Pre GE2025 Jinsi Freeman Mbowe anavyoenda kumfuta Lissu kwenye siasa za Tanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wanaccm wanapomuunga mkono Mbowe kwenye huu uchaguzi ndio tunapozidi kupata shaka kilicho nyuma ya pazia.
 
Umeandika Vibaya na umemlisha maneno Mbowe huku ukimtia Ubaya Lissu, hukufanya kwa haki
Lissu ni mbaya wa Chadema lengo lake ni kuibomoa chadema. Anajua hashindi uongozi ila kaamua avuruge chama.
 
KWA NINI MBOWE HATAKI KUACHIA UENYEKITI WA CHADEMA

Mbowe ni Mwanachama pekee asiye na hasara ndani ya CHADEMA na mnufaika Mkuu japo wengi hawaoni kwa macho ya kawaida na anatumia mbinu zifuatazo;

1. Pesa yake yoyote ile anayoitumia ndani ya CHAMA inaandikwa kama mkopo na CHAMA kikipata fedha kwa njia ama ya Ruzuku, Chadema Digital ama Join the Chain analipwa kama mfadhiri wa chama.

Kama Mbowe yeye kila pesa yake anayoitumia ndani ya CHADEMA analipwa kama deni na anaitwa mfadhiri wa chama; sisi wengine anaotuita wabangaizaji ni nani anatulipa hizo chenji zetu za jero jero ambazo tunaamua kushinda ama kulala njaa ili tuki-support chama?

Hakika haya ni mambo ya aibu sana yasiyovumilika kwa kila mpenda mabadiliko wa nchi hii.

2. Mbowe ndiye Mwanachama pekee wa CHADEMA ama wa upinzani kwa sasa anayeweza kuipinga Serikali ya CCM hadharani; na ASITEKWE wala kuumizwa mwili wake hata kwa rungu ama jiwe na dola hii ya CCM ama huyu Mbowe hajawahi kupata athari yoyote ile kutokana na kukaa kwake gerezani kwa sababu; Mbowe akipelekwa gerezani inakuwa fursa ya kuweka sawa mipango yao na watu wa dola na mipango ikishakaa sawa anatolewa na anaambiwa aandike hasara zake zote alipwe na serikali na kweli analipwa.

Kama ni uongo, Mbowe atoke hadharani akatae kama hajalipwa Mabillioni ya Shilingi na Serikali ya CCM kama fidia ya hasara za kisiasa. Haya yote ni yanatokea hivi kwa sababu; Mbowe ni; mwenzao tangu enzi japo tulipoteza muda wetu mwingi sana kumuamini pasipo kujua.

Tazama Tundu Lissu anavyohangaika kudai hata hayo madai yake ya halali aliyotibiwa kama Mbunge baada ya kumuumiza vibaya sana kwa risasi za moto.

Kwamba, wapo tayari kumhonga Lissu Mabillioni ya Shilingi kupitia kwa Wenje na Abdul, lakini hawako tayari kumlipa gharama zake za matibabu ambazo ni halali yake kwa mujibu wa sheria za nchi.

3. Mbowe ni Mwanachama pekee ndani ya CHADEMA ambaye hajawahi kuishi nje ya nchi kama MKIMBIZI kutokana na usalama wake kuwa hatarini wala familia yake haijawahi kupata msukosuko kama ambavyo tunaona kwa wapinzani wa kweli walio committed kutaka CCM iondoke madarakani kama akina Godbless Lema na huyu Tundu Lissu.

Unahisi ni kwa nini Mbowe na familia yake hawajawahi kupata msukosuko serious wa kuwalazimu kuikimbia nchi ili hali na yeye anaikisoa serikali? Jibu liko Behind the Scene. Tuendelee kunywa mchuzi, nyama ziko chini.

Garatwa Francis,
Sauti ya wasio na Sauti.
29 Desemba, 2024.
 
Mbowe ataachia chama kwenye box la kura. Lissu asubiri sanduku la kura Mbowe apige kwenye mshono.
 
Mtapigwa Hadi mchakae
 
Wajinga waliisha enzi za TYL.

Ni mjinga tu ndio atabeba na kuamini hiki ulichoandika.
Nakwambia Lissu sio mtu wa maana sana pale chadema kama wapambe wake wanavoamini. Ndio maana Mbowe anamchukulia kama mjinga mwingine yoyote anajua sio muda atatafuta mlango wa kutokea.
 
Nakwambia Lissu sio mtu wa maana sana pale chadema kama wapambe wake wanavoamini. Ndio maana Mbowe anamchukulia kama mjinga mwingine yoyote anajua sio muda atatafuta mlango wa kutokea.
Ndio maana nakwambia wajinga waliisha enzi za TYL hujanielewa?
 
Mimi pia Nina mawazo kama hayo . Siyo uadui kugombea nafasi hizo na Cha muhimu CHADEMA waandae uchaguzi HURU na WA haki ili kila aliyeshinda Kwa haki apatikane na uwe uchaguzi wa mfano wa kuigwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…