Jinsi Bikra Maria alivyompa mtihani kiongozi wa Kanisa, Nabii Zakaria..

Unaweza nitumia magombo uliyokuwa unayatumia kusoma na mm nifanye kupitia pitia tu,,,
Wadau wa fikra,

Nafahamu kuwa muongozo wa Jukwaa hili unatutaka tuweke serious reports & discussions on Corruption, Politics na etc kwa ajili ya mijadala yakinifu. Tofauti na Jukwaa la Dini ambalo lengo lake kuu ni kuhamasishana kuhusu masuala ya kiimani na kufundishana yale yaliyo mema.

So, uzi huu hauna lengo la kuhamasishana kuhusu imani bali kujadiliana kwa kina kuhusu mambo ya kale (historical facts) yanayoingiliana kidogo na dini/imani. Naamini nimejaribu kuweka utofauti ili isionekane naleta mjadala wa kidini kwenye jukwaa hili makini.

Kupitia historia fupi ya Maria, nitaeleza mtihani wa Bikra Maria kwa Mkuu wa Kanisa/Hekalu alimolelewa, ambaye alikuwa ni Nabii Zakaria. Ni matarajio yangu tutaulizana maswali na kurekebishana kwa uungwana ili sote tuweze kuelimika na kufahamishana mambo mengi tusiyoyajua.

Hebu tuipitie historia hiyo kidogo..

Wazazi wake
Maria alizaliwa na Mzee Joachim na Bi. Anna ambao walikuwa ni wachamungu haswa. Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachamungu wa enzi hizo, Mungu aliwapa mtihani wa ugumba Mr. & Mrs Joachim kiasi cha kudharaulika katika jamii kabla ya kuwainua kwa kuwapatia msichana mtakatifu Maria, baada ya kuzidisha kwao ibada na maombI.

Malezi yake
Watakatifu zamani walikuwa wakiweka nia kwa watoto wao watakaowazaa. Familia hii ya mzee Joachim na mkewe waliweka nadhiri kwamba endapo Mungu atawajaalia mtoto, basi watamtoa wakfu - yaani atatumika kwenye kazi za Mungu (utumishi). Hivyo, baada ya uzao wa Maria na kufikisha umri wa miaka 2/3 baada ya kuacha ziwa, walitekeleza ahadi yao kwa kumpeleka hekaluni kulelewa na Kiongozi wa hekalu ambaye alikuwa ni mzee Zakaria, mume wa Elizabeth (mama yake Yohana Mbatizaji).

Hekaluni palikuwa pakilelewa mabinti bikra kwa kuwa walizingatiwa kuwa wasafi na watakatifu zaidi. Kwahiyo binti Maria aliishi humo pamoja na mabinti bikra wengine na kufundishwa maadili mema pamoja na sheria za Mungu. Wazazi wake walikuwa wakimtembelea mara kwa mara mpaka alipofikia umri wa miaka 10 wakafariki dunia.

Ndoa
Alipofikisha umri wa miaka 13, yaani miaka mitatu baada ya wazazi wake kufariki, uongozi wa Kanisa uliamua Maria atoke hekaluni ili aweze kupata mume. Kwa mila na desturi za hekalu enzi hizo, binti akishavunja ungo anakuwa sio msafi tena hivyo hahitajiki kubaki hekaluni kwa sababu atalichafua. Hata hivyo, Maria alijenga hoja kwamba yeye wazazi wake waliamua kumtoa wakfu hivyo ameamua ataitunza bikra yake na kumtumikia Mungu maisha yake yote.

Jambo hili lilileta mtihani kidogo kwa mzee Zakaria kwa sababu ni unprecedented. Akalazimika kuitisha baraza la ushauri namna ya kudeal nalo ambapo uamuzi ulifikiwa kuwa aende altareni akiwa pekee aombe hekima ya Mungu. Usiku wake, alifanya hivyo na Malaika akamtokea na kumpa Muongozo kwamba aitishe mkutano wa wagane wachamungu ambapo mmojawapo atateuliwa na Mungu kwa ishara kwa kuwa bado Mungu ana kusudi maalum na Maria.

Basi, ndipo katika kusanyiko la wanaume hao wagane, alikuwemo mzee wa miaka takribani 80 aitwaye Joseph. Fundi seremala mchamungu haswa, ambaye mkewe Salome alifariki mwaka mmoja uliopita na alijaaliwa naye watoto 7.

Kufupisha story, mzee huyo alifanikiwa kuteuliwa kwa ishara ya mng'ao wa kitambaa. Naye binti Maria (13) hakuwa na pingamizi kwenye uamuzi wa Muumba. Akakubali kuolewa.

Na historia maarufu ya Bikra Maria sasa inaanzia hapo na kuendelea. Kuna haja ya kuisimulia zaidi?!
 
Wakati Yesu anaanza kazi ya kutangaza ufalme wa Mungu Yosefu kuna uwezekano mkubwa alikuwa marehemu. Nasema kuna uwezekano kwa sababu hakuongelewa so hakuna uhakika kutoka biblia(kabla sijaombwa mstari wa kifo chake) lakini kuna viashiria.

Yesu akiwa msalabani alimkabidhi Mama yake kwa Yohana (Yohana 19: 26-27) ikimaanisha kuwa Yosefu alikuwa marehemu hivyo mama yake angebaki mpweke. Sababu hii ya kifo cha Yosefu ndiyo hupelekea dhana ya kuwa Yosefu alikuwa mzee hivyo alikufa kutokana na uzee.

Kingine ni kuwa Maria anaaminika kubaki bikra hadi kufa kwake. Hii inaweza kuaminika endapo tu Yosefu alikuwa mzee wa makamo hivyo hakuwa na shauku na mwali wake.

Vilevile Yesu alikuwa na kaka zake kama inavyoelezwa kwenye injili ya Mathayo 13:55-56 wakitajwa kwa majina Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda. Hawa wanaaminika walikuwa watoto wa Yosefu aliwapata kabla ya kuwa na Maria. Hitimisho ni kuwa maandiko japo hayajasema ila yanaashiria Yosefu alikuwa mzee wa makamo.
Angalau wewe umekuja na maelezo yenye ushawishi
 
Sio kweli! Maria alikuwa mke halali wa Mzee Joseph. Kugundulika kwa mimba changa ya Yesu hakukuzuia mahusiano ya kindoa baina ya Maria na Joseph. ..Jiongeze!
Biblia inasema hakumuingilia wakati wa ujauzito ila baada ya kuzaa ndio sijui
 
Hivi nyie watu mnasoma Bible ipi hadi leo mnasema Bikra Maria! Basi Mama ngu ni Bikra bado kwani alinizaa na ka endelea kuzaa , upo wapi Ubikra wa Maria wakati aliendelea kuzaa na Joseph kwa kawaida tu hamjui kuwa YESU anao Ndugu wa Damu kwa Maria?
Aliwazaa akina nani?
 
Unataka kusema nini?

Kwamba Nabii Zakaria siye baba wa Yohanna, nduguye na Yesu? Au hufahamu kwamba Yesu na Yohanna hawakupishana sana umri?

Hivi uajua kuwa Manabii wengi walirithi Unabii kutoka kwa Baba zao?

Nahisi sijaelewa unataka kusema nini.
Anamaanisha alikuwepo nabii na kuhani, huyo kuhani ndio alikuwa baba yake Yohana mbatizaji na sio nabii kama wewe ulivyoandika kwenye mada yako
 
Sahihi kabisa mkuu. Ukiisoma vizuri Injili ya Luka utakutana na simulizi. Ama ukitafuta agano la kale na baadhi ya vitabu vinavyofafanua zaidi mambo ya nyakati utakutana nayo. Nilichofanya ni ku-compile tu ili iwe kwenye mtiririko mzuri.
Weka marejeo kwa uhakika zaidi, yaani, mfano, sema Luka 20:20-40.
 
Kwa jinsi,ulivyoandika ni kwamba una ufinyu wa Neno la MUNGU
Asante kwa nia njema ya kutaka kuweka rekodi sawa. Napenda mwendo huu.

Hata hivyo, Joseph mkewe alikuwa akiitwa Salome na mmoja kati ya mabinti zake watatu naye alikuwa akiitwa Salome pia. Mengineyo uliyoeleza nakubaliana nayo isipokuwa hapo kwa Yohana.

Kama unamaanisha Mtume Yohanna Mbatizaji, wazazi wake walikuwa ni Zakariya na Elizabeth. Hawa walimpata uzeeni baada ya Mzee Zakaria kushuhudia neema ya Mungu kupitia kwa Maria aliyekuwa akimlea ambapo naye akafanya sala ya kuomba apatiwe moto na Mungu kukubali ombi lake.

Na hapo ndipo inaonesha umri wa Maria kuozwa ulikuwa mdogo sana kiasi kwamba Maria anaenda kuolewa huku nyuma mlezi wake Mzee Zakaria naye anapata mtoto wa uzeeni. So mimba ya Yesu na Yohana hazikupishana sana. Ndio maana wote walikuwa vijana na walishiriki mission pamoja.

Story ya Zakaria nayo inasisimua. Alifanyiwa ishara ya ububu kumjulisha kuwa mkewe amenasa ujauzito. Anyway, hii sio mada kuu.

Ila kama ulimaanisha Yohana tofauti, basi sawa.

Shukrani kiongozi.
 
Bado una ufinyu wa Neno la MUNGU
Unataka kusema nini?

Kwamba Nabii Zakaria siye baba wa Yohanna, nduguye na Yesu? Au hufahamu kwamba Yesu na Yohanna hawakupishana sana umri?

Hivi uajua kuwa Manabii wengi walirithi Unabii kutoka kwa Baba zao?

Nahisi sijaelewa unataka kusema nini.
 
Point of correction:

Salome alikuwa si mke wa Yusuph. Salome alikuwa binti wa Yusuph kwa mke wake marehemu. Salome huyu aliolewa na Zebedayo ambapo alimzalia watoto wakiwemo mitume wawili wa Yesu Kristo ambao ni Yohana na Yakobo. Salome alikuwa kaka yake Yesu kupitia kwa Yusuph baba yake. Mtume Yohana na Yakobo walikuwa na undugu na Yesu Kristo, ambapo Yesu alikuwa mjomba wao.

Kuna mengine umeandika vzr sana. Nilitaka tu kurekebisha hapo huenda umeandika kwa kuchanganya, lakini hapo ulipofika katika uandishi ninaamini kuwa unakijua unachokiandika.
...Solome anakuwaje binti, na hapo hapo anakuwa kaka!??
Au ni salome wawili tofauti, mmoja mwanaume na mwingine mwanamke!??
 
Hekaluni, Sinagogini, Msikitini yote ni yale yale. Point muhimu ni alilelewa kwenye nyumba ya ibada.

Mfumo wa malezi aliyopata, unafanana sana na mfumo wa malezi ya watoto katika Kanisa la Roman Catholic kwa zama hizi tulizonazo sasa!
NIMEKUSOMA MKUU
 
Teh! Labda alimaanisha Yesu alikuwa kaka yake Salome maana walishare baba yani Yusufu.
...Solome anakuwaje binti, na hapo hapo anakuwa kaka!??
Au ni salome wawili tofauti, mmoja mwanaume na mwingine mwanamke!??
 
Ni kweli mkuu.

Biblia haikuandika kila kitu lakini imeruhusu rejea ya habari zake mbalimbali kwenye maandiko mengine.

Seriously ulitarajia mambo yote yaandikwe kwenye Biblia? Yangetosha?

Yaliyomo kwenye Biblia ni summary.
Mungu wangu umetoa wapi huo ujinga??wapi imeandikwa kuwa yaliyomo kwenye biblia ni summary tu?
 
sinagogi mkuu.
Miskiti ya kiyahudi.
Kanisa Lilianza baada ya kuja Paulo.
hivi kanisa na maria nani wa kwanza kuzaliwa, maana kwa uelewa wangu huyu akilelewa ktk sinagogi ambayo ni sehemu takatifu kwa imani yao wakati huo. je kipi sahihi kanisa au sinangogi naomba ufafanuzi
 
Unataka kusema nini?

Kwamba Nabii Zakaria siye baba wa Yohanna, nduguye na Yesu? Au hufahamu kwamba Yesu na Yohanna hawakupishana sana umri?

Hivi uajua kuwa Manabii wengi walirithi Unabii kutoka kwa Baba zao?

Nahisi sijaelewa unataka kusema nini.
Alichomaanisha zekaria nabii na zekaria babaye yohane ni watu wawili tofauti.zekaria babaye yohane hakuwa nabii bali kuhani yaani mwongoza ibada madhabahuni
 
Wadau wa fikra,

Nafahamu kuwa muongozo wa Jukwaa hili unatutaka tuweke serious reports & discussions on Corruption, Politics na etc kwa ajili ya mijadala yakinifu. Tofauti na Jukwaa la Dini ambalo lengo lake kuu ni kuhamasishana kuhusu masuala ya kiimani na kufundishana yale yaliyo mema.

So, uzi huu hauna lengo la kuhamasishana kuhusu imani bali kujadiliana kwa kina kuhusu mambo ya kale (historical facts) yanayoingiliana kidogo na dini/imani. Naamini nimejaribu kuweka utofauti ili isionekane naleta mjadala wa kidini kwenye jukwaa hili makini.

Kupitia historia fupi ya Maria, nitaeleza mtihani wa Bikra Maria kwa Mkuu wa Kanisa/Hekalu alimolelewa, ambaye alikuwa ni Nabii Zakaria. Ni matarajio yangu tutaulizana maswali na kurekebishana kwa uungwana ili sote tuweze kuelimika na kufahamishana mambo mengi tusiyoyajua.

Hebu tuipitie historia hiyo kidogo..

Wazazi wake
Maria alizaliwa na Mzee Joachim na Bi. Anna ambao walikuwa ni wachamungu haswa. Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachamungu wa enzi hizo, Mungu aliwapa mtihani wa ugumba Mr. & Mrs Joachim kiasi cha kudharaulika katika jamii kabla ya kuwainua kwa kuwapatia msichana mtakatifu Maria, baada ya kuzidisha kwao ibada na maombI.

Malezi yake
Watakatifu zamani walikuwa wakiweka nia kwa watoto wao watakaowazaa. Familia hii ya mzee Joachim na mkewe waliweka nadhiri kwamba endapo Mungu atawajaalia mtoto, basi watamtoa wakfu - yaani atatumika kwenye kazi za Mungu (utumishi). Hivyo, baada ya uzao wa Maria na kufikisha umri wa miaka 2/3 baada ya kuacha ziwa, walitekeleza ahadi yao kwa kumpeleka hekaluni kulelewa na Kiongozi wa hekalu ambaye alikuwa ni mzee Zakaria, mume wa Elizabeth (mama yake Yohana Mbatizaji).

Hekaluni palikuwa pakilelewa mabinti bikra kwa kuwa walizingatiwa kuwa wasafi na watakatifu zaidi. Kwahiyo binti Maria aliishi humo pamoja na mabinti bikra wengine na kufundishwa maadili mema pamoja na sheria za Mungu. Wazazi wake walikuwa wakimtembelea mara kwa mara mpaka alipofikia umri wa miaka 10 wakafariki dunia.

Ndoa
Alipofikisha umri wa miaka 13, yaani miaka mitatu baada ya wazazi wake kufariki, uongozi wa Kanisa uliamua Maria atoke hekaluni ili aweze kupata mume. Kwa mila na desturi za hekalu enzi hizo, binti akishavunja ungo anakuwa sio msafi tena hivyo hahitajiki kubaki hekaluni kwa sababu atalichafua. Hata hivyo, Maria alijenga hoja kwamba yeye wazazi wake waliamua kumtoa wakfu hivyo ameamua ataitunza bikra yake na kumtumikia Mungu maisha yake yote.

Jambo hili lilileta mtihani kidogo kwa mzee Zakaria kwa sababu ni unprecedented. Akalazimika kuitisha baraza la ushauri namna ya kudeal nalo ambapo uamuzi ulifikiwa kuwa aende altareni akiwa pekee aombe hekima ya Mungu. Usiku wake, alifanya hivyo na Malaika akamtokea na kumpa Muongozo kwamba aitishe mkutano wa wagane wachamungu ambapo mmojawapo atateuliwa na Mungu kwa ishara kwa kuwa bado Mungu ana kusudi maalum na Maria.

Basi, ndipo katika kusanyiko la wanaume hao wagane, alikuwemo mzee wa miaka takribani 80 aitwaye Joseph. Fundi seremala mchamungu haswa, ambaye mkewe Salome alifariki mwaka mmoja uliopita na alijaaliwa naye watoto 7.

Kufupisha story, mzee huyo alifanikiwa kuteuliwa kwa ishara ya mng'ao wa kitambaa. Naye binti Maria (13) hakuwa na pingamizi kwenye uamuzi wa Muumba. Akakubali kuolewa.

Na historia maarufu ya Bikra Maria sasa inaanzia hapo na kuendelea. Kuna haja ya kuisimulia zaidi?!
We Jamaa acha kupotosha mambo ndivyo mnafundishwa katoroka huko?
 
...Solome anakuwaje binti, na hapo hapo anakuwa kaka!??
Au ni salome wawili tofauti, mmoja mwanaume na mwingine mwanamke!??
makosa ya uandishi tu. ulishaambiwa ni wajomba zake. hivyo Salome alikuwa dada yake.
 
Back
Top Bottom