Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Ukikutana na mtu usie mjua halafu akakusemesha MPIGE KOFI KALI SANA.

Hiyo ndio formula
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]nimecheka kwa saut
 
Kutapeliwa hakuna formula kabisa

unaweza kutapeliwa na mtu wako wa karibu, i.e ndugu jamaa ama marafiki

watu wasiokujua watatumia madawa kukupiga.

kuna mganga ashanisimulia jinsi watu wanavyoenda kwake kutafuta hizo dawa.

Hayo madawa huwa yanachanganywa na dawa za mvuto pamoja na kupewa mapepo maalum ya utambuzi na kupumbaza.

Madawa mengine makali wanayotoa ni ya kusahaulisha wadeni, kuua kesi mahakamani, n.k

hii dunia ni nzito sana sio kama tunavyoijua
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ukiweza kujizuia na tamaa za pesa za haraka ,
Kamwe huwezi kutapeliwa

Nakumbuka siku moja zamani kidogo,
Nilikuwa pale ubungo maji,, Daresalam.
kabla ya hii barabara ya mwendo Kasi kujengwa.

Niliisubiri daladala kwa muda mrefu baadae daladala la posta likafika,
nikatulia zangu mbele kwa dereva

Kati ya watu tuliokuwapo ndani ya daladala alikuwapo dada mmoja umri kama 30 hivi,

Muda wote alikuwa na wasiwasi kama ana Jambo linamsumbuwa..

Baada ya daladala kufika kituo cha manzese,
Yule dada alifunguwa mkoba wake akatoa bahasha fulani ya rangi ya kakhi,

Baada ya kufunguwa alipiga Kelele kwa sauti

'''Mama!! Nimetapeliwa,""
Nitamueleza nini mume wangu.

Ikabidi nijaribu kumbembeleza na kujuwa kulikoni?
Baada ya kumsikiliza kwa makini,

Nikagunduwa tamaa ya pesa za haraka hupelekea kutapeliwa..

Yule dada alitoka na mumewe kimara,
Wote wakashuka kituo cha ubungo maji,Ila walikuwa na safari tofauti.

Mumewe akavuka barabara upande wa pili wa jengo la Tanesco ,
Ili akapande magari yanayoelekea buguruni.
Wakati huo bado Pana stand ya daladala pale ubungo Tanesco.

Sasa yule dada anasema wakati anaagana na mumewe,
Alipita Kaka mmoja akadondosha bahasha fulani ya rangi ya khaki.

Yule dada aliiona Ile bahasha akataka kumuita yule kaka aliyoangusha Ile bahasha,

Akatokea jamaa mwingine akaokota Ile bahasha,mbele ya yule dada.
Akaifunguwa Ile bahasha ilikuwa na pesa kibunda cha noti ndani yake.

Kabla hajakaa Sawa akarudi yule Kaka wa mwanzo aliyedondosha Ile bahasha akaja kuulizia pale.

Nimeangusha bahasha ina 1.5 million,
Yule Kaka alilalamika pale mbele za watu,
Lakini jamaa alikana kuokota Ile bahasha.

Pale pale yule jamaa aliyeokota bahasha akamwambiya yule dada,
Hizi ni pesa nyingi,
Na huyu kijana lazima atarudi tena kabla daladala halijaja,

Sasa chukuwa hii bahasha nisubiri kituo cha mbele pale shekilango.
Mimi nakuja.
Jamaa alimwambiya yule dada

Muda wote mume wa yule dada yupo upande wa pili anaona tukio zima,
Ikabidi ampigie simu mkewe ,
vipi mbona upo na hao jamaa kuna nini?
Dada akamwambiya ni jamaa tu mgeni anauliza njia,
Lakini mumewe bado akawa anasumbuwa kwa simu,
Mwisho dada akawa hapokei simu ya mumewe.

Kilichofata baada ya dada kupewa bahasha,
Yule jamaa aliyeokota bahasha, akamwambiya yule dada,

Sasa Mimi nakuamini vipi?
Kukupa 1.5 milion wakati sikujuwi?

""Kama vipi niachie simu yako,''
Tangulia shekilango kituoni,
"Nakuja tugawane."
Dada alikuwa na simu nzr Sana smart.

Kabla dada hajatoa maamuzi ya kutoa simu ,
Yule aliyeangusha pochi akarudi tena,
Akasema jamani nimeangusha milioni na nusu,
Atakayeona bahasha plz ni pesa za Ada ya chuo.
Please, please,jamaa alijiliza pale kituoni

Yule dada akaona simu kitu gani mbele ya 1.5.
Akampa jamaa simu,
Akaingia ndani ya gari.

Kufika manzese ndy dada akaamua kufunguwa Ile bahasha ili azihesabu pesa vizuri.

Anakutana na makaratasi yaliyopangwa vzr kama kibunda cha noti

Na mbaya zaidi hata yule dada mwenyewe,
alipanga kumdhulumu aliyeokota bahasha,
Sababu aliambiwa ashuke shekilango,
Matokeo yake akaamua kupitiliza kituo hadi manzese..

Tamaa hupelekea kutapeliwa.
 
Mshana Jr

Hebu liweke sawa hili swala kama hujawai lizungumzia,,, watu waelewe wanakwepaje...
 
Hebu fafanua vyema huo Ujinga wa Muathirika. Utakuwa umesadia wengi...!
Mkuu; Ndg. yangu, neno Ujinga (by Definition) ni Hali ya Mtu yeyote yule mimi au wewe kutokujua au kuwa na ufahamu kuhusu jambo fulani.
Kwa mantiki hiyo, kila mtu/binadamu ni MJINGA kubali-usikubali.
Kwa hiyo yule mtu muathirika-mtarajiwa ambaye hadi leo 02/04/2022 hajafahamu kwamba kuna watu wanaowalaghai watu kwa mtindo huo ni kwamba bado yeye ni mjinga hadi hapo atakapotanabahi na kufahamu kwamba.. "Aah, kumbe wapo watu wadanganyifu/matapeli wanaotumia njia ovu kuwaibia watu...." hapo sasa atakuwa sio mjinga tena katika jambo hilo. Atabaki kuwa mjinga kwa jambo jingine. Tuko pamoja BabaDesi?
 
Bro heshimu kazi za watu unatafuta mbinu ya kukwepa kutapeliwa ili sisi tukale wapi? Hamna mbinu mbinu ni moja tu utembee na boksa maana hata suruali utavuliwa tu ukikutana nao
 
Habari wakuu

Kwa muda mrefu nimekutana na kesi mbalimbali za watu kuibiwa kwa namna ya kupumbazwa akili ( hypnosis).

Unakutana na mtu anakusalimia, ukishaitikia tu ndo kosa lako[emoji51][emoji51] .. Unakuja kushtuka ulishampa simu, wengine huenda hata bank na kutoa hela na kuwapa hao matapeli.[emoji2365] imagine enzi niko sekondari kuna classmate yeye aliwapa mpaka mkanda wake wa kiunoni manzese pale[emoji16]

Binafsi sijawahi kukutwa na hayo maswaibu, ila najiuliza ni nini kinga ya watu kama hao au hii mbinu ina Apply kwa baadhi ya watu tu ?
Asante mkuu kwa tahadhari. Anayedharau huu ujumbe wako mwache abaki hivyo hivyo mpaka yamkute. Nimeshafunga kumsikiliza mtu nisiyemfahamu. Sasa hivi mtu yeyote anayetaka msaada kwangu wa kuuliza kitu chochote simsikilizi wameshawaharibia hata watu wema. Sina muda kabisa. Mwaka jana kuna mdada kanipumbaza mpaka nikaenda kutoa pesa benki tena kwa wakala badala ya ATM. Mambo ya kipumbavu kabisa. Sasa hivi wanahitaji msaada wa kutu chochote kwangu kabla sijajibu chochote nawakata jicho la hatari mpaka wanakimbia wenyewe!
 
Ukiweza kujizuia na tamaa za pesa za haraka ,
Kamwe huwezi kutapeliwa

Nakumbuka siku moja zamani kidogo,
Nilikuwa pale ubungo maji,, Daresalam.
kabla ya hii barabara ya mwendo Kasi kujengwa.

Niliisubiri daladala kwa muda mrefu baadae daladala la posta likafika,
nikatulia zangu mbele kwa dereva

Kati ya watu tuliokuwapo ndani ya daladala alikuwapo dada mmoja umri kama 30 hivi,

Muda wote alikuwa na wasiwasi kama ana Jambo linamsumbuwa..

Baada ya daladala kufika kituo cha manzese,
Yule dada alifunguwa mkoba wake akatoa bahasha fulani ya rangi ya kakhi,

Baada ya kufunguwa alipiga Kelele kwa sauti

'''Mama!! Nimetapeliwa,""
Nitamueleza nini mume wangu.

Ikabidi nijaribu kumbembeleza na kujuwa kulikoni?
Baada ya kumsikiliza kwa makini,

Nikagunduwa tamaa ya pesa za haraka hupelekea kutapeliwa..

Yule dada alitoka na mumewe kimara,
Wote wakashuka kituo cha ubungo maji,Ila walikuwa na safari tofauti.

Mumewe akavuka barabara upande wa pili wa jengo la Tanesco ,
Ili akapande magari yanayoelekea buguruni.
Wakati huo bado Pana stand ya daladala pale ubungo Tanesco.

Sasa yule dada anasema wakati anaagana na mumewe,
Alipita Kaka mmoja akadondosha bahasha fulani ya rangi ya khaki.

Yule dada aliiona Ile bahasha akataka kumuita yule kaka aliyoangusha Ile bahasha,

Akatokea jamaa mwingine akaokota Ile bahasha,mbele ya yule dada.
Akaifunguwa Ile bahasha ilikuwa na pesa kibunda cha noti ndani yake.

Kabla hajakaa Sawa akarudi yule Kaka wa mwanzo aliyedondosha Ile bahasha akaja kuulizia pale.

Nimeangusha bahasha ina 1.5 million,
Yule Kaka alilalamika pale mbele za watu,
Lakini jamaa alikana kuokota Ile bahasha.

Pale pale yule jamaa aliyeokota bahasha akamwambiya yule dada,
Hizi ni pesa nyingi,
Na huyu kijana lazima atarudi tena kabla daladala halijaja,

Sasa chukuwa hii bahasha nisubiri kituo cha mbele pale shekilango.
Mimi nakuja.
Jamaa alimwambiya yule dada

Muda wote mume wa yule dada yupo upande wa pili anaona tukio zima,
Ikabidi ampigie simu mkewe ,
vipi mbona upo na hao jamaa kuna nini?
Dada akamwambiya ni jamaa tu mgeni anauliza njia,
Lakini mumewe bado akawa anasumbuwa kwa simu,
Mwisho dada akawa hapokei simu ya mumewe.

Kilichofata baada ya dada kupewa bahasha,
Yule jamaa aliyeokota bahasha, akamwambiya yule dada,

Sasa Mimi nakuamini vipi?
Kukupa 1.5 milion wakati sikujuwi?

""Kama vipi niachie simu yako,''
Tangulia shekilango kituoni,
"Nakuja tugawane."
Dada alikuwa na simu nzr Sana smart.

Kabla dada hajatoa maamuzi ya kutoa simu ,
Yule aliyeangusha pochi akarudi tena,
Akasema jamani nimeangusha milioni na nusu,
Atakayeona bahasha plz ni pesa za Ada ya chuo.
Please, please,jamaa alijiliza pale kituoni

Yule dada akaona simu kitu gani mbele ya 1.5.
Akampa jamaa simu,
Akaingia ndani ya gari.

Kufika manzese ndy dada akaamua kufunguwa Ile bahasha ili azihesabu pesa vizuri.

Anakutana na makaratasi yaliyopangwa vzr kama kibunda cha noti

Na mbaya zaidi hata yule dada mwenyewe,
alipanga kumdhulumu aliyeokota bahasha,
Sababu aliambiwa ashuke shekilango,
Matokeo yake akaamua kupitiliza kituo hadi manzese..

Tamaa hupelekea kutapeliwa.
Mjini shule sana yani[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukijua hivyo mute mike ya sim yako,then endelea na ishu zako.
 
Aise hatari sana..one sunny day nikapigwa simu samsung galaxy s3 ya kupewa + kitochi cha itel+350+K + jinsi+t shirt mpya nlzonunua..nlibakiwa na nauli 500 ya kurudi home nlkuwa nimeitenga pamoja na kad ya benki...
25th september ...Sitasahau ila nlijifunza sana na imenisaidia kukwepa watu wanaokuja kwa style hio..
Yote tisa, kumi cha muhimu uhai,pesa zinatafutwa.
 
Nindi ujinga kusemeshwa na mtu usiyemfamu mjibu atumie goggle.
 
Asante mkuu kwa tahadhari. Anayedharau huu ujumbe wako mwache abaki hivyo hivyo mpaka yamkute. Nimeshafunga kumsikiliza mtu nisiyemfahamu. Sasa hivi mtu yeyote anayetaka msaada kwangu wa kuuliza kitu chochote simsikilizi wameshawaharibia hata watu wema. Sina muda kabisa. Mwaka jana kuna mdada kanipumbaza mpaka nikaenda kutoa pesa benki tena kwa wakala badala ya ATM. Mambo ya kipumbavu kabisa. Sasa hivi wanahitaji msaada wa kutu chochote kwangu kabla sijajibu chochote nawakata jicho la hatari mpaka wanakimbia wenyewe!

[emoji122] [emoji122] nothing can beat experience, yakishakukuta unakuwa kauzu bila wasiwasi
 
Hawatumii dawa wala nini,ni tamaa zako tu.
Watakuulizia sehemu,unapowapeleka mnatembea ndio wanaanza kukupigisha story za maisha sijui kuna issue ya kupiga pesa nyingi.
Kwa hiyo unaambiwa uweke kiasi flani ili upige zaidi kumbe hapo ndio unapigwa.

Tamaa yako ndio msingi wao

Ni kweli mkuu mara nyingi tamaa ndo msingi wa utapeli, lakini mara nyingine sio tamaa ni ustaarabu ule wa kiungwana ndo unatucost

Mfano mtu anaulizia wapi jirani kuna hospital, kitendo cha wewe kumjibu unakuja kushtukia baadaye ushaibiwa. Hapo hakukuwa na tamaa yoyote, ila ni kama kupumbazwa fulani ambako hauna ufafanuzi
 
Back
Top Bottom