Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 4

Wakati naanza hii kazi Mama Junior alikua hayupo home, alikua kwao ni mimi ambaye nilimpa ruhusa aende akapumzishe akili baada ya dada wa kazi kwenda kwao. Niliona mazingira ya kubaki peke yake na mtoto bila mtu wa kumsaidia mke wangu angeteseka, uzuri kwao ni hapahapa dar. Mama Junior ni mwanamke ambaye ana wivu sana na mimi kiasi kwamba huwa anahisi mimi nachepuka, inshort niseme ni mwanamke ambaye ananipenda sana.

***
Naam! ilikua ni jumatatu tulivu sana, nikakurupuka kitandani kucheki muda saa 5 asubuhi. Wakati naangalia muda nakutana na mcd calls za kutosha, nikakutana na messages,

“Bro! Good morning, how you doing??” -Manuel
“I’m worried about you..”- Manuel

“Kaka habari yako, ni mimi maggy uliyenipeleka Airpot last week, nahitaji tuonane leo if possible”- 0712*********

“Bae! Kwanini hupokei simu zangu? Upo na nani?”- Mama Junior

Kabla sijajibu hizo message nikacheki missd calls

“Mama Junior, 6 “
“Manuel, 2”
“New number, 1”

Akili yangu ikawa inawaza nianze na nani kati ya hao, nikaanza kupigia Manuel kwanza akapokea nikamshukuru kwa kampani ya pale Kidimbwi akanambia kama ntapata nafasi nipitie pale Sea cliff kuna kazi nyingine ya kufanya.

Nikampigia simu Maggy tukaongea akanambia anytime ukifika Posta utanicheki nikamwambia “sawa”.

Nikapiga simu namba ngeni, kupokea alikua ni mama mmoja hivi nilishawai mpakia, na yeye anafanyia kazi moja ya bank pale Posta, Azikiwe.

Nikampigia simu Mama Junior niliamua awe wa mwisho sababu namfahamu vzr, na kwa kitendo cha kutopokea simu zake na kujibu messages nilijua lazima atakua kafura.

Nikampigia simu … [emoji338]

Mama Junior: “Umeshaagana na wanawake zako ndo umeona sasa unitafute kwa muda wako…, Unaweza kunambia jana ulikua wapi? na umelala wapi?”

Mimi: “ Jamani… ndo salamu hiyo?”

Mama Junior: “ Baba Junior tafadhali naomba maelezo…, mwezi umepita hata kuja kutuona na mwanao hutaki, una mambo yako wewe”

Mimi: “ Mke wangu usifike huko… jana nilikua na washikaji walinipa mwaliko, nikaingia night sana, hapa ndo naamka…, hata hvo nimekupigia nikupe habari njema”

Mama J: “Habari zipi..?”

Mimi: “Mwezi wa 12 huu Christmas nataka wewe na Junior mpendeze, piga hesabu na gharama zote then Nitumie”. Hapa nilikua nimemmaliza hata hasira zikaisha kabisa.

Mama J: “Sawa haina shida, I love you. Takecare”


Nikaamka kitandani kwenda kuoga, kwanza nilikua na mahangover ya pombe, nilipeleka backet 2 za heineken sio mchezo, na ukicheki mpaka muda huo sijapata hata soup, kwa wanywaji nadhani huwa mnajua. Dizaini kama nikawa na kauvivu ka kwenda mzigoni, lakini nikasema hapana lazima niende nipige hata kidogo then nionane na hawa watu.

Nilikua napambana sana kutafuta wateja wa private ili niwe na uhakika wa kazi na kupata pesa nyingi. “Nakumbuka Dullah alinisisitiza sana nijitahid sana kuwa na wateja wa private maana hawa ndo kila kitu, App sometimes zinazingua kuna siku kazi zinakua ngumu”. Mfano kwa kila trip kamisheni ya Uber/bolt ni 25% yaani kama ubao unasoma 100,000/= hapo 25,000 ni yao yako 75,000, kwenye hio 75 hujatoa cost za mafuta, parking fee nknk. Ili uweze kupata faida ya angalau 30,000 kwa siku inabidi uingize kuanzia 70,000.

Kuna wale ambao wanaendesha kwa mikataba unakuta kwa bossy anapeleka 25,000-30,000, inabdi apambane kwa siku apate kuanzia 100,000/=, hapo unaona inabdi akili ya ziada sana.

********
Nikaingia mzigoni kama kawaida nikapiga mzigo nikapata mteja wa kwenda pale Aga khan, baada ya kumshusha mteja nikawaza kuonana na Maggy nijue anaishu gani na pia nikakumbuka na yule mama wa azikiwe. Nikasema leo ni “Two birds one stone” napiga ndege wa2 kwa jiwe moja.

Nikamvutia waya Maggy, akanilekeza ofisi yake ni pale Golden Jubilee tower, bhasi mimi nikasogea mpaka pale mtaa wa Ohio nikapark gari oppositie na Golden jubilee. Nikamtext [emoji187] ilikua saa inasoma 9 kasoro mchana.

MIMI: “hey boss niko around”

Maggy: “Umepark wapi?”

Mimi: “Opposite hapa na jubilee, near kibanda cha Mpesa”

Maggy: “Ok nakuja soon, bossy!”

Haikuchukua dakika 10 Maggy akawa amefika kwenye eneo la tukio tayari, nikamsalimia na nikamsifia “you look great”, akatabamu akanambia “nawe pia”.

“So tunafanyia haya maongezi hapahapa, au ndani ya gari??”. Nilimwuliza

Akanambia sijala kwanini tusiende cafe? nikakumbuka hata mimi nilikua sijala chakula cha maana toka niamke, lakini nilikua sisikii njaa.

Nilikokuwa nimepark gari kwa nyuma yake au tusema opposite na “IT plaza” kulikuwa na cafe pale, bhs ndo tuliingia pale, mimi nikaagiza “dona choma” yeye akaagiza “kiepe yai, kuku”. Hiki kicafe ndo niliingia kwa mara ya kwanza, ofcourse nilikipenda wanachakula kitamu afu ni cheap, so kila nikija Posta hapa ndo nilikua nakula msosi.

Tukaanza pale kupiga story sana, Maggy alikuwa anaongea “mimi usafiri wangu ni Uber kila siku asbh pamoja na kurudi so kama upo tayari uwe unakuja asubuhi kunichukua unanipeleka ofisn then jion sa12 unanirudisha home. Pia ninakazi nyingi sana huwa zinatokea hata za siku nzima, Uber wengi gari zao sio safi na wateja wetu wengi ni foreigners, jinsi ulivyo smart na gari yako safi ntakua na amani na wateja wangu.

Nikamwuliza before mimi ulikua unafanyaje? Akanambia nilikua namtu nafanya naye kazi ila hazingatii usafi wa gari. Mimi nikatabasamu pale,

Mimi nikamwambia suala la kuja kukuchukua niachie nilifanyie kazi ntakucheki badae tuyajenge kama tutaafikiana tutafanya kazi lakini suala la wateja wako mimi sina shida hili naweza kupa jibu la direct hapahapa, nikamwambia hao muda wowote nipigie simu hata Arusha tunakwenda, hata kama unasafari nje ya mkoa mim sina tatizo.

Tukaagana pale huku nikimwahidi badae nitamtafuta, palepale nikamcheki mama yangu wa azikiwe, Palepale nikampigia simu lakini hakupokea ghafla ikaingia text “Call you letter”, nikamtext back chap “niko Posta”, akanijibu “Na kikao nitakupigia nikitoka”. Nikamjibu “Ok”.

Kucheki muda ilikua saa 10 kasoro tayari nikasema acha nimsubiri huyu mama then nielekee Masaki kuonana na Manuel. Ukweli nilikuwa natamani sana kupiga story na Manuel maana ni mtu ambaye alitokea kunikubali sana afu hakuwa na roho ya kinyongo ni mtu poa sana. Nilitamani kuongea naye mengi kuhusu Siwtzerland ( “Switzerland ni moja ya nchi nzuri sana kwa foreigners, kusoma, hata upatikanaji kazi”). Plan zangu kubwa ni kutengeneza connection nijue namna kufika kule na masuala mengine.

Wakati narudi kwenye gari yangu nikaona kuna Uber kibao wametega around na mimi, nikaona kikundi cha washikaji wakipiga story nikajua wale ni Uber, bhs nikasogea pale kujumuika na mimi.


Matajiri kwema? za kazi?, wote wakajibu nikawaambia bila shaka nyinyi ni Uber, ndomana namimi nimesogea hapa nimevutiwa na story. Kwa muda mfupi tukawa kama watu ambao tunajuana kitambo.

Unajua story za madereva wa Uber nyingi ni kuhusu madem tu[emoji3][emoji3], ukiona Uber wamekaa kwenye vijiwe vyao hizo ndo story zo kubwa huji kuta wakipiga story za maendeleo hata siku moja. Inshort madem wanaliwa sana na madereva wa Uber.

Pale Posta najuana sana na maderva wa Uber wengi wananiitaga “Wakishua” sababu mimi muda wote niko smart na gari nayo ipo smart, hii ilipelekea kupendwa sana wa abiria.

********
Tulikua watu 6 pale lakini kadri muda ulivyokua ukienda na wahuni walizidi kupungua ikafika stage tukabaki wawili,, “Request ndo zilikua zinatupunguza maana kuanzia saa 11 jion ni muda ambao request zinakua nyingi sana Posta, demand ya ya Uber inakua juu sana hata rate ya nauli inakua juu sana.

Mpaka saa 11 naona kimya yule mama wa Azikiwe hajanitafuta, sikutaka kumtafuta kwanza nitaonekana kama mimi ndo nashida, then ataniona cheap sana, kwanza kitendo cha kumsubiri mpaka saa11 nilijiona fala sana.

Nika switch online App yangu nikaset destination ya kwenda Sea cliff, “ipo hivi kama unataka mteja wa kwenda Masaki au Posta, bhs kwenye App unaset destination, hivyo utapata request zinazoelekea usawa huo inaweza isiwe exactly point ila atlist inasaidia”. So kitendo cha kuweka destinationa haikuchukua muda nikapata request ya mteja alikua anaelekea Coral beach.

Nikamshusha customer pale Coral beach nikachukua uelekeo wa Sea cliff, kutoka Coral mpaka Seacliff sio mbali sana, ilikua chap tu niko pale tayari. “Wakati nakaribia Coral nilikua nishampanga tayari Manuel so akanambia nitamkuta pale Karambezi”.

Nikafika pale Karambezi nikamzoom Manuel kwa mbali ofcourse hapakua na watu wengi sana palikua kawaida tu. Tukasalimiana pale story zikaanza, story kubwa nilikua namwuliza namna ya kufika Switzerland na ishu za kazi especially unskilled jobs. “Njia rahisi ya kuingia chap ni scholarship au kusoma, hapo ni rahisi sana ila kama unakua umepata kazi bhasi mwajiri wako akupambanie visa japo huwa inachukua muda sana na gharama yake kubwa. Kama unataka kuingia wewe apply chuo, I recommend you to use this way, ukishafika ukaanza masomo kama mastars ni mwaka mmoja tu umemaliza, ukiwa unasoma kuna mishe nyingi sana za kufanya kule kama viwandani, mashambani, migahawani nknk” Manuel alikua akiongea.

Manuel mbinu nyingine ya kutumia ya haraka bhasi uoe mswiss hapo unapewa na uraia kabisa, “Nigerians wanatumia sana hii mbinu, wanaoa sana wamama watu wazima” nilicheka sana.

Ishu nyingine kubwa pia jumatano na alhamis nitakua na ratiba ya kutembelea vituo vya watoto yatima kwa Dar, ijumaa tutakwenda kibaha na Bagamoyo, ila kwa Jumamosi utaangalia wapi unatupeleka, then J2 tutaondoka kurudi Switzerland. Manuel alikua akiongea.

Akanionesha vituo tutakavyotembelea nikaona kuna sinza, tegeta, bunju, Kunduchi, Kimara, Kigamboni. Tukakubaliana 600,000/= ( 200,000/= per day) kuhusu jumamosi nikamwambia ntawapa offa, muda ule tulikua tunaikimbiza “pearly bay wine”. Nikamwambia bro jana dizaini kama haukuwa free kule Kidimbwi, alicheka sana akanambia “bro! next time gonna be lit,”. Tukaagana pale.

“The way nilivyomwona Manuel nilihisi kama mtu wa madem sana” huko mbele mtaona.

Before sijatoka pale Karambezi mama yetu alikua kanipigia simu ila sikupokea, so wakati natoka ilikua ishapita saa tayari, na saa yangu ilikua inaonesha ni saa 19:05. Nikampigia simu akanambia karudi home kama vipi niende kwake haina shida, “nikaona mama anaongea ujinga, yaani mimi niende kwake??”. Nikamwambia mama haiwezekani kama muhimu sana tuonane pale Raibow , huyu mama alikua anakaa kule chini Mbezi Beach karibu na Rainbow. “So hakukataa akakubali tuonane pale tuongee”.

Nikawa nawaza huyu mama anataka nini kwangu? Nikachoma mafuta mpaka pale Rainbow mbili kasoro dakika nikawa pale, wakati niko Kawe alikua kanijulisha kafika tayari.

Kufika pale nikaingia ndani nikamkuta amekaa anakunywa savannah, duu! nilijisemea huyu mama hatari au ndo anaongeza nyege!??.

Mimi: Habari yako bossy

Mama: Salama tu, ndo unatoka mishemishe?

Mimi: kama unavyoona, umeniweka sana pale Posta

Mama: jamani pole, kwani ulikua unanisubiri?!

Mimi: Ndio, maana hukusema niondoke! anyway nimeitikia wito bossy wangu, nakusikiliza, what’s a deal?

Mama! Ninataka asubuhi uwe unanichukua na mwanangu, lakini mtoto unamwacha pale mikocheni Warioba( hii shule ipo karibu na msikiti wa mwinyi).

Mimi: Sawa mama, sasa mbona hili lilikuwa lakuongea kwenye simu tu na tukamaliza, au ulitaka kuniona??( nilikua nimekazia macho)

Mama: Huku akicheka, unaonekana mpole sana ila ni mwongeaji sana, unavituko sana.

Mimi: Una watoto wangapi?

Mama: Wawili tu, wakwanza wa kike yuko form 5, wapili yuko standard 3, wote wa kike.

Mimi: wow! am luckiest man, huyo wa form 5 nitunzie ntakua mkwe wako.

Mama: utanibakia mwanangu bure!!

Mimi: So unakunywa beer usiku huu, baba watoto akirudi inakuaje??

Mama: Mume namtolea wapi mimi?, naishi na wanangu tu. Unajua wewe haunywi kama unanichora hapa!

Mimi: Hilo tu usijali, siku ntakupeleka Kidimbwi tukanywe wote.

Mama: Huku akicheka, unavituko sana mimi nishachuja tayari huko wanaenda damu mbichi.

Mimi: unaweza kujiona umechuja ila mimi bado nakuona upo hot sana.

“Huyu ni mama wa kichaga mweupe anashepu nzuri, ni mama kijana afu anajipenda sana huyu age yake anavyoonekana ni 40s ni mama kijana.

Mama: huku akicheka, we kaka unavitukoa sana,

Kwa muda tulio kaa na mama nilikua nishamcontol kwa maongezi na kila kitu kama ningetupia voko angeingia king.

Tukakubaliana pale atanilipa 12,000 kwa trip ila nikamwambia nitaanza jumatatu ya week inayokuja, mama hakuwa na shida kabisa.

“Unajua hawa wateja sometimes nilikua nawapa utani ili kuendelea kuwasogeza karibu na awe huru, haipendezi muda wote kuwa kauzu.”(Kanuni ni kwamba kama mteja ni mwongeaji na wewe kuwa mwongeaji, kama kauzu na wewe kuwa kauzu, hii ndo iliku principle yangu).

*****
Nikatoka pale na furaha sana, hesabu kichwani ni kumalizana ma Maggy hapo tayari na vichwa 2 na vyote vinakwenda Posta. Ilikua saa 3 usiku tayari nikamtext Maggy, palepale akani text back ni kama alikua anasubiri text yangu. Nikampandia hewani nikamwuliza anakaa Mikocheni gani akanambia karibu na shule ya Alpha. Nikamwambia nitakuwa nampeleka tu ila kurudi kama nitakua around nitakuwa namcheki, hakuwa na noma akakubali, tukakubaliana 10,000.

Mnajua kwanini sikutaka kazi ya kumpeleka na kumrudisha? niliwaza nitakua mtumwa, kwanza utakua na stress upo zako mbweni huko afu sa11 umfuate mteja Posta unakua mtumwa, sikutaka hii kitu kabisa, au jambo lingine muda wa kwenda kazini unaeleweka wakati wa kurudi hauleweki, sikutaka kuchoma mahindi bila sababu ya msingi.

Palepale nikapata idea ya kutengeneza mkataba wa kazi, nikachukua laptop nikadizaini mkataba wangu vizuri kabisa, nikaweka mpaka sehem ya kusaini mwanasheria, sikutaka masikhara na kazi kabisa, na pia nilitaka wateja wanione niko serious.

******
Jumatano ilifika huyo nikaenda Seacliff pale kumchukua Manuel lakini this time alikua yeye na Alex tu, tukasalimiana pale. Tulielekea kwenye hivyo vituo walikua wanafanya research zao na kupiga picha. Tulitembelea vituo vyote tukamaliza kwenye sa11 jioni, nikawarudisha mimi nikaendelea na kazi yangu. Kesho yake tukatembelea vituo vingine ile kazi tuliimaliza jioni pia.

Ijumaa ndo siku ya kwenda kibaha na Bagamoyo, kama kawaida tukaenda huko wakafanya mambo yao hii siku tulirudi usiku sana, nikawadrop pale Seacliff lakini Manuel akaomba tukapate dinner then niondoke, sikukataa tukaelekea Karambezi pale.

Ile tunaingia mlango mkubwa wa kwenda Karambezi nakutana na Ex wangu, Tangu nimemaliza chuo sikuwai onana naye ilikua ishapita miaka 3 na yeye alikua 2nd yr that time, nilikua nimemwacha mwaka 1 mbele.

Yeye ndo aliyeniona akaniita jina langu “INSIDER”, Manuel ndo aliyeskia wakati akiniita. Bro somebody is calling you, kucheki namwona Angel (code), wow akaja akanihug kwa nguvu, mpaka Manuel akashangaa!!!

Nilishangaa sana kukutana naye pale ofcourse alikua na rafiki yake afu walikua wakitoka, huyu alikua dem wangu wa chuo enzi hizo baada ya kumaliza chuo aliniacha asee!!, this time tunakutana nimebadilika, nimenawiri,afu niko na wazungu.

Akaomba namba yangu sikutaka kumpa, nikamwambia anipe yake ntamcheki…..

Angel ni mwanamke ambaye nilianza naye mahusiano wakati niko chuo, so wakati wao wanaanza first year mimi ndo nilikutana naye na kuweka ukaribu hatimae tukaanza mahusiano. Tulidumu kwa kipindi chote cha miaka 2, tulipendana sana mpaka masela zangu wa chuo walikua wanaamini huyu mrembo namwoa. Kilichotokea baada ya kumaliza chuo zilianza sababu, mara hapokei simu, ubusy mwingi, nikaanza pata report kutoka kwa masela anaonekana na mwanaume uyo moja kila maeneo, mimi kama mwanaume nikajua hapa sina mtu, nika move on.

********
Tuliagana ma Manuel pale Seacliff ili asubuhi niwai kuwabeba twende misele, ile jumamosi asubuhi by saa 3 nilikua pale. Wakatoka wote hao tukaanza safari plan yetu tuanze na “Ununio beach”, Manuel akaomba twende na “Haile Selasie Road” kuna vitu akanunue vya asili. Sehemu yenyewe tuliyokwenda ni karibu na filling station ya Puma au kama unatokea “Samaki samaki” kuna barabara inakunja kulia kama unakwenda CCBRT, sasa kwenye ile kona kushoto kuna supermarket inaitwa “Shrijee”, sasa pembeni ya supermarket kuna jamaa wanauzaga vitu vya asili kama, picha, vinyago, kacha nknk.

Manuel aliingia na ndugu zake wakanunua picha, vinyago, kacha kuna vingine waliweka kwenye mfuko vingi. Wakati tunatoka pale akanambia tupitie pale Puma, akamwambia dada ajaze full tank, “nilivyosikia full tank, nilihisi moyo wangu kupasuka kwa furaha”, huyu Manuel anaroho nzuri sana, ni moja wa wazungu wenye roho nzuri sana.

Kwenye saa 5 tulikua tuko pale Ununio Beach Ofcoz walipapenda sana na ile mandhari walienjoy sana, mimi ndo nilikua kama director pale. Nakumbuka tulikwenda “Mahaba Beach” kule kulikua kuna samaki wengi sana wabichi, wavuvi ndo kama centre yao, bhs tulichoma sana samaki pale.

Tulitoka pale mchana tunaenda “Coco beach” tukala sana mihogo pale na mishikaki, usiku ilikua imefika muda unagonga kwenye moja kasoro, Manuel akasema twende tukapate dinner moja ya cafe nzuri pale Masaki afu tukamalize bata letu Samaki Samaki. “Wakati tunapita pale samaki samaki asubuhi Manuel alipaona akanambia badae tunakuja hapa”.

Nikawadrop wajiandae then tukaenda pale “The tribe” tukapata dinner hao tukamalizia pale Samaki samaki. Kama mnavyojua vibe la Samaki samaki tulienjoy sana lakini hawakukaa sana maana jumapili ndo walikua wanatakiwa kuondoka. Nikawarudisha Seacliff na mimi nikarudi kulala ili asubuhi mapema niwe pale kuwachukua kuwapeleka Airpot.

Naam asubuhi mapema saa 2 na madakika nilikua pale, wao walikua wanatakiwa “kuchek in “ pale Airpot 10:00 AM. Nikaingiza gari mle ndani Seacliff karibu na mlango wa kuingilia tukapark vitu hao safari ya Airpot, ndani ya nusu saa tulikua tumefika Termninal 3, hakukua na foleni kabisa.

Tulipiga picha za pamoja pale kama ukumbusho, wale wazungu walifurahi sana, nilipata nafasi ya kuongea na Sophie lakini sikuchukua namba nikaopotezea.

Nikawa escot mpaka ndani pale tunaongea sana na Manuel akanambia “You are my brother here in Tanzania, I’ll never stop calling you bro!”, alitoa noti 2 za Dolla 100 akanipa, nilimkatalia akanambia “bro hizi pesa sio zako nampa Junior, mfikishie”. Pale nikaishiwa pozi ikabidi nipokeee tukapeana hug na mimi nikatoka zangu kurudi parking ili niondoke.

Niseme kwamba kukutana kwangu na Manuel ilikua baraka sana kwani ndani ya week 2 niliingiza pesa nyingi sana na pia niliishi maisha mazuri sana. Nikapiga hesabu ndani ya siku ambazo nimefanya nao kazi nilikua nimeingiza $1,050 na bado alikua ananipa offa za lunch, dinner nknk.

Nikawaza hapa leo niende kwa Mama J nikamsalimie na Junior maana ilikua inakwenda mwezi wa 2 hatujaonana live zaidi ya video call tu. Nikasema hizi pesa nimepewa kwaajili ya junior acha nikanunue baadhi ya mazaga niwapelekee itakayobaki ntampa mama J.

Nikaingia Mlimani city nikanunua baadhi ya vitu nikaelekea boko kwenda kuiona familia yangu, ile nimeingia kwenye gari nikamkumbuka Angel, nikasema ngoja nimpigie maana alionesha anahamu sana ya kuongea na mimi, nikachukua simu ili nimpigie..

ITAENDELEA

Ntarudi
 
EPISODE 5

Kutokana na lile tukio la kukutana na Angel, ndugu yetu Manuel kumbe alikua akilitizama kwa makini sana, aliniuliza ili apate ubuyu, nikampa story kuhusu mimi na Angel. Manuel akanambia uyo dada the way nimemwona ni anakutaka, cha kukushauri achana naye kabisa,
EX’s are toxic my brother especially in a relationships, mara 100 utembee na mtu mwingine lakini sio Ex.

“Vipi ulimpa namba yako” Manuel aliuliza, nikamwambia hapana, akanambia bro you’re genius.

Niliamua kufuta namba ya Angel na sikutaka kuweka ukaribu naye kabisa, mtu aliyekuacha unapata wapi nguvu ya kumtafuta??, bora ningemwacha mimi hapo sawa, nilikua nikijiambia moyoni.

Wakati bado niko parking pale ghafla simu ikaanxa kuita, kucheki ni Maggy nikapokea alikua anasisitiza na kukumbushia suala letu tulilokubaliana, nikamwakikishia hakuna jambo litakalo haribika.

Kumbuka hapo nina wateja wawili na wote wanaelelea Posta, nikajiambia hakuna shida nitawapanga mapema kila mtu ajue atakua na mwenzie.

*****

Nikawasili pale kwa wakwe nikamkuta Mama mkwe, dada zake, wadogo zake, tukasalimiana, akanikaribisha ndani. Nikamsalimia mtoto, ukweli hakuna raha ambayo wanaume huwa tunapata kama ukiwa na mtoto ambaye mnafanana, kuna kafeeling huwa tunakapata sana (Nikimwangalia Junior na mimi ni copyright). Sikukaa sana pale maana mimi ni mtu ambaye huwa sipendelei kwenda mara kwa mara ukweni au kukaa sana.

Nikaaga pale, mama J tulikua tumeongozana mpaka kwenye gari, nikampa cash 300k hii ni ile pesa ya Manuel, baada ya kununua mazaga hio ndo ilibaki, nikaona nimpe mama yake. Nikamwambia pesa ilikotoka, maana nilijua wazungu huwa hawasahau na wanapenda uaminifu sana, ipo siku atauliza tu.

Baada ya pale nikasema acha nirudi home nikalale niweke mambo sawa kwaajili ya kesho.

Nikampigia simu Maggy na Mama ( tumwite mama wawili(2)) nikawapa mpango mzima kuhusu mkataba na kila mmoja nikamtumia soft copy. Sasa pale home nilikua na jamaa yangu mwanasheria nikampa hardcopy anipigie mhuri.

*****
Ilikua jumatatu njema kabisa nikaamka mapema sana, nikajiandaa vizuri kabisa nikapulizia na unyunyu wangu huyo nikawasha chombo kuingia mzigoni, ilikua 06:25 asubuhi nilikua tayari kwa mama wawili. Mimi nilikua nakaa mbezi beach shule so haikua mbali lakini huyu mama sikumwambia nakokaa.

Nimefika pale nikampigia uzuri na yeye alikua tayari na mtoto wake, Nikamsalimia, akanambia uko sharp sana. Nikamdrop mwanaye pale shuleni, nikamwambia kuna mtu pia tunamchukua pale Alpha uzuri Maggy alikua yuko pale barabarani nikamchukua akaja akaa mbele, Mama wawili siku hiyo alikaa nyuma na mwanae.

Nikawadrop pale Posta, nilianza na Mama wawili pale Azikiwe nikampa mkataba wake nikamwambia utausoma afu utajaza, nikasogea mpaka pale Golden nikamdrop Maggy naye nikampa mkataba akanambia ntakucheki kaka, nikamwambia sawa bossy wangu.

Kukamilika kwa deal la Maggy & Mama wawili nikawa na uhakika wa kuingiza 484,000/= kwa mwezi, nikajisemea mwanzo mzuri.

Nikapark gari yangu palepale ambapo nilimiti na Maggy nikiwa nasubiri request, saa yangu ilikua inaonesha ni saa 2 mbili tayari na madakika yamekata. Nilikua nimeshuka kwenye gari baada ya kumwona dada wa TARURA na kimashine chake akisogea upande wa gari yangu, nikawa namzingua , “Dada mapema hivi unataka kuchora subiri kidogo kukuche” kwanza Kaka gari yako inadaiwa 5,000 inabdi ulipe.

Hawa dada wa TARURA walikua wananikera sana yaani usipark gari pembeni chap kashakuja kuchora, sasa mimi nilikuaga nazinguana nao sana.

Muda uleule nikapata request ilikua location inaonesha customer yuko pale Serena Hotel, akanitext via App, gari yako ina AC? Nikamjibu ndiyo, akanambia njoo chap hapa Serena. Kufika pale namwona mfanyakazi wa pale anatoka, ndo yeye alikuwa karequest akaniuliza wewe ndo INSIDER?, nikamwambia ndo mimi, Ok subir anakuja, Park vizuri na wengine waweze kupita.

Ndani ya dakika 5 akafika mzee, tuseme ni mzee kijana, “kijana wangu hujambo?”…sijambo mzee pole na majukumu “salama sana” si umeona tunakwenda Ununio, nikamwambia sawa mzee wangu.

Nikampeleka mpaka Ununio nikamshusha nikamsaidia kutoa bag lake, sasa kijana itabid unipe namba yako ntakupigia, sawa mzee haina shida huyo nikaondoka.

Nikadrive mpaka pale Ununio shuleni nilikua najua pale lazima nikutane na wahuni na pale huwa ndo kijiwe cha Uber. Nikawa nimechili pale huku nikicheza draft na masela, kila nilikokua natega au kila kijiwe bhasi nilikua najitahidi sana niwe na ukaribu na watu wa eneo hilo.

Nikacheki whatsapp chats nikakuta Manuel kanitext “Hey bro! Good morning, we arrived safely, I’ll call you later”,.

Hii siku biashara kwangu haikuniendea vizuri nakumbuka nilikaa pale mpaka saa 6 mchana ndo nikaja kupata request mteja alikua anakwenda mwenge.

*********
Kazi ya kuwachukua akina Maggy ilikua ikiendelea vizuri na wote walikua washarudisha mikataba yangu ile jumanne wakati mama anarudisha mkataba alinambia wewe kaka upo serious asee, mpaka umegonga mhuri wa mwanasheria nimekuvulia kofia…” nikamwambia mama hii ni ofisi lazima niwe serious kama nimeandaa mkataba wa kijinga ukanikimbia itakuaje??”. Upande wa Maggy yeye alifurahi jinsi navyofanya kazi serious, Maggy ni dada ambaye nilikua nikimwona yuko serious sana na maisha.

Licha ya kuwapa mkataba tu pia niliomba copy za vitambulisho vyao, na kwenye mkataba wangu vipengele muhimu nilivyoweka ni pamoja na, mkataba ulikua wa siku 22 kwa mwezi toa jumamosi na jumapili


*****

Hii tulikua tumeanza week ya Christmas ukweli ni kwamba kipindi hiki kazi zilikua nyingi sana na pesa ilikua inaonekana, sasa nakumbuka kuna tukio lilinitokea siwezi kulisahau kwakweli.

Ilikua ni jumatano usiku nilikua nimemchukua dada mmoja hivi kutoka pale Slipway Masaki ilikua ni saa 3 usiku alikua anaelekea Sinza, sasa wakati nimefika anapokaa nika end trip na nauli ilikuja 10,000 tu. Dada akanambia kaka mimi sina hela tumegombana na boyfriend wangu hajanipa hela, nikamwambia sasa mbona hukusema mapema kama huna?, umenyamaza kimya mpaka tunafika hapa.

Nikamwambia dada wewe sema leo biashara imekua ngumu ila usianze kudanganya hapa mimi mzoefu naelewa, nikamwambia sasa naipataje hela yangu?, nikupeleke lodge au humuhumu kwenye gari??…. Kwanza lodge mbali ntapoteza pesa zangu namalizana na wewe hapahapa, mvua nguo chap (huku nimemkazia macho)…. Eeh dada si kweli akaanza kufungua kifungo cha pant yake. Dada stop! mimi sio kama wanaume wengine hii kwangu ni ofisi naomba nitumie hiyo pesa kwenye nmba yangu kama utanidhulumu ni wewe.

Kaka ahsante ntakutumia una roho nzuri sana, nisave nani jina lako nikamwambia wewe utavyoona sawa, huyo nikasepa. Kesho yake dada kweli akatuma pesa, akanipigia simu kaka nimetuma, nikamwambia hapo umetisha sasa tuongee biashara wewe nakupataje?? anytime wewe ukiwa tayari [emoji3][emoji3], nikajisemea kwa hali hii madereva wa Uber tutakufa kwa ngoma, hata maendeleo tutasahau.

*******
Ilikua imeshakata week yule mzee ambaye nilimchukua pale serena hotel kumpeleka Ununio alinipigia simu, ilikua ni 24/12 usiku,

[emoji338]….

Mzee: kijana naomba kesho uje pale nyumbani, si unapakumbuka??,

Mimi: ndio mzee napakumbuka,

Mzee: bhasi kesho uje saa 3 asubuhi, tutakwenda Mbweni na Kigamboni, gharama zako zikoje?

Mimi: Mzee inategemea na root zako ila gharama zangu kwa siku kutoka asubuhi- Jion 18:00 ni 150,000/= na kuendelea ila maongezi yapo.

Mzee: kijana gharama zako ziko juu sana, punguza kidogo

Mimi: mzee kipindi hiki cha sikukuu rate za nauli zimeongezeka sana na pia kumbuka nakua na wewe siku nzima, top kabisa 120,000/=

Mzee: Haina shida bhasi kesho mapema uwai kijana, nakusisitiza

Mimi: haina shida mzee wangu, [emoji3513]

Ilikua ni Christmas afu sasa ilikua ni jumamosi sasa hii ni siku ambayo nilikua na miadi na Mzee. Nilifika mapema sana pale Ununio kama tulivyokubaliana, mlinzi akanifungulia geti nikawa namsubiri pale parking. Mzee parking yake ilikua na VX na BMW X5, nikasema Kuna watu wana hela asee, kwanza nyumba yenyewe ni ya kibabe.

Baada ya nusu saa mzee akaja pale na bag dogo la kuvuta, nikaliweka kwenye buti, safari yetu ilikua inaanzia kwenda Mbweni. Mzee mbweni alikua anakagua nyumba yake pale, tulikaa kama saa 2 hivi tukatoka kuelekekea Kigamboni.

Saa 7 tulikua kigamboni sikumbuki panaitwaje ila ni mbele ya Pweza beach, kufika pale ilikua ni apartment ya nyumba 3 ndani. Mzee akanambia Kigamboni tunakwenda kwa mchepuko wake atakaa mpaka jioni afu tutarudi Ununio ana wageni badae.

Baada ya kufika akatoka dada pale kumpokea mzee (mchepuko wake), baada ya kuuchunguza kwa makini mchepuko wa Mzee, nikajisemea Mzee anajua kuchagua. Mzee akanipa 30k, akanambia niende nakojua mimi ila 17:00 ontime niwe pale, kumchukua, nikasema acha niende Pweza Beach nikapoteze muda tu.

Mnajua hizi kazi za Uber sometimes ni za ki**nge sana, naonaga hazinaga utofauti na utumwa, ndomana mimi nilikua sibembelezi sana customer wa kufanya naye kazi kama hafikii rate zangu namwacha. Nilikua najiamini course nilikua napata kazi nyingi so sikua na shida na tamaa za kijinga.

Nikachili pale Pweza beach nikasema simpigii Mzee simu mpaka anicheki mwenyewe, kucheki muda ilikua saa 11 na madakika kadhaa tayari hapo mzee hajanicheki, nikasema acha nisubiri mpaka ifike 17:30 nimpandie hewan, japo alisisitiza sana muda huo niwe pale.

Muda ukawa umefika 17:30 nikaona bado kimya nikasema nimpigie au niache?? Lakini nikawa najiuliza mwenyewe kama nayeye anasubiri nimpigie??. Nikampigia simu lakini cha ajabu naambiwa namba haipatikani, nikarudia tena namba haipatikani, nikaamua kwenda tu kumfuata.

Nafika pale lakini gate likikua limefungwa na hakuna mtu around wa kunifungulia, nikaanza kujiuliza kwamba mzee kapelekewa moto sana?, nikashuka kwa gari, nikagonga geti lakini hollaa! hakuna anayekuja kufungua.

Hii siku ilikua jumamosi afu Christmas demand ya usafiri ilikua juu sana na nauli pia zilikua juu sana licha ya kumaliza kazi ya mzee nilitamani sana niingie barabarani niendelee na mzigo. Dullah before alikua kanicheki whatsapp afu kanitumia ubao wake, yaani mpaka sa10 mchana alikua kashakusanya 120k, niliingiwa na roho ya wivu.

“Kipindi kama hichi cha sikukuu Uber huwa tunaringa sana sehemu ambayo haina manufaa huwa hatuendi maana request zinakua nyingi sana.”

Wakati nikiendelea kutafakari pale nje getini, Mama J akaanza kunipigia simu, nikakumbuka aliniambia niende kwao kuna chakula cha pamoja kama mimi moja ya familia natakiwa niende na baba yake (baba mkwe) atakuwepo, “nilikumbaliaga kuwa nitakwenda”. Nikapokea simu yake akanambia mbona mpaka sasa hujaja?, sikutaka ugomvi nikamwambia ntakuja badae wewe usiwe na wasiwasi.

******

Ilikua ishafika 12 na madakika tayari ndo kuna dada alikua anatoka, nikamwuliza kama ana mazoea na yule mchepuko wa mzee, akanambia sina. Nikaingiza gari ndani ikabidi nigonge mlango kama dk 3 dada akatoka, nikamwambia mzee hapatikani na alinambia 17:00 niwe hapa ontime. Dada akanambia mzee kalala toka saa 10, nikajikuta nataka kucheka, nikamwambia dada amwamshe tuondoke maana tushachelewa tayari.

Baada ya dk 15 mzee alikua tayari katoka kwaajili ya safari, nikamwambia mzee nilikua nasubiri unipigie lakini nikaona kimya, kukupigia hupatikani akanmbia bhs dada alizima simu yangu, kucheki kweli simu ilikua imezimwa. Mzee akaniomba tuondoke chap maana saa 1 anawageni muda huo ilikua sa1 kasoro tayari.

Tukatoka pale Kigamboni lakini barabarani kulikuwa na foleni sana tukajikuta tunafika Ununio saa 3 kasoro, mzee akanipa pesa zangu akanambia atakuwa ananicheki, nikamwambia haina shida.

Muda huo nilikua nishawasha App yangu muda sana nasubiri request, haikuchukua muda niakapata request ya kwenda Airpot, ile nime accept tu, ni kama dada alikua anashida sana ya usafiri palepale akapiga simu, “kaka naona haupo mbali na mimi,please njoo haraka nachelewa”. Ofcourse alikua mtaa wa pili unaofuata, nikamkuta yuko nje getini tayari, ile nashuka dada anambia yaani kaka kama bahati leo usafiri wa shida sana, nikamwambia dada hujui leo ni sikukuu??

Tukatoka hapo chap kuelekea JNIA so dada alikua na haraka sana, alikua anaomba nikimbize gari, ni kwamba dada alikua anaondoka na ndege ya 22:30 afu alikua anatakiwa kuchek in 20:30 na muda huo tunaondoka ilikua ni 21:45. Nikamwambia dada mimi huwa siendeshagi zaidi ya 60km/hr kwa mjini humu, kutokana na kusema Uber zilikua za shida na mimi natambua hili nitakuwaisha ili uwai ndege, dada akashukuru.

Sikutaka kutumia Bagamoyo road maana nilijua kutakua na foleni tu watu wanakwenda mjini kula bata. Nilikua nazijua shortcuts baadhi ya njia so nilipita chini kwa chini nikaja kutokea Ununio, hii barabara niliyopita kipindi kile ilikua inatengenezwa lakni sahivi ina lami. Nikatembea chinichini kwa chini kufika kunduchi nikaingia na barabara inayopita cota za Police hao tukatokea kwa “Mwamnyange” nikaunga na Mwaikibaki road, hao Mikocheni nikaingia na barabara ya ubalozini ghafla tunajikuta tushafika namanga huyo nikaunga na “Alli Hassan Road”. Dada muda wote macho kwenye simu akiangalia muda huku aniangalia mimi starring navyopambana na Road.

Ilinichukua dk 40 kuingia JNIA terminal 3, dada alifurahi sana hakuamini kama angewai lakni bado alikua na wasiwasi kama kachelewa.

Vipi unaondoka na ndege gani?, KLM nikamwambia usiwe na wasiwasi umewai sana, nauli ilikuja 32,000 dada akanipa 40,000 nikataka mpa change akanambia keep it. Nikamsindikiza dada mpaka anaingia ndani mimi nikakaa pale nje kwenye vile vibaraza, “ Sheria za Airpot hauruhusiwi kukaa ndani ya gari”, haikuchukua dk 5 dada akanipigia simu kaka ahsante nimefanikiwa, namba yako nimesave ntakucheki nikirudi, nikamwambia sawa, safari njema.

Wakati nimekaa pale nje nikisubiri request nilikua napiga story na moja ya mlinzi wa pale, nilikua najaribu kila nakokwenda niwe na watu naowajua hata kama kuna jambo au msalaa nakuwa ba backup. Nilikua namuuliza jamaa kwanini Uber tunazinguliwa sana mle ndani, jamaa akanifungukia akanambia zile gari/tax za Airpot ni mradi wao na pia ni gari za wakubwa humu ndani, uwepo wenu nyie Uber umepelekea biashara zao kuwa mbaya. Hapo ndo nikajua kumbe ni biashara za wakubwa mle ndani ndomana kuna vita na madereva wa Uber.

Wakati story zikiendelea na jamaa nikapata request, kuwasiliana na mteja akanambia yuko Airpot pale Puma filling station, nikamwambia mteja mimi niko terminal 3 kutoka hapa si unajua lazima nilipie getin pale akasema hiyo 2,000 mimi ntakupa fanya chap mimi nachelewa.

“Huyu mlinzi alikua mshikaji wangu sana alikua ananipa ratiba za ndege kutua nknk, alikua ni asset kwangu”, huko mbele mtaona.

Nikamwaga jamaa tukaexchange number nikampa buku 5 ya soda huyo nikapotea, kufika kwa jamaa pale Puma nikampakia alikua na demu wake, safari yetu ilikua ni kuwapeleka pale Whitesand hotel. Wakati nakaribia Whitesand nikiwa pale Ramada hotel nikapata request juu kwa juu “hii mara nyingi inatokea kama upo karibu na mteja au kama usafiri wa shida”, muda uleule customer akapiga simu, dereva njoo hapa “The wave” nikamwambia ASAP.

Nikamdrop jamaa na demu wake nikapitia kumchukua mteja pale “The wave”, hao ulekeo ulikua ni Tips Mikocheni, Pale sikukaa hata nikapata mteja alikua anakwenda Samaki samaki, Masaki. Mpaka muda huo ilikua ishafika Saa 7 usiku na madakika kadhaa, nikasema acha nitafute sehem nipark na pia nipunguze mafuta yangu ya mwilini.

Ile mitaa ilikua imejaaa sana magari sana yaani kulikua kumefurika kumbuka ilikua ni Christmas, kuanzia kule Elements yaani mpaka unakuja Samaki samaki, kumefura hatari, parking za shida afu Masai wakiona IST wanajuaga ni Uber wanazinguaga hatari [emoji23][emoji23][emoji23].

“Masai huwa hawatupendi kwasababu huwa hatuwapi hela, mimi kutokana na gari yangu nilikua natumia vibao vya njano, nilikua hawanisumbui kabisa, kama ukipark usiposhuka anakugongea anauliza wewe ni Uber au laah”

Nikasema ngoja nisogee mpaka kule chin kama unakwenda Village supermarket, sasa nikaamua kupark pale kwenye corner inayokwenda UN pale kuna ka uwazi mitaa , Ile napark gari tu aisee si nikavamiwa na wale “DADA POA” sikujua kama ni chimbo lao lile, ila walikua mapini hatari.
Sikupenda ule usumbufu nikaamua kutoka pale wakaanza kusonya huku wananitukana, nikasema leo nimevamia mtumbwi wa vibwengo.

Nikapata request pale Samaki samaki nikamfuata mteja alikua ni dada lina mahips hatari afu lizuri, akanambia kaka mimi naelekea bwawani ila map iko sawa, wewe twende. “Bwawani ni mtaa ambao unaingilia pale Kinondoni kanisani sijui kwa Selebonge ni maarufu sana kwa mapishi, sasa unakunjia corner pale au njia nyingine unaingilia pale mbele baada ya jengo la Vodacom kuna mataa pale, barabara za kule ni za nzege”.

Nikamsusha yule dada pale, kucheki muda saa 9 na madakika yake nikasema ngoja nikatege pale Tips then nikalale, kutoka pale Bwawani mpaka Tips sio mbali. Nikasogea pale Tips napo palikua pamejaa hatari si unajua sikukuu imeangukia jumamosi kila mtu katoka out.

Mida kama ya sa10 ilikua imefika nikapata request ya kwenda Maison club, hii club ipo karibu na Sea cliff mitaa ileile. Wakati nimemdrop pale mteja nikasema acha niset destination ya mbezi beach mimi pia nikalale ili kesho niendelee na mzigo mapema. Kipindi cha sikukuu ndo kipindi ambacho Uber wanaingiza sana Pesa ni kipindi cha kuwa serious na kazi.

Palepale Maison nikapata request na mteja alikua anakwenda Mbezi beach kwa Zena, nikafurahi sana maana destination mpaka uipate ni bahati sana. Huyu alikua ni demu ana uchotara flani hivi aisee ni pini hatari akaingia akakaa mbele, akakilaza kiti ili alale vizuri mimi namwangalia tu, akanambia kaka fata ramani “alitoa sauti ya kudeka”. Ilikua ni pini balaa, kama wewe ni mwanaume rijali lazima utingishike, kwanza dem toka anaingia kwenye gari wahuni walikua wanamtolea macho balaa.

Alivyonambia fata ramani mimi sikua na swali tena kwani ramani ilikua inanionesha uelekeo ni mbezi beach, tukaanza safari pale nilipita ile barabara inayokuja tokea pale Tanesco Mikocheni, tukaunga wakati tunafika pale round about ya Kawe, dizaini kama dada akaanza mitego, mara atanue miguu, kama mtu ambaye anahangaika hivi.

Tulivyofika pale Rainbow kwa mbele si kuna filling station ya GBP, nikazama pale ili kuweka wese, nikashuka pale ili nipate na kaupepo kidogo huku jamaa akiweka mafuta, so ile naingia kwenye gari nakuta kile kigauni kimepanda mpaka saizi ya kiuno yaani naona kila kitu live, naiona chupi hii hapa live, paja hilo huku kwangu frequency zishachange muda, afu namuda sijapata ile kitu si unajua wife alikua hayupo.

Kwa muda ule nilikua sielew nini cha kufanya maana tamaa ilinijia haraka sana ya kumla yule dada, nikamgusa chupi pale katikati nikaona dada anaanza kuhangaika, huku akitoa ushirikiano, nikasema leo Mbuzi kafia kwa Muuza soup, naiachaje pisi kali kama hii….

Tutaendelea,

Okkk
 
Dah hii stori nimeifatilia kuanzia saa nne paka saa tisa kasoro... Kudos to the writer you know how to spark the interest of your readers and keep them glued to the pages/threads...
The mystic of is it real or is made up stories is very clever.. But midway you diverged from the theme the protagonist began with(au ndo character development [emoji1787]) that's we know its not a real story but it is a good story nonetheless. [emoji1490][emoji1490][emoji1490] Hongera sana mtoa uzi we ni muandishi mzuri
 
ADDITIONAL

Wakati nimeondoka pale home kwa Uncle sio kwamba niliwakataa mazima hapana bali nilikua nakwenda wasalimia. Sikua na kinyongo nao kabisa sababu hata watoto zao ni marafiki zangu sana. Mnakumbuka niliwaambia wakati natoka pale home niliwaaga nakwenda safari ya kikazi.

Baada ya kupita miezi 3 nilirudi kuwasalimia nilikwenda na mazaga ya kutosha kama zawadi. Sasa siku hiyo sikumkuta Uncle ila alikwepo Aunt tu. Bhasi tuliongea pale ila sikukaa sana na nikamwachia 100,000, mimi nikaondoka.

Mimi nilikua napiga simu kuwasalimia wote, sasa baada ya kwenda na kumpa ile pesa, Aunt alikua ananitafuta ananinasalimia. Japo mimi sikutaka kuweka mazoea sana maana niliona mwisho wa siku nitakua ATM.

Wakati Uncle wangu mambo yake yameanza kuwa mabaya alikua hashindi home na sometimes haachi pesa ya matumizi. Aunt alikua ananitafuta mimi nitamtumia pesa na sometimes alikua anamtumia yule mtoto wake wa mwisho wa kike (huyu dogo tulikua tunapatana sana mpaka sasa). Alikua ananipigia simu ananambia Kaka Insider sina hela ya kutumia shule, bhasi mimi nilikua najua, kama nina 20,30,50k nitatuma.

Jambo lingine ambalo sikulipenda kwa hawa ndugu ni hili, kipindi nimemtia mimba Mama J nilikwenda kwa Uncle ili niongee naye suala la kwenda Ukweni. Lengo langu ilikua nimwambie nataka niishi naye kama mke wangu, lakini huwezi amini nilifika pale kwa Uncle na nilimkuta Aunt seblen. Tuliongea pale nikamwuliza kama Uncle yupo aksema yuko ndani anachezea simu. Nikaomba aniitie kwani nina jambo nataka kuongea naye. Aunt alikwenda kumuita ila hakuweza kutoka, nilikaa karibu 45 mins mtu hatoki, nikaamua kuondoka zangu.

Wakati wa kwenda kupeleka mahali nilikwenda kuwapa taarifa ili kama ndugu zangu wanipe kampani. Nilifika pale kutoa taarifa na uncle alikwepo lakini hakutoka tena chumbani. Hata Aunt sikumwambia kilichonipeleka pale, nikaamua kuondoka na nilihapa sitokanyaga tena pale.

Nilitoka pale nikampigia simu mama kuhusu jambo lililotokea, mama akanambia mwanangu usiwe na wasiwasi, kama umefanya kila jambo na hawataki wewe fanya mambo yako. Mama akanambia hata hivyo huyo sio Uncle yako halisi, angekua ni kaka yangu halisi asingekufanyia hivo.

Ipo hivi Mama yangu mzazi amekua hamjui Mama wala Baba. Mama yake mama (Bibi) alikufa wakati mama ana miezi 3 tu, wakati anakufa alimwachia mtoto (ambaye ni mama yangu) dada yake, ambaye mama yangu alikua anamuita “Mama mkubwa”. Sasa huyo Mama mkubwa ndo aliye mlea mama na alikua na watoto pamoja na huyo Uncle. Uncle alikua kama kaka kwa mama yangu na walikua wote na wamepishana miaka 5.

Sasa upande wa Baba yake Mama ambaye ndio Baba yangu ni kwamba alimtelekeza mtoto tangu mama yake mama afariki (Bibi). Na huyu Babu ni moja ya wanajeshi ambao walikua na vyeo vikubwa jeshini na mama anamjua yule ni Baba yake, lakini mama alisema kama Baba yake anajua alikua na mtoto lakini hakuwai mtafuta bhasi na yeye hawezi mtafuta. Mama alikua ni mtoto pekee kwa mama yake mzazi so hakuwai kuwa na dada wala kaka.

Mama alisoma mpaka darasa la saba na alifaulu kwenda Sekondari lakini hakua na mtu wa kumshika mkono. Baada ya hapo akapata kazi za ndani kwa Mhindi, yule Mhindi akamjaza Mimba mama yangu na huyo mhindi alikua na mke.

Sasa Mama mhindi baada ya kujua ile mimba ni ya mme wake aliamua kumlea na hakua na kinyongo naye. Kwa upande mwingine yule Mhindi alikua anataka kumfanya mama awe kama mke mdogo. Lakini kutokana na mama kuwa na ukaribu sana yule mama Mhindi alikataa katakata. Mzee Mhindi baada ya kuona Mama amemgomea akasema ile mimba hata ilea mpaka amkubalie.

Mama Mhindi akaamua kumtoa mama pale kwake na kumpangia chumba sehemu nyingine ambapo mama alimtafuta dada yake wa kijijini wakawa wanaishi. Mama mhindi ndo alikua analipa kodi pamoja na pesa za kula alikua anatoa. Mama anasema huyu mama Mhindi alikua na roho nzuri sana, mpaka sasa amekua ni Bibi ila mama huwa anakwenda msalimia.

Mama alijifungua mtoto ambaye ndo dada yangu (Rafiku yake na Tyna, alonisaidia Airport). Mama mhindi aliendelea kumuhudumia kwa kila kitu yeye pamoja na mtoto, Mzee mhindi dizaini kama aliwatelekeza.

Wakati mama anakutana na Mzee wangu ambaye ndo Baba yangu mzazi (Mzee Insider). Mzee wangu alimwambia mama atamlea mtoto ila amuhakikishie hata wasiliana tena na wale wahindi. Mama alikubali ndo baba akachukua hayo majukumu so dada alikua akijua Mzee wangu ndo baba yake ila uhalisia ni Mhindi.

Hata mimi nilikuja kujua haya mambo wakati nimemaliza Form 6. Siku ya kujua nilishangaa sana the way mzee alivyokua anamlea kama binti yake. Kweli kabisa ukiangalia mzee na dada walikua hawaendani kabisa maana dada alikua anauhindi flan wa mbali, kuanzia nywele, weupe.

Baada ya dada kukua na kuanza kujitegemea kimaisha ndo alipewa hio taarifa na mzee akamwambia ana haki ya kumjua Baba yake na kudai urithi. Mzee alimwambia kazi ya kumlea na kumsomesha ameikamilisha kilichobaki sasa ni kujua ukweli na aamue mwenyewe kama atamtafuta baba yake au laah ni juu yake.

Licha ya mama kuolewa na mzee wangu lakini Mama mhindi aliendelea kumtafuta mama yangu na aliwaambia watoto zake kwamba wana mdogo wao. Baada ya dada kujua ukweli ndo mama kuwakutanisha na ndugu zake hao Wahindi. Dada yangu alikwenda na kumwona mzee wake ni wamefanana hatari asee, mpaka na ndugu zake ni copyright. Kuna ile kauli inasema damu ni nzito kuliko maji.

Mzee mhindi kwakweli ni tajiri kama Pesa anazo na anamali nyingi sana kuanzia viwanja, nyumba , biashara nknk. Dada yangu mwezi March tulikua tunaongea akanmbia mama amesema nikapambanie nipate sehemu ya Urithi wangu. Japo dada yangu licha ya kutambua yule ni Baba yake lakini anajua alimtelekeza, yeye bado anatambua Mzee wangu ndo Baba yake mlezi aliye mkuza na kumsomesha.

Kuna kaka yake mmoja upande wa mhindi ndo wanapatana na dada ndo amempa ushauri pia apambanie apate urithi maana ni mtoto halali wa mzee. Japo kuna baadhi ya ndugu zake hawampendi dada sababu wanajua dada anataka urithi.

Ndugu zangu mnatoa ushauri upi juu ya hili, dada yangu apambanie urithi wake au apotezee? Mimi binafsi nimemshauri apambanie urithi wake maana Mzee akifa ndo asahau.

Nyie kama wana Jf mnatoa ushauri gani kwa hili suala.
Ok.
 
Haya nyie mlio kua mnasema story ni ya uongo haya leteni hiyo ya ukweli sasa.

Ndio maana mm mnanionaga Sifai nina majibu mabovu kisa watu wa sampuli hii na kupitia watu wa sampuli hii wamefanya hadi account yangu iwe limited (but I don't care) kwa sababu ya moyoni nilisha yatoa.

Hata hii account ikiwa burned kabisa kisa nyie wapumbavu fresh tu. Maana kama ndio uhuru wa maoni huu sasa sio ni uharibifu.

Ona sasa thousands of good peoples wana katiliwa haki yao ya kupata kile wanacho kipenda kisa wapumbavu watano tu. I do hate them.

Now Mr mello ulisha ni limit baadhi ya features kwenye account yangu kisa watu wa sampuli hiyo. Kwa sasa naomba uni burn completely. Hadi hapa hakuna cha maana uzalendo umenishinda kupenda vya nyumbani ngoja nikamuunge tu mkono bwana meta,Twitter, tiktok na kubwa la maadui telegram .
Mwanaune una lia lia kisa kuprove story niya kweli .are you normal ? au wahuni washa ku mix hormones[emoji97]
 
Malalamiko yako haya yameegemea wapi mbona hueleweki, unalalamika kulimitiwa, unalalamika waharibu uzi au unamlalamikia melo?
Soma kwa kutulia , nililimitiwa kwa sababu ya hao watu wa chai kwa sababu nilishindwa kuwavumilia nikajikuta naenda sanbamba na ujinga wao. Nikaishuwa kulimitia kwa sababu yao...na sijui anawafufa wa nn kwa sababu ni waharibifu ...hata insider akiamua kula nao sahani moja nae kitamkuta kibaya wakati yeye ndio kachokozwa
 
Ultimately the day we've been waiting for....has come!.....

Sijapita huku siku ya 5.....nikiisubiri Jumaaa kareem!....

Njo vile weather iko byeee. leo...

Papaaa iko nasubiri Kutomboka! Na schauffeur wa UBER!!!!
 
Story si itakuwa kuanzia ijumaa, jumamosi na jpili?
Tutulie tu kwa wale wanaosema ni chai temaneni nayo tunachotaka sisi tusome mpaka mwisho!!
Humu watu wenye changamoto za akili ni wapo pia
Jamaa umemstahi uliposema unatuma picha ameingia mitini hahaha
 
Back
Top Bottom