Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Nishakutana na kesi nyingi sana za hawa watu lakini mimi sijabahatika kukutana nao
Huwa natamani sana kukutana nao

Katika mara kadhaa maeneo ya magomeni/kkoo nikiwa katika mishe zangu
from nowhere mtu anatokea,
Anakusalimia/anakuulizia sehem. Wengine ni vijana wengine ni wazee

Salam huwa nawajibu kwa kuinua kichwa
Au nakataa kwa kutikisa kichwa
Then nikitembea hatua tatu nageuka nyuma kumuangalia, naishia kucheka tu

Wengine wanakufata uliposima, wanjiongelesha ili utoe reply, kwanza uwa navimba alafu nawaangalia kwa Shari Shari
Mara nyingi huwa sitpi jibu alafu naangalia pembeni/ au natoka pale niliposimama
Huku nikimuangalia

Ila watu wengine najikuta najibu salam zao ata kuwaelekeza, huwa nawapa ushirikiano mzuri tu

Nahisi ni machale ya mtu
Sisi wengine tumezaliwa na mizimu yetu pia. Hatugusiki[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hamna jini wala nini, watu tamaa na ujinga ndo vinawaponza!
Mkuu unaonekana ww mgeni wahaya mambo labda yakukute ila hawa wana wanatumia mapepo na maagano yao walio ekeana kinyume na hapo hakuna mtu mjinga anaekubali kutoa pesa, simu, Atm card kwa hiyari na mtu humjui kisa kakusalimia. Nipepo linakuingia na unakuwa siww naanakutoa eneo latukio than anarudi kwa mmiliki wake baada ya kufanikisha zoezi.
 
Ni madawa.uwa wanatafuna Kama BIG G.hapo akili anakupumbaza hata mbele hauoni vizuri na kichwa kitaanza kukuuma.
Kuna boda boda alichukuliwa bagamoyo akapelekwa mlimani city kuibiwa .kuamka boda imekwenda na hela hanaa
Ila Dar nyoso sana mm ndomana nikiwa na hela sicheki na mtu kwenye daladala kabisa haswa pale Mlimani City ndo pabaya pale kuna rafiki yangu kipindi niko Advance mama ake alikuwa hawezi pirika ikitokea huwa anampa Card mwanae akatoe pesa za matumizi.

Ile kutoka tu pale mlimani City wana hawa hapa Salimia wakaanza story za nyota jamaa akawapa pesa alizotoa kwenye ATM na Simu fahamu zilimjia baada ya kufika kwamama yake kwao Full kilio asahau ile siku.

Ila hawa jamaa kwa haraka na fikra zinazonijia aidha wanatumia Jini au Dawa na haswa zaidi ni jini kitendo cha kuitikia inamaana ummempa ruksa jini akuvae na akutawale na akuamrishe na wengi wahanga niwanawake kuliko wanaume na haswa ukiwa mchafu, pombe na mtu wazinaa ni rahisi sana kufanikiwa kwao.
 
Siku ya kwanza nilikuwa nimetoka shule naingia mitaa ya mjini nakuta kuna watu wengi wamezunguka huku kuna screen za kutosha,mabegi makubwa,gari carina kama nne, simu utasema shop imehamia pale na yote kwa yote pesa ya kutosha ipo.
Inanadiwa kuwa wamepewa kibari na serikali hivyo wapo kisheria baada ya kuona mchezo wao unanufaisha zaidi wananchi. Kuna namba za bahati anazungusha kwa hela yoyote au kitu chochote ulichonacho na namba hiyo inawakilisha kitu fulani cha thamani. Ile sijakaa poa kuna mtu anashangilia carina kwa elfu 5,mara paa mwingine screen amebeba kwa saa aliyokuwa amevaa mkononi.
Nikaona hapa hapa leo narudi shulena na bab kubwa carina au kompyuta. Nikaweka kiswaswadu ikasoma elfu 20, akasema unaweka hii zawadi yako nikakubari ndio, ikasoma hakuna zawadi ah nilichoka. Nikaomba laini nikapewa nikajiondokea taaratibu hiyo wiki ilikuwa ngumu sana na ile simu ilikuwa ya rafiki yangu hadi tuligombana ila nilimficha ukweli na nilimdanganya simu imepotea kwenye daladala
[emoji16][emoji16] Yani kama ulikuwepo, huo mchezo wa namba ndio ulinilizaga Mimi. Sina hamu mpk leo nimejifunza, na sijui wanatumia dawa ata haieleweki, mana ata walivyonipokonya sikuwa na habari. Nimekuja kushtuka nimetoa Kila kitu, Sina ata nauli. Na sikuwaza kabisa km nachelewa natakiwa kwenda mkoani.
 
Msiwe mnapenda kuitikia tu kila mtu, wote tumekuja mjini hatujuani...

Huwa namchunia kila mtu anayetaka kuniuliza kwa sababu miaka kadhaa nyuma hao wapumbavu washawahi towesha mshahara wa ndugu yangu ukiwa nyumbani, ilihali kapumbazwa akiwa town kazini, pia walimchapa simu na vichenji chenji alivyokuwa kabeba kwenye wallet...

Mataccor kabisa hao watu
 
Dar sio kama kwenu tunduru sijui mbambabay kule,[emoji2]

We unadhani kwanini paliitwa "BONGO"

Dedication:

Bongo daresalaamu -Proj J FT jay dee
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka mnoooo.
Ila..... Au bas tyuuh
 
[emoji16][emoji16] Yani kama ulikuwepo, huo mchezo wa namba ndio ulinilizaga Mimi. Sina hamu mpk leo nimejifunza, na sijui wanatumia dawa ata haieleweki, mana ata walivyonipokonya sikuwa na habari. Nimekuja kushtuka nimetoa Kila kitu, Sina ata nauli. Na sikuwaza kabisa km nachelewa natakiwa kwenda mkoani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaah wee ulikua unasafiri?
 
Habari wakuu

Kwa muda mrefu nimekutana na kesi mbalimbali za watu kuibiwa kwa namna ya kupumbazwa akili ( hypnosis).

Unakutana na mtu anakusalimia, ukishaitikia tu ndo kosa lako[emoji51][emoji51] .. Unakuja kushtuka ulishampa simu, wengine huenda hata bank na kutoa hela na kuwapa hao matapeli.[emoji2365] imagine enzi niko sekondari kuna classmate yeye aliwapa mpaka mkanda wake wa kiunoni manzese pale[emoji16]

Binafsi sijawahi kukutwa na hayo maswaibu, ila najiuliza ni nini kinga ya watu kama hao au hii mbinu ina Apply kwa baadhi ya watu tu ?
Suluhisho TUNAPOTOKA NYUMBANI KWENDA KWENYE MIHANGAIKO TUFANYE MAOMBI/DUA ILI MOLA MLEZI AKUKINGE na mabala hays yote...
 
Ni madawa.uwa wanatafuna Kama BIG G.hapo akili anakupumbaza hata mbele hauoni vizuri na kichwa kitaanza kukuuma.
Kuna boda boda alichukuliwa bagamoyo akapelekwa mlimani city kuibiwa .kuamka boda imekwenda na hela hanaa
Ndo hayohayo mapepo mkuu nishazunguka sana kwenye minada ya mifugo kuna mzee rafiki yangu sana huwa anatafuna mizizi na kumpiga kofi muuzaji hachomoi lazima anunue kwa bei anayotaka. Na mfugaji akili inamjia mnyama yuko kwenye Gari nikawa namdadisi nikajua mpaka chimbo anapoenda huko Kwa Babuu, ni Jini na hizo dawa maana baada ya mda lazima urudi ukarenew[emoji1787][emoji3]
 
Habari wakuu

Kwa muda mrefu nimekutana na kesi mbalimbali za watu kuibiwa kwa namna ya kupumbazwa akili ( hypnosis).

Unakutana na mtu anakusalimia, ukishaitikia tu ndo kosa lako[emoji51][emoji51] .. Unakuja kushtuka ulishampa simu, wengine huenda hata bank na kutoa hela na kuwapa hao matapeli.[emoji2365] imagine enzi niko sekondari kuna classmate yeye aliwapa mpaka mkanda wake wa kiunoni manzese pale[emoji16]

Binafsi sijawahi kukutwa na hayo maswaibu, ila najiuliza ni nini kinga ya watu kama hao au hii mbinu ina Apply kwa baadhi ya watu tu ?
yah hyo michezo ipo sana lakini ukiwa unafanyiwa huo mchezo lazma unakuwa unajiskia hali ya tofauti(uvutano wa nguvu 2 moja toa nyingne inakwambia usitoe)

sasa ukijiona upo kwenye hali hiyo haraka sana geza viatu vyako yani vya kushoto vaa kulia na kulia vaa kushoto mchezo unakuwa umeishia hapo na ndo maana huwezi kuskia mchezo huo kafanyiwa mtu aliyevaa sandalz au ndala asilani bali aliyevaa raba au viatu vya kudumbukiza
 
Back
Top Bottom