Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Daah
Tuliwaza mambo mengi sana kumbe hakuna hata 1 lililo sahihi wabongo tunawaza ngono tu [emoji23][emoji23]

Ila iryn hakutaka kumtambulisha mapema huyo ndugu yake lengo amkomoe Insider na apime upepo sasa akakuta ngoma imedunda akazd kuwa na mawazo kumbe asichojua ni kuwa hata tukiwa tunateseka huenda asijue tofauti na wao wanawake lazm utawajua tu

Sasa mkuu usije kuremba tena iryn akijileta kwenye mfumo mpelekee moto adi akili zikae sawa
Ikiwezekana ampakie hadi mkongo.
 
EPISODE 56

“A TRUE STORY BY INSIDER.”

“Ok twende kama unataka hivyo chukua vitu tuondoke.”

Kwenye maisha yangu sipendagi kugombana au kubishana na mwanamke ndo mimi nilivyo.

CONTINUE:

Na mimi muda huu sikutaka kubishana na Prisca kabisa maana mwanaume ni mtu wa vitendo tu na sio kelele. Suala la kwenda naye lisingeweza kutokea maana ningekuwa nimetembea na bom la nyuklia na mimi nilikuwa na mipango yangu kichwani.

Tulitoka pale kwake muda huu na nilitumia barabara ya upande wa geti maji ili nije nitokee Barabara ya Sam Nujoma.

Hii siku kulikuwa na foleni sana na ilikuwa haitembei kabisa na ilianzia pale Magufuli hostel. Wakati tumefika Mlimani city Iryn alipiga tena simu lakini niliamua kuipotezea sikutaka hata kupokea simu zake, lakini alinitumia text kunitaarifu kuwa amefika ananisubiri.

Kutokana na foleni kuwa kubwa na Iryn alikuwa amefika tayari eneo la tukio ilibidi nimwambie Prisca afanye kurequest Bolt ili impeleke kwao na mimi niwahi kuonana na Iryn lakini alinigomea akasema tunakwenda wote.

Sikutaka kubishana naye pale na mimi nilifanya kurequest kwa simu yangu na nilifanikiwa kupata Bolt na nilimwambia anisubiri pale mpakani bus stand nitamkuta hapo.

“Insider kwanini hutaki twende wote ni nini ambacho unanificha?”

“Nashangaa kuona una wivu kumzidi hata mke wangu, yule ni Bossy wangu kwenda na wewe kule anaweza chukulia ni dharau maana ni masuala ya kazi.”

“Sasa kuna ubaya gani? Mimi si ninakaa sehemu nyingine nawaacha nyie mnaongea kuna tatizo?”

“Prisca I said No, utapanda Bolt kwenda nyumbani pia unatakiwa utambue muda umeenda inabidi uwahi kurudi hali yako si waiona?”

Na muda huu tulikuwa tumefika tayari pale Mpakani na mimi nilishuka nikaanza kutoa vitu vyake kuvipeleka kwa Bolt na baada ya kurudi kwa gari ili tuagane nilikuta Prisca analia, ilibidi nishangae maana niliona ameanza utoto.

“Prisca acha utoto wako nitakubadilikia hapa sasa hivi, nafikiri unanijua huwa sipendi mambo ya kitoto, shuka upesi kwenye gari uwahi home nachelewa na Bossy ananisubiri muda mrefu.”

Na muda huu nilitoa cash elfu 20 na nikampa kwaajili ya nauli lakini alichonijibu,

“I don’t need your money, kama umeamua kwenda huko kwa malaya wako na usinitafute tena.”

Na mimi sikutaka maneno naye bali nilikwenda kwa Dereva nikamlipa elfu 20 maana nauli ilikuwa elfu 13, nilimwambia dereva change atampa dada na mimi nilifungua mlango wa nyuma kumuaga Prisca lakini alikuwa kaninunia.

Baada ya kuachana na Prisca niliendelea na safari ya kwenda triple 7 kwa upande wangu nilikuwa najua nakwenda achishwa kazi na siwezi toboa. Lakini sasa kwa upande wangu sikuwa hata na wasiwasi wowote ule maana nilikuwa nishamtumia CV mama wa2 hivyo nilijua muda wowote mambo yatanyooka.

Saa yangu ilikuwa inaonesha ni saa 1 usiku na muda huu nilikuwa niko mataa ya mwenge nasubiri kuruhusiwa tu. Niliamua kumpigia simu Iryn maana alikuwa amepiga simu mara 3 na sikupokea, baada ya kupokea simu yangu alionekana kukasirika sana.

IRYN: “Insider mbona hupokei simu zangu na unajua kabisa niko hapa nakusubiri zaidi ya lisaa, kama huji nambie niondoke you’re wasting my time for nothing.”

MIMI: “Kama nakupotezea muda kwanini bado unanisubiri?. Mimi niko njiani nakuja kuna foleni sana leo ndani ya dakika 10 nitakuwa hapo.

IRYN: “Nakusubiri bhasi kuwa hurry” Na aliongea sauti ya upole sana muda huu.

Baada ya kuona Iryn kawa mpole nilijua hana jeuri ya kuniachisha kazi na muda huu kiburi kilianza kunijia kwa kasi sana.

Niliwaza pale suala la kuterminate mkataba lingekuwa gumu sababu toka nianze majukumu mauzo yameongezeka sana. Na mimi kwasasa ndo engine ya kampuni reputation niliyoweka kwake, Mama Janeth na kwa wafanyakazi ni kubwa sana, hivyo nilijua asingekuwa na jeuri ya kunitema.

Na mimi niliendesha gari kwa spidi sana mpaka nafika pale Triple 7 na baada ya kuwasili pale niliiona gari yake Range akiwa ameipark pale nje na mimi nikapark kwa pembeni yake.

Baada ya kuingia ndani nilimwona amekaa na yule jamaa yake na mimi nilikwenda moja kwa moja mpaka pale kwenye meza yao, nikavuta kiti nikakaa.

“I’m sorry for being late kulikuwa na foleni sana.”

Iryn aliishia kuniangalia tu na mimi nilimsalimia jamaa yake vizuri kabisa na alionekana kunifurahia sana muda huu.

Mhudumu naye hakuwa mbali sana kuja kunisikiliza na mimi nika order heineken 2.

Iryn alimwomba jamaa yake atupishe kidogo ili tuongee na Jamaa alikwenda kukaa angle nyingine na tulikuwa tukitizamana.

IRYN: “Insider ni nani aliyepokea simu yangu muda ule? Maana imekuwa saprise sana leo ndo umefikia stage hii.?”

MIMI: “Bossy haya ndo umeniitia tuzungumze?”

IRYN: “Mmh! Okay uko sahihi una….” Na mimi nilimkatisha maongezi yake maana sikutaka kuendelea na hii mada.

MIMI: “Samahani kwa kukuweka sana hapa nafikiri sijawai kukuweka kama leo hii ndo mara yangu ya kwanza.”

IRYN: “It’s okay Insider mimi nimekuita ili tuzungumze suala la mkataba wako sababu niliongea na mama Janeth. So tumeshauriana tukuongezee majukumu mengine ili uanze nayo mwezi ujao na tuongee suala la mshahara.”

MIMI: “Nilijua nakuja kuachishwa kazi leo.”

IRYN: “Kwanini uachishwe kazi? kwa kosa gani umefanya?, nimeona kazi yako uliyofanya ya kupendezesha ofisi pamoja na sare za T-shirts hongera sana.”

MIMI: “Leo ndo umeona bora unipe pongezi na ulikuwa wapi siku zote? hata kupiga simu ulishindwa? What kind of bossy do I have?”

Na muda huu Iryn alikuwa kimya na mpole ni kama alijua kweli alizingua.

IRYN: “Sorry niliplan leo tungeonana ninge kupongeza face to face pia nina suala lingine muhimu sana linaniumiza kichwa. Tujadili kwanza suala lako la mkataba, kutokana na majukumu mapya kampuni itakulipa million 3 kwasasa. Vipi unakubalina na majukumu mapya na mkataba mpya?”

MIMI: “Vipi kama nikisema No?”

IRYN: “Why? Mshahara ni mdogo?

MIMI: “Behavior uliyoonesha kwangu sijapenda kabisa mpaka nimefikiri nikuachie kazi yako, haiwezekani nimechelewa kutuma ripoti kwa bahati mbaya unanikaripia kama mtoto, umeshindwa hata kuuliza sababu?. Bora nilipwe hata mshahara kidogo lakini niwe na amani na sio kunyanyaswa kama ulivyofanya. Ulinikuta hapa mjini napambana hata nilikuwa sikujui hata nikiacha kazi yako sitalala njaa hapa mjini naamini familia yangu itakula.”

Nilianza kuona mabadiliko ya Iryn taratibu na machozi yalianza kumjaa machoni na yakaanza kushuka taratibu mashavuni, Iryn ni aina ya wanawake ambao wanamachozi ya karibu sana.

IRYN: “Insider unajua ni jinsi gani umeniumiza? Unaniona mimi kama malaya sindio?, trust yote niliyokupa leo hii wewe ndo wakuniuza mimi kwa Muajemi.?”

Na mimi baada ya kuona machozi yameanza kuangukia meza ilibidi nitoe kitambaa changu nikamfuta machozi taratibu, kwa upande mwingine jamaa alikuwa anashuhudia lile tukio na mimi hata sikuwa najali.

MIMI: “Utakuwa ni mpumbavu kama unaamini maneno ya Muajemi na sio mimi mtu ambaye tuko pamoja kwa muda mrefu. Kwahiyo chuki zote hizi juu yangu kumbe kisa ndo hiki?, kwamba umeshindwa kukaa na mimi chini ukaniuliza?. Kama unaona Muajemi yuko sawa na maneno aliyokujaza bhasi nafikiri endelea kumwamini.”

IRYN: “Unajua nilimbana sana Muajemi na alifunguka kila kitu hata zile Pesa ulizonidanganya kipindi kile kule Zanzibar ilikuwa sababu ya mimi kukubali kwenda Zanzibar.”

MIMI: “Hivi kuna hata siku ambayo mimi nilikulazimisha kuonana na Muajemi? Suala la Zanzibar wewe sindo ulisema tunakwenda wote?. Hata ile siku ya kwanza kukutana ilikuwa sababu unataka connection za Dubai na kuhusu hizo pesa nilimkopa kuna jambo nilikwama na sio kwasababu yako na yeye alisema amenipa tu bure.”

IRYN: “Sasa mbona ulinidanganya kuwa umeagizwa?”

MIMI: “Nilifanya hivo ili kuepusha maswali lakini sio kama Muajemi alivyokwambia ni muongo sana.”

IRYN: “Insider kama unashida ya pesa ulishindwa nini kunambia nikusaidie?” Anyway ila best yako ni stupid sana najua siri ya Wanaume hutakiwi kusema wala kumchoma mwenzio ila yeye nimembana kidogo kafunguka kila kitu.”

MIMI: “Ukweli kazingua ila hayo maneno yote ni uongo, so mmekubalianaje? maana Muajemi alinambia mtaonana lakini baada ya kuonana na wewe hata simu zangu hapokei wala text hajibu sijui mmekubaliana nini toka muonane kwa siri.”

IRYN: “Nilimwambia hatuwezi kuwa na mahusiano kwanza anamke na watoto ila bado ana hangaika.”

MIMI: “Ni vizuri alivyojua ukweli kuliko angeendelea kupoteza muda, ila hayo maneno aliyosema sio kweli Muajemi alitaka kuniharibia kwako.”

IRYN: “Haya yote unataka kusema Muajemi alitaka tugombanisha?

MIMI: “Exactly maana toka ile siku atukute wote room kule Zanzibar mpaka leo anahisi sisi ni wapenzi, atakuwa amefanya hivo ili kutugombanisha ili tukose wote.”

IRYN: “Nilikuwa mjinga sana kumuamini bila kufikiria kwa hili naomba nisamehe but naomba kwasasa tufocus na kampuni, please nakuhitaji sana kwenye kampuni.”

MIMI: “Ok mkataba mpya nakubaliana nao lakini malipo ni kidogo ujue naumia sana, mshahara wa kwanza karibu 50% unaishia kwenye mafuta na service, si unajua movement nazozifanya kwa siku?. Pia hii gari ni ya Bossy natakiwa peleka hesabu kila mwisho wa mwezi, atleast ungefanya 3,500,000/= itakuwa ni mutual benefit kwa pande zote.”

IRYN: “Suala la mafuta siwezi kukupinga hata mimi nimeona, okay nimekubali hio 3,500,000/= sio mbaya, kama ikitokea kwasiku umetumia mafuta zaidi ya elfu 30 uwe unaandikia sawa?”

MIMI: “Sawa haina shida Bossy, pia naomba nisamehe kama kuna sehemu nimekukwaza.”

IRYN: “It’s okay Insider mimi sina shida na wewe ila kwasasa naomba tufocus na kampuni kila mtu aendelee na mambo yake personal.”

MIMI: “Hapa umeongea point sana, pia naomba masuala yetu ya kazi yabaki kuwa ya kazi sio unaanza mshirikisha mama J, kwa hili tutagombana.”

IRYN: “Sawa Insider nimekuelewa.”

Na muda huu Iryn alimuita yule Jamaa ili afanye utambulisho na mimi muda huu mapigo ya moyo yaliongezeka sana maana nilijua naenda pigwa na kitu kizito.

IRYN: “Insider huyu anaitwa Jimmy ni kama kaka kwangu ni mtoto wa Mamkubwa wangu (Dada wa mama yake). Yuko hapa kwasababu ya masuala ya organization aliyoacha mama kule Ethiopia nafikiri tulishaongea haya.”

Baada ya huu utambulisho kidogo nikawa na amani.

MIMI: “Hapana hujawai kunambia hili.”

Kwa upande wangu nilikuwa najua suala la Organization kupitia kuisoma ile Diary ya mama yake lakini nilijifanya sijui.

IRYN: “Bhasi sikukukwambia, ndo hivyo mama aliacha hio Organization ndo nitashirikiana na kaka yangu Jimmy na pia Jumamosi nitaondoka kwenda huko.”

MIMI: “Mr Jimmy it’s my pleasure meeting you again.”

JIMMY: “Thank you brother for caring my sister and she told me everything about you. I really appreciate that.”

MIMI: “Thank you brother, Iryn mimi nilijua jamaa ni shemeji maana nilishangaa hutaki kunitambulisha.”

Niliongea kiswahili sababu nilijua jamaa asingejua tunacho zungumza na muda huu Iryn alicheka sana.

IRYN: “Insider bhana, remember nilishakwambia before sisi Waafrica tunawaza mabaya tu.”

MIMI: “Mimi nilifurahi tu hata ingekuwa kweli ningekuunga mkono, napenda kuona ukiwa na furaha, sasa mbona anakaa mbali na wewe wakati apartment yako ina room 2.”

IRYN: “Insider unaweza kulala kwa mdogo wako wa kike na ukawa comfortable?”

MIMI: “Mmh inadepend na mazingira.”

IRYN: “Okay yeye alitaka kuwa huru ndomana nikamtafutia apartment pale ya muda ili tuwe jirani.”

Yalikuwa ni mazungumzo ya karibu masaa 2 na tulifanikiwa kumaliza tofauti zenu na jambo kubwa alisema kila mtu afanye mambo yake binafsi na tu-focus na kampuni tu.

Nilimshukuru Iryn kwa kunipa mkataba mpya na kuhusu suala la mkataba Iryn alisema anaundaa then atanitumia kwa email. Na baada ya kuachana pale tuliagana na mimi niliondoka kuelekea home.

******
Baada ya mkataba na deal mpya majukumu yaliongezeka kama masuala ya Kodi, kuandaa budget na masuala ya mapato/mauzo nk. Kwa upande mwingine ukweli nilikuwa najiongeza sana maana nilikuwa sikosi pesa asee, bado nilikuwa naingziwa pesa za operation kama Umeme, maji, usafi na zile za emergence.

Kwa asubuhi nilikuwa na kazi ya kukusanya mauzo ya siku husika pamoja na kukagua mashine za EFD na malipo yaliyolipwa kwa simu kupitia lipa namba au bank. Baada ya kukagua taarifa zote na kuridhika nilikuwa nakwenda kudeposit pesa Bank.

Kwa salon ya Masaki ndo ilikuwa inaongoza kwa mauzo maana pale ni ushuani hata wateja wengi walikuwa ni foreigners.

Huduma zinazotolewa saloon zote ni pamoja na Kuuza mawigi, kupamba maharusi, make up, kupaka kucha rangi, kusuka, massage lakini kwa upande wa wanawake tu nknk.

Kwa upande mwingine hata heshima yangu iliongezeka sana ofisi zote kuanzia Mikocheni mpaka Masaki na wafanyakazi walikuwa wananipenda na kunikubali sana.

Ijumaa jioni baada ya kutoka kwenye mishe zangu nilipitia pale Salon Mikocheni na baada ya kushuka kwenye gari niliingia ndani na kuna kopo la maji lilikuwa linazagaa chini, bhasi nikaanza kuwachimba mkwara pale kwa kutozingatia usafi wa salon.

“Nyie ladies sijui nani atakuja kuwaoa nimewawekea dustbin kubwa la uchafu lakini hamjali wala nini”

Na muda huu nilianza kumzingua Lucy,

“Nambie babe wangu Lucy naona upo busy na kazi safi sana.”

Lucy alikuwa amenipa kisogo kumbe alikuwa na Iryn mimi sikumtambua maana Lucy alikuwa amesimama nyuma yake anamtengeneza nywele zake. Kwa upande mwingine kila mtu alikuwa busy na wateja, na mimi niliendeleza mautani yangu kwa Lucy.

MIMI: “Lucy sema upo vizuri sana Mungu kakujalia mambo flani amazing.”

LUCY: “Hivi Insider unajua niko na Bossy hapa anasikia ujinga wako.” Na lucy alimtoa nywele usoni Iryn ili nimtambue.

MIMI: “Bossy kumbe upo hapa,mwenyewe umetulia unatengenezwa.”

IRYN: “Mhh leo Lucy itabidi unambie ni nini kinaendelea kati yako na Insider.”

LUCY: “Insider ni mtu wa matani sana hata usimzingatie.”

IRYN: “Manager bora nimekuona unisubiri kidogo unirudishe home nikupe na ratiba za kesho.”

MIMI: “Sawa bossy mimi sina shida na nitakuwa ofisini nakusubiri.”

Sasa wakati niko ofisini nikiandaa ripoti zangu za kazi simu yangu ilianza kuita na ile kuangalia ilikuwa ni namba ngeni ya Airtel na mimi nikapokea simu.

Naam, alikuwa ni Mzee Juma aliyepiga na alikuwa ananipa taarifa za kurudi Dar es salaam na kubwa alisema Jumamosi saa 1 usiku tuonane pale Serena hotel ili tuzungumze suala langu aliloachiwa na Mzee, pia tupate na dinna ya pamoja.

Baada ya kuwasiliana na Mzee Juma ukweli nilifurahi sana muda huu maana nilijua tayari nakwenda kupata deal la maana. Na nilijisemea pale kama nitapata deal bhasi hili la Iryn nitapiga chini na baada ya dakika 5 alikuja Lucy pale ofisini na tukaanza kupiga story pale,

LUCY: “Insider mbona unaonekana kuwa na furaha sana?.”

MIMI: “Sababu nimekuona ndomana.”

LUCY: “Ushaanza mautani yako, leo weekend naham na savanna tupitie Mlimani City badae.”

MIMI: “Leo nataka kurudi home mapema nina mazungumzo na mama watoto wangu, tufanye kesho kama vipi.”

LUCY: “Afu simjui wifi yangu embu nioneshe hata picha yake, Junior namjua alikuja na Iryn na pia umemuweka kwa profile Whatsapp.”

Na mimi nikatoa simu nikaanza kumuonesha picha za Mama Junior na yeye akawa anaangalia.

“Wifi yangu mzuri ndomana Junior amechukua uzungu wa baba na mama.”

Na wakati tunapiga story Lucy alikuwa amekaa pembeni yangu maana ofisini kuna coach na muda huu Iryn alifungua mlango na akaingia ndani.

IRYN: “Lucy sikuelewi best yangu mama Junior ana taarifa hizi?”

LUCY: “Ndo nilikuwa naangalia picha za wifi yangu hapa ili nimjue, maana namjua Junior tu. Ukweli wifi yangu ni mzuri sana Insider unajua kuchagua mke.”

IRYN: “Insider huyu hata simuamini kabisa ila Mama Junior ametulia anajitambua sana, umri wake ni mdogo ila ana mambo yake ni smart sana. Insider kwa hili nakupongeza kwakweli kama mke unaye na anakupenda sana acha utani wako na kina Sumaiya.”

LUCY: “Bora umwambie ukweli maana anasahau kama yeye ni mme wa mtu.”

Na mimi muda huu nilikuwa mpole wakinipa vichambo ikabidi nibadili mada pale,

MIMI: “Lucy unajua kumpendezesha sana Bossy inabidi akupe hela ya savanna leo.”

LUCY: “Umeona eeh ila bossy hanaga noma atanipa tu.”

IRYN: “Insider mpe Lucy elfu 30 nitakupa home tukirudi.”

Na mimi nilitoa elfu 30 nikampa Lucy, ukweli ni kwamba Iryn anampenda sana Lucy sababu ya uchapaji kazi wake. Pia alimwongezea mshahara kutoka laki 6 mpaka 8 na bado alikuwa na bonus za kila mwezi, bado hajapiga deal so alikuwa vizuri tu.

Baada ya hapo tuliondoka na Iryn kwenda kwake na tulitumia muda mchache kufika pale na mimi nilimkabidhi mkataba maana nilikuwa nimesha ujaza. Pia nilimuuliza kuhusu suala la bonus na alinambia mimi niko treated as Manager hivyo masuala ya bonus mpaka mwisho wa mwaka na nitapata bonus kutokana na faida itakayo patikana kwenye kampuni.

Iryn pia aligusia kuhusu lile suala la gharama za T-shirts pamoja na canvas akasema atanirudishia cost zangu. Kwa upande mwingine alipendekeza kuanzia tarehe 1 wafanyakazi wote waanze kuvaa sare hivyo itabidi niprint T-shirts nyingine nyingi.

Na muda huu tulianza kuongea masuala ya safari yao ya kesho,

IRYN: “Sasa kesho tunaondoka na Ethiopian Airlines ya saa 11 jioni so uwai kufika hapa unipe kampani.”

MIMI: “Ok no problem unanijua vizuri kwenye suala la muda, twende nikusindikize mpaka ndani au kaka yupo?”

IRYN: “Amenambia yuko Masaki, hivi unajua kaka yangu ni mtu wa madem sana ndomana hakutaka kukaa na mimi hapa ili awe huru. Yuko addicted sana na wanawake maisha ya Ufaransa yamemuharibu sana kwakweli maana anapenda sana ngono.”

MIMI: “Anaonekana ni kiwembe kama kafika Tanzania kwa mara ya kwanza na ameyajua machimbo ya watoto wazuri bhasi ni hatari sana.”

Na mimi nilichukua nafasi hii kumpa zawadi yake ya canva na ilikuwa kwenye bahasha na nikamwambia ataifungua akiingia ndani. Baada ya kumaliza maongezi tuliagana na mimi niliondoka kurudi home.

Hii siku nilikuwa na kikao na mama J hivyo sikutaka kuchelewa kurudi home na wakati niko njiani Iryn alinipigia simu na alinishukuru sana kwa zawadi ya canva pamoja na suala la kukubali mkataba mpya. Kwa upande mwingine aliendelea kukazia suala la kila mtu kufocus na maisha yake binafsi.

Baada ya kuwasili home nilikuwa na kikao na wife na kubwa ilikuwa ni kuhusu suala la kuhama nyumba sababu mazingira hayakuwa salama kwa mtoto na Junior alikuwa amenza kutembea. Hivyo tulipanga mpaka kufikia mwisho wa mwezi tuwe tumehama tayari.

Pia tulijadili suala la kwenda Dodoma site ili wife aione nyumba pamoja na mazingira yake na tulipanga kwenda mwisho wa mwezi maana alikuwa kafunga chuo tayari kipindi hiki.

Kwa upande mwingine tulizungumza suala lake la ukaribu na Iryn na nilimwambia awe makini sana na asivuke mipaka, atambue yule ni Boss wangu na anatakiwa kuheshimu hili.

Pia kupitia haya maongezi nilibaini kwamba wife hakupiga simu ile jumapili bali ni Iryn aliyepiga simu kwa mama J na ndo kujua sikutumwa bandarini.

*******
Jumamosi saa 7 mchana nilikwenda kumchukua Bossy lady kwaajili ya kumpeleka Airport na baada ya kuwasili pale kwake nilimpa taarifa na akasema anatoka.

Msimamo wangu ulikuwa ni uleule kutoingia ndani kwake na baada ya dakika 10 alitoka amewaka sana lakini mimi nilivunga sikutaka hata kumsifia.

Alikuja upaka usawa wa gari yangu na akanigongea dirishani na akanambia tunaondoka na Range then nitaipeleka kwa Mama Janeth. Ukweli hii ndo ilikuwa siku yangu ya kwanza kuendesha Range hivyo nilikuwa na wasiwasi sana.

“Bossy nitaweza kweli huu mziki?”

“Kwanini ushindwe? Wakati gari zingine unaendesha vizuri?”

Niliingia ndani ya gari na Iryn alikuwa upande wangu wa kushoto akinielekeza vitu vidogo na tukaanza safari, lakini tulipitia Palm village ili kumchukua kaka yake na baada ya kuwasili pale ilitubidi tuingie parking za ndani kabisa kumchukua.

Baada ya dakika 10 jamaa alitoka akiwa na demu na muda huu Iryn alinikonyeza na alionekana kumsikitikia sana kaka yake kwa zile tabia za umalaya. Kwa upande mwingine jamaa alionekana akiagana na demu na dizaini kama walikuwa wanabadilishana namba za simu na wakaishia kukumbatiana.

Jamaa alikuja usawa wa gari yetu akaweka bag lake kwa buti na akaingia ndani akakaa seat za nyuma. Jamaa alitusalimia muda huu na wakaanza kuongea na Iryn kwa kifaransa na mimi nilihisi lazima atakuwa anamchamba kaka yake.

Ndani ya lisaa tuliwasili pale JNIA Terminal 3 na tulikuwa tumewahi hivyo tulienda kukaa pale BAO cafe tukipata bites na juice na story zilikuwa zikiendelea. Iryn pia aliniachia maagizo na akanambia ijumaa atakuwa amerudi tayari na mimi baada ya nusu saa niliwaaga na niliwatakia safari njema, sasa ile wakati naondoka Iryn aliniita “Insider….” na akaja kuni-hug.

Wakati natoka pale Airport saa yangu ilikuwa inaonesha ni saa 9 mchana hivyo niliwaza kwanza kwenda kurudisha gari Masaki, then niendelee kubuy time pale Salon kwa Sumaiya navyosubiri muda wa kwenda kuonana na Mzee Juma.

Baada ya kuwasili kwa mama Janeth nilipark gari na niliambiwa yeye hayupo hivyo niliondoka nikaenda kwa Sumaiya. Pale ofisini mazingira yalikuwa na wateja wengi sana hivyo niliamua kuondoka niende nikapoteze muda Cocobeach.

Baada ya kuwasili pale nilikwenda kukaa kwa siku zote na jamaa alikuja kunisikiliza pale,

“Tajiri si heineken kama kawaida?”

“Hahahaa hapana Tajiri leo nataka dafu na mishikaki tu.”

“Juzi shem alikuja peke yake hapa na alionekana kuwa na mawazo sana.”

“Ulimuuliza shida ni nini?”

“Kaka hivi naanzaje kuongea na kisu kama kile? Hata kumsalimia napataga tabu. Braza hongera sana maana una bahati ya kuwa na mrembo mkali sana hapa bongo.”

“Hahahah kaka kalete odda yangu kwanza mengine tutaongea ukija.” Na muda huu wote tuliishia kucheka tu.

Namimi niliendelea kukaa pale mpaka jioni ya saa 12 ndo nilimpigia simu Mzee Juma na akanambia saa1 niwe niko pale nimefika. Baada ya dakika 20 nilifanya kurequest Uber ya kunipeleka Serena Hotel na mapema nilikuwa nimewasili pale hotelini.

Nilimpigia simu Mzee Juma kumpa taarifa nimewasili na akanambia niende Restaurant amekaa ananisubiri pale. Nilikwenda moja kwa moja mpaka restaurant na nilimwona mzee Juma kwa mbali na mimi nilisogea mpaka kwenye meza aliyokuwa amekaa.

Baada ya kufika pale mezani tulisalimiana na mimi nilivuta kiti nikakaa na Mzee alisema tupate kwanza dina then maongezi mengine yaendelee.

Dina Ilikuwa ni bufee unajisevia tu mwenyewe na wakati tukipata dina tulikuwa tunapiga story za kawaida tu kama za maisha nk. Sasa baada ya kumaliza dinna ndo tulianza kuongea masuala ambayo yalinipeleka pale,

“Kijana nina deni kubwa kwako ni maagizo niliyoachiwa na rafiki yangu Pama, labda nikwambie jambo marehemu alikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana na amenisaidia mambo mengi sana. Kabla ya kifo chake nilikuwa naye hospital na alinambia nikusaidie suala la kazi na pia suala la maisha yako liko mkononi mwangu. Kwasasa sifahamu lolote kuhusu wewe hivyo naomba unambie ukweli kuhusu elimu yako, kazi unayo fanya kwa sasa na maisha yako kwa ujumla.”

“Mzee kwanza nashukuru sana kwa kunitafuta, kuhusu elimu nina digrii ya uchumi na ndani ya kipindi cha miaka 2 nilifanya kazi na taasisi X. Baada ya kumaliza mkataba nilianza kazi ya Uber na ndo nilikokutana na mzee Pama na ninafanya hii kazi mpaka sasa. Wakati naongea na mzee nilimuambia changamoto ya hii kazi kwasasa maana bei za mafuta zipo juu na wateja wamekua washida sana na yeye aliniahidi kunitafutia kazi, lakini mauti ikampata.”

“Suala la mafuta ni shida dunia nzima hili lipo wazi na unaishi wapi kwasasa.”

“Mimi nina ishi Mbezi Beach shule, pia nina mke na mtoto wa mwaka 1.”

“Hongera sana kwa kuwa na familia, kuhusu suala la kazi acha nilifanyie kazi then nitakupa majibu ila utanitumia CV yako pamoja na certified certificates. Naomba unambie kwasasa ni jambo gani umekwama na kiasi gani utahitaji ili nione ni namna gani naweza kukusaidia.”

“Jambo nililokwama Mzee ni ada ya shule ya wife pamoja na suala la Kodi, kwa vyote ni kama milion 3.”

“Sawa nitakupa cash million 5 ufanye kuclear hivyo vipengele pamoja na balance itakayobaki itakusaidia masuala mengine.”

“Ahsante sana Mzee nashukuru sana na Mungu akubarikia sana.”

“Inshaalaah! Pama alikupenda sana na alikuamini alinambia hata nyumba ya Jane wewe pia ulisimamia finishing, Jane juzi pia kanambia ulimpelekea gari aliyokuwa amenunua Pama. Kuhusu suala la gari hili Mzee hakunambia kabisa ila kwa jambo ulilofanya ni kubwa sana, uaminifu ndo kila kitu kwenye maisha ya sasa.”

“Kweli Mzee upo sahihi, Mzee Pama alinambia nisimpe gari mpaka nihakikishe Jane yupo vizuri barabarani. Baada ya kuona yuko vizuri nikaona sinabudi kumpelekea gari yake.”

“Naona Jane anaimani sana na wewe so nafikiri endelea kuwa naye karibu na hili jambo nitaomba unisaidie maana mimi mara nyingi nakuwa nje.”

“Hili Mzee usiwe na shaka kabisa, na kwa hapa Dar unaishi wapi?”

“Kwa hapa Dar ninaishi Mikocheni karibu na Tips na Familia yangu ipo pale, soon bint yangu atakuja hapa kunichukua utamwona.”

Muda huu tulikuwa tunapiga bia na wote tulikuwa tunakunywa Heineken. Tuliongea mambo mengi sana na Mzee Juma na nilijua Pama alimsisitiza sana kuhusu suala langu. Kwa upande mwingine Mzee Juma alisema Jumatano tutakwenda Mbweni kumsalimia Jane na Mrs Pama.

Saa 4 usiku bint yake alikuja pale hotelini na Mzee alinitambulisha kuwa yule ni binti yake wa pili na wa kwanza ni Kijana yake ambaye yuko nje anafanya kazi.

“Kijana huyu ndo bint yangu niliyekwambia ndo wapili kuzaliwa, Camilla huyu anaitwa Insider ni kama kijana wangu.”

Na muda huu tuliishia kusalimiana na Camilla pia alionekana kuwa na aibu sana.

Tuliondoka pale hotelini na mimi niliomba waniache pale Msasani ofisi za Zantel na kabla sijashuka mzee alitoa bahasha ya kaki akanikabidhi, nilimshukuru sana na tukaishia kuagana.

Muda huu niliona ni bora nichukue bodaboda kwaajili ya usalama wa zile pesa na sikutaka kuendelea kuzubaa pale.

Baada ya kufika nyumbani nilikwenda moja kwa moja mpaka chumbani na nilizitoa zile pesa kwenye bahasha na zilikuwa bunda 10 noti za elfu 5 na zilioneka zimetoka Bank.

Muda huu ilibidi nimkumbuke Mzee Pama licha ya kupatwa na umauti lakini bado aliniachia mtu wa kuniangalia na kunitafutia kazi. Na bado nikiwa nimekaa pale kitandani simu yangu ilianza kuita na baada ya kuangalia alikuwa ni mama wa2 akinipigia simu.

Nilipokea simu yake na good news ni kwamba mama wa2 alinambia kuwa kazi imepatikana hivyo itabidi niende Mtwara. Mama wa2 alinambia kesho ambayo ni Jumapili tuonane kwa maongezi zaidi na mimi sikutaka kumwambia chochote muda huu na niliishia kumkubalia.

Kwa upande wangu hili deal la mama wa2 sikuwa tayari kulipokea hivyo nikawaza kama nafasi imepatikana ni bora nikamuunganishia mtu kuliko nafasi ikapotea bure.

Niifanya kuwasiliana na mshikaji wangu anaitwa Dav ambaye tumesoma wote Advance (EGM) na pia tukasoma chuo kimoja ila yeye alikuwa anasoma Finance. Kwa kipindi hiki alikuwa anapiga kazi na kampuni ya wahindi kwa kujishikiza na alikuwa analalamika sana kuwa hali ni mbaya.

Baada ya kumpandia hewani Dav alisema yuko tayari kwenda ilimradi uwe mkataba wa uhakika na nikamwambia aandae CV na vyeti viwe karibu.

TO BE CONTINUED
Kati ya jambo ulilo nifurahisha ni msimamo wa uamuzi wa kutokwenda na Prisca pale Iryin apokuwa anakisubili, mwanaume mara nyingine unatakiwa kuwa mkorofi kwa muda na kuamua maamuzi magumu yenye faida kwa maisha.
 
Ni wanawake wachache sana hawasimulii kwa wengine kilichotokea baina yake na mwanaume anayempenda. Sumaiya lazima kuna siku aliamua kumkomoa boss Iryn ajue anatoka na mzee baba. Unakuta tu from No where anaropoka "halafu unajua Insider jana kashinda kwangu, ni kiwembe sana huyo ingawa ni mchapakazi". Lengo ni kuhakikisha anakuzibia kwa wengine.

Muendelezo wa story ni mzuri nafikiri watu wamepumua kwa sasa.
"Ni wanawake wachache sana hawasimulii kwa wengine kilichotokea baina yake na mwanaume"

Hili ni bonge la point Yaani insider angekaa vibaya na wafanyakazi wa saloon+kutanguliza kichwa cha chini kuliko cha juu, mapema Sana asingekuwa na chake
 
Nimekuona muda mrefu sana ukitafuta attention kwenye huu uzi ila kwa kukusaidia tu ni kwamba wanaume kwenye huu uzi huwa hawazagamui wanaume wenzao so jaribu kwenye thread nyingine
umemaliza ili nianze? mwenye uzi kakaa kimya kinachokuwasha nn, au nikufuate pm tuyajenge, i have a big dck and i know how to use it, utaenjoy sana.
 
Uzi unazidi kunoga inogile stori imefikia patamu
•Kazi zinamfuata INSIDER MAN
•Tusikurupuke kufanya maamuzi mara nyingine tenah mawazo yetu KWA iryn yanaangukia pua🤣🤣🤣


Nasubiri muendelezo tu asee stori ni tamu balaa inaelimisha,inaburudisha,inasisimua ..Ndugu INSIDER MAN chukua 🌹💐yako Bravo⭐⭐⭐⭐
 
Haya maisha hayana usawa insderman ana uhakika wa kazi 3,kwa iryn,mzee juma na mama wa2.
Sisi wengine hata kazi za saidia fundi tunatolewa mbio

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kila mtu na alichoandikiwa endelea kupambanaa ipo siku milango itafunguka tuu MUNGU tunaemwomba wote ni mmoj na hana upendeleo ni swala la muda tuu mkuu
 
Back
Top Bottom