Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 02
EPISODE 21:

“BY INSIDER MAN”

ILIKOISHIA:
Kwa lile tukio hata Hilda alibaki anashangaa maana hakutegemea kuona mama akinifanyia vile, ukizingatia mimi ni mtu ambaye ananikubali na kuniamini, ukweli nilijisikia vibaya sana baada ya hili tukio…..

ENDELEA:

Hilda uvumilivu ulimshida na alianza kuniuliza pale shida ni nini? Mbona kama mama anaonekana hayuko sawa toka anione na walikuwa wakiongea vizuri tu?

HILDA: “Insider what’s is really going on? Mbona mama kabadilika ghafla?”

MIMI: “Hata sijui labda kuna kitu nitakuwa nimezingua, acha niende ndani nikaongee nae.”

HILDA: “No usiende hayuko sawa, wewe mtafute private muongee hapa ni ofisini inaweza leta matatizo, cha kukushauri wewe ondoka.”

Niliwaza kwa sekunde kadhaa nikaona Hilda yuko sawa, cha kufanya nimtafute mama private ili tuongee. Ofcourse nilikuwa nishajua tatizo ni nini na hapa nikaanza kumblame Iryn maana tangu muda mrefu nilikuwa namsisitiza aongee na mama kabla mambo hayajaharibika.

Niliondoka kurudi tena kwa Allen na muda wote ambao niko njiani nilikuwa nawaza kuhusu mama Janeth maana alionekana kunichukia sana. Sasa, kumpigia simu Iryn sikuwa na nguvu sababu alikuwa kaniblock, palepale nilipata wazo niende kwa Sumaiya nikaongee nae maana yeye na mama ndo zinaiva sana.

Nilipiga U-turn nikaanza safari ya kwenda kwa Sumaiya afu hata sikumpigia simu na baada ya kuwasili ofisini kwake nilitulia parking, nilimpigia simu akanambia nimsubiria soon atakuwa kafika. Baada ya dakika 10 Sumaiya alikuja na alikaa siti ya mbele, kama kawaida yake alianza kunifanyia vituko vyake, lakini mimi mawazo yangu yalikuwa mbali sana, hata yeye alihisi something wrong;

SUMAIYA: “Insider upo sawa? Sijakuzoea hivi.”

MIMI: “Sumaiya nimeharibu tayari sijui hata mama atanielewaje kwahili.”

SUMAIYA: “Mama Janeth huyuhuyu?”

MIMI: “Ndio mshikaji wangu yaani daah!”

SUMAIYA: “Kwani amejua unatoka kimahusiano na binti yake? ila hata kama akijua shida ni nini? Au anataka umkaze na yeye?”

MIMI: “Hivi kuna jambo lolote Iryn kakwambia kuhusu yeye?.”

SUMAIYA: “Hapana ni muda hatujawa intouched, embu niambie ni nini kinaendelea kati yako na mama?”

Nilijifikiria pale nikaona acha nimwambie kinachoendelea hakuna haja ya kumficha,

MIMI: “Sikia, Iryn ni mjamzito ana mimba yangu ina miezi 4 sasa…”

Alinikatisha maongezi yangu,

SUMAIYA: “Wewee usinambie! Hapa sasa nakupa nyota zote umecheza kama Messi, yaani usingempa mimba ningekulaumu sana.”

MIMI: “Sijamaliza kuongea, hapa unavyoniona nina mke na mtoto, sikuwahi kukwambia hii kitu.”

SUMAIYA: “Wee Insider una mke toka lini?.”

MIMI: “Kitambo sana na mtoto anafukuzia miaka 2.”

SUMAIYA: “Duuh! Unasiri sana Insider kumbe ulikuwa unanichora tu, kwanini hukunambia?.”

MIMI: “Hata ningekwambia ingekusaidia nini?.”

SUMAIYA: “So, Iryn anafahamu kuwa una mke?”

MIMI: “Anafahamu na alibeba mimba kwa ridhaa yake.”

SUMAIYA: “Aisee upo vizuri, nyota yako ni international.”

MIMI: “Mama anajua kinachoendelea ndomana amenichukia ghafla, na kibaya zaidi anajua mimi nina mke na mtoto, hili pia limechangia mama kunichukia, ukizingatia alishawahi kuniuliza kuhusu mahusiano yangu na Iryn.”

SUMAIYA: “Hapo kweli pagumu na mama anavyompenda Iryn lazima akuchukie kwa hili, Kuna jambo pia nafikiri hulifahamu hata Iryn pia halijui ila mimi najua.”

MIMI: “Ni jambo gani hilo tena?”

SUMAIYA: “Insider hii ishu nakwambia ila naomba ufunge mdomo wako usije kujaribu kuropoka kwa Iryn, nakwambia iwe siri yako na nina kuamini.”

MIMI: “Usiwe na wasiwasi you have my word.”

SUMAIYA: “Yule Smith mtoto wa mwisho wa mama ni mdogo wake Iryn, mama kazaa na baba yake.”

Mimi nilikuwa najua kuhusu hii ishu kupitia Iryn mwenyewe, lakini bado alisema anaendelea na uchuguzi, sasa kusikia Sumaiya naye anajua kila kitu, bhasi nilijisemea Sumaiya atakuwa anajua siri nyingi sana, mimi nilijifanya sijui kinachoendelea;

MIMI: “Umejuaje hili? Mbona kama siamini amini.”

SUMAIYA: “Ndo uniamini sasa, mama na baba Iryn wanamahusiano ya siri sana na mama anakwenda sana South Africa, hata juzi kati kabla ya kurudi alikuwa huko kupewa dudu.”

MIMI: “Wewe ulijuaje Smith ni mdogo wa Iryn?”

SUMAIYA: “Mama mwenyewe aliniambia, ndomana unaona anampenda sana Iryn sababu ya hii.”

MIMI: “So mama Janeth alikuwa anamzunguka mama yake Iryn kwa kutembea na mume wake sindio?”

SUMAIYA: “Insider haya mambo mengine sisi hayatuhusu, tujadili jambo lako uliloweka mezani.”

MIMI: “Embu nipe mawazo nini nifanye? Kidogo wewe una mazoea na mama unajua namna ya kumuingia na kutoka, nisaidie kwa hili, lengo langu tuongee tuliweke sawa hili.”

SUMAIYA: “Insider huna haja ya kuhangaika kwa hili, Master ni Iryn ndo anatakiwa aliweke sawa hili, wewe hata usihangaike, mama atakaa sawa tu hata usijipe stress, wewe fanya yako hata usiwaze kuhusu yeye.”

MIMI: “Sometimes ni bora ukajifanya mjinga ili mambo yaende, mimi lengo langu niliweke sawa hili jambo, kwahiyo unanishaurije?”

SUMAIYA: “Wewe tulia hayo ni mambo ya familia waachie wao, the truth is, she can’t hate you forever, wewe ni mkwe tayari atake asitake, mama nae uchi wa Iryn afu yeye anaumia.”

Akaanza kucheka pale,

MIMI: “Nawaza mpaka kuacha kazi ujue, sitoweza kufanya kazi kwa mazingira kama haya.”

SUMAIYA: “Acha ufala wewe, upo kwaajili ya mama au Iryn? Yaani uache kumsaidia mke wako kisa mama? Acha ujinga Insider, Iryn anakutegemea usifanye maamuzi ya kijinga, kwanza mama ataona umemwogopa, wewe fanya yako.”

MIMI: “Sawa bhana kumbe unaweza kumshauri mtu, ukiwa serious unakuwa na akili nzuri.”

SUMAIYA: “Leo unanipa gari yangu, najiona niko vizuri kuingia road.”

MIMI: “Nilitaka nikuwekee android TV ni vile nimekuwa na mambo mengi, kama unaharaka nayo ichukue.”

SUMAIYA: “Kwahiyo unataka kunipa lini?”

MIMI: “Ijumaa na leseni yako itakuwa tayari ili nikupe vyote kwa pamoja.”

SUMAIYA: “Sawa, ila unanipeleka home.”

MIMI: “Sawa haina shida, ila ndani sitaingia naishia nje tu”

SUMAIYA: “Haya baba twende.

Nilimpeleka Sumaiya kwake na muda ambao ninarudi home nilikuwa nawaza kuhusu mama Janeth pamoja na maneno aliyokuwa anaongea Sumaiya, niliwaza huenda anajua siri nyingi sana, hivyo itabidi nianze kumchimba taratibu.

Kwenye hili suala lawama zangu zote zilikuwa kwa Iryn maana alipaswa kumwambia mama hili jambo mapema sana, lakini alikuwa anasuasua mpaka mama amefahamu. Jambo lingine lililokuwa linaniumiza kichwa ni vile Iryn kuninunia afu nashindwa kuwasiliana nae ili tuyaweke mambo sawa.

Kwa upande mwingine allen alinitafuta kuniuliza kama narudi tena tuendelee na topic yetu maana nilikuwa nimemuaga kwa kumpa ahadi ya kurudi tena, nilimwomba kumtafuta kesho ili tumalize maongezi yetu.

Baada ya kurudi home nilikwenda chumbani kuoga na nilimkuta Junior akichezea simu ya mama yake, nikapata wazo la kuipekua simu yake, kimbembe Junior alikuwa hataki kunipa simu, kila nikitaka kuchukua alikuwa analia. Palepale nikapata wazo nimuwekee cartoon kwenye PC ili atoe simu, na nilifanya hivo plan yangu ikawa imetiki.

Nilianza kuipekua simu upande wa whatsapp na nilianza direct kutafuta chats zake na Iryn, lakini hakukuwa na chats zozote walizochat hivi karibuni, na niliendelea kuangalia chats zingine na nilibaini kuna Mafisi wanamtongoza sana, nikapotezea. Niliona chats za dada yake na nilifungua ili nisome chats zao, baada ya kufungua niliweza kugundua kwamba dada yake ndo anayemkomalia wife kuhusu mimi na Iryn kuwa na mahusiano, na mbaya zaidi alikuwa anamwambia afanye investigation ya ukaribu wetu.

Wife kwa upande wake alikuwa amemwambia dada yake kuhusu ujio wa Iryn pale home ile usiku na kuhusu mapenzi yake kwa Junior, dada yake alikuwa anakamia sana mimi na Iryn tuko kwa mahusiano. Alikuwa anamwambia mdogo wake aendelee kuwa karibu na Iryn maana yeye ndo rahisi kumchunguza na kujua ukweli, mbaya zaidi alimwambia itabidi waonane kwa maongezi zaidi.

Baada ya kusoma hizi chats zao hapa sasa nikajua tatizo sio mama J bali ni dada yake ambaye anasmell something fishy kati yangu na Iryn. Nilijisemea nitakuwa makini sana kuanzia kwenye simu yangu hasa kwenye chats zangu na Iryn, niliona niko vitani hivyo natakiwa kuwa makini sana kwa kipindi hiki.

Baada ya dakika 15 nilimsikia wife akija chumbani na alikuwa akimuita Junior;

“Junior nipe simu yangu nimpigie bibi.”

Na ile kuingia chumbani anatuona tuko busy na cartoon, akachukua simu yake akaondoka.

Muda huu nilipata wazo la kumcheki Iryn ili tuongee lakini alikuwa bado kaniwekea tofali. Niliwaza pale labda nimcheki kwa namba nyingine ili tuongee huenda ikasaidia, lakini niliona nitakuwa kama najimbeleza kwake, cha msingi nipotezee, kwa upande mwingine yale maneno ya kaka Allen yalikuwa yananipa jeuri na kiburi.

Kesho yake niliwahi sana kwenda Masaki na kipindi niko ofisini nilibaini Iryn bado hajaingiza mishahara kwa wafanyakazi maana yeye ndo huwa anahusika, sasa tumeanza mwezi mpya february afu hajafanya chochote niliona anazingua.

Nilimtumia mail kumkumbusha hili suala maana ni muhimu na mimi niliendelea kuandaa ripoti zingine, niliendelea kuwaza namna ugumu wa kazi unavyokuwa hasa ukichanganya mapenzi na kazi. Suluhisho na kuepusha matatizo kama haya niliona ni bora nika quit sababu vitu binafsi vina impact mpaka utendaji wa kampuni.

Baada ya nusu saa Hilda aliwasili ofisini huku kavaa skirt fupi sana kiasi kwamba ilikuwa ikimchora barabara. Mimi baada ya kumuona vile nilijifanya niko busy na kazi zangu na sikutaka kuongea chochote, ila yeye ndo alinza kunisalimia na akakaa kwenye sofa;

HILDA: “Insider tangu jana nafikiria kuhusu mama mkwe wako.”

Niliona Hilda ameanza kuvuka mipaka, niliona ameanza kufuatilia mambo yasiyo mhusu,

MIMI: “Ulikuwa unafikiria nini?”

HILDA: “Au hajapenda kumuona Iryn vile, afu na wewe ndo mhusika?”

MIMI: “I don’t know, ikifika muda kila kitu kitakuwa wazi.”

HILDA: “Jana nimekutumia ripoti ya mwezi, stock imeisha sidhani kama itaweza kusurvive muda mrefu.”

MIMI: “Stock haina shida kuna mzigo soon utakuwa bandarini, mimi natoka mara moja soon narudi.”

HILDA: “Sawa uwahi kurudi ili twende lunch.”

MIMI: “Leo nipo na wewe mpaka jioni sema ulivyovaa hivo utanifanya niingie matatizoni.”

Hilda aliishia kutabasam na niliondoka kwenda kuonana na Allen ofisini kwake ili tumalizie maongezi yetu.

Nilitumia muda mfupi sana kuwasili pale kwenye kampuni yao na nilikwenda moja kwa moja ofisini kwake nikaambiwa yuko kwenye kikao. Nilimtumia ujumbe kumpa taarifa na akanambia tuoanane mchana muda wa lunch kuanzia saa 7 mchan ili tuongee vizuri, na mimi kuondoka kurudi ofisini.

Kabla ya kurudi ofisini nilipitia shoppers kununua mazaga ya kupeleka ofisini kwaajili ya sisi na wateja kama maji ya kunywa, juice, soda na bites. Kipindi nanunua vitu simu yangu ilianza kuita na alikuwa ni Mary akinipigia na nilipokea kwa haraka sana;

MIMI: “Hi Mary.”

MARY: “Hi Insider za wewe?”

MIMI: “Salama mummy, nimefurahi kusikia sauti yako hata sikutegemea.”

MARY: “Ahsante sana dear, nilikuwa nakusalimia tu.”

MIMI: “Thank you, unasomeka pande zipi?”

MARY: “Niko Posta ofisini kwa mama but I won’t be here for too long.”

MIMI: “Karibu Masaki upajue ofisini kwangu.”

MARY: “Thank you leo nitakuja, navyotoka huku nitakujulisha.”

MIMI: “Karibu sana Mary.”

Saa sita na nusu Allen alinipigia simu ili tuoane kwaajili ya mazungumzo na tulikubaliana tukutane pale Salt restaurant. Sikutaka kupoteza muda na niliondoka kwenda eneo la tukio na yeye alikuwa ameshafika tayari na tulisalimiana tukaanza story;

ALLEN: “Bro sorry sana nilikuwa nina kikao afu sikutegemea kama ungekuja asubuhi.”

MIMI: “Usijali mimi ndo nilizingua nilipaswa kukupa taarifa mapema.”

ALLEN: “Mama kijacho anaendeleaje?”

MIMI: “Hakuna lolote kutoka kwake anajiandaa na mitihani kwasasa. Tuendelee na topic yetu ya jana maana tulizungumza vingi lakini hatukamaliza.”

ALLEN: “Ni sawa kabisa ila leo tutakuwa na solution ya hili jambo, usiwe na wasiwasi.”

MIMI: “Toka jana tuongee kidogo naona mabadiliko, ila kaka kuna jambo inatakiwa ujue, hata kama tukisubiri Iryn ajifungue ndo twende, bado mimi siwezi kumuoa unafikiri wazazi watakubali?”

ALLEN: “Una uhakika hutakuja kumuoa Iryn?”

MIMI: “Ndio siwezi kumuoa, yeye ni kama mchepuko kwangu na anajua hili.”

ALLEN: “Our future is an uncertainty, you never know, kinachomtofautisha Iryn na mama J ni kutambulika kwa wazazi na vile umemlipia mahali, lakini vingine vyote wako sawa na huyu soon atakuwa na mtoto wako.”

MIMI: “Upo sahihi lakini sasa…”

Alinikatisha maongezi yangu,

ALLEN: “Bado sijamaliza ipo hivi, mimi naona ni busara Iryn akaongea ukweli huko kwao kuhusu wewe kuwa una mke na mtoto, na ameridhia kuwa mke mdogo kwa hiyari yake.”

MIMI: “Kaka huoni kama nitaweza kukosa mtoto kizembe wakijua ukweli?”

ALLEN: “Toka jana nakwambia kuhusu hili, mwenye maamuzi na hii mimba ni dada mwenyewe na sio wazazi au sisi, yeye akisema ninazaa na kweli atazaa huna haja ya kuwa na wasiwasi.”

MIMI: “Sidhani kama atakuwa tayari kuwaambia wazazi hivyo, hawezi kubali anaweza kutengwa na ukoo.”

ALLEN: “Sasa ni bora kuwa wakweli kuhusu hili au tudanganye? Na kama tukiwaambia tutamuoa kumbuka tutakuwa tumeshaingia kwenye makubaliaono ya wazazi na tusipofanya hivyo tutakuwa matatizoni, kama unaona ni sawa kuwadanganya niko tayari kukupa kampani mpaka Ethiopia.”

MIMI: “Hapana naona option ya pili imekaa kimkakati sana ila kuna possibility ya kumkosa mtoto au hata akizaliwa akapewa ukoo wa kwao.”

ALLEN: “Haiwezekani huyo mtoto ni wako na sifikirii kama mama yake atakuwa tayari kukuweka mbali na mwanao, never. Hili suala wa kulimaliza ni Iryn mwenyewe wala sio sisi ni mwenyewe akae na familia yake awaambie ukweli kuhusu wewe na maridhio yake.”

MIMI: “Kaka usije ukanijaza kichwa afu mambo yakaenda viceversa maana sitaki kumpoteza huyu mtoto.”

ALLEN: “Na ukionesha weakness ya uhitaji sana wa mtoto ndo utampoteza sasa, just kuwa normal usioneshe wenge lolote.”

MIMI: “Duuh sawa bro nashukuru kwa mawazo yako.”

Wakati tunaendelea na mazungumzo Mary alipiga simu kunipa taarifa anatoka Posta hivyo nimuelekeze ofisi ilipo ili aje na mimi nilimwambia aje Salt atanikuta hapa, alisema haijui ilipo nimtumie location, nikamwambia akifika Cocobeach anipigie nimuelekeze.

Ndani ya dakika 30 alinipigia kunipa taarifa anakaribia na nikamueleekeza mpaka anafika na kwa mbali nilimuona akishuka kwa Vanguard, alikuwa amependeza sana na alizidi kuonekana ni mrembo sana.

Aliingia ndani akaja usawa wetu na tulianza kusalimiana pale na nilimtambulisha kwa Allen na story zingine zikaendelea;

MIMI: “Nambie mummy, mama mkwe hajambo?”

MARY: “Afu anakuulizia sana na mbaya zaidi Prisca anakosaga majibu ya kutoa.”

MIMI: “Hahahaa, msalimie sana, kumbe unajua kudrive ndinga nilikuwa sijui.”

MARY: “Yeah kimtindo kama hivi.”

MIMI: “Agiza food ule ili tuondoke najua hujala.”

Allen aliniaga anawahi ofisini na niliendelea kubaki pale na Mary nikimsubiri amalize kula, na baada ya kumaliza tuliondoka kwenda ofisini.

Baada ya kufika ofisini nilimpeleka moja kwa moja mpaka show room ili aangalie mawigi, kwa upande wake alionekana kuyapenda na alikuwa akishangaa bei zake,

MARY: “Insider wigs ni nzuri ila kwa hizi bei hapana mimi siwezi.”

MIMI: “Wig la gharama kuvaa ni bei gani?”

MARY: “Nakumbuka laki 5 na mama ndo alinunuliaga, hii Lace nimeipenda kwakweli niambie sifa zake.”

MIMI: “Huku sasa mimi ndo sijui ngoja nikuitie mtaalamu wa hizi kitu akuelekeze.”

Nilimuita Winny ili amuelekeze Mary kwa sifa za wigi ambazo atahitaji maelekezo;

WINNY: “Mrembo hio ni frontal lace natural hair black kutoka France, hio ni mkataba utavaa mpaka uichoke, haipukutishi na ni laini kama unavyoiona. Ukinunua hio wigi utapewa wig cap, brush, shampoo, sprays, gels na wig stand, bado una offa ya kuja hapa kusetiwa free mara 3.”

MARY: “Wow amazing, Insider hii wigi nimeipenda kwakweli ila sasa milion 2 ninatolea wapi?”

MIMI: “Kama umeipenda, nakupa offa ichukue kama zawadi yangu kwako, umenifanyia mambo mengi sana hio ni shukrani yangu.”

MARY: “Thank you Insider.”

Winny alishangaa sana kuona nampa Mary ofa ya wigi na nilimwambia yeye ndo atakaye mhudumia Mary. Mary alisema atakuja jumamosi kwaajili ya kuweka wigi na tuliondoka tukaenda ofisini kuendelea na mazungumzo.

MARY: “Insider Salon yenu ni international sijaona Salon hapa Dar ya kushindana na nyie.”

MIMI: “Ofcourse hata wateja wetu alimia 95 ni foreigners, naona unazidi kuwa mrembo nipe siri ya mafanikio.”

MARY: “Nakula vizuri, nalala kwa wakati, sina stress kwanini nisiwe mzuri?”

MIMI: “Hahahaaa hata mimi naona sio kwa kung’aa huko mpaka unafanya mapigo ya moyo wangu yaongezeke spidi.”

MARY: “Mhhh! Prisca mnawasiliana?”

MIMI: “Yeah tuko intouched ila sio sana, nafurahi kuona amemove on.”

MARY: “How did you know?”

MIMI: “I know na ni jambo zuri, tuachane na haya yalishapita, vipi kuhusu wewe usinambie bado upo single sitokuelewa.”

MARY: “Bado niko sokoni, soko gumu sana huku nje..”

Tulianza kucheka wote pale na aliendelea kuongea;

“Insider kuna kitu nataka kushare na wewe, nimepata kazi Posta, kuna kampuni nitakuwa nafanya nayo kazi but nataka nitafute apartment karibu.”

MIMI: “Unataka kuondoka home? Kwamba utashindwa kuamka mapema uwahi kazini?.”

MARY: “Si unajua nasoma pia, bado research na muda mwingi nitakuwa nashinda library, pia nimekuwa mtu mzima nahitaji kukua.”

MIMI: “Mimi sikushauri uhame home, unataka majukumu ya nini mapema hivi? Hizo pesa za kodi si bora uziweke zije zikusaidie hapo baadae?”

MARY: “Bhana, wewe na mama lenu moja naye hataki kabisa kusikia hizi habari, but weekend nakuwa narudi home.”

MIMI: “Mmh, wewe fanya kutokana na moyo wako unavyotaka na angalia mipango yako, ukiona kuna haja ya kupanga ni sawa.”

Hilda aliingia ofisini alikuwa lunch na baada ya kumuona Mary walisalimiana, kisha akaanza kunilamikia nimemdanganya kuhusu kwenda kula lunch na mimi nikajitetea nilikuwa na mgeni ndomana nikashindwa.

Mary aliniaga anaondoka kwa ahadi ya kurudi jumamosi kwaajili ya kuweka wigi, na mimi sikuchukua muda nikamuaga Hilda naondoka kwenda Mikocheni kuonana na Lucy. Lengo la kwenda kuonana na Lucy ni sakata la Landlord na niliona ni busara tukaonana face to face kuliko kuongea kwa simu.

Baada ya kuwasili Mikocheni ofisini nilionana na Lucy tukaanza mazungumzo na kubwa alisema ameongea na Iryn ila yuko kwenye maandalizi ya mitihani hivyo mpaka weekend ndo watapanga vizuri.

MIMI: “Unajua Iryn kaniblock.”

LUCY: “Uliniambia, si hutaki nikumbelezee unaleta ubeberu shauri zako.”

MIMI: “Shida ukiongea nae atajua mimi nimekwambia kinachoendelea afu yeye mpaka sasa hajakwambia, atleast akufungukie hapo kidogo itakuwa na nguvu.”

LUCY: “Sema mke wako kabadilika sahivi, sijui ndo mimba inamchanganya yaani simuelewi kabisa.”

MIMI: “Afadhali hata wewe umeliona hili maana unaonaga mimi ndo mwenye shida.”

Baada ya maongezi ya muda mfupi nilimuaga Lucy nikaondoka kurudi home mapema kabisa.

Kipindi niko home nilikuwa nikitafakari ushauri wa Allen na niliona yuko sahihi ni bora Iryn akasema ukweli huko kwao kuhusu mimi before it’s too late au wazazi wakajua kupitia mama Janeth.

Usiku Jane alinipigia simu kunipa taarifa kuwa ameanza biashara na nilimuahidi kwenda dukani siku ya kesho na nitashinda siku nzima. Jane alionesha kuwa na furaha sana baada ya kuanza biashara hata mimi kwa upande wangu nilijisikia vizuri sana kuona Jane akiwa na furaha ukizingatia marehemu Pama alinipa task ya kuhakikisha Jane anakuwa salama na mtoto.

Kesho yake nilikwenda dukani kwa Jane kama nilivyokuwa nimemuahidi ili kuona maendeleo kwa ujumla, duka lilikuwa limejaa sana na lilionekana kupendeza sana, wateja nao hawakuwa mbali walikuwa wanakuja kwa wingi.

Nilishinda siku 2 mfululizo dukani na nilikuwa nikisaidiana kazi na dada ambaye alimtoa home na kumleta dukani sababu alikuwa anamuamini, Jane alikuwa anakuja pale shop na kuondoka maana asingeweza kumwacha mtoto home.
******

Jumamosi nikiwa ofisini nilipata wazo nimpigie simu mama niombe kuonana nae ili tuzungumze, nilipiga simu mara 2 bila majibu na niliamua kumtumia ujumbe ambao niliandika kuomba kuonana nae kwaajili ya mazungumzo, lakini sikujibiwa ni kama vile hakuiona message yangu.

Nilikumbuka maneno ya Sumaiya nikaona alikuwa sahihi kusema haya mambo ni ya familia, hivyo niwaachie wao wenyewe wayamalize na nikiendelea kujibembeleza nitapoteza thamani yangu. Kwa upande mwingine kuendelea kufanya kazi kwenye mazingira haya niliona nitazidi kuwa kwenye wakati mgumu, ukizingatia sipo kwenye maelewano mazuri na hawa wahusika wakuu, Iryn na mama yake.

Muda huu Mary alinipigia simu kunipa taarifa kuwa yuko njiani anakuja kuweka wigi lake na kufikia saa 7 mchana atakuwa around. Nilimpanga Winny mapema kuhusu ujio wa Mary, nilitaka yeye ndo amuhudumie na sio mtu mwingine.

Saa 7 mchana Mary aliingia na Vanguard pale ofisini na mimi nilitoka kumpokea na tuliishia kukumbatiana, sasa Mary alikuwa katembea na mdogo wake Ivy, ilikuwa ni surprise kwakweli na sikutegemea kabisa.

MIMI: “Karibu sana naona leo umeamua kunisirprise, Ivy hujambo?”

MARY: “Ahsante, ameforce tuje wote ndomana na sijamwambia nakuja kwako.”

IVY: “Sijambo shem tumekumiss, why can't you come home?”

MIMI: “I will come Ivy, today I am happy to see you again."

IVY: “Me too.”

MARY: “Insider utanisaidia kumpeleka Ivy lunch hajala mchana.”

IVY: “I’m not hungry.”

MIMI: “Ivy tutakwenda wote kula sawa?. Mary wewe kaendelee huko ndani dada anakusubiri zoezi lianze.”

Mary alikwenda ndani, tulikaa nje kibarazani tukipiga story na Ivy maana ni muongeaji, huwezi jutia kuwa naye karibu;

MIMI: “Nani alikwambia mimi ni shem kwako?”

IVY: “Dada Prisca told me.”

MIMI: “Niite Uncle Insider sawa eeh?”

IVY: “Sawa uncle.”

MIMI: “Let’s go tukale lunch, unataka kula nini?”

IVY: “Pizza”

Tuliondoka kwenda kula Pizza, muda ambao tuko njiani mama alinipigia simu, habari kubwa alisema anaona kuna jambo linanisumbua akili lakini siko tayari kushare na mtu, aliendelea kunisisitiza kama nipo tayari bhasi nimwambie ili aangalie namna ya kunisaidia hata kimawazo au ushauri.

Kwa upande wangu sikuwa tayari kumwambia mama kuhusu hili jambo na niliendelea kumkatalia kuwa sio kweli na mimi niko sawa, licha ya kutokubaliana na mawazo yangu

Hili jambo siwezi kushare na wazazi kwa kipindi hiki mpaka pale mambo yatakapokuwa sawa ndo nitashare ila kwasasa mtu wa kushare nae ni sister tu.”

Baada ya kuwasili Pizzahut niliagiza pizza medium na nilikwenda kula pizza kwaajili ya kumpa kampani Ivy, haya madude mimi huwa siyapendelei kabisa. Nilipiga slice 2 nikamuachia Ivy aendelee kula, nikatoa simu kumpigia sister ili nimpe taarifa za kwenda Arusha anipe na ratiba zake mapema kabla ya kwenda.

Tulipiga story nyingi sana na sister na tulikubaliana niende Arusha mwezi wa pili mwishoni maana atakuwa likizo, hivyo atakuwa na muda mzuri wa kukaa na mimi mdogo wake.

Kwa upande mwingine Ivy alikuwa amemaliza kula na alimwambia dada afunge slice 2 zilizobaki na alisema kwaajili ya dada yake Mary na tukaondoka kurudi ofisini.

Kufikia saa 10 jioni Mary alikuwa tayari kamaliza kutengenezwa na alipendeza sana mpaka nikajikuta naanza kupagawa, alikuwa kawaka sana kwa jinsi alivyo mzuri by nature na wigi alilokuwa kawekewa plus madikodiko mengine alikuwa bonge la pisi hata yeye aliishia kufurahi tu.

MIMI: ”Umependeza sana yaani umebadilika umekuwa pisi ya kimataifa.”

MARY: “Thank you Insider, ukweli hata mimi najishangaa sipati picha huko home leo na shoga zangu wakiona lazima waulize nilikokwenda.”

MIMI: ”Wewe wakaribishe sana waje hapa.”

MARY: “Insider naenda home kumpeleka Ivy but naomba badae tutoke kama unanafasi please.”

Nilijifikiria kwa sekunde kadhaa nikaona sina ratiba yoyote, acha nikubali ili niendelee kumfurahisha Mary;

MIMI: ”Sawa haina shida, mimi nitabaki nikikusubiri hapa ofisini so utanambia ukiwa tayari.”

MARY: “See you soon, Ivy twende, mwambie Ahsante shem Insider.”

IVY: ”No, he wants me to call him Uncle Insider.”

Mary aliniangalia afu akatabasamu kwa kutingisha kichwa na nilimsindikiza mpaka parking na kabla ya kuingia kwa gari alikuja akanikumbatia na wakaondoka, kugeuka nyuma namuona Winny yuko kibarazani anatabasamu, nilisogea mpaka usawa wake tukaanza story;

MIMI: “Leo umetisha sana itabidi nikupe zawadi.”

WINNY: “Namuona kafurahi mwenyewe hata haamini kama ni yeye, ni nani uyo?”

MIMI: “Huyo alikuwa shem wangu, nilitokaga na mdogo wake but tuna mawasiliano mazuri.”

WINNY: “Insider unapendwa sana na watu, just imagine umeachana na mdogo wake lakini bado mnacheka vizuri, ni wanaume wachache wenye bahati kama yako.”

MIMI: “Winny umeanza kunichokoza.”

Na nilianza kuslap makalio yake akakimbia ndani na mimi nikaenda ofisini na niliamua kumpa Hilda utawala akapumzike na nilimwambia aniachie ofisi na yeye aliishia kufurahi akaondoka.

Nilikaa ofisini mpaka saa 2 za usiku ndo Mary kunipigia simu kunipa taarifa anatoka home anakuja Masaki, nilikuwa nishasahau kama nina miadi ya kukutana na Mary.

Baada ya lisaa aliwasili na tulikutana ofisini nje ya geti alikuwa na Uber, nilimpick tukakubaliana twende Wavuvi Kempu. Baada ya kuwasili eneo la tukio na kushuka hapa sasa ndo namuona Mary vizuri, aisee alikuwa kapendeza sana maana alivaa skin jeans ya light blue ambayo imemkaa vizuri na kiuno kilichoreka na juu alikuwa kavaa top nyeusi iliyoishia chini ya kitovu na glass nyeusi.

Mary kabarikiwa shepu nzuri sana, sasa jinsi alivyokuwa kawaka niliishia kumsifia pale na nilimshika mkono tukazama ndani, tukatafuta sehemu nzuri tukakaa na mhudumu alikuwa tayari kafika kutusikiliza, tukaagiza Hennesy na mixers.

Ndani ya muda mfupi dada alikuwa katuletea kinywaji tukaanza kunywa huku tunapiga story, ofcourse tulikuwa tumemisiana sana maana ni kitambo tulikuwa hatujakaa pamoja.

Story zetu kubwa zilibase kwenye mahusiano na maisha kwa ujumla, Mary kwa upande wake alitaka kujua kama bado nina pasha kiporo na mdogo wake, nilimkatalia katakata.

Tulikuwa deep sana kimaongezi na kadri muda unavyozidi kwenda na pombe kukolea tulianza kuoneshana hisia za kimapenzi waziwazi, kuna muda tulikuwa tunacheza pamoja na kukumbatiana.

Mida ya saa 6 usiku wife alinipigia simu, baada ya kuona ni wife niliwaza haraka nikaona wacha nikapokee simu yake kwenye gari, nisipo-pokea italeta shida, nilimuaga Mary nakwenda washroom lengo nikaongee na wife.

Simu ilikuwa imekata tayari na aliendelea kupiga kwa mara ya pili na baada ya kuingia kwa gari nikapokea na tukaanza mazungumzo;

“Nambie mke wangu hujalala tu?”

“Napataje usingizi na wewe mpaka sasa hujarudi, umepitia wapi?”

Nilipiga hesabu za haraka nikaona acha niwe mkweli,

“Mke wangu siko sawa kabisa nimeona nipitie kunywa ili nikae sawa.”

“Hivi unaakili wewe? Sasa pombe ndo zinakuweka sawa?”

“Nikirudi home makelele si bora ninywe tu.”

“Baba J umekaa chini na mimi kunambia matatizo yako? Nini maana ya kuishi pamoja kama hunambii shida zako? Sijapenda naomba urudi home mapema tuongee, kama huwezi nambie ulipo nikufuate.”

“Haina haja mimi niko sawa na nitarudi home, usiwe na wasiwasi.”

“Haya, sisi tunalala byee, Takecare.”

Baada ya kurudi ndani Mary alianza kulalamika nimemuacha alone, ilibidi nimbembeleze ili atulie na nilimwambia ukweli kwamba nilikuwa naongea na wife.

Mary alikuwa close sana na mimi ‘zero distance’ na tuliendelea kucheza pamoja huku nazungusha mikono kwenye makario yake na yeye alizungusha mikono kwenye kiuno changu. Network yangu ilikuwa ishahama muda mrefu sana na yeye alikuwa kalainika sana, tulikuwa kwenye huba zito sana kiasi kwamba tulianza kupeana makiss bila aibu, licha ya nyomi ya watu iliyokuwepo maeneo haya.

Nilicheki muda simu yangu ilikuwa inaonesha ni saa 7 usiku na madakika, nikamwambia Mary tuondoke akasema sawa. Ile kufika kwenye gari tulianza kuexchange saliva tena kwa fujo kwelikweli na sikuchukua muda nikapandisha mkono kwenye vifuu vyake. Hapa sasa alianza kutoa kelele za nguvu na ile kushusha mkono kwenye bustani yake ilikuwa tapatapa yaani imemwagiliwa vya kutosha na muda huu alikuwa hoi akinitizama tu kwa macho ya kurembua.

Nilimwacha afu nikaanza kujifikiria niondoke naye au nirudi home? Maana kufikia stage hii Mary asingeweza kuwa na jeuri ya kunikazia, kuondoka nae ilikuwa ni lazima 100%.

Wakati naendelea kutafakari, alianza kuongea pale,

“Insider where are you taking me?”

“I don’t know.”


EPISODE 22
COMING SOON:
Baada ya Mary atafuata Hilda na Winny.
 
SEASON 02
CHAPTER 22


PREVIOUS:
Nilimwacha afu nikaanza kujifikiria niondoke naye au nirudi home? Maana kufikia stage hii Mary asingeweza kuwa na jeuri ya kunikazia, kuondoka nae ilikuwa ni lazima 100%.

Wakati naendelea kutafakari, alianza kuongea pale,

“Insider where are you taking me?”

“I don’t know.”

CONTINUE:

“Please take me home.”

“Do you want me to take you home?”

“Yes, please.”

“Ok let’s go.”

Alitaka nimpeleke home na nilianza safari ya kuondoka maeneo haya, sasa wakati tunatoka pale Coco alisogea akanilalia mapajani na alianza kunichezea ndevu zangu, hakuishia hapo alianza kuingiza mkono kwenye kingdom yangu, hapa sasa akaamsha muwashawasha wangu nikawa sina ujanja na ilinibidi nitafute eneo la kupark gari.

Nilikuja kupark gari hapa opposite na Village supermarket kwenye makutano ya Haileselasie na chole road, Uber pia wanapenda sana kupark hapa, bhasi tulianza romance upya maana muda huu hata mimi kwa upande wangu engine ilikuwa moto sana.

Nilianza kurub, kulick na kus*ck vifuu vyake kwa fujo sana na bila kuchelewesha nilianza kutalii hifadhi ya Ngorongoro japo ilikuwa ni usiku lakini niliweza kuyatambua mazingira yake vizuri sana. Mary alikuwa yuko Sayari nyingine kabisa na alionesha kuwa na upwiru sana maana hifadhi ilikuwa na maji sana kama mvua kubwa ilinyesha.

Niliendelea kuset antena yake ya kwenda Mars kama Elon na ulisikia mlio wa kelele kubwa na hapa nikajua engine ishamwaga maji na kilichobaki ni kuenda kumalizia utalii wetu. Sikuona sababu ya kumchelewesha, hivyo niliwasha gari kuondoka maeneo haya na break yangu ilikuwa moja ya hotel ipo nyuma ya “Alpha school” Mikocheni, chap nilifanya malipo ya room tukaingia ndani.

Baada ya kuingia room tuliendeleza zoezi letu na this time sikutaka kupoteza muda, kwani nilishusha vioo vya gari vyote ili niweze kuona uumbaji wa Mungu live bila chenga. Aisee nilifanikiwa kwakweli maana mtoto kabarikiwa kuwa na hifadhi nzuri sana tena imetuna na imejaa vizuri, sikujutia pesa yangu ya kiingilio.

Niliendelea na umakini wangu kwa kuendelea kutalii maeneo mengine na nilifanikiwa kukamata vizuri nyash yake na nilianza kuhakikisha kama kweli ni laini kwa kwa kubinyabinya kwa utaratibu. Muda wote alikuwa kimya zaidi ya kutoa milio ya radi na mvua ikiendelea kumwagika, nilimkunja vizuri kwa ajili ya kuanza shughuli na nilimsikia akianza kuongea;

“Insider…..not today, please.”

“What? Are you serious?”

“Please take me home, I can’t do this today.”

Just imagine naona kila kitu live na anasema hivo, sikutaka kumforce na nilimwambia avae nguo tuondoke sababu hakuwa kwenye akili yake, kumla ningekuwa nimefanya kosa kubwa sana maana hajitambui. Sheria yangu siwezi kula mwanamke ambaye amelewa otherwise awe dem wangu au tuna historia, nje na hapo siwezi kabisa maana ni kubaka.

Niliona nimuache na kama kunibless, bhasi awe kwenye akili yake ya kujitambua, afanye maamuzi huku anajielewa na sio kujutia baadae ukizingatia nina historia na mdogo wake.

Nilimpeleka mpaka kwao na kabla hajashuka alinivuta akanipa tongue kwa sekunde kadhaa, kisha nikasubiri aingie ndani na mimi ndo kuondoka kurudi home.

Baada ya kurudi home nilimkuta wife kalala sebleni peke yake na mezani kulikuwa na bible, nilijiskia vibaya sana ikanibidi nimuamshe pale ndo kwenda chumbani kulala.

Asubuhi wife aliniamsha nijiandae ili twende church misa ya pili, ni kitambo kidogo nilikuwa sijaingia church, hivyo nilikubali kinyonge kwenda na niliamka nikaanza kujiandaa.

Tuliondoka familia nzima kwenda church na wife alinambia nisiondoke kutakuwa na kikao cha vijana na mchungaji, hivyo nisubiri maana ni muhimu sana kuwepo kwenye hiko kikao.

Kipindi nakwenda church niliacha simu chaji sasa ile kurudi mchana nakutana na missed call 9 kutoka kwa Mary na missed call 3 kutoka kwa Prisca, nikajisemea mtu na dada yake wamenitafuta nitakuwa nimeshaharibu mambo huko.

Mary alikuwa kanitumia na messages pia, nilifungua ili nisome ujumbe aliokuwa amenitumia maana alituma texts nne ambazo zilisomeka;

“Hi Insider, why can’t you pick-up my phone calls?”

"I’m sorry for today. I know you’re angry with me for what I did."

“Please pick up the phone, let’s talk about this please.”

“But I’m glad you saw me.”


Nilitabasamu na palepale nikampigia simu ili nimsikilize na haikuchukua muda alipokea tukaanza maongezi,

MIMI: “Nambie mummy unaendeleaje?”

MARY: “Naendelea vizuri vipi kuhusu wewe?”

MIMI: “Niko poa, sorry nilikuwa church, afu niliaacha simu chaji ndomana calls zako zikawa hazipokelewi.”

MARY: “Nilianza kuwa na wasiwasi labda umenimind.”

MIMI: “Niko sawa hata usiwe na wasiwasi I understand, kwanza sorry haikuwa nia yangu kukufanyia vile ni pombe.”

MARY: “No, I’m cool with that, I enjoyed it and thank you.”

MIMI: “Really?”

MARY: “Thanks for everything Insider jana nilipendeza kwaajili yako.”

MIMI: “Prisca amenitafuta pia, anajua kinachoendelea?”

MARY: “Yeah anahisi jana nilikuwa na wewe maana karudi jana home night, wakati nimeondoka kuja kwako.”

MIMI: “Sitaki kuwaingiza kwenye ugomvi na Prisca na nikavuruga mahusiano yenu.”

MARY: “Ni kweli Insider, badae twende kwa dada Jane tukamsalimie.”

MIMI: “Sawa tutawasiliana hilo badae.”

Baada ya kumalizana ka Mary nilijifikiria nimpigie Prisca ili tuongee na nimsikilize anasema nini, nilimpigia simu na kubwa alisema ananisalimia hata hakuuliza kuhusu Mary, tuliendelea kupiga story pale na tukaagana.

Jioni niliondoka kwenda kwa Jane na nilimpitia Mary tukaendelea na safari, lakini sasa alikuwa na aibu sana hata kuniangalia ilikuwa ni kwa mbinde sana, nilimsoma nikawa nampa story ucheshi ili awe comfortable.

Baada ya kuwasili kwa Jane tulikaribishwa ndani na uso kwa uso nakutana na Vicky amekaa seblen na dada yake. Jane baada ya kutuona alifurahi sana maana hakutegemea ujio wangu na tulisalimiananna nikaenda kukaa na Vicky.

JANE: “Guys kwa surprise ya leo naona twende sehemu tukale dinna.”

VICKY: “Dada Jane tulichemsha kuku wa nini?”

JANE: “Sawa dogo utakula Kuku sisi tunatoka, ngoja nikaoge guys soon nitakuwa hapa.”

MARY: “Nipe mume wangu nimshike.”

VICKY: “Kwahiyo tunakwenda wapi?”

JANE: “Nikirudi tutadiscuss pamoja.”

Vicky hakupenda suala la kutoka out na mimi nilianza kumzingua kwa kumwambia tutamuacha alinde nyumba, bhasi akaanza kunipiga kichokozi na muda huu Mary alikuwa akituangalia kwa kuibia sana.

Baada ya Jane kurudi tuliona ni bora tukaenda sehemu ya karibu home, na Bahari Beach hotel ndo ilikuwa sehemu sahihi ya kwenda, bhasi tuliondoka wote mle ndani kuelekea huko.

Baada ya kuwasili pale hotelini tuliamua kukaa upande wa juu na kila mmoja aliagiza chakula huku story zikiendelea, mimi nilikuwa busy sana na Mary na tulikuwa tunajadili kuhusu kazi anayotaka kuanza na suala la kupanga.

Baada ya kula dinna tuliagiza vinywaji na mimi niliishia kuagiza wine tu ambayo tulishare na Mary, kwa upande mwingine Lucy alianza kunipigia simu, iliita mara ya kwanza nikaipotezea, ikaita mara ya pili nikatoka kwenda pembeni kuipokea, nilihisi kuna jambo muhimu anataka kuongea na mimi;

LUCY: “Bossy mambo, sorry nakusumbua utakuwa batani.”

MIMI: “Sina wa kutoka naye afu na wewe ushakuwa mke wa mtu.”

LUCY: “Ahh bhana! Hio sio sababu ni hujataka tu.”

MIMI: “Niambie una jambo gani?”

LUCY: “Insider nambie ukweli kama jambo ni kweli, please usinidanganye.”

MIMI: “Umeanza kunitisha, leo inaonekana kuna jambo zito sana, nakusikiliza.”

LUCY: “Upo kwenye mahusiano na Asmah?”

MIMI: “No.”

LUCY: “Labda nibadili swali, Did you and Asmah have sex recently?"

MIMI: “No.”

LUCY: “Are you sure? It’s better ukawa mkweli.”

MIMI: “Trust me Lucy, hakuna jambo lolote kati yangu na Asmah, mbona maswali mengi kuna nini?”

LUCY: “Iryn amenipigia simu leo tumeongea kama lisaa pamoja na ishu ya Landlord, anadai wewe na Asmah mmesex hivi karibuni na huenda mna mahusiano ya siri sana, ila ameamua kunyamaza.”

MIMI: “Umemuuliza hizi taarifa kampa nani? Maana asijekuwa anapewa taarifa ambazo si kweli nayeye anazipokea tu.”

LUCY: “Insider Iryn ni zaidi ya CIA naamini kama kweli umefanya bhasi anajua kinachoendelea, tatizo lako unajisahau sana mshikaji wangu.”

MIMI: “Hamna kitu kama hiko na niko makini sana maana najua ananifuatilia.”

LUCY: “Bhasi elewa hivo, na mmefikia wapi mpaka sasa?.”

MIMI: “Ngoma bado ngumu sana.”

LUCY: “Insider yule ni mjamzito wewe ndo chanzo ya haya yote, unatakiwa uyamalize acha kuleta ubeberu.”

MIMI: “Sasa kama ameniblock mimi nafanyaje?”

LUCY: “Tafuta means yoyote ya kumcheki hata kwa mail ya ofisini, snapchat sema hujataka tu.”

MIMI: “Lucy yule ni mtu mzima huna haja ya kuwa na wasiwasi kama ni mtoto anajua nini anafanya, kama hayo yote nishafanya.”

LUCY: “Ngoja niwaache na mapenzi yenu, kuhusu Landlord amesema tumuulize bei anauzaje then nimjulishe, naomba uongee na mzee bhasi ili tumpe feedback mapema.”

MIMI: “Sawa haina shida kesho mapema nitaongea nae afu nitakupa feedback.”

LUCY: “Kesho tena na sio leo?”

MIMI: “Kufikia kesho asubuhi nitakuwa na majibu niachie hili.”

LUCY: “Okay sawa byee.”

Baada ya kuachana na Lucy niliwaza kwa sekunde kadhaa nikahisi hili jambo la Asmah huenda kweli Iryn anajua kinachoendelea, swali lililonijia kichwani kama kweli amejua kinachoendelea why anyamaze kimya kipindi kile tumeonana Serena Hotel??.

Niliamua kurudi zangu kujumuika na kina Jane na ile kukaa kwa kiti Mary alianza kuniuliza nilikuwa wapi na mbona nimechelewa sana?, Ni swali ambalo sikulitegemea kabisa na ilibidi nimdanganye ni masuala ya kiofisi.

Tulikubaliana tuondoke mapema ili tukajiandae kwaajili ya jumatatu na kabla ya kuondoka Jane aliniita pembeni kunishukuru kwa kuyamaliza na Mary na alisema tutawasiliana ili tuonane katikati ya wiki.

Niliondoka na Mary kurudi home, sasa kipindi tupo njiani nilikuwa nikimsifia sana jinsi alivyoumbika na yeye aliishia kutabasamu tu na nilimsifia amebarikiwa nyashi laini na hapa alicheka.
*****

Jumatatu asubuhi kabla ya kwenda ofisini nilipitia kwanza Morocco kuonana na jamaa na alikuwa kashusha gari mpya, nilitokea kuipenda Premio na nikamwambia akamilishe masuala ya registration nitaipitia badae na niliamua kuisajili kwa jina la wife.

Baada ya kufika ofisini nilimkuta Winny kafika mapema maana alikuwa yuko zam, hivyo aliwahi mapema, na ile kuniona alikumbushia zawadi yake ikabidi nimpe elfu 30 ya kumpendezesha Mary na nikachoma ndani.

Nilicheki mails kama kuna taarifa yoyote kutoka kwa maboss lakini hakukuwa na taarifa zozote na niliwatumia ripoti ya week, nikaendelea kuandaa hesabu za VAT kwaajili ya kufile TRA.

Nilikumbuka kumpigia simu Landlord kuhusu kuongea gharama ya nyumba na yeye alisema anauza nyumba kwa Tshs. billioni 2, nilishtuka sana baada ya kusikia hio bei na nilimwambia tutampa jibu soon.

Gharama ya nyumba ilikuwa kubwa sana sijui sababu ya location ni Mikocheni maana hata kiwanja kilikuwa na ukubwa wa 30x30 sqm. Nilimpigia simu Lucy kumpa feedback hata yeye alibaki akiduwaa baada ya kusikia hio amount na alisema kwa hio bei, Iryn hawezi kununua ni bora tukatafuta sehemu nyingine ya kufanyia biashara.

Mida ya mchana Mary alinipigia simu na kubwa alikuwa ananisalimia na alisema kuna rafiki yake amelipenda wigi lake, hivyo atamleta ofisini na mimi nilifurahi kusikia hizo taarifa na tulianza kupiga story zingine ndo kuagana.

Baada ya kuongea na Mary mawazo yalianza kunijia kichwani hasa zile romance tulizokuwa tunapeana ile siku na nilijikuta nasimamisha mnara wa babeli kwa kasi sana.

Suala la kudate na Mary binafsi lingekuwa gumu hasa ukizingatia tayari nina historia na mdogo wake, niliwaza sijui nipite naye kibishi?, lakini nikaona hapana Mary anajitambua na hawezi kuniruhusu kufanya ujinga kama huu, ile siku zilikuwa ni pombe haikuwa akili yake.

Hilda hii siku hakuja ofisini maana alinipa udhuru mapema na sababu kubwa alisema tumbo linamsumbua sana. Niliondoka na Nolie kwenda kupata lunch moja ya mgahawa wa karibu na ofisi yetu, na hii siku tulipiga story sana na kubwa alikuwa kamaliza UDSM, story zilikuwa motomoto.

Jioni nilikwenda kwa Sumaiya ili nimkabidhi gari yake, nilikuwa nimetimiza ahadi yangu kama nilivyokuwa nimeahidi na yeye aliishia kufurahi sana. Kwa upande mwingine nilimuuliza kama walionana na mama, alisema walionana na alimuaga kuwa anatarajia soon kwenda Europe ila hawakuongea jambo lolote jipya.

Nilimkabidhi gari yake na kumpa baadhi ya maelekezo kuhusu gari na nilimuaga kwa kumtia kofi la kalio, nikaondoka kwenda Morocco kuonana ka jamaa maana alikuwa kashanipa taarifa kila kitu kipo tayari.

Baada ya kuwasili kwa jamaa nilifanya malipo nikakabidhiwa gari na nilipitia kwanza sheli nikajaza wese full tank, huyo moto kurudi home, sasa ile napark gari namuona wife anatoka nje na akakaa kibarazani, hakujua ni mimi niko ndani ya gari.

Baada ya kushuka nilianza kuikagua gari tena, kwa mara nyingine ofcourse ilikuwa imenyooka sana na wife alisogea karibu tukaanza story;

“Baba J hii gari ni mpya umenunua?”

“Yeah kama unavyoona namba E mpya kabisa.”

“Umeagiza Japan kama ile ya kwanza?”

“No hii nimenunua showroom.”

“Unanunua gari mimi hata sijui kuendesha, kuna siku utaumwa huko ndani afu utakosa msaada shauri zako.”

“Nilikwambia uanze mafunzo ila hutaki, sitaki lawama.”

“Nikifunga chuo nitaanza na mimi nitanunua gari yangu.”

“Najua unahela mzee kashakupa urithi nini?”

“Namichongo yangu ikitiki tu nanua gari yangu.”

Tuliingia ndani huku tunapiga story na yeye alionesha kuwa na furaha sana hii siku.

Nilikuwa nimetulia chumbani nikiangalia picha zangu na Iryn ambazo tumepiga maeneo tofauti na nilijikuta naanza kum-miss sana kwakweli na bado alikuwa kanipa kufuli.

Nilianza kujiuliza maswali magumu na kujijibu mwenyewe;

Hivi mimba ya Iryn kweli ni yangu? Siamini kama kweli kabeba mimba yangu. Mhh ila kama sio yangu asingenambia, sidhani kama anaweza kunibambikia mimba ambayo sio yangu, yule mtoto ni wangu.”

Niliona haina haja ya kuwa Beberu kama Lucy anavyodai na nilitoa simu nikafungua snapchat nikamtext kuonesha nimemmiss yeye na mtoto tumboni, na baada ya nusu saa niliona ameisoma ile message, japo hakunijibu.
*****

Siku ya Alhamisi Iryn alinitafuta na nilifurahi sana kuona simu yake ikiita na nilipokea tukaanza mazungumzo,

MIMI: “Nambie mke wangu leo umeamua kunisurprise.”

IRYN: “I’m not your wife, I’m just wasting my time on someone else's husband.”

MIMI: “Wewe ni mke wangu tambua hili.”

IRYN: “Nimemaliza mitihani tayari, nadhani unakumbuka kuhusu jambo letu la kwenda Ethiopia?.”

MIMI: “Yeah nakumbuka kipenzi changu lakini sitoweza kwenda kwasasa, naomba uwaambie najipanga na tutakuja.”

IRYN: “Unajipanga mpaka lini? Do you really think watanielewa?”

MIMI: “Baby, kwanini wasikuelewe? Point ni kwamba nataka nitafute ndugu wa kwenda nae pamoja Ethiopia, mimi niko pamoja na wewe na naomba uwahakikishie wazazi mimi nakuja.”

IRYN: “Nataka kusikia kutoka kwako ni lini utakuja?”

Hapa sasa sikuwa na jibu la kumpa moja kwa moja maana niliona nitajiweka kitanzini kwa kumpa ahadi ya uongo, na nilinyamaza kwa sekunde kadhaa, na aliendelea kuongea,

“Darling, please tambua hili ni kwaajili ya huyu mtoto, uwepo wako pale ni wa muhimu sana.”

MIMI: “Baby wazazi wanataka assurance ya ndoa wala sio kingine, na wewe unajua fika hili haliwezekani, sasa naomba uwaambie wazazi ukweli kuhusu mimi. Ni bora tukawa wakweli mapema kuliko kudanganya na kuleta matatizo makubwa huko mbeleni na mtoto kwa ujumla.”

IRYN: “Yaani! Unataka niwaambie wazazi ukweli kuhusu wewe, naona ni jinsi gani humpendi na humtaki huyu mtoto.”

MIMI: “Why baby nawapenda wote.”

IRYN: “Si kweli, usingesema hivo nafikiri hujacalculate risks ambazo zitatokea baada ya kuwambia ukweli kuhusu wewe, please.”

MIMI: “Embu wewe niambie, tuwadanganye kuhusu kukuoa na nisitimize ahadi yangu, huoni kama nitakuwa najiweka matatizoni?. Mimi naona waambie ukweli kuwa ilitokea bahati mbaya na huyu mtoto hana hatia, na upo tayari kuzaa, wazazi watakuelewa na hakuna binadamu ambaye hajawahi kukosea.”

IRYN: “Nitakuwa nimejitengezea mazingira magumu sana kule nyumbani kama nitasema hivo, kwanza wale ni watu wazima watasema hakuna mimba ya bahati mbaya, naweza kutengwa hivihivi.”

MIMI: “Naomba umshirikishe na mzee kuhusu hili jambo afu uone anasemaje, wale ni familia yako lakini baba yako bado ananguvu juu ya maamuzi yako.”

IRYN: “Mzee hana shida kuhusu hili na anafahamu kinachoendelea, tatizo ni kwamba nitatengwa na familia ya upande wa mama, hawa ndo mama zangu na ndo ndugu zangu ambao naweza kukimbilia na wakanisaidia. Ndugu wa Baba wapo separate na wengi siwajui, nilishakwambia historia ya Baba maisha yake yote amekulia South na historia ya kizazi chake tangu Boer trek. Just think leo hii nikigombana na familia ya mama nitakimbilia wapi? Kumbuka Mzee hana maisha marefu sana ni pesa ndo zinamfanya aendelee kuishi.”

Ukweli alikuwa kaongea point tupu lakini sasa mimi bado sikuwa tayari kwenda Ethiopia kutoa ahadi za uongo,

MIMI: “Mummy nakujua wewe ni moja ya wanawake strong na unaweza kujieleza, naamini hili hutashindwa na litapita na naomba utambue mimi niko pamoja na wewe kwa kila hatua.”

IRYN: “Upo pamoja na mimi? Ungekuwa umekubali twende Ethiopia, now I realise you’re wasting my time.”

Na alikata simu pale kwa hasira,

Niliamua kuachana nae kwa lengo la kumtafuta badae na kumbembeleza ili akae sawa, japo kwa upande wangu bado nilikuwa nina wasiwasi sana maamuzi yangu, na nilijisemea kama nitamkosa mtoto bhasi sitapaswa kujilaumu kwa hili.

Kesho yake wakati niko ofisini mama alikuja pale ofisini na mimi nilikuwa ndani, sikuwa najua kinachoendela ni Hilda ambaye alikuja kunitonya kuwa mama yuko around, ndo kutoka ili nikaonane nae.

Mama alikuwa nje anaongea na simu, nilisogea mpaka usawa wake nikamsalimia na nikamwacha aendelee kuongea na simu lakini sasa alianza kuondoka kwenda kwenye gari, na mimi niliendelea kumfuata kwa nyuma.

Nguvu ya kumuita nilikuwa sina sababu isingekuwa heshima kumuongelesha wakati anaongea na simu, niliona ni busara nikasubiri kwanza amalize, kisha na mimi nianze kuongea nae.

Mama baada ya kufika kwenye gari yake alisimama na alikuwa kamaliza kuongea na simu na mimi niliamua kumuita;

“Mama…”

Aligeuka,

“Yes, I’m listening.”

“Sorry for the disturbance, but can I have 3 minutes to speak with you, please?”

“I'm currently busy and unable to talk right now. Insider, you have caused a lot of trouble for Iryn. All the best.”

Alifungua mlango wa gari akaingia na kuondoka na kuniacha nimebaki kwenye mataa,

CHAPTER 23
 
Back
Top Bottom