Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 02
CHAPTER 36

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

IN LOVING MEMORY OF MR. PAMA (2022).

PREVIOUS:

Baada ya nusu saa mama Janeth ananipigia simu, kwanza kabisa nilishangaa kuiona simu yake, hivyo nilimuaga mzee naenda washroom mara moja. Nilipokea simu ya mama na habari kubwa alisema tuonane usiku huu kwani kesho ana safari, pia ana maongezi muhimu sana nami.

CONTINUE:

Nilipovuta kumbukumbu, nilikumbuka jinsi alivyonifanyia nyodo siku za nyuma. Je, sasa anataka niende kwa sababu Iryn kaenda? Alikuwa wapi muda wote huu? Nilijaribu kufikiria kwa haraka, lakini nikaona hakuna haja ya kukubaliana. Acha nivimbe, kwanza siwezi kumuacha mzee Juma, hasa wakati bado tuko kwenye maongezi muhimu.

Niliamua kumjibu kwa utulivu na kumwambia kuwa niko mbali sana, na nitarudi usiku wa manane, hivyo tuonane akirudi kutoka safari yake. Baada ya kumalizana na mama, nilirudi kwa mzee Juma kuendelea na mazungumzo yetu, nikiwa na utulivu na mtazamo mpya.

Niliendelea kuzungumza na mzee, na habari kubwa aliyonieleza ni kwamba itabidi tuondoke Ijumaa kwenda Tabora kwa ajili ya ukumbusho wa kifo cha marehemu Pama. Nilijikuta nawaza kwa haraka, nikiweka kila kitu kwenye mizani, na nikaona sina sababu ya kuukataa wito huu. Kwa kweli, marehemu Pama alikuwa ni mzee muhimu sana kwangu, na heshima yangu kwake haiwezi kupuuzwa.

MZEE: “Tutaondoka pamoja na Cami naye lazima aende.”

MIMI: “Sawa mzee haina shida, kesho nitaanza kujiandaa kwaajili ya safari.”

MZEE: “Tutaondoka kwa ndege, hivyo tutawahi kufika, na zoezi lenyewe litafanyika Jumamosi.” Aliongeza mzee Juma, akisisitiza umuhimu wa safari hiyo.

MIMI: “Sawa mzee wangu.”

Tuliendelea na maongezi na mzee hadi saa nne za usiku ndipo tukamaliza na kuondoka. Wakati huo, simu yangu ilikuwa ikiita mara kwa mara, ni Iryn alikuwa akinipigia sana. Pia alikuwa amenitumia ujumbe akiniomba nimnunulie maziwa ya mtindi.

Nilipokuwa kwenye Uber nikirudi, njiani niliamua kumpigia Jane na kumtaarifu kwamba nami nitakwenda Tabora. Jane alifurahi sana kusikia taarifa hizi na akaniambia kwamba yeye ataondoka kesho pamoja na Mary.

Nilibaki nashangaa kwa muda,

MIMI: “Kwani uliongea na Mary kuhusu kwenda Tabora?"

JANE: “Ndiyo, tuliongea kwa simu tangu jana, maana sina kampani."

MIMI: “Sawa, vizuri. Mimi hajanambia kabisa kuhusu hili."

JANE: “Hata mimi nimeshangaa kusikia kwamba unaenda Tabora. Nilijua una ratiba nyingi."

MIMI: “Ni kweli ratiba zangu hazieleweki, lakini sina jinsi, lazima niende."

JANE: “Sawa, sisi mtatukuta Tabora."

Baada ya mazungumzo na Jane kumalizika, nilianza kufikiria namna ya kumweleza mama kijacho wangu, Iryn, kuhusu safari hii. Mawazo yangu yalinipeleka mbali, kwanza kwa hali aliyokuwa nayo, kumuacha peke yake nyumbani ilikuwa hatari. Pili, niliwaza haitakuwa rahisi kukubaliwa kuondoka, hasa kwa kipindi hiki kigumu kwake.

Suala la kwenda Tabora tulikuwa tumezungumza na Jane kipindi tulipoenda na Mary pale kwake. Hata hivyo, kwa upande wangu niliona ni ngumu sana kuamua kwenda kwa sababu ya hali ya Iryn. Niliamua kwamba nitakwenda siku nyingine kwa nafasi yangu, pindi nitakapokuwa na uhuru zaidi.

Baada ya kufika kwenye apartment, nilimkuta Iryn amelala sebuleni, akiwa uchi kama kawaida yake. Nilimsalimia kwa upole, kisha nikapita moja kwa moja hadi chumbani kwenda kuoga. Nilihisi ni bora nifanye hivyo haraka, maana nilikuwa nimekunywa, na sikutaka ajue chochote kuhusu hilo.

Nilioga haraka huku nikijisafisha vizuri, ikiwemo kinywa changu ili kusiwe na dalili zozote za harufu ya pombe. Baada ya kumaliza, nilirudi sebuleni na nikakaa pembeni yake. Macho yake yalikuwa yamenikazia, akinitazama kwa makini, kana kwamba alikuwa akisubiri niseme kitu au kufanya jambo.

IRYN: “Ulikuwa wapi?” Aliuliza.

MIMI: “Mishemishe, halafu kuna jambo nataka nikwambie.”

IRYN: “Jambo gani?”

MIMI: “Ijumaa nitaondoka kwenda Tabora kwa ajili ya ukumbusho wa kifo cha mzee wangu. Kwa hivyo, itabidi uende kwa mama Janeth hadi nitakaporudi. Sawa, mummy?"

IRYN: “Darling, kwa nini? Unajua jinsi gani ninavyokuhitaji kipindi hiki. Kwa nini usiende nikiondoka?"

MIMI: "Baby, yule alikuwa kama mzee kwangu. Jumamosi ndiyo siku ya tukio, na nitaenda pamoja na mzee Juma, ingekuwa ni dhihaka kumkatalia. Pia, ingeonekana kama sina heshima kwa marehemu. Nakuhakikishia nitarudi haraka iwezekanavyo."

IRYN: “Kwanini unanipa taarifa kwa kunishtukiza?”

MIMI: “Sikuwa na mpango wa kwenda huko, lakini sasa sina jinsi, lazima niende. Nitarudi Jumapili mapema sana, mpenzi wangu. Tafadhali, nakuomba uende kwa mama Janeth ili kama kuna jambo lolote, iwe rahisi kusaidiwa."

IRYN: “Mama hajakwambia ana safari?”

MIMI: “Ameniambia, lakini kuna dada wa kazi wawili kwa mama, na bado huwa hapakosi wageni.”

IRYN: “Claire amerudi kutoka safari, nitaongea naye aje tukae pamoja.”

MIMI: “Umekula?”

Alitikisa kichwa kukubali ‘ndio nimekula’ na nilienda chumbani, nikaanza kupitia taarifa za dukani Dodoma na kuwapa maelekezo vijana wangu.

Asubuhi, Mary alinipigia simu na kunitaarifu kwamba ataenda Tabora pamoja na Jane, na atanijulisha atakaporudi. Alisema hatuwezi kuonana weekend kama tulivyokubaliana. Kwa upande wangu, sikutaka kumwambia kuhusu mpango wangu wa kwenda pia, nilitaka kumsurprise kwa hilo.

Niliendelea na usafi pamoja na kumuandalia chakula mama kijacho wangu. Iryn alikuja jikoni na kunijulisha kwamba Claire yuko njiani. Baada ya dakika tano, Claire alifika, na Iryn alitoka kumpokea. Claire alinikuta nimekaa sebuleni wakati waliporejea.

CLAIRE: “Waow! I didn’t think Insider would be here."

MIMI: “Umeanza unafiki, sema kilichokuleta hapa ni nini.?”

IRYN: “Mhh na wewe ushaanza mambo yako.”

CLAIRE: “Nambie shemu wangu za siku? Mara ya mwisho kuonana unamtafuta Iryn.”

MIMI: “Miezi imekata ni muda mrefu, juzi tu hapa niliambiwa uko safari na umerudi lini?”

CLAIRE: “Nimerudi jana, mnaweza kunipa majibu kwanini wote mlikuwa hampatikani kwenye simu?”

MIMI: “Claire achana na hizi story utanipa hasira bure, ukitaka majibu muulize best yako.”

CLAIRE: “Hongera lakini, unaenda kuwa baba.”

MIMI: “Malizia baba wa watoto wawili.”

Na waliishia kucheka na Iryn maana hawakutegemea jibu langu,

“Nikuletee kinywaji gani?”

CLAIRE: “Maji yanatosha shem wangu.”

Nilimletea maji na nikawaacha waendelee na maongezi yao, nikaenda chumbani.

Wakati nikiwa chumbani, nilijipanga kwenda Mikocheni kuonana na Lucy ili tumalize tofauti zetu, kwani alikuwa kachukia sana. Niliona ni busara kumuomba msamaha, kwani nilijua kwamba nilikuwa nimemkosea sana kama mtu wangu wa karibu.

Niliingia bafuni kuoga na baada ya kutoka nilianza kujiandaa kwa haraka sana. Simu ilianza kuita na kucheki alikuwa ni Allen akinipigia na baada ya maongezi, alisema niende ofisini kwake, kwa mazungumzo muhimu ambayo tulihitaji kuyashauriana.

Allen alikuwa ananisaidia kuandaa taarifa za fedha kwa ajili ya kutuma TRA (Financial Statement). Alikuwa na mambo ya kodi aliyotaka tushauriane kabla hajamaliza kazi yake, ili kuhakikisha kwamba kama kuna marekebisho yanayohitajika, yafanyike mapema.

Nilitoka seblen na nikawaaga natoka mara moja na sitachelewa kurudi;

IRYN: “Darling, pitia nyumbani kwa mama uchukue gari, huoni tunavyoteseka?.”

MIMI: “Mama anataarifa?”

IRYN: “Ile gari ni yangu alinipa mwenyewe, na jana alinikumbusha niichukue.”

MIMI: “Sawa nimekuelewa, point yangu ni kwamba, funguo zipo? Maana amesafiri leo asubuhi.”

IRYN: “Funguo za gari huwa zinakaa kwenye droo yake, wewe nenda kachukue. Jessie anajua funguo zinako kaa.”

MIMI: “Sawa mpigie simu.”

IRYN: “Darling, nani ambaye hakujui pale kwa mama?.”

Nilijiona mjinga na nikamuaga kwa kumkiss shavuni. Break ya kwanza ilinipeleka nyumbani kwa mama, ambapo nilipata fursa ya kuzungumza na Jessie kuhusu dhamira yangu. Bila kusita, Jessie alikubali na alileta funguo za gari kwangu.

Jessie ni mfanyakazi wa nyumbani kwa mama na ni mzungu kutoka Ulaya. Ameajiriwa kwa kazi kubwa ya kuwahudumia watoto wake. Huenda ukashangaa kuona wazungu wakifanya kazi za nyumbani, lakini ni kweli na wana elimu ya hali ya juu katika sekta hiyo. Jessie amesomea Housekeeping na analipwa mshahara mkubwa kwa juhudi zake za kipekee katika kuangalia watoto wa mama.

Baada ya kuchukua gari, niliondoka kutoka kwa mama kuelekea kwa Allen. Niliona ni bora kumalizana na Allen kwanza kwa sababu kulikuwa na suala muhimu, na baada ya kumaliza hilo, ndipo ningeweza kuelekea kwa Lucy.

Nilitumia muda mfupi kufika ofisini kwake, ambapo tuliweza kuonana na kujadili suala aliloniitia. Baada ya kufikia makubaliano, tuliendelea na mazungumzo mengine, ambapo Allen alieleza kuwa angependa kumjua Iryn.

Hakuwa na lengo hilo pekee, pia alianza kuzungumzia kuhusu Hilda na mipango yake ya kumtafuta, huku akiniuliza mbinu za kumsaidia, kufanikisha jambo hili.

MIMI: “Kaka unamtaka Hilda kwa lengo la mahusiano au kupita tu.?”

ALLEN: “Niwe namla tu mambo ya mahusiano hapana.”

MIMI: “Hilda huwezi kumpata kihivyo amini kwamba.”

ALLEN: “Chief nampango wa kuweka mzigo, sidhani kama atachomoa hapa.”

MIMI: “Hilda sio b*tch, hana tamaa kabisa, usijaribu kufanya hivyo.”

ALLEN: “Kaka Hilda akiwa kwako hawezi kuonesha rangi zake, kwanza wewe ni bossy wake lazima ajue ku-behave.”

MIMI: “Nimemsoma vizuri sana tangu anavyoajiriwa na kuwa karibu naye. Kama Hilda angekuwa mtu mwenye tamaa, ningemsoma mapema sana. Ananunua vitu vya kuweka nyumbani kwake kwa mshahara wake, mpaka pesa zingine nilikuwa namkopa.”

ALLEN: “Duuh! Kwahiyo unashauri nisiweke mzigo.”

MIMI: “Ungekuwa huna mke ningekuweka pale, ila sitaki lawama pambana mwenyewe hapo. Umedata kwa Hilda tayari, pole sana.”

ALLEN: “Kaka acha tu, nimeoa lakini bado nahangaika.”

Wakati nilipokuwa nikizungumza na Allen, Iryn alinitumia ujumbe akiniambia kuwa ananisubiri nimpeleke Cocobeach. Alisema anahamu sana na mihogo, na pia anajisikia njaa kubwa.

Niliona ni vyema kumuaga Allen kwani hatukuwa na mazungumzo ya muhimu, na nikaona bora nimpeleke mama kijacho akale. Nilirudi haraka, nikawakuta wakiwa sebleni, kisha nikawaambia tuondoke.

Tulienda moja kwa moja hadi Coco Beach kwa jamaa wa sikuzote, na baada ya kutuona alifurahi sana kwani hakutegemea ujio wetu pale. Tuliagiza mihogo na mishikaki, na jamaa aliniomba pembeni ili tuzungumze mara moja, lakini Iryn alimzuia.

IRYN: “Kaka huwezi kuongea hapahapa mpaka pembeni?”

MIMI: “Mhh! Baby, sio kila jambo ni busara kuongea mbele yenu. Unataka kujua ni jambo gani anataka kunambia hata kama haliwahusu?.”

Niliongozana na jamaa huku tukizungumza, na habari kuu ilikuwa kuhusu Sia. Aliniambia kwamba Sia alifika pale mwezi wa nne na alimpa namba yangu ya simu, lakini nikawa sipatikani.

MIMI: “Ni kweli kaka nilikuwa sipatikani, nilikuwa nje ya nchi.”

JAMAA: “Nitakupa namba zake umtafute, subiri nichukue simu nikupe.”

MIMI: “Si unamuona mama kijacho alivyo makini kuangalia huku? Nafikiri anahisi kuna jambo linaendelea. Wewe cha kufanya nitumie namba kwenye simu, mimi nitaiona.”

Nilirudi kuendelea kujumuika nao na Iryn uvumilivu ulimshinda na akaanza maswali;

IRYN: “Darling! Anashida gani?”

MIMI: “Mambo ya wanaume mummy, hakutaka kuongea hapa mbele yenu, haitakuwa busara nikisema.”

Muda huu, Claire alikuwa akitabasamu, na nilihisi kama aliona kwamba Iryn anazingua, kwani alikuwa na maswali mengi kama vile ni polisi.

Nilianza mazungumzo na Claire na nikamuomba anisaidie kumuangalia Iryn kwa kipindi ambacho sitokuwepo. Kwa upande wake, hakuwa na shida na aliahidi kumuangalia kwa jicho la kipekee, ukizingatia kuwa ni rafiki yake wa kitambo.

Tulishinda Coco hadi jioni, kisha tukaondoka kurudi na tukamuacha Claire pale Marina kabla ya kurudi kwenye apartment yetu. Baada ya kurudi, nilifanya mawasiliano na Jane, ambaye alisema wamefika Tabora salama. Niliendelea kumsisitiza asimwambie Mary kuhusu mpango wangu wa kuja kesho.

Baada ya kuongea na Jane, nilimpigia simu Cami ili anipe ratiba ya safari ya kesho. Alisema safari itaanza saa sita mchana, hivyo ni lazima niende kwao mapema sana.
*****

Ilikuwa Ijumaa saa tatu asubuhi nilipoondoka mapema kuelekea Mikocheni kwa mzee Juma kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda Tabora. Nilipofika, nilikaribishwa sebleni na Cami, kisha akaaga akienda kujiandaa.

Nilikaa kwa muda mrefu sebuleni nikimsubiri, na baada ya nusu saa, Cami alitoka. Tulianza kuzungumza taratibu, tukijadili mambo mbalimbali. Dakika ishirini zilipita, wazee walitoka, na nilishangazwa kugundua kuwa tutaenda na Mrs. Juma. Nilimsaidia Cami kubeba mabegi na kuyaweka kwenye gari, kisha tukaanza safari ya kuelekea JNIA.

Tulipofika uwanja wa ndege, tulikutana na marafiki zake wengine wawili, hivyo tukawa jumla ya watu sita. Safari yetu ilianza saa 7 mchana kwa kutumia private jet kuelekea Tabora, na tulifika saa 9 kasoro. Tulipowasili Tabora, gari aina ya Noah lilitufikia na kutupokea, tayari kutupeleka kijijini.

Barabara ndefu ya lami ilijaa mandhari ya kijani, miti ya miembe na migomba ikipita haraka pembeni. Kulikuwa na utulivu wa kina, kama kwamba tulikuwa tunaelekea mahali pa heshima kuu na tunapaswa kuwa kimya. Mzee Pama alikuwa mtu wa heshima, na urithi wake ulikuwa na athari kubwa kwa kila mmoja wetu.

Tulipofika kijijini jioni, hali ya hewa ilibadilika ghafla na kuwa baridi kali. Bila kupoteza muda, tulienda moja kwa moja hadi kwenye lodge maarufu kijijini pale. Mzee Juma alitazama mazingira kwa utulivu kisha akasema kwa sauti ya kujiamini, "Tutafikia hapa, kule kwa Pama hapatatosha, watu ni wengi sana na hatuwezi kupata sehemu ya kulala."

Mzee alikuwa amelipia vyumba vitatu, kimoja kwa ajili yao, kimoja kwa Cami, na kimoja kwa ajili yangu. Alituambia tupumzike kwanza, kisha baadaye tutaenda msibani kutazama mazingira.

Saa moja usiku tulifika nyumbani kwa Mzee Pama na tulielekea moja kwa moja ndani, kwaajili ya kuwasalimia ndugu na kuwapa pole. Mrs. Pama alikuwa pale, pamoja na Jane, wote wakiwa na huzuni nyusoni mwao. Kulikuwa na ukimya mzito, lakini tulihisi upendo wa familia iliyoungana kwenye kipindi hiki kigumu. Mary, alishtuka sana kuniona. Macho yake yalionyesha mshangao, hakutarajia kabisa ujio wangu Tabora.

Cami na mama yake walibaki sebuleni, wakijumuika na wengine, huku mimi na Mzee Juma tukatoka nje. Tulijiunga na wazee wenzetu waliokuwa wamekaa kwenye garden, wakiendelea na mazungumzo ya taratibu, yakiwa na mchanganyiko wa huzuni na kumbukumbu za maisha ya Mzee Pama.

Kwa upande mwingine, vinywaji vilikuwa vya kutosha, soda, bia za local na za kisasa, wines na spirit zikiwa zimepangwa kwa ustadi, bila kusahau nyama choma ya ng'ombe na mbuzi. Watu walikuwa wengi, wengi zaidi kuliko nilivyotarajia. Marafiki wa Mzee Pama, wafanyakazi wenzake, na wafanyabiashara waliokuwa wakishirikiana naye walikuwa wamejaa kwenye viunga vya nyumba.

Kila kona ilijaa sauti za mazungumzo ya taratibu, huku wengine wakiwa kwenye makundi wakikumbuka safari ndefu ya maisha ya mzee Pama, aliacha alama nyingi kwa watu waliomzunguka.

Saa 5 za usiku Mary alikuja niliko na alianza kumsalimia mzee Juma na wazee wengine waliokuwa jirani. Macho yangu yalivutwa kwake, nikijiuliza, "Mary amekuja kufanya nini hapa tena?". Alikuja mpaka nilikokaa maana nilikuwa na vijana wenzangu na nikasogea kumpa seat, akakaa.

MARY: “Bae, kwanini hujanambia kama unakuja? Sijapenda.”

MIMI: “Jane anajua, ila nilitaka nikusurprise, usichukie bhana.” Huku nikimtuliza kwa kumchezea paja lake.

MARY: “Honey, nakuonea huruma, umetoka safari na sijui utalala wapi maana vyumba vimejaa.”

MIMI: “Usijali, mzee Juma alitutafutia lodge ya kufikia.”

Huku akitabasamu,

MARY: “Nimefurahi kukuona mpenzi wangu, acha nirudi ndani, kabla ya kuondoka niambie sawa?”. Mary aliambia kwa upole, akinihakikishia kwa macho ya upendo.

MIMI: “Usijali mpenzi wangu.”

Mary aliondoka nami niliendelea kupiga story na masela pale tukicheka na kubadilishana mawazo kama kawaida. Ghafla, jamaa mmoja akauliza, "Vipi huyu ni shemu wetu?"nikamjibu, "Ndiyo, bro." Kisha akaanza kumsifia Mary. "Aisee, huyu dada ni mzuri sana. Niaje sasa, una miliki chombo kikali mno, sio wa kawaida huyu." Jamaa alikuwa ni mtu wa Arusha.

Tulicheka pale kwa furaha, kila mmoja akitoa maoni yake. Jamaa wengine nao walijiunga kwenye mazungumzo, wakimsifia sana Mary. "Aisee, huyo ni pisi kali," wakionekana kuvutiwa na uzuri wa Mary. Maneno yao yalileta ufahari kidogo moyoni mwangu, nikatambua kwa undani zaidi thamani ya Mary.

Ilipofika saa sita kasoro, nilipokea ujumbe kwenye simu kutoka kwa Mary uliosomeka, "Mpenzi wangu, nimekumiss sana, naomba tuonane, tafadhali." Ujumbe wake ulinigusa sana, bila kusita nilimjibu kwa kumuandikia, "Baby, si tulikuwa pamoja hapa muda si mrefu?"

Tukaanza kuchati zaidi, akaniambia, "Naomba tukutane sehemu tulivu, tuzungumze tafadhali."

Nilijiuliza wapi ningeweza kukaa na Mary katika mazingira haya yenye watu kila kona. Nikamuuliza, "Baby, unaona mazingira haya? Unafikiri tutaongelea wapi?"

Jibu lake lilinishangaza sana, hakika sikutegemea kama angenipa wazo zito namna ile. Aliniandikia, "Mpenzi wangu, twende nje ya geti, kuna magari mengi, hatutakosa sehemu tulivu ya kuzungumza."

Nilireply, "Sawa, ngoja nianze kutoka nikague usalama, nitakutumia ujumbe uje."

Nilitoka nje ya uzio kukagua usalama, na kukuta magari mengi sana yakiwa yamepaki pale nje. Nilitafuta sehemu nzuri ya kuweza kusimama kwa usalama, kisha nikamtumia ujumbe aje. Nilimsisitiza sana afiche uso wake hata kwa kutumia ushungi, ili asiwe rahisi kutambulika.

Haikuchukua muda Mary aliwasili eneo la tukio. Aliponiona, alinikumbatia kwa nguvu na kunibusu kwa shauku, akianza kunipa ulimi wake, na tukaanza kubadilishana lita kazaa. Mary alisema tunaondoka wote kwenda kulala, lakini kwa upande wangu niliona ni jambo lisilowezekana.

Baby hili haliwezekani kabisa, na Jane atalala na nani?”

“Nimemuaga nakuja kukesha na wewe, pia nimemuachia simu yangu, lazima tuondoke wote.”

Mary alionekana kuwa na hamu sana ya kuwa nami, na nilihisi hisia zake. Nilijiwazia kwa muda pale, kisha nikaamua, "Wacha tu niondoke naye tukalale pamoja." Kurudi ndani kuaga niliona itakuwa shida, kwanza mzee Juma alikuwa bize sana na marafiki zake, wakiongea na kucheka. Nikaona haina haja ya kuvunja mazungumzo yao, bora niondoke kimyakimya na Mary.

Tulipofika lodge, tukaanza kupiga stori, na gumzo kubwa likawa suala la Mary kunizalia mtoto. Alikuwa na mawazo mengi kuhusu hilo, lakini kwa upande wangu, niliona wazi kwamba Mary alikuwa mwanamke sahihi wa kunizalia mtoto. Pia, mtoto angekuwa sehemu salama, mtu ambaye ningeweza kumtegemea kwa maisha yetu ya baadaye.

Hata hivyo, sikutaka kumlazimisha kabisa. Nilijua kwamba hili lilikuwa suala nyeti, na nilitaka afanye maamuzi kwa hiari yake mwenyewe. Nilimwambia hilo, ili asijisikie shinikizo lolote na afanye maamuzi sahihi.

Lakini mawazo yangu hayakuishia hapo. Nilianza kuwa na wasiwasi kuhusu familia yake. Nikajiuliza, ikijulikana kwao itakuwa vipi? Nini kitakachotokea hasa pindi mdogo wake, Prisca, atakapojua? Je, atalichukuliaje? Lakini mwishowe, niliamua kujituliza. Nikajisemea kimoyomoyo, "Potelea mbali, ni maisha yangu."

Baada ya nusu saa kupita nilisikia mlango ukigongwa, na nilisogea taratibu kwenda kufungua, niliuliza ‘nani?’ Akajibu ‘Cami’ ndo kufungua mlango na kutoka pale koridoni.

Cami alikuwa amevaa sweta la Prova na mkononi alikuwa kashika mfuko, alinikabidhi pale;

CAMI: “Mama alisema nikuletee, nikakukosa. Nakupigia hupokei simu, nikahisi utakuwa umerudi kulala.”

MIMI: “Ahsante sana! Nimechoka nikasema nitoroke nirudi.”

CAMI: “Haya wewe lala tutaonana asubuhi.”

Niliingia chumbani, na Mary hakuwa na nia ya kupoteza muda hata kidogo. Zoezi letu lilianza kwa kasi ya ajabu, kama vile tupo kwenye mbio za ushindani. Kadri dakika zilivyozidi kusonga, mchezo ulionekana kuwa mrefu zaidi, kila sekunde ikihesabika. Ilikuwa mechi ndefu, sauti za mashabiki zilisikika kwa mbali, zikiongezeka na kupungua, kulingana na jinsi ambavyo spidi ya mchezo ilikuwa inabadilika. Baada ya timu zote kufungana bao za kutosha, hatimaye mechi iliisha kwa timu zote kupumzika.

Saa 11 alfajiri, Mary aliondoka kurudi kwa Jane ili kusaidia na majukumu, maana ilikuwa siku maalum ya ukumbusho wa kifo cha Pama. Nami niliingia bafuni haraka kuoga na kujiandaa ili niwahi kufika eneo la tukio kusaidia kazi. Kabla ya kuondoka, nilijaribu kumpigia simu mama kijacho, lakini hakupokea. Niliwaza huenda bado amelala, kwa hiyo nikamwandikia ujumbe mzuri wa kumtakia asubuhi njema.

Nilipofika eneo la tukio, nilikutana na vijana wenzangu ambao tulikuwa tumekaa pamoja usiku uliopita. Kazi kubwa iliyokuwa ikiendelea ilikuwa ni kuandaa mahema, kupanga viti vya wageni, na baadhi ya wengine walikuwa wameenda makaburini kufanya usafi. Kila mtu alikuwa na majukumu yake, na hali ya maandalizi ilikuwa imechukua kasi.

Kwa upande mwingine, nilipowaona binti watatu wa Pama wakiwa wamesimama kwa mbali, nilisogea taratibu na kwenda kuwasalimia. Walionekana wenye furaha kuniona, na tulibadilishana salamu kwa heshima. Nilipata pia nafasi ya kuonana na Jane, na tukafanya mazungumzo ya kina, kwani nilikuwa na hamu ya kujua jinsi ndugu wa Pama wanavyomchukulia na kumtendea pale nyumbani.

Siku hii ilikuwa na ugeni mkubwa sana wa watu, na idadi yao ilizidi matarajio. Hata baadhi ya viongozi wakubwa walifika eneo la tukio. Kila mmoja kwa nafasi yake alienda kutembelea kaburi la mzee Pama, akitoa maneno ya faraja na mawazo ya dhati kutoka moyoni, kwa heshima ya kumbukumbu yake. Mazingira yalikuwa ya utulivu na ya heshima kubwa kwa marehemu.

Saa 11 jioni nilipanga niondoke nikapumzike lodge na kichwani nilikuwa na mipango ya kesho kuanza safari ya kurudi Dar es Salaam. Hata hivyo, sikuwa bado nimempa taarifa Mzee Juma, kwani alikuwa na shughuli nyingi mchana kutwa. Niliwaza kumtafuta baadaye ili kumfahamisha kuhusu mpango wangu wa kuondoka kesho.

Wakati natoka nakutana na Cami getini akiwa na binti mkubwa wa mzee Pama, na alinivuta pembeni ili tuzungumze;

CAMI: “Insider unaenda wapi?”

MIMI: “Unataka twende wote.?”

CAMI: “Kama sio mbali naweza kukupa kampani.”

MIMI: “Mimi naenda kulala ili badae niwe na nguvu ya kukesha.”

CAMI: “Halafu wewe mwanaume, kwahiyo umeamua kuhonga sweta nililokuletea jana.”

Nilicheka pale;

MIMI: “Mary aliomba, nisingeweza kumkatalia ukizingatia ni mtoto wa kike.”

CAMI: “Haya, kapumzike hata mimi nitakuja sio muda mrefu.”

Nilipanda bodaboda na kuelekea lodge, lakini nilipofika, nilikuta dada wa mapokezi hayupo, na nilikuwa tumeacha funguo kwake. Nilimuulizia lakini hakupatikana, na baada ya kupewa namba zake, nilijaribu kumpigia lakini hakupokea. Nikiwa sina njia nyingine, nikaamua kukaa kwenye sofa kupumzika kidogo nikisubiri.

Baada ya kama dakika 15, dada wa mapokezi alirudi. Alivyoniona, aliomba radhi kwa kuniweka nikisubiri, akisema alikuwa ameenda kutafuta chakula. Mimi sikuwa na la kusema, hivyo nilichukua funguo kimya kimya na kuelekea chumbani. Nilikuwa nimechoka sana, hivyo mara tu nilipofika, nikalala.

Saa 2 usiku, baada ya kuamka, nilikuta ujumbe kutoka kwa Cami ukisomeka, "Hey Insider, unavyoenda msibani nijulishe." Wakati huohuo, mama kijacho pia alikuwa amenitafuta, hivyo nilimpigia simu haraka. Iryn alitaka kujua lini narudi Dar es Salaam, kwani nilikuwa nimeahidi kurudi kesho Jumapili. Nikamwambia nitaweka mambo sawa na kuhakikisha narudi kama nilivyoahidi.

Baada ya hapo, nilimpigia simu Cami na kumtaarifu ajiandae kwa ajili ya kuondoka. Baada ya dakika 10, alinigongea ili tuondoke na tukiwa njiani, nilimwambia kwamba kesho nitaondoka kurudi Dar es Salaam. Hata hivyo, Cami alinijulisha kwamba haitowezekana kwa sababu mzee alikuwa amekata tiketi za kurudi, hivyo, tutaondoka wote jumatatu.

Baada ya kufika, niliona mazingira yalikuwa yamebadilika sana, kwani kulikuwa na projector kubwa ikionesha highlights za fainali ya ‘UEFA Champions League’. Hapo ndipo nilikumbuka kwamba leo ni fainali kati ya Manchester City na Inter Milan.

Nafasi za kukaa zilikuwa zimejaa sana, hasa kwa upande wa mbele ambapo kila meza ilikuwa na watu wanne. Nilijitahidi kutafuta sehemu nzuri mwishoni, nikaamua kukaa hapo kusubiri mechi. Haikuchukua muda, Mary alifika na tukakaa pamoja. Aliniuliza kuhusu mechi inayoendelea, nikamweleza kuhusu fainali ya ‘UEFA Champions League’. Baada ya dakika 20, Cami alifika akiwa na binti wa pili wa mzee Pama ambaye anasoma Australia, na hivyo tulikuwa jumla wanne.

Tuliletewa wine mbili, lakini binti wa Pama alisema yeye hatumii kilevi, hivyo alikunywa maji. Nilipata nafasi ya kuongea naye kwa mara nyingine na kwa undani zaidi, aliniambia kuwa alikuwa na taarifa zangu, lakini hakuwa ananijua kwa sura.

Mary alisema baada ya mechi, tutaenda wote kulala lodge, na kwa kuwa sikuwa na nguvu ya kumkatalia kutokana na mazingira, niliamua kukubaliana na mpango huo. Cami naye alisema tutaondoka wote kurudi lodge. Hii ilifanya niwe na wasiwasi, kwani nikisema tuondoke wote, atajua kinachoendelea kati yangu na Mary. Nilihitaji kufikiria jinsi ya kuondoka na hawa wanawake, bila Cami kujua kinachoendelea.

Mnakumbuka kwamba nilishawahi kuwambia kuhusu Cami na Mary kwamba wanasoma chuo kimoja, ingawa wanachukua faculty tofauti?. Tangu kipindi kile walipokutana hospitalini na kutambuana, Cami alikuwa na hisia kwamba mimi na Mary tuna uhusiano wa kimapenzi toka muda mrefu. Kwa kwenda nao wote lodge, Cami angeweza kujihakikishia kuwa hisia zake ni za kweli.

Nilimwambia Mary atangulie lodge, na mimi nitarudi ndani ya muda mfupi. Mary alipofika, alinitumia ujumbe kunijulisha kuwa amefika salama. Hapo ndipo mimi niliondoka na Cami kuelekea lodge.

Jumapili asubuhi nilionana na mzee Juma, ambaye alinipa taarifa kwamba tutaondoka kesho asubuhi kurudi Dar es Salaam na aliniaga anaenda kuendelea na kikao chake. Nilirudi chumbani kuendelea na mambo yangu, nikifanya kupitia mipango yangu na ku-update baadhi ya taarifa za biashara yangu na kampuni kwa ujumla.

Simu yangu ilianza kuita, na nilipoangalia, niliona kuwa ni mama kijacho akipiga video call. Kwa hiyo, niliamua kutoka kwenda kupokea simu mbali, kwani Mary alikuwa bado amelala kitandani. Nilienda hadi mapokezi, nikakaa na kupokea simu yake ambayo imeita kwa muda mrefu. Tulianza maongezi, ambapo alitaka kujua kama kweli narudi leo. Nikiwa na hisia mchanganyiko, nilijikuta nikimdanganya kuwa ndiyo, ingawa itakuwa usiku.

Wakati nilikuwa naongea na Iryn, simu ya Jane ilikuwa inaingia. Baada ya kumaliza maongezi yangu na Iryn, nilimpigia Jane. Aliniuliza kama niko na Mary, kwani tangu aamke hajamuona na simu yake aliiacha kwake. Nilimjibu na kumwambia kuwa Mary yupo pamoja nami na atarudi hivi karibuni.

Mary alikuwa bado amelala, hivyo nilimuamsha ili kumpa taarifa kuhusu Jane aliyekuwa akimtafuta, na alisema atarudi mchana. Nilimwambia ajiandae ili tukatafute kitu chochote cha kula, na alikubaliana kwani pia alisema anasikia njaa. Vita ya usiku ilikuwa ngumu sana.

Tulienda katika mgahawa mmoja wa karibu na lodge, tukapata supu. Katika muda huu, nilitumia nafasi kumuuliza Mary atarudi lini Dar, lakini alijibu kuwa bado hajapata taarifa kutoka kwa Jane. Baada ya hapo, tulirudi lodge na kwa bahati mbaya tukakutana uso kwa uso na Cami pale mapokezi.

Cami alionyesha kushangazwa kumuona Mary maeneo haya, na nilihisi kama alihisi kuwa kuna something fishy kinaendelea kati yetu. Tulisalimiana, na mimi nikaondoka kuelekea chumbani nikiwaacha wakiendelea kuongea.

Mchana tulienda nyumbani kwa Pama ambapo watu walizidi kuja kutembelea kaburi lake na kuondoka. Pia, nilimuaga Jane pamoja na ndugu wengine wa Pama, akiwemo mama yake mzazi. Nilifanikiwa kuonana na Mrs. Pama, nikamsalimia na kumpa pole kwa mara nyingine tena. Mrs. Pama alifurahi sana kuniona na alinishukuru kwa ujio wangu.

Niliendelea kushinda eneo la tukio hadi jioni, na baada ya kuona kwamba hakuna jambo muhimu lililobaki, niliondoka kurudi lodge ili nijiandae kwa safari. Mama J alinipigia simu na kuuliza nitarudi lini nyumbani, kwani muda umeenda na bado sijarudi, hivyo alikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hali yangu.

Baada ya lisaa kupita, Mary alikuja lodge akiwa na karata, na tukaanza kucheza mchezo wa 'last card'. Tulikubaliana masharti, mimi nilikuwa naweka pesa kwa kila mzunguko, ambapo kama Mary atashinda, angechukua 10,000. Kwa upande wake, tuliweka sharti kwamba ikiwa ningeweza kumshinda, angevua nguo moja kwa kila mara ningeweza kumshinda. Na kama ningemvua nguo zote, ningeonekana mshindi, na mchezo wa kwichikwichi ungeanza. Ilikuwa ni game ndefu sana ambayo mshindi kupatikana ilikuwa ni ngumu, lakini baadae uvumilivu ulitushinda tukaanza kupeana kwichikwichi.

Jumatatu asubuhi na mapema tulianza safari ya kurudi Dar es Salam na tuliwasili JNIA saa sita mchana. Kwa upande mwingine mama kijacho wangu alikuwa amenuna sana, maana nilimdanganya nimepitia Dodoma mara moja kuweka mambo sawa.

Gari lilifika kutuchukua pale JNIA, na safari yetu kuelekea Mikocheni ikaanza kwa kutumia barabara ya Posta ili kuepuka foleni. Nilipendekeza wanishushe 'Dar Free Market' ili iwe rahisi kwangu kufika Masaki. Mzee Juma aliniambia kuwa baada ya kumaliza mipango yetu, tuwasiliane kwa ajili ya kupanga tukutane tena.

Nilichukua bodaboda ya kunipeleka na ndani ya muda mfupi niliwasili, na kwa bahati mbaya Iryn hakuwepo. Nilimpigia simu akanambia yuko kwa Claire na atarudi sio muda mrefu, hivyo niliingia bafuni kuoga.

Baada ya hapo nilimkumbuka Sia na nilitamani sana kuongea naye maana ni muda mrefu sana ulikuwa umeshapita. Nilimpigia simu na iliita kwa muda mrefu na akapokea;

MIMI: “Hello Sia, ni mimi Insider.”

SIA: “Insider au Khalid?”

Nikakumbuka kuwa nilimdanganya jina langu siku tuliyokutana Coco beach;

MIMI: “Nimekumiss sana mrembo.”

SIA: “Namba yako ilikuwa haipatikani mpaka nikahisi labda kaka alikosea kuniandikia, hata baada ya kurudi tena alinambia ipo sawa nayeye alisema hupatikani pia.”

MIMI: “Ni kweli nilikuwa nje ya mji, lakini nimerudi. Nambie lini tuoanane maana nina maongezi muhimu sana na wewe.”

SIA: “Kesho kutwa nina safari ya kwenda nje, kesho nitakuwa busy sana, naomba tuonane nikirudi kama inawezekana.”

MIMI: “Alright, unatarajia kurudi lini?”

SIA: “After one week, nitakuwa nimerudi.”

MIMI: “Alright, no problem.”

Baada ya kuagana na Sia, nilipanda kitandani kisha nikalala, ajabu sikuwa na usingizi kabisa, nilijikuta naanza kuingia kwenye mawazo tofauti kuhusu maisha yangu yote kwa ujumla.

Baada ya masaa 2 kupita, Iryn alirudi na habari kubwa aliyonipa ni kwamba anajisikia dalili za kujifungua, hivyo ijumaa ataondoka kwenda South Africa. Nilitamani kujua huko South Africa atajifungulia wapi? Na alisema atajifungulia kwake.

Kujifungulia kwake niliona ni wazo baya, kwani alihitaji kuwa na mtu mwenye uzoefu na haya mambo;

MIMI: “Baby kwanini usiende kwa mzee uwe karibu na mama mdogo?”

IRYN: “Kwa mama mdogo? You can’t be serious. Mara 100 nikaenda Ethiopia kwa mama mkubwa nitakuwa salama.”

MIMI: “Unamaanisha mama mdogo atakufanyia kitu kibaya? Sindo wewe ulisema mpo cool?”

IRYN: “Anaweza kupretend, lakini hawezi kuwa na upendo wa kweli.”

MIMI: “Sasa utakuwa na nani huko South, ushaanza kunipa wasiwasi mapema hivi.”

IRYN: “Dada yangu ‘Vivian’ wa Ethiopia atakuja Dar siku ya alhamis na tutaondoka wote kwenda South Africa.”

Niliwaza pale nikaona kuna haja ya kuwasiliana na dada yangu na kumpanga kuhusu hili suala ili kama itawezekana, bhasi awahi kwenda South Africa na wifi yake.

Nilimpigia simu Sister na kuzungumza naye kuhusu suala la Iryn. Alisema kwamba lilikuwa kwenye mipango yake, lakini alikuwa anasahau kuniuliza tarehe sahihi ambayo Iryn anaweza jifungua. Sister aliongeza kuwa atakuja Dar siku ya Ijumaa, na siku ya Jumamosi wataondoka pamoja na Iryn kuelekea South.

Nilimpa Iryn taarifa kuhusu safari yake ya kuelekea South pamoja na dada yangu. Alifurahi sana kusikia habari hizi na alinishukuru kwa kumjali. Aliomba nijiandae ili tuende Karambezi kwa ajili ya chakula cha mchana.

Tukiwa Karambezi, tulipanga mipango mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuitisha kikao cha dharura kitakachohusisha viongozi pekee. Pia, tulijadiliana kuhusu sakata la ofisi ya Mikocheni, kwani muda tuliopatiwa ulikuwa umekwisha na tulitakiwa kuondoka kutoka ofisini.

MIMI: “Baby, hivi kwanini ulishindwa kupanunua pale na uwezo unao.”

IRYN: “Nilikuwa tayari kupanunua, tatizo bei ni kubwa sana mpaka nikakata tamaa.”

MIMI: “Alitaka kiasi gani?”

IRYN: “Alikuwa anaanza na billion 1, mwisho kabisa alisema million 900. Unaona hio bei ni sawa na thamani ya kiwanja? Ndomana niliamua kuacha tu.”

MIMI: “Duuh! Mzee wa watu anazingua, au sababu ni Mikocheni?”

IRYN: “Hata kama ni Mikocheni kuna maeneo ukiambiwa hiyo amount unatoa maana unaweza kufanya investment yoyote na pesa yako ikarudi, pale labda ujenge apartments napo pesa yako kurudi itachukua muda mrefu sana.”

MIMI: “Wewe ulikuwa tayari kulipia kiasi gani?”

IRYN: “Kwa 500M ningelipia maana ni fair price. Lakini bado alinikatalia akasema ninamtukana.”

MIMI: “Bhasi, tutatafuta plan B.”

IRYN: “Nakuachia hii kazi, ijumaa tunapokutana uwe na majibu juu ya hili.”

Tulitumia masaa mawili pale Karambezi, kisha tukaondoka kurudi kwenye apartment yetu. Baada ya kufika, nilianza kumtengeneza nywele zake na kuzipaka mafuta, kwani alisema hana mpango wa kwenda salon au kusuka. Wakati huo, simu yangu ilikuwa ikilia, na aliichukua kwa haraka sana, alisema, “Hivi huyu Asmah anataka nini kwako? Nafikiri hanijui vizuri.”

TO BE CONTINUED.
be blassed bro
 
Unamsifu Mary ana akili ila naona ni bint mpumbavu hana akili kwa sababu kwanza mwanaume wa mdogo wake yaani X unaombwa vipi kuzaa na mwanaume ambae ana mwanamke kama mkewe wana mtoto bado ana mwingine ana mimba yake na wote hajaoa anaomba uzae ina maana atakuwa single mama malezi ya mama tu sio na baba kwa pamoja 😂ilitakiwa akatae hapo hapo ibaki anadinywa basi ila kwa alivyo mpumbavu atabeba mimba.

Insider ni kama wanaume wengi walivyo malaya sijui Mrangi sio kwa kupenda papa huko halafu roho mbaya ubinafsi kutaka kumzalisha bint wa watu unaharibu future yake huna mpango wa kuowa gonga tu upite sio uzalishe halafu hujifunzi kutokana na makosa.
 
Kwani amesema hatamuoa Mary?
 
hilo n suala bnafs mdogo angu
kaa chini kula mua skiliza stor uburudke yaishe mengne anajua mungu kama ni kwel au laaah
kikubwa n burudan mana sote hatuna hakika kikubwa iman mana kila mmoja ana yake
kwaio kijana tuliza kula mua na stor usikilizie utamu😁
Weeee, mi mzee wewe. Wa umri wangu humu ni kina Watu 8 nk. Tuendelee kuburudika na story ya mchumi msomi bwana INSIDER MAN
 
Asmah😂😂😂
 
Hii stori ipo interesting inafundisha na inafikirisha!!🤔😊

-Mwanamke una gubu,kitandanai hujitumi,kitu kidogo unafungasha kwenda kwenu,una safari kusalimia kwenu unamuachia mumeo week tatu nne na hamu zake,akichwpuka unalalamika unafungasha kwenu!!

-Tangu lini kukawa na ubest friend kati ya mwanaume rijali na mdada unaona kabisa pisi Kali hata bibi yako aanakuonya kabisa we hutilii maana I,boss gani anaipenda familia yako hivo?sawa upendo ila shtuka

-washkaji na maarafiiki wote wanajua na kumpa Hongera mumeo Kwa kumpa hawara mimba,we huna habari,huna hata shushushu wako,wanakuzoom tu.
Umelala unafua kibarazani unacheza na mtoto unatoka mtaani siku zinaenda unajua mumeo Yuko mkoani kikazi kumbe kaja Yuko mtaa wa pili tu hapo na hawara ake Kwa raha zao na watu wanajua.we hujui maskini.ndugu wa mume wanajua we hujui.

-dada wa kitasha anaumia sanaaa akiona mwanaume ana mwanamke mwingine akisahau ye pia ni mchepuko anamuumoza mwenzie mwenye mume.hafikirii hisia za wengine,zake ndo anajali bila kuwaza hata yeye anakosea Kwa mwingine.peisca anapambania kumtukana iryn bit*ch kumbe nae anatoka na mwanaume wa mtu🤣
-binti unamtamani ex wa mdogoako,unajua ni mume wa mtu,ana mchepuko una mimba yake nawe unataka kuwa mchepuko unakubali kumzalia..wadada wakishua wakipenda🤣

Mwisho wa siku nimejifunza wanaume kuchepuka haiepukiki pia.hata asipopenda bado atapendwa.ni yeye tu kukosa msimamo

Bado naendelea kujifunza
 
Hapo kwenye kuwa na shushushu nimepapenda 🤣 mama mjengo alitakiwa awe na shushu wake yaani mume anapuyanga town ye katulia tu anajua yupo Dom ni dharau. Mbaya zaidi sio mnyonge kivile pesa anayo
 
Back
Top Bottom