Jinsi gani uliweza kuendelea baada ya kuachana na mpenzi uliyekuwa unampenda sana?

Mkuu umenifariji sana kwa hii comment, nakushukuru sana, najipa matumaini ipo siku ntafurahi na mimi, i still believe mapenzi ya kweli yapo ni suala la muda tu. Ahsante uwe na siku tulivu.
 
Kumbe alikuacha inaonekana jamaa alipata hitaji la moyo wake, Kwahiyo na wewe omba Mungu kuna siku atakuja mwanaume wa atakaye endana na wewe,
Ila mm katika maisha sijawahi kuumizwa na mwanamke kwa kuniacha
 
Napitia ktk hiki kipindi kigumu kwa sasa,haya mambo uyasikie kwa mwengine ila maumivu yake ni makubwa sana,ukisikia mtu amejinyonga usimcheke ameshindwa ku control hisia na maumivu yake.Naona kabisa itachukua muda mrefu sana kurudi ktk hali yangu ya kawaida
 
Niliwahi mpenda mtoto wa mtu wa kike nikaweka kila kitu rehani hadi nikagombana na wazazi wangu maana niliridhia hadi kuishi nae pamoja japo wazazi hawakutaka wakihofia umri wangu bado mdogo na atanisumbua lakini sikuelewa, ila now ni miezi mitatu imepita toka tuachane, alinifanyia uhuni sana huyu mdada sikuwahi kuumia kama nilivyoumia hiki kipindi mwezi mzima nilikuwa ndani nikilia, chakula nilishindwa kula nikawa nampigia cm na kumuomba msamaha kama vile mimi ndie nilimkosea ili tu asiniache lakini wapi, after mwezi niliamua kumsahau na kiukweli hadi sasa naona nimeshamsahau kabisa na sasa yeye ndo anaaza kunisumbua, Me sitaki tena kupenda.

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
 
Pole pitia visa vya humu na ushauri vitakufanya usonge mbele
 
Mwanaume unajifungia ndani unalia
Pole sana jitahidi kuwa mwanaume kamili
 
Aisee pole sana mkuu, ila maisha lazima yaendelee kupenda kupo tu wala usijali utapenda na utapendwa na wengine. Maumivu huja kutukomaza kihisia, umakini unaongezeka
 
Mkuu usijali mimi naamini machaguo yetu sahihi yapo ni suala la muda tu, ukiona umeachwa/umeacha basi jua hakua mtu sahihi. Jipe muda naamini atatoke mwingine mtakayependana na kusahau machungu yote
 
Mkuu usijali mimi naamini machaguo yetu sahihi yapo ni suala la muda tu, ukiona umeachwa/umeacha basi jua hakua mtu sahihi. Jipe muda naamini atatoke mwingine mtakayependana na kusahau machungu yote
Wewe mpaka leo ujamsahau wakat mwenzak yule nishaga msahau na maisha yanasonga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…