Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Nina hofu sana ya kuibiwa kitu kinachoongeza umakini yani ata nikitoka bank huwa nacheki nyuma kama kuna mtu ananifatilia,yani kifupi sipendi ujinga wa kujeruhiwa au kuuliwa na pesa zangu!!

Hawa jamaa nahisi nshakutana nao sana…ila mm huwa najibu huku Nipo kasi..anaongea mm namwambia Hapana afu niko serious wakat mwingine najilaumu nahisi kama ni mtu mwenye uhitaji Kweli ila Ndio ivo najifariji na usemi wa dunia hii usimwamini mtu “The world is not safe any more”.
Kuna siku nimetoka ku-change hela posta natoka tuu kuna mzee ananipa mia 500 eti kichwa kina muuma nikamnunulie dawa Phamarcy!! Nikaona napigwa hapa yaani alikua kama amesimama na watu kuniona tu anaanza kunifata, nkajiuliza ina maana ni mm tu ndo naweza kumnunulia dawa wengne hawawezi?
Daah mm jib langu moja tu Hapana huku nasepa…siku ile Yani mda ote naangalia begi langu kama hela hazijapotea!!
 
Mtu mwingine wa kuwa nae makini yule mlie potezana nae mda mrefu haswa labda mlisoma pamoja miaka au Lah , kuna jamaa nilisoma naye o'level nilikuta mjini baada ya miaka mingi akakimbia na simu yangu . Yaani kaomba simu katika nje kama anaongea na kuacha viatu vyake kachukua makubazi ya pale home ndio kasepa moja kwa moja hadi leo sijamuona tena
Mmmh Yani hii ndiyo hatari, najuta Mimi [emoji18][emoji3064]. Siwez ata kuelezea.
 
Na wew ilikuwaje[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
[emoji1787][emoji1787] acha tu mkuu ilikuwa ni kiboko. Unamuamini mtu unayemfahamu. Hamjakutana miaka mingi, Siku anafika Nyumbani unamkaribisha anaomba simu aongee, anatoka nje akijifanya network haipo, looh [emoji28] simu 2 nilibebewa Mimi. Hakuonekana mazima tangu muda huo [emoji1751].
 
Utapeli huo ushatokea kwa rafiki zangu tu.

KISA CHA KWANZA. Ni kile kipindi cha corona, kuna rafiki yangu alikuwa anatoka posta anakuja kigamboni, ile baada ya kuvuka tu maji katika ule mkusanyiko wa watu wengi alitokea jamaa mmoja akawa kama anapiga nae stori as if wanafahamiana muda mrefu maana jamaa alimwendea huyo rafiki yangu kwa confidence sana kiasi akashindwa kujizuia kwenda nae sawa kwa style ya uchangamkaji aliyokuja nayo.

Basi bhana baada tu ya kuanza mazungumzo, ye mwenyewe haelewi ilitokea vipi na jamaa aliishia kona gani ila tu alikuja kushituka akiwa hana simu mfukoni na barakoa pia aliyokuwa amevaa nayo pia alimpatia yule jamaa tapeli [emoji1] na mfukoni hakubakiwa na chochote kitu

KISA CHA PILI. Rafiki yangu mwingine na maeneo ni yaleyale Kigamboni. Ilikuwa mida ya jioni amechoka kukaa nyumbani akaamua aingie mtaani kidogo kunyoosha miguu.

Kule njiani alikutana na mtu ambaye alionekana mgeni wa eneo lile na alihitaji msaada wa kuelekezwa eneo alilokuwa akitaka kwenda, na bahati nzuri au mbaya eneo lile alilohitaji kuelekezwa, rafiki yangu yule alikuwa anapafahamu basi ki usamalia mwema akaamua amuelekeze eneo lilipo ila baada tu ya kuanza kumuelekeza, alikuja kushituka akijikuta yupo njiani kurudi nyumbani na ile kuvuta kumbukumbu vizuri ya kilichotokea ni nini alikumbuka kuwa baada ya kumuelekeza tu yule mgeni hapo hapo yeye mwenyewe alitoa simu yake mfukoni na akamuelekeza mpaka pattern ya simu yake, yaani mpaka na neno la siri la laini zake za simu [emoji1]
 
Kuna mwana JF alisema alichangamkiwa pale karume na mtu asiyemfahamu akijifanya anamfahamu akampa na juice ya miwa na yeye akanywa kweli. Lengo la kumchangamkia ilikuwa tu kuuza juice yake. je, angekuwa tapeli si tungekuwa tunaongea habari nyingine!
 
Sasa bwana Yuda, ina maana unatakuwa uwe na principal ya kutokuangalia watu usoni na kutowasikiliza ? Utachujaje sasa mkuu
Huna haja ya kuchuja, msimamo ni mmoja, hakuna kuitikia salamu, wala samahani ya mtu anakuita. Kama anakujua, itafika muda atakuita jina, mwachie aite kama mara 3 hivi, pengine utaijua hata sauti yake na kumsikiliza.
 
Back
Top Bottom