Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 40

THIS EPISODE IS SPECIAL FOR IRYN.

CONTINUE…..

Mama Janeth muda huu hata hakuwa na pingamizi kwa jinsi Iryn alivyokuwa na furaha ya kuniona asingeweza kumzuia wala kumkataza. Na muda huu Mama Janeth alionekana kuwa na furaha sana na mimi nilitumia nafasi hii kumsalimia na alinambia kwa taratibu “please! takecare of her.”

Tuliongozana na Iryn mpaka nilikokuwa nimepark gari na tukaanza safari ya kuondoka pale Airport. Wakati tuko kwenye gari Iryn alikuwa ananiangalia sana na alikuwa na uso wenye furaha sana. Na mimi sikutaka kumwuliza jambo lolote muda huu,

MIMI: “How was your flight.”

IRYN: “Thanks God nimefika salama.”

MIMI: “Umetua na ndege gani?”

IRYN: “Qatar Airways japo tulichelewa ku-land.”

MIMI: “Haina shida cha muhimu umefika salama tu.”

IRYN: “Insider unanipeleka wapi? Naskia njaa.”

MIMI: “Nafikiri twende Mliman city ili tuongee pia.” Na muda huu nilikuwa serious kidogo.

IRYN: “Sawa haina shida.”

Baada ya kuwasili pale Mlimani city na kupark gari tulikwenda moja kwa moja mpaka instanbul restaurant ndo sehemu ambayo naonaga imetulia sana na inafaa kwa mazungumzo.

Baada ya kufika pale tulichagua sehem nzuri ya mwishoni kabisa na tukakaa na muda huu mhudumu alikuwa amefika kutusikiliza, tuli odda chakula na Iryn alikuw akiniangalia sana kama mtu anayetaka kusema jambo ila kama anasita.

MIMI: “Mbona kama una wasiwasi upo sawa kweli?”

IRYN: “Insider I’m really sorry for what all happened.”

MIMI: “Nakusikiliza kwa makini sana unambie kwanini uliamua kuondoa bila kuniaga hapo ndo nitaangalia nikusamehe au laah. Hivi unajua ni jinsi gani uliniweka kwenye wakati mgumu sana? Ilibaki kidogo sana kwenda Police kutoa taarifa hivi unafikiri mimi ningekua kwenye wakati gani?”

IRYN: “I know Insider, I am really sorry sikuu……”na muda huu Iryn alianza kutoa machozi.

Nilijisikia vibaya sana muda huu kuona akilia na ilibidi nitoe leso yangu nikaanza kumfuta machozi. Niliingiwa na huruma sana ikabidi nianze kumbembeleza nilihisi huenda Iryn alikuwa kwenye wakati mgumu sana huko alikokuwa.

MIMI: “Mummy I’m sorry na niko hapa kwaajili yako be free kunambia kilichotokea, no matter what tuko pamoja ndomana nilikuja kukupokea Airport.”

IRYN: “Insider I’m really sorry naomba utambue sikufanya makusudi kuondoka bila kukuaga ila ile siku nilipewa habari mbaya sana na Mama Janeth. Ni habari ambazo zilinikosesha raha nilijikuta na hatia sana ile siku.”

MIMI: “Kwanini unasema hivo? Ni habari gani mama Janeth alikupa?”

IRYN: “Ile siku nilikuwa chumbani nimelala nikapigiwa simu na Mama Janeth Kuwa Baba yangu amelazwa yuko hali mbaya na anahitaji kuniona haraka wakati ule. Insider unajua licha ya kuwa na uhasama na Baba yangu lakini nilikuwa bado nampenda sana.

Mama Janeth aliniambia nijiandae haraka tuondoke kwani kuna ndege imepatikana na itaondoka saa 00:30 usiku. Ilibidi niamke nianze kujiandaa haraka na kupanga nguo baadhi ya kuondoka nazo na wakati najiandaa nilipigiwa simu kuwa gari iko nje tayari inanisubiri ili tuondoke. Insider niliondoka kwa haraka sana muda huu na wakati tumeshaondoka nilikuja kugundua nimesahau simu na sikuwa na jinsi tena.

Baada ya kufika Airport nilikutana na Mama Janeth akasema ananisindikiza mpaka South Africa afu yeye atakwenda USA ana kikao cha mwaka kule. Tulifika South Africa alfajiri na tukaenda moja kwa moja mpaka Hospital aliyokuwa Baba amelazwa Cape town. Insider nilimkuta Baba akiwa hali mbaya sana alikuwa anapumulia mashine tu alikuwa ICU. Nililia sana maana nilijua nakwenda kumpoteza baba na nina kuwa yatima.”

Na muda huu alianza kulia tena na dada alikuwa kashaleta chakula pale mezani. Na mimi niliendelea kumfuta machozi na kitambaa changu.

MIMI: “Aisee pole sana mummy ukilia hivi unaniumiza na mimi.”

IRYN: “Ahsante, Insider unajua nilianza kusali sana muda ule na nilikaa pale nje namsubiri kwa bench. Nilisema siondoki mpaka niongee na Baba, saa4 asubuhi ndo tuliitwa tuingie tena ndani tukamwone. Nilimkuta Baba kidogo afadhali na alikuwa anaongea japo kwa shida, kitendo cha kuniona ni kama nilirudisha furaha yake kwake na nilimsogelea tukaanza kulia wote pale.

Tuliondoka pale na mdogo wangu ambaye ndo mtoto wa kwanza wa mzee kwa upande wa mamdogo mpaka home na mama Janeth aliniaga anaondoka kwenda USA. Insider nilikuwa nashinda nasali tu maana mzee angekufa sidhani kama Mungu akangenisamehe maana nilikuwa na kinyongo na Baba, na toka msiba wa mama sikuwai kaa naye chini japo alikuwa akinisisitiza sana tuzungumze.”

MIMI: “Kweli kabisa Mungu asingusamehe maana sisi sote ni watenda dhambi hakuna mkamilifu.”

IRYN: “You’re right, Jumapili Baba alikuwa yuko vizuri kiafya na aliruhusiwa kwenda nyumbani, Insider baba yangu anasumbuliwa na kansa hivyo anahesabu siku za kuishi tu hapa duniani.”

MIMI: “Very sad najisikia vibaya sana kwakweli lakini nashukuru Mungu Mzee bado mzima tuendelee kumwombea.”

IRYN: “Nashukuru Mungu tumeyamaliza na Baba na nimetambua baba hakuwa na kosa alikuwa sahihi kuoa mke mdogo.”

MIMI: “Kwanini unasema sahihi wakati alisababisha kifo cha mama yako?”

IRYN: “Insider Baba alioa mke mdogo kwa siri sababu mama yangu hakuwa na uwezo wa kuzaa tena baada ya kunizaa mimi. Kwahiyo mimi ndo mtoto pekee niliyebahatika kuzaliwa kwa mama. Baba anasema kama Mwanaume asingeweza kuwa na mtoto mmoja hivyo ilimlazimu kufanya hivyo ili awe na watoto wa kuendeleza ukoo. Niliona baba alikuwa sahihi kufanya vile, mwenyewe niliwaza hakuna Mwanaume kwasasa ambaye yuko tayari kuwa na mtoto mmoja, Insider wewe ungeweza?”

MIMI: “Hapana kwakweli baba alikuwa sahihi maana wewe ukiolewa unakuwa upande wa mwanaume.”

IRYN: “Huo ndo ukweli, Insider baba anataka mimi kuwa msimamizi wa mali na kampuni zake zote zitakuwa chini yangu, maana mimi ndo binti yake pekee ambaye nina jitambua na Mzee ameona mimi nitafaa kuwa msimamizi.”

MIMI: “Kwani watoto wa mamdogo wana umri gani?”

IRYN: “Wa kwanza ni wa kike ataanza bachelor mwakahuu na wengine wawili ni wa kiume bado wadogo.”

MIMI: “Ulinambiaga mzee ana mtoto wa nje mkubwa vipi?”

IRYN: “Yule ameshaharibika Insider anatumia heroin afu ni mtoto wa nje, baba anampango wa kumsaidia kivingine. Kama pesa za mitaji kapewa lakini hakuna alichofanya cha maana mpaka sasa.”

MIMI: “Aisee! Huyo mamdogo wako amekubaliana na mawazo ya mzee hajaonesha sign yoyote mbaya?”

IRYN: “No she is very happy na amefurahi sana mimi kuyajenga na Baba, kampuni zote zitakuwa za familia but under my watch. Na ninavyoongea na wewe hapa Baba amenikabidhi documents zote muhimu za kampuni na password za account za kampuni.”

MIMI: “Aisee hongera sana huku mama kule Baba na kote unahitajika itabidi ufocus now.”

IRYN: “No way na October nitarudi South Africa kusoma Masters, naenda kule ili niwe karibu na baba na pia ndo nitakabidhiwa rasmi madaraka na Baba.”

MIMI: “Utaweza kumanage South Africa na huku?”

IRYN: “Insider unasahau kama nina bachelor ya Business Administration? kitu kidogo hiko kinishinde?, kuna mpango nauandaa nitakushirikisha.”

MIMI: “Kwahaya yote mimi nimekusamehe pole sana kwa yote.”

IRYN: “Insider nilikuwa kwenye wakati mgumu sana hata kukumbuka kuna Insider naanzaje wakati baba ana hali mbaya?. Hivi unajua namba yako nimeipataje? Ile Jumapili ambayo tumerudi na Baba kutoka hospital nilianza kukumbuka wewe, maana nilijua utakuwa unanitafuta sana. Japo sikufikiria kama ungewaza kwenda Police.”

MIMI: “Tulianza kuogopa maana kuna mlinzi wa Jiran alisema aliiona Noah nyeusi imepark getini nje na ilitoka kwa spidi sana. Sisi mawazo yetu umetekwa maana baada ya kufungua mlango tuliona simu kitandani na imezimwa na baada ya mlinzi kusema hayo tulipagawa sana.”

IRYN: “Maskini poleni sana simu ilikuwa haina chaji afu ile iliyonifuata ni Mercedes Van nyeusi ina muundo kama wa Noah tu, ila kwa mbali mtu angesema ni Noah.”

MIMI: “Si unajua wabongo? So uliipataje namba yangu?”

IRYN: “Dada yule Agent ulikochukua mizigo ndo alonisaidia kupata namba yako. Baada ya kumtafuta Mama Janeth hakuwa online na nikapata wazo la kumtafuta yule dada Agent mpya. Nilikuwa na history ya kuchat nae kupitia email na nilijua lazima tu angekuwa na namba zako. Baada ya kumtext huwezi amini alirespond within 30mins na akanitumia namba yako unajua sikuaamini Insider.”

MIMI: “Daah ulitumia akili sana, unajua nilikwenda mpaka ofisini kwa Mama Janeth na niliambiwa hayupo? Lakini niliwapa details zangu wamtumie mama incase akizipata anirudie lakini mpaka leo kimya.”

IRYN: “Pole sana Insider mama Janeth alikuwa busy sana maana baada ya kwenda US ilibidi aende Ukraine si unajua masuala ya Social Protection? Kuna Research walikuwa wanafanya kule.”

MIMI: “Ina maana hata ujumbe wangu hakuupata?”

IRYN: “Aliupata, Jumatatu alinitafuta akanambia amepata ujumbe wako kuwa umtafute, so yeye alinitafuta mimi ndo nikamwambia niliondoka bila kukuaga ila nimesha kucheki tayari. Insider kitendo cha kwenda mpaka ofisini kwake Mama Janeth amekuelewa na kukubali sana, amenambia wewe ndo rafiki mwema, thank you so much for everything.”

MIMI: “Wewe kama mtu wangu wa karibu ilibidi nifanye vile. Na imekuwaje tena mmerudi wote?”

IRYN: “Aliomba nimsubiri aje amwone Mzee afu turudi wote Dar es Salaam, pia tulikuwa na mazungumzo ya pamoja.”

MIMI: “Sawa anakujali sana, tuondoke zetu nikupeleke mapema ukapumzike utakuwa umechoka sana.”

IRYN: “Insider mimi siendi kwangu nataka twende kwako na hii week nitalala kwenu sawa?”

MIMI: “Sawa karibu pale ni home tu hata usiwe na wasiwasi.”

Nilifanya malipo na tukaondoka pale Mlimani city kurudi home na njiani story zilikuwa zimekolea sana.

MIMI: “Hivi unajua una kesi za kujibu kwa Mama Junior?”

IRYN: “Kesi gani hiyo?”

MIMI: “Si aliziona zile picha za kule Zanzibar ujue.”

IRYN: “Insider umezidi sana uzembe picha kama zile ulishindwaje kuzihide au kuzifuta? Au hujui jinsi ya kuhide picha nikufundishe?. Huo ni uzembe mkubwa sana unaweza kuwa serious kwenye vitu vikubwa ukapuuzia vidogo na ndo vikakufelisha. Hivi unanitengenezea mazingira gani kwa Mama Junior? hata kama hatuna mahusiano kwa Mke hawezi kukuelewa even to me siwezi kukuelewa kabisa.”

MIMI: “Kweli nilizingua sana kwa hili, ujue toka tumetoka Zanzibar sikukaa chini nikatulia na suala lako lilinipa sana stress. Na aliziona baada ya kumpa simu Junior aangalie Cartoon ndo alipata chance ya kukagua.”

IRYN: “Insider unajua Mama J wako ana wivu sana na wewe, na pia anakupenda, inatakiwa hili ulitambue. Ilinde simu yako kama uhai wako wewe ni Mwanaume unawasiliana na watu tofauti usipokuwa makini itakucost siku kama nilivyokwambia awali.”

MIMI: “Uko sahihi this time nitakuwa makini sana, ila alielewa mpaka leo hajawai kuulizia tena.”

IRYN: “Uzuri nilimwambia kwamba tuko wote Zanzibar hili nalo limesaidia, nisingemwambia na akaona hizo picha ingekuwaje?. Mama Junior nilishamsoma mapema sana na nitaendelea kumweka sawa taratibu.”

MIMI: “Sawa bhana ngoja nione reaction yake akikuona.”

Tuliwasili pale home nikatoa mabag yake na nikamkaribisha ndani na muda huu dada alikuwa katoka nje kunipokea.

“Dada peleka haya mabag chumbani kwako.”

Tulikaa pale seblen na Iryn alikuwa busy sana na Junior maana alionekana kum-miss sana. Na muda huu aliomba bag lake kubwa aletewe na baada ya dada kulileta alilifungua bag na lilikuwa limejaa mazawadi tu.

Kwa upande wangu alikuwa ameniletea zawadi za viatu, nguo, saa na laptop ya Macbook Air mpya kabisa.

IRYN: “Insider hii Laptop itakusaidia kuandaa kazi zako na report za kampuni.”

MIMI: “Thank you Mummy.”

Ukweli sikutegemea kama Iryn angeniletea zawadi ya Macbook na niliifurahia sana hii zawadi. Kwa upande wa Junior alikuwa kamletea Ipad ya kuchezea, nguo za kutosha na viatu.

IRYN: “Hizi za Mama Junior wewe hazikuhusu ataangalia mwenyewe badae, dada rudisha bag ndani. Dada wewe nimekusahau sorry nitakupa hela ukafanye shopping.”

DADA: “Ahsante Dada.” Dada Junior alionesha kufurahia baada ya kusikia atapewa hela akafanye shopping.

IRYN: “Insider mimi si nipo hapahapa kesho tutakwenda naye Sinza au unaonaje?”

MIMI: “Sawa haina shida itapendeza zaidi.”

IRYN: “Vipi kuhusu maendeleo ya ofisi?”

MIMI: “Salama kabisa nikiwa na Lucy na Sumaiya mambo yanakwenda vizuri kabisa.”

IRYN: “Kesho tutakwenda wote kuangalia maendeleo.”

MIMI: “Sawa haina shida mummy.”

Tulikaa pale tukiendelea na mazungumzo yetu na jioni Mama Junior alirudi kutoka chuo na baada ya kuingia ndani na kumwona Iryn alikwenda mbio na wakakumbatiana.

TO BE CONTINUED

“Sorround yourself with People that love you for you and love them back. Because love is the one thing in this world that’s worth fighting for.”

Week hii sitakuwepo tukutane Jumapili [emoji120]

EPISODE 41[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
40
 
Nikupongeze mno insider, umetuburudisha na kutuelimisha. Sikuwahi kucoment chochote tangu mwanzo wa uzi, lakini nilikuja pm wakati furani Hali ya hewa ilipochafuka humu juu ya kama Uzi huu ni real story au fiction.


Some men are just lucky, and you are one of them. Umekutana na mwanamke aliyebadili maisha Yako, hongera .
 
EPISODE 41

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

Tulikaa pale tukiendelea na mazungumzo yetu na jioni Mama Junior alirudi kutoka chuo na baada ya kuingia ndani na kumwona Iryn alikwenda mbio na wakakumbatiana.

CONTINUE…..

MAMA J: “Ilikuaje ukatukimbia bila taarifa? ulijua kutuweka Roho juu.”

IRYN: “Acha tu mpenzi ilikuwa ghafla nilikuwa nauguza mwenzako afu nilisahau simu am really sorry.”

Na mimi muda huu niliondoka nikaingia chumbani na niliwaacha pale seblen wawe huru kuongea. Na wakati niko chumbani nikishangaa zile zawadi zangu nilizoletewa, simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikuwa ni Lucy anapiga.

“Lucy mambo.”

“Poa Insider nimeshindwa kuvumilia mwenzio, Iryn amekuja leo kweli?”

“Yeah niko nae hapa home.”

“Wow anasema alikuwa wapi?”

“Tutaongea Lucy huu sio muda mzuri kwa sasa.”

“Poa Insider byee”

Lucy alionekana kufurahia sana hizi taarifa za kurudi kwa Iryn. Na muda huu nilitoka pale seblen na walioneka Mama J na Iryn kuwa na furaha sana wakiongea na kucheka.

IRYN: “Insider badae utatutoa out tukapate Dinna as family.”

MIMI: “Mnataka niwapeleke wapi?”

IRYN: “Mimi nime-miss kula Pizza”

MAMA J: “Mimi nataka kuku wa KFC”

MIMI: “Ok ladies nitawapeleka Mikocheni Plaza nafikiri pale kila mtu atapata anachotaka.”

Saa 1 usiku tuliondoka wote mle ndani na tulikwenda mpaka Mikocheni Plaza. Na muda huu Iryn alikuwa busy sana na Junior utafikiri mwanaye. Iryn anampenda sana Junior mpaka sasa navyoandika hapa.

Na wakati tukiendelea kuenjoy Muajemi alinipigia whatsapp call na baada ya kupokea aliulizia kama nimempata Iryn, nilimwambia yuko Ufaransa akirudi nitamwambia asiwe na wasiwasi na yeye alisema anategemea kurudi katikati ya June.

Hii siku kila mtu alionekana kuwa na furaha pale na tulikaa mpaka saa 4 usiku tukarudi home kulala. Tukivyorudi home tulifanya maombi ya pamoja na kila mmoja alikwenda kulala.

*******

Jumamosi asubuhi nilifanya kuwasiliana na Jane nikampa taarifa kwamba sitoweza kwenda kumchukua sababu nina emergence. Jane kwa upande wake hakuwa na shida akasema atarequest uber ya kumpeleka Posta, hivyo nisiwe na wasiwasi.

Asubuhi baada ya kupata breakfast niliondoka na Iryn ili kwenda kuziangalia Saloon zote na alisema tuanze na ya Sinza. Baada ya kufika pale Sinza tuliwakuta wafanyakazi wote na walishtuka sana kumwona Iryn maana ilikuwa ni kama saprize kwao. Baada ya Iryn kuridhika na mazingira ya pale tuliondoka na kwenda Mikocheni.

Baada ya kuwasili pale Saloon, tulishuka kwa gari na Lucy ndo alikuwa wakwanza kutuona na alikuja speed kumkumbatia Iryn.

“Wow Bossy nilikumiss sana ulituacha kwenye mataa wenzako.”

“Hamna Lucy Nilikuwa na matatizo tu.”

“Tulikuwa Roho juu wenzio mpaka nikawaza inamaana hii simu nilipewa ya ukumbusho?”

“Hamna Ahsante sana kwa kujali.”

Iryn na Lucy waliingia ndani na mimi nilikuwa nje nikiwasubiri, mara nyingi nilikuwa sipendelei kuingia ndani maana Saloon ni ya kike. Mambo ya kuingia ndani kuanza kuangaliana na wanawake nilikuwa sipendelei kabisa.

Ilimchukua kama dakika 15 Iryn kufanya ukaguzi pale na alitoka akiwa ameongozana na Lucy na aliingia kwenye gari tukaondoka kwenda Masaki.

Baada ya kufika Masaki na kupark gari tulishuka na Iryn alionesha kufurahishwa na mazingira ya nje kwa usafi uliokuwa umefanywa.

“Insider ume organise hili wewe?”

“Yes Bossy It’s me.”

“Congratulations umefanya vizuri sana kwa hili. Twende wote ndani uni-company.”

Tuliingia ndani na palionekana kuwa busy sana,si mnajua tena mambo ya weekend dada na mama zetu wanakwenda saloon kujiweka sawa. Kwa Saloon ya Masaki asilimia kubwa ya wateja ni foreigners. Iryn alifanya kusalimiana na wafanyakazi wake na tulikagua angle zote mle ndani, nilimwacha ndani akiendelea kuongea na mimi nilitoka nje.

Baada ya dakika 5 hivi Sumaiya alitoka nje na akaja nilikokuwa nimekaa. Na mimi nilikuwa niko kibarazani nimekaa kwenye coach so alikaa kwa pembeni yangu.

SUMAIYA: “Kwanini umeshindwa kunambia kama Queen anakuja?”

MIMI: “Hata ningekwambia ungeongezeka uzuri?”

SUMAIYA: “Naona Queen kaongezeka uzuri alikuwa wapi?”

MIMI: “Hayakuhusu wewe fanya kazi zako, si umuulize akwambie?”

SUMAIYA: “Sawa bhana umeshinda kwa leo. Umenunua gari mpya?”

MIMI: “Ndo maana yake vipi unataka nikupe lift?”

SUMAIYA: “Sijaomba lift nimeuliza maana nimeona umekuja na gari mpya nikajua itakuwa ya Queen.”

MIMI: “Unaonekana unapenda sana magari wewe mtoto.”

Sumaiya alianza kunipiga muda huu na Iryn alitoka akauona ule mchezo, maana nilikuwa nimemkamata mikono Sumaiya na yeye alikuwa anafurukuta kujinasua.

“Insider tuondoke.”

Nilimuachia Sumaiya na tuliongozana wote muda huu kuelekea parking, Iryn na Sumaiya walikuwa wanazungumza. Mimi nilikuwa wa kwanza kuingia kwa gari na baada ya kumaliza mazungumzo yao Iryn aliingia kwenye gari piana Sumaiya alikuja upande wangu.

“Insider leo weekend uliniahidi kunitoa out au umesahau?”

“Huna hadhi ya kutoka out na mimi”

“Wewe si ndo uliniomba? unajishaua sahivi.”

Nikawasha gari kuondoka maeneo haya na muda huu Iryn alikuwa akininitazama sana

MIMI: “Nambie Bossy wangu?”

IRYN: “Sikuelewi na Sumaiya naona mmeshazoeana kwa kipindi kifupi sana.”

MIMI: “Achana na Sumaiya ni mwongeaji by nature na utani mwingi.”

IRYN: “Mtimizie ahadi yake ya kumtoa out.”

MIMI: “Anazingua tu hakuna ahadi niliyompa tunakwenda wapi? au nikupeleke ukasalimie majirani?”

IRYN: “Today? sijisikii kwenda huko kabisa.”

MIMI: “Hapana inabidi uende ukachukue na simu, majirani nilikuwa nao bega kwa bega.”

IRYN: “Okay lets go”

Tulitumia muda mchache kuwasili pale Kijitonyama na niliingiza gari ndani. Tulikwenda moja kwa moja kwa Rose na baada ya kumgongea alitoka haraka, na alivyomwona Iryn alifurahi sana wakaishia kukumbatiana tu muda huu. Na mimi niliwaacha waendelee na mazungumzo yao nikaingia ndani kwa Iryn nika-kaa kwenye coach.

Baada ya dakika 10 Iryn alirudi ndani na aliingia moja kwa moja mpaka chumbani kwake na mimi nilimfuata hukohuko.

“Insider suala la Apartment ulifikia wapi?”

“Dada analifanyia kazi on monday tutaenda kuziangalia.”

“Insider hapa sirudi tena, navyotoka kwako nakwenda kwenye apartment mpya.”

“Sawa haina shida nitafanya mawasiliano na dada afu nitakupa mrejesho.”

“Sawa tuondoke hapa, mimi sitamani kuendelea kuwa hapa.”

“Leo hupapendi kwako?

“Pamenikinai acha niwai nikacheze na Junior wangu.”

Tuliondoka Kijitonyama na tukarudi home na tulikuta lunch ikiwa tayari mezani. Baada ya kula Iryn alisema itabidi tutoke tena kwenda Sinza kwaajili ya kumnunulia nguo Dada yake Junior maana alikuwa amemuahidi.

Jioni tulitoka wote kasoro mama J tu alikuwa amebaki, na tulikwenda Sinza na tulitumia Barabara ya Mbezi chini. Lengo langu ni kupita chini kwa chini ili tukaibukie pale ITV kuepuka foleni ya pale Mwenge.

Na wakati tuko Barabara ya kule chini Iryn aliyapenda maeneo na mazingira ya kule chini.

IRYN: “Insider huku chini kumekutulia sana nimekupenda sana kama nitapata huku nitakuwa jirani na Junior.”

MIMI: “Dada nilimwambia atafute mpaka huku so ngoja tuone hio jumatatu atakuwa amepata maeneo gani.”

IRYN: “Sawa eti Junior nikikaa huku sindo vizuri niwe nakuja kukufuata home nakurudisha jioni sindio mme wangu….”

MIMI: “Junior hata hakuelewi hapo.”

IRYN: “Ananielewa sana huoni anacheka hapa.”

MIMI: “Hivi Iryn unajua kuendesha gari?”

IRYN: “Insider mimi mpaka Manual naendesha na nina cheti cha mafunzo nilijifunzia Ufaransa, naendesha gari vizuri kabisa.”

MIMI: “Itabidi siku nikuachie uendeshe nikuone.”

IRYN: “Kesho tutakwenda Masaki kuangalia nyumba yetu sikukwambia afu.”

MIMI: “Nyumba ipi ile ya mama au?”

IRYN: “Tuliyokuwa tunakaa zamani before mama hajafariki, Mzee alinipa kazi ya kuisimamia nataka nikaonane na dalali wa pale.”

MIMI: “Sawa kesho hiyo nitakupa na gari uendeshe nimechoka kukuendesha.”

IRYN: “Sawa wewe unataka tu kuniona nikiendesha gari? Kesho si hakuna Police? sina licence ujue.”

MIMI: “Traffic wa Tanzania tunawamudu wewe wakikudaka ongea kifaransa tu watakimbia wenyewe.”

IRYN: “Hahahahahaa usinifundishe uhuni wako.”

Tuliwasili Sinza na tulifanya shopping ya Dada Junior na alinunuliwa mazaga mengi sana. Na baada ya kumaliza tulikwenda Mlimani city tukafanya shopping ya nyumbani. Iryn alikwenda na Junior kucheza kwenye ile michezo ya watoto na baada ya nusu saa alirudi na tukaondoka kurudi home.

Hii siku tuliimalizia pale EB 25 Lounge Makonde na tulitoka mimi, Mama J na Iryn.

*******

Jumapili asubuhi niliwasiliana na Mzee Pama na nilimpigia ili kujua kama amerudi maana alisema weekend hii angerudi.

MZEE PAMA: “Kijana kuna vitu bado sijaweka sawa nafikiri katikati ya week nitakuwa nimerudi.”

MIMI: “Sawa Mzee nilikuwa nakujulia na hali pia.”

PAMA: “Ahsante sana maendeleo ya Jane yapoje?”

MIMI: “Yuko vizuri kwakweli nasubiri sauti yako nimpe gari au laah!”

PAMA: “Subiri kwanza nirudi, vipi na wewe maendeleo yako? Biashara inakwendaje.”

MIMI: “Mzee biashara ngumu kwakweli.”

PAMA: “Una elimu gani?”

MIMI: “Nina Bachela ya Uchumi.”

PAMA: “Naweza kukupa assist ya kazi na ukapata mshahara mzuri tu kama upo tayari kuajiriwa.”

MIMI: “Sawa Ahsante Mzee mimi sina shida kabisa.”

PAMA: “Nikirudi tuta discuss hili, ila nakuomba sana umwangalie Jane maana ana kiumbe wangu.”

MIMI: “Usiwe na wasiwasi Mzee nakuhakikishia.”

PAMA: “Kama kuna lolote utanipigia simu usiwe na woga kama unashida uwe unasema usikae kimya.”

MIMI: “Ahsante Mzee nitakuwa nakutafuta.”

PAMA: “Nikirudi tutaongea mustakabali wa future yako nione mipango yako, umri wako sio wa kucheza unatakiwa kuwa na mipango madhubuti.”

MIMI: “Uko sahihi Mzee, Ahsante sana.”

PAMA: “Mimi nakuacha tutawasiliana. Naomba uzingatie niliyokwambia.”

MIMI: “Sawa Mzee uwe na jumapili njema.”

Mchana nilitoka na Iryn kwenda Masaki kuangalia nyumba na nilimwachia gari aendeshe hii siku na mimi nilikaa pembeni nikimwangalia kwa shauku sana.

Alifunga mkanda akawasha gari na akageuza gari na tukaanza safari ya kwenda Masaki na alikuwa yuko vizuri sana.

MIMI: “Aisee kumbe upo vizuri hivi nilikuchukulia poa sana.”

IRYN: “Insider au kwakuwa sina gari ndomana unafikiri mimi sijui kuendesha?”

MIMI: “Ufanye kununua gari sasa.”

IRYN: “Unataka ninunue gari gani? Sema.”

MIMI: “Marcedes Coupe kwako wewe itakupendeza sana.”

IRYN: “Nikajua utaniambia Lamborghin Urus SUV kumbe Marcedes? Bila shaka umeipenda ya Muajemi.”

MIMI: “Hamna ile inawapendeza sana wanawake.”

IRYN: “Hivi Muajemi anajitambua?”

MIMI: “Kwanini unasema hivyo?”

IRYN: “Teach him to act like a Man, asifikiri Pesa ndo kila kitu. I know what’s going on.”

Muda huu ilibidi niwe mpole tu maana sikukuwa na chakusema na nikachange topic palepale.

MIMI: “Kwanini tusingemaliza jana hili suala la nyumba na tulikuwa huku?”

IRYN: “Mzee alikuwa haja wasiliana na dalali ambaye anasimamia hii nyumba.”

Iryn aliendesha gari na baada ya kufika Marina Towers tulikata kona kulia na tulikwenda mbele kidogo ndo nyumba yao ilikuwa huko. Tulipark gari nje ya fense na baada ya dakika 5 dalali alikuwa kafika tayari.

DALALI: “Bila shaka wewe ndo bint wa Mzee Virgil.”

IRYN: “Ndo mimi hujakosea.”

DALALI: “Sikuwai jua kama Mzee ana Bint mkubwa hivi na mzuri namna hii.”

IRYN: “Ulitaka akuambie kama ana bint au maswala ya kazi?”

Dalali hakuwa na neno tena na tuliingia ndani muda huu na mbele yangu ilikuwa inaonekana nyumba ya ghorofa moja.

IRYN: “Insider hapa ndo nimekulia.”

MIMI: “Memories never die.”

IRYN: “Dalali hii nyumba itabidi ifanyiwe ukarabati kwakweli ndani mpaka nje.”

DALALI: “Nilimwambia Mzee wako akasema atalifanyia kazi, mkifanya ukarabati hata kodi itaongezeka, hapa ni pazuri sana.”

IRYN: “Hawa wanamaliza lini muda wao?.”

DALALI: “Bado miezi 3 na mwingine miezi miwili.”

IRYN: “Itabidi uwape wateja zako taarifa mapema hakutakuwa na extensions kwaajili ya ukarabati.”

DALALI: “Sawa haina shida.”

Iryn alifanya ukaguzi wa mazingira yote lakini tulishindwa kuingia ndani sababu ya wapangaji.

IRYN: “Insider tuondoke nilikuwa nataka kuangalia mazingira ya nyumba nimeshaona tayari.”

MIMI: “Si unaendelea kuendesha?”

IRYN: “Sahivi utadrive mwenyewe.”

Tuliondoka pale Masaki na tulirudi home moja kwa moja na tuliwasili pale home saa 10 kasoro hivi.

Muda huu mawazo yalinijia ya kwenda kwa kina Prisca niliona ananifanyia utoto, niliplan kwenda kumwonyesha mimi sio wa kufanyiwa utoto na nitamwonesha palepale kwao.

*********
41
 
Uzi umekuwa poa sana, umejaa mafunzo ya kutosha. Kiupande wangu kuna mengi sana niliyojifunza. Hongera sana mkuu INSIDER MAN
Zao la mwisho (final product) kutokea kwa heading ya story, mwanzo ilivoanza na mpaka sasa inavoishia ni hicho kiumbe ambacho kimebebwa tumboni kwa Iryn na ni kitu ambacho nilikitarajia kulingana namna ambavyo mambo yalikuwa yamepamba moto kati yenu... Mapenzi yalikuwa moto sana
The whole story ndo iko apo... Hii story inamuhusu yeye kabisaaa 100%.
 
Ningeumia sana kama Iryn angeondoka bila ujauzito👏👏 hongera sana kwa kweli nimefurahi, kwa sasa mtoto ameshazaliwa sio vibaya ukatwambia atleast ni wa kike au wa kiume na mnaendeleaje wazazi na mtoto
 
EPISODE 43

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

CONTINUE……

Jumatatu asubuhi niliamka mapema kwenda kuwachukua Mama wa2 na Maggy ili niwapeleke Posta. Baada ya kumpick Maggy pale kwake alivyoingia ndani ya gari hakuonesha kunifurahia kama zamani hata mama wa2 alihisi kuna kitu hakipo sawa kati yetu.

Nilianza kumdrop Mama wa2 ofisini kwake na nikammalizia Maggy.

MIMI: “Maggy are you ok? Nisamehe najua kilicho kukwaza.”

MAGGY: “Insider ungetoa hata taarifa kama huwezi kuja na simu zangu ukawa hupokei.”

MIMI: “Nilibanwa sana afu hii simu ndogo nilisahau home chukua hii namba yangu ya Tigo incase kama hii voda nakuwa sipatikani au haipokelewi.”

MAGGY: “Ok sawa haina shida I understand.”

MIMI: “This week tutafanya kweli I promise, vipi na huko Dodoma wanasemaje?”

MAGGY: “Natarajia kuondoka Jumatano ya kesho kutwa.”

MIMI: “Na utarudi lini?”

MAGGY: “Sitokaa kule ni kusaini mkataba na kuondoka mambo mengine nitafanyia huku, nitakwenda na ndege kama sitofanikiwa nitarudi alhamis.”

MIMI: “Sawa utanambia nikupeleke Airport.”

MAGGY: “Sawa, sasa mpaka sasa nina apartments mbili kuna zingine mbili nasubiri confirmation so nitakupigia simu, kama itashindikana leo bhasi hata kesho.”

MIMI: “Sawa haina shida japo yeye alikuwa anataka leo amalize hili suala.”

MAGGY: “Hata leo inawezekana acha tuone.”

Baada ya kuachana na Maggy nilifanya mawasiliano na Iryn na nikampa taarifa kuhusu apartments na hakuwa na shida.

Niliondoka Posta na kwenda Mbweni kumchukua Jane ili aendelee na mafunzo yake ya udereva maana ndo walikuwa mwishoni wanamalizia. Katika vitu ambavyo sikutaka kufanya masikhara ni pamoja na hili maana sikutaka kabisa kumkera mzee.

Baada ya kuwasili Mbweni nilimchukua Jane na tukaendelea na safari ya kwenda Posta. Baada ya kuwasili nili mdrop Jane driving school na muda huu nilipigiwa simu na Dullah akanambia kama niko Posta tufanye kuonana ana jambo anataka tuzungumze. Tulikubaliana tukutane kwenye ule mgahawa wangu wa siku zote ambao huwa napenda kula opposite na IT plaza.

Mimi nilisogea mpaka pale cafe na nilikuwa nikimsubiri Dullah afike eneo la tukio na ndani ya dakika 10 aliwasili pale.

MIMI: “Senior umeniweka sana utafikiri namsubiri demu bwana.”

DULLAH: “Mzee nisamehe shem wako alikuwa kaniganda sana.”

MIMI: “Ushazama kwenye dimbwi la mapenzi fala wewe.”

DULLAH: “Mzee acha hata hapa kuna taarifa nataka kukupa mzee baba.”

MIMI: “Nakusikiliza funguka chap.”

DULLAH: “Mzee u-senior wangu kwisha kwasasa licha ya kula pisi nyingi huku kwenye Uber hatimae nimezama kwa Latifah mazima.”

MIMI: “Sasa unajisifia au? Nenda direct una jambo gani?”

DULLAH: “Mzee nataka kuoa chombo ile na nataka kulipa mahali kabisa.”

MIMI: “Duuh aisee mbona fasta hivi naona unataka kuteleza kwenye ganda la ndizi umeona Bolt biashara imekuwa ngumu.”

DULLAH: “Ms*nge nini mbona wewe unateleza kwa yule mrembo na sisemi kitu.”

MIMI: “Tofauti ni kwamba mimi namkataba wa kazi wewe je?”

DULLAH: “Unajua nimeshamjaza mimba tayari mtoto wa watu ndomana unaona nimeamua kuchukua haya maamuzi.”

MIMI: “Aisee hata hivyo hongera sana mtoto yuko bank pale hutapata shida, kama umeona yuko vizuri wewe chukua jiko hilo, mimi nitakupa support utakapo nihitaji mzee baba.”

DULLAH: “Hayo ndo maneno sasa kumbuka mimi ndo Senior wako.”

MIMI: “Wewe ndo bhasi tena nishakuvua cheo tayari na harusi lini sasa?”

DULLAH: “Subiri nitakupa jibu acha nimalize kipengele cha mahari kwanza.”

MIMI: “Usikute hata hiyo mahari demu ameamua kulipa.”

DULLAH: “Hahahaa si namkaza vizuri, hamna bhana Senior niko vizuri kifedha nadhani unanijua.”

MIMI: “Haya bwana mimi sina neno, kwenye ndoa mimi sasa nitakuwa senior wako.”

DULLAH: “Wewe si hutaki kuoa ila umemzalisha mtoto wa watu.”

MIMI: “Akimaliza masomo nafunga ndoa ya kanisa kabisa.”

DULLAH: “Tutaona kama utafanya hivo Uber isha kuchanganya tayari na huyo mrembo wako sijui ni suala la muda tu.”

MIMI: “Acha upimbi.”

DULLAH: “Mzee baba mimi nasepa tutawasiliana acha nikamchukue mteja.”

Naam! Dullah alinipa taarifa za kuoa, na mrembo anayetaka kumu-oa ni mimi niliye mconnect naye awe anamchukua asubuhi.

Saa 6 mchana nilikwenda kumchukua Jane na kama kawaida tulipitia kwanza Masaki kuwachukua madogo. Baada ya kuwachukua madogo tuliondoka maeneo yale na baada ya kuwashusha madogo, nilimkabidhi Jane gari ili aendeshe huku nikiendelea kumfundisha taratibu.

Baada ya kuwasili Mbweni niliagana na Jane na mimi nikaondoka maeneo yale. Hii siku nilikuwa na kazi ya kusupply mizigo Sinza na Mikocheni na baada ya kutoka Mbweni nilikwenda moja kwa moja mpaka Kijitonyama kwa Iryn kuchukua ile mizigo.

Niliifanya ile kazi chap chap na baada ya kwenda Mikocheni nilimkuta Lucy na tukaanza story na kubwa alikuwa anataka kujua Iryn alikuwa wapi. Ilibidi nimwambie Iryn alikuwa South Africa kumuuguza Baba yake na sio kama tulivyokuwa tunafikiri. Sikutaka kumfungukia kuhusu mambo ya kule South Africa huwa sinaga imani na wanawake kabisa.

Na muda huu simu yangu ilianza kuita kucheki alikuwa ni Iryn akipiga na nilipokea simu yake,

MIMI: “Nambie Bossy wangu.”

IRYN: “Poa vipi utakuwa maeneo gani now?”

MIMI: “Niko Mikocheni hapa vipi unanijitaji?”

IRYN: “Sisi tuko Mlimani city hapa ukiwa unaondoka uje utuchukue.”

MIMI: “Sawa si ungesema kama unatoka ili nikupe funguo za gari?”

IRYN: “Nili request Uber.”

MIMI: “Soon nitapita kuwachukua.”

Nilimuaga Lucy na mimi nikaondoka kuelekea Mlimani city. Baada ya kufika pale nilimpigia simu akanambia yuko ndani amekaa kwenye Bench karibu na Shoppers.

Niliingia ndani na nilimwona Iryn alikuwa akicheza na Junior the way ungemwona hata wewe ungesema ni mwanae, maana walikuwa wanafanana rangi.

Na mimi muda huu nilikaa pembeni nikiangalia jinsi ambavyo alikuwa anamfundisha Junior kutembea. Na baada ya Iryn kugeuka nyuma aliweza kuniona na akasogea akakaa kwenye bench.

MIMI: “Nakuona na Junior utafikir mwanao kabisa.”

IRYN: “Junior ni mtoto mzuri sana sio wa kulialia.”

MIMI: “Anakupenda sema, watoto wanajua.”

IRYN: “Sema Insider umefanana sana na Junior ulijitahidi sana kutoa copy.”

MIMI: “Nambie na wewe unataka mtoto?

IRYN: “Junior ananifanya nitamani kuwa na mtoto afu Insider sogea hapa tuongee.”

MIMI: “Aya nimesogea unataka kunambia nini?”

IRYN: “Insider jana ulikuwa kuchepuka prove me wrong.”

MIMI: “Hamna bhana hayo ni mawazo yako tu.”

IRYN: “Ok ila unamchepuka Mama Junior, kwa mwanaume aliyekamilika hawezi kuwa na mwanamke mmoja na huu ndo ukweli.”

MIMI: “Unachosema ni kweli lakini sio kwa upande wangu.”

IRYN: “Vipi kuhusu yule mwanamke niliyekutana naye kule Palm Village?.”

MIMI: “Yule ni mteja wangu kama wewe tu, unajua hata wewe kuna watu wanahisi sisi ni wapenzi, lakini sijawai hata kukuvua chupi.”

IRYN: “People always think negative. So plan yako univue chupi sindio.?

MIMI: “Sijawai kuwa na hii plan na kama kufanya hivo ningekuwa nilishakuvua zamani sana hata wewe unatambua hili. Ila mimi ni mwanaume ninaye jitambua angekuwa mwingine huenda alishakutongoza muda sana. Sio kwamba sina hisia na wewe za kimapenzi naomba utambue mimi kama mwanaume nina hisia tena ziko Maximum. Usifikiri sitamani kulala na mwanamke mrembo kama wewe katika maisha yangu ila sijataka kuchanganya mapenzi na kazi na pia naheshimu kuwa na mke.

IRYN: “So unataka kusema nini Insider.”

MIMI: “Namaanisha mimi nakuheshimu sana, heshima nayokupa wewe hata mama J hapati ila naomba utambue wakati sahihi bado hujafika wa mimi kufanya hivyo.”

Na muda huu Iryn alikuwa akinitizama na alikosa majibu ya kutoa. Junior naye alikuwa akifurahi tu muda huu ni kama alikuwa anajua kinacho endelea.

“Tuondoke jioni sahivi anatakiwa akanywe uji huyu.”

IRYN: “Okay, Junior tuondoke mme wangu.”

Tuliondoka pale Mlimani city na tulirudi nyumbani moja kwa moja na tulimkuta Mama J amerudi tayari.

Usiku nilifanya mazungumzo na Iryn nikamwambia kesho tutakwenda kuangalia apartments. Kwa upande mwingine the way ambavyo nilikuwa naishi nao mle ndani ungesema ni wake zangu.

*********

Asubuhi nilifanya mawasiliano na Maggy na alinambia ana apartments tano mkononi hivyo hatunabudi kwenda kuziangalia. Pia niliwasiliana na Mary aliomba tuonane jioni kama nitakuwa na nafasi na mimi nilimwambia kama nitapata nafasi nitamcheki.

Baada ya kumaliza majukumu yangu ile asubuhi niliwasiliana na Iryn ajiandae na pia nilimpigia simu Dullah kumwomba awachukue madogo pamoja na mke wa Pama, na yeye hakuwa na noma.

Saa 6 mchana ndo muda ambao tulianza kuziangalia zile apartments na tulikutana na Maggy pale Engen filling station Mikocheni. Baada ya kuingia kwa gari alikaa seat za nyuma na tukasalimina muda huu.

MIMI: “Maggy huyu ndo Bossy mwenyewe aliyetupotea.”

MAGGY: “Jamani ulikosa apartment nzuri sana. Pole sana kwa matatizo.”

IRYN: “Ahsante sana sina wasiwasi leo utakuwa nazo nzuri.”

MIMI: “Maggy kwanza apartments ziko wapi ili tujue tunaanza na ipi na kumaliza na ipi.”

MAGGY: “Ya kwanza ipo hapo Highland villas, ya pili ipo karibu na Capetown, ya tatu ipo Mikocheni, ya nne ipo Round about ya kawe upande wa chini karibu na Beach, na ya mwisho ipo mbezi Beach karibu na Kota za BOT.”

MIMI: “So hapa tunaanza na villa sindio?”

Tuliondoka pale Engen na tukaanza kuzitembelea hizo apartments na tulianza na hiyo ya Highland villas na apartment ilikuwa ni kali sana. Hatukwenda kuiangalia ya kule Capetown sababu Iryn aliigomea hakuyataka mazingira ya kule na tulikwenda kuangalia apartments zingine zote zilizokuwa zimebaki.

Tulitumia kama masaa 2 hivi kuangalia apartments zote. Apartments ambazo zilikuwa kali ni ile ya pale Highland villas na Kawe. Lakini Iryn alichagua ya Kawe sababu aliyapenda mazingira jinsi yalivyotulia na kingine haikuwa mbali sana na nyumba ya Rais wetu kipenzi JK. Maeneo yote ya upande wa chini mpaka beach yanakuwa na ulinzi mkali hivyo ilikuwa ni sehemu sahihi kwa Iryn.

Apartment haikuwa mbali na Bahari ya Hindi na ilikuwa ya vyumba viwili na ilikuwa full furnished, yaani ni wewe unahamia na nguo zako tu kila kitu kipo ndani. Baada ya hapo alikamilisha process zote za malipo na gharama ilikuwa $1,500 per month.

Suala la mikataba Maggy alisema atanikabidhi mimi kesho asubuhi na baada ya hapo Iryn aliomba nimpeleke Mikocheni saloon ili akatengeneze nywele zake. Baada ya kumfikisha tuliagana,

“Insider wewe unaweza endelea na mambo yako mimi nitafanya mchakato wa usafiri wakati wa kurudi.”

“Sawa haina shida.”

Na mimi nilifanya kumpigia simu Mary maana nilikuwa na miadi naye toka asubuhi. Baada ya kuwasiliana naye alinambia yuko Mwenge, hivyo tukakubaliana tukutane pale Triple 7 jioni.

Saa yangu ilikuwa inaonesha ni saa 10 jioni kasoro hivyo niliamua kwenda kuosha gari pale Texas Rose garden Road. Wakati niko pale Mary alinipigia simu akanambia yeye ndo yuko njiani na soon atakuwa amefika pale 777.

Na baada ya dakika 10 na mimi niliondoka Texas kuelekea eneo la tukio. Mary alikuwa amefika muda mrefu hivyo alikuwa akinisubiri mimi na baada ya kuingia pale nilikwenda moja kwa moja upande wa nyuma ndo alinambia amekaa huko.

MIMI: “Nambie mrembo pole kwa kukuweka.”

MARY: “Haina shida hata hivyo sina muda mrefu hapa.”

MIMI: “Mbona umeagiza maji tu.?”

MARY: “Nimeagiza chakula kitakuja soon.”

MIMI: “Nambie ni kitambo sana hatujakaa hivi tukaongea.”

MARY: “Insider wewe si umenitenga sahivi huna hata habari na mimi au Prisca amekukataza?”

MIMI: “Hapana kwakweli na kwanini anizuie ilihali wewe ni shem wangu?”

MARY: “Okay mimi nimekuita ili tuonane maana ni muda mrefu na pia tuongee suala la kwenda Mikumi.”

MIMI: “Sawa mnakwenda lini huko?”

MARY: “Tunakwenda next week itakuwa ijumaa.”

MIMI: “Sawa haina shida mimi nitakupeleka ila hakikisha Prisca anajua hili.”

MARY: “Sawa haina shida.”

MIMI: “Na vipi kuhusu suala la Mama liliendeleaje?”

MARY: “Kwani hujaongea na Prisca?”

MIMI: “Hata hajui kama ulinambia suala la mama na hawezi kunambia yule.”

MARY: “Prisca alirudi usiku ile siku bila shaka wewe ndo uliye mleta home. Kwa mazingira yake aliyorudi Mama alihisi something mmefanya ila hakutaka kusema kitu.”

MIMI: “Something gani hiyo unayoongelea mbona sikuelewi?”

MARY: “Insider sisi sote ni watu wazima, Prisca alionekana kuwa na uchovu wa sex hata alivyorudi alikuwa hajiamini alikwenda kulala moja kwa moja.”

MIMI: “Sawa bhana so mama hajamind?”

MARY: “Mama always hanaga shida, sisi ni watu wazima tayari ila hapendi haya mambo tuyafanye mbele ya kina Ivy na Loraine (wadogo zao).”

MIMI: “Hapo nimekuelewa na Mzee vipi?”

MARY: “Mzee ni mtu wa safari sana hanaga noma pia. So you guys mna mipango gani sasa?, mpaka sasa pale home kila mtu anajua mna date.”

MIMI: “Mapema sana Mary haya mambo kuyaongelea.”

MARY: “Insider mimi naomba usije ukamuumiza Prisca, ni dhaifu sana kwenye suala la mapenzi na anaonekana kakolea kwako mazima kabisa. Mimi naomba whatever mmetoka out make sure anarudi home asilale nje, Prisca ana maamuzi ya haraka na ya ajabu.”

MIMI: “Usijali Mary niko makini naye.”

MARY: “Hivi unajua leo amemwambia mama anataka kurudi hostel? Na alikuwa anataka pesa za matumizi.”

MIMI: “Hapana hajaniambia ila mimi sioni kama ni tatizo kurudi hostel.”

MARY: “Prisca dislike hostels ila nahisi anataka kuwa karibu na wewe awe huru kukuona anytime.”

MIMI: “Unajua soon wanaanza UE mimi nafikiri yuko sahihi kuwa karibu na mazingira ya chuo.”

Na muda huu Iryn alinipigia simu na mimi nikapokea nimsikilize anasema nini.

IRYN: “Insider sorry utakuwa around uje unichukue tuondoke?”

MIMI: “Niko hapa Triple 7.”

IRYN: “Ndo wapi huko?”

MIMI: “Haufiki roundabout ya Kawe ni nyuma kidogo kama unakwenda kwenye apartment yako mpya.”

IRYN: “Okay Lucy amekusikia na ameshapajua hapo atamwelekeza dereva wa pikipiki.”

MIMI: “Sawa mwambie akifika hapo akate kushoto aje geti la huku juu utaliona gari, ukifika utanipigia.” Na Iryn alikata simu.

Tuliendelea na maongezi yetu pale na Mary baada ya dakika 10 Iryn alipiga tena simu.

IRYN: “Insider niko hapa parking uliko park gari, njoo haraka tumpe na dereva pesa yake yeye hana change.”

MIMI: “Sawa nakuja soon.”

Tulitoka nikiwa nimeongozana na Mary na tulikwenda moja kwa moja mpaka kwa parking na nilimkuta Iryn kasimama kwenye gari na alikuwa kapendeza balaa.

Na wakati huu Iryn alikuwa akimtizama sana Mary, na Mary naye alikuwa akimtizama Iryn kwa makini na wakasalimiana.

IRYN: “Insider mpe 3,000 dereva.”

MIMI: “Dereva 3,000 kwa umbali gani? na wewe unapigwa tu unakubali.”

Na mimi nikatoa elfu 3 kwa gari nikampa dereva, na muda huu Iryn alifungua mlango wa gari na akakaa seat za nyuma.

MARY: “Insider unapita njia gani?”

MIMI: “Tukuache pale Rainbow maana sisi tunakwenda home au unaonaje?”

MARY: “Sound great.”

Mary akakaa seat ya mbele na hao tukaondoka pale na mimi sikutaka kufanya utambulisho wowote maana Iryn alikuwa busy akiongea na simu. Kwa upande mwingine mimi na Mary story zilikuwa zinaendelea kama kawaida mpaka tunafika pale Rainbow na nikampa elfu 10 imsaidie usafiri wa kwenda kwao.

Baada ya Mary kushuka na sisi tuliendelea na safari ya kurudi home na muda huu Iryn alikuwa amemaliza kuongea na simu.

“Insider huyu mwanamke sindo yule wa Palm village?”

“Hapana umewafananisha huyu ni dada yake sema wamefanana.”

Prisca na dada yake Mary wamefanana sura kama hujawazoea kwa mara ya kwanza unaweza kuwafananisha.

“Okay kumbe ulikuwa na appointment zako.”

“Iryn unatakiwa utambue mimi pia na marafiki wa kike wengi sio wewe tu. Wewe kwangu ni Bossy na pia ni rafiki, naomba usipende kujudge mambo yangu private.”

“Uko sahihi Insider, samahani kama nitakuwa nimekukosea.”

“Na kama ningekuwa na jambo baya nisingekwambia kama niko around, ningeishia kudanganya.”

Baada ya kuwasili home yeye alikuwa wa kwanza kushuka na alikuwa akinisubiri mimi nipark gari. Na baada ya kupark vizuri nilishuka tukaongozana kuelekea ndani na Mama J alikuwa amerudi tayari yuko seblen.

MAMA J : “Karibuni wageni zangu

IRYN: “Ahsante mpenzi pole na masomo.”

MAMA J : “Ahsante vipi umefanikiwa kupata nyumba?”

IRYN: “Tumepata hata sio mbali.”

MAMA J : “Itabidi nije nipajue, ngoja mimi niingie jikoni niwapikie wali na samaki.”

IRYN: “Nakuja kukusaidia sio muda.”

MIMI: “Kule utahamia lini?”

IRYN: “Seems like hutaki mimi niendelee kuwa hapa kwako?”

MIMI: “Nimekuuliza kwa mazuri tu jamani hata usinifikiri vibaya.”

IRYN: “Insider nilikupa task unakumbuka?”

MIMI: “Nikumbushe.”

IRYN: “Unaonaje ijumaa hii tukienda kuwatembelea yatima?”

MIMI: “Ni sawa haina shida ila kwanini tusiende jumamosi? Ijumaa wanakuwa mashuleni kwa jumamosi unaweza kuwaona wote.”

IRYN: “Sawa ulipata kituo gani?”

MIMI: “Kwa Research niliyofanya niliona Bagamoyo ndo ingependeza sababu vituo vya kule havifikiwi sana na watu.”

IRYN: “Bagamoyo mbali sana wakati kuna vituo vingi tu hapa Dar vina uhitaji huko tutakwenda mwezi ujao.”

MIMI: “Nafikiri twende hata Bunju bhasi sio mbaya.”

IRYN: “Bunju iko wapi?”

MIMI: “Kama unakwenda Bagamoyo ni kama km 20 kutoka hapa home.”

IRYN: “Sawa ila usitafute vituo vyenye majina maana najua vinatembelewa sana, tafuta ambavyo havina majina na uwape taarifa ya ujio wetu jumamosi ikiwezekana upate na idadi ya watoto itapendeza.”

MIMI: “Sawa haina shida.”

Ile usiku baada ya kupata dinna ya pamoja nilikwenda chumbani kuoga na baada ya kutoka nilimkuta mama J akiwa anasoma. Na mimi niliamua kutoka nje ili nikapunge upepo

Baada ya kutoka nje nilimkuta Iryn anacheza na mbwa kibarazani.

IRYN: “Insider kumbe hapa mnafuga mbwa?”

MIMI: “Za mwenye nyumba hizo anazifunguliaga usiku. Na wewe ni mpenzi wa mbwa?”

IRYN: “Sana nakumbuka kule Masaki Baba alifuga mbwa 3.”

MIMI: “Angalia atakuachia wadudu.”

Na mimi nilimfukuza yule mbwa muda huu

“Vipi tena usiku huu huku nje.”

IRYN: “Nimeona nitoke tu nipoteze muda nilikuwa naongea na simu.”

Na mimi muda huu nilisogea nikakaa kwenye ngazi karibu yake.

MIMI: “Umempa nini mama J maana sahivi hana hata wasiwasi na wewe.”

IRYN: “Nothing atakuwa amejua mimi sio adui yake.”

MIMI: “Sawa bhana na kweli iwe hivyo.”

IRYN: “Jumapili nitahamia kwangu, byee mimi nakwenda kulala.”

Muda huu nilitumia kuongea na Prisca ili kumjulia hali na akanambia kashaanza kutafuta nyumba tayari. Tuliongea masuala mbalimbali ya kuhusu afya yake na future yake kama mama kijacho. Ukweli kutokana na huli suala la mimba upendo wangu kwa Prisca ulianza kuongezeka kwa kasi ya 4G. Tuliagana na nilimwambia asilipie nyumba bila mimi kuiona na mimi nikaingia ndani kwaajili ya kwenda kulala.

INAENDELEA
43
 
Kwa kweli kabisa INSIDER MAN umeifikia paradiso ukiwa hapa hapa duniani.

IRENE bado anaendelea kuku spy kwa kuwatumia WORKMATES na Mama J. Hizo simu zote alizogawa ni dead boxes zake kwa ajili ya surveillance juu yako.
Ndo maana kila wakati anakusisitiza kutomuona mwanao endapo utafanya ufuksa.

Hata hivyo, bahati yako kubwa ni kipaji chako cha kuusoma upepo mara moja na kuchukua uelekeo sahihi. Bossylady akija juu unajidhili, mama J naye akileta zake unampimia na kumtuliza.

Hadithi hii ni inspiration kwa vijana na watu wazima pia. Kutokata tamaa na kufanya mambo sahihi wakati sahihi.

NINAKUSHUKURU SANA mzeebaba kwa muda wako.
 
Na niliwasha gari nikaondoka kwa fujo sana pale JNIA nikiwa na Audi Q7.

THE END

Hongera sana mkuu na shukrani kwa simulizi hii ya kuvutia na kusisimua...

Pamoja na kwamba umeimaliza lakini naamini Mungu alimjaalia Iryn kujifungua (kihesabu ya stori Iryn atakuwa alijifungua kati ya March hadi May) na kwa sasa wewe ni baba wa mwanaye...

Mkuu The Monk kama ambavyo tangu mwanzo niliamini Iryn ataliwa, na mwisho atapata kibend na ndivyo imekuwa, heko kwa bazazi INSIDER MAN
 
Toka mwanzo mnaanza kukulana nilisema utamjaza mimba iryn na kumbe imekua hivo. Hongera mkuu. Huu uzi uliutendea haki. Ila itakua poa saana ukitupa result za kijacho akizaliwa kama tayari kote kote kwa iryn na pia yule jane mke wa mzee pama. Hii story inatufundisha jambo kubwa saana.
Ni kweli upo mushkeli kwenye Hii episode FINALE(EP70)/thread. HAIFUNGUKI. Mimi nimefanya kusoma kwenye quote ya huyu mtaalamu.

#11215
 
Hongera sana mkuu na shukrani kwa simulizi hii ya kuvutia na kusisimua...

Pamoja na kwamba umeimaliza lakini naamini Mungu alimjaalia Iryn kujifungua (kihesabu ya stori Iryn atakuwa alijifungua kati ya March hadi May) na kwa sasa wewe ni baba wa mwanaye...

Mkuu The Monk kama ambavyo tangu mwanzo niliamini Iryn ataliwa, na mwisho atapata kibend na ndivyo imekuwa, heko kwa bazazi INSIDER MAN
Atakuwa amejifungua hivi karibuni mwezi wa sita au wa saba, kumbuka ujauzito wa wiki 4 ilikiwa oct
 
Insaida hapo mwisho hujabadili gia angani kweli???

Kuna koments zako fulani nimewaza nje ya box nikahisi hapo mwisho umebadili gia sijui kwanini!

1. Pale upokua unakanusha kuhusu suala la iryn kukubali abebe ujauzito na wakati anaenda chuo kusoma huku hamuelewi mustakabali wenu! Memba fulani simkumbuki alipokuambia kuhusu hilo ni kama uling'aka kana kwamba ni kitu ambacho kwa muda huo hakiwezekani!

2. Episode 69 kuna mahala ulikoment kuwa hutamani kuend story kwa scene ambayo inaonesha mwisho wa kuhuzunisha.

Naona Hapo mwisho Ujauzito wa Iryn umekua ghafla sana!

Anyways ni mawazo tu lakini!
 
Back
Top Bottom