EXTRA EPISODE 01
Sikuwai kuwapa muendelezo kwa kilichotokea kwa Uncle wangu. Alihama pale Mikocheni alijenga nyumba yake huko Bunju. Sasa mwaka 2020 wachina waliondoka Tanzania, sababu kubwa ilikua ni kodi. Kama mnavyojua Wachina ni wakwepaji wakubwa wa kodi.
Uncle wangu ni mhuni sana alificha gari ya kampuni mpaka leo analo, na baadhi ya madeni alokuwa anakusanya alikua anaficha. Kesi ilikua kubwa ikapelekea wachina kuamisha stoo yao ya Mabag ili kuzikwepa mamlaka za serikali.
Walikua wanafanya kazi ya kuuza mabag store pamoja na kukopesha na kupunguza bei ili yatoke haraka wao waondoke.
Baada ya kuona hali so hali wakaondoka chap, Uncle pesa alizobaki nazo pamoja na madeni ilikua ni zaidi ya million 80, hizi ni taarifa za ndani kabisa nilipata. Sio hivyo tu, walimwachia na Godown kile kiwanda cha assembling, hivyo kulikua na assets kibao kama ma AC, ma fan, na mazaga kibao. Nyumba walokua wanakaa waliacha mashine nyingi kama mashine za kufulia, yaani waliacha mazaga kibao.
Mzee baba akalifumua lile Godown akauza Mabati, mbao, nyaya za umeme, ma AC, ma fan na mitambo kibao. Unaambiwa kupitia lile godown aliingiza si chini ya 20 million. Bado vitu vingine vilivyoachwa na wachina mle ndani.
Baada ya hapo mzee baba alishindwa kupanga mipango mizuri ya zile pesa akaanza kula bata na madem zake, unaambiwa hata home akawa harudi, ukifungua gari lake unakutana na machupa ya wine na bia tu.
Zile pesa hatimae zikaisha na hakufanya jambo lolote la maana la kimaendeleo, Since 2021 life ni gumu sana. Aunt yangu alikuaga mtu wa nyumbani tu, kuna kipindi nilimpaga ushauri afungue hata biashara ya Mabag hata hakutaka kunisikiliza sababu pesa zilikuwepo. Hata Uncle nilimshauri afungue biashara ya kuuza jumla na rejareja bag zote lakini hakunielewa kipindi kile.
Life limegeuka now wanahali mbaya sana kiuchumi, wale watoto zake hawasomi shule japo walifaulu form 4, yule mtoto mkubwa niliongea naye nimsapoti arudi shule lakini aligoma kabisa, alisema anataka akomae na mambo yake shule hapana. Dogo nilishamsapoti na kiasi cha pesa tayari, mambo mengine atajua yeye.
Aunt aliyekua ananiona mimi fala, now ndo ananitafuta niwe namsaidia. Kuna jambo moja ambalo anataka kulifanya ni kuhusu yule mtoto wa mwisho wa kike. Tulikua tunapatana sana hivyo nitamsapoti kwenye masomo yake akianza secondary hiyo ndo plan yangu.
Kipindi nakwenda kuwasalimia nilienda na mke wangu na mtoto, maana hata familia yangu walikua hawaijui na pia niliwakaribisha kipindi cha kutoa mahali na hawakutaka kuja. That time nilienda na gari kabisa.
Maisha ni fumbo kubwa sana, yule unayemdharau ndo anakuja kuwa msaada kwako. Muheshim kila unayemwona mbele yako, hakuna anayejua ya kesho. Kesho yetu sote hapa ni fumbo.[/JUSTIFY]
EPISODE 10[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu