Wakuperuzi
JF-Expert Member
- Mar 31, 2023
- 2,348
- 5,841
Iryn hawezi kuwa na kidevu ka ngazi ya uda # lanii la kuishiwaMtoto Iryn karudi kutoka chimbo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Iryn hawezi kuwa na kidevu ka ngazi ya uda # lanii la kuishiwaMtoto Iryn karudi kutoka chimbo
Ah nyie critiques tunatamani sana kujua mnakulaga pisi gani! Ila mara nyingi huwa mnakula pisi mbovu sana! Basi tu hatujuaniIryn hawezi kuwa na kidevu ka ngazi ya uda # lanii la kuishiwa
Una nongwa we kiumbe[emoji1787]Tulio na kazi za kufanya hata hatuteseki tunaenjoy tu hata ikiletwa mwakani fresh tu. Pole yenu majobless [emoji16][emoji16][emoji16][emoji1635][emoji1635]
Uko sahihi mkuu jf si maisha yetu halisi hta wewe na ufahamu wako hebu. vuta tu picha jinsi Iryn alivyosifiwa humu ndani kiasi mpka story hii inaenda ukingoni lkn hatujaona kasoro ya Iryn kiasi kila mahali wanapoingia watu wanaacha shughuli zao waume kwa wake ili tu wapate muda wa kumuangalia Star wetu wa hii movie ila hta wewe uko vzuri ni mrembo ila mnazidianaAh nyie critiques tunatamani sana kujua mnakulaga pisi gani! Ila mara nyingi huwa mnakula pisi mbovu sana! Basi tu hatujuani
Aisee ..EPISODE 37
“A TRUE STORY BY INSIDER”
Muda huu milango ilikuwa wazi ikitusubiri sisi kuingia ndani ili tujihakikishie kama Iryn yuko ndani ama laah. Kila mmoja alionekana kuwa na wasiwasi sana na hofu ilitawala mahali hapa, mimi ndo niliyekuwa wakwanza kufungua mlango na kuingia ndani.
ENDELEA………..
Baada ya kuingia ndani alifuatia jamaa na kisha Lucy ila Rose alishindwa kuingia maana alikuwa analia pale nje. Seblen mazingira yalikuwa sawa na mimi nilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye mlango wa chumba chake. Mlango ulikuwa hujafungwa ila umerudishiwa tu na nilifungua na kuingia ndani.
Mbele yangu nilikuwa nakitizama kitanda ambacho kilikuwa nashuka la kujifunika ambalo halijakunjwa, ni kama mtu aliamka bila kutandika kitanda na kukunja shuka. Na pale kitandani ilionekana simu yake ya iphone na ilikuwa imezimwa. Na mimi niliitambua ndo simu yake anayotumia siku zote.
Chumba chake kilikuwa kinatoa harufu nzuri sana kwakweli na muda huu Rose alikuwa ameingia chumbani.
Tulikagua bafuni na hakukuwa na dalili yote mbaya na tulikwenda chumba kingine na jikoni lakini hakukuwa na sign yoyote.
MIMI: “Mpaka sasa tumejidhirisha mtu hayupo na mlango ulifungwa kwa nje.”
JAMAA: “Kitandani panaokena alikuwa kalala na kwanini simu asahau kitandani na wakati inaonekana kabisa?.”
ROSE: “Hata mimi nina wasiwasi na hili kwakweli, unataka kusema ametekwa?”
JAMAA: “Inawezekana na hawa waliofanya hii kazi watakuwa ni professional kabisa.”
ROSE: “Haiwezekani simu usahau kitandani na inaonekana kabisa kwa macho.”
JAMAA: “Kweli sio rahisi hata hili mimi ndo linanitia mashaka sana.”
LUCY: “Mimi nahisi atakuwa kaondoka na huyo Muajemi ila wanakuchora tu.”
ROSE: “Sasa tunafanyaje guys?”
JAMAA: “Nafikiri tujadiliane kuhusu next step.”
LUCY: “Mimi nafikiri Insider ufanye juu chini kesho umpate mama Janeth.”
MIMI: “Guys kesho mimi nitakuwa na majibu yaliyokamilika, suala la Police siliungi mkono kabisa.”
JAMAA: “Kesho fundi atakuja kuweka vitasa vipya tutawasiliana but kesho tuwe na maamuzi sahihi.”
Baada ya makubalino tulirudishia mlango vizuri na tukaagana pale.
Baada ya kumaliza maongezi mimi niliondoka na Lucy lengo nim-escort nimwache pale Mlimani city achukue bajaji za Makongo Juu. Muda huu ilikuwa saa 4 usiku tayari, baada ya kufika maeneo yale ya Mlimani tukaona bora twende Samaki samaki tukapoteze mawazo.
Baada ya kufika pale Samaki samaki tulikaa kwenye meza za nje kabisa na baada ya mhudumu kufika niliagiza Heineken na Lucy aliagiza Desperados.
MIMI: “Nakunywesha hapa ili nika kut*mbe”
LUCY: “Hahahaa namwonea huruma sana mke wako, mpaka sasa hujarudi home unahangaika na kina Lucy.”
MIMI: “Mke wangu sio msumbufu hanaga nongwa.”
LUCY: “Mhh haya, Insider mimi nawazo hapa.”
MIMI: “Wazo gani?”
LUCY: “Mimi nahisi Iryn ameamua kukufanyia mchezo na Mama Janeth.”
MIMI: “Kwanini unasema hivyo?”
LUCY: “Hauna muda mrefu toka upewe mkataba mpya na majukumu mapya what if kama wanataka kuona maamuzi yako na jinsi utakavyo deal na hili suala kwenye kampuni?.”
MIMI: “Lucy mimi sidhani ikawa hivyo.”
LUCY: “Kwanini wote hawapatikani na hakuna taarifa yoyote juu yao?, Iryn atakuwa na mama Janeth roho inaniambia hivyo.”
MIMI: “Kidogo maneno yako yananiingia.” Na muda huu nilikuwa namalizia bia yangu ya kwenye glass.
LUCY: “Insider vipi kuhusu mishahara maana mwisho wa mwezi ni week ijayo sio mbali.”
MIMI: “Next week mbali naamini atakuwa karudi na tumejua aliko.”
LUCY: “Ni sawa ila wewe kama Operation manager inabidi uanze kuandaa mchakato just incase.”
MIMI: “Una wafanyakazi wangapi kwenye ofisi zako?”
LUCY: “Mikocheni wako 4 na sinza 3, pamoja na mimi jumla tuko 8.”
MIMI: “Na mshahara anawalipaje?”
LUCY: “Mimi nalipwa 600,000 na wengine 300,000/= , pia kuna bonus za kila mwisho wa mwezi.”
MIMI: “Ok sawa mimi nitawalipa mshahara ila masuala ya bonus ataclear mwenyewe, na hizo bonus zinakuwaje?”
LUCY: “Inategemea na idadi ya wateja walionunua wigi na gharama za wigi, kwa pale ofisini mtu akikosa sana hakosi 100,000 kama bonus kwa mwezi.”
MIMI: “Hivi Lucy ulifahamianaje na Iryn?”
LUCY: “Nilianza kufanya kazi na mama yake mwishoni kabisa kabla hajafariki ndo mpaka sasa. Kipindi hicho nilikuwa simjui Iryn ila nilikuwa najua mama yake ana bint mkubwa.”
MIMI: “Una elimu gani?”
LUCY: “Nina Diploma ya Procurement”
MIMI: “Umeridhika kuwa saloon?”
LUCY: “Insider nimeridhika kabisa licha ya mshahara bado napewa Bonus, bado najiongeza mle ndani mimi ndo top kila kitu lazima wanifate mimi. Kwa siku kama mambo magumu sikosi 20,000 weekend naweza ingiza pesa mingi tu kama wigi zitatoka nyingi, bado nawauzia saloon zingine napata cha juu. Nikipiga hesabu kwa mwezi si haba unafikiri ofisi gani naweza pata hela kama hapa kwa Iryn?. Nilikuwa napewa na pesa za matumizi ya ofisi ya kila mwezi ila kwa sasa yatakuwa chini yako, hata hapa nawaza kama Iryn asiporudi itakuwaje.”
MIMI: “Aisee kumbe leo kidogo umenipa mwanga, sasa naomba wafanyakazi wako wasijue lolote linaloendelea kuhusu Iryn. Pia naomba nitumie report za toka jumatatu ulizotuma kwa Iryn, na kuanzia jumatatu mauzo usiingize kwa bank utakuwa unanikabidhi cash ili niangalie suala la kuwalipa mishahara.”
LUCY: “Sawa haina shida Insider.”
Tulikaa pale mpaka saa 6 na tuliongea mengi sana na Lucy na nilimkodia Uber ili impeleke kwake na mimi nikarudi home.
Wakati nimefika mataa ya Kawe Prisca alianza kupiga simu na mimi nikapokea simu yake.
MIMI: “Prisca hizi simu za usiku vipi? Mbona unakuwa huelewi unasahau makubaliano yetu?”.
PRISCA: “Sorry nilijua leo weekend utakuwa hujarudi home.”
MIMI: “Acha mazoea tafadhali, ningekuwa home na wife akapokea? Prisca usiniletee matatizo tafadhali. Niambie unataka nini?”
PRISCA: “Insider mimi siwezi kukaa bila kusikia sauti yako, hapa nimekusikia sasa nitalala kwa amani.”
MIMI: “Prisca mimi naona tuachane kama mambo yenyewe ndo haya, sitaki kuona Mke wangu anaondoka kwaajili yako.”
PRISCA: “Insider unajua unanitesa sana hivi unanipenda kweli?”
MIMI: “Prisca byee Usiku mwema.”
Ni maongezi yaliyochukua muda mrefu mpaka nafika home, na muda huu niliwaza kumpiga chini Prisca maana niliona kadri siku zinavyokwenda anazidi kuwa hatari, na angeniletea shida kwenye ndoa yangu.
********
Jumapili asubuhi nilijaribu kumtafuta Mama Janeth kwa whatsapp lakini hakuwa online, nikawaza kesho nitakwenda ofisini kwake Masaki.
Kwa upande mwingine niliwasiliana na Sumaiya nikamwambia anitumie report zote alizotuma kwa Iryn kuanzia Jumatatu, na akiwa anatuma report awe anatuma na kwangu pia mpaka Iryn atakaporudi.
Baada ya kupata breakfast nilikwenda Mbweni ili kuonana na Jane kwa lengo la kuendelea na mafunzo ya udereva. Hii siku nilimpeleka mpaka barabara za lami na tulikwenda Ununio road, na ndo tulikofanyia zoezi huko.
Maendeleo yake yalikuwa mazuri kwakweli na Jane alikuwa na hamu ya kujua kuendesha gari mapema. Tuliendelea na zoezi letu mpaka mchana ndo nikamrudisha kwake, na mimi sikutaka kukaa pale kwake nikaaga na nikaondoka kurudi home.
Baada ya kurudi home niliingia chumbani na nilikuwa na mawazo sana, niliwaza huenda Muajemi kafanya kitu mbaya kwa Iryn. Niliamua kumtafuta kwa Whatsapp na hakuwa online muda huu. Nilianza kuingia na maswali kwanini Muajemi hapatikani? na toka jana hajanirudia niliwaza something fishy is going on.
Kutokana na mawazo nikiwa pale kitandani hatimae nilipitiwa na usingizi nikalala. Lakini nilishtushwa na simu iliyokuwa inaita baada ya kuangalia alikuwa ni Rose akipiga na nilipokea simu yake kwa haraka sana.
“Hi Rose”
“Insider njo hapa home haraka we got something.”
“I’m coming ASAP”
Kucheki muda ilikuwa 17:30 jioni hivyo nikawasha gari nikaondoka kuelekea Kijitonyama, na nilifanya kuwasiliana na Lucy akasema anachukua boda nitamkuta pale.
Nilitumia dakika 20 kuwasili Kijitonyama na baada ya kupark gari pale nje niliingia ndani na niliwakuta wapo na Mzee wa makamo akiwa amevaa sare za mgambo. Tulisalimiana pale na muda huu Lucy alikuwa anafika pale kwa Iryn.
ROSE: “Jiran sisi leo tuliendelea na uchunguzi wetu kwa majirani na huyu mzee ni moja ya walioshuhudia jambo.”
MIMI: “Jambo gani Jirani.”
ROSE: “Huyu Mzee ni Mlinzi nyumba ya pili ile nyeupe, anasema Jumatatu usiku aliiona Noah nyeusi hapo getin nje, aliiona wakati inaingia na haikuchukua dakika 5 ikaondoka kwa kasi.”
MIMI: “Mzee ilikuwa muda gani kama unakumbuka?”
MZEE: “kwenye saa 7 Usiku hivi, wakati inaingia niliiona mpaka inapark hapo nje getini na mimi niliendelea na mambo yangu, wakati inatoka ilikuwa kwa kasi sana na niliona inamaliza kukata kona kushoto.”
JAMAA: “Bro! unakumbuka nilisema jana hawa waliohusika ni professional sana, haiwezekani mtu aondoke asahau simu kitandani na ikiwa inaonekana vile ni ngumu sana.”
LUCY: “Inawezekana waliingia ndani wakamkuta kitandani au aliwafungulia mlango mwenyewe.”
MZEE: “Kama alivyosema kaka hapa hawa waliohusika ni wazoefu, hii milango inafunguka vizuri kabisa na kuna vifaa special wanatumia. Ingekuwa hii milango ni salama sisi hata tusingekuwa na kazi ya kulinda usiku.”
JAMAA: “Bro labda nikuulize maana wewe ndo unamjua vizuri Iryn, katika sehem zote mlizopita ana ndugu au rafiki mwenye gari ya aina hii nyeusi?”
MIMI: “Hapana Iryn sio wa marafiki kabisa kwa maelezo ya hapa hata mimi napatwa na wasiwasi wa kutekwa.”
LUCY: “Insider Bossy Iryn ametekwa kwa mazingira tuliyoona jana na maelezo ya leo naona huu ndo ukweli.”
Nilishangaa sana kuona Lucy leo amekubaliana na kutekwa kwa Iryn, wakati alikuwa mgumu sana kukubali hili jambo na muda huu alikuwa ameanza kutia huruma. Nilihisi atakuwa anawaza kibarua chake itakuwaje.
ROSE: “Guys nadhani wazo la Police leo mtalitilia maanani.”
MZEE: “Mkaripoti mapema aanze kutafutwa, upelelezi na uchunguzi uanze, mkizidi kuchelewa mtazidi kujiweka kwenye wakati mgumu.”
LUCY: “Insider vipi kuhusu Mama Janeth umefanikiwa kumpata?”
MIMI: “Mama Janeth nataka kwenda kesho mapema ofisini kwake. Mama Janeth ndo ameshika Karata ya mwisho kwenye hili suala na kesho mapema mimi nitakwenda ofisini kwake hata kama sitompata pale najua nitapata mawasiliano yake.”
JAMAA: “Nafikiri tusubiri kesho hiyo asubuhi tutakuwa na majibu tayari, ikishindikana twende Police na mimi kesho siendi kazini.”
LUCY: “Kesho ikishindikana twendeni Police.”
ROSE: “Same here kesho siendi Kazini nitasubiri majibu.”
MIMI: “Guys kesho tumekubaliana kama itashindikana tunakwenda Police, no hesitation this time.”
Saa mbili usiku nilitoka pale na nilikuwa na Lucy ambaye nilimpa lift ili nimwache pale Mlimani City mimi niondoke. Lakini huku njiani Lucy alionekana kuwa na mawazo sana mpaka nilipatwa na huruma.
“Ulisema unakaa Makongo juu ipi?”
“CCM palepale kituoni.”
Niliamua kumpa lift mpaka Makongo CCM kituoni na mimi nilikwenda moja kwa moja na Goba Road kurudi home.
Baada ya kufika home na kushuka kwa gari niliwakuta Junior na dada yake wako nje kibarazani. Na muda huu Junior alianza kunililia ikabidi nimnyanyue na tukaingia ndani. Maana nilikuwa nataka kwenda kuoga kwanza ikabidi nitoe simu nimwekee katuni awe anaangalia ili nipate upenyo wa kukimbia.
Baada yakutoka kuoga nilikuwa na mawazo sana na nilikuwa pale kitandani nawaza nani atakuwa amemteka Iryn?. Niliwaza mimi ndo nitakuwa mstari wa mbele kuisaidia Police katika kufanya uchunguzi na suala la Mama Janeth kutokupatikana ndo lilikuwa linazidi kunipa mawazo sana.
Muda huu simu yangu ndogo ilianza kuita na kucheki alikuwa ni Prisca sikupokea nikapotezea, alipiga tena kwa mara nyingine ikabidi nipokee tu nimsikilize anasema nini.
MIMI: “Prisca mbona mgumu sana wewe kuelewa?”
PRISCA: “Insider mimi sina story ila kuna jambo unatakiwa ulifahamu before its too late.”
MIMI: “Nakusikiliza Go on”
PRISCA: “Insider I’m pregnant.”
MIMI: “What? Una mimba yangu?
PRISCA: “Ndio nasifikirii kuitoa, kama utamkataa mtoto wako sawa ila tambua hivyo hii mimba ni yako.”
Na prisca alikata simu muda huu, taarifa za Prisca hazikuwa nzuri kwa upande wangu sababu nilikuwa na mke tayari na sikuwahi kufikiri kama kuna siku nitakuja kuwa na mtoto wa nje.
Nilianza kujuta muda huu nikajisemea kwakweli “HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA”. Hili bom la nyuklia nilitengeneza mwenyewe sasa limelipuka na hapa ni mwanzo tu. Nilikuwa kwenye majuto makubwa sana maana hata condom nilikuwa situmii tukikutana.
Na wakati bado niko kitandani niko kwenye mawazo mazito aliingia wife akiwa ameshika simu na mbele yangu nilikuwa nikiitizama picha niliyopiga na Iryn swimming kule Zanzibar.
“Muda mrefu sana nilikuwa na wasiwasi na huyu Iryn kumbe hata Zanzibar mlienda kwaajili ya kula bata, picha zenu zinaonesha mlikuwa kwenye HUBA zito sana.”
TUTAENDELEA
JUMAMOSI
Acha genye, tamaa na shobo km hz utakuwa ulishapoteza utu wako huko nyuma😳😳Episode ya 39.
Tunaendelea wadau.
.....basi bwana, kumbe baada ya kutoka kule Zanzibar, Irylin alihitajika haraka kwa mama mzungu (Mama Janeth) ili aunganishwe na mchongo mpya wa kazi katika shirika kubwa lenye hadhi, shirika ambalo wanaofanya kazi huko ni wale wenye akili timamu wasio na asili ya kusoma kwenye Shule zenye upungufu wa matundu ya vyoo.
Kwa kuwa Irylin anamheshimu sana mama Janeth na anamchukulia kama mlezi wake, hakuona shida ya kukataa kwa sababu kabla aliwahi kudokezwa kuhusu mpango huo.
Kuhusu kumuaga Insider hakuona haja kwa sababu tayari Insider aliyafanya mambo yake kuwa siri.
Hivyo utaratibu ule ule aliyokuwa ametumia Insider, Irylin aliamua kupitia mle mle ili Insider aonje ugumu wa kufanya mambo kimya kimya.
************************
Kuhusu alipo Irylin na ni lini atarejea jumlisha mustakabali wa kazi....
Itaendelea na mtu asiguse komenti yangu.
Huyu wanamtekenya Masega nn?!Episode ya 39.
Tunaendelea wadau.
.....basi bwana, kumbe baada ya kutoka kule Zanzibar, Irylin alihitajika haraka kwa mama mzungu (Mama Janeth) ili aunganishwe na mchongo mpya wa kazi katika shirika kubwa lenye hadhi, shirika ambalo wanaofanya kazi huko ni wale wenye akili timamu wasio na asili ya kusoma kwenye Shule zenye upungufu wa matundu ya vyoo.
Kwa kuwa Irylin anamheshimu sana mama Janeth na anamchukulia kama mlezi wake, hakuona shida ya kukataa kwa sababu kabla aliwahi kudokezwa kuhusu mpango huo.
Kuhusu kumuaga Insider hakuona haja kwa sababu tayari Insider aliyafanya mambo yake kuwa siri.
Hivyo utaratibu ule ule aliyokuwa ametumia Insider, Irylin aliamua kupitia mle mle ili Insider aonje ugumu wa kufanya mambo kimya kimya.
************************
Kuhusu alipo Irylin na ni lini atarejea jumlisha mustakabali wa kazi....
Itaendelea na mtu asiguse komenti yangu.
Dr wa ID acha maneno na wewe umesikilizwa kwani umewakilisha wote kwa kutumia!!!Acha kulilia story hapa tulia jamaa ataleta kwa wakt unao fah
VawulenceAlafu ukishaziona?
Vawulence
Muache mambo zenu hizo za kudandía mambo ya watuEpisode 39
Baada ya kupokea cm ya kutoka njee ya nchi na kugundua ni Irene nilishituka Sana
Endelea
Irene alinisimulia jinsi alivyo ondoka kwa kubebwa na Interpol kwa tuhuma za kujihusisha na ujasusi hivo mpaka mda huo yupo chini ya ulinzi ila alikuwa akiomba niangalie biashara zake akirudi atanipa taaamuuu
Tukutane jumamos kwa mwendelezo
Dr wa ID acha maneno na wewe umesikilizwa kwani umewakilisha wote kwa kutumia!!!
Kama haupendi kusoma Uzi wote ukakakutana na posts zake INSIDER MAN uliza urahisi tunaotumia wengine kusoma posts zake kwanza bila wasi na tukiamua kusoma wengine tunawasoma humu kama kawaida..
Waanzisha nyuzi wanaweza kurusha muda wowote na kila mtu akawasoma wao kwanza kama mtu hataki kusoma nyuzi posti kwa posti.
Anayetaka kujua aulize, ajibiwe.
Jumapili njema
Insider man ili kuondoa vishoka kwenye izi wako pendwa naomba uwe unashusha episodes tatu kwa mkupuo maana naona uzi umevamiwa kwa nguvu.Muache mambo zenu hizo za kudandía mambo ya watu
*150 *INSIDER MAN # okNafanyaje nikitaka kusoma posts za INSIDER MAN pekee?
hujamsoma Lara Moko...Hivi wakuu mpaka hapa tulipofikia kila moja list yako ya GREATEST Story tellers wa JF ni ipi?. Mimi japo sijasoma nyingi lakini hawa jamaa wafuatao nawaheshim
1. leadermoe R.I.P
2. UMUGHAKA
3. INSIDER MAN
4. LwandaMagere
5. Bado Sijasoma nyingine ila kuna room ya kupatikana wa nafasi hii km nikikuta story matata 😀