Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maria kaendelea kuzaa na Joseph? Hapana.Hivi nyie watu mnasoma Bible ipi hadi leo mnasema Bikra Maria! Basi Mama ngu ni Bikra bado kwani alinizaa na ka endelea kuzaa , upo wapi Ubikra wa Maria wakati aliendelea kuzaa na Joseph kwa kawaida tu hamjui kuwa YESU anao Ndugu wa Damu kwa Maria?
Unataka kusema nini?Nabii Zekaria aliishi miaka 500 kabla ya Yesu kuja dunia. Tofautisha kati ya kuhani na nabii.
Swali zuri.hivi kanisa na maria nani wa kwanza kuzaliwa, maana kwa uelewa wangu huyu akilelewa ktk sinagogi ambayo ni sehemu takatifu kwa imani yao wakati huo. je kipi sahihi kanisa au sinangogi naomba ufafanuzi
Mzee Zakaria alikuwa kuhani na nabii au kuhani tu?Karibu tena mkuu..
Alikuwa Kuhani. Inadaiwa alikuwa Nabii pia kwa kigezo cha ushirika wake na Mungu hata akamtumia Malaika kumbashiria atapata mtoto wa uzeeni.Mzee Zakaria alikuwa kuhani na nabii au kuhani tu?
je unakubaliana na mimi kuwa Maria akilelewa katika sinagogiSwali zuri.
Mfumo wa Kanisa umerithi ule wa Masinagogi. Hata misikiti pia. Yaani ni lile kusanyiko la watu mahala pamoja (jengo, hekalu) kwa ajili ya ibada.
Enzi za Maria, viongozi wa mahekalu walikuwa wanaitwa Makuhani ambao siku hizi wanaitwa Wachungaji.
Inawezekana kuna maelezo mazuri zaidi ya haya!
Hekaluni, Sinagogini, Msikitini yote ni yale yale. Point muhimu ni alilelewa kwenye nyumba ya ibada.je unakubaliana na mimi kuwa Maria akilelewa katika sinagogi
UMEIOKOTA WAPI HII HABARI?? Maana kwenye biblia haipo labda vitabu vingine vya dini zingine ila sio ukristo maana haipo katika hivyo vitabu,labda ni story yako ka kubuni tu umejiskia kutunga utakavyo wewe?!Wadau wa fikra,
Nafahamu kuwa muongozo wa Jukwaa hili unatutaka tuweke serious reports & discussions on Corruption, Politics na etc kwa ajili ya mijadala yakinifu. Tofauti na Jukwaa la Dini ambalo lengo lake kuu ni kuhamasishana kuhusu masuala ya kiimani na kufundishana yale yaliyo mema.
So, uzi huu hauna lengo la kuhamasishana kuhusu imani bali kujadiliana kwa kina kuhusu mambo ya kale (historical facts) yanayoingiliana kidogo na dini/imani. Naamini nimejaribu kuweka utofauti ili isionekane naleta mjadala wa kidini k
Na historia maarufu ya Bikra Maria sasa inaanzia hapo na kuendelea. Kuna haja ya kuisimulia zaidi?!
naisubiri ili niisomeKaribu mkuu. Leo nitaandika nyingine.
Ni kweli mkuu.UMEIOKOTA WAPI HII HABARI?? Maana kwenye biblia haipo labda vitabu vingine vya dini zingine ila sio ukristo maana haipo katika hivyo vitabu,labda ni story yako ka kubuni tu umejiskia kutunga utakavyo wewe?!
This is humility. Great!!!Napenda maoni mbadala lakini yasiwe conclusive kama hivi. Umeniita Muongo lakini ukashindwa kuweka ukweli sijui unamaanisha nini?
1. Unasema hakuna ushahidi kuwa Joseph alikuwa ameoa, mimi nimekupa clues za ushahidi mpaka jina la mkewe na idadi ya watoto waliozaa (ninayafahamu mpaka majina yao wote). Nadhani hapo palitosha kukupa sehemu ya kuanzia kwenda kufuatilia zaidi mkuu wangu.
2. Sikukataa kuendelea na story kwa sababu ulizozitaja wewe mkuu. Nimeeleza vizuri tu kwamba story inavyoendelea kila mtu anafahamu kwa kuwa masimulizi ya Bikra Maria kupokea ujumbe wa Mungu yapo popular na ndicho kilichokuwa kinafuata. Mimi nilitoa background tu ambayo wengi hawaifahamu kwa sababu haipewi kipaumbele ila IPO.
3. Unasema nimeshindwa kutoa maandiko halafu hapo hapo unakiri nimeeleza kuwa source ni Injili ya Luka, kipi ni kipi boss?
4. Asante kwa kunisahihisha ndugu yangu. Hivi ndivyo yapaswa kuwa. Nilisahau kutumia Mgane badala ya Mjane. Ni makosa ya kawaida hayo boss kikubwa ujumbe umeeleweka.
Cha msingi, naomba nieleweke kuwa sijaweka historia hii kwa lengo lolote baya, ni katika kupeana elimu tu. Nilitoa ruhusa pia ya kuulizana maswali na kueleweshana juu ya niliyoyaandika. Ni vyema sehemu unayohisi nimepotosha, ukaweka usahihi wake ili twende pamoja kiongozi.
Au unaonaje?