Kuna mtu humu ndani aliandika nilikuwa sina mipango ya maisha kama kufungua biashara nk, niseme sitaki kushare personal life yangu humu ndani ila nin miradi mingi ambayo nai run.
Kitu cha kwanza niliona kwanza ni busara wife akawa na miradi yake ili kupunguza dependecy kwangu, na hizi ni project ambazo tulizijadili na wife ilikua April, 2022.
View attachment 2768463
MCHANGANUO.
1. Biashara ya kwanza ilikuwa ni butchery ambapo wife angeuza Kuku, samaki, Mayai nknk, changamoto ilikuwa kuanza ni mahitaji mengi yangehitajika kuanzia frem, ukarabati, mashine nknk so cost zilikuwa kubwa sana, tukaipiga chini.
2. Biashara ya pili ilikuwa ni kuuza nguo za watoto na tulianza kufanya Research namna ya kupata suppliers wa mizigo nknk, mizigo ni China na Uturuki lakini kwa Uturuki kwa nguo za watoto wako vizuri. Ilibidi nimcheki jamaa yangu yuko Ulaya nilishandika baada ya kutoka kwenye ile taasisi yeye alikwenda Ulaya kusoma, sasa alikuwa ana connection za huko, niliomba anisaidie kufanya Research
View attachment 2768476
Changamoto ilikuwa ni mtaji wa kuagiza mzigo mkubwa, maana mzigo mdogo ungekata sana hata faida isingeonekana. Tukashauriana tuachane nayo tutadeal nayo baadae,
3. Biashara ya 3 ndo ambayo tunaifanya mpaka sasa na inafanya vizuri na ipo chini ya mchaga wangu mama J. Masuala ya fedha ofisi ipo Mbezi Beach pamoja na biashara ya Vinywaji ila zipo maeneo tofauti. Ukirefer post zangu za nyuma nilishawai kuja humu ndani kuomba connection za kreti na chupa za soda, ilikuwa kwaajili ya hii Biashara.
4. Biashara ya 4 na 2 Wife ana mpango wa kuja kuzifanya baadae akimaliza chuo.
Kuhusu mama J sina shida naye anafanya vizuri sana na ana akili ya biashara sana, anajitegemea kifedha ukiniuliza ni lini nimempa pesa za matumizi nimesahau. Matumizi ya home anatake care mwenyewe labda mimi niwe safari ndo nitakuja na Kuku, mafuta nknk ila pesa zitoagi.
Hata leo nikifa naamini Junior hata pata shida maana mama yake ni mchacharikaji atakuwa sehemu salama.
Mimi niliamua kuwekeza Dodoma ndo mpaka sasa na project zangu huku,
Mnaomdharau Mama J wangu kwenye hii story poleni sana, namuheshimu sana huyu mwanamke, anahudumia watoto church, anasoma bado anasimamia biashara na zinakwenda vizuri.
Leo hii baada ya kutoka church wife kanambia anataka December aaagize gari yake mwenyewe, nimefurahi sana baada ya kupata hizi taarifa.