Jinsi gani uliweza kuendelea baada ya kuachana na mpenzi uliyekuwa unampenda sana?

Jinsi gani uliweza kuendelea baada ya kuachana na mpenzi uliyekuwa unampenda sana?

Nakuelewa madam mana nilishapitia inahitaji roho yakikatili kukubaliana mimi ilinitesa mwaka mzima lakini sasa ishapita miaka nilichojifunza usikurupuke kuanzisha mahusiano jipe muda mpaka akili yako itakapokuwa sawa ufanye maamuzi sahihi.
 
Habari wakuu.

Hivi mliwezaje kumove on, mimi nashindwa kabisa kumsahau huyu EX mpenzi niliyetokea kumpenda sana ila kutokana na sababu kadhaa hatukuweza kuendelea na mahusiano, ni muda sasa umepita tangu alivoniacha ila bado namfikiria sana na nilijipa muda huenda angeweza kurudi ila ndiyo kwanza yeye alishaendelea na maisha mengine huko.

Sijawahi kufikiria kama mimi ninavyojionaga mgumu ningeweza kusumbuliwa na mahusiano hivi ila ndiyo hivo imetokea, najitahidi kujikeep busy ili nisipate mda wa kufikiria sana lakini haisaidii.

Nifanye nini wakuu?😪😪

Kwenye mpira wa miguu,Kuna kushindwa,kushinda au kutoka sare.
 
Back
Top Bottom