Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?


Huyu kweli tamaa ilikuwa online tena kifurushi cha mwezi unlimited [emoji16]
 
Hivi hkna dawa ya ukikutana na pisi kali ukimsalimia2 tayari unabeba2 kiulaini hadi geto Mbona matapeli wa ivyo cjawackia
Niliwahi kukutana na dogo mmoja ila ni zamani miaka ya 2001 alikuwaga mtoto wa mganga maarufu kijijini kwetu miaka hiyo
Yule dogo alikuwaga kachanjiwa dawa akimshika mkono demu tu hapohapo demu analegea anamfuata jamaa anaenda kula zigo
 
[emoji23][emoji23]mkuu sijasikia mtaani, waliobiwa naowajua ni watu wa karibu.. Halafu tahadhari ni bora kuliko ajali
Just use you common sense na endelea na hamsini zako bipa kushangaa

Kwa nini uanzishe story ghafla tu na strangers uliokutana nao barabarani? Ndio maana mnaibiwa. Pole
 
Duh! Pole sana
 
Hakuna ''wizi wa kusemeshwa'' bali huu ni utapeli. Kinachotokea ni kwamba watu wanalaghaiwa kwa maneno mpaka wanajikuta wanatoa vitu walivyonavyo kwa sababu ya tamaa zao! Narudia tena. Huu ni utapeli wa maneno tu na anayekusemesha anatumia udhaifu na tamaa zako kukupiga. Namna ya kukabiliana na huu utapeli ni kutopenda short-cut au vitu vya bure na kuepuka kuzoeana na watu ambao huwajui kwa urahisi. Hivi dunia ya leo mtu anakukuta anaanza kukusemesha semesha na kukuzoea ghafla wewe unakubalije?
 
Wote hawa walitapeliwa kwa tamaa zao za kupenda vya bure. Hakuna cha dawa wala nini. Mimi nimejaribi kuuliza sana kwa undani kuhusu watu waliodai walitapeliwa kwa kutumia ''dawa'' lakini katika cases zote niligundua kitu kimoja. Walitekwa kimawazo kwa tamaa zao za kupenda short cut na walipokwisha kupoteza mali au fedha zao wakazingizia kuwa hawakuwa na ufahamu.
 
Asante sana mkuu. Kwale watu waliofika nchi zilizoendelea kama Ulaya watakuelewa lakini kwa wabongo wengi hawawezi. Eti dunia ya leo unaanza kuzoeana na mtu ghafla humjui wala hakujui!
 
Kuna dawa inaitwa Scopolamine....unaweza kuangalia documentary hapo chini


Pia soma:
 
Kungekuwa na wizi wa kutumia jini au dawa mjini hakuna mtu angepona au kuepuka. Watu wangekuwa wanapigwa kila siku na kila saa. Na wezi wangekuwa wanatumia kitu kama mwezi mmoja tu kuiba na wangekuwa matajiri wa kutupwa. Infact matajiri wakubwa kwenye kila mkoa wangekuwa ni hao wezi kwani fedha zingekuwa zinaingia kama utani.
 
Fiksi. Kamba! Chai!
 
Tatizo wabongo tunapenda sana salamu mtu Hata hakujui humjui mmekutana tu anakusalimia,haya mambo huez kukuta Kenya yan mpaka nilishangaa pale Nairobi kila mtu yuko bize ila bongo sasa haha unaeza pita sehemu usiposalimia wanamind hatar yes sio mbaya but asilimia kubwa hao matapeli wanaanza kukusalimia na kukuongelesha ukijibu tu imekula kwako anyways tuwe makini barabarani huko sio kila mtu anania njema!
 
Mwaka 2014 nilikutana nao Bamaga nilikua naelekea sayansi nipo kwa mguu nilikutana na huyo kaka anaulizia hospitali jina nimesahau nikamuambia sipajui muda huo huo akatokea kaka mwingine, huyu kaka alienisimamisha mara ya kwanza akamsimamisha yule kaka mwingine akamuuliza hiyo hospital yeye akasema anaijua ipo barabara ya kuelekea Sinza ila hana muda anielekeze mimi nimpeleke.

Sijawah elewa nini kilitokea kweli niliondoka nao tumefika karibu na Afrikasana nikajiuliza naenda huku kufanyaje nikawaambia jamani mnanipotezea muda wewe kaka unaeijua hiyo hospital mpeleke mwenyewe mie nna safar zangu wakaanza kulalamika tusaidiane mimi nikasepa. Nipo njiani kurudi nikawa najiuliza ilikuaje nikaondoka nao ila hawa hawakuniibia chochote nilikua na begi la mgongoni lina nguo, simu na hela kidogo tu.

Toka pale sijawahi kutana tena na watu wa namna ile ila stori za watu kuibiwa kwa namna hizi zipo nyingi sana.
 
Duuuuuh poleeeh ila ungeibiwa km usingeshtuka yaan.
 
Huu ni uongo wa hali ya juu alikuambia huyo mganga. Watu kama nyie ndiyo huwa mnatapeliwa sasa. Unaona aliweza kukuaminisha kuwa anaweza kufanya wadeni wako wasahau kama wanakudai au ushinde kesi hata kama umekosa! Utapeli ndivyo unavyofanya kazi na hakuna dawa wala pepo wala jini. Mtu anakuaminisha anaweza kufanya kitu fulani ambacho una shida nacho, anakuteka kimawazo wewe unakuwa umejikita kwenye ile ''habari njema'' uliyopewa na kusahau mengine yote. Anakupiga. BTW kutapeliwa na ndugu au jamaa au rafiki hii ni kesi nyingine kabisa kabisa na sidhani inaweza kukwepeka hasa kwa maisha yetu ya kiafrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…