Ukiweza kujizuia na tamaa za pesa za haraka ,
Kamwe huwezi kutapeliwa
Nakumbuka siku moja zamani kidogo,
Nilikuwa pale ubungo maji,, Daresalam.
kabla ya hii barabara ya mwendo Kasi kujengwa.
Niliisubiri daladala kwa muda mrefu baadae daladala likafika la posta,
nikatulia zangu mbele kwa dereva
Kati ya watu tuliokuwapo ndani ya daladala alikuwapo dada mmoja umri kama 30 hivi,
Muda wote alikuwa na wasiwasi kama ana Jambo linamsumbuwa..
Baada ya kufika kituo cha manzese,
Yule dada alifunguwa mkoba wake akatoa bahasha fulani ya rangi ya kakhi,
Baada ya kufunguwa Ile bahasha alipiga Kelele kwa sauti
'''Mama!! Nimetapeliwa,""
Nitamueleza nini mume wangu.
Ikabidi nijaribu kumbembeleza na kujuwa kulikoni?
Baada ya kumsikiliza kwa makini,
Nikagunduwa tamaa ya pesa za haraka hupelekea kutapeliwa..
Yule dada alitoka na mumewe kimara,
Wote wakashuka kituo cha ubungo maji,
Mumewe akavuka barabara upande wa pili wa jengo la Tanesco Ili akapande magari yanayoelekea buguruni.
Wakati huo bado Pana stand ya daladala pale ubungo Tanesco.
Sasa yule dada anasema wakati anaagana na mumewe,
Alipita Kaka mmoja akadondosha bahasha fulani ya rangi ya khaki.
Yule dada aliiona Ile bahasha akataka kumuita yule kaka aliyoangusha Ile bahasha,
Akatokea jamaa mwingine akaokota Ile bahasha,mbele ya yule dada.
Akaifunguwa Ile bahasha ilikuwa na pesa kibunda cha noti ndani yake.
Kabla hajakaa Sawa akarudi yule Kaka wa mwanzo aliyedondosha Ile bahasha akaja kuulizia pale.
Nimeangusha bahasha ina 1.5 million,
Yule Kaka alilalamika pale mbele za watu,
Lakini jamaa alikana kuokota Ile bahasha.
Pale pale yule jamaa aliyeokota bahasha akamwambiya yule dada,
Hizi ni pesa nyingi,
Na huyu kijana lazima atarudi tena kabla daladala halijaja,
Sasa chukuwa hii bahasha nisubiri kituo cha mbele pale shekilango.
Mimi nakuja.
Jamaa alimwambiya yule dada
Muda wote mume wa yule dada yupo upande wa pili anaona tukio zima,
Ikabidi ampigie simu mkewe ,
vipi mbona upo na hao jamaa kuna nini?
Dada akamwambiya ni jamaa tu mgeni anauliza njia,
Lakini mumewe bado akawa anasumbuwa kwa simu,
Mwisho dada akawa hapokei simu ya mumewe.
Kilichofata baada ya dada kupewa bahasha,
Yule jamaa aliyeokota bahasha, akamwambiya yule dada,
Sasa Mimi nakuamini vipi?
Kukupa 1 milion wakati sikujuwi?
""Kama vipi niachie simu yako,''
Tangulia shekilango kituoni,
"Nakuja tugawane."
Dada alikuwa na simu nzr Sana smart.
Kabla dada hajatoa maamuzi ya kutoa simu ,
Yule aliyeangusha pochi akarudi tena,
Akasema jamani nimeangusha milioni na nusu,
Atakayeona bahasha plz ni pesa za Ada ya chuo.
Please, please,jamaa alijiliza pale kituoni
Yule dada akaona simu kitu gani mbele ya 1.5.
Akampa jamaa simu,
Akaingia ndani ya gari.
Kufika manzese ndy dada akaamua kufunguwa Ile bahasha ili azihesabu pesa vizuri.
Anakutana na makaratasi yaliyopangwa vzr kama kibunda cha noti
Na mbaya zaidi hata yule dada mwenyewe,
alipanga kumdhulumu aliyeokota bahasha,
Sababu aliambiwa ashuke shekilango,
Matokeo yake akaamua kupitiliza kituo hadi manzese..
Tamaa hupelekea kutapeliwa.