Jinsi carryover ya mwaka wa kwanza ilivyotaka kunisababisha nisi-graduate chuo

Jinsi carryover ya mwaka wa kwanza ilivyotaka kunisababisha nisi-graduate chuo

Fountain of Youth

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
1,026
Reaction score
2,299
Mwaka wa kwanza chuoni niliikuta hii course katika harakati za hapa na pale nikapata coursework ya 11/40 kupiga UE nikala mzinga. Kufanya sup ikanishinda nikacarry.

Mwaka wa pili nikawa natumia uzoefu kuisoma hii course darasani siingii. Lahaula coursework kutoka nina 9/40 kufanya UE sikuchomoa. July mwishoni nikaripoti field muda wa kusoma hakuna kushituka September hio kufanya sup sikuchomoa ikabidi nicarry tena (Kimoyo moyo nikajisemea next time nitaipiga KO kwenye UE tu 🤣 ngoja niikamie)

Mwaka wa mwisho mambo yakazidi kuwa mengi zaidi research na course zikawa nyingi nikajikuta narudia yale yale makosa nikawa siingii class coursework kutoka ikasoma 8/40 kupiga UE nikafeli tena kumfata Lecturer alikua mmama akaniambia "yani wewe ujikaze tu kwa coursework hiyo sidhani kama utatoboa".

July-September nilisoma kama kichaa sikuwahi soma hivi kabla soma sana vitabu, articles, zurura sana YouTube nikapiga pepa la sup Septemba nikatoboa matokeo kuja nina C nikagraduate.

Sikuwahi kufeli somo lingine zaidi ya hili katika maisha ya chuoni lakini nikiri hili somo lilinipeleka mpela mpela kila nikikumbuka sina hamu tena na kusoma.

Kitu nilichojifunza: Kosa kubwa nililolifanya ni kuruhusu kufeli sup na kubeba somo kwenda nalo mwaka unaofuata nikidhani nitapata muda wa kulisoma wakati ni tofauti kabisa muda unakuwa mdogo na mambo yanazidi kuwa mengi.
 
Duh hater umecarry zaid ya mara moja alafu ujadsco kha iko chuo kinamahaba na wanafunzi wanasheria nyepesi kweli hiko ndo chuo cha kushauri wadogo zetu wasome ya nn kujitesa bhana
Chuo kipi ukicarry zaidi ya mara 1 unadisco? Sikuwahi sikia hiyo sheria
 
Na mimi huwa sielewi mwanafunzi anafanyaje UE wakati coursework haijafika nusu. Chuo changu cha kata asingefanya UE kabisa. Kushindwa coursework maana yake hujaielewa course.
COET hio mkuu. UDSM college wanaozingatia coursework ya kuingia UE lazima iwe 16 ni za COSS,COHU na SOED ila kwa ugumu wa kozi college za COET na CONAS hio haiapply ukiwa na coursework chini ya 16 unaingia UE wangesema waweke kigezo cha kuingia UE lazima uwe na above 16 wanafunzi wengi wangekua wana carryover sababu baadhi ya masomo unakuta nusu ya darasa wanapata coursework za <16 wengine hadi single digit

Mfano kuna wahadhiri wenyewe kila mwaka ukiangalia coursework wanazotoa hakuna mwanafunzi anayepata coursework juu ya 16 kwa darasa zima na mkifanya UE robo tatu ya darasa mmesup shida sio kwamba hamkuelewa course bali wanatunga mitihani migumu ambayo ni ngumu kutoboa
 
Sio tu uki carry zaidi ya mara moja.
Hata hiyo course work yako ya under 16 usingefanya UE.
Kuna vyuo kwenye hii nchi, ni kama wako vitani
Coursework kuwa above 16 haiapply kwa college za CONAS na COET- UDSM kutokana na ugumu wa kozi na utata wa wahadhiri
 
Coursework kuwa above 16 haiapply kwa college za CONAS na COET- UDSM kutokana na ugumu wa kozi na utata wa wahadhiri
Kwa upande wa coursework ainashidah hata ukiwa below 16 kuingia UE hila sasa unacarry coz. Mfululizo 3 times alafu unagraduate nazani ni kitu kizuri kilichonivutia kwenye hicho chuo hapo gamba utabeba tu wanachofanya wao ni kukuchelewesha chuo akina kudisco hcho kizuri sana
 
Kwa upande wa coursework ainashidah hata ukiwa below 16 kuingia UE hila sasa unacarry coz. Mfululizo 3 times alafu unagraduate nazani ni kitu kizuri kilichonivutia kwenye hicho chuo hapo gamba utabeba tu wanachofanya wao ni kukuchelewesha chuo akina kudisco hcho kizuri sana
Kwa hilo nawapongeza pia ingawa pamoja na kufanya hivyo bado watu wengi wanadisco kila mwaka mfano sisi tulianza kama 63 ila tuligraduate 30 wengine walidisco
 
Yaani unacarry mara mbili na bado unaendelea kuwa mwanafunzi? Hicho chuo wanatumia system ama inakuaje make mi najua ukicarry mara mbili system inakukataa
 
Sio tu uki carry zaidi ya mara moja.
Hata hiyo course work yako ya under 16 usingefanya UE.
Kuna vyuo kwenye hii nchi, ni kama wako vitani
Yah, kuna baadhi ya course below 16 hata UE hauingii umesoma kimasihara sana
 
Back
Top Bottom