Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kabla ya Iran kutawaliwa katika mfumo wake wa sasa wa Ki- Ayatollah ilikuwa ikitawaliwa kwa mfumo aina fulani karibia na Ufalme hivi ambao watawala wake walikuwa wakiitwa Shah.
Mashah wawili wa mwisho, baba na mtoto wake walitokana na mapinduzi ya ufalme halisi wa muda mrefu wa Qajar mwaka 1925 ambapo Shah Reza Pahalavi alimpindua Ahmed Shah Qajar na baadaye yeye mwenyewe akapinduliwa na kurithiwa na mtoto wake Mohammed Reza Pahlavi mwaka 1941 aliyekuwa Shah wa wa mwisho wa Iran.
Ufalme wa Qajar uliopinduliwa na mashah wawili waliotokana na mapinduzi walikuwa ni watu wapenda mabadiliko ya kisasa sana, lakini zaidi sana Shah wa mwisho, Reza Pahlavi. Huyu aliipelekea mbio Iran kipindi hicho inaitwa Persia katika kukumbatia usasa (modernization).
Aliweka rasmi katika sheria kuwa Persia(Iran) ni taifa secular(lisilio la kidini), aliwapa wanawake uhuru wote walioutaka, alipiga marufuku wanawake kuva hijab au niqab sehemu nyingi za umma ni pia aliweka uzito wanawake wanaovaa mavazi hayo kuajiriwa katika kazi za umma, alisisitiza na alitoa elimu dunia kwa raia wake, alijenga miondombinu mingi ya kisasa ya barabara, reli, hospitali n.k Lengo lake hasa alitaka kuipeleka Iran njia ya Uturuki ya Mustafa Kemal Atartuk.
Hii spidi kubwa ya mabadiliko ndiyo iliwaibua mashia akina Ayatollah na makundi mengine mengi ya wahafidhina waliotokea katika mlengo wa kidini.
Hawa ni watu waliokuwa na mtazamo wa kizamani sana waliokuwa washamba na maamuma kabisa wa ulimwengu wa kisasa. Walitofautiana na kukosana vibaya sana na Shah Mohammed Reza katika mipango yake ya usasa (modernisation) hadi ikabidi aanze kutumia udikteta kulazimisha mabadiliko. Akaanza kuwafunga wapinzani wake na wengine akawapeleka uhamishoni akiwemo Khomeini(hili lilikuwa mojawapo ya kosa kubwa sana kwake kwani Khomeini alianza kuzungukazunguka mataifa mengine kama Iraq, Uturuki na mwishowe Ufaransa akiendeleza harakati zake ndani ya Iran).
Miaka ya 1970- biashara ya mafuta ikawa mbaya sana pia uchumi wa Iran ukazorota vibaya sana kutokana na kupungua mapato hali iliyozidisha nguvu kwa wapinzani wa Shaha hadi wakaweza kumpindua mwaka 1979 na wakaanzisha mfumo wa Ki-Ayatollah na kufuta au kugeuza mabadiliko karibia yote waliyoanzisha wakina Shah watatu wa mwisho.