SEASON 02
EPISODE 21:
“BY INSIDER MAN”
ILIKOISHIA:
Kwa lile tukio hata Hilda alibaki anashangaa maana hakutegemea kuona mama akinifanyia vile, ukizingatia mimi ni mtu ambaye ananikubali na kuniamini, ukweli nilijisikia vibaya sana baada ya hili tukio…..
ENDELEA:
Hilda uvumilivu ulimshida na alianza kuniuliza pale shida ni nini? Mbona kama mama anaonekana hayuko sawa toka anione na walikuwa wakiongea vizuri tu?
HILDA: “Insider what’s is really going on? Mbona mama kabadilika ghafla?”
MIMI: “Hata sijui labda kuna kitu nitakuwa nimezingua, acha niende ndani nikaongee nae.”
HILDA: “No usiende hayuko sawa, wewe mtafute private muongee hapa ni ofisini inaweza leta matatizo, cha kukushauri wewe ondoka.”
Niliwaza kwa sekunde kadhaa nikaona Hilda yuko sawa, cha kufanya nimtafute mama private ili tuongee. Ofcourse nilikuwa nishajua tatizo ni nini na hapa nikaanza kumblame Iryn maana tangu muda mrefu nilikuwa namsisitiza aongee na mama kabla mambo hayajaharibika.
Niliondoka kurudi tena kwa Allen na muda wote ambao niko njiani nilikuwa nawaza kuhusu mama Janeth maana alionekana kunichukia sana. Sasa, kumpigia simu Iryn sikuwa na nguvu sababu alikuwa kaniblock, palepale nilipata wazo niende kwa Sumaiya nikaongee nae maana yeye na mama ndo zinaiva sana.
Nilipiga U-turn nikaanza safari ya kwenda kwa Sumaiya afu hata sikumpigia simu na baada ya kuwasili ofisini kwake nilitulia parking, nilimpigia simu akanambia nimsubiria soon atakuwa kafika. Baada ya dakika 10 Sumaiya alikuja na alikaa siti ya mbele, kama kawaida yake alianza kunifanyia vituko vyake, lakini mimi mawazo yangu yalikuwa mbali sana, hata yeye alihisi something wrong;
SUMAIYA: “Insider upo sawa? Sijakuzoea hivi.”
MIMI: “Sumaiya nimeharibu tayari sijui hata mama atanielewaje kwahili.”
SUMAIYA: “Mama Janeth huyuhuyu?”
MIMI: “Ndio mshikaji wangu yaani daah!”
SUMAIYA: “Kwani amejua unatoka kimahusiano na binti yake? ila hata kama akijua shida ni nini? Au anataka umkaze na yeye?”
MIMI: “Hivi kuna jambo lolote Iryn kakwambia kuhusu yeye?.”
SUMAIYA: “Hapana ni muda hatujawa intouched, embu niambie ni nini kinaendelea kati yako na mama?”
Nilijifikiria pale nikaona acha nimwambie kinachoendelea hakuna haja ya kumficha,
MIMI: “Sikia, Iryn ni mjamzito ana mimba yangu ina miezi 4 sasa…”
Alinikatisha maongezi yangu,
SUMAIYA: “Wewee usinambie! Hapa sasa nakupa nyota zote umecheza kama Messi, yaani usingempa mimba ningekulaumu sana.”
MIMI: “Sijamaliza kuongea, hapa unavyoniona nina mke na mtoto, sikuwahi kukwambia hii kitu.”
SUMAIYA: “Wee Insider una mke toka lini?.”
MIMI: “Kitambo sana na mtoto anafukuzia miaka 2.”
SUMAIYA: “Duuh! Unasiri sana Insider kumbe ulikuwa unanichora tu, kwanini hukunambia?.”
MIMI: “Hata ningekwambia ingekusaidia nini?.”
SUMAIYA: “So, Iryn anafahamu kuwa una mke?”
MIMI: “Anafahamu na alibeba mimba kwa ridhaa yake.”
SUMAIYA: “Aisee upo vizuri, nyota yako ni international.”
MIMI: “Mama anajua kinachoendelea ndomana amenichukia ghafla, na kibaya zaidi anajua mimi nina mke na mtoto, hili pia limechangia mama kunichukia, ukizingatia alishawahi kuniuliza kuhusu mahusiano yangu na Iryn.”
SUMAIYA: “Hapo kweli pagumu na mama anavyompenda Iryn lazima akuchukie kwa hili, Kuna jambo pia nafikiri hulifahamu hata Iryn pia halijui ila mimi najua.”
MIMI: “Ni jambo gani hilo tena?”
SUMAIYA: “Insider hii ishu nakwambia ila naomba ufunge mdomo wako usije kujaribu kuropoka kwa Iryn, nakwambia iwe siri yako na nina kuamini.”
MIMI: “Usiwe na wasiwasi you have my word.”
SUMAIYA: “Yule Smith mtoto wa mwisho wa mama ni mdogo wake Iryn, mama kazaa na baba yake.”
Mimi nilikuwa najua kuhusu hii ishu kupitia Iryn mwenyewe, lakini bado alisema anaendelea na uchuguzi, sasa kusikia Sumaiya naye anajua kila kitu, bhasi nilijisemea Sumaiya atakuwa anajua siri nyingi sana, mimi nilijifanya sijui kinachoendelea;
MIMI: “Umejuaje hili? Mbona kama siamini amini.”
SUMAIYA: “Ndo uniamini sasa, mama na baba Iryn wanamahusiano ya siri sana na mama anakwenda sana South Africa, hata juzi kati kabla ya kurudi alikuwa huko kupewa dudu.”
MIMI: “Wewe ulijuaje Smith ni mdogo wa Iryn?”
SUMAIYA: “Mama mwenyewe aliniambia, ndomana unaona anampenda sana Iryn sababu ya hii.”
MIMI: “So mama Janeth alikuwa anamzunguka mama yake Iryn kwa kutembea na mume wake sindio?”
SUMAIYA: “Insider haya mambo mengine sisi hayatuhusu, tujadili jambo lako uliloweka mezani.”
MIMI: “Embu nipe mawazo nini nifanye? Kidogo wewe una mazoea na mama unajua namna ya kumuingia na kutoka, nisaidie kwa hili, lengo langu tuongee tuliweke sawa hili.”
SUMAIYA: “Insider huna haja ya kuhangaika kwa hili, Master ni Iryn ndo anatakiwa aliweke sawa hili, wewe hata usihangaike, mama atakaa sawa tu hata usijipe stress, wewe fanya yako hata usiwaze kuhusu yeye.”
MIMI: “Sometimes ni bora ukajifanya mjinga ili mambo yaende, mimi lengo langu niliweke sawa hili jambo, kwahiyo unanishaurije?”
SUMAIYA: “Wewe tulia hayo ni mambo ya familia waachie wao, the truth is, she can’t hate you forever, wewe ni mkwe tayari atake asitake, mama nae uchi wa Iryn afu yeye anaumia.”
Akaanza kucheka pale,
MIMI: “Nawaza mpaka kuacha kazi ujue, sitoweza kufanya kazi kwa mazingira kama haya.”
SUMAIYA: “Acha ufala wewe, upo kwaajili ya mama au Iryn? Yaani uache kumsaidia mke wako kisa mama? Acha ujinga Insider, Iryn anakutegemea usifanye maamuzi ya kijinga, kwanza mama ataona umemwogopa, wewe fanya yako.”
MIMI: “Sawa bhana kumbe unaweza kumshauri mtu, ukiwa serious unakuwa na akili nzuri.”
SUMAIYA: “Leo unanipa gari yangu, najiona niko vizuri kuingia road.”
MIMI: “Nilitaka nikuwekee android TV ni vile nimekuwa na mambo mengi, kama unaharaka nayo ichukue.”
SUMAIYA: “Kwahiyo unataka kunipa lini?”
MIMI: “Ijumaa na leseni yako itakuwa tayari ili nikupe vyote kwa pamoja.”
SUMAIYA: “Sawa, ila unanipeleka home.”
MIMI: “Sawa haina shida, ila ndani sitaingia naishia nje tu”
SUMAIYA: “Haya baba twende.
Nilimpeleka Sumaiya kwake na muda ambao ninarudi home nilikuwa nawaza kuhusu mama Janeth pamoja na maneno aliyokuwa anaongea Sumaiya, niliwaza huenda anajua siri nyingi sana, hivyo itabidi nianze kumchimba taratibu.
Kwenye hili suala lawama zangu zote zilikuwa kwa Iryn maana alipaswa kumwambia mama hili jambo mapema sana, lakini alikuwa anasuasua mpaka mama amefahamu. Jambo lingine lililokuwa linaniumiza kichwa ni vile Iryn kuninunia afu nashindwa kuwasiliana nae ili tuyaweke mambo sawa.
Kwa upande mwingine allen alinitafuta kuniuliza kama narudi tena tuendelee na topic yetu maana nilikuwa nimemuaga kwa kumpa ahadi ya kurudi tena, nilimwomba kumtafuta kesho ili tumalize maongezi yetu.
Baada ya kurudi home nilikwenda chumbani kuoga na nilimkuta Junior akichezea simu ya mama yake, nikapata wazo la kuipekua simu yake, kimbembe Junior alikuwa hataki kunipa simu, kila nikitaka kuchukua alikuwa analia. Palepale nikapata wazo nimuwekee cartoon kwenye PC ili atoe simu, na nilifanya hivo plan yangu ikawa imetiki.
Nilianza kuipekua simu upande wa whatsapp na nilianza direct kutafuta chats zake na Iryn, lakini hakukuwa na chats zozote walizochat hivi karibuni, na niliendelea kuangalia chats zingine na nilibaini kuna Mafisi wanamtongoza sana, nikapotezea. Niliona chats za dada yake na nilifungua ili nisome chats zao, baada ya kufungua niliweza kugundua kwamba dada yake ndo anayemkomalia wife kuhusu mimi na Iryn kuwa na mahusiano, na mbaya zaidi alikuwa anamwambia afanye investigation ya ukaribu wetu.
Wife kwa upande wake alikuwa amemwambia dada yake kuhusu ujio wa Iryn pale home ile usiku na kuhusu mapenzi yake kwa Junior, dada yake alikuwa anakamia sana mimi na Iryn tuko kwa mahusiano. Alikuwa anamwambia mdogo wake aendelee kuwa karibu na Iryn maana yeye ndo rahisi kumchunguza na kujua ukweli, mbaya zaidi alimwambia itabidi waonane kwa maongezi zaidi.
Baada ya kusoma hizi chats zao hapa sasa nikajua tatizo sio mama J bali ni dada yake ambaye anasmell something fishy kati yangu na Iryn. Nilijisemea nitakuwa makini sana kuanzia kwenye simu yangu hasa kwenye chats zangu na Iryn, niliona niko vitani hivyo natakiwa kuwa makini sana kwa kipindi hiki.
Baada ya dakika 15 nilimsikia wife akija chumbani na alikuwa akimuita Junior;
“Junior nipe simu yangu nimpigie bibi.”
Na ile kuingia chumbani anatuona tuko busy na cartoon, akachukua simu yake akaondoka.
Muda huu nilipata wazo la kumcheki Iryn ili tuongee lakini alikuwa bado kaniwekea tofali. Niliwaza pale labda nimcheki kwa namba nyingine ili tuongee huenda ikasaidia, lakini niliona nitakuwa kama najimbeleza kwake, cha msingi nipotezee, kwa upande mwingine yale maneno ya kaka Allen yalikuwa yananipa jeuri na kiburi.
Kesho yake niliwahi sana kwenda Masaki na kipindi niko ofisini nilibaini Iryn bado hajaingiza mishahara kwa wafanyakazi maana yeye ndo huwa anahusika, sasa tumeanza mwezi mpya february afu hajafanya chochote niliona anazingua.
Nilimtumia mail kumkumbusha hili suala maana ni muhimu na mimi niliendelea kuandaa ripoti zingine, niliendelea kuwaza namna ugumu wa kazi unavyokuwa hasa ukichanganya mapenzi na kazi. Suluhisho na kuepusha matatizo kama haya niliona ni bora nika quit sababu vitu binafsi vina impact mpaka utendaji wa kampuni.
Baada ya nusu saa Hilda aliwasili ofisini huku kavaa skirt fupi sana kiasi kwamba ilikuwa ikimchora barabara. Mimi baada ya kumuona vile nilijifanya niko busy na kazi zangu na sikutaka kuongea chochote, ila yeye ndo alinza kunisalimia na akakaa kwenye sofa;
HILDA: “Insider tangu jana nafikiria kuhusu mama mkwe wako.”
Niliona Hilda ameanza kuvuka mipaka, niliona ameanza kufuatilia mambo yasiyo mhusu,
MIMI: “Ulikuwa unafikiria nini?”
HILDA: “Au hajapenda kumuona Iryn vile, afu na wewe ndo mhusika?”
MIMI: “I don’t know, ikifika muda kila kitu kitakuwa wazi.”
HILDA: “Jana nimekutumia ripoti ya mwezi, stock imeisha sidhani kama itaweza kusurvive muda mrefu.”
MIMI: “Stock haina shida kuna mzigo soon utakuwa bandarini, mimi natoka mara moja soon narudi.”
HILDA: “Sawa uwahi kurudi ili twende lunch.”
MIMI: “Leo nipo na wewe mpaka jioni sema ulivyovaa hivo utanifanya niingie matatizoni.”
Hilda aliishia kutabasam na niliondoka kwenda kuonana na Allen ofisini kwake ili tumalizie maongezi yetu.
Nilitumia muda mfupi sana kuwasili pale kwenye kampuni yao na nilikwenda moja kwa moja ofisini kwake nikaambiwa yuko kwenye kikao. Nilimtumia ujumbe kumpa taarifa na akanambia tuoanane mchana muda wa lunch kuanzia saa 7 mchan ili tuongee vizuri, na mimi kuondoka kurudi ofisini.
Kabla ya kurudi ofisini nilipitia shoppers kununua mazaga ya kupeleka ofisini kwaajili ya sisi na wateja kama maji ya kunywa, juice, soda na bites. Kipindi nanunua vitu simu yangu ilianza kuita na alikuwa ni Mary akinipigia na nilipokea kwa haraka sana;
MIMI: “Hi Mary.”
MARY: “Hi Insider za wewe?”
MIMI: “Salama mummy, nimefurahi kusikia sauti yako hata sikutegemea.”
MARY: “Ahsante sana dear, nilikuwa nakusalimia tu.”
MIMI: “Thank you, unasomeka pande zipi?”
MARY: “Niko Posta ofisini kwa mama but I won’t be here for too long.”
MIMI: “Karibu Masaki upajue ofisini kwangu.”
MARY: “Thank you leo nitakuja, navyotoka huku nitakujulisha.”
MIMI: “Karibu sana Mary.”
Saa sita na nusu Allen alinipigia simu ili tuoane kwaajili ya mazungumzo na tulikubaliana tukutane pale Salt restaurant. Sikutaka kupoteza muda na niliondoka kwenda eneo la tukio na yeye alikuwa ameshafika tayari na tulisalimiana tukaanza story;
ALLEN: “Bro sorry sana nilikuwa nina kikao afu sikutegemea kama ungekuja asubuhi.”
MIMI: “Usijali mimi ndo nilizingua nilipaswa kukupa taarifa mapema.”
ALLEN: “Mama kijacho anaendeleaje?”
MIMI: “Hakuna lolote kutoka kwake anajiandaa na mitihani kwasasa. Tuendelee na topic yetu ya jana maana tulizungumza vingi lakini hatukamaliza.”
ALLEN: “Ni sawa kabisa ila leo tutakuwa na solution ya hili jambo, usiwe na wasiwasi.”
MIMI: “Toka jana tuongee kidogo naona mabadiliko, ila kaka kuna jambo inatakiwa ujue, hata kama tukisubiri Iryn ajifungue ndo twende, bado mimi siwezi kumuoa unafikiri wazazi watakubali?”
ALLEN: “Una uhakika hutakuja kumuoa Iryn?”
MIMI: “Ndio siwezi kumuoa, yeye ni kama mchepuko kwangu na anajua hili.”
ALLEN: “Our future is an uncertainty, you never know, kinachomtofautisha Iryn na mama J ni kutambulika kwa wazazi na vile umemlipia mahali, lakini vingine vyote wako sawa na huyu soon atakuwa na mtoto wako.”
MIMI: “Upo sahihi lakini sasa…”
Alinikatisha maongezi yangu,
ALLEN: “Bado sijamaliza ipo hivi, mimi naona ni busara Iryn akaongea ukweli huko kwao kuhusu wewe kuwa una mke na mtoto, na ameridhia kuwa mke mdogo kwa hiyari yake.”
MIMI: “Kaka huoni kama nitaweza kukosa mtoto kizembe wakijua ukweli?”
ALLEN: “Toka jana nakwambia kuhusu hili, mwenye maamuzi na hii mimba ni dada mwenyewe na sio wazazi au sisi, yeye akisema ninazaa na kweli atazaa huna haja ya kuwa na wasiwasi.”
MIMI: “Sidhani kama atakuwa tayari kuwaambia wazazi hivyo, hawezi kubali anaweza kutengwa na ukoo.”
ALLEN: “Sasa ni bora kuwa wakweli kuhusu hili au tudanganye? Na kama tukiwaambia tutamuoa kumbuka tutakuwa tumeshaingia kwenye makubaliaono ya wazazi na tusipofanya hivyo tutakuwa matatizoni, kama unaona ni sawa kuwadanganya niko tayari kukupa kampani mpaka Ethiopia.”
MIMI: “Hapana naona option ya pili imekaa kimkakati sana ila kuna possibility ya kumkosa mtoto au hata akizaliwa akapewa ukoo wa kwao.”
ALLEN: “Haiwezekani huyo mtoto ni wako na sifikirii kama mama yake atakuwa tayari kukuweka mbali na mwanao, never. Hili suala wa kulimaliza ni Iryn mwenyewe wala sio sisi ni mwenyewe akae na familia yake awaambie ukweli kuhusu wewe na maridhio yake.”
MIMI: “Kaka usije ukanijaza kichwa afu mambo yakaenda viceversa maana sitaki kumpoteza huyu mtoto.”
ALLEN: “Na ukionesha weakness ya uhitaji sana wa mtoto ndo utampoteza sasa, just kuwa normal usioneshe wenge lolote.”
MIMI: “Duuh sawa bro nashukuru kwa mawazo yako.”
Wakati tunaendelea na mazungumzo Mary alipiga simu kunipa taarifa anatoka Posta hivyo nimuelekeze ofisi ilipo ili aje na mimi nilimwambia aje Salt atanikuta hapa, alisema haijui ilipo nimtumie location, nikamwambia akifika Cocobeach anipigie nimuelekeze.
Ndani ya dakika 30 alinipigia kunipa taarifa anakaribia na nikamueleekeza mpaka anafika na kwa mbali nilimuona akishuka kwa Vanguard, alikuwa amependeza sana na alizidi kuonekana ni mrembo sana.
Aliingia ndani akaja usawa wetu na tulianza kusalimiana pale na nilimtambulisha kwa Allen na story zingine zikaendelea;
MIMI: “Nambie mummy, mama mkwe hajambo?”
MARY: “Afu anakuulizia sana na mbaya zaidi Prisca anakosaga majibu ya kutoa.”
MIMI: “Hahahaa, msalimie sana, kumbe unajua kudrive ndinga nilikuwa sijui.”
MARY: “Yeah kimtindo kama hivi.”
MIMI: “Agiza food ule ili tuondoke najua hujala.”
Allen aliniaga anawahi ofisini na niliendelea kubaki pale na Mary nikimsubiri amalize kula, na baada ya kumaliza tuliondoka kwenda ofisini.
Baada ya kufika ofisini nilimpeleka moja kwa moja mpaka show room ili aangalie mawigi, kwa upande wake alionekana kuyapenda na alikuwa akishangaa bei zake,
MARY: “Insider wigs ni nzuri ila kwa hizi bei hapana mimi siwezi.”
MIMI: “Wig la gharama kuvaa ni bei gani?”
MARY: “Nakumbuka laki 5 na mama ndo alinunuliaga, hii Lace nimeipenda kwakweli niambie sifa zake.”
MIMI: “Huku sasa mimi ndo sijui ngoja nikuitie mtaalamu wa hizi kitu akuelekeze.”
Nilimuita Winny ili amuelekeze Mary kwa sifa za wigi ambazo atahitaji maelekezo;
WINNY: “Mrembo hio ni frontal lace natural hair black kutoka France, hio ni mkataba utavaa mpaka uichoke, haipukutishi na ni laini kama unavyoiona. Ukinunua hio wigi utapewa wig cap, brush, shampoo, sprays, gels na wig stand, bado una offa ya kuja hapa kusetiwa free mara 3.”
MARY: “Wow amazing, Insider hii wigi nimeipenda kwakweli ila sasa milion 2 ninatolea wapi?”
MIMI: “Kama umeipenda, nakupa offa ichukue kama zawadi yangu kwako, umenifanyia mambo mengi sana hio ni shukrani yangu.”
MARY: “Thank you Insider.”
Winny alishangaa sana kuona nampa Mary ofa ya wigi na nilimwambia yeye ndo atakaye mhudumia Mary. Mary alisema atakuja jumamosi kwaajili ya kuweka wigi na tuliondoka tukaenda ofisini kuendelea na mazungumzo.
MARY: “Insider Salon yenu ni international sijaona Salon hapa Dar ya kushindana na nyie.”
MIMI: “Ofcourse hata wateja wetu alimia 95 ni foreigners, naona unazidi kuwa mrembo nipe siri ya mafanikio.”
MARY: “Nakula vizuri, nalala kwa wakati, sina stress kwanini nisiwe mzuri?”
MIMI: “Hahahaaa hata mimi naona sio kwa kung’aa huko mpaka unafanya mapigo ya moyo wangu yaongezeke spidi.”
MARY: “Mhhh! Prisca mnawasiliana?”
MIMI: “Yeah tuko intouched ila sio sana, nafurahi kuona amemove on.”
MARY: “How did you know?”
MIMI: “I know na ni jambo zuri, tuachane na haya yalishapita, vipi kuhusu wewe usinambie bado upo single sitokuelewa.”
MARY: “Bado niko sokoni, soko gumu sana huku nje..”
Tulianza kucheka wote pale na aliendelea kuongea;
“Insider kuna kitu nataka kushare na wewe, nimepata kazi Posta, kuna kampuni nitakuwa nafanya nayo kazi but nataka nitafute apartment karibu.”
MIMI: “Unataka kuondoka home? Kwamba utashindwa kuamka mapema uwahi kazini?.”
MARY: “Si unajua nasoma pia, bado research na muda mwingi nitakuwa nashinda library, pia nimekuwa mtu mzima nahitaji kukua.”
MIMI: “Mimi sikushauri uhame home, unataka majukumu ya nini mapema hivi? Hizo pesa za kodi si bora uziweke zije zikusaidie hapo baadae?”
MARY: “Bhana, wewe na mama lenu moja naye hataki kabisa kusikia hizi habari, but weekend nakuwa narudi home.”
MIMI: “Mmh, wewe fanya kutokana na moyo wako unavyotaka na angalia mipango yako, ukiona kuna haja ya kupanga ni sawa.”
Hilda aliingia ofisini alikuwa lunch na baada ya kumuona Mary walisalimiana, kisha akaanza kunilamikia nimemdanganya kuhusu kwenda kula lunch na mimi nikajitetea nilikuwa na mgeni ndomana nikashindwa.
Mary aliniaga anaondoka kwa ahadi ya kurudi jumamosi kwaajili ya kuweka wigi, na mimi sikuchukua muda nikamuaga Hilda naondoka kwenda Mikocheni kuonana na Lucy. Lengo la kwenda kuonana na Lucy ni sakata la Landlord na niliona ni busara tukaonana face to face kuliko kuongea kwa simu.
Baada ya kuwasili Mikocheni ofisini nilionana na Lucy tukaanza mazungumzo na kubwa alisema ameongea na Iryn ila yuko kwenye maandalizi ya mitihani hivyo mpaka weekend ndo watapanga vizuri.
MIMI: “Unajua Iryn kaniblock.”
LUCY: “Uliniambia, si hutaki nikumbelezee unaleta ubeberu shauri zako.”
MIMI: “Shida ukiongea nae atajua mimi nimekwambia kinachoendelea afu yeye mpaka sasa hajakwambia, atleast akufungukie hapo kidogo itakuwa na nguvu.”
LUCY: “Sema mke wako kabadilika sahivi, sijui ndo mimba inamchanganya yaani simuelewi kabisa.”
MIMI: “Afadhali hata wewe umeliona hili maana unaonaga mimi ndo mwenye shida.”
Baada ya maongezi ya muda mfupi nilimuaga Lucy nikaondoka kurudi home mapema kabisa.
Kipindi niko home nilikuwa nikitafakari ushauri wa Allen na niliona yuko sahihi ni bora Iryn akasema ukweli huko kwao kuhusu mimi before it’s too late au wazazi wakajua kupitia mama Janeth.
Usiku Jane alinipigia simu kunipa taarifa kuwa ameanza biashara na nilimuahidi kwenda dukani siku ya kesho na nitashinda siku nzima. Jane alionesha kuwa na furaha sana baada ya kuanza biashara hata mimi kwa upande wangu nilijisikia vizuri sana kuona Jane akiwa na furaha ukizingatia marehemu Pama alinipa task ya kuhakikisha Jane anakuwa salama na mtoto.
Kesho yake nilikwenda dukani kwa Jane kama nilivyokuwa nimemuahidi ili kuona maendeleo kwa ujumla, duka lilikuwa limejaa sana na lilionekana kupendeza sana, wateja nao hawakuwa mbali walikuwa wanakuja kwa wingi.
Nilishinda siku 2 mfululizo dukani na nilikuwa nikisaidiana kazi na dada ambaye alimtoa home na kumleta dukani sababu alikuwa anamuamini, Jane alikuwa anakuja pale shop na kuondoka maana asingeweza kumwacha mtoto home.
******
Jumamosi nikiwa ofisini nilipata wazo nimpigie simu mama niombe kuonana nae ili tuzungumze, nilipiga simu mara 2 bila majibu na niliamua kumtumia ujumbe ambao niliandika kuomba kuonana nae kwaajili ya mazungumzo, lakini sikujibiwa ni kama vile hakuiona message yangu.
Nilikumbuka maneno ya Sumaiya nikaona alikuwa sahihi kusema haya mambo ni ya familia, hivyo niwaachie wao wenyewe wayamalize na nikiendelea kujibembeleza nitapoteza thamani yangu. Kwa upande mwingine kuendelea kufanya kazi kwenye mazingira haya niliona nitazidi kuwa kwenye wakati mgumu, ukizingatia sipo kwenye maelewano mazuri na hawa wahusika wakuu, Iryn na mama yake.
Muda huu Mary alinipigia simu kunipa taarifa kuwa yuko njiani anakuja kuweka wigi lake na kufikia saa 7 mchana atakuwa around. Nilimpanga Winny mapema kuhusu ujio wa Mary, nilitaka yeye ndo amuhudumie na sio mtu mwingine.
Saa 7 mchana Mary aliingia na Vanguard pale ofisini na mimi nilitoka kumpokea na tuliishia kukumbatiana, sasa Mary alikuwa katembea na mdogo wake Ivy, ilikuwa ni surprise kwakweli na sikutegemea kabisa.
MIMI: “Karibu sana naona leo umeamua kunisirprise, Ivy hujambo?”
MARY: “Ahsante, ameforce tuje wote ndomana na sijamwambia nakuja kwako.”
IVY: “Sijambo shem tumekumiss, why can't you come home?”
MIMI: “I will come Ivy, today I am happy to see you again."
IVY: “Me too.”
MARY: “Insider utanisaidia kumpeleka Ivy lunch hajala mchana.”
IVY: “I’m not hungry.”
MIMI: “Ivy tutakwenda wote kula sawa?. Mary wewe kaendelee huko ndani dada anakusubiri zoezi lianze.”
Mary alikwenda ndani, tulikaa nje kibarazani tukipiga story na Ivy maana ni muongeaji, huwezi jutia kuwa naye karibu;
MIMI: “Nani alikwambia mimi ni shem kwako?”
IVY: “Dada Prisca told me.”
MIMI: “Niite Uncle Insider sawa eeh?”
IVY: “Sawa uncle.”
MIMI: “Let’s go tukale lunch, unataka kula nini?”
IVY: “Pizza”
Tuliondoka kwenda kula Pizza, muda ambao tuko njiani mama alinipigia simu, habari kubwa alisema anaona kuna jambo linanisumbua akili lakini siko tayari kushare na mtu, aliendelea kunisisitiza kama nipo tayari bhasi nimwambie ili aangalie namna ya kunisaidia hata kimawazo au ushauri.
Kwa upande wangu sikuwa tayari kumwambia mama kuhusu hili jambo na niliendelea kumkatalia kuwa sio kweli na mimi niko sawa, licha ya kutokubaliana na mawazo yangu
“Hili jambo siwezi kushare na wazazi kwa kipindi hiki mpaka pale mambo yatakapokuwa sawa ndo nitashare ila kwasasa mtu wa kushare nae ni sister tu.”
Baada ya kuwasili Pizzahut niliagiza pizza medium na nilikwenda kula pizza kwaajili ya kumpa kampani Ivy, haya madude mimi huwa siyapendelei kabisa. Nilipiga slice 2 nikamuachia Ivy aendelee kula, nikatoa simu kumpigia sister ili nimpe taarifa za kwenda Arusha anipe na ratiba zake mapema kabla ya kwenda.
Tulipiga story nyingi sana na sister na tulikubaliana niende Arusha mwezi wa pili mwishoni maana atakuwa likizo, hivyo atakuwa na muda mzuri wa kukaa na mimi mdogo wake.
Kwa upande mwingine Ivy alikuwa amemaliza kula na alimwambia dada afunge slice 2 zilizobaki na alisema kwaajili ya dada yake Mary na tukaondoka kurudi ofisini.
Kufikia saa 10 jioni Mary alikuwa tayari kamaliza kutengenezwa na alipendeza sana mpaka nikajikuta naanza kupagawa, alikuwa kawaka sana kwa jinsi alivyo mzuri by nature na wigi alilokuwa kawekewa plus madikodiko mengine alikuwa bonge la pisi hata yeye aliishia kufurahi tu.
MIMI: ”Umependeza sana yaani umebadilika umekuwa pisi ya kimataifa.”
MARY: “Thank you Insider, ukweli hata mimi najishangaa sipati picha huko home leo na shoga zangu wakiona lazima waulize nilikokwenda.”
MIMI: ”Wewe wakaribishe sana waje hapa.”
MARY: “Insider naenda home kumpeleka Ivy but naomba badae tutoke kama unanafasi please.”
Nilijifikiria kwa sekunde kadhaa nikaona sina ratiba yoyote, acha nikubali ili niendelee kumfurahisha Mary;
MIMI: ”Sawa haina shida, mimi nitabaki nikikusubiri hapa ofisini so utanambia ukiwa tayari.”
MARY: “See you soon, Ivy twende, mwambie Ahsante shem Insider.”
IVY: ”No, he wants me to call him Uncle Insider.”
Mary aliniangalia afu akatabasamu kwa kutingisha kichwa na nilimsindikiza mpaka parking na kabla ya kuingia kwa gari alikuja akanikumbatia na wakaondoka, kugeuka nyuma namuona Winny yuko kibarazani anatabasamu, nilisogea mpaka usawa wake tukaanza story;
MIMI: “Leo umetisha sana itabidi nikupe zawadi.”
WINNY: “Namuona kafurahi mwenyewe hata haamini kama ni yeye, ni nani uyo?”
MIMI: “Huyo alikuwa shem wangu, nilitokaga na mdogo wake but tuna mawasiliano mazuri.”
WINNY: “Insider unapendwa sana na watu, just imagine umeachana na mdogo wake lakini bado mnacheka vizuri, ni wanaume wachache wenye bahati kama yako.”
MIMI: “Winny umeanza kunichokoza.”
Na nilianza kuslap makalio yake akakimbia ndani na mimi nikaenda ofisini na niliamua kumpa Hilda utawala akapumzike na nilimwambia aniachie ofisi na yeye aliishia kufurahi akaondoka.
Nilikaa ofisini mpaka saa 2 za usiku ndo Mary kunipigia simu kunipa taarifa anatoka home anakuja Masaki, nilikuwa nishasahau kama nina miadi ya kukutana na Mary.
Baada ya lisaa aliwasili na tulikutana ofisini nje ya geti alikuwa na Uber, nilimpick tukakubaliana twende Wavuvi Kempu. Baada ya kuwasili eneo la tukio na kushuka hapa sasa ndo namuona Mary vizuri, aisee alikuwa kapendeza sana maana alivaa skin jeans ya light blue ambayo imemkaa vizuri na kiuno kilichoreka na juu alikuwa kavaa top nyeusi iliyoishia chini ya kitovu na glass nyeusi.
Mary kabarikiwa shepu nzuri sana, sasa jinsi alivyokuwa kawaka niliishia kumsifia pale na nilimshika mkono tukazama ndani, tukatafuta sehemu nzuri tukakaa na mhudumu alikuwa tayari kafika kutusikiliza, tukaagiza Hennesy na mixers.
Ndani ya muda mfupi dada alikuwa katuletea kinywaji tukaanza kunywa huku tunapiga story, ofcourse tulikuwa tumemisiana sana maana ni kitambo tulikuwa hatujakaa pamoja.
Story zetu kubwa zilibase kwenye mahusiano na maisha kwa ujumla, Mary kwa upande wake alitaka kujua kama bado nina pasha kiporo na mdogo wake, nilimkatalia katakata.
Tulikuwa deep sana kimaongezi na kadri muda unavyozidi kwenda na pombe kukolea tulianza kuoneshana hisia za kimapenzi waziwazi, kuna muda tulikuwa tunacheza pamoja na kukumbatiana.
Mida ya saa 6 usiku wife alinipigia simu, baada ya kuona ni wife niliwaza haraka nikaona wacha nikapokee simu yake kwenye gari, nisipo-pokea italeta shida, nilimuaga Mary nakwenda washroom lengo nikaongee na wife.
Simu ilikuwa imekata tayari na aliendelea kupiga kwa mara ya pili na baada ya kuingia kwa gari nikapokea na tukaanza mazungumzo;
“Nambie mke wangu hujalala tu?”
“Napataje usingizi na wewe mpaka sasa hujarudi, umepitia wapi?”
Nilipiga hesabu za haraka nikaona acha niwe mkweli,
“Mke wangu siko sawa kabisa nimeona nipitie kunywa ili nikae sawa.”
“Hivi unaakili wewe? Sasa pombe ndo zinakuweka sawa?”
“Nikirudi home makelele si bora ninywe tu.”
“Baba J umekaa chini na mimi kunambia matatizo yako? Nini maana ya kuishi pamoja kama hunambii shida zako? Sijapenda naomba urudi home mapema tuongee, kama huwezi nambie ulipo nikufuate.”
“Haina haja mimi niko sawa na nitarudi home, usiwe na wasiwasi.”
“Haya, sisi tunalala byee, Takecare.”
Baada ya kurudi ndani Mary alianza kulalamika nimemuacha alone, ilibidi nimbembeleze ili atulie na nilimwambia ukweli kwamba nilikuwa naongea na wife.
Mary alikuwa close sana na mimi ‘zero distance’ na tuliendelea kucheza pamoja huku nazungusha mikono kwenye makario yake na yeye alizungusha mikono kwenye kiuno changu. Network yangu ilikuwa ishahama muda mrefu sana na yeye alikuwa kalainika sana, tulikuwa kwenye huba zito sana kiasi kwamba tulianza kupeana makiss bila aibu, licha ya nyomi ya watu iliyokuwepo maeneo haya.
Nilicheki muda simu yangu ilikuwa inaonesha ni saa 7 usiku na madakika, nikamwambia Mary tuondoke akasema sawa. Ile kufika kwenye gari tulianza kuexchange saliva tena kwa fujo kwelikweli na sikuchukua muda nikapandisha mkono kwenye vifuu vyake. Hapa sasa alianza kutoa kelele za nguvu na ile kushusha mkono kwenye bustani yake ilikuwa tapatapa yaani imemwagiliwa vya kutosha na muda huu alikuwa hoi akinitizama tu kwa macho ya kurembua.
Nilimwacha afu nikaanza kujifikiria niondoke naye au nirudi home? Maana kufikia stage hii Mary asingeweza kuwa na jeuri ya kunikazia, kuondoka nae ilikuwa ni lazima 100%.
Wakati naendelea kutafakari, alianza kuongea pale,
“Insider where are you taking me?”
“I don’t know.”
EPISODE 22
COMING SOON: