Jinsi Bikra Maria alivyompa mtihani kiongozi wa Kanisa, Nabii Zakaria..

kwahiyo wakati Yesu anaanza kazi ya kutangaza ufalme wa Mungu akiwa na umri wa miaka 30 Yosefu alikuwa ameshagonga miaka 100?
Wakati Yesu anaanza kazi ya kutangaza ufalme wa Mungu Yosefu kuna uwezekano mkubwa alikuwa marehemu. Nasema kuna uwezekano kwa sababu hakuongelewa so hakuna uhakika kutoka biblia(kabla sijaombwa mstari wa kifo chake) lakini kuna viashiria.

Yesu akiwa msalabani alimkabidhi Mama yake kwa Yohana (Yohana 19: 26-27) ikimaanisha kuwa Yosefu alikuwa marehemu hivyo mama yake angebaki mpweke. Sababu hii ya kifo cha Yosefu ndiyo hupelekea dhana ya kuwa Yosefu alikuwa mzee hivyo alikufa kutokana na uzee.

Kingine ni kuwa Maria anaaminika kubaki bikra hadi kufa kwake. Hii inaweza kuaminika endapo tu Yosefu alikuwa mzee wa makamo hivyo hakuwa na shauku na mwali wake.

Vilevile Yesu alikuwa na kaka zake kama inavyoelezwa kwenye injili ya Mathayo 13:55-56 wakitajwa kwa majina Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda. Hawa wanaaminika walikuwa watoto wa Yosefu aliwapata kabla ya kuwa na Maria. Hitimisho ni kuwa maandiko japo hayajasema ila yanaashiria Yosefu alikuwa mzee wa makamo.
 
Aisee
 
Asante sana kusaidia kunyoosha maelezo. Umeshiba neno. Nikifungua kanisa utakuwa mama mchungaji (kidding).

Kwa kujazia tu, Mzee Yosefu (nimezoea Joseph au Yusuf) alikuwa na hekima sana. Nadhani alitumiwa ujumbe wa kutomnajisi bibie Maria kwa sababu za kiungu ambazo pengine hazijajulikana bado.

Hiyo line ya mwisho hapo ni mawazo yangu binafsi
 
Mtaendelea kudanganyana hadi mtaingia kaburini aliye kuwambia Zakaria alikuwa Padri nani
 
Mtaendelea kudanganyana hadi mtaingia kaburini aliye kuwambia Zakaria alikuwa Padri nani
Ila mie siwezi mbishia mleta mada kuna wengine wanae yesu mwingine labda ndiye
anamsimulia sio huyu Yesu Kristo aliye sulubiwa msalabani
 
Hivi anakuwaje bikra maria na wakati umeshasema aliolewa na joseph ??

Au mimi ndio sijakuelewa??
 
Nabii Zakaria na kanisa wapi na wapi

Zakariya alikuwa Kuhani Mkuu wa Hekalu katika kipindi chake. Kipindi hicho halikuwa linaitwa Kanisa bali Hekalu ambalo ni Jumba la Ibada sawa tu na useme Kanisa kwa sasa. Na ndiye mlezi wa Bikra Maria..
 
Hivi anakuwaje bikra maria na wakati umeshasema aliolewa na joseph ??

Au mimi ndio sijakuelewa??
Joseph hakumuingilia. Roho Mtakatifu alitangulia akavuruga mipango. Ndio maana kuna wengine wanagoma kuiita ndoa bali uchumba tu.
 
Ila mie siwezi mbishia mleta mada kuna wengine wanae yesu mwingine labda ndiye
anamsimulia sio huyu Yesu Kristo aliye sulubiwa msalabani
Sawa tu. Masuala ya imani hayataki kulazimishana. Na nilishasema sio lengo langu kujadili imani.
 
Mtoto wa wa Zakaria na Elizabeth ni Yohana mbatizaji aliyekatwa kichwa na mfalme kabla hatavya Yesu kusurubiwa
Naam. Na ndiye niliyemtaja hapo awali. Aliyeenda kuishi msituni akila asali na nzige baada ya wazee wake kufariki dunia ili kujitenga na maovu ya walimwengu..
 
Hapo ndipo kanisa katoliki linawaacha na kubakia kanisa lenye weledi na hazina kubwa sana duniani.

Wengine vyanzo vya habari za Mungu ni biblia tu.
 
Hapo ndipo kanisa katoliki linawaacha na kubakia kanisa lenye weledi na hazina kubwa sana duniani.

Wengine vyanzo vya habari za Mungu ni biblia tu.
Biblia pekee haitoshi. Yameandikwa yale machache muhimu tu, very selective.

Na sidhani kama Bible inakataza kutumia taarifa kutoka vyanzo vingine kwa maana itakuwa ajabu kwamba yote yatoshe mule. Haiwezekani!
 
Hivi anakuwaje bikra maria na wakati umeshasema aliolewa na joseph ??

Au mimi ndio sijakuelewa??
Na utaendeleaje kuwa bikira angali umeshazaa hata kama aliyekupa mimba ni njiwa ukweli utabaki kwamba tupu yako imefunguka kwa hiyo swala LA ubikira ni ngonjera na mbembwe za kiimani.
 
Na utaendeleaje kuwa bikira angali umeshazaa hata kama aliyekupa mimba ni njiwa ukweli utabaki kwamba tupu yako imefunguka kwa hiyo swala LA ubikira ni ngonjera na mbembwe za kiimani.
Bikra ya kutoingiliwa na bikra utepe. Maria alibakiza Bikra ya kutoingiliwa, utepe ulikatika punde tu alipomzaa Jesus. Simple logic.
 
Bikra ya kutoingiliwa na bikra utepe. Maria alibakiza Bikra ya kutoingiliwa, utepe ulikatika punde tu alipomzaa Jesus. Simple logic.
Sio kweli! Maria alikuwa mke halali wa Mzee Joseph. Kugundulika kwa mimba changa ya Yesu hakukuzuia mahusiano ya kindoa baina ya Maria na Joseph. ..Jiongeze!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…