Jinsi gani uliweza kuendelea baada ya kuachana na mpenzi uliyekuwa unampenda sana?

Jinsi gani uliweza kuendelea baada ya kuachana na mpenzi uliyekuwa unampenda sana?

Ni suala la muda tu, utapenda tena. Kama mimi nimependa tena basi naamini kila mtu anaweza kupenda tena aisee.
Haya mambo hayana mwenyewe hata ww.😀😀😂
 
USIJARIBU nkamu

Haya mambo moyo upo kwa A, unaenda kujilazimisha kuwa na B: ni kujitesa nafsi yako na kumtesa huyo B ambaye possibly ana pure intention kwako. Na kama hujamtoa mtu kwenye nafsi yako; ni ngumu sana hata kuona na kukubali upendo unaonyeshwa na wengine huku nje. Huwezi kuendelea na mahusiano mengine au maisha yako tu kwa sababu utakuwa bado una matumaini kuwa fulani atarudi. Muachilie nafsini mwako, amini kuwa hakuwa wako.
Ahsante sana nkamu, nimeanza kuachilia na kukubaliana na matokeo kwamba he wasn't mean for me😪
 
Hiii unaweza kukusaidia kumove on.
Sikia,
Kumkumbuka ex sio kuwa hujamove on aiseeh.

Unamkumbuka kwa kuwa yupo maisha uliwa kuwa nayo pamoja nae.
Hii inatosha kabisa kutomsahau.

Kutokumove on ni pale, bado unamtamani, bado unaumia kumuona ana mahusiano mengine, bado unamfuatilia issue zake.

Lakini kumkumbuka tu nimetoka kitu mutual mlifanya ndo uone hujamove on.
Relax, huwa inaenda na muda.

Kikubwa ishi mama, katika kuishi unaona maisha yalivyo bado yana furaha na yanahitaji kuyafurahia kuliko kuumia na vilivyokwisha pita.

Ila, nakuelewa.
Ahsante !naanza kujifunza kuishi bila yeye, nimekubali matokeo
 
alinitumia text whatsapp "mpenzi kukweli nmejitahid sana ila naona sina hisia za kimapenz na ww".

baada ya muda kidogo akaweka clip status jamaake mpya anamfundisha kuendesha gari nikawa nasikia "baby siku 3 mbele ntakuachia uwe unaendesha mwenyew unaonekana una kichwa chepesi" demu wangu akajibu kwa madeko huku akikanyaga mafuta "thawa sweetheart"


sikilizia ayo maumivu.
Pole mkuu hadi nimecheka hiyo "thawa sweetheart "😄
 
Una uhakika nikikwambia cha kufanya utakifanya kweli mkuu ili uweze kuondokana na hizo moments & memories kuhusu huyo Ex wako?
Mkuu am serious kama unahisi kuna kitu kitanisaidia niambie tu am ready ili mradi kiwe ni halali na kinachofuata maadili yetu
 
Ahsante sana nkamu, nimeanza kuachilia na kukubaliana na matokeo kwamba he wasn't mean for me[emoji25]
Kandamizia na maombi nkamu; cut all the soul ties formed between you two, and renounce the covenants you made.
Likija kupita hili; kuna siku utakumbuka halafu utatamani hadi ujipige kofi kwamba ulikuwa unachanganyikiwa nini
 
Bado unamchunguza sana mpaka unajua kuwa ananenepa. Na nakuhakikishia kama unaendelea kumfatilia utaendelea kuumia mwisho ukaribishe maradhi mengine.
Ni kweli huwa nafatilia na nadhani ndiyo kinachonikumbusha na kuumiza zaidi sirudii maana namuona tu anapendeza huku mimi nikichakaa sana tu😒
 
Mkuu umenikumbusha jinsi nilivyo mpenda mrembo huko kijijini nilimpenda sana kupitiliza,sku moja mama yeke mzazi akaugua ilibidi niuze baisekeli yangu ili mama yake akatibiwe lakini niliachwa kisa umasikini nilikonda kabisa,nika amua kukimbilia mjini tukapotezana kabisa miaka ikasonga,ili nichukua mda sana kumsahau,baada ya miaka kadhaa kupita nikaenda kijijni msibani akaniona eti akajiliza umenenepa umependeza mara nisamehe turudiane nikawa na mcheki tu,baada ya msiba kuisha nikaanzisha na ujenzi kabisa hapo nyumbani ujenzi ukaenda halaka,akaja kuomba kibarua cha kusaidia mafundi nikamwambia aongee na fundi mm si husiki akawa ananisema eti nimepata pesa kidogo nimeaanza kuringa,nikawa namshangaa tu wakati huo namona sio saiz yangu tena maana alikua amepigwa na maisha amechoka,ila namshukuru asinge niacha ningekua bado kijijini mpaka leo.
Dah hongera kwa kumove on mkuu, huyo dada alichezea bahati mwenyewe sahivi angekua ndiye mother house badala ya kuomba kibarua hapo
 
Pole Sana.
Mambo gani yanakufanya ushindwe kumtoa kichwani????
Je,umezaa naye?
Umejenga naye?
Alishakutolea mahari? n.k

Ni Heri uchumba uliovunjika kuliko ndoa mbovu.
Uchumba siyo ndoa,lolote linaweza kutokea.

Mapenzi ya kweli hayalazimishwi.

Mshukuru Mungu kwa yote na muombe akusaidie kuendelea mbele.
Kufikiria Sana hakutatatua tatizo lako.
Ni mahusiano tu ya kawaida boyfriend n girlfriend hatukufikia hatua ya uchumba hata ila ni vile nilikua nampenda sana naona zile good memories zinanisumbua . Ila najitahidi kutoka huko
 
Nyamaza kimya kabisa, usimtafute wala usimbembeleze, akiona kimya ataanza kujisexisha arudi. Be careful he might hurt you twice as much ukimpa nafasi ya pili. Mtu akishakuonyesha hakutaki mwache aende anakotaka, usimzuie. Mapenzi ni hiyari. Amini kuwa atakuja mwingine
Ahsante sana, najikeep busy tu sitaki kumsumbua tena kwa namna yoyote
 
Kama bado unaweza kuona status zake na ye anaona zako jipe muda kula unenepe msambwanda uongezeke,wanaume wakiona unapendeza baada ya break up roho huwa zinawauma,ukishapendeza tupia pamba jipost status,wee sikilizia balaa lake!atakusaka mwenyewe na we usikubali kurudi kwake tena!
Akishakutafuta hapo tayari utapata ujasiri wa kumove on as utajua kumbe jamaa bado anakuelewa,hii nimeona kwa wengi imewasaidia!
😂 mi sitaki kuona zake from now! Ahsante mkuu
 
Hahaaa eti sauti nzuri kubwaaaa

Huyo muhusika wala hayupo humu, sababu zakuachana kiukweli ni just Petty things,kama wivu(mimi) na long distance relationship kiasi ingawa tulikua tukitembeleana nk.

Tumekaa chini na kuongelea kuhusu kupeana chance nyingine ila ilishindikana na mwenzangu akawa ameshapata mahusiano mengine.

I just loved him so much na si kwamba alikua ananipa chochote, basi tu nilimpenda jinsi alivo na niliona naye ananipenda nilivo.ila alikua na sauti nzuri kuubwa dah[emoji31]
 
Back
Top Bottom