Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Sahivi ruksa kunishauri kuhusu sakata la mama J. Huko nyuma watu mlikuwa na hisia kali sana nilikuwa nacheka tu, mlikuwa mnatoa ushauri kwa mambo yaliyopita.

Kwasasa unaweza kushauri kwa suala la mama J, maana siku atakayojua ukweli anaweza nichoma kisu. I feel karma, ila ninaamini kila kitu kinatokea kwa sababu, ni mipango ya Mungu.
Ile biasharaa yako ya lubricants and cars spare parts bado unaendelea nayo.
 
Sahivi ruksa kunishauri kuhusu sakata la mama J. Huko nyuma watu mlikuwa na hisia kali sana nilikuwa nacheka tu, mlikuwa mnatoa ushauri kwa mambo yaliyopita.

Kwasasa unaweza kushauri kwa suala la mama J, maana siku atakayojua ukweli anaweza nichoma kisu. I feel karma, ila ninaamini kila kitu kinatokea kwa sababu, ni mipango ya Mungu.
Nawaza tu, simfahamu Iryn wala mama J lakini moyo wa mtu kichaka, giza nene

1. Mama J akipima akaona jinsi ume'faidika' kutoka kwa Iryn, anaweza akaweka kwenye mzani akaona sio mbaya. Wacha mfaidike wote, akubali aolewe aache lipite kwa makubaliano hautakuwa na makandokando mengine

2. Hell hath no fury as a woman scorned. Mama J mtoto wa kaskazini kule. Anaweza akakubali kuolewa na kuvumilia just kwaajili ya issue za mali. Kumbuka kuna influence za ndugu na nani, muda si muda ukapigwa na tukio. Nadhani unaelewa nisiende mbali, jiongeze...

3. Iryn doesn't need you, she wants you mipango yake iende sawa. You just happened to be the right guy for the job, both jobs (sperm donor na msimamizi mzuri wa mali)

4. Sikiliza mama insider atakachokuambia, mama zetu wanaona mbali
 
SUMMARY YA KILICHOENDELEA

Just in case:

Iryn anatarajia kujifungua jumapili hii kwa taarifa za haraka nilizopata.

Mama mkubwa wake kavimba sana baada ya kupata taarifa binti yake anamimba nyingine. Kwasasa ndugu anao wasiliana nao ni upande wa mama yake mkubwa tu, ameamua kujitenga na tamaduni za Ethiopia.

Griezmann alikuja kujua Aria ni mtoto wangu, alimind sana.

Marehem mama Iryn, ndiye aliyeongea na mama Janeth azae na Mzee Virgil.

Sumaiya anatarajia kuolewa mwezi wa 11, alibahatika kupata tajir, atakuwa mke wa 3. Maisha yake kwasasa ni mazuri, hadi kazi kwa mama aliacha.

Dullah alipata watoto mapacha mwaka huu, alinivimbia sana.

Prisca alikuja kufahamu kinachoendelea kati yangu na dada yake. Walipigana sana, hadi mama yao kuwakalisha kikao.

Tangu Iryn ajifungue, hajawahi kuonana na mama J.

Ukweni wanaforce sana suala la ndoa maana niliwaahidi mwaka huu ningetisha, lakini sijafanya hivyo.

Asmah, hatuna mawasilino sana, alienda Qatar kusoma, sidhan kama anampango wa kurudi Dar.

Lucy tuligombana na aliacha kazi, hatuna mawasiliano kwasasa, sijui maendeleo yake pia. Bad news mwaka huu alifiwa na mama yake, nilishawagusia kuhusu afya ya mama yake.

Jane tuko cool hadi sasa, tulifungua biashara ya pamoja Kkoo, tunauza mapazia, urembo nknk. Sia ndio alinipa hizi connection, nikaamua kushare na Jane. Mdogo wake Vicky kavalishwa pete tayari, mwakani tunaweza kula pilau.

Kingine mama wawili ana mtoto mchanga, kupitia mwanaume mwingine.

Mwisho, mama Janeth alinusurika kifo Palestine, ni Mungu alimsaidia. Mwakani ataondoka rasmi Tanzania, amehamishiwa HQ.
INSIDER MAN ulitudokezea kuwa ulimpoteza mtu mmoja wa karibu! Ni nani huyo mbona mpaka hapa ujatuambia? Naomba unitag ikikupendeza!
 
INSIDER MAN unatumiaga condom kwa hao manzi akina Mary, Sumaiya, Asmah au unapekua? Uogopi umeme na kupoteza maisha na hao uwapendao? Unawaaminije kama unapekua?
 
hongera Insider Man .. hakuna mkamilifu ila muhimu kujua ulipokosea na kusawazisha.... Allah azidi kubariki
 
INSIDER MAN unatumiaga condom kwa hao manzi akina Mary, Sumaiya, Asmah au unapekua? Uogopi umeme na kupoteza maisha na hao uwapendao? Unawaaminije kama unapekua?
Ni asilimia ndogo sana walioa kutumia condom wakichepuka na ikifanyika ni siku za mwanzo wakikutana tena wanaaminiana bila kupima. Condom kwa mwanamke mzuri ni changamoto sana. Huu ni mtihani.
Ila kuna group moja la whatsapp malaya wanajiuza kwa kweli condom ni muhimu unaweza punguza makali fulani. Kuna wanawake wazuri mnooo wenye figure hatari wanadanga balaa. Nawengine wana kazi na biashara zao nje ya umalaya
 
BONUS CHAPTER 1

Nimeanza kuandika story hii nikiwa South Africa, ule wakati ambao nilikuwa na muda wa ziada, ndipo nilipoanza kuandika Season 1 na kuwapostia. Lengo langu kuu ni kuwapa ujumbe kuhusu safari ya maisha yangu, kutoka mwanzo hadi sasa, maisha ambayo bado ninaishi. Sikutaka kukata tamaa, hata baada ya kumaliza mkataba wangu na taasisi X niliamua kujiingiza kwenye uber, huku ndo nilikopata mafanikio makubwa sana.

Nilichowaandikia ni kama asilimia 30 ya maisha yangu; bado kuna mengi ambayo sijagusia kutokana na sababu za usalama wangu pia.

Kwa ufupi, tangu Iryn alipojifungua, maisha yangu yalianza kubadilika kwa kasi sana. Niliamua kuelekeza nguvu zangu kwenye familia zangu na kujituma zaidi kutafuta hela kwa bidii.

Mwezi Januari 2024, nilikutana na mzee na kumueleza kuhusu suala la kuzaa na Iryn. Alishtushwa sana na habari hizi, na hakusita kunilaumu vikali juu ya hilo. Hata hivyo, nilijitahidi sana kujitetea, hasa kwa kutumia mbinu nzuri ambazo Sister aliniambia.

Mzee aliweza kuelewa hali halisi, na mwezi Februari mwaka huu alikutana na Iryn. Tulienda Zambia kwa ajili ya hili, na baada ya kumuona Aria, mzee alikiri kwamba ni damu yetu. Changamoto iliyobaki sasa ni namna ya kumwambia mama yangu mzazi. Tumepanga kumtaarifu mwezi huu, na safari hiyo itakuwa mimi, mzee, na sister.

Kuhusu mama J, tuko shwari kabisa, na upendo kati yetu umeendelea kukua kwa kasi; tunapendana sana. Junior mwaka huu alianza shule na anaendelea kufanya vizuri sana darasani. Kampuni ya Masaki bado ipo na inaendelea kufanya vizuri sana, na pia mama mtoto amefungua biashara nyingine hapa Dar es Salaam.

Kuhusu mtoto wetu Aria, sasa ana mwaka mmoja na miezi mitatu, na tumefanana sana. Ninajitahidi kumtembelea mara kwa mara kule South, hata wiki iliyopita nilikuwa huko kumuona.

Habari njema nyingine ni kwamba mwezi wa 10 huu ninatarajia kupata mtoto wa pili na Iryn. Baada ya kuja Disemba mwaka jana, tulikutana na hali hiyo ikapelekea kushika mimba. Ingawa hatukupanga hili, hatukuwa na namna zaidi ya kukubaliana yeye kuzaa. Hali hii imefanya niwe nasafiri mara kwa mara kwenda South Africa.

Kuhusu Mary, alipata kazi Mwanza katika moja ya taasisi nyeti inayoshughulika na masuala ya BOP. Hatuko kwenye mahusiano ya kimapenzi rasmi, lakini bado tunakutana kisela.

Mipango yangu ni kuhakikisha kwamba kufikia mwakani kila kitu kiwe wazi kwa mama J. Hata hivyo, hili linasubiri wazazi watoe maamuzi, kwani tunasubiri kuona mama atachukua hatua gani akijua ukweli. Nia yangu ni kumuoa mama J kwa kufunga naye ndoa, lakini hilo litafanyika tu endapo atajua ukweli na kukubali kwa hiari yake.

Mbali na mama J, pia nina mpango wa kumfanya Iryn awe mke wangu wa pili. Sijui wazazi watasema nini kuhusu hili, lakini anatarajia kupata mtoto wa pili. Hali hii inahusisha majadiliano mazito na maamuzi ambayo ni muhimu kabla ya kuchukua hatua zozote.

Nitarudi kuwapa hadithi fupi pale ambapo nitamuweka wazi mama J kuhusu hili suala. Sijui itakuwa lini—labda mwakani au baada ya miaka miwili au mitatu. Lakini nitawapa mrejesho wa kilichotokea kwa kuwapa Season 3 au lah. Nitawapa muendelezo wa mambo yalivyokuwa, kuanzia niliporudi Dar es Salaam mwezi Julai 2023. Hapa katikatika nimepitia mambo mengi sana, hadi sasa ni vile hamjui kinachoendelea nyuma ya pazia, kumekuwa na vikao vingi sana.

Mwisho kabisa, mwakani Mungu akijalia nitaondoka Tanzania na familia yangu kwenda kufanya kazi nje. Jambo la muhimu tuendelee kuombeana uzima na mapambano mema, tuache chuki na Roho mbaya.

Bonus, inayokuja tutachambua wote fursa zinazopatikana Dar es Salaam na huenda nikawa na thanks giving kwa baadhi ya watu watakao bahatika, nikaangalia namna ya kuwa support kwenye harakati zao. Lakini hadi kufikia sasa nimeshatoa kwa watu wengi tu, ambao walikuwa wanakuja inbox na sababu zilizonyooka, na wengi ni matapeli.

Tukutane kesho!
Asante Sana INSIDER MAN
Umetutendea haki kwa kweli.

Ila usinisahau kwenye ufalme wako unajua nini namaanisha boss.
Mambo yamekuwa sio kipande hiki.
 
3. Iryn doesn't need you, she wants you mipango yake iende sawa. You just happened to be the right guy for the job, both jobs (sperm donor na msimamizi mzuri wa mali)
Kama atapaelewa vizuri hapa Insider nae inabidi ajitahidi amtumie vizuri Irene ili siku mambo yatakavyokuwa ndivyo sivyo awe amefaidi vya kutosha. Iwe Both team to score.

Ukweli mchungu ni kwamba hakuna narudia duniani hapa hakuna mwanamke anayekubali kushare au kuwa mchepuko ( second ) kama hakuna anachofaidika so Insider asorelax akijua Irene kampenda ana plan zake akae kwa machale.
 
Wengine umeturuka maswali yetu🤔🤔🤔
Kubali maoni ya watu, hata usemeje ukasirike.. Mary kicheche 🤮atakumaliza one day mkimbie haraka 😅😅😅

Ila tukia umekuwa mmmmmh.. Kubali nondoz ukipewa hata kama haupendi.

As umeruka makusudi haya tufukuze wengine kwa uzi wako.. Ciao utaelewa si Iryn kakufundisha na Gize wake eeeeh nikuite wivu. Mama J subiria tu, ila usimuumize tulia acha kuranda randa nae akipata marafiki wa kiume kama akina Jane akafungua nao biashara eeeeh.. Kweli haujamtamani Jane ukamsaidia uoekwe wewe wewe mmmmmh!!!
cocochanel Mary kakukosea nini? 🤣
 
Back
Top Bottom