Siku ya kwanza nilikuwa nimetoka shule naingia mitaa ya mjini nakuta kuna watu wengi wamezunguka huku kuna screen za kutosha,mabegi makubwa,gari carina kama nne, simu utasema shop imehamia pale na yote kwa yote pesa ya kutosha ipo.
Inanadiwa kuwa wamepewa kibari na serikali hivyo wapo kisheria baada ya kuona mchezo wao unanufaisha zaidi wananchi. Kuna namba za bahati anazungusha kwa hela yoyote au kitu chochote ulichonacho na namba hiyo inawakilisha kitu fulani cha thamani. Ile sijakaa poa kuna mtu anashangilia carina kwa elfu 5,mara paa mwingine screen amebeba kwa saa aliyokuwa amevaa mkononi.
Nikaona hapa hapa leo narudi shulena na bab kubwa carina au kompyuta. Nikaweka kiswaswadu ikasoma elfu 20, akasema unaweka hii zawadi yako nikakubari ndio, ikasoma hakuna zawadi ah nilichoka. Nikaomba laini nikapewa nikajiondokea taaratibu hiyo wiki ilikuwa ngumu sana na ile simu ilikuwa ya rafiki yangu hadi tuligombana ila nilimficha ukweli na nilimdanganya simu imepotea kwenye daladala