usiku kuna mambo mengi ya siri na aibu yanafanyika kila siku. Usiku ndo muda ambao mashoga yanatoka ni mengi sana hapa Dar na usafiri wao ni uber ni masumbufu sana haya mawatu. Kuna illegals nyingi zinafanyika kwenye huu mkoa bado uzinifu ni hatari, kama weekend huwa tunapishana kwenye Apartments tunawashusha na kuwabeba dada zetu ni hatari sana.

“Ilifika stage nikasema hii kazi licha ya kupata pesa ila ni kijishushia hadhi mfano unabeba mishoga inaanza kukutongoza, hawa watu sijawai kuwakubali lakni kutokana na hii kazi lazima ukutane nao, na wanasumbua sana, ni waongeaji mpaka wanakera”.

Mimi binafsi before ya kwenda mzigoni nilikua nasali kwanza ile asubuhi ndo naondoka, hata mambo mengi nilikua nayashinda sababu ya Mungu na sio akili zangu, ni ngumu sana kukwepa mishale yote pia.

*******

Asubuhi niliamshwa na simu ya Mama junior kama kawaida yake alikua akilalamika kwanini sijaenda jana na niliahidi ntakwenda, ikabidi nimpe sababu ili aelewe

Mama J: Toka nitoke hapo home sikuhizi sikuelewi kabisa ni umebadilika sana Baba J, hautujali kabisa, sasa kesho mimi narudi nyumbani na mtoto maana nikiendelea kukuacha nitakuta umeweka mwanamke humo ndani, hapana bora nirudi tu.

Mimi: Hapana mke wangu huko unafika mbali sana na plan mkesha huu wa mwaka mpya tuwe hapo home wote nina mpango wa kununua mbuzi kwaajili ya mkesha. Baada ya mwakampya nitakuja kukuchukua, wewe endelea kutafuta dada wa kukusaidia kazi.

“mama J ni mtu ambaye anakuaga na hasira sana ila ukishamalizana naye akaona sababu ina mantiki hanaga shida”.

Hii siku ilikua jumapili boxing day hapo muda unasoma saa5 asubuhi nilikua nimechoka sana na ile mikiki ya jana, nikasema hapa acha nipumzike mchana nianze kazi. Soon Maggy akaanza kupiga simu, nikapokea “Bossy wangu naomba leo kama unaweza uje hapa home utupeleke Tabata Segerea, please”. Sikutaka kumkatalia ukitegemea Maggy kashakua tayari familia na mteja wangu.

Palepale nikasema acha nipeleke gari car wash ikapigwe soap, gari mimi nilikua napenda kuoshea pale Juliana pub, wale jamaa wa pale ni washikaji zangu sana.

Kuna jamaa pale anaitwa “Kelvin” ndo mtu ambaye nilikua napenda sana kumpa gari aoshe, bhasi nikaona Kelvi anakuja kwangu akanmbia kaka ulidondosha simu huku anikabidhi mkononi, nilikua nashangaa simu!!??, nikajua lazima kuna mteja aliidondosha, kelvin akanimbia ilikua chini ya kiti cha pembeni kwa dereva upande wa chini karibu na mlango.

Simu yenyewe ilikua ni iphone 13 Pro Max latest kabisaa, wakati nikiendelea kufikiria itakua ya nani nikasema niiwashe lakini ilikua haina chaji. Nikaiweka mfukoni nikaingia zangu ndani kula kitimoto “Juliana wanakitimoto kitamu sana”.

Nikarudi home ili nianze kujiandaa ili nikameet na Maggy kule Mikocheni, nikaichomeka ile simu kwenye chaji mimi nikaingia kuoga, sasa wakati niko bath Maggy alikua ameshaanza kupiga simu kwa kasi na 14:00 ilikua inabidi niwe nimefika eneo la tukio.

Kutokana na ile haraka mimi nikaisahau ile simu home, nikafika kwa Maggy mapema sana na nilikua nimependeza nimetupia jeans, raba yangu ya nike, shati ya jeans na cap [emoji3449], sikutoka kizembe.

Karibu ndani bossy wangu ilikua sauti ya Maggy huku akitabasamu “umependeza” nikamwambia sitaki kukutia aibu huko unakokwenda, kweli hata mimi naona sio kwa kuwaka huko.

Maggy alikua na best zake wawili hao tukaelekea Tabata tulitumia saa 2 kufika eneo la tukio sababu ile Mandela Road ilikua na foleni sana. Tukio lenyewe ilikua ni “BABY SHOWER” kama mnavyojua mambo ya wanawake matukio mengi, nikajisemea kweli “Mama Junior Bora haya mambo alikua hana time nayo”.

Kutokana na wageni wengi walikua ni wanawake pale japo na baadhi ya wanaume walikuwepo, hivyo niliamua kutafuta sehem niende kupoteza muda. Sasa ile natoka Maggy akanifata akanambia usiondoke please, nimewaambia wewe ni ndugu yangu hivyo ukiondoka haitakua vizuri.

Nilibaki kwenye hilo tukio lakini sikuwa na mzuka nalo wala nini maana niliona hayo ni mambo ya wanawake sana.

Event ilikwenda mpaka mida ya saa 2 usiku ndo ikaisha hivyo tukaanza kurudi, wakati tuko njian wakawa wanadiscus jamani na hili vibe tunakwenda malizia wapi??

“Kidimbwi..? aahh pale sipapendi nyie…, shoga pale pana watu wengi sana, sasa twende wapi?? Maana wewe kila sehem hutaki….” Walikua wanajadiliana mwisho wa siku wakakubaliana waende Samaki samaki, Mlimani city.

Kuna dada akaniuliza “eti kaka Samaki samak pazuri??”, ndio kwa jumapili pale Mlimani pana vibe na leo sikukuu bado kitawaka sana.

Nikawarudisha mpaka Mikocheni ilikua ishafika saa3 muda huo, wakabadilika chap aisee walikua wamewaka sana hapo nikagundua kumbe Maggy naye ni pini sana, tukaanza safari ya Mlimani city. Nikawadrop pale Maggy akanambia nijoin nao maana mimi nilitaka kusepa, nikaamua kuwajoin.

Tulikaa pale mpaka saa7 usiku nikamwambia Maggy kesho kazin vipi? akanmbia kesho haendi wako off. Muda ule nikawarudisha Maggy na best yake pale kwake best yake mmoja ambaye alikua anakaa Kimara ali request usafiri wa kumpeleka kule kwake.

Baada ya kuwadrop pale tulikua tukipiga story na Maggy baada ya best ake kutangulia ndani, akanambia jumla itakua kiasi gani? nikamwambia leo nakupa offa angalia pesa ambayo haitakuumiza wala kuniumiza mimi, akanipa 70k, mimi nikarudi zangu kulala.

Wakati nimerudi home niliangalia ile simu kuangalia kama kuna watu walipiga kama nilivyohisi nitakuta watu wamepiga sana. Nilikua siwezi kufanya chochote maana ilikua na password.

Asubuhi niliamka mapema sana kwenye saa1 asubuhi ile simu ilianza kuita nikapokea chap.

Anonymous: Mambo Prisca(code), mbona hupokei simu zangu toka jana mchana?

Mimi: Kaka mambo vipi, unamjua mwenye hii simu?

Anonymous: Ndio kwani wewe ni nani? na inekuwaje unapokea simu zake??

Mimi: Bro tulia kwanza, mimi ni dereva Uber jana nimepakia wateja wengi sana kama unavyojua ilikua ni sikukuu, jana nimeiona simu saa6 baada ya kuipeleka car wash ilikua iko off, baada ya kurudi nikaisahau kwenye chaji mimi nikawa nimekwenda mzigoni, kama unamjua huyu mtu naomba anitafute nimpe simu yake.

Anonymous: Ok, kuna best yake namjua ngoja nimpigie simu, nitumie na namba yako.

Mimi: No problem, 0765*******

Nikatoka hapo chap kuelekea kumchukua Mama wawili nimpeleke kazini, this time mama wawili alikua peke yake. Vipi mke wangu yuko wapi leo?,,Aah hizi week 2 zilizobaki nimeona apate likizo, sikutaka afunge shule mapema ili apate mafunzo ya computer.

Baada yakufika pale Posta na kumdrop mama wawili haikuchukua muda simu ikaanza kuita ile iphone 13, nikapokea ile simu “Kaka mimi ni Prisca ndo mwenye hii simu ulinichukua pale Maison ukanileta mpaka kule Shoppers,

“Sawa dada nimekukumbuka sasa simu yako ntakupaje..?”

“Mimi niko home tu, niletee ntakulipa pesa yako”

Ok haina shida, nipe namba ya kuwasiliana na wewe.

**********

Mimi niliendelea na majukumu yangu ya kazi kama kawaida tena hii siku nilikua na bahati sana. Nilipiga kazi mpaka jioni nikampigia simu yule dada kwamba niko njian nampelekea simu yake, akaniambia ukifika wewe piga honi nitatoka.

Kwenye saa1 jion nilikua nimefika pale akatoka,

Prisca: Kaka mambo!

Mimi: Safi mzima? za toka siku ile!

Prisca: Ukaniacha na hisia zangu, wewe ulikua wangu tu mpaka nikasahau simu jinsi nilivyokua nimepagawa na wewe.

Mimi: Sema uliacha kwa makusudi ili nikutafute, huna lolote.

Prisca: Karibu ndani bhasi,

Mimi: Huko ndani mimi siingii.

Prisca: Ok ngoja niingie kwenye gari!

Mimi: Simu yako ni aina gani?

Prisca: Kwa madaha, Iphone 13 Pro Max, colour gold, na nimeweka wallpaper yangu.

Mimi: Nitajie password, huku naitoa simu kwenye droo

Prisca: 234567

Mimi: kweli dada simu yako, nikamkabidhi

Prisca: Kaka ahsante sana yaani sijui nikupe zawadi gani, maana nilikua najua nimeipoteza kule Maison yaani idea itakua nimesahau kwako sikua nayo kabisa. Nilijua nimepoteza simu yangu, una roho nzuri sana.

Mimi: Usijali hii ni vitu vya kawaida!, mimi nataka kuondoka.

Prisca: Nisubiri nakuja, huku akiingia ndani.

“Prisca aliingia ndani nikawa namsubiri pale nje getini, baada ya dk5 akawa amerudi kashika kibahasha.”

Prisca: Kaka hii mimi ndo Shukran yangu huku akinikabidhi ile bahasha ndogo na hii ni nauli yako alitoa cash 20,000.

Mimi: Ahsante mrembo ila sikuhitaji shukrani yako!, sasa ilikuaje mpaka ukalewa vile siku nyingine utabakwa, shukuru Mungu ulikutana na mimi mstaarabu.

Prisca: hivi ulinichukulia mimi kama malaya hivi?

Mimi: Ndiyo au hapana ila kwa Mwanaume anayejitambua hawezi kusex na mwanamke ambaye hajitambui kama ulivyokua wewe jana, pale ningekua nakubaka.

Prisca: Ni wanaume wachache sana wenye kariba kama yako ambao wanaweza kujizuia, natamani sana kupata mwanaume dizaini yako.

Mimi: Biblia inasema utapata wa kuendana nae kama wewe ni mlevi utapata hivyohivyo mlevi mwenzio, sio unataka mwanaume anayetambua afu wewe hujitambui, thubutu!

Prisca: Sawa bhana naona unanikandia, jana nimelewa kwa stress tu lakni mimi siko hivyo kaka, I swear

Mimi: Ina maana jana angekua mtu mwingine ungeliwa sio kwa zile ny*ge.

Prisca: Sijui hata niseme nini, ukweli wakati na request nikaona ID yako nilitokea kukuelewa na nilikua nafeel niko sehem salama.

Mimi: Wewe jitetee kama ni tabia zako ntakuotea tu!

Prisca: kweli, so bado upo kazini au unakwenda kwako?

Mimi: Vipi unataka tuondoke wote?

Prisca: Muda umekwenda mzee anarudi sio muda, wewe niambie nikutafute lini?

Mimi: Muda wowote utakaohisi mimi niko free!

Baada ya kuona story haziishi ndokama zinazidi kupamba moto nikamwambia mimi nasepa, tutawasiliana. Ofcourse Prisca alitokea kunielewa na kile kitendo cha kutokumla inaonekana kilimpa maswali sana, hata yeye alikua haamini kama nilimwacha salama.

Nilivyorudi home kucheki kile kibahasha nikakuta dada aliweka 300,000/= ya shukran. Ilikua ni saa 3 kasoro tayari simu ikaanza kuita kupokea alikua ni Prisca akanishukuru sana akampa simu na dada yake niongee naye. Dada yake anashukuru pia “kaka una roho nzuri afu inaonekana huna tamaa, maana kwa maelezo yake jana Prisca hakutegemea kama ingekua kwako, tutakutafuta siku tufahamiane nakama na kazi ntakua nakutafuta”, nikamwambia haina shida dada karibu.

******
Ilikua alhmisi tukiwa week ya kumalizia mwaka 2021, nikiwa mzigoni kama kawaida yangu simu ikaanza kuita ilikua namba ngeni, nikaipokea ile simu kumbe alikua ni mchepuko wa mzee so alikua ananiambia mzee anasema hakupati kwenye whatsapp yeye yuko Egypt, nimtafute kupitia whatsapp.

Baada ya kuanza kazi niliamua kusajili namba nyingine kwaajili ya mambo ya Uber sikupenda kuchanganya mafile, wateja wangu wote nilikua nawapa namba ya voda.

Palepale nika download “Whatsapp business” nikamtext mzee, ilipita 1hr akaja kunicheki, akaniambia yuko safari anarudi ijumaa so nikamchukue Airpot afu nitampeleka Bagamoyo na mchepuko wake na watarudi jumapili.

Nikawa na mawazo mzee anakuja ijumaa na sijui ataingia muda gani na pia itakua 31/12 nlishamwambia wife lazima niende kwenye mkesha kwao. This time mama J hawezi nielewa kabisa na mzee kumkatalia siwezi so hapo nilikua naomba sana Mungu mzee awai kufika.

Ile ijumaa asubuhi mzee akanitext kwamba mchana atakua amewasili airpot niwe ontime pale, aisee nilifurahi sana kusikia mzee ataingia mapema, nikaenda kukutana na jamaa ambaye nafahamiana naye pale tegeta nyuki ni anauza bucha, nilimwagiza dume la mbuzi lenye afya lije limeandaliwa kabisa. Nikamwagiza boda apeleke ukweni.

Wakati tunachat na mzee alikua anauliza kama na mimi ntabaki huko Bagamoyo au laah, nikamwambia mzee mimi siwezi kubaki huko ntawapeleka then ntakuja kuwafata siwezi kulala huko usiku 2 ntakupa sana cost. Nikamweleza mzee kazi jinsi ilivyo tukakubaliana 300,000/=. Huyu mzee tumuite (Mzee Pama), alinipa sana maisha huyu mzee kwakweli, alikua na roho nzuri sana.

Nikawasiliana na mchepuko wake nikamwuliza tunakwenda wote kumpokea mzee au niende afu yeye nimpitie Posta?, akasema nimpitie Posta tunavyorudi itapendeza.

Mzee aliwasili 11 jioni nikampokea safari ilikua kwenda Posta kumpick dada then twende Bagamoyo. Ilikua kama bahati ile tunafika pale kivukoni na Panton ilikua ndo inashusha, tukamchukua dada hao Bagamoyo.

Tuliingia Bagamoyo kwenye saa 2 kasoro kuna Hotel niliwapeleka ipo karibu na Beach pazuri sana pale sipakumbuki jina. Mzee akanipa 100,000 akanambia nenda kale sikukuu kijana wangu hakikisha unakuja mchana mapema kutuchukua, ntakupigia simu pia. Nilimshukuru sana mzee nikageuka kurudi Boko kwa wife maana hapo alikua anapiga simu mpaka bhasi.

Nilitumia nusu saa tu kufika pale Boko nilikuta mbuzi ishaanza chomwa pale watu walikua kama wote nazungumzia dada zake, nk tulikesha pale kuupokea mwaka mpya. Kiukweli mwakampya 2022 niliupokea vizuri sana mambo yalikua mazuri sana siku ile.

Nilitoka pale saa 7 nikaenda moja kwa moja home kulala, nikaplan asubuhi niende church then niingie mzigoni “leo lazima nikeshe”. Wakati nimeingia home tu Prisca akanipigia simu eti ananiwishi “Happy new year” nikamwambia ahsante, akaendelea Insider kesho tuonane bhas if possible nitakua na dada yangu anataka akuone…, “mmh dada yako umemwambia nini wewe mbona spidi sana?”…. Sikia mimi kesho ntakua busy sana siwezi kukupa ahadi yoyote kwa sasa tutacheki siku nyingine itakua vizuri zaidi.

*********

Ile jumamosi nilianza mzigo saa6 mchna baada ya kutoka church nilipiga sana kazi hii siku maana request zilikua zinaita tu afu sasa zilikua zile trip ndefu na hizi trip zinakuaga na hela sana.Hizi trip ukipiga zako 4 unakuta ubao unasoma 100k tayari.

Nilipiga kazi mpaka inafika saa 2 usiku nilikua nishaingiza laki na point kadhaa, bhasi nilikua pale karibu na 5N pembeni kuna jamaa huwa anauza soup ya pweza ni mtaalam sana. Nilikua napata soup yangu pale mdogo mdogo hapo nilikua nimezima App sikutaka usumbufu kabisa pia nilikua navuta pumzi.

Nilitumia 1hr kupumzika na kujiweka fiti kwenye saa3 tayari nilikua nimepata request tayari ya kwenda Madale huko, mimi nilikua sichagui request sehem yoyote kambi kama mteja anaingia barabara mbaya namkodia bodaboda impelekee.

Nilimpeleka mteja Madale kwa bashasha zote siku nzma nilikua nasikiliza album ya The weeknd “After hours ”, gari safi inanukia vzr na kale ka mziki kwa mbali ilikua burudani sana.

Nilimmdrop mteja pale wakati nageuza gari naitafuta barabara kuu, nikapata request nikampgia mteja “Kaka njoo haraka niko Montana hapa” nakumbuka mteja alikua anakwenda Ilala, pale Ilala nikapata request nyingine ya kwenda Slip way Masaki.

Pale Slip way nilisubiri subiri kama nusu saa nikapata request ya kwenda Mbagala- Rangi tatu, lakini nikawa nawaza niende au laah, nikaamua kwenda, nikamwambia mteja nakuja, “kaka siamini kabisa maana Bolt hawataki kwenda kule”. Yule alikua ni mama mpemba alikua mwongeaji sana ile trip ilikua ni stori sana, nilimdrop mteja palepale Rangi 3.

Pale mbagala nilikaa karibu nusu saa lakini sikupata request, nikachoma wese mpaka zakhiem pale nikashuka kwenye gari ili nipunge hewa. Nilikaa pale kama nusu saa nikapata mteja alikua anakwenda Kigamboni kibada nilitaka nigome lakini nikasema acha niende, nikamdrop mteja, kama zali ile namshusha mteja napata request ya kwenda Masaki “Havoc pale Barometer”, nilifurahi sana.

“Kaka fata ramani nachelewa toll fee pale darajani ntalipia” ilisikika sauti nzuri ya mrembo, nilifika dada alikua ananisubiri kama alikua na haraka sana.

Nilimdrop pale mteja, kucheki ubao ulikua ushafika 200k tayari, hii siku nikasema hivi kama ningeanza asubuhi si ningekua niko parefu sana. Nikaamua kwenda kupark gari pale Masaki mwisho zinakogeuzia daladala. Pale mara nyingi huwa navizia requests za maeneo ya pale, coral beach, na seacliff “kuna jamaa alinipaga hii trick kwamba niwe natega pale ni pazuri, unachomoka haraka”.

Muda huo ilikua saa 9 tayari wakati naenda kuchili maeneo yale, ninakuta wahuni wa 2 wa uber washatia kambi tayari, zikaanza story kila mtu anaonesha ubao wake, kila mtu ubao ulikua uko vizuri siku hiyo. Nilikaa pale jamaa mmoja akatoka alipata request tukabaki na jamaa kidogo jamaa nae akatoka nikabaki mimi pale peke yangu.

Nikaingia kwenye gari baada ya kuona niko peke yabgu, iliku sa10 kasoro tayari muda huo nakumbuka, nikasema acha nikalale tu nipumzike zangu tu kwa leo inatosha sana. Nikaamua kuset destination ya Mbezi beach home, baada ya dk 5 hivi nilipata request mteja anakwenda mwenge lakini alikua mbali nikaamua potezea.

Sasa baada ya dk 10 nikaona kama sipati request nikaamua kucancel tu nikomae na za kawaida kama ntabahatisha inayokwenda huko sawa. Haikuchukua dk 2 nikapata request mteja alikua “Marina Towers” apartments, hapo tayari nime accept ile request lakini nikawa nawaza niende au nipige chini??, ghafla text ikaingia “Niko Marina Towers, ukifika nijulishe”. Nikawaza nimeshakaa sana pale acha niende tu, nikafika pale Marina Towers hii ndo ilikua siku ya kwanza naingia kwenye hizi apartments.

Baada ya kufika pale mlinzi akafungua geti “Uber eeh, ingia paki pale” hawa walinzi bwana wakionaga IST tu wanajua uber. Nikaingia ndani nikamtext “Niko parking”….. nikasubir mpaka dk 10 kimya mtu hatokei, kutokana na kuwa na usingizi nikaamua kuegemea kiti palepale nikapitiwa na usingizi.

Nilishtuka baada ya kuona mtu anahangaika kufungua mlango maana ulikua locked, nika unlock akaingia “kaka samahani nimekuweka sana” nikamwambia si umeona karibu dk 40 nakusubiri, “kaka usijali ntakurefund”, wakati tunatoka getini “kaka si umeona wapi tunakwenda?” ndio si Sinza??… “Mmhh mmh wewe ni kijitonyama karibu na Grand villa hotel”… Ok nishakusoma dada.

“Kaka sorry can I sleep?”, dada alikua anauliza, nikamwambia dada hii gari ya abiria wanapanda watu wengi kama utakua comfortable unaweza lala ni wewe tu. Muda huu nilikua simzingatii kabisa huyu dada maana nilikua na usingizi si unajua ile ukiwa unadrive afu unahisi usingizi.

Nilifika mpaka kijitonyama nikamdrop dada, before hajashuka akaniambia kaka ntakupigia simu ili tuongee kuhusu biashara, naomba namba yako, nikamwomba simu nikachora 0765******, ahsante uwe na kazi njema.

Sasa ile ametoka anafungua geti sindo namwona dada vizuri aisee moyo ulipiga “paaahhh”, aisee mbona hii pisi kali sana ni huyu dada ambaye nimempakia??, nilikua nawaza pale huku nikishuhudia dada akimalizia kuingia ndani.

Ndugu zangu yule dada alikua ni mzuri sana tuache masikhara kwakweli japo ilikua usiku lakini nilisema sijawai pakia dada mzuri kama huyu….

Tutaendelea….,

Huyu dada alikua ni nani??, Vipi kuhusu Prisca?, tukutane Jumanne.
295
 
Madereva wa Uber mnazingua sana, una request mtu ana accept unaamua kumpigia simu anakwmbia huko mimi siendi, sasa uli accept ili iweje?

Leo tulikua posta tukaamua kurequest kwenda Chamanzi kuna dada yangu amejenga kule, sasa lengo letu ilikua twende na kurudi. Kila uber tunaye request anagoma ndo mmoja akaja tukaenda naye na kurudi.

Kama umeamua kuwa Uber ukianza kuchagua request nakwambia utapata tabu sana. Ukianza kutopata request mnaanza makasiriko kumbe tatizo ni wewe.

Uber wanavyokupa request afu unazikataa unazidi kujiweka kwenye nafasi mbaya, kama unakataa request bhasi uwe na sababu maalumu mfano labda usiku umepata request mteja anakwenda Mbagala Rangi 3 ndani ndani huko sasa hutaki kwenda huko.

Unaweza kucancel ile request afu ukaandika “Nimewasiliana na mteja, nikamwambia nitamuacha Rangi 3 stand sababu ya usalama wangu, lakini amegoma”. Hapo hata Uber watakuelewa sio una cancel afu unanyamaza tu itawacost sana.

Wengi mnataka request za kwenda Posta, Masaki, Mikocheni, Mbezi Beach, Kariakoo, Mliman city, Sinza nknk.

Jitahidi sana uwe na rating za juu pamoja na recommendation nzuri kutoka kwa wateja kitakufanya upate request nyingi.
 
Madereva wa Uber mnazingua sana, una request mtu ana accept unaamua kumpigia simu anakwmbia huko mimi siendi, sasa uli accept ili iweje?

Leo tulikua posta tukaamua kurequest kwenda Chamanzi kuna dada yangu amejenga kule, sasa lengo letu ilikua twende na kurudi. Kila uber tunaye request anagoma ndo mmoja akaja tukaenda naye na kurudi.

Kama umeamua kuwa Uber ukianza kuchagua request nakwambia utapata tabu sana. Ukianza kutopata request mnaanza makasiriko kumbe tatizo ni wewe.

Uber wanavyokupa request afu unazikataa unazidi kujiweka kwenye nafasi mbaya, kama unakataa request bhasi uwe na sababu maalumu mfano labda usiku umepata request mteja anakwenda Mbagala Rangi 3 ndani ndani huko sasa hutaki kwenda huko.

Unaweza kucancel ile request afu ukaandika “Nimewasiliana na mteja, nikamwambia nitamuacha Rangi 3 stand sababu ya usalama wangu, lakini amegoma”. Hapo hata Uber watakuelewa sio una cancel afu unanyamaza tu itawacost sana.

Wengi mnataka request za kwenda Posta, Masaki, Mikocheni, Mbezi Beach, Kariakoo, Mliman city, Sinza nknk.

Jitahidi sana uwe na rating za juu pamoja na recommendation nzuri kutoka kwa wateja kitakufanya upate request nyingi.
Tumekusoma
 
Madereva wa Uber mnazingua sana, una request mtu ana accept unaamua kumpigia simu anakwmbia huko mimi siendi, sasa uli accept ili iweje?

Leo tulikua posta tukaamua kurequest kwenda Chamanzi kuna dada yangu amejenga kule, sasa lengo letu ilikua twende na kurudi. Kila uber tunaye request anagoma ndo mmoja akaja tukaenda naye na kurudi.

Kama umeamua kuwa Uber ukianza kuchagua request nakwambia utapata tabu sana. Ukianza kutopata request mnaanza makasiriko kumbe tatizo ni wewe.

Uber wanavyokupa request afu unazikataa unazidi kujiweka kwenye nafasi mbaya, kama unakataa request bhasi uwe na sababu maalumu mfano labda usiku umepata request mteja anakwenda Mbagala Rangi 3 ndani ndani huko sasa hutaki kwenda huko.

Unaweza kucancel ile request afu ukaandika “Nimewasiliana na mteja, nikamwambia nitamuacha Rangi 3 stand sababu ya usalama wangu, lakini amegoma”. Hapo hata Uber watakuelewa sio una cancel afu unanyamaza tu itawacost sana.

Wengi mnataka request za kwenda Posta, Masaki, Mikocheni, Mbezi Beach, Kariakoo, Mliman city, Sinza nknk.

Jitahidi sana uwe na rating za juu pamoja na recommendation nzuri kutoka kwa wateja kitakufanya upate request nyingi.
Unatumia Muda vibaya Sana huo muda unatoa elimu ungesha maliza episode inayofata au unataka Hadi tukupopoe ndio uandike
 
EPISODE 8
A TRUE STORY BY INSIDER MAN’

Nilirudi nyumbani huku barabara nzima nikiwa nawaza mambo mawili kichwani. Jambo la kwanza nilikua nawaza Iryn atakua anafanya kazi gani?, nilikua bado najiuliza kazi gani hii ya usiku??, au anafanya illegal?, …mmh hapana yule dada ni mrembo, pia kaniambia ana saloon sidhani kama anafanya hizi dili.

“….Anyway mimi naangalia pesa mambo mengine mimi hayanihusu kabisa, atajua yeye na maisha yake bwana, as long I get paid no problem”

Lakini pia nilikua nafuraha ya kufahamiana na mrembo kama yule niliamini pia ni bahati na nyota.

Upande mwingine nilikua nawaza jinsi ya kudeal na mama Junior maana sikutaka kumuweka wazi juu ya hili suala.

Nilikua bado najiuliza muda ule….

“Hivi kama nitarudi usiku bila kuwa na reason maalum inayoeleweka ,sindo chanzo cha ugomvi na makelele?, au nimwambie tu kieleweke??”. Lakini bado nilikua nakosa maamuzi kwa upande wa Mama J.

Wakati muda ule nikiwa nawaza simu ilianza kuita kucheki naona Dullah….Nikapokea.

“Dullah vipi ndugu yangu hatuonani”

“Tuonane wapi wakati ushaanza kuwa busy na watoto wazuri?”

Nikampa story Dullah jinsi ambavyo nimekutana na Iryn na mpaka kunipa kazi. Dullah akanambia “naona ushaanza kupagawa mapema hivi ndugu yangu hio ni intro tu”

Nikakatisha maongezi na Dullah baada ya kuona mama anapiga simu:

“Mwanangu hujambo?, hivi mama Junior karudi nyumbani?”

“Mama amerudi, haujaongea na mkamwana wako?”

“Sijaongea naye na muda kweli”

“Mhh mama yakweli hayo, maana naona kama haiwezekani”

“Kama amerudi nimefurahi msalimie Mjukuu wangu” (Mama yangu na Junior wamefanana sana, humwambii kitu kuhusu mjuu wake)

Ipo hivi mama yangu na mama J ni marafiki sana, hata mama alivyokua ananiuliza kuhusu mama J kurudi home nilikua najua lazima anafahamu ila ananizunguka tu.

Sielewagi mama J alitumia mbinu gani kuwa close sana mama yangu yaani ni wanapatana balaa, sio kwa upande wa mama tu hata dada yangu pia. Yaani anaweza kuwa na kosa yeye ila mimi ndo nikaonekana mkorofi.

*******

Kesho yake niliwai kuamka ili niwai kumchukua Mama wawili na mwanae, baada ya kumdrop mwanae nikampitia Maggy hao Posta. Japo kuamka asubuhi sometimes ilikua inakera sana unakua kama mtumwa. Lakini ukicheki una mkataba wa kazi na watu huwezi kuleta ufedhuli inabidi uwe mpole tu.

Upande mwingine yule dada wa kule Masaki- Olive alikua kanicheki kwamba kama nitaenda masaki tuonane ili tukubaliane bei, jumatatu nianze kazi ya kuwachukua watoto.

Nikaenda Kariakoo kuchukua Rim za gari na tairi mpya ili kubadilisha muonekano wa gari yangu. Baada ya kutoka hapo nikaelekea “@thewheel” Mikocheni, tukabadilisha tairi na Rim, aisee gari ikawa kali balaa, pale garage kila mtu akawa anaisifia IST yangu (nitawatumia picha chini).

Nikatoka hapo kuelekea Masaki kuonana na dada, nilikua pale saa 9 mchana, tukaongea pale, watoto walikua watatu (3) ambapo wakwanza nitakua namuacha pale Mikocheni karibu na Clouds media, hawa wawili walikua wanakaa Kunduchi- Bahari Beach ila maeneo tofauti.

Tukakubaliana kwa watoto wa Kunduchi atanipa 13,000 kwa kichwa na yule wa mikocheni atanipa 7,000. Japo baada ya week 2 aliongezeka mtoto 1 mwingine alikua anakaa kawe jumla nikawa na watoto 4, ila huyu mtoto wa kawe sikutaka kumtoza niliamua kutoa shukran kwa dada.

Hapo nilikua na uhakika wa kuingiza 165,000/= kwa week na tulikubaliana malipo yawe yanafanyika kwa week.

Baada ya deal kuwa done nikafurahi sana hapo tayari nilikua na uhakika wa kuingiza zaidi ya 2,000,000/= kwa mwezi.

Nilijiona na bahati sana kwa muda mfupi kupata wateja wa uhakika, hapo nilikua na uhakika hata nisipowasha App pesa itaingia tu.

******

Ijumaa ndo siku ambayo nilikua na miadi na Iryn kama tulivyokubaliana, niliamka asubuhi mapema sana 06:00. Kwa siku za weekend nilikua napenda sana kuvaa buti au sando, tshirt na cap kichwani, nikivaa buti/raba bhasi lazima nitembee na sando kwenye buti.

Nikapata trip ya kwenda Pwani “Marian boys school” kuna mzee alikua anampeleka mtoto wake shule.

Nikampigia simu chap

MZEE: “Kijana wangu hujambo nataka kumpeleka kijana wangu Marian schools pwani”

MIMI: “Mzee unakwenda na kurudi?”

MZEE : “Hapana kijana kuna kikao pia nitakuweka sana”

MIMI : “Mzee mimi sina shida kama utanilipa muda wangu”

MZEE : “si nitatumia gharama kubwa sana, maana sijui kikao kitachukua muda gani”

MIMI: “Sawa mzee wangu ila sasa kama unataka twende huko itabidi tusitumiee App, tukubaliane bei maana ukishaingia Pwani Uber haisomi, mpaka nirudi tena Dsm ndo nitaweza pata request. Na uhakika wa request mpaka nirudi Bunju atlist, kama upo tayari nikupeleke”

MZEE: “Sawa kijana wangu nimekuelewa unataka kiasi gani?”

MIMI: “Mzee kwenye App ilikua inaonyesha kiasi gani?”

MZEE: “30,000/=“

MIMI: “Bhasi utanipa 50,000”

MZEE: “Nitakupa 45,000 kijana wangu, uje haraka tuondoke”

MIMI: “Sawa mzee nakuja”

Mzee hakuwa mbali sana na mimi nakoishi yeye alikua anakaa nyuma ya Hospital ya Massana.

Unajua hawa watu ambao walikua wanaishi ushuani nilikua siwachekei kabisa, nilikua najua kabisa wanahela. Huwezi mpeleka mtoto Marian kama hauna hela.

Nikawapeleka mpaka Marian school, mzee akachukua namba yangu mimi nikageuka kurudi Dsm. Nilichoma wese, sasa wakati nakaribia “Bunju mwisho” nikapata request ya kwenda Airport.

Kufika pale nashangaa kumbe alikua ni kigogo wa serikalini.(Naibu waziri wa Wizara X)

“Mzee shikamoo hata nyie huwa mna request kumbe?”

“Kijana unashangaa tena, huu ni usafiri wangu sana”

“Nilijua unapiga simu, dereva anakuja chap kukubeba”

“Dereva naye ni binadamu leo ni weekend pia na haraka acha apumzike najali pia maisha yao binafsi”

“Sawa mzee hata hivyo tunashukuru hata mimi hapa nimepata ridhiki”

“Ni kweli ndo kutegemeana huku, sasa tutapitia pale TFNC kumchukua mke wangu afu tutaelekea Airport”

Tukatoka pale huku tukipiga story na yule Kigogo, akawa anauliza hali ya Maisha huku anamsifia Mama Samia na mimi namuunga mkono. Na mimi palepale sikutaka kuwa mzembe nikaanza kutengeneza connection maana nilisema hizi chance zinatokea mara chache sana.

Tulifika pale TFNC hizi ofisi zipo kule chini Ocean Road, bhasi tukafika pale tukasubiri kama dk 10 mke wake akawa amekuja hao tukaelekea Airport.

Kigogo alinisifia sana gari yangu kuwa safi, akanambia nimepanda Uber nyingi ila hii ni kiboko sana, akaniahidi atakua ananitumia. (Ila hakuwai nitafuta na alipigwa chini kwnye nafasi yake)

Niliwadrop pale Airpot Terminal 2, palepale kuna ndege ilikua inashuka nikapata request ya kwenda Mikocheni.

Baada ya kupiga kazi mpaka sa12 jioni nikasema acha nipumzike ofcoz ubao ulikua unasoma vizuri sana, kwenye ubao ulikua unasoma 95,000 ukijumlisha na ile 45,000 ya Asubuhi nakua na 150,000 tayari. Wakati nimemshusha yule kigogo pale Airport aliniongezea 10,000 ya ahsante nikasema hii nitaoshea gari badae.

“Ipo hivi mimi pesa ya kuoshea gari huwa sitoi kwenye faida zangu bali huwa natoa kwenye zile ahsante ambazo mteja ananipa, kuna wateja wako poa sana akifurahia huduma utakuta anakuachia chenji, sasa hizi nilikuaga nazitunza kwenye droo”

Nikapeleka gari carwash lipigwe usafi maana likikua lishachafuka tayari, nilitaka gari ing’ae kabla ya kumiti na Iryn. Nilitaka akute gari ikiwa safi.

Muda huo ilikua sa12 na madakika tayari, Iryn akanipigia simu kunikumbusha niwe on-time, nikamwuuliza timetable ikoje tunakwenda wapi na wapi?.

“Leo tutakwenda Ledger Plaza na Serena Hotel”, Iryn alijibu hivo.

Muda huo nilikua zangu pale Texas nimechili nimepumzika huku napiga story na wahuni. Texas nilipazoea sababu Uncle wangu alikua anapenda sana kuoshea gari pale.

********

Hatimae muda ulifika, ontime nilikua pale kumchukua dada kama kawaida alikua kawaka sana asee, niliishia kumtamani tu. Aliweka bag lake kwa nyuma ya siti “duffel bag” akaingia kwenye gari akakaa siti ya mbele, tukasalimiana hao tukaanza safari ya kwenda Bahari Beach, Ledger plaza Hotel.

Wakati tuko njian IRYN alinambia atakua ananitambulisha mimi kama dereva wake kwa mabosi zake, nikamwambia sawa haina shida.

Tulifika pale Ledger Plaza nikapark gari mrembo akashuka akachukua bag lake akanambia kaka sitokaa zaidi ya masaa 2, nikamwambia usiwe na wasiwasi bossy wangu. Nikaishia kumtizama mpaka anavyopotea.

Mimi nikashusha kiti nikalala zangu nikiwa pale Parking, sikutaka kutoka ndani ya gari na muda huo ilikua saa 3 tayari.

Kwa muda wa usiku pale Ledger panakuaga pametulia sana, sikutaka kwenda upande wa kule chini maana hata ningeenda wahudumu wangenisumbua tu. Na sikuwa na mpango wa kutumia pesa yangu niliona bora nichill kwenye gari.

Nilikaa pale parking, nilipitiwa na usingizi nakuja kushtuka ilikua ni text ya wife “Unarudi sangapi?”

“Wife leo ntachelewa kidogo samahani sikukupa taarifa nilikua nimebanwa, nimetembea na key zangu usiwe na wasiwasi”

“Okay, takecare” alijibu hivo.

Kuangalia muda ilikua ni saa 5 tayari lakini Iryn hakua na dalili za kurudi nikalala tena. Nilikuja kushtuka pale niliposikia mtu anagonga dirishani, nikashusha kioo fasta

“Huku aki tabasamu, Kaka sorry nimekuweka sana”

“Hapana usiwe na wasiwasi Bossy wangu, upo tayari tuondoke?”

Nilimwona kabadili mavazi sio yale ambayo alikuja nayo, akaweka bag lake nyuma, hao tukaanza safari ya kwenda Serena hotel.

Baada ya kufika Serena hotel, huyo akaingia ndani mimi nikaenda kutafuta parking. Kwa mazingira ya hotel kama zile huwezi kutoka nje kushangaa lazima utakutana na upinzani wa Askari na mimi sikutaka kukaa reception, hivyo niliamua niwe nakaa ndani ya gari tu.

Alitumia masaa 2 pale akanipigia simu nisogee mpaka reception ili tuondoke, kufika pale nikaona kasimama na Mzungu. Akanambia Insider shuka msalimie bossy wangu, mimi nikashuka akanitambulisha pale.

“Mr Robert, huyu anaitwa Insider ni dereva wangu” (kwa kiingereza)

“Nimefurahi kukufahamu Mr Insider naomba uwe makini sana na Iryn”

“Don’t worry Mr Robert, Iryn ni Boss wangu”

Palepale mzungu akatoa €20 akanipa, nikamshukuru, hao tukaondoka nimrudishe kwake. Nikamdrop pale kwake na mimi nikarudi home.

Wakati niko njian nilikua nawaza Iryn anafanya mishe gani hizi? “Huyu dem anajiuza ila atakua ni International maana hata hotel anazoingia ni 5 star”. Upande mwingine nilikua najiuliza mbona anaingia na kibag ndani au anauza sembe??

“Ila mambo yake binafsi mimi hayanihusu, hiyo sio kazi tuliokubaliana lakini siku nitamwuliza.”

Niliingia home saa 9 kasoro mama J alikua kalala, na mimi sikutaka kumuamsha nikaoga nikapanda kulala.

*****
Kwa biashara ya Uber siku za kupiga hela ni weekend nazungumzia ijumaa, jumamosi na jumapili kwa siku za kawaida bhasi jumatatu na alhamis (mwisho wa hii story nitawaelezea)

Kama kawaida niliamka jumamosi nikaaendelea na majukumu yangu ya kutafuta hela, nakumbuka hii siku niliimalizia kisarawe huko. Nilipata customer alikua anakwenda huko akaomba nimsubiri amalize kikao afu nimrudishe Dar.

Mimi kama nalipwa pesa nilikua sijali kabisa cha msingi tukubaliane sina neno. Tulikaa sana pale kisarawe kulikua na kikao mambo ya chama, walimaliza kwenye saa 10 jioni.

Tulirudi mpaka Dar nikamdrop jamaa pale Lumumba, tulichelewa sana kuingia sababu ya foleni pale Mbagala, sababu barabara ilikua inatanuliwa.

Nilivyotoka hapo uelekeo ulikua ni Kijitonyama kuonana na Iryn, saa 2 kasoro ilinikutia getini. Nikampigia simu kuwa nimefika akasema anakuja.

Alivyofika akanipa time table za usiku huo ilikua tunakwenda sehem 3, ratiba haikua ngumu sana kwani tulikua tunakwenda Hyatt, Golden tulip hotel ya Masaki na Palm village.

Yeye akasema tuanze na Golden tulip hotel, kama kawaida yake na kibag chake kakiweka nyuma tukaanza safari. Pale Golden alitumia masaa 2 tutatoka kuelekea Hyatt Posta, mimi kama kawaida yangu nikatafuta parking nikatulia.

Wakati niko parking mlinzi alikuja akanambia siruhusiwi kukaa parking, kama namsubiri mtu bhasi niende reception. Kama mnavyojua pale Hyatt ulinzi ni mkali sana.

Baada ya saa na nusu hivi Iryn akanipigia simu kwamba niende “level 8” ananisubiri, akaniambia niulizie nitaoneshwa iliko, ndo mara yangu ya kwanza naingia Hyatt. Kufika pale namkuta yuko na jamaa (kwa kumtizama alikua ni mtu wa S. Africa).

Level 8 ni restaurant ya pale Hyatt Hotel.

Akanitambulisha kwa jamaa kama dereva wake, Iryn akanambia niagize chakula tule then tuondoke. Mimi niliagiza seafood maana nilikua hata sioni cha kuagiza.

Jamaa akatusindikiza mpaka parking wakakumbatiana na Iryn, jamaa akaja upande wangu akanambia “Takecare of her”, mimi nikatingisha kichwa kama kukubaliana naye.

Tukaondoka, uelekeo ulikua ni Palm village. Iryn akatoa $100 akanipa, akanambia jamaa alinipa hii pesa ya mafuta itakua so busara nikiiweka mfukoni so keep it.

Kwenye gari tulikua tunazungumza kwa nadra sana, wakati tuko pale mataa ya NMB HQ/Puma filling station, tulikua tunatokea Ohio street ili tuingie Alli hassan road, nikaamua kuvunja ukimya, nikamwuliza kwa utani “Iryn wewe ni Mtanzania?”

IRYN: “Huku akicheka, kwani sionekani Mtanzania?”

MIMI: “Kabisa hapa bongo kama umevamia hivi”

IRYN : “Mama yangu alikua Mmursi-Ethiopia ila baba yangu ni Msouth Africa”.

MIMI: “Sasa ilikuaje mpaka ukaja Tanzania?”

IRYN: “Baba ameishi Tanzania toka 1995 kuna kampuni zake alikua anazisimamia huku na mimi nimekulia Masaki na nimesoma pale FK international school”

MIMI: “Ndomana umebarikiwa kwa uzuri Bossy wangu maana watu wa Ethiopia ni hatari”

Maongezi yetu yalipotea ghafla baada ya simu yake kuanza kuita, nilimind sana kimoyo moyo.

Tulifika pale Palm Village nikamdrop akanambia huku sitakaa sana, pale alitumia kama 1hr hivi akawa ametoka, muda huo ilikua saa7 tayari. Nikamrudisha kwake na mimi nikarudi home kulala.

Ile nimefika home namkuta wife hajalala yuko seblen anaangalia movie. Nikamsalimia nikakaa kwenye kiti.

WIFE: “Baba Junior umetoka wapi sahivi?”

MIMI: “Nilikua nimemsindikiza Michael Airpot, anakwenda masomoni Scottland” niliamua kumdanganya tu.

Michael ni jamaa yangu sana mpaka sasa, wakati tumetoka kwenye ile Taasisi X yeye aliamua kwenda kusoma Mastaz huko Ulaya. Wife anamjua vizuri sana hyu jamaa yangu.

WIFE: “Mbona kaondoka haraka hivyo hata kuniaga ameona shida”

MIMI: “Mambo mengi wife si unajua sisi wanaume, umepika nini? Naskia njaa sana” ilibidi nipotezee mada.

Huku wife akiniandalia msosi,

WIFE: “Mwanao anasumbua sana halali, kalala sio muda”

MIMI : “Pole ndo maana ya kuwa mama”

Baada ya kumaliza msosi nikamwambia wife mimi naenda kulala baada ya kuona yuko busy na movie yake.

Nikachomeka simu kwenye chaji nikakutana na message ya Iryn akinitakia usiku mwema, nikareply “Same to you Bossy wangu”.

*********
Jumapili sikwenda church kwanza nilichelewa kuamka, wife akaniamsha akaomba nikamsaidie kununua vitu sokoni.

Sababu dada alikua mgeni ikabidi niondoke naye hata akiwa peke yake awe anayajua mazingira.

Iryn akanipigia simu akanambia leo tutaenda sehemu 1 tu by 21:00 niwe around, tutakwenda Peninsula hotel. Hii Peninsula hotel ipo “Haile selasie road” karibu na Puma Filling station.

Nilitoka zangu home mapema nikaenda poteza muda pale survey, ilivyofika 3 kasoro nikaelekea Kijitonyama. Katika vitu ambavyo Iryn nilikua namsifu ni pamoja na kwenda na muda yaani akikwambia muda wa kufika utamkuta yuko tayari.

Nikamsifia pale, umependeza sana Bossy wangu,
akajibu “thank you, Gentleman”.
Siku ya leo hakua na kibag chake bali alikua na mkoba.

Kwenye upande wa kuvaa au kupendeza dada alikua yuko vizuri sana.

Ndani ya nusu saa tulikua tumeshawasili Peninsula hotel nikamdrop nikamwambia mimi nakwenda Samak samak kupoteza muda. Atakapokuwa tayari bhasi anipigie ili nikamchukue.

Nikachili pale Samaki samaki huku napiga zangu heineken mdogo mdogo. Wakati niko pale Samaki samaki kuna jamaa nilimkuta so nikaamua kumjoin story zikawa zinaendelea mdogo mdogo.

Iryn akanipigia simu nikamchukue yuko tayari nikamwaga jamaa huyo nikamchukua mrembo nikamrudisha kulala.

Wakati niko njiani nilijikuta ni mtu mwenye furaha sana. Nikawa najisemea huyu Iryn anaroho nzuri sana, kama anaweza kunipa $100 alopewa ya mafuta, je angekua mtu mwingine angenipa?? Na bado amenilipa 300,000 yangu.

Nikasema acha niendelee kuwa mpole tu, ni watu wachache sana wenye roho kama yake, mwingine asingenipa kabisa.

Nikawa nakumbuka jinsi anavyo nitambulisha kwa watu wake, nikasema huyu dada ananithamini na anaheshimu kazi yangu. Acha na mimi niheshimu kazi zake naamini ipo siku nitajua mishe zake.


Nilivyorudi home kama kawaida nilimkuta wife yuko seblen na movie yake, muda huo ilikua saa7 tayari. Nikamsalimia, hakujibu ila alikua akiniangalia, na mimi sikutaka kupoteza muda nikaingia chumbani then nikaenda kuoga.

Wakati naoga kumbe wife kachukua key na kwenda kukagua gari, ile natoka bafuni naona mtu kashika lipstick mkononi.

“Nilijua tu lazima una mwanamke maana nilishaona dalili mapema, ukirudi tu breki ya kwanza kuoga. Toka ijumaa unarudi usiku afu unarudi umechoka kumbe kuna mwanamke anakuchosha huko. Hii lipstick ni yanani? Gari nzima inatoa harufu ya mwanamke, Baba Junior nataka maelezo yakueleweka mimi sio mtoto”

Ghafla wife akaanza kubadilika

Tutaendelea:

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
 
Back
Top Bottom