Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 2
CHAPTER 05:

CONTINUE…….

Ukweli hata mimi sikuwa na idea na nilibaki najiuliza zile picha kazipata wapi? Maana toka kipindi kile tumetoka na Iryn hospital sikuwahi kuziangalia tena. Nilitoa zile picha za Ultrasound kwenye bahasha, good news hakukuwa na sheet ya mwanzoni ambayo huwa inakuwa na jina la mhusika na maelezo ya matokeo ya vipimo.

Sijui hata nisemeje, ipo hivi mwanamke akifanyiwa vipimo vya ultra sound kuna fomu huwa inajazwa kuonesha matokeo ya vipimo, so huwa inaelezea umri wa mimba na kama kuna tatizo lolote, pia Jina la mhusika huwa linaandikwa kwenye hii sheet, then wana attach za zile picha za ultrasound. Sijajua kwa hospital zote kama wanafanya hizi ila most wanafanya hivi.

Tuendelee, ilibidi nifanye kumbembeleza kwanza ili atulie then tuendelee na maongezi maana tayari nilikuwa na jeuri ya kukataa sababu hakukuwa na ushahidi. Kwa upande mwingine nilikuwa nawaza labda Iryn atakuwa kaamua kufunguka ukweli ili tukose wote.

MIMI: “Baby kwanini unakimbilia kusema mimba ya Iryn ? Kwanini unasema mimi ni mhusika una uhakika wa hili unaloongea? Kwanza hata sijui hii bahasha ulikoitoa.”

WIFE: “Baba J kwa muda mrefu sana mimi nimekuwa mvumilivu kwa mambo unayonifanyia lakini sasa naona uvumilivu utanishinda. Kama hatujafunga ndoa unafanya haya je tukifunga ndoa itakuwaje?, unakumbuka kuhusu yule malaya wako wa kazini kipindi kile? Unakumbuka yule dada niliyeona chats zenu? (Prisca).

MIMI: “Hayo yote yalipita na kumbuka suala la yule mwanamke wa ofisini tatizo ni wewe ndo ulipelekea mimi kufanya vile lakini haya yaliisha na wazazi walisuluhisha, kuendelea kuyazungumzia inaonesha bado hukuridhia maamuzi.”

WIFE: “Nakukumbusha uone jinsi ambavyo unanikosea sana, au nilifanya kosa kukuzalia? Sahivi na mtoto unaona siwezi kwenda kokote? Ndomana unanichezea unavyotaka.”

MIMI: “Hapana mke wangu uko unakwenda mbali, unanikosea sana kusema hii mimba ni yangu wakati hata sijui hii bahasha ulikoitoa, niambie ulikoitoa na kwanini ukimbilie kusema ni yangu?”

WIFE: “Nimeikuta kwenye gari yake ndomana nina uhakika 100% Iryn ni mjamzito na amendoka Dar sababu ya hii.”

MIMI: “Hio gari si ya Iryn ni ya mama yake mlezi, mimi mwenyewe sijawahi kuipekua hio gari, hivi umepata wapi nguvu ya kwenda kukagua gari ya watu? Mbona unakosa heshima na adabu?”

WIFE: “Hii gari tunamaliza wiki ya 3 hauirudishi, hii inanipa wasiwasi Iryn kakuachia gari uendelee kuitumia na kama gari ipo kwangu nitaendelea kuikagua.”

MIMI: “Mama hayupo ndomana nashindwa kuirudisha but leo karudi kamuona na Junior, anakusalimia na anataka akufahamu.”

WIFE: “Mimi sina shida wewe ukiwa tayari utanambia twende. Ila Baba J kama kuna jambo lolote la siri linaendelea kati yako na Iryn mimi nitajua tu, When I catch you cheating, it will be over between us, and I swear.”

Ilibidi ninyamaze tu maana sipendagi kelele na wanawake pia kuendelea kumjibu ningeendelea kumpa airtime ya kuongea zaidi.

Baada ya wife kuondoka nilikaa pale kitandani maana hata sikuamini kama msala umeisha kwa haraka namna hii. Na muda huu mawazo yalianza kuniandama, kwanza niliwaza suala la mimba litakuja kuleta shida hapo baadae pale ambapo wife atajua, pili suala la Iryn kutopokea simu zangu na kuni-block liliendelea kunipa mawazo sana.

Bado niliendelea kuwaza kuhusu mama Janeth,

“Mama Janeth leo amefahamu mimi nina mtoto na mke na anataka kumjua wife, hapana kwasasa siko tayari kuwakutanisha labda hapo baadae. Na siku ambayo mama Janeth atajua Iryn ana mimba yangu itakuaje? Atalichukuliaje hili suala na anajua fika mimi nina mke na mtoto?. Vipi kuhusu ndugu zake wa Ethiopia hawajui pia, na siku watakayopata hizi taarifa itakuaje? Nilijiona niko kwenye wakati mgumu sana na kikwazo kikubwa ni mimi kuwa na familia.”
*******
Asubuhi nilifanya mawasiliano na Sumaiya mshikaji wangu maana kila akinipigia simu tulikuwa tunashindwa kuongea na mara ya mwisho mimi na yeye kuonana ni kipindi kile tuko Serena hotel kwenye kikao.

SUMAIYA: “We mwanaume leo ndo unakumbuka kunipigia?. Unaringa sana, simu zangu na texts huzioni sindio?”

MIMI: “Umenitafuta mara moja tu kama sikosei.”

SUMAIYA: “Mhh si sawa dawa yako wewe bado ipo kuna siku utaingia 18 zangu.”

MIMI: “Hahahaa sawa bhana, niambie lakini nimeku-miss.”

SUMAIYA: “Fyooh umem-miss nani? Next week nitakucheki kuna ishu tuongee very important.”

MIMI: “Ishu gani hio kwanza?.”

SUMAIYA: “Mbona unakuwa na haraka kama bao la kwanza?, utajua siku hiohio.”

MIMI: “Duuh sawa bhana, utanambia when and where.”

SUMAIYA: “Poa ila acha maringo, usitudharau kisa unamt*mba Iryn.”

MIMI: “Seems unamwonea wivu.”

SUMAIYA: “Dawa yako soon utaipata, Insider next week tuonane serious mshikaji wangu, kuanzia J4.”

Baada ya kuagana na Sumaiya niliamua kumpigia simu Prisca maana alikuwa anasumbua sana mpaka kero. Maongezi yetu yalikuwa kuhusu suala la kurudiana tena, lakini mimi nilimkatalia na kumwambia hili suala haliwezekani na tuendelee kuwa washikaji. Licha ya Prisca kutoyakubali maamuzi yangu kwa upande wake alionekana kuto tamaa kabisa na aliomba appointment kwa mara nyingine tena.

Hii siku nilikuwa nina miadi na Bob (Mjeshi) na tulikubaliana tunaonana pale Samakisamaki ili tuangalie na match ya ufunguzi wa kombe la Dunia. Jioni mida ya saa 11 nilikuwa nimewasili pale Mlimani city na nilikwenda ndani madukani kununua Jazz. Mimi ni mshabiki wa Messi na Argentina hivyo nilinunua Jaz 4 za Argentina kwaajili yangu, wife, Junior na dada.

Nilikwenda kwenye gari kuvaa jazz yangu na nilikwenda pale Samakisamaki, kwa upande mwingine palikuwa na watu wengi sana hivyo ilibidi nifanye kutafuta angle nzuri. Wakati namsubiri Bob nilikuwa nachat na Lucy na nilimwambia aje tujumuike pamoja tuangalie na match.

Mida ya saa 12 Bob alikuwa kawasili pale Samakisamaki na tukaendelea na story maana ilikuwa ni kitambo sana.

MIMI: “Mzee ilikuwaje ukarudi jeshini? Ulikuwa ni doja sana wewe fala.”

BOB: “Hahahaa mzee acha tu niliapply kibishi, baada ya kupata chance nikaamua kurudi tu.”

MIMI: “Aisee noma sana mimi huko toka niondoke Kigoma sitaki hata kukusikia.”

BOB: “Demu wako Nana mliishia wapi? Maana yule dem alikupendaga sana.”

MIMI: “Nana tuliachana since first year ameolewa na ana watoto wawili sahivi. Upo Dar toka lini?”

BOB: “Dar nimekuja mwezi wa 6 na nipo Lugalo hapo, niliomba ruhusa ya kusoma ndo nikapata.”

MIMI: “Hongera sana, so upo chuo gani na unasomea nini?”

BOB: “Mzee mimi napiga Engineering chuo cha Ardhi na nikakaa Survey. Wewe upo pande zipi mzee?”

MIMI: “Kaka mimi nina familia ujue karibu sana niko Mbezi Beach hapo hata sio mbali.”

BOB: “Dadeki wewe Insider wakuoa? Kweli Dunia inazunguka kwa kasi.”

MIMI: “Maisha yanabadilika kaka, Nashukuru Mungu kwa hili pia.”

BOB: “Kaka nitakuja kukutembelea by next week tuombe uzima.”

Tulipiga story sana na Bob ukizingatia alikuwa ni mwanangu sana kule Jeshini. Kwa ufupi mimi demu wangu wa kwanza nilimpatia jeshini ndo huyu Nana, huyu ndo mwanamke wa kwanza kuona uchi wake.

Baada ya kama dakika 45 Lucy aliwasili na akajiunga nasi na mimi nilifanya utambulisho na story zikaendelea. Lucy alinionesha video alizopost Rebby kwenye snapchat yake na walionekana kuwa na Hilda, seems walitoka out.

LUCY: “Insider nilivyokuwa nakwambia kuwa makini sana na Hilda sikuwa na bahatisha, si unaona jana wametoka out? Kama kuna jambo la siri linaendelea wewe na Hilda hesabu umeumia tayari.”

MIMI: “What do you mean?”

LUCY: “Insider ngoja nikupe hii siri japo unajua ila leo nakazia, Rebby ni CIA wa Iryn na hapo huenda katumiwa hela kaamua kutoka na Hilda ili amchimbe vizuri. Becareful.”

MIMI: “Hiki unachoongea kina make sense, nikija found out Rebby anasnitch nitamfanya mbaya sana huyu mwanamke.”

LUCY: “Ndo hivo mshikaji wangu kuwa makini sana, hapo Rebby atapiga ndege wa2 kwa jiwe moja. Hapo atapata taarifa za Asmah na za Hilda pia, Hilda hajui kama Rebby yuko kazini.”

MIMI: “Unajua Iryn kaniblock tumemaliza week bila mawasiliano yoyote.”

LUCY: “Serious? Duh mbona lishakuwa tatizo hili sasa.”

MIMI: “Sijui ana mpango gani, nahisi huenda anajambo lingine mpaka kaamua kuniblock hii sio kawaida.”

LUCY: “Iryn ni mjamzito kumbuka, huenda kuna mabadiliko anayapitia. Sometimes inatokea mimba haikupendi ila atakumiss na atakutafuta mpe space kwasasa na usiforce.”

MIMI: “Yeah upo sahihi ngoja nimpe space atanitafuta mwenyewe.”

Tulikaa mpaka mida ya saa 4 usiku mimi niliwaga nikaondoka na niliwaacha pale wakiendelea na burudani. Baada ya kuingia kwa gari nilimpigia simu mama yangu mzazi maana tangu muda mrefu alikuwa akinipigia simu. Kwa upande wangu nilihisi mama anataka kujua lile jambo la siku ile, lakini mimi sikuwa tayari kumwambia maana niliona bado mapema sana.

Baada ya kumpigia simu mama taarifa kubwa aliyonipa ni kuhusu kuja Dar mwanzoni mwa December na alisema anakuja kwaajili ya harusi na atakuja kukaa home. Nilifurahi sana kusikia taarifa hizi na nilimkaribisha aje akae hata mwezi maana nime m-miss sana.

Baada ya kuwasili home niliwakuta akina wife pale seblen wanaangalia movie na mimi nikajumuika nao, na nilimbeba Junior.

WIFE: “Baba J umeshika nini?”

MIMI: “Zawadi zenu hizi nimewaletea.” Na nilimpa zile jazz maana zilikuwa kwenye mfuko.

WIFE: “Sasa haya majazz mimi ya nini? Ulishindwa kuona zawadi za kununua?”

MIMI: “Najua sahivi huwezi elewa ila soon utaona umuhimu wa hii zawadi.”

Mimi nilitoa jazz ya Junior nikamvalisha pale ila wife aliishia kunisikitikia tu! maana aliona nazingua sana, niliwaaga na nilikwenda chumbani kuendelea na mambo yangu.

Muda huu chumbani nilikuwa nawaza namna ya kuachana na kampuni ya Iryn, niliwaza sometimes anakuwa na nyodo sababu mimi niko chini yake, hivyo mazoea yanakuwa mengi.

Niliwaza niendelee kujipanga taratibu pamoja na kuanzisha biashara zangu kwa hapa Dar na Dodoma. Kuhusu wife sikuwa na wasiwasi naye maana tayari nilikuwa nishampa support ya kutosha, kama kuanza uwakala wa Bank na biashara ya Bajaji ilikuwa inafanya vizuri. Mpango mwingine tuliokuwa nao ni kufungua biashara ya vinywaji na alikuwa bado anafuatilia location.

Kuhusu Junior sikuwa na wasiwasi maana nilikuwa najitahidi sana kumwekea pesa za ada kwenye account yake, hata akianza shule nitakuwa sina stress. Kwa upande wangu niliwaza kuna umuhimu wa kufungua account ya saving UTT ili niwe nadumbukiza pesa huko kwaajili ya future.

Muda huu ndo nilipata wazo la kumtafuta Sia yule dada tuliokutana kipindi kile Cocobeach (Ref: Season 1, Episode 52). That time niliongea mambo mengi sana na Sia na alinambia anafanya biashara Kariakoo na ana connection nyingi sana.

Ile siku nakutana na Sia sikumzingatia kabisa maana nilikuwa na stress za Iryn jinsi alivyokuwa ananipiga na vitu vizito. Sia ndo mtu ambaye niliona angeweza kunipa connection namna ya kuingia Kariakoo na kuanza biashara na Roho ilikuwa inanituma nimtafute yeye she can help.

*******
Jumanne nilikwenda kwa mzee Juma kumtembelea na kumjulia hali lakini nilitaka iwe surprise. Niliwaza kila siku mzee ananitafuta acha leo mimi niende nikamsalimie mzee wangu, na ile asubuhi nifanya mawasiliano na Cami akanambia mzee yupo.

Saa 5 asubuhi niliwasili pale kwake Mikocheni baada ya kuingia ndani nilimkuta kaka mkubwa na mimi kwa haraka nilijua ni kijana wake. Nilisalimiana na jamaa na mimi nilikaa kwenye coach nikimsubiri mzee maana hata sikuwa na story na jamaa.

Baada ya dakika 20 hivi mzee alitoka ndani na alifurahi sana kuniona maana hakutegemea ujio wangu pale kwake. Kwa upande mwingine mzee alinitambulisha kuwa yule ni kijana wake ambae anafanya kazi nje, na alinitambulisha kwa kijana wake mimi ni kama kijana wa Mzee Pama. Jamaa baada ya kusikia hivi kidogo alianza kunichangamkia na tukaanza story kwa mbali.

Tuliongea masuala mengi sana na mzee kuhusu Jane na jinsi ambavyo nilipambana mpaka akajifungua salama. Mzee alinipongeza sana kwa hili na alishangaa namna nilivyoweza kuwa jasiri mpaka kufanikisha Jane kujifungua salama.

Mzee aliulizia maendeleo pamoja na familia yangu kwa ujumla na nilimwambia tuko salama kabisa na aliuliza suala la ndoa sanabu aliona hakuna sababu ya kuendelea kupoteza muda. Nilimwambia mzee suala la ndoa mpaka mama J amalize chuo kwanza sababu kwasasa bado anasoma na tumepanga hivi. Mzee alinambia tukiwa tayari tutamwambia na atatusupport kwa 100%.

Baadae mzee alinambia anatarajia kuanza ujenzi January kule Bahari Beach na pindi utakapoanza ataomba sana niwe nasimamia ule mradi na atakuwa ananilipa. Zilikuwa taarifa njema sana kwangu na nilimwambia mzee hakuna tatizo mimi nitasimamia mradi wake na hakuna kitakacho haribika. Mzee Juma alinambia before hajaondoka atanitafuta kwani bado kuna mambo mengi ya kuzungumza mimi na yeye.

Nilitumia lisaa kwa mzee, nikaondoka kuelekea Masaki na wakati niko njiani niliwasiliana na Sumaiya akanambia yuko ofisini. Na Ndani ya muda mfupi niliwasili pale ofisini kwake.

SUMAIYA: “Insider karibu Bossy wangu.”

MIMI: “Thank you naona unazidi kuwa mzuri ni nini siri ya mafanikio yako?”

SUMAIYA: “Sahivi nina bwana lina Pesa kunihonga ni suala la kawaida kwake ndomana nang’aa, ushaanza kunitamani?”

MIMI: “Thubutu! Uzuri nakujua ulivyo so huna cha kuniringishia.”

Hizi ni kauli ambazo zilifanya Sumaiya anune ghafla maana siku ile nilimpiga na kitu kizito sana,

SUMAIYA: “Insider unajua ulichofanya siku ile sio kizuri, mpaka leo huwa najiuliza ulikuwa na mpango gani?.”

MIMI: “Tuachane na hayo, nimetii wito wako mama kwanza nimefurahi kukuona mshikaji wangu.”

SUMAIYA: “Now ni lunch time twende tukale then tuongee mambo muhimu.”

Tuliondoka kwenda moja ya mgahawa wa karibu kwaajili ya kupata lunch na mazungumzo yetu yaliendelea,

MIMI: “Nambie unaishu gani unataka kushare mama.”

SUMAIYA: “Insider nataka kununua gari kufikia February, unanishauri ninunue gari gani?”

MIMI: “Aisee upo vizuri kama mara hii unataka kununua gari bhasi huku unapiga sana hela.”

SUMAIYA: “Kawaida tu! Bwana wangu atanipa assist pia ndomana nakuwa na jeuri.”

MIMI: “Kama unaanza nakushauri nunua gari ndogo kwanza afu ukishapata uzoefu barabarani nunua gari kali, IST inakufaa kwasasa.”

SUMAIYA: “Eti, mimi nilitamani sana Dualis kama yakwako naipenda sana ile gari.”

MIMI: “Nunua Ist kwanza upate uzoefu wa kutosha barabarani then baadae nunua gari unayoipenda, hio pesa inayobaki isave. Uzuri ni kwamba Ist hata ukiigonga service zake sio gharama na ni nzuri kwa kujifunzia.”

SUMAIYA: “Sawa ni ushauri mzuri Insider, ndomana huwa nakukubali japo unaringa sana.“

MIMI: “Hata kwa bwana wako huwa unalalamika kama unavyolia-lia hapa?”

SUMAIYA: “Yeye ndo analialia kwangu sasa, hivi wewe unaona mimi wa kusumbuliwa na mapenzi?”

MIMI: “Bado hujabananishwa tu! Ni suala la muda.”

Baada ya kuachana na Sumaiya nilikwenda moja kwa moja mpaka ofisini na lengo kubwa nipitie ripoti za weekend hasa kwenye mauzo, na risiti za EFD zilizotolewa na kama kuna difference bhasi reconciliation ifanyike mapema kubaini tatizo liko wapi.

Pale ofisini alikuwepo Asmah, kama kawaida nilimsalimia na mimi nikaendelea na majukumu yangu. Asmah alikuwa kanilia buyu kama sikuzote na sikutaka kujipendekeza na nilifanya mambo yangu nikaondoka bila hata kumwaga.

Nilitoka kwenda Cocobeach na lengo nionane na jamaa ili nimuulize kama bado Sia anakwenda pale iwezekana nipate na mawasiliano yake, nilihisi jamaa hawezi kukosa.

Baada ya kuwasili pale kama kawaida jamaa alikuja kunihudumia na nilifanya kuagiza mihogo na mishikaki,

MIMI: “Kaka hivi yule dada bado anakuja hapa?”

JAMAA: “Kaka alikuja mara moja tu, na sijawahi kumuona tena labda amehama kiwanja hatuwezi kujua.”

MIMI: “Aisee hatari sana, labda kaondoka mjini hapa huwezi jua.”

JAMAA: “Hata siku ya mwisho kuja nilikuwa nimetingwa sana nikashindwa hata kuchukua namba yake.”

MIMI: “Usiwe na wasiwasi nakuachia namba yangu siku akija utampa anicheki.”

JAMAA: “Haina shida ngoja nikafate simu uandike kabisa maana usije ukasahau. Na vipi kuhusu yule shem wetu mbona simwoni?”

MIMI: “Daah! Yule kasafiri maramoja but atakuja usiwaze.”

JAMAA: “Poa kaka karibuni sana maana alikuwa ananipa sana maisha, akija hapa lazima aache kuanzia elfu 50, mteja kama yule ni muhimu sana.”

Jamaa alikwenda kufuata simu ili niache namba zangu na mimi muda huu nilikuwa nawaza Sia nishamkosa tayari, hivyo nianze kufikiria plan B nyingine. Niliendelea kufikiri Iryn ananifanyia ujinga sababu nafanya kazi chini yake ndomana analeta mambo ya kijinga, sasa ngoja nimwachie kampuni yake nione jeuri zake.

Saa 12 kasoro nilitoka pale Coco na nilikwenda Samakisamaki ya pale Masaki kuendelea kuangalia game za kombe la Dunia na hii siku Argentina ile mchana alikuwa kafungwa 2-1 na Saudi Arabia.

Nilikuwa nimetupia Jazz yangu ya Argentina na nilikutana na jamaa pale Samakisamaki yeye alikuwa ni shabiki wa Ufaransa na alikuwa ananicheka sana hii siku. Nakumbuka nilimwambia Argentina atachukua Worldcup lakini aliishia kunicheka sana maana aliona dizaini kama nazingua hivi,

“Yaani unafungwa na Saudi Arabia utaweza kupambana na France?.”

“Kaka unasahau Spain alianzaje 2010?”

“Sio kwa hii Argentina bossy nyie hata makundi hamvuki tupo hapa.”

“Kaka nachukua namba zako nitakukumbusha hili.”


Hii siku nilirudi home late sana maana ilibidi nisubiri na game ya France na Australia. Sasa baada ya kurudi home wife aliniwakia sana ni kama alikuwa anasubiri niingie kwenye 18 zake ili akiwashe,

“Baba J hivi ni lini utakuwa unawahi kurudi home na ukatulia na familia yako? Maana kila siku uko late ni mwanamke gani huyo anayekupelekesha hivi.?”

“Swahiba embu tulia kwanza, angalia hata hapo kwenye TV ni matangazo ya kombe la Dunia, sasa niwahi kurudi home wakati mnaangalia tamthlia zenu? Utakubali mimi niangalie mpira?.”

“Ndio mimi niko tayari ila uwahi kurudi home.”

“Wewe upo tayari how about Elena?.”

“Mimi nataka kuona unarudi home mapema sitaki sababu zako.”

“Angalia hata Junior kule anakucheka sababu anajua haiwezekani.”

Na wakati naondoka nilisindikizwa na ngumi ya mgongo “Ndiiiii” na mimi nikaenda kuoga. Baada ya kutoka bath nilikutana na missed call 2 za Prisca, sababu wife alikuwa seblen nikamcall back kumsikiliza anasemaje.

Prisca alipokea simu yangu na taarifa aliyonipa ni kuwa amekubaliana na msimamo wangu wa kuwa marafiki, lakini alinipa condition ya kuwa tuna-sex ambapo atanimiss na mimi nilimwambia sawa, maana sikutaka maongezi naye zaidi pale.

*******
Ijumaa mchana nilikwenda kumsalimia Jane Mbweni maana ilikuwa wiki inakata bila kukanyaga pale kwake. Baada ya kuwasili home niliingia ndani na huwezi amini ana kwa ana nakutana na Mrs Pama wa Ununio.

Ukweli sikutegema kama ningemkuta pale na mimi niliwasalimia wote nikaendelea kuzuga pale kwa dakika kadhaa nikatoka nje. Kwa upande mwingine Vicky alikuwa karudi kutoka hostel hivyo, tulikuwa tunapiga story pale nje kibarazani.

Hii siku sikuweza kuonana na Jane kabisa maana alikuwa busy sana na wageni, na Vicky alinambia Mrs Pama ameingia so muda mrefu. Nilimuuliza Vicky kama Mary bado anakuja home na akanambia jana alikuwepo pale siku nzima, niiliamua kumuaga Vicky na nikaondoka maeneo yale.

Toka sakata la Mary hatukuwa na mawasiliano na kwa upande wangu nilikuwa najisikia vibaya sana kuona Mary ananichunia namna hii ukizingatia ananipa kampani kwenye mambo mengi sana. Niliwaza kumpigia simu ili tuyajenge na nimwombe msamaha ili tofauti zetu ziishe, muda huu nilikuwa nipo njiani narudi home.

Baada ya kumpigia simu Mary alipokea simu na sauti nzuri nyororo ilikuwa ikisikika muda huu,

“Mary mambo unaendeleaje?”

“Salama! Nakusikiliza Insider.”

“Mary seriously? Sorry for all what happened. Naomba tumalize tofauti zetu wewe ni mtu muhimu sana kwangu.”

“Really? I don’t think so Insider.”

“Trust me, naomba kesho tuoanane Mary tukapate na Dinna ya pamoja usiku, please!.”

“Insider It’s impossible, thank you.”

“Why Marry?”

“I’m very busy thus why.”

“So when?”

“I don’t know.”

Hapa nikaona Mary hana mpango kabisa na mimi ni kama ameshaamua kukaa mbali na mimi, so sikutaka kuendelea kumbembeleza,

“Sawa Mary ukiwa tayari please letme know. Thank for your time” na nikakata simu.

Barabarani kote mpaka nafika home nilikuwa nawaza why Mary kachange haraka hivi? Nini kinaendelea? Au Jane kamchana ukweli Mary kuwa mimi sina mpango naye? Ni maswali ambayo yalikuwa yanakosa majibu na nilikuwa dilemma.

Mapema sana nilikuwa nimewasili home na nilikwenda jikoni kumsaidia wife kupika hata yeye alibaki anashanga leo kulikoni? Maana sio kawaida yangu kabisa, na muda huu nilikuwa nakatakata kachumbari maana wife alikuwa anapika chips yai kwaajili ya dinna.

Jumamosi asubuhi mapema mama Janeth alinipigia simu kunipa taarifa amerudi na anahitaji sana kuoanana na mimi kwani hana muda mrefu hapa Dar. Tulikubalina na mama tuoane mchana lakini sehemu ya kukutana alisema ata confirm.

Saa 6 mchana mama alipiga simu na alinipa taarifa tukutane Mlimani city, lakini aliniomba nikawachukue watoto zake kule Masaki then niende nao Mlimani.

Nilitoka home kwenda Masaki kuwafata na walikuwa na dada wa kizungu wakapanda kwenye gari tukaendelea na safari. Hawa watoto zake mimi wananijua sana na huwa napiga nao sana story nikienda pale kwa mama Janeth. Huyu dada wakizungu ndo nilikuwa namwona kwa mara ya kwanza na baada ya kusalimiana niliendelea kuongea naye pale na nilijua ni ndugu wa mama Janeth.

Baada ya kuwasili pale Mlimani city mama alikuwa amekaa pale Instanbull akitusubiri na tulikwenda mpaka pale. Nilisalimiana na mama na kila mmoja aliagiza chakula anachotaka story zikaendelea pale. Mama alinitambulisha yule dada ni mtoto wa dada yake na amekuja Tanzania kutembea pamoja na kufanya research, hivyo itabidi niwe nampa kampani ya usafiri.

Mama alinambia dhumuni kubwa la kuniita pale ni kuhusu suala la kuanza kuandaa Financial statement mapema pamoja na ile ya kule kwa kina Sumaiya. Ni biashara mbili tofauti lakini zilikuwa chini ya kampuni moja na mama alisema hata Sumaiya anajitahidi sana kwenye kutafuta tenda za usafi.

“Insider itabidi ufanye mawasiliano na Iryn ili muone jinsi ya kuanza kuandaa hizi statements mapema.”

Kwa upande mwingine mama alinambia kuna Equipments amenunua kwaajili ya Salon na jumatatu zitafungwa salon zote ili kuongeza ufanisi kwenye biashara.

Kwa mwaka huu tulikuwa tumeuza sana mpaka mama alifurahi na alinipa pongezi kubwa kwa kazi niliyofanya maana mauzo yalikuwa yako juu sana na mimi nilimwambia kama faida bhasi tuna supernomal profit.

Wakati niko na mama kwa upande mwingine Mary alinitext kuwa yuko tayari kutoka out na mimi. Ofcourse nilifurahi sana kuona Mary kakubali na tulikubaliana nitampitia saa 12 jioni.

Mida ya saa 9 mchana baada ya mazungumzo nilimuaga mama na nikaondoka kurudi home ili nipumzike, then badae nikutane na Mary kwaajili ya mtoko.

Mida ya saa 11 jioni simu yangu ilianza kuita ni Iryn alikuwa anapiga, kwanza nilishangaa maana sikutegemea kuwa ni yeye ambaye anapiga na nilipokea kwa haraka sana.

“Hey Darling za wewe?”

“Poa baby unaendeleaje?”

“I’m great, niko Serena Hotel, I am waiting for you, please be hurry and I miss you so much.”

“What? Upo serena hotel?”

“Yes baby, you don’t trust me? Please I need you here right now na mwanao kakumiss sana.”

“I am coming baby soon!”

GOODNIGHT
Thank you for your time Niggar
 
Tulipoishia, Kama unawazazi jitahidi uwapende wazazi wako wakiwa hai, wazazi wanatuombea sana. Itoshe kusema baada ya kurudi home milango ikafunguka sikukaa muda nikapata kazi.

INAENDELEA… EPISODE 02:

Ghafla simu yangu ikaanza kuita prirrr[emoji338] priirrr[emoji338][emoji338]ilikua namba ngeni, nikapokea, halooo

SIMU: Kwa majina naitwa “Rose Mutesi” napiga simu kutoka taasisi “X” nitakua naongea na INSIDER MAN?, nikamwambia yes ni mimi karibu. Dada akanambia hongera kwa kufaulu interview umechaguliwa kupata mafunzo kazi (Internship) kwenye taasisi yetu, jiandae mwanzoni October tutakupigia simu kwaajili ya kuanza kazi. Baada ya kuongea nae akakata simu [emoji3513].

Kiukweli sikuamini kama nikweli maana niliona kama ndoto hivi, nikasema hawa wanaweza kuwa matapeli, inshort sikuwa interested na ile simu. Sikumwambia mtu yoyote juu ya hili jambo hata mama sikumwambia maana niliogopa wasije wakawa matapeli. Hapo nilikua tayari nina miezi 2 niko home, wakati nimefika mzee wangu alikaa siku 3 akarudi Zambia.

Mzee wangu ni engineer kule kuna kampuni anafanyia kazi na pia mzee wangu kurudi home ni nadra sana anaweza kukaa hata miezi 3 na zaidi bila kurudi nyumbani. Nilikua naongea na mama mambo mengi sana hasa alikua anataka kujua pale kwa Uncle kama ninaishi vizuri. Ni kwamba mama yangu anamjua vizuri sana Aunt ni mtu wa namna gani, sikutaka kumwambia mama lolote kuhusu pale kwa Uncle niliamua kuyaweka moyoni. Japo mama alihisi kuna jambo halipo sawa,lakini alinisistiza sana kuwa na adabu na heshima. “Kila siku usiku tulikua tunapiga maombi na mama” mama yangu ni mtu wa dini sana.

Mwezi wa 9 mwishoni 2019, nikaamua kurudi Dar ili kuwa karibu endapo ningepigiwa simu na ile taasisi. Nikamwaga mama, akanifungia mchele wa kutosha, unga, mafuta ya kupikia gallon, maharage akanambia mpelekee Uncle. Niliamua kurudi palepale kwa Uncle lakini this time nilikua naplan zangu kichwani tayari. Baada ya kurudi Dar haikupita week nikapigiwa simu nikareport kazini nianze training.

Uncle nilimwambia kwamba kuna sehem nimepata part time, kazi ya muda nitakua natoka asubuhi, lengo langu nipate mkataba niwe na uhakika wa kumwambia. Lakini alisisitiza niwe nahakikisha mbwa wake wanakula ontime pamoja na kumwagilia maua yake. Kutoka na kurudi jion Aunt hakupenda siku nimerudi jion akanambia wewe sikuhizi umepata kazi na husemi?… nikamwambia hapana ningekua nimepata kazi mbona ningeliwaambia ila Uncle nilimwambia nimepata kazi ya muda. Dizaini hakupenda akanambia kwahiyo ukamwambia Uncle wako tu?, nikamwambia Aunt kwan kuna shida?. Akanambia sikuhizi hata kazi hufanyi… daah! . Nikamwambia huoni napikia mbwa chakula kila nikirudi jion? bado namwagilia miti namaua au unataka nifanye kazi gani??.

Aunt yangu alikua mtu wa gubu sana alikua na roho mbaya sana kama mtu wa hasira unaweza mtukana kabisa. Alikua ananichongea maneno sana kwa Uncle mpaka nikaona dizaini mzee baba kama anakua mbali na mimi.Kuna siku niliondoka na gari ya uncle kwenda kumchukua dogo shule, Uncle mara nyingi alikua anapenda kutumia gari ya ofisi ile yake inakaa home tu.
Sasa Uncle alivyorudi Aunt akamjaza maneno kuwa niliendesha gari yake eti siku nzima na nimeichibua gari. Uncle aliongea sana ile siku usiku “Sitaki uendeshe gari yangu kwanza hujui kuendesha gari, umenichubulia gari yangu. Gari ikiharibika unahela ya kulipa?? “. Ukweli ni kwamba ile michubuko ilikua vilevile, yale maeneo yalinichoma sana nikahapa kutokuja gusa ile gari hata aombe nimpelekee wapi.

Baada ya kumaliza training hatimaye nikapangiwa kituo cha kazi na nikaambiwa kesho niripoti pale ofisini. Sikuamini nilovyopewa ule mkataba kweli kesho yake nikaanza kazi nikapangiwa moja ya Idara kwenye ile ofisi. Hii ni moja ya taasisi kubwa sana hapa nchini na inategemewa sana sana.

Nilianza hii kazi bila malipo then nilikua niko vibaya sana kiuchumi ndugu zangu, mama Junior ndo alikua ananipiga tafu za nauli sometimes. Ilibidi nimwambie Aunt kwamba nimepata kazi kwenye taasisi X that day Uncle alikua safari nikaplan ntamwambia Uncle officially akirudi kwamba nimepata kazi face to face, Ukweli hizi taarifa Aunt hakuzifurahia ni kama nilimpiga na kitu kizito sana akaanza kuulizia mambo ya salary sikutaka kumwambia lolote.

Uncle akarudi toka safari nikaongea naye kuhusu kupata kazi na taasisi “X” japo hakuonesha ile furaha halisi niliona kuna unafiki hapa hajapenda. Akaniuliza nani kakutafutia nikamwambia nilifanya interview nikapigiwa simu, akauliza mambo ya mshahara nikamwambia hili suala bado ila ni kama nafanya kujitolea, kama kuna malipo nitakuambia. Huwezi amini Uncle hata hakusema neno “hongera”, nikaanza pata picha ninaishi na ndugu wa aina gani, hata mama alinambia niwe makini sana.

Pale ofisini baada ya mwezi nilikua nimeshazoeana na maofisa wa pale hasa idara yangu kama incharge/supervisor wetu alikua na roho nzuri sana. Alitokea kunikubali sana hizi ten ten nilikua nakula sana kila siku, yaani nilikua nafanya kazi kwa bidii sana na kujituma nikaweka urafiki na watu wa idara.

Pale kwenye kile kitengo chetu interns tulikua wawili mimi na dada mmoja hivi. Kadri siku zilivyokuwa zinakwenda nikawa nimezoeana na maofisa wa idara zingine wakawa wananipa kazi zao nafanya wananipa hela sikuwa nakataa kazi. Ikafika muda nikajikuta kwasiku sikosi 20,000 kuna kipindi napata mpaka 50,000/= au zaidi, hizi hela nikawa naziweka maana nilikua na mipango yangu kichwani ya kwenda kupanga.

Hii Taasisi niliyokuwa nafanyia kazi ina deal sana na wafanyabiashara hivyo nikaanza kupata connection na wafanyabiashara mbalimbali hasa pale Kariakoo.

Baada ya miezi 2 taasisi ikasema itaanza kutulipa 450,000 kwa mwezi zitusaidie bhasi kwangu ikawa sherehe. Nikaanza kununua vitu taratibu naacha madukani kwaajili ya kuanzia maisha. Nikawa nawaza njia ya kutokea pale kwa Uncle maana wangeanza maneno kapata kazi ameondoka sikutaka hizi kelele. Nikawaza hapa nitawaambia naenda safari ya kikazi Dodoma ndo itakua gia yangu ya kusepa pale.

Baada ya hapo sikuchelewa nilikua na iphone 7 plus nikaiuza 740,000 nikawa kidogo napesa ya kuanzia maisha. Nikamtafuta dalali tukapata chumba sebule na jiko kodi ilikua 180,000 kwa mwezi, nikalipa kodi ya miezi 4 kwanza. Eneo nililopata ilikua ni salasala (Mabanda mengi) pale Mbuyuni mataa ya kwenda tegeta na kunduchi, sasa kwa mbele kama unakwenda Tegeta kuna kibarabara kinakata kushoto kwenda salasala, kule ndo nilikoanzia maisha.

Nikaweka godoro langu chini, nikaweka jiko langu la gas, nikanunua gas mtungi mkubwa, sufuria na baadhi ya vyombo vya kuanzia maisha bila kusahau subwoofer “Sea piano” [emoji3], raha ya geto mziki uwe unasikika.

Baada ya hapo nikaanza kuamisha vitu vyangu bila kushtukiwa mpango wangu. Baada ya hapo nikawaaga nitakwenda kikazi Dodoma sijui nitarudi lini wakaniambia safari njema, maisha ya geto niliyaanza March 2020.

Nimeingia pale sasa akili ya maisha ikaanza kuja kichwani, kwanza nimelala pale kuna baridi hatari sina hata shuka la kujifunika, madirisha hayana mapazia[emoji2][emoji1]. Week ileile niliyohamia kwangu nikapambana nikanunua mapazia mazuri nikayaweka. Bad news haikupita hata week nikaibiwa yale mapazia na laptop [emoji22].

Pale palikua na wapangaji watatu na wote tulikua tunatoka afu fense ilikua fupi mtu rahis kujua kama hakuna mtu, na pia geti lilikua tunarudishia si unajua tena maisha ya kupanga geti huwa halifungwi. Uzembe ulikua wangu maana sikufunga madirisha ilikua rahsi kuibiwa jama alichomoa mapazia yote mpaka seblen. Nilihisi aliyeniibia ni mzoa taka wala sio mtu mwingine maana ndo alikua na mazoea ya kuja pale home.

Mungu akaendelea kufungua milango, kutokana na kuwa na changamoto nikipika chakula kikibaki kinachacha nikaona kuna umuhimu wa kununua fridge. Nikafanya research yangu pale Kariakoo nikaona bora ninunue fridge la size ya kati bei ilikua ni 720,000 kwa kipindi kile.

Nikapambana sana pamoja na kukopa nikaweza kununua fridge, mama Junior naye hakua mbali akaniletea Micro wave ya kupashia chakula na mazaga mengine kama mashuka nknk. Ndani ya muda mfupi nikawa nimekamilika na kila kitu ndani kiasi kwamba ukiingiza pisi ndani lazima ipagawe. Baada ya hayo niakaanza kusave hela kila senti nayopata nikawa nasave kupitia vicoba na kucheza michezo.

November 2020, mama junior akaja kwangu akanambia ana mimba yangu hivyo kwao amekimbia hawezi kurudi anamwogopa baba yake. Hapo alikua anasoma chuo na mzee wake katoka kulipa ada afu sasa mzee wake ni mkorofi hatari ndomana akakimbilia kwangu hakutaka kutoa ile mimba.

Zile habari hazikunishtua niliona mtoto ni jambo la kheri then hata yeye nampenda nikamwambia kama mtoto ni wangu bhasi utakaa hapa huko kwenu tutaweka mambo sawa, si unajua wazee wa kichaga.

Nikampigia simu mama yake kumwambia bint yake yupo kwangu asihangaike kumtafuta mimi naandaa utaratibu nitakuja, mama yake alikua anajua natoka na bint yake hakua nashida na mimi. Akanambia kama yuko kwako mimi sina shida najua yuko sehem salama ila sasa baba yake ndo shida.

Tulikwenda hospital kuchek mimba ilikua na week 6, ikabd nichukue hatua zingine za haraka ili kukamilisha hili jambo, hatimaye tukalipa mahari.

Baada ya kuanza kukaa na mama Junior hapo ni mjamzito mambo yangu yakazidi kunyooka sana, nikawa mtu wa bahati sana. Kuna mwanamke ukiwa naye mambo yananyooka yenyewe. Nikaanza kutengeneza connections na wafanyabiashara wakubwa, stakeholders na watu mbalimbali maana sikuwa naona future ya kuajiriwa na hii taasisi.

Nikaanza kujiongeza mlemle Kariakoo na kufanya deals zingine nyingi, nikafungua biashara “workshop” ya kupaka rangi magari, services, lubricants, polishing nknk pale gerezani. Kwa kufupisha hii story baada ya kumaliza mkataba tukastopishwa kwenda kazini na mimi sikutaka kuhangaika na kuomba na kutafuta kazi. Hapo ilikua ni September 2021.

Sikushtuka sana, mimi binafsi nilikua nishajipanga tayari na nilishaona dalili mapema, savings binafsi nilizokuwa nazo za haraka cash in hand ni 24 million. Nikaagiza Toyota IST kutoka Japan iwe inanisaidia mishe zangu za hapa napale. Baada ya kununua gari, kukamilisha kila kitu nilitumia 14 million, nikalipa deni la kiwanja full 5,600,000/=nikamwekea wife 3 million kwa account maana mwakani 2022 alikua inabidi arudi chuo kuendelea na masomo alikua kashajifungua tayari. Nakumbuka sikubaki na kitu katika ile saving lakini nilikua na shares zangu kwa watu hivyo hata bila kazi ningesurvive.

Maendeleo ya Biashara yalikua mazuri sana nilikua na wateja wengi sana na pesa nilikua naiona kama faida. Ile September mwisho wa mwezi mwenye eneo/Landlord akanipigia simu.

LANDLORD: Kijana wangu hujambo? sasa nina habari mbaya nataka kukupa maana ipo chini ya uwezo wangu. Kutokana na ujenzi unaoendelea na upanuzi wa barabara nimepewa order ya kwamba nyumba zetu zitaweza bomolewa muda wowote. Na wewe kodi yako inaisha mwezi ujao, itabidi utafute eneo lingine mambo yatakapo kamilika nitakutaarifu kijana wangu.

Ukweli taarifa za Mzee zilinipa stress sana maana biashara ilikua imechanganya sana na kwa ile location ilikua nzuri sana. Niwaambie biashara ya workshops inalipa sana faida inaonekana sana. Mchawi ni location tu maana pale nilikua nakamata magari yanayotoka bandarini nknk.

Ofisi yangu ilikua Gerezani karibu na Round about [emoji3534] ya kwenda Kurasini. Kama unatokea central before hujafika kwenye ile Round about kuna yard ya magari bhs mitaa ileile. Baada ya kuongea na mzee nikawa sijui niende wapi maana nilikua dilemma, pia watu wakanishauri ujenzi wa barabara unaondelea biashara itakua ngumu sana maeneo yale hivyo nisubiri niangalie upepo. Ikabidi nistop kwenye hii biashara kwanza,nikaplan nitarudi barabara ikikamilika. Ilikua kama mkosi naacha kazi na biashara nafunga niliona kama mtu ananichezea hivi.

Nikafunga biashara katikati ya October kodi ndo iliisha tarehe hizo, baada ya hapo nikawa sina hela maana hakuna nilichokua naingiza. Ile ile october kuna mhindi alikua jamaa yangu sana niliweka kiasi cha pesa kwenye biashara yake ni muda. Jamaa alinicheki akanambia anakwenda India na pale watasimamia ndugu zake itaweza sumbua kupata gawio zangu hivyo akanipa pesa magawiwo yote 6,000,000. Nikakusanya na madeni yangu na pesa zingine nikapata 3,400,000 jumla nikawa na 9,400,000/=.

Ikabidi nikae na wife chini tupange mipango maana alikua anajua kinachoendelea. Nikalipa kodi ya nyumba 1,800,000/= kwa miezi sita. Nikampa wife 2,500,000/= kwaajili ya matumizi ya mtoto, mshahara wa dada, bill za umeme na maji na mahitaji ya nyumbani yote (Miezi 6). Nikamlipia mtoto bima pamoja na mama yake kama 245,000/=.

Ilibaki kama 4,800,000 tukaplan hii amount tufungue biashara ya vinywaji. Lakini kuna dogo langu anayenifuatia yeye alikataa shule alisema anapoteza pesa za wazazi na muda. Toka muda alikua ameniomba nimkopeshe million 3, “alipataga hasara walimtapeli” dogo anaduka la vifaa vya simu na Huduma za kifedha. Dogo pia alinisave sana kipindi kile nakosa nauli za kwenda kazini, so nikampa dogo million 2 kama kaka yake. Nikamlipia dogo ada “yule ambaye mama alisema anataka sayansi ila math haipandi” nililipa million 1. Hapo unaona jinsi ambavyo pesa haikai kabsa.

Nilibakiwa na 1,500,000/= hivi nikasema hizo nilizotoa nitajazia. Ukitaka kuona mambo yanabadilika acha kazi ndo utaona kila rangi. Bhasi nikaanza kuwaza namna ya kutafuta pesa nikisema nisubiri pesa iishe nitakuja aibika huko mbeleni. Nikafikiri kuingia kwenye uber maana gari nilikuwa nayo tena yangu, kumpa mtu hapana bora nikomae mwenyewe tu. Kuna jamaa yangu wa uber alikua mshikaji sana nikamcheki…[emoji338]

DULLAH: oya tajiri vipi hatutafutani sikuhizi umenitenga hunipi kazi kama zamani hali ni mbaya.

MIMI: Tajiri sijakutenga sema pale nimetoka ndomana unaona kimya mwenyewe sina maisha ndomana nimekucheki unipe ramani.

DULLAH: Sasa tajiri mimi nakupa mchongo gani hapa nakomaa na uber tu hapa, siku za kati ya wiki tunafanya kuokoteza, cha muhimu mkono uende kinywani.

MIMI: Tajiri nahitaji tuonane nina jambo langu muhimu sana unipe code nianzie wapi ili kufanikisha.

DULLAH: Jambo gani tajiri unanitisha, kesho nitakua home siku nzima, leo nitakudanganya boss wangu. Wewe kesho njoo muda wowote tutayajenga.

MIMI: haina noma kesho asubuhi nitakucheki unipe code.

DULLAH: Imeisha hio tajiri [emoji3513]

Asubuhi nikamcheki Dullah ilikua kama saa 2 asubuhi hivi akapokea akanielekeza anakaa Sinza madukani unakunja pale kwa vunja bei. Bila kupoteza muda nikaenda chap nikafanikiwa kufika kwa jamaa, tukaanza story…

DULLAH: Tajiri karibu sana naona upo na chombo mpya kabsa hii hata week haina. Hii chombo umechukua yard au umeagiza?

MIMI: [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3], Tajir huoni kabisa hadi alama za bandarini hizo chuma imetoka Japani. Sikia ndugu yangu mchongo wenyewe naotaka tuongee ndo huo unaoushangaa.

DULLAH: Sijaelewa Tajiri unauza hii IST?? au

MIMI: Nataka kusajili Uber tajiri unanisaidiaje? Nataka maelekezo kutoka kwako wewe una experince ya muda mrefu.

DULLAH: Unataka kuendesha wewe au nikutafutie dereva?

MIMI: camon mimi bro!

DULLAH: Kama wewe sikushauri hii gari ubadilishe vibao tumia hivyohivyo vya njano, akaifungua ndani akaona gari nimetia seat cover, full unyunyu, Android Tv nch 10 imekaa pale, chini carpet. Mzee hii gari utapiga sana hela niamini mimi kama hawa mademu watakutafuta sana, utapata root privates nyingi, kama nilivyokwambia usiweke vibao vyeupe.

MIMI: kwanini nisiweke vibao vyeupe?

DULLAH: Vibao vyeupe miyeyusho ndugu yangu traffic mikono mingi, bado TRA yaani tunapata shida wahuni sikuhizi wanatumia vya njano.

MIMI: Basi poa nimekuelewa sasa najisajilije?

DULLAH: Kuna jamaa namjua ila sijawai kumwona kwa sura ni kama “Ghost” anakusaidia chap wewe andaa 100k. Kama unayo hata leo anaanza kazi baada ya siku 3 kila kitu kinakua sawa. Hapa anza na Bolt hii haichelewi huku unasubiri uber hii kidogo utasubiri.

MIMI: ongea na jamaa then nipe namba yake mwambie huyu ni ndugu yangu wa damu. Afu unaongeaje na mtu usiyemjua?? Kama tapeli?

DULLAH: [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], Tajiri nishafungua account nyingi sana na yeye hana noma usiwe na wasiwasi.

Dullah akaongea na jamaa walitumia muda kidogo baada ya hapo akanirudia akanambia nimeongea naye Freshy utampa 90,000 atafanya hiyo kazi. Nikamshukuru nikampa 10,000 ya Ahsante.

Nikampigia simu Ghost tukaongea maana alikua anajua tayari kuhusu mimi. Akanambia nimtumie baadhi ya documents kama kadi ya gari, ID, bima na picha ya gari na taktaka zingine. Akanambia ndani ya siku 3 itakua tayari.

Baada ya siku 3 akanicheki ghost akanambia account yako ipo tayari, akanipa password akanambia download bolt driver app kwa simu then anza kazi. Kweli nikafanya nikaona mambo yako supa nikaona sehem ya kwenda online kama unataka request, nika touch pale nikaona inasearch nikazima data nikalala, nikaplan kuingia mzigoni jioni.

Nimeshapata account ya bolt tayari nini kitaendelea? Mama Junior hajui kama nimeamua kufanya hii kazi atakubali?? Usikose mwendelezo story tamu ndo zinaanza sasa, usikose bando tu.

ENDELEA….

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Nzuri juu
 
SEASON 02
CHAPTER 06:

A TRUE STORY BY INSIDER MAN

PREVIOUS:
Mida ya saa 11 jioni simu yangu ilianza kuita ni Iryn alikuwa anapiga, kwanza nilishangaa maana sikutegemea kuwa ni yeye ambaye anapiga na nilipokea kwa haraka sana.

“Hey Darling za wewe?”

“Poa baby unaendeleaje?”

“I’m great, niko Serena Hotel, I am waiting for you, please be hurry and I miss you so much.”

“What? Upo serena hotel?”

“Yes baby, you don’t trust me? Please I need you here right now na mwanao kakumiss sana.”

“I am coming baby soon!”

CONTINUE:

Sikutaka kumlaumu kabisa kwanini alikuwa kaniblock maana niliona naweza sababisha matatizo mengine, ukizingatia alionekana kuwa kwenye mood nzuri.

Nilishusha pumzi nzito muda huu na nilianza kufikiri namna ya kudeal na Mary maana tulikuwa tushapanga tayari kuonana badae. Ukweli nisingeweza kutoka na Mary afu nimwache Iryn kitu ambacho kisingewezekana, kwa upande mwingine Iryn alikuwa kaharibu mipango yetu.

Niliwaza namna ya kumpanga Mary vizuri ili anielewe lakini nilikuwa nakosa namna ya kumweleza, niseme nini?. Kama ni sound nishampiga sana tena za kutosha na leo ndo ilikuwa final chance ya kuonana naye.

Niliamua niache kufucos na Mary na nifocus namna ya kumpanga mama J sababu nakwenda kukaa na Iryn huko hotelini na sijui itachukua muda gani. Mama J alikuwa yuko dukani kwenye goli lake hivyo nilimpigia simu na kumdanganya nakwenda Dodoma,

“Baby nimepata emergence nakwenda Dodoma mara moja sababu ofisi ya Ardhi watakuwa wanapima viwanja na lile eneo letu jipya kesho litapimwa. Nimeona ni busara nikaenda mimi kuliko kumtumia mtu baki maana tukizembea tunaweza kudhulumiwa eneo letu.”

Mama J hakuwa na shida kabisa na alinipa baraka zote maana ni jambo muhimu sana.

Baada ya kumalizana na wife niliingia bafuni kuoga na wakati najiandaa kwa upande mwingine Mary alianza kupiga simu. Na muda huu nilikuwa nafikiri sound ya kumpiga Mary na nilisema acha liwalo na liwe, siwezi kumkera Iryn kwaajili yake.

Niliondoka kwenda Posta na kipindi niko njiani nilimpigia simu Mary ili nimpange kuwa nimepata emergence ya msiba hivyo niko njiani naelekea. Mary kwa upande wake hakuwa na say lakini alionekana kumind sana, ukizingatia alikuwa kajiandaa tayari kwaajili ya mtoko. Ilibidi nimwombe msamaha sana kwa jambo hili, nilimwambia tutatoka next time.

Baada ya kumalizana na Mary niliwaza sana, Why nikitaka kutoka na Mary lazima jambo lolote litokee? Kuna siri gani hapa? Kwanini iwe kwa Mary tu?. Nilijiona kama sina bahati naye na mimi nilijisemea sometimes huwezi jua mipango ya Mungu ananiepusha na nini.

Saa 12 za jioni ndo muda ambao nilikuwa nawasili Serena Hotel, pale reception niliweza kufanya utambulisho na nilikwenda moja kwa moja mpaka room ya Iryn. Niligonga mlango na haikuchukua muda alifungua na ile kuingia ndani tu! Nilipokelewa kwa kumbatiwa ni kama alikuwa akinisubiri kwa hamu sana pale.

“Baby I have missed you so much.”

Kwa upande wangu sikuwa na say zaidi na mimi niliendelea kumkumbatia na nilikuwa nikivuta harufu nzuri sana kutoka kwake. Joto nililokuwa nalifeel pale nilijikuta mnara umeanza kusaka mawimbi ghafla, hata yeye alianza kuhisi kitu kigumu kikimtekenya.

“Baby I can feel your Cock.”

Palepale tulianza kupeana makisi hatukuwa hata na muda wa kuongea ni romance zilianza na ndani ya muda mfupi nilikuwa nashuhudia uumbaji wa Mungu live. Jinsi nilivyokuwa nime-mmiss na ule uzuri wake RPG yangu ilizidi kuwa ngumu sana. Zoezi la kutengeneza njia ya mtoto ilifanyika barabara na baada ya hapo tulianza maongezi na muda huu alikuwa kajilaza kwenye kifua changu,

MIMI: “Baby mimba inakufanya unazidi kuwa mzuri.”

Ni kweli Iryn alionekana kuwa mrembo sana kuliko siku zote.

IRYN: “Hata wewe nakuona umebadilika baba mtoto, hii mimba imenipenda hainisumbui sana.”

MIMI: “Na kwanini umekuja bila kunipa taarifa?”

IRYN: “Baby I wanted to suprise you.”

MIMI: “Unajua kabisa mama J mambo yake, ungesema mapema unakuja mimi ningefanya maandalizi hata kuja kukupokea, sijapenda.”

IRYN: “Baby unatakiwa utambue mimi na mama J wote ni sawa, do you want to tell me that you only care about her? What about me?”

MIMI: “I do care about you.”

IRYN: “Seems unataka kuondoka uniache alone here, na nitakuwa na wewe hapa mpaka naondoka.”

MIMI: “Mimi niko na wewe mpaka unaondoka, ukweli nimekumiss sana na natamani urudi Tanzania ili niwe nacheza na mwanangu kama hivi.”

Iryn aliniangalia kwa tabasamu zuri sana maana maneno niliyompa yalikuwa matamu kwake na alisogea ili niendelee kumchezea tumbo.

“Kwanini ulini-block?”

IRYN: “I didn’t want to talk to you.”

MIMI: “Unamaaninisha nini?”

IRYN: “Mkataba wetu unaukumbuka? Sasa wewe endelea kufanya upuuzi wako, I think humtaki huyu mtoto ndomana unafanya hivi. Do you love Asmah? I am asking you.”

MIMI: “Sielewi point yako unamaanisha nini, na kwanini useme hivyo? Unanikosea heshima baby.”

IRYN: “Soon unakuwa baba wa watoto wawili, Insider tulia na focus na future za hawa watoto kwasasa achana na hawa akina Asmah maana watakusababishia matatizo. Nina appreciate kwa kazi mnayofanya kwenye kampuni lakini unavuka mipaka. How come you are dating the woman you had sex with? It's just like opening the Fanta and putting it on the table, ready for whenever you want to drink it again.”

MIMI: “Baby mimi naona wivu wako umevuka mipaka, Asmah tumetoka out ile juzi baada ya kumaliza mafunzo. Kumbuka mimi ni manager na ingekuwa ngumu kuwakatalia ndomana nilijumuika nao na nilirudi home mapema sana ile siku.”

IRYN: “Na kilichokuwa kinafanya msipokee simu ni nini? Kama hakukuwa na tatizo lolote?”

MIMI: “Simu ilikuwa kwa gari ndomana lakini hakuna kinachoendelea na hakiwezi kutokea.”

IRYN: “Be careful with this, by the time I turn around, our history will be over. Usinione mjinga sana kwa maamuzi niliyofanya ukajiona ume win, still ni mapema sana.”

Ni maneno aliyotoa Iryn na alionekana kuwa serious sana na kauli zake, lakini kwangu mimi ni kauli ambazo ziliniingia sana na niliona kweli nazingua.

“Baby tunaenda Capetown kula prawns sindio?”

MIMI: “Jiandae tuondoke ndo mida yenyewe hii.”

Tuliingia bath kuoga na nilitumia nafasi yangu kumuonesha utundu wangu kumuogesha, kwa upande wake alifurahi sana kwa kitendo nilichofanya. Kadri ya muda unavyozidi kwenda tulianza utoto wa kumwagiana maji mle ndani na tulijikuta tukianza tena kwichi kwichi.

Baada ya kutoka Iryn alifungua bag lake na alitoa zawadi alizoniletea kutoka Ufaransa ikiwemo perfume, nguo na raba. Muda huu aliendelea kujiandaa na ndani ya muda mfupi alikuwa kapendeza sana, niliishia kumwagia masifa pale.

Kwa upande mwingine tumbo lake ilikuwa bado dogo sana na hakuonesha kuwa na mimba. Tuliondoka huku tumeongozana na nilikuwa nimemshika kwa mkono wa kushoto na mkono wa kulia nilikuwa nimeshika handbag yake.

Tuliishiwa kupigwa macho mpaka tunafika parking ukizingatia jumamosi huwa panakuwa na movement ya watu sana pale hotelini. Iryn ni mwanamke mzuri sana pale ambapo utafanikiwa kumwona kwa mara ya kwanza lazima ugeuke umtizame kwa mara ya pili. Baada ya kufika kwa gari nilimfungulia mlango akaingia, nilikuwa namtreat kama malkia na yeye aliishia kufurahi tu. Ukweli tulikuwa tumemisiana sana-sana na story ziliendelea,

IRYN: “Darling mama kanambia unataka kurudisha hii gari, why?”

MIMI: “My turn! Why hukunambia hii gari ni yako?”

IRYN: “Mama ndo anasema hivyo but its okay, wewe endelea kuitumia tu!”

MIMI: “I wish lakini kwa hii gari hapana nitakuwa naendesha mara moja moja, kwa usalaama zaidi.”

Na muda huu nilikumbuka lile sakata la picha za ultra-sound.

“Hivi unajua mama J aliziona zile picha za vipimo vya ultra?”

IRYN: “My God! How did she get those pictures?”

MIMI: “Ulisahau kwenye gari, sijui alikuwa anatafuta nini akaziona japo…..”

Nilikatishwa maongezi yangu,

IRYN: “Then ilikuwaje?”

MIMI: “Nilimwambia hizo picha sio zako, japo yeye anaamini wewe ni mjamzito na umeondoka Dar kisa hiki. Why ulizisahau kwa gari? Kama mama Janeth angelitumia gari si angeziona?”

IRYN: “I don’t know how I forgot but nakumbuka sheet ya mwanzo niliitoa nikaichana.”

MIMI: “Na hii ndo ilisaidia otherwise siri ingekuwa ilifichuka. Itabidi uende ukamtembelee mama J hata kesho baby, ili aridhike.”

IRYN: “Sawa no problem nitakwenda kesho mchana kumsalimia mke mwenza.”

MIMI: “Why mchana huoni kama anaweza akahisi wewe ni mjamzito?”

IRYN: “Hii mimba inanisumbua sana nyakati za usiku ndo huwa najisikia vibaya ila sio sana. Nikienda usiku inaweza kuwa mbaya zaidi bora niende mchana, nitavaa gauni langu.”

MIMI: “Mama alikuja South mlionana?”

IRYN: “Yeah tulionana but she was so busy, How the hell did she find out you have a child?"

MIMI: “Niseme ilikuwa surprise maana nilikwenda na Junior ofisini jumamosi.” Ilibidi nimpe mkanda mzima jinsi ilivyokuwa,

IRYN: “Mama alinipigia simu akanambia kila kitu, japo alionesha kutopenda hii siri tuliyomficha. But nilimwambia hayo ni maisha yako binafsi na suala la wewe kuwa na familia halina impact na kazi.”

Ndani ya dakika 20 tulikuwa tumewasili pale Capetown kwa bahati mbaya kwa siku za weekend pale huwa panajaa sana, hivyo ilibidi tupark gari mwanzoni kabisa. Maeneo kama haya huwezi wakosa Masai na ndo aliyenipa nafasi ya parking na nilimsisitiza sana ulinzi wa ile gari.

IRYN: “Hey mpenzi tunakuachia gari yetu tulindie eeh! Nikirudi nitakufurahisha.”

MASAI: “Tajiri unamiliki kisu hatari sana, unakojolea pazuri sana.”

MIMI: “Masai wewe ilinde hii gari ndani ya saa 2 tutakuwa tumerudi.”

Iryn aliishia kutabasamu tu maana maneno ya Masai yalionekana kumfurahisha sana. Na aliniuliza kwanini Masai huwa wanatabia ya kuongea maneno kama haya tena bila aibu?. Licha ya sifa zote ambazo huwa anamwagiwa lakini yeye kwa upande wake huwa anajiona wa kawaida tu.

Niliimshika mkono kama kawaida yangu na tuliongozana kuingia ndani na niseme njiani macho yote yalikuwa kwa Iryn. Tulipokelewa na tulioneshwa sehemu ya kukaa na tulifanya kuagiza prawns na maongezi yaliendelea maana tulikuwa na vitu vingi sana vya kuongea.

Mpaka tunafika pale Capetown nilikuwa natamani sana kusikia taarifa za kutoka huko Ufaransa pamoja na Ethiopia kwa ujumla.

MIMI: “Baby now ni muda wa kudiscuss kilichokupeleka Ufaransa.”

IRYN: “Thank God everything went well, next month tunaweza kuanza business.”

MIMI: “Nimefurahi sana kusikia hivyo, ni project gani?”

IRYN: “Baby you know siwezi kutoka out na field ya Beauty. Pia sikukwambia South nimefungua biashara hiohio ya beauty na massage.”

MIMI: “Najivunia kuwa na wanawake wapambanaji hata mama J anafanya vizuri kwa nafasi yake.”

IRYN: “Mama J anaakili ya biashara ana mipango yake mingi tu huwa anashare kwangu.”

MIMI: “Nafurahi kuona mnapatana, na vipi kuhusu Ethiopia?.”

IRYN: “Sijakwenda baby maana mwezi ujao nitakwenda kwaajili ya ukumbusho wa kifo cha mama. Pia nilitaka kukwambia itabidi twende wote baby, I really need your company there, ukawajue na ndugu zangu taratibu.”

MIMI: “Mhhh! Hii ni bad idea utanitambulishaje kule? Na hio mimba vipi?”

IRYN: “Come down kinachofanya uogope ni nini? Nikuzalie mtoto afu home usijulikane? Unaona ina make sense?. Okay, mimi mpenzi wako unataka niende alone kwenye tukio muhimu kama hili?

Suala la kwenda Ethiopia kwangu mimi niliona ni mtihani maana niliwaza najiwekea kitanzi shingoni mwenyewe. Na muda huu Iryn alianza kubadilika na furaha yake ilianza kupotea, ilibidi nikubali kinafiki ili kurudisha furaha yake.

MIMI: “Baby sijamaanisha hivyo, will go together na tutakaa muda gani?”

IRYN: “Maximum three days.”

Na muda huu kwenye luninga ilionekana match ya Argentina na Mexico ikitaka kuanza na macho yangu yote yaliekeza kwenye luninga, ukizingatia mimi ni shabiki wa Argentina. Hii game nakumbuka nilikuwa naingalia kwa presha sana maana tulikuwa tunahitaji kushinda, afu sasa Argentina ikawa inacheza kama haitaki ushindi.

MIMI: “Baby wewe timu gani unashabikia kombe la Dunia.?”

IRYN: “France always and forever, kwa huo userious ulionao kwenye hii match wewe ni Argentina.”

MIMI: “Yeah baby

Mpaka kufikia half-time hii game ilikuwa bilabila na muda huu Iryn alianza kujisikia vibaya maana alisema anajisikia kichefu chefu. Nilimpa kampani kwenda washroom na mimi nikamsubiri mpaka anatoka, lakini baada ya kumwambia tuondoke alinigomea katukatu.

Kipindi cha pili dakika ya 60 na Messi anaweka goli wavuni watu tulipiga kelele balaa ilikuwa ni furaha sana kwetu hii siku. Mpaka game inaisha tulishinda 2-0 na sisi ndo kuondoka kwenda kulala.

Jumapili asubuhi Iryn alikuwa wakwanza kuamka, aliniamsha kwaajili ya breakfast na tuliongozana kwenda restaurant. Wakati tuko pale Iryn aliomba twende wote kwa Jane ili amsalimie, then wakati tunarudi apitie kwa Mama J amsalimie naye.

Saa 4 asubuhi ndo muda ambao tulitoka kwenda Mbweni na baada ya kuwasili maeneo yale, kulikuwa na magari uwanjani na mimi niliwaza lazima kuna wageni wakutosha huko ndani.

Baada ya kuingia ndani sebleni nilikutana na Mary, Vicky, mama yake na Pama nk na walikuwepo wageni wengine ambao siwajui. Jane alikuwepo pale sebleni na niliweza kumtambua best yake Mary wa kule Palm village.

Iryn confidence kwake ni suala dogo sana na aliwasalimia wote, alikwenda mpaka usawa wa Jane akamsalimia kisha akaomba kumbeba mtoto. Muda huu Mary macho yote yalikuwa kwa Iryn maana ilikuwa ni surprise afu hata mimi sikutegemea kukutana na Mary pale.

IRYN: “Dada Jane hongera sana, Insider alinipa taarifa nikaplan nikija Tanzania nije kukusalimia.”

JANE: “Thanks sana dear nakumbuka tulikuwa wote kwenye msiba ule usiku, nashukuru sana kwakuja.”

Iryn hakuwa mgeni machoni mwa baadhi ya watu pale seblen maana wengi wanamjua kasoro wageni ambao hawamfahamu ndo walikuwa wakimshangaa. Kwa upande mwingine mama yake Jane naye alionesha kufurahi sana kumwona Iryn na kila mtu pale alifurahi.

Iryn aliendelea kupiga story na Jane, kwa upande wangu nilikuwa naongea na mama yake Jane kuhusu maendeleo ya Jane kwa ujumla. Baada ya dakika 20 nilitoka kwenda nje kibarazani na haikuchukua muda Vicky alitoka pale nje na nilisikia akiniita,

VICKY: “Insider….”

MIMI: “Nambie Vicky za masomo?”

VICKY: “Safi, hivi yule dada uliyekuja naye nilimwona kipindi cha msiba ni nani?”

MIMI: “Vicky na wewe kwa maswali kama Police, na ukimjua ni nani itakusaidia nini?”

VICKY: “Insider kwanini unamajibu ya kukera? Nimekukosea nini?”

MIMI: “Yule dada ni Bossy wangu ndo ananiweka mjini hapa. Vipi umeridhika sasa?”

VICKY: “Nimeona da Mary anamwangalia sana mimi nikahisi labda ndo mke wako.”

MIMI: “Hapana sio mke wangu na Mary anamjua ndomana.”

VICKY: “Ni mzuri kwakweli amebarikiwa, kingine tarehe ya Mbwa kuchoma chanjo imekaribia. Naomba uongee na yule doctor aje kuwachoma chanjo.”

MIMI: “Usijali nitamkumbusha pia hata yeye atatupigia simu kutukumbusha, nafurahi kuona upo makini.”

Tuliendelea kuongea na Vicky pale nje kibarazani na nilimuomba akaniitie Mary ili niweze kuongea naye pale nje. Baada ya Vicky kurudi jibu alilonipa ni kuwa amesema anakuja na tukaendelea na story pale. Ilipita dakika 15 Mary hajatokea, nikawaza huenda atakuwa kachukia tena na kitendo cha kwenda na Iryn pale ndo nimeongeza petrol kwenye moto.

Vicky naye alihisi something fishy kinaendelea kati yetu hasa kitendo cha Mary kutokuja pale nje na alianza maswali kama kawaida yake, lakini sikumwambia chochote na nilirudi ndani.

Baada ya kurudi seblen Iryn alikuwa bado kamshika mtoto, na mimi niliishia kumpiga madongo pale na nikaanza kuongea na Jane. Haikuchukua dakika 5 Mary alisimama na best yake na wakamuaga Jane kuwa wanaondoka, lakini ilikuwa tofauti kwangu, hakunisemesha wala nini na wakaondoka.

Iryn aliusoma mchezo mzima unaondelea pale lakini niliishiwa kupigwa jicho, lakini kwa upande wa Jane yeye alinyamaza kimya maana ndo masta plan.

Tulitumia kama masaa 2 pale kwa Jane, na kabla ya kuondoka Iryn alimuomba Jane ampe Bank account No. ili amtumie pesa ya zawadi ya mtoto. Jane alitusindikiza mpaka nje, Iryn ndo alikuwa wakwanza kuingia kwa gari na sisi tuliendelea kuongea.

Mchezo mzima uliofanyika pale seblen Jane aliuona na alinambia next time tutakayo onana itabidi tukae chini tuongee. Maana stage aliyofikia Mary ni mbaya zaidi hivyo hatuna budi ya kumaliza tofauti zetu, ukitegemea sisi ni zaidi ya ndugu kwake.

Niliagana na Jane na yeye aliishia kumsifia Iryn pale na ile kuingia kwa gari maswali yalianza,

IRYN: “Darling! Kwanini yule dada hajakuaga wakati anaondoka pale kwa Jane?”

Lilikuwa ni trick question kwangu na sikuwa natarajia kuulizwa swali kama hili muda huu, na sikujua najibu nini.

MIMI: “Baby kwanini unauliza hivyo?”

IRYN: “I know yule ni dada yake na yule girlfriend wako, lakini kitendo cha kuondoka bila kukuaga kinatia maswali. What the f*ck is really going on?.”

MIMI: “Baby sikia toka niachane na mdogo wake hatukuwahi kuonana na leo imekuwa surprise. Reason ya kutoniaga sidhani kama ni big topic ya kudiscuss hapa.”

IRYN: “Doesn’t make sense to me! Insider mimi sio mtoto wa kudanganywa na kwa jinsi nilivyomuona kuna something kinaendelea kati yenu, huu ni ukweli ambao huwezi kuukubali. “

MIMI: “Maybe hajapenda mimi kuachana na mdogo wake you never know.”

IRYN: “Anyway tuachane na haya, now nakwenda kuonana na mama J. Tupitie supermarket ili ninue na vitu vya kupeleka, then ninunue na zawadi kwaajili ya Junior.”

Tulikwenda Shopperz ya pale Mbezi Beach kwaajili ya shopping na alinunua mazaga kibao ya kupeleka. Hatukutumia muda mrefu sana na tuliondoka, baada ya kuwasili Rainbow nilipark gari pale GBP na nilifanya kurequest usafiri wa kumpeleka home. Uber ilikuwa imeshasogea pale, hivyo tuliagana na mimi niliondoka kwenda Mikocheni Triple 7 kumsubiri maeneo yale.

Mida ya saa 11 jioni nilipata ujumbe kutoka kwa Iryn kupitia whatsapp na baada ya kufungua alikuwa kanitumia picha ambayo iliwaonesha akiwa na mama J pamoja na Junior. Mimi nilifurahi sana kuona wake zangu wanafuraha na wakati nikiendelea kuizoom ile picha, alituma text kuuliza niko wapi? Na chap nilimwambia nilipo.

Saa 12 jioni Iryn alikuwa kawasili pale Triple 7 na tulianza safari ya kwenda Masaki Coral beach Hotel. Kipindi tuko njiani alikuwa ananipa mrejesho wa kilichokuwa kianendelea kule home na alisema mama J kafurahi sana na mimi nilimuuliza ataondoka lini?.

MIMI: “Baby hujanambia unaondoka lini?”

IRYN: “Niliplan kuondoka kesho but nitaondoka jumatano. Nataka kesho tukawasalimie team yangu.”

MIMI: “What? Mama J hawezi nielewa kabisa na leo akiona kimya ataanza kusumbua.”

IRYN: “Darling unatakiwa ujue mimi pia nina haki ya kuwa na wewe maana ushakuwa baba mtoto kwangu kama mama J. Kama hutaki niendelee kuwa hapa Dar nambie niondoke but sitaki uanze kunipa masharti utafikiri mimi sina umuhimu kwako.”

MIMI: “Baby sijamaanisha hivyo, kwanza tambua umekuja bila taarifa na hapa umekosea sana, pia mazingira yangu unayajua vizuri.”

IRYN: “I told you before nikitoka France nitapitia Tanzania for you au umesahau?. Na kesho tutakwenda wote kumsalimia mama na utakaa na mimi mpaka naondoka.”

Bhasi ilibidi niwe mpole tu maana sikuwa na jinsi na niliamua kunyamaza kimya na muda huu alianza kunichezea ndevu taratibu.

Break yangu ilikuwa Coral Beach hotel na nilishangaa sana kumuona rafiki yake Claire akitusubiri pale. Kwangu mimi sijukua kama tungeonana naye na Iryn alinambia alimpa taarifa best yake ya kukutana hapa.

Claire baada ya kumwona Iryn alikuja spidi wakakumbatiana na muda huu mimi nilikuwa kama mpenzi mtizamaji. Baada ya kumalizana na Iryn, Claire alisogea kwangu na tukasalimiana na tukaondoka kwenda kukaa usawa wa beach.

Claire na Iryn walionekana kumisiana sana maana hata baada ya kukaa pale waliendelea na story na nilitega sikio vizuri baada ya Claire kumuuliza Iryn kuhusu maendeleo ya mimba. Nilikuwa nataka kusikia Claire akiongea nini, lakini nilijua hawezi kuwa huru kama mimi nikiendelea kuwepo pale. Niliwaza niweke voice record afu niage nakwenda washroom na simu nitaiacha mezani ili niwape uhuru wa kuongea.

Nilikuwa namwona Claire kama ni snitch kwangu, hivyo ilibidi nitumie mbinu za kijasusi kuwajua maadui zangu. Niliweka simu kwenye voice record na nilimuaga Iryn nakwenda washroom kisha nika-mkiss shavuni. Niliwaacha pale wakiendelea na story na nilikwenda washroom kisha nikazuga kwa dakika 10 ndo nikarudi.

Baada ya kurudi walionekana kucheka na mazungumzo yao yalikuwa ya kawaida, nilichukua simu yangu na ilikuwa bado inarecord, nikaiweka mfukoni. Muda huu Claire alianza utani wake kwangu,

CLAIRE: “Shem unanitupa sana utafikiri huijui apartment yangu?.”

MIMI: “Sijapewa ruhusa ya kuja kwako, soon nikipewa nitakuja shem.”

IRYN: “Claire thubutu, aje kwako kufanya nini?.”

CLAIRE: “Jamani si shem wangu kuna tatizo akija kunipa salamu?.”

IRYN: “Darling na usithubutu kabisa kwenda I said NO.”

Mimi nilinyamaza kimya sikutaka kusema kitu na muda huu nilikuwa busy na chakula changu.

Saa 4 usiku tuliondoka lakini tulianza kumdrop Claire Mariana apartments na tukaendelea na safari ya kurudi Serena. Wakati tuko Tanzanite Bridge kwa upande mwingine simu yangu ilianza kuita na alikuwa ni mama J akipiga.

“Mama J anapiga lazima anauliza narudi lini.?”

“Pokea msikilize anasemaje.”

Baada ya kuongea na wife ilibidi nimdanganye kuwa nimeshindwa kufanikisha mpaka kesho jumatatu. Wife alinielewa kwa upande wake na muda huu tuliishia kupigana macho na hakuna aliyemsemesha mwenzie mpaka tunafika hotelini.

********
Asubuhi mimi ndo nilikuwa wakwanza kuamka na ilikuwa saa 3 asubuhi tayari, nilimuasha Iryn ili tukaoge then tuondoke, lakini akanambia nisubiri kwanza anamalizia kutype assignment ili asubmit.

Mimi nilitoka kwenda parking kuchukua laptop yangu ili nipitie report za weekend before sijakwenda na Iryn kule ofisini. Sasa baada ya kurudi nilikuta Iryn anaongea na simu, sikumzingatia, sasa ile kusogea ndo naona ni simu yangu.

“Huyu hapa amerudi ngoja nikupe uongee naye.”

Muda huu nilikuwa nimepigwa na butwaa nilijiuliza anaongea na nani huyu mwanamke? Na alinipa simu yangu, ile kuangalia naona ni mama yangu mzazi. Nilimind sana na ilibidi nitoke chumbani ili niweze kuongea na mama,

MIMI: “Mama shikamoo mnaendeleaje huko?”

MAMA: “Tuko salama mwanangu, huyo aliyepokea simu ni nani mwanangu?”

Moyo ulipiga PAAAH! Nikajisemea Iryn kashafunguka nini? Na kama hajafunguka nimjibu nini mama?, niliwaza kwa haraka sana pale.

MIMI: “Mama kwani yeye kajitambulishaje?”

MAMA: “Hamna kapokea simu kanisalimia kwa adabu, akauliza maendeleo yangu na hapa nyumbani, wakati nataka kumuuliza yeye ni nani ndo kunambia wewe umerudi.”

MIMI: “Ooh! Ni bossy wangu mama yule nilokwambia kipindi kile.”

MAMA: “Sawa mwanangu anaonekana ana nidhamu na adabu sana.”

MIMI: “Hana shida kama utawahi kuja utamuona umfahamu pia.”

MAMA: “Mimi nakuja jumamosi hii na harusi itakuwa next week tarehe 10.”

MIMI: “Sawa mama karibu sana, nikukatie tiketi ya ndege au unakuja na bus?”

MAMA: “Mwanangu hiyo hela ya ndege si bora unipe niongezee mtaji kwenye biashara yangu ya kuku?”

MIMI: “Hahahaa mama kupanda ndege sahivi hata maskini tunapanda ni cheap.”

Wakati naendelea kuongea na mama ghafla Iryn alikuja na akanikumbatia kwa nyuma na mikono yake aliizungushia tumboni. Mimi sikutaka kuendelea mazungumzo na mama, hivyo tukaagana pale na nilimgeukia Iryn,

MIMI: “Baby kwanini umepokea simu ya mama? Huoni utaniweka matatizoni kama ataongea na mama J?”

IRYN: “Baby nilitaka kuisikia sauti ya mama, then hata hatujaongea sana na mama. Baby nataka wewe mwenyewe unitambulishe kwa mama mkwe wangu, hiki ni kiumbe chako kina haki ya kumjua bibi yake sawa?”

MIMI: “Sio kwasasa lakini, baadae huko nitakutambulisha taratibu.”

IRYN: “This is for your child not me.”

Iryn alirudi chumbani na mimi niliendelea kubaki pale koridoni na nilianza kuona Iryn anazingua mapema sana, kaanza kusema yeye na mama J ni sawa. Tena anaanza habari za kutaka kutambulishwa kwa mama yangu, yaani daah niliona kadri siku zinavyokwenda na mambo yanazidi kuwa magumu.

Saa 5 asubuhi tuliondoka na kila kitu pale hotelini maana alisema atakwenda kumalizia siku zake pale Coral hotel, Masaki. Tulianza kwanza kwenda ofisi ya masaki na baada ya kufika pale, Hilda ndo alikuwa wa kwanza kumuona Iryn pale reception na wakasalimiana.

Ilikuwa ni surprise maana hatukutoa taarifa ya ujio wake na wakati Hilda akiendelea kushangaa, wafanyakazi wengine walikuwa wamemwona na kelele zilianza na kila kila mtu alitoka pale reception kwaajili ya kumwangalia.

Mimi nilikwenda ndani ofisini, nilimkuta Asmah akiendelea na kazi zake na tukasalimiana pale lakini alionekana kuwa busy, nikaendelea na mambo yangu.

Baada ya dakika 10 Iryn aliingia ofisini na Asmah baada ya kumuona Iryn alishtuka sana maana hakutegema ujio wake kabisa, na Asmah aliniangalia kama mtu ambaye amemind kwanini sijampa taarifa?.

Asmah alionekana kumwogopa sana Iryn na mimi nilikuwa makini sana kumsoma muda huu, Iryn alimsalimia Asmah afu akakaa kwenye coach.

IRYN: “Asmah kipenzi changu habari yako?”

ASMAH: “Safi bossy karibu sana, umeamua kutufanyia surprise.”

IRYN: “Na nitakuwa nawasurprise sana this time.”

Kwa upande wangu niliona ni busara nikaondoka maeneo haya ili niwaache waongee kwa uhuru maana Asmah alikuwa na kesi za kujibu kwa Iryn. Nilitoka nje nikawa napiga story na mlinzi pale getini na baada ya dakika 20 hivi Iryn alitoka na kunipa ishara ya kuondoka.

Safari yetu ilikuwa kwenda Mikocheni na alisema tunavyorudi ndo tutapitia kumsalimia mama Janeth ofisini kwake. Ndani ya muda mfupi tulikuwa pale getini na baada ya kuingia ndani tuliwakuta akina Julieth pale reception na baada ya kumwona Iryn walikuja speed sana kumkumbatia. Kutokana na zile kelele za pale reception haikuchukua muda Lucy naye alitoka na baada ya kumwona Iryn walikumbatiana.

Lucy ndo kipenzi pekee cha Iryn kwa wafanyakazi wote, pia Iryn anawapenda sana wafanyakazi wa Mikocheni kuliko Masaki. Iryn aliendelea kupiga nao story pale na mimi niliingia ndani ofisini, haikuchukua muda Lucy akaja,

LUCY: “Insider unatabia mbaya sana, hivi kwanini hujanambia kama Iryn karudi?”

MIMI: “Hata mimi hakunambia na mimi nikaamua nisiwambie.”

LUCY: “Unatabia mbaya sana, amezidi kuwa mzuri sana wifi yangu.”

MIMI: “Usifananishe South na Dar mama, Dar chafuchafu hii.”

Na muda huu Iryn aliingia tukaanza kupiga story kwa pamoja pale na baadae alisema tutoke na team yote tukapate lunch ya pamoja pale Golden fork.

Baada ya kupata lunch ya pamoja tuliwaaga na tukaondoka kurudi tena Masaki na tulianza kwanza kupitia ofisi ya mama Janeth. Baada ya kufika pale getini kama unavyojua ile ni organization kubwa hivyo ukaguzi wake huwa mkubwa sana.

Iryn alijitambulisha na uzuri wanamjua hivyo tuliruhusiwa kuingia ndani. Tulikwenda moja kwa moja mpaka pale reception na Iryn aliomba kuonana na mama. Japo alimwambia dada asimwambia mama kama ni yeye maana anataka kumsurprise.

Ilimchukua dakika 20 mama kutoka na hakuamini kumuona Iryn pale ofisini na waliishia kukumbatiana kwa furaha sana. Mama alikaa chini na tukaanza kupiga story na alisema kesho ataondoka kwenda USA. Iryn alimwambia kafikia Coral hotel na badae atakwenda kumsalimia akirudi toka kazini, japo mama hakupenda kuona Iryn kafikia hotelini.

Baada ya kuagana na mama tuliondoka kwenda hotelini maana Iryn alionekana kuchoka sana. Baada ya kuwasili pale hotelini tulipelekwa mpaka kwenye room yetu. Nilimuacha Iryn apumzike na nilikwenda kuangalia Worldcup Samakisamaki na nilikutana na yule Jamaa ambaye mara ya mwisho tulikuwa pamoja kwenye game ya Ufaransa. (Huyu jamaa tumuite Allan).

Hii siku niliweza kumjua Allan vizuri na alinambia yeye ni Auditor na anafanyia kazi moja ya Auditing firm kubwa hapa nchini. Tuliongea mambo mengi sana kuhusu uhasibu na alinishauri sana nifanye mitihani ya CPA kama muda ninapata na atanisaidia sana kwa hili.

Mida ya saa 1 usiku Iryn alinipigia simu kuuliza niliko maana alikuwa hanioni, nilimwambia naangalia match Samakisamaki. Na akanambia anakwenda kumsalimia mama Janeth kwake, then anavyotoka atanambia nikamchukue. Muda huuhuu niliwasiliana na mama J na nilimwambia nitarudi home jumatano mchana kwani mambo hayajakwenda vizuri bado.

Mida ya saa 2 za usiku alinipigia simu kunipa taarifa nikamchukue ili turudi wote hotelini. Nilimuaga Allan then nikaondoka kwenda kumfuata pale kwa mama. Baada ya kufunguliwa gate kwa mbali niliwaona wamesimama wakiongea na mimi baada ya kushuka nilikwenda nikamsalimia mama.

Mama Janeth alimsisitiza Iryn suala la kuanza mchakato wa kuandaa Financial statements mapema. Kwa upande mwingine mama aliniaga anaondoka kwenda USA na alisema atachelewa kurudi, pia alinikumbushia suala la kumsaidia usafiri yule mgeni wake.

Iryn aliagana na mama yake kwa kukumbatiana na sisi tukaondoka maeneo haya kurudi hotelini. Iryn aliniomba tukifika hotelini twende swimming pool kwani amemiss sana kuswim na angependa twende wote, ofcourse anajua mimi sio mpenzi na haya mambo.

Baada ya kuwasili tulikwenda room kubadilika chap na tukaenda swimming maana Iryn anapenda sana kuswim na yuko vizuri. Kwangu mimi nilitamani sana kujua mipango yake hasa baada ya kumaliza chuo na nilitamani kujua ataishi wapi?. Yeye kwa upande wake alinambia angependa sana kuishi Ufaransa na watoto kwa hapo baadae ila kipindi hiki ataendelea kuishi na mzee wake.

MIMI: “Baby siku ambayo mama Janeth atagundua huo ujauzito ni wangu unafikiri itakuwaje? Si atanichukia sana?”

IRYN: “Why akuchukie? Wewe ndo uliyeni-force mimi nibebe hii mimba?. Insider embu jiamini, pia tambua kwenye hii Dunia huwezi pendwa na kila mtu.”

MIMI: “What do you mean?”

IRYN: “Wewe unamuona mama kama mtu mkamilifu sana lakini leo nakwambia ukweli kuhusu yeye. Nitashangaa sana kuona kama atakuchukia kwa hili wakati hata yeye amefanya haya, sidhani kama atakuwa na hii jeuri otherwise awe anakupenda.”

MIMI: “Baby ujue sikuelewi haya unayoongea ni nini ambacho kinaendeelea?”

IRYN: “Mama ana watoto watatu lakini kila mtoto ana baba yake. Na yule mtoto wa mwisho wa mama (Smith)ni mdogo wangu wa damu kabisa…”

Na nilimkatisha maongezi yake,

MIMI: “What? Babe sikuelewi ujue kwamba Mama Janeth kazaa na Baba yako?”

IRYN: “Insider hivi huoni Smith kafanana sana na Baba yangu Mzazi?”

CHAPTER 7
 
Back
Top Bottom