Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Mpaka sasa tuseme tumeshafikia nusu ya Story ya maisha ambayo niliyapitia kwa kipindi kifupi.

Mpaka sasa nimesha mla Prisca, je ni nini hatima yetu? Prisca nitadate naye? Je ataubali kuwa mchepuko?

Na vipi kuhusu dada yake Mary ilikuaje?

Vipi kuhusu Iryn?, mpaka sasa nishafanikiwa kumweka karibu yangu, Iryn anataka anifahamu kiundani kuhusu maisha yangu nknk, je nitamwambia?

Vipi huko mbele itakuaje nilifanikiwa kumla Iryn na kuweka historia ya kutembea na moja ya warembo wazuri?

Vipi kuhusu Muajemi atafanikiwa kumpata Iryn?, maana Muajemi anampenda Iryn seriously.

Vipi kuhusu Mama wawili? ni nani huyu mtu? Hana mume ila ana watoto wa2, shida zake anatolea wapi??.

Vipi kuhusu jamaa yangu Grizz kwa muda mfupi sana ametokea kunikubali nini kitaendelea btn us?

Vipi kuhusu Mama watoto wangu “Mama J”? nini kiliendelea?

Story nitaindika yote na mtapata Epsodes kwa wakati, na itaisha yote siwezi kuishia njiani maana ni matukio yaliyopita tayari.

Maana kuna matukio mengi sana niliyopitia kupitia hii biashara ya Uber. Tukutane kesho mapema jioni.
Oya lete kazi
Teleza
Tuondoke
 
Okay hapo sawa maana nimejiuliza maswali hapa inamaana hayupo tena! Au kimetokea nini! Hasa mpaka tutumie alikuwa
Hongera kwa simulizi na uandishi wako mzuri big up bro! Ila kwa prisca unahitaji umakini na unatakiwa kumweliza ukweli wako kabla hujamla tena mara ya pili, hapo utakuwa salama!
Kashamla Kumbe anatufcha Mkuu[emoji23]
 
Mpaka sasa tuseme tumeshafikia nusu ya Story ya maisha ambayo niliyapitia kwa kipindi kifupi.

Mpaka sasa nimesha mla Prisca, je ni nini hatima yetu? Prisca nitadate naye? Je ataubali kuwa mchepuko?

Na vipi kuhusu dada yake Mary ilikuaje?

Vipi kuhusu Iryn?, mpaka sasa nishafanikiwa kumweka karibu yangu, Iryn anataka anifahamu kiundani kuhusu maisha yangu nknk, je nitamwambia?

Vipi huko mbele itakuaje nilifanikiwa kumla Iryn na kuweka historia ya kutembea na moja ya warembo wazuri?

Vipi kuhusu Muajemi atafanikiwa kumpata Iryn?, maana Muajemi anampenda Iryn seriously.

Vipi kuhusu Mama wawili? ni nani huyu mtu? Hana mume ila ana watoto wa2, shida zake anatolea wapi??.

Vipi kuhusu jamaa yangu Grizz kwa muda mfupi sana ametokea kunikubali nini kitaendelea btn us?

Vipi kuhusu Mama watoto wangu “Mama J”? nini kiliendelea?

Story nitaindika yote na mtapata Epsodes kwa wakati, na itaisha yote siwezi kuishia njiani maana ni matukio yaliyopita tayari.

Maana kuna matukio mengi sana niliyopitia kupitia hii biashara ya Uber. Tukutane kesho mapema jioni.
[emoji23] Hp umenifurahsha Sasa km uliwala mkuu, big up
 
EPISODE 15

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

TUNAENDELEA

Jumanne asubuhi niliweza kuongea na Muajemi na kama kawaida alikua anauliza jambo lake limefikia wapi. Nikamwambia lipo pazuri na asiwe na haraka soon mambo yatakua mazuri.

Jumanne hii pia nilikua na miadi na Iryn kwaajili ya kumpeleka kwa Mama Janeth ambaye alisema kwake ni kama mama mlezi.

Niliwasili pale kwa Iryn na hii siku Iryn hakunitafuta kwenye simu kabisa, niligonga mlango na akafungua. Baada ya kunifungulia mlango na kunikaribisha alikimbilia jikoni, alionekana anapika wakati huo.

Mimi nilikua nimetulia pale seblen kama Baba mwenye nyumba sina hata habari. Baada ya dakika kadhaa Iryn alianza kuniita;

“Insider……”

MIMI: “Nambie Mummy”

IRYN : “Unaweza kupika ugali?.”

MIMI: “Yeah, kitu kidogo hicho, nije nikusaidie?

IRYN : “Nataka nile ugali leo nimepika samaki”

MIMI : “Mimi nisingekuwepo nani angekusongea?”

IRYN : “Ningepika wali, njoo bhasi na mimi nijifundishe.”

MIMI : “Mrembo kama wewe kuzungusha ule mwiko utaweza.?”

IRYN: “Shida yako unanichukuliaga poa sana”

Nilienda pale jikoni nikabandika maji kwaajili ya kupika ugali, na muda huo Iryn macho yake yote yalikua kwangu.

IRYN : “Insider upo vizuri sana ungekua Ulaya sahivi ungekua unafanyia kazi moja ya 5 - star hotel.”

MIMI: “Shida connection tu, angalia vizuri stage zote nazo fanya kesho sitokusaidia.”

Akanipiga na teke mguuni, lilikua teke la kichokozi flani hivi.

Nilisonga ule ugali vizuri mpka ukaiva na ulikuwa laini, bhasi Iryn alishangaa sana.

MIMI : “Na wewe unakulaga ugali?”

IRYN: “Na mwaka sijala ila naupenda sana. Nimeona stage zote kesho nitakusongea ugali wangu.”

Tulikula ule Ugali na Iryn alikwenda kujiandaa,
Baada ya hapo tuliondoka na kuelekea Masaki kwa Mama Janeth. Sikutaka kuuliza tunakwenda kufanya nini huko ila nilisubiri aniambie mwenyewe.

MIMI: “So mama Janeth ndo alikua rafiki wa Mama yako?”

IRYN: “Yeah, pia ndo alikua msaidizi wa Mama kazini kwa cheo, mama alikua coördinator yeye alikua kama Assistant. Nje na hapo walikua pia marafiki wakubwa sana.”

MIMI: “Leo hajakwenda kazini?”

IRYN: “Alikua safari karudi Jumapili nahisi watakua wamempa off”

Tulifika Masaki mapema na moja kwa moja tulikua getini kwa Mama Janeth yeye alikua anakaa karibu na zahanati ya IST, ukishavuka ukuta wa IST kuna kibarabara cha vumbi kinakata kushoto.(INTERNATIONAL SCHOOL OF TANGANYIKA).

Tulifunguliwa na Mlinzi na muda huo Mama Janeth alikua katoka nje kibarazani. Bhasi baada ya sisi kushuka kwenye gari, Mama Janeth alitoka kibarazani na Iryn naye alitembea kwa spidi wakakumbatiana.

“Waow my daughter I have missed you so much”

ili onekana ni watu ambao wamemisiana sana n hawajaonana kwa muda mrefu.

Mama Janeth alikua ni Mzungu na pia alikua anajua kuongea kiswahili vizuri kabisa. Tulikaribishwa ndani na muda ule ule zikaletwa popcorn kwenye vibakuli, Iryn akaanza maongezi na Mama Janeth. Na Iryn alichukua nafasi hiyo kunitambulisha kwa Mama Janeth kama mimi ni rafiki yake kwa hapa Dar.

Maongezi makubwa ambayo nilikua nikiyaskia ni pamoja na suala la nyumba alizoacha Mama Iryn. Mama Janeth alikua anamwambia Iryn haoni sababu ya kuendelea kuzisimamia zile nyumba wakati Iryn yupo.

Nyumba zilikua zimepangishwa na hivyo walikubaliana wale wapangaji watakapo maliza mikataba yao bhasi Iryn ataanza kuwa incharge. Pia walikubaliana kwenda kuzitembelea hizo nyumba zote siku ya alhamis.

Kwa upande wa biashara walizokuwa wanafanya na Mama yake, Mama Janeth alisema zinakwenda vizuri na akamwambia wakimaliza mazungumzo watakwenda kuitembelea Saloon.

Pia walizungumza suala la kubadilisha taarifa za kampuni ambapo Iryn angekua Director. Na sababu alikua na Bachelor ya Usimamizi wa Biashara kwake lisingekua shida, na Mama Janeth alifurahi maana aliamini Iryn angeenda kuwa msaada mkubwa kwenye biashara kutokana na elimu yake.

Iryn alikubali kuanza mchakato wa kubadilisha hizo taarifa za kampuni na wakawa wanaplan pale. Mama Janeth alimwambia Iryn kuhusu Mwanasheria watamtumia wa palepale ofisni, yeye atume TIN na documents zingine muhimu.

Baada ya hayo mazungumzo kuisha walikuja kudiscuss suala la mafao ambayo mama yake alikua anaweka kama kiinua mgongo.

Mama Janeth aliikwenda ndani na akarudi na bahasha mbili za (A4) ambapo bahasha moja nyeupe yenye nembo ya Blue ya organization, akatoa form moja pale na akaamwambia Iryn anatakiwa kuzijaza kwa makini sana.

“Hizi form utaondoka nazo Iryn kasome kwa makini sana angalia mshahara wa mama yako toka anajiliwa, total utakayopata uta times 30%. Nimekuwekea salary slips zote toka mama yako ameanza mkataba na Organization.”

Hio bahasha ya kaki ina taarifa za kampuni yetu na kila kitu kinachohusu kampuni. Pia kuna form za mikopo ipo humo ambayo mimi na mama yako tulikopa kupitia kampuni yetu, utapitia kwa makini ujue kiasi kilichokopwa na tulichorudisha. Kuna taarifa zote humo utaziona, kama kuna sehemu utakwama bhasi utanipigia simu mwanangu.

Mama Janeth alionekana kumpenda sana Iryn kweli kweli. Muda huo mimi nilikua kama mpenzi msikilizaji maana sikua nachokuzungumza pale, niliishia kula popcorn mpaka zikaisha.

Ni mazungumzo yaliyochukua masaa 2 na baada ya kumaliza walikubaliana alhamisi siku watakayo onana bhasi Iryn aende na zile form.

Muda huo Mama Janeth alikwenda ndani na akarudi na Camera aina ya Canon na akaomba niwapige picha na Iryn. Alinielekeza namna ya kupiga na mimi bila kukosea nikawapiga picha pale.

Tulitoka hapo tukaenda kwenye Saloon palepale Masaki na ilionekana kuwa busy sana. Mama Janeth akamtambulisha Iryn kwa wale wafanyakazi kama Bossy wao mpya akiwa kama mrithi wa Mama yake, hapo ndo wakajua Iryn alikua ni mtoto wa Marehemu. Ilikua ni Saloon kubwa tu ambayo inafanya mambo mengi sana mpaka kupamba maharusi.

Baada ya kilakitu na mazungumzo yao kukamilika waliagana na Mama Janeth aliendelea kubaki pale saloon. Baada ya kutoka hapo Iryn akasema twende Coco beach nikale mihogo, nimeimiss.

Muda mfupi tulikuwa tumewasili pale Coco na wakati tunaingia walionekana watu wakiifukuzia gari, si mnajua pale Coco ukienda jinsi watu wanavyo gombania mteja?.

Tulipark gari yetu vizuri na baada ya kushuka kwenye gari, Iryn alinambia nimfuate. Alionekana mtu ambaye anayajua mazingira vizuri ya pale. Tulikwenda na tukaa sehemu moja ipo na mwishoni huku, tukatulia pale huku tukipulizwa na upepo mzuri wa Bahari.

Kuna Kaka alikuja pale na alioneka kufahamiana na Iryn vizuri tu.

“Sister karibuni sana, karibuni jamani”

IRYN : “Nataka mihogo mizuri laini na mishikaki. Utaleta mihogo 4 na mishikaki 20.”

MIMI: “Mbona unaagiza mishikaki mingi sana hivyo?”

IRYN : “Kaka pia niitie yule wa madafu. Insider akileta ndo utajua kwanini nimeagiza mingi hivo.”

MIMI : “Sawa Bossy wangu mimi siwezi kupinga.”

IRYN: “Afu hilo jina silipendi, hujui tu.”

MIMI : “Sasa unataka nikuite nani? Kwani wewe sio Bossy wangu.?

IRYN: “Niite jina langu, simple tu.”

Na muda huo jamaa wa dafu alikua kafika wakati tukiwa kwenye mazungumzo, jamaa akatukatia madafu 2 pale na Iryn akamwambia jamaa amkatie mengine 2 ya kuondoka nayo.

IRYN: “kaka kama mabaya sikulipi, kama unajua ya leo sio mazuri bora usikate”

“Dada mimi ndo mtaalamu wa madafu hapa umefika hata usiwe na wasiwasi.”

Jamaa baada ya kutukatia madafu na kuondoka story ziliendelea pale taratibu huku tukifurahia utamu wa dafu.

IRYN : “Insider unapaona pale?”

MIMI: “Pale ndo ilikua siku yangu ya mwisho kumpiga mama picha”

Na muda huo Iryn alitoa simu kwenye mkoba na alinionesha picha alokuwa kampiga mama yake eneo lile. Alinionesha picha zingine za Mama yake nyingi tu ambazo walikua pamoja na zile ambazo na mama yake alikua peke yake.

Nikaomba anioneshe na picha za Baba yake, bhasi akanionesha picha ambazo walikuwa pamoja yaani yeye, baba na Mama yake. Pia akanionesha picha ambazo alikua na Baba yake.

Baba yake Iryn alikua ni Mzungu ila alikua ni M-South Africa, Iryn alinambia origin ya Baba yake ni Uholanzi.

Mama yake Iryn alikua mzuri sana alikua na ule urangi wa ki-Ethiopia nafikiri sote tunajua Waethiopia walivyobarikiwa kwa uzuri. Na Iryn alifanana na sana na mama yake na alichukua kidogo kwa Baba yake kutokana na picha nilivyoziona na yeye alikiri hivo kafanana sana kwa mama.

Muda huo jamaa alikua kaleta mihogo na mishikaki na hapo ndo nikagundua kwanini Iryn aliagiza mishikaki mingi.

IRYN : “Insider umeelewa sasa kwanini niliagiza mishikaki mingi?”

MIMI : “Nimeelewa ni vidogo sana asee. Ila ni vitamu sana.”

IRYN : “Mimi na mama tulikuaga tunakuja hapa tunakula mihogo na mishikaki na tulikua tunakaa hapa.”

MIMI: “Nashangaa kuona hata wewe unakula mihogo.”

IRYN : “Shida yako Insider unanichukulia mimi kama slay queens, pole yako.”

MIMI : “Jinsi ulivyo ni ngumu mtu kukuelewa, mrembo kama wewe kula mihogo ni ajabu sana, hii waachie akina Mwajuma”

IRYN: “Napenda sana traditional foods”

Muda huu pia nilikua nawaza namna ya kumuingia kuendeleza mada ya Muajemi, maana ile pesa yake nilikua naipigia malengo sana.

MIMI: “Afu unakumbuka kule Kidimbwi ulisema tutadiscuss ishu ya Muajemi, nasubiri jibu lako ili nimpe kirungu chake.”

Muda huu Iryn alikua akiniangalia….

IRYN: “Si anataka tuonane? Haina shida, nikigundua ni Important person nitamkip close.

MIMI : “Hayo ni wewe ila nahisi atakua ni Potential sana, hata kwangu pia.”

IRYN : “Kwani wewe Insider una mipango gani ?”

MIMI: “Na mpango wa kufungua biashara ya Lubricants, atlist nina experince nayo.”

IRYN : “Good, I love your hustles. Sitaki kukuuliza maswali but you promised utaniambia kuhusu wewe.”

MIMI: “Usijali hata home nitakupeleka, ukale ugali wa mlenda.”

IRYN: “I will be waiting for that day”

MIMI: “Muajemi tunameet naye lini?

IRYN: “Alhamis tukimaliza mizunguko tunaonana naye, you said he can be trusted but I trust you”

MIMI: “Nipe tano bhasi”

Ile kunipa tano nikampa tano ya nguvu akaanza kulalamika pale… “Au au… ndo nini hivi Insider…”

Nikamwambia inuka bhana inuka bhana nataka nikusaprize.

Nikamwinua nikampeleka pale aliponionesha alimpiga picha mama yake. Nikamwambia anipe simu yake nimpige picha, bhasi akaweka mapozi nikampiga picha za kutosha.

Licha ya yote kuna mambo ambayo nilikua namfanyia Iryn sababu nilijua anaya miss kutoka kwa mwanaume. Jamaa yake Grizz alikua Ufaransa ambapo nilikua najua lazima atakua na demu kule, hakuna mapenzi ya mbali kwnye Dunia hii. Na yale mambo nilokua namfanyia alikua akiyafurahia sana tena sana, hata kitendo cha kumpiga picha alifurahi sana.

Tukalipia ile Bill kwa jamaa na sisi tukaondoka pale Coco, sasa wakati tuko kwenye gari Prisca alikua anapiga simu, nikakumbuka nilimuahidi nitakwenda kumuona chuo na sikwenda lazima atakua kamind. Muda huo na mimi sikusita palepale nikapokea simu yake, tukaongea na nikamwambia nitakwenda kwao kumwona.

Tulikwenda na Haile selassie Road na tulikuja kutokea pale Kanisani “St peters”, sasa wakati tuko pale mataa tunasubiri folen, ile mitaa huwa wanauzaga sana maua. Nilipata wazo nimnunulie Ua Iryn kama zawadi nifanye kumsaprize na ua, nikamwita dogo mmoja akaja chap na maua.

“Dogo maua unauzaje?

“Bro park gari pale tuongee vizuri.”

Muda huu Iryn alikua akiniangalia ni kama alikua anajiuliza Insider ananua ua kwa ajili ya nani? Na alikua akitizama kinachoendelea kwa makini, na mimi nilimsoma akili yake.

“Dogo kwani hapa huwezi fanyia biashara? Pale mataa hatutoki sahivi si unaona kuna traffic pale?.”

“Bro haya utanipa elfu 20 na haya elfu 30”

Nilipiga jicho kali na nikalipenda Ua moja lilikua jekundu afu ni zuri sana,

“Nimelipenda hili, dogo bei za maua nazijua vizuri nipe bei za jioni mimi nilipie.”

“Bro hilo top nipe 25 hata wewe si unaliona lilivyo zuri?”

Japo nilikua najua bei yake ni 20k bhasi sikutaka kubargain naye sana na nikatoa pesa nikampa kiroho safi na palepale nikapandisha kioo cha gari.

Sikutaka kumpa Iryn nafasi ya kuongea hata kidogo na nikamkabidhi lile ua palepale.

“This gift is for you mummy”

Ni kama Iryn alipigwa na shock hakuamini kama lile ua lilikua ni kwaajili yake ni ilikua saprizi moja ya kutotegemea. Kama ni point bhasi pale nilibeba point 10, na muda huo Iryn alikua anafuraha sana.

Nikamwambia Iryn hii ni zawadi yangu kwako kwa yote unayonifanyia, sina uwezo wa kukunulia saa ya gharama, sina uwezo wa kununulia necklace ya gharama, lakini kwa hiki kidogo naomba ukipokee kwa mikono miwili.

“No Insider It’s means alot to me, Ahsante sana kwa hii zawadi hujui to what do I feel right now. Nashukuru sana hii ni zawadi kubwa sana kwangu hujui tu.”

Wakati tuko njiani Iryn aliendelea kulitizama lile ua kwa furaha sana.

Tulifika kwake nikapark gari pale getini nje, nikamfungulia geti nikamsindikiza mpaka kwake na nikamfungulia mlango. Nikamuaga nawai tutawasiliana badae bhasi na palepale akanihug kwa nguvu, aisee nililifeel lile joto lake na lilikua amazing [emoji2956] afu lile OG.

Tukaachana pale na mimi uelekeo ulikua ni kwenda kuonana na Prisca, sasa wakati niko njiani nilikua nawaza zawadi ya kumpeleka Prisca. Ua ndo ilikua zawadi nzuri kwake lakini mazingira yalikua magumu kurudi tena pale namanga. Niliwaza sana lakini sikuona zawadi ya kumchukulia, nikasema nitaingia pale Shoppers hapohapo nitajua cha kumpelekea.

Hatimae nilifika pale Shoppers Mbezi Beach na nikazama ndani lakini huwezi amini hata sikuona cha kumnunulia. Nilizunguka mle ndani kama mtalii na nikaishia kununua popcorn na bubblegum “Mentos” zinakuwaga kwenye vikopo vidogo hivi.

Na muda mfupi nilikua getini kwao, nikampigia simu akanambia niingie ndani daah “what the fvck” nilijisemea moyoni. Sikutegemea angenambia niingie ndani, na muda huo mlinzi alikua kafungua geti tayari.

Muda huo nikijifikilia jamaa akaja akanambia amesema uingie ndani,

“Prisca ameanza ujinga gani huu…..”. Nilishindwa kataa nikaingia nikapark gari na yeye alikua katoka tayari kunipokea.

Nikampa ule mfuko nilokuja nao akanambia niingie ndani, sikuweza kukataa maana wanasema maji ukishayavulia nguo sharti uyaoge.

Nikaingia ndani nikamkuta Mary yuko seblen, lakini pia pale seblen palikua na dada mkubwa mmoja na madogo wawili wa kike.

Mary alivyoniona akanisalimia pia akanikaribisha kwa tabasamu.

MARY: “Insider leo umeamua uingie ndani”

MIMI: “Nimeingia sababu ya mgonjwa lasivyo nisingethubutu”

MARY: “Hakuna anachoumwa huyo anakusumbua tu.”

Prisca alinitambulisha kwa ndugu zake na alinza na yule dada mkubwa ambaye alinitambulisha kama Mamdogo wake, hakuishia hapo akawatambulisha wale madogo wa2 wakike ni wadogo zao. Hapo nikajua kumbe familia yao wako watoto wa4 lakini wote ni wa kike.

Na muda huo dada alikua kaniletea juice na mimi nikaanza ikaifakamia palepale. Ofcourse sikuwa confident sana mle ndani ukizingatia Mwanaume nilikua peke yangu naye koroma mle ndani.

MARY : “Insider leo utanipa namba yako ya simu, sometimes huwa nahitaji huduma ila nashindwa kukupata.”

Wakati anaongea hivyo, alipigwa jiko kali sana na Prisca

MIMI: “Haina shida, Prisca ameshindwa kukupa?”

MARY : “Insider Prisca hawezi kunipa namba yako, na sijui kwanini hataki niwe na namba yako.”

MIMI: “Lete simu nikuandikie hapahapa.”

Na muda uleule Mary alikuja akaa pembeni yangu, nikamwandikia namba na akabaki palepale hakuondoka.

Muda huu Mamdogo wao alikua akiniangalia kwa macho ya kiwizi wizi, nikama mtu ambaye alikua anasikia story zangu ila alikua hajapata bahati ya kukutana na mimi. Prisca naye muda wote alikua kimya hakusema neno lolote.

PRISCA: “Insider can we talk private?”

MIMI: “Yeah,sure”

Tulitoka pale tukakaa kibarazani lakini nilikua sijiamini kabisa maana nimeingilia Himaya ya watu. Prisca japo alinitoa wasiwas kwamba wazazi wake sio minder hawana shida kabisa.

Pale kibarazani kulikua na coach vidogo flani hivi vi-nne na meza ndogo duara ya kioo.

MIMI: “Nambie unaendeleaje Mummy”, nilikua ninamshika mashavu.

PRISCA : “Safi tu”

MIMI: “Mbona kinyonge sana? Umepooza sana, shida nini?.”

PRISCA : “Insider you fvcked me hard that day, but now am okay”

MIMI: “Ooh sorry, seems like unataka tena.”

Prisca kama alipata na ka-aibu fulani ila aliishia kutabamu na akachange mada. Lakini mimi nilielewa anachohitaji.

PRISCA : “Nimefurahi umeingia ndani leo.”

MIMI : “Nimeingia leo sababu unaumwa ila hutoniona tena humu ndani.”

PRISCA : “Usijali hata mimi nitakuja kwenu.”

Nikaona huyu mwanamke ameanza kuleta mambo ya kichawi, aje kwangu kufanya nini?

MIMI: “Mimi nasepa hata hivyo muda umekwenda, na muda huo ilikua saa1 usiku na madakika tayari”

Na muda huo Mary alikua amekuja pale kibarazani na akakaa.

MARY : “Insider unavyoondoka nishtue nataka unipe lift.”

MIMI: “Mimi ndo naondoka hapa, nilikua na mpango wa kuja kuwaaga huko ndani.”

Tukaondoka pale na Mary tukaingia kwenye gari hao tukaondoka.

MIMI: “Unaelekea wapi.?”

MARY : “Nataka kwenda stationery na kazi ya kufanya nataka nimpe mtu kazi. Insider wewe unakaa wapi?”

MIMI: “Mimi nakaa Massana kule.”

MARY : “Pale si pana stationery nzuri”?

MIMI : “Yeah ipo”

MARY : “Twende hapo.”

MIMI: “Ila sitokurudisha utarequest”

MARY : “Sawa”

Wakati tuko njiani tulikua tunapiga story mbalimbali na Mary akili yake ilionekana kukomaa sana. Tulifika pale Massana nikamdrop kwenye stationery mimi nikaondoka, nikamwambia ukirudi home utanijulisha.

Mimi nilivyorudi kama kawaida niliingia bafuni, baada ya hapo nikachukua laptop yangu nikaanza kuangalia mipango yangu. Pia mimi nilikua nimeandaa Excel sheet ambayo nilikua naweka taarifa za biashara kila siku kwa nilichoingiza na kutoa. Kama mafuta nilikua nachukua risiti kila napo jaza ili zinisaidie katika mahesabu, mwisho wa mwezi ndo nilikua napiga accounting za mwezi husika hasa kwenye mapato na matumizi na faida iliyopatikana.

Baadae kidogo Iryn alinipigia simu na tuliongea sana hii siku kwenye simu kuliko zote. Na zaidi aliifurahia sana ile zawadi ya UA akanambia mtu wa mwisho kumpa zawadi ya Ua alikua ni mama yake. Na mimi ndo nimekua mtu wa kwanza kumpa zawadi hio baada ya kifo cha mama yake. Tuliongea sana na simu na akaomba kesho niende kwake nikamsaidie kuzipitia zile form pamoja.

TO BE CONTINUED.
Siku ya alhamis ujafanya Kaz kbsa tokea asbh unadhurura tu na bibie iryn[emoji41]
 
Ndugu zangu wana Jf habari zenu.

Unajua kwenye haya maisha tunapitia mengi sana hasa katika utafutaji kwa upande wa Wanaume. Tunakutana na mambo mengi sana ya aibu, kukatishwa tamaa, kuachwa na tuwapendao na mauzauza mengi sana.

Nakumbuka mzee mmoja alinambia mapambano ya kupata maisha mazuri sio rahisi inatakiwa ujasiri, kujitoa na kuwa na maamuzi magumu sana. Kila aliyefanikiwa ana siri nyingi ambazo sio rahisi kushare na mtu mwingine, sometimes tunakutana humu jf, tuna marafiki zetu wote hapa duniani tuna matatizo lakini matatizo yetu yametofautiana.

Mimi INSIDER nimepitia mambo mengi sana kiasi kwamba nilikata tamaa ya maisha unaweza ukasoma huu uzi wangu “Sitaomba kazi acha niwe jeuri tu”

Sitaomba kazi tena, wacha niwe jeuri tu!!

https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/Sitaomba-kazi-tena%2C-wacha-niwe-jeuri-tu%21%21.1619876/ , na story yangu itaanzia hapa, ilikuaje mpaka nikaingia kwenye biashara ya uber??.
Hii ni story ya kweli na siyo ya kutunga, lengo langu nataka ndugu zangu mpate ujumbe kuhusu haya maisha. Kiufupi usikubali kukata tamaa hata kidogo, no matter what you fall, keep fighting, God has plans for all of us. Kwa wale ndugu zangu wa Uber/Bolt ambao mnataka kuingia kwenye hii biashara utaweza kupata mwanga mzuri kuhusu hii biashara maana nina experience ya kutosha. Tusichoshane acha nianze kumwaga asalii……..,,

…….wakati naandika ule uzi wa “ Sitaomba kazi tena wacha niwe jeuri” , nilikua nimerudi mkoani kwa wazazi kuwasalimia. Ofcourse maisha ya mkoani na niko home sikua na wasiwasi kabisa wazungu wanasema “HOME SWEET HOME””. Chuo mimi nimemaliza moja ya chuo kikubwa hapa Dsm, baada ya kumaliza chuo sikutaka kurudi home kabisa. Maana niliwaza hata nikienda home kule nitafanya nini? Nikakae na mama tu? Niwe nakula na kulala? nikakukumbuka ule msemo unaosema mtoto kwa mama hakui bali analemaa akili.
Niliamua kwenda kwa Uncle wangu kukaa huku nikiendelea kutafuta kazi hapa mjini, alikua anaishi Mikocheni. Kipindi cha weekend nilikua natoka chuo nakwenda Mikocheni nashinda kule kwa Uncle then jumatatu narudi chuo, pale palikua kama home tu.

Nikaanza kusambaza CV kwenye mataasisi, makampuni, NGO’s kwenye mabank na sehem nyingi tu hapa Dsm lakini patupu sikufanikiwa kupata sehemu hata ya kujitolea. Kuna siku nilikuwa nimekaa na Uncle tunaongea akaniuliza umemaliza chuo sasa una mpango gani?. Nikamwambia abc zote kwamba nimepeleka maombi yangu sehemu mbalimbali nasubiri majibu kama nitafanikiwa ama laah. Akanambia kuanzia jumatatu tutaanza kwenda wote kazini, lakini utaweza mikiki ya Kariakoo?, nikamwambia ni bora nishinde huko kuliko kubaki hapa home, I hate that.

Kweli jumatatu ikafika tukaenda huko kwa Wachina, ile siku sikutaka kuuliza ni kazi gani lakini nilikua najua Uncle anafanya kazi kiwanda cha mabag. Tulivyofika pale kiwandani Uncle akanitambulisha kwa Mchina.

UNCLE: Hey Mr ping that is my Uncle, My sister’s son. Call him INSIDER.

MCHINA: Ooh you look alike I thought is your son, akacheka. huyu mchina alikua hajui kiswahili hata ngeli alikua anaibia kwa mbali. Mchina akanambia hey “Rafiki” karibu.

MIMI: Thank you.

Uncle akaniita niingie store akanambia kazi yangu itakua ni kusupply mabag kule Kariakoo. Hii kampuni yeye alikua ni Sales and Operation manager. Kampuni ilikua inatengeneza journey bags na backpack bags na pilot bags. Canter ilikua imefika pale tayari kwa upakizi, so tukaanza kupakia mabag mle kwa gari na kuyapanga kuyapeleka Kariakoo kwa wateja. “Ipo hivi pale kiwandani sio kwamba ndo wanaanza kutengeneza hapana wanafanya assembling tu, material zote zinatoka China, pale ni kuassemble na kuyapeleka sokoni”.

Ile siku nilipiga sana kazi nakumbuka tulipiga trip 2 ila kila tripu ilikua na bag 200, sio poa kupakua bag pale Kariakoo ni mtihani yaani foleni za watu zilikua zinakera sana. Uncle akawa ananilipa cash kwa siku 10,000/=, wakati naanza alikua ananinulia chakula ila baadae akaanza kunikataa so nikawa najilipia, kuhusu kwenda kazini tulikuwa tunaondoka wote kwa gari asubuhi.

Nikaimasta kazi kwa muda mfupi sana ikafika stage akawa ananiacha niende peke yangu na dereva mitaa ya Kariakoo na wateja nikawa nimewajua tayari haikuwa ngumu kwangu. Uncle akanambia upo vizuri ikafika stage hata madeni nikawa nakwenda kukusanya then napeleka bank, yaani unakuta nimekusanya madeni mpaka 80million, hiki ndo kipindi nilikua nashika pesa nyingi sana.

Nilikua nimejenga urafiki na baadhi ya wafanyakazi wa pale kiwandani, siku katika kupiga story jamaa akanambia naona sikuhizi umepanda cheo unapeleka mabag mwenyewe Kariakoo. Nikamwambia nimemasta kimtindo akanambia safi inabidi mzee wako majukumu yapungue maana umri unakwenda huko Kariakoo atuachie vijana. Jamaa akaniuliza posho si unapewa ukienda kupeleka mzigo?? nikamwambia sio haba kuliko kukaa bure, akauliza kwani unalipwa kiasi gani? nikamjibu 10,000. Jamaa akasema Uncle wako anakupiga atlist angekupa hata 50,000/= nikamwuuliza kwanini?, jamaa akanambia posho ya kwenda kupeleka mabag kwa siku ni 100,000/=

Jamaa akasema mzee wako anakuonea sio haki ile kazi ni risk, “hii kazi kama jamaa anavyosema kweli ni risk sababu unaweza kuibiwa kweupe, Kariakoo si mnaijua? “Kuna siku tulikua tunapakua mabag nilikua na moja ya wafanyakzi wa pale sasa jamaa alichanganya mafile akampa bag muhuni mwingine. Ilibidi akatwe kwenye mshahara, ni hivi tukikaribia Kariakoo tunawapanga wateja mapema. Kama mnavyojua maduka ya kariakoo yako barabarani plus yale mafoleni ni kichefuchef so huwa tunapakua mabag mlemle kwenye foleni. Mhusika anakuja na vijana wake wabebaji, inatakiwa uwakariri vzr maana ukizingua tu unaweza mpa mzigo mtu mwingine.”

Jamaa baada ya kufunguka hayo pia akanambia mzee wako kila bag anapata commision kwa bag la set 3 analipwa 1,000 na set 2 analipwa 700 (Zile bag za safari, set 3 ndani zinakuwa mbili yaani ukifungua zipu za bag kubwa ndani kuna kuwa na bag 2. Na hizi set 2 ukifungua zip ndani kunakuwa na bag 1). Nikawaza hata lunch najilipia, uncle anaplay fouls sio haki. Nikakumbuka matukio mengi tu mfano sometimes nikipeleka mzigo before sijaondoka atanambia ukifika Kariakoo piga simu kwamba TRA wamekukamata risiti sio sahihi, then utasema wanataka million 2, so mchina alikua anatuma hela. Nilikua nafanya hayo yote afu atanipa 50,000 tu au asinipe kabisa, nikikusanya madeni kama na million 30 atanambia ingiza kwa account ya kampuni maybe million 27 then million 3 nampelekea. Zile ndo zilikua commission zake, Uncle wangu alikua anapiga sana hela shida alikua na madem wengi sana.

Kufupisha hii story, Mchina akaanza kunikubali sababu nilikua nampa ushauri baadhi ya mambo, akawa close sana mimi. Hiki kitendo Uncle hakupenda aliona kama nataka kumpokonya ugali wake, nikaona anaanza kunikataa mara anipe kazi ya kwenda kuangalia madogo shuleni, sababu zikawa nyingi mara biashara imekua ngumu sijui mambo yakikaa sawa ataniita. Kama msomi nikajua hapa sina changu, maana jamaa kule kazini alikua ananipa mkanda mzima kinachoendelea. Ukweli hii kazi ilikua inanisaidia sikosi hata pesa za vocha na matumizi yangu binafsi.

Nikaanza kukaa home na Aunt yangu, yeye alikua ni mama wa home tu. Hakuna kitu kigumu kama kuishi na ndugu inahitaji moyo na uvumilivu sana. Aunt yangu ni mvivu sana hata kwenye masuala ya mausafi hayuko active, nafikir ni moja ya sababu Uncle akawa na michepuko mingi. Ubaya sasa Uncle alikua anamsikiliza sana Aunt kwa lolote alilokua anasema yaani ni shida. Sasa hapa home tulikua tunabaki mimi na Aunt, madogo 2 wako boarding mmoja wa kike ndo alikua mdogo ansoma anatoka asbh anarudi jioni.

Nikaanza kuwa house boy wa mle ndani naamka Asubuhi sa12 nimpikie mtoto chai, baada ya hapo nitafanya usafi na kuosha vyombo, mchana nitapika chakula, jioni ninakazi ya kupikia mbwa chakula na kumwagilia miti na maua. Hizo kazi zote nilikua nafanya mwenyewe kila siku na nilikua nafanya kwa moyo wote. Unaweza kushangaa mwanaume nawezaje kufanya hizo kazi lakini nilifunzwa nikiwa mdogo na mama yangu mzazi pamoja na dada yangu. Ikafika stage akaanza kunipa kufua nguo za Uncle na mdogo wangu ambaye ni mtoto wa mwisho (ambaye huwa naamka asubuhi kumpikia chai), nikaona haya mazoea yamezidi sasa.

Kuna siku nilikua natoka pale home Asubuhi kwenda mjini kwaajili ya interview na kusaka fursa, wahenga wanasema fursa haikufuati nyumbani unatakiwa ukaitafute. Sasa nikiondoka pale asubuhi mara nyingi anakua amelala na uncle wangu huwa anatoka sa11 au 12. Sometimes kuepusha makazi kama hayo nilikua nakwenda mjini au kwa washikaji kupoteza muda tu. Aunt wangu akawa anampa taarifa Uncle kwamba huwa naondoka bila kuaga afu narudi usiku. Kuna siku Uncle alinikaripia sana nikamwambia Uncle navyotoka huwa anakua kalala kumwamsha sio busara, napia nikitoka sio naenda kuzurura nakwenda kutafuta kazi. Uncle akasema kama umekua mkubwa humu ndani nenda kapange ili uwe huru. Kama mwanaume niakanza kufikiri namna ya kutoka pale ikiwezekana nikapange nianze maisha yangu ya kujitegemea.

Nikapata wazo tangu nimalize chuo sijawai kwenda home mkoa kusalimia acha niende home nikasalimie wazazi wanipe na baraka. Kuna siku Aunt alinitia hasira sana, ilikua usiku inakwenda saa 2 nikatoka kwenda dukani kununua vocha niliacha simu chumbani. Kumbe wakati nimetoka Uncle alirudi akaniulizia hakunikuta ikabidi apige simu ikawa haipokelewi. Wakati nimerudi nikaona gari ipo uwanjani nikajua mzee karudi naingia ndani namkuta seblen kavimba hatari. Nikamsalimia Uncle shikamoo pole na kazi hakujibu, akaniuliza ulikuwa wapi usiku huu? Maana simu hupokei, kabla sijajibu Aunt akaropoka “huyu alikua kwa kidem chake kule bondeni taarifa zake zote ninazo kazi umalaya tu”. Nikaona hizi dharau sasa nakua kama mtoto nikamwambia Aunt mimi tayari ni mtu mzima hupaswi kunipangia mambo ya kufanya, mimi kama kijana pia nahitaji kuwa na mpenzi na haki yangu naomba uwe na mipaka, nikaenda zangu chumbani. Aunt akasema kama umekua mkubwa si uende ukapange ili uwe huru??, nikajua hapa nishachokwa sipaswi kuendelea kung’ang’ania, akufukuzaye hakwambii toka.

Huyu mwanamke ambaye Aunt alikua anasema kidem changu ndo mama junior wangu mpaka sasa. Ni mke wangu japo sijafunga ndoa ila taratibu zote nimekamilisha kama kulipa mahari, bado ndoa ya kanisani tu. Niseme tumetoka mbali sana from Nothing to something, ni mwanamke anayenipenda sana na kunijari anasifa zote za kuitwa mke. Namshukuru Mungu kwa kuniletea huyu mwanamke kwenye maisha ni moja ya mtu ambaye ameplay part kubwa kwenye mafanikio niliyonayo. Tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume ana miaka 2 sasa tumwite Junior.

Nilikua kwenye dimbwi kubwa la mawazo sana. Wakati niko room nikawaza jumamosi acha niondoke niende home mkoa kusalimia na pia niongee na wazazi juu ya mustakabali wa future yangu. Kesho yake nikamwaga mama Junior alishtuka sana mbona ghafla? something wrong? Nikamwambia NO! nataka nikawasalimie wazazi lakini nitarudi ASAP. Mama Junior akaomba tusex ilikua ni miez 5 toka tuanze mahusiano hatujawai kukutana. Ile jioni nikaona acha niwaage na hawa akina Uncle wanaweza kufikiri vibaya, nikategea Uncle amekaa seblen nikamsalimia, then nikamwambia Uncle Jumamosi mimi nitakwenda home kusalimia then nitarudi. Uncle akashtuka mbona haraka hivyo kulikoni? nikamwambia ni muda sijakwenda huko ni vizuri kwenda kuwajulia hali wazazi. Uncle akanambia bhasi kesho uende hata Kariakoo ununue vitenge vya mama, nikamwambia kesho ambayo ni “ijumaa” nitakwenda chuo kufuatilia cheti changu hivyo sitoweza kwenda Kariakoo. “Kumbe nilikua na timetable na mama Junior”, uncle akatoa hela akanipa kuhesabu ilikua 100,000 cash.

Jumamosi kweli nikaondoka kwenda home jioni nikiwa na bashasha nikafika mkoa nikashangaa jinsi mji ulivyojengeka maana ni miaka 3 ilipita bila kukanyaga. Nikachukua bajaji mpaka home kushuka mama akaja akanikumbatia….

MAMA: waaoohh mwanangu nilikumisi sana jamani, naona umepungua sana shida nini?
MIMI: Mama maisha haya na stress za ajira nitanenepaje?
MAMA: umerudi sasa ule kwa bidii, maziwa, mayai yapo yakutosha akatabasamu, twende ndani. “Maana wakati tunaongea haya tulikua nje getini”.

Kiukweli nilivyofika home nilifarijika sana moyo wangu ulijawa na furaha sana. Bhasi ile jioni tukala dinna as family, wakati tunakula mama akaongea huyu mdogo wako anasoma science lakini hesabu hawezi zero kabisa, itabidi uangalie namna ya kumsaidia. Nikamwambia mama haina shida kesho nitakaa naye chini tuongee vizuri. Baada ya dinna nikakaa na wazee tukaongea sana kuhusu maisha, wakanitia moyo sana, tukafanya maombi tukaenda kulala.

Kipindi naandika ule uzi “Sitaomba kazi acha niwe jeuri tu” nilikua nimeridhika na maisha tayar sina stress niko home. Ilikua ni kucheza PlayStations na masela wa huku home full raha niko home kwa mama stress za maisha natolea wapi!?. Naamka asubuhi chai ya maziwa, mayai 2 ya kuchemsha ya chienyeji, mkate umejaa blue band. Kama unawazazi jitahidi uwapende wazazi wako wakiwa hai, wazazi wanatuombea sana.

Itoshe kusema baada ya kurudi home milango ikafunguka sikukaa muda nikapata kazi.

ITAENDELEA...

Hapo kwenye kudunga maombi na wazazi kumenitoa chozi!

Amini nakuambia, wazazi wanazo funguo za ustawi wa watoto wao. Kongole mkuu
 
Inamaana kwenye huo mtandao aliomo Irene demu wa kibongo maarufu aliemo ni HAMISA MOBETO! tu!!!.....

Maana ndie Demu aliekuwa akitoka na Rozay...
Hata majuzi tu 2021 walionekana na MnyamweZ rozay batani Dubai.
Na ameshasema kuwa wanaume wanaomtongoza Ni wa nje tu so Hana time na wa ndani, or Bei iko juu mno. Kama vipi una namba yake ya mobeto nitupie hapa
 
Back
Top Bottom