Jinsi Iran ilivyojipata chini ya utawala wa Ki-Ayatollah

Jinsi Iran ilivyojipata chini ya utawala wa Ki-Ayatollah

Mbona hujaishangaa India nchi ya tano kwa nguvu za kiuchumi ulimwenguni kuwa na GDP per capital ya 2600$,kwahiyo Iran imeendelea kuliko India?
India sio nchi ya tano kwa nguvu za kiuchumi, usichanganye ukubwa wa uchumi na nguvu za kiuchumi.
Ni mataifa mawili tu hapa duniani kwa sasa unayoweza kusema yana nguvu za kiuchumi, nayo ni Marekani na China.
Haya ndio mataifa ambayo hata uchumi wake ukitikisika ndio unaweza kusema yanatikisa na uchumi wa dunia. Mataifa mengine ni mpaka yawe katika miungano kama OPEC, EU au Arab League n.k
 
Kabla ya Iran kutawaliwa katika mfumo wake wa sasa wa Ki- Ayatollah ilikuwa ikitawaliwa kwa mfumo aina fulani karibia na Ufalme hivi ambao watawala wake walikuwa wakiitwa Shah.

Mashah wawili wa mwisho, baba na mtoto wake walitokana na mapinduzi ya ufalme halisi wa muda mrefu wa Qajar mwaka 1925 ambapo Shah Reza Pahalavi alimpindua Ahmed Shah Qajar na baadaye yeye mwenyewe akapinduliwa na kurithiwa na mtoto wake Mohammed Reza Pahlavi mwaka 1941 aliyekuwa Shah wa wa mwisho wa Iran.

Ufalme wa Qajar uliopinduliwa na mashah wawili waliotokana na mapinduzi walikuwa ni watu wapenda mabadiliko ya kisasa sana, lakini zaidi sana Shah wa mwisho, Reza Pahlavi. Huyu aliipelekea mbio Iran kipindi hicho inaitwa Persia katika kukumbatia usasa (modernization).

Aliweka rasmi katika sheria kuwa Persia(Iran) ni taifa secular(lisilio la kidini), aliwapa wanawake uhuru wote walioutaka, alipiga marufuku wanawake kuva hijab au niqab sehemu nyingi za umma ni pia aliweka uzito wanawake wanaovaa mavazi hayo kuajiriwa katika kazi za umma, alisisitiza na alitoa elimu dunia kwa raia wake, alijenga miondombinu mingi ya kisasa ya barabara, reli, hospitali n.k Lengo lake hasa alitaka kuipeleka Iran njia ya Uturuki ya Mustafa Kemal Atartuk.

Hii spidi kubwa ya mabadiliko ndiyo iliwaibua mashia akina Ayatollah na makundi mengine mengi ya wahafidhina waliotokea katika mlengo wa kidini.

Hawa ni watu waliokuwa na mtazamo wa kizamani sana waliokuwa washamba na maamuma kabisa wa ulimwengu wa kisasa. Walitofautiana na kukosana vibaya sana na Shah Mohammed Reza katika mipango yake ya usasa (modernisation) hadi ikabidi aanze kutumia udikteta kulazimisha mabadiliko. Akaanza kuwafunga wapinzani wake na wengine akawapeleka uhamishoni akiwemo Khomeini(hili lilikuwa mojawapo ya kosa kubwa sana kwake kwani Khomeini alianza kuzungukazunguka mataifa mengine kama Iraq, Uturuki na mwishowe Ufaransa akiendeleza harakati zake ndani ya Iran).

Miaka ya 1970- biashara ya mafuta ikawa mbaya sana pia uchumi wa Iran ukazorota vibaya sana kutokana na kupungua mapato hali iliyozidisha nguvu kwa wapinzani wa Shaha hadi wakaweza kumpindua mwaka 1979 na wakaanzisha mfumo wa Ki-Ayatollah na kufuta au kugeuza mabadiliko karibia yote waliyoanzisha wakina Shah watatu wa mwisho.
Yaani ukisoma jinsi shah mwisho alivyosikitika sana kuona iran inakuwa ya kidini....

Yule alikuwa anaona mbali sana ..
 
Ukishavaa umevaa, hakuna kuvaa uchi,
Huu ndio ushamba walio nao Wa-Iran wanaosumbua nao raia kupitia Guidance/Morality police.
Wewe mwenyewe unaweza kukuta ulizaliwa kwa uzinzi
Kwa nini wewe unataka watu wafanane kwa kila kitu,kila taifa lina customs zao why uone za kwako ni bora kuliko zao??.huo ni ulimbukeni.
 
Ukishavaa umevaa, hakuna kuvaa uchi,
Huu ndio ushamba walio nao Wa-Iran wanaosumbua nao raia kupitia Guidance/Morality police.
Wewe mwenyewe unaweza kukuta ulizaliwa kwa uzinzi
Tatizo lenu mnashinda media za Magharibi, hebu ingia youtube, tafuta youtuber yoyote ambaye katembelea mji wowote wa Iran, anaenda kula ama kufanya jambo la kawaida angalia Wa Iran wanaishi vipi then utaona kila siku unafanywa zwazwa na kudanganywa tu.

Hii street walk ya iran

View: https://m.youtube.com/watch?v=PVCLqfcBNZA&pp=ygULVGVocmFuIGZvb2Q%3D
 
Yaani ukisoma jinsi shah mwisho alivyosikitika sana kuona iran inakuwa ya kidini....

Yule alikuwa anaona mbali sana ..
Alipambana sana kuipeleka Iran njia sahihi ila hakuwa mwanamikakati mzuri pia wa siasa
 
Inategemea unailinganisha Iran na nchi gani,
Iran GDP per capita ni 4700USD ambayo inazidiwa hata na Botswana na Namibia,
Huwezi pata takwimu sahihi za uchumi wa Irani maana wapo nje ya mifumo ya kifedha ya Dunia kwa muda mrefu.
 
Yaani ukisoma jinsi shah mwisho alivyosikitika sana kuona iran inakuwa ya kidini....

Yule alikuwa anaona mbali sana ..
Shah ndo wameiharibu Iran, hata Wa Iran wasio penda utawala wa kiisilamu ukiwa Ambia wachague shah na Ayatolah wanachagua Ayatolah. Yoda kapuliza puliza tu hapo ili awakandie Ayatola.
 
Inategemea kwako maendeleo ni nini,
Kama kwako maendeleo ni nyuklia, makombora na mabomu basi Korea Kaskazini, Pakistan na Iran wameendelea kuliko hata Korea Kusini, Japan, Canada na Brazil.
Jibu kulingana na definition inayotambulika ya neno maendeleo.
 
Kwa nini wewe unataka watu wafanane kwa kila kitu,kila taifa lina customs zao why uone za kwako ni bora kuliko zao??.huo ni ulimbukeni.
Waulize Iran sasa kwa nini wanao guidance patrol/morality police kama huo unaolazimishwa na ma- ayatollah kwa sasa ni utamaduni na mila zao asili.
Vinginevyo soma kwa kirefu historia ndefu ya Iran tangu ikiitwa Persia enze za Medes na Peresi ndio utaelewa vizuri utamaduni wa asili wa Iran.
 
Shah ndo wameiharibu Iran, hata Wa Iran wasio penda utawala wa kiisilamu ukiwa Ambia wachague shah na Ayatolah wanachagua Ayatolah. Yoda kapuliza puliza tu hapo ili awakandie Ayatola.
Kama hujui historia kaa kimya kijana sio lazima ujibu.....uislam ni dini ambayo imeirudusha iran nyuma kwa miaka 1400 sasa ndo maana sasa hv vijana wa iran hawatak tena hilo dini

Wairan ni wa persia soma historia ya iran kabla ya uislam kuingia ndo utajua ni kina nani???

So uislam popote ulipo ni uharibifu kama sio fujo basi ujinga utawala ...kama sio ujinga basi uhuru ukosekana ......
 
Shah ndo wameiharibu Iran, hata Wa Iran wasio penda utawala wa kiisilamu ukiwa Ambia wachague shah na Ayatolah wanachagua Ayatolah. Yoda kapuliza puliza tu hapo ili awakandie Ayatola.
Shah waliiharibu Iran kivipi? msingi wa haya maendeleo yote kidogo unayoyaona Iran kwa sasa umejengwa na Shah.
Tatizo kubwa mojawapo la Shah alijaribu kufanya mabadiliko/modernization kwa matumizi makubwa ya nguvu badala kujenga hoja na ushawishi kwa makundi yote. Halafu Wa-Iran wengi wa sasa ni vijana waliochoshwa na utawala wa kidini wa Ayatollah na wanaotamani aina ya uhuru uliokuwepo enzi za Shah.
 
Huwezi pata takwimu sahihi za uchumi wa Irani maana wapo nje ya mifumo ya kifedha ya Dunia kwa muda mrefu.
Hayo ni makadirio ya juu kupitia proxy na taarifa za kijasusi.
 
Shah waliiharibu Iran kivipi? msingi wa haya maendeleo yote kidogo unayoyaona Iran kwa sasa umejengwa na Shah.
Tatizo kubwa mojawapo la Shah alijaribu kufanya mabadiliko/modernization kwa matumizi makubwa ya nguvu badala kujenga hoja na ushawishi kwa makundi yote. Halafu Wa-Iran wengi wa sasa ni vijana waliochoshwa na utawala wa kidini wa Ayatollah na wanaotamani aina ya uhuru uliokuwepo enzi za Shah.
1. Shah walianzisha kundi linaitwa SAVAK ambalo specific lilikuwa na kazi ya kuua wapinzani wake, Maelfu waliuliwa kikatili kabisa, kuanzia waisilamu hadi Wajamaa.

2. Asilimia 80 ya Wa Iran wakati wa shah hawakuwa na Ardhi, Bali Shah walijilimbikisha ardhi yote ya Nchi.

3. Asilimia 60 ya Wa Iran hawakuwa wakijua kusoma na kuandika wakati wa Shah

4. Hakukuwa na Rule of law anachoamua shah ndo hicho hicho

5. Minorities wote walipigwa marufuku kusoma lugha zao ama kujifunza chochote kuhusu historia yao

6. Walipopata Mafuta badala ya Kutumia kuwaneemesha wananchi wakaanza kununua Silaha Marekani, Hela zote wakawa wanawapa mabwana zao wakati wananchi maisha magumu

Source

Hio article imeandikwa mwaka 1979 Marekani mwaka wa Mapinduzi ku summarize utawala wa Shah.

So mkuu usitudanganye eti Iran ya Sasa imejengwa na Shah nchi ambayo asilimia 35 tu walijua kusoma na kuandika imebadilika hadi zinatengenezwa silaha zake zenyewe na kusupply mataifa makubwa kama Urusi, Shah wangekuepo wangekuwa wananunua tu Marekani kama mwanzo.

Iran imefanya mapinduzi makubwa ya kiteknolojia miaka ya karibuni na sio zamani. By mwaka 2000 Iran ilikuwa nchi ya 53 kwa publications za sayansi, mpaka kufikia 2011 walikuwa wa 17 na mpaka mwaka jana Walifika nafasi ya 15

Sasa kutoka asilimia 80 ambao hata ardhi hawamiliki zaidi ya asilimia 60 ya Wa Iran wa sasa wanamiliki nyumba zao wenyewe.
Kama hujui historia kaa kimya kijana sio lazima ujibu.....uislam ni dini ambayo imeirudusha iran nyuma kwa miaka 1400 sasa ndo maana sasa hv vijana wa iran hawatak tena hilo dini

Wairan ni wa persia soma historia ya iran kabla ya uislam kuingia ndo utajua ni kina nani???

So uislam popote ulipo ni uharibifu kama sio fujo basi ujinga utawala ...kama sio ujinga basi uhuru ukosekana ......
Just warning kama unataka kudiscuss mambo discuss kwa heshima, otherwise nitaku ignore tu.
 
India sio nchi ya tano kwa nguvu za kiuchumi, usichanganye ukubwa wa uchumi na nguvu za kiuchumi.
Ni mataifa mawili tu hapa duniani kwa sasa unayoweza kusema yana nguvu za kiuchumi, nayo ni Marekani na China.
Haya ndio mataifa ambayo hata uchumi wake ukitikisika ndio unaweza kusema yanatikisa na uchumi wa dunia. Mataifa mengine ni mpaka yawe katika miungano kama OPEC, EU au Arab League n.k

Mbona Urusi na Ukraine baada ya kuingia vitani uchumi wa dunia nzima litetereka wakati hizo nchi zinachangia % ndogo kwenye uchumi wa dunia?
Leo baada ya taarifa za Israel kuishambulia Iran masoko ya hisa kote barani Asia yalianguka.

Kila nchi hapa duniani ina umuhimu wake sisi Africa ni masikini lakini ikitokea dunia ikakosa rasilimali zetu dunia itaathirika sana.

Kwani nguvu na ukumbwa vinautofauti gani?
India ni nchi ya 5 kwa uchumi mkubwa baada ya USA, China,Japan na Ujerumani sasa sijui unacho bisha ni kitu gani?
 
Kwanini awazidi ,ya kwamba wao wamelala tu ili wazidiwe na Iran?
Hata hivyo Iran anawazidi mambo mengi hao ulio wataja.
walitakiwa wawe karibia sawa, ila yeye kaachwa mbali sana.. iran alichowazidi wao ni kipi?
 
1. Shah walianzisha kundi linaitwa SAVAK ambalo specific lilikuwa na kazi ya kuua wapinzani wake, Maelfu waliuliwa kikatili kabisa, kuanzia waisilamu hadi Wajamaa.

2. Asilimia 80 ya Wa Iran wakati wa shah hawakuwa na Ardhi, Bali Shah walijilimbikisha ardhi yote ya Nchi.

3. Asilimia 60 ya Wa Iran hawakuwa wakijua kusoma na kuandika wakati wa Shah

4. Hakukuwa na Rule of law anachoamua shah ndo hicho hicho

5. Minorities wote walipigwa marufuku kusoma lugha zao ama kujifunza chochote kuhusu historia yao

6. Walipopata Mafuta badala ya Kutumia kuwaneemesha wananchi wakaanza kununua Silaha Marekani, Hela zote wakawa wanawapa mabwana zao wakati wananchi maisha magumu

Sasa kutoka asilimia 80 ambao hata ardhi hawamiliki zaidi ya asilimia 60 ya Wa Iran wa sasa wanamiliki nyumba zao wenyewe.
1. SAVAK lilikuwa shirika la ujasusi kama zilivyo TISS, CIA, FSB n.k halikuwa kundi kama ambavyo unapotosha hapa.

2.Shah alimiliki asilimia 10 tu ardhi wakati wake, na hiyo ilikuwa ni ardhi ya kifalme. Ardhi nyingine yote iliyobaki ilimilikiwa na mabwanyenye(landlords), wakuu wa kidini(clergy) na viongozi maarfu wa kijamii/kimila. Shah ndio alianza kufanya mabadiliko ya ardhi na alipata upinzani mkali sana kutoka hayo makundi hali iliyosababisha serikali yake kutumia nguvu kubwa kuchukua ardhi kutoka kwao kuwagaia wanavijiji na alizidisha zaidi nguvu ya haya mabadiliko kupitia "White revolution" mwaka 1963.

3.Iran kama zilivyokuwa nchi nyingi za ukanda huo zilikuwa nyuma katika elimu dunia japo Iran ilikuwa na nafuu, lakini ni Shah aliyenzisha mpango wa Literacy corps ambapo vijana wenye elimu ya degree waliajiriwa kwa wingi kuzunguka vijiji kufundisha watoto na kupitia mpango huo pekee watoto zaidi ya milioni 2 ambao waliweza kupatiwa elimu kwa haraka.

4. Wakati wa Shah kulikuwa na utawala thabiti wa sheria, ugomvi ulitokana na viongozi wa kidini na kimila waliokuwa na ushawishi kwa jamii hasa vijijini kupinga mengi ya mabadiliko ya kisasa ya Shah huku wakisisitiza masuala ya kidini kupewa kipaumbele na umuhimu zaidi katika serikali na nchi.

5. Ni kituko na upotoshaji tu kusema Shah aliwaonea minorities wakati yeye mwenye alikuwa anatoka kabila la watu wachache la mazandaranis. Iran haijawahi kuwa na matatizo makubwa ya kikabila na udini katika sehemu kubwa ya historia yake isipokuwa mpaka pale ma-Ayatollah walipochukua madaraka mwaka 1979 ndipo mpasuko mkubwa wa uhasama wa kidini kati ya Shia na Sunni ulipozuka.

6. Kama ufahamu sababu hasa Marekani na Uingereza kotomsapoti na kumpa msaada wowote Shah wakati anapambana na kuvurugana na waliompindua ni hilo suala la mafuta na uchumi ambapo waliona anaelekea uelekeo wa kuifanya Iran taifa imara la kisasa lenye kujitegemea na wao kupoteza maslahi yao na ushawishi wao ukanda huo.
 
1. SAVAK lilikuwa shirika la ujasusi kama zilivyo TISS, CIA, FSB n.k halikuwa kundi kama ambavyo unapotosha hapa.
Iite savak jina utakaloiita ila role yake ilikua ni kuua wapinzani, Iite hata Nursery school haitabadilisha fact maelfu ya waisilamu, wajamaa, wakurd, Turkmenistan etc waliuliwa sababu walikua against government,
2.Shah alimiliki asilimia 10 tu ardhi wakati wake, na hiyo ilikuwa ni ardhi ya kifalme. Ardhi nyingine yote iliyobaki ilimilikiwa na mabwanyenye(landlords), wakuu wa kidini(clergy) na viongozi maarfu wa kijamii/kimila. Shah ndio alianza kufanya mabadiliko ya ardhi na alipata upinzani mkali sana kutoka hayo makundi hali iliyosababisha serikali yake kutumia nguvu kubwa kuchukua ardhi kutoka kwao kuwagaia wanavijiji na alizidisha zaidi nguvu ya haya mabadiliko kupitia "White revolution" mwaka 1963.
Haijalishi ni bwanyenye ama clergy, the issue ni kwamba Asilimia 80 ya nchi hawakumiliki ardhi, je ni sawa? Na shah ardhi haikua yake yeye ndio alidhulumu Ardhi ya wananchi na kujimilikisha, Alikuwa na ndio biggest land owner, so kufanya reform na kupunguza ardhi yake kidogo means nothing kama hio ardhi alipora

The regime that was headed by the semiliterate Reza Shah became increasingly authoritarian and finally dictatorial. His brutality, which included the murder of many of his closest supporters, and his mania for land acquisition, through which he had become the largest landowner in the country, made his regime increasingly unpopular.
Encyclopedia ya Reza Shah hio

3.Iran kama zilivyokuwa nchi nyingi za ukanda huo zilikuwa nyuma katika elimu dunia japo Iran ilikuwa na nafuu, lakini ni Shah aliyenzisha mpango wa Literacy corps ambapo vijana wenye elimu ya degree waliajiriwa kwa wingi kuzunguka vijiji kufundisha watoto na kupitia mpango huo pekee watoto zaidi ya milioni 2 ambao waliweza kupatiwa elimu kwa haraka.
Hizi propaganda tu, waliokua nyuma ni ukanda wa jangwani maeneo kama Saudi ila waarabu na wa Iran wa Mjini for Long time hayo maeneo yalishaendelea na watu walijitambua, Anzia Palestina nenda mpaka Beirut, nenda Damascus, Baghdad hadi Persia huko Iran ndio ilikuwa Civilazition kubwa, waliendelea kushinda nchi nyingi za Ulaya.

Wakati wa Shah Global average ilikuwa ni Asilimia 65 ndio educated, ila Iran ni 35 unaona ni sawa?
images (20).jpeg

Kugongomelea msumari Tanzania miaka ya 80 tulikuwa na literacy rate 59%, kama unaamini jamaa yako Shah alipromote Elimu hali ya kuwa Alipitwa na nchi kibao za ki Africa sawa, Endelea kuamini.

4. Wakati wa Shah kulikuwa na utawala thabiti wa sheria, ugomvi ulitokana na viongozi wa kidini na kimila waliokuwa na ushawishi kwa jamii hasa vijijini kupinga mengi ya mabadiliko ya kisasa ya Shah huku wakisisitiza masuala ya kidini kupewa kipaumbele na umuhimu zaidi katika serikali na nchi.
Unapomkamata mtu kimya kimya na kumuua ni utawala wa kisheria? Nimekuekea link hapo inaelezea kwanini haukuwa utawala wa kisheria, imeandikwa 1979 wakati wa mapinduzi toka chuo chako pendwa Havard, ama nao ni vilaza na propaganda zako ni sahihi?

Jimmy carter Raisi wa Marekani wakati huo baada ya kuingia madarakani alikuwa akigombana nao kila siku kwa dikteta wao, Shah alikuwa ni dictator Kama dictator wengine. A
5. Ni kituko na upotoshaji tu kusema Shah aliwaonea minorities wakati yeye mwenye alikuwa anatoka kabila la watu wachache la mazandaranis. Iran haijawahi kuwa na matatizo makubwa ya kikabila na udini katika sehemu kubwa ya historia yake isipokuwa mpaka pale ma-Ayatollah walipochukua madaraka mwaka 1979 ndipo mpasuko mkubwa wa uhasama wa kidini kati ya Shia na Sunni ulipozuka.
You are kidding right?
shah na hata utawala wa sasa wanawatesa sana wa kurd, Shah aliwaua wengi tu 1967

In short kama ilivyo Taliban Shah alia mini kwenye persianization, Minorities wengi walikuwa suppressed utawala wake.
6. Kama ufahamu sababu hasa Marekani na Uingereza kotomsapoti na kumpa msaada wowote Shah wakati anapambana na kuvurugana na waliompindua ni hilo suala la mafuta na uchumi ambapo waliona anaelekea uelekeo wa kuifanya Iran taifa imara la kisasa lenye kujitegemea na wao kupoteza maslahi yao na ushawishi wao ukanda huo.
Hebu kasome vizuri Historia ya Shah na uhusiano wake na Marekani na Usa,

Mwaka 1941 shah mtoto anampindua Shah baba, na Shah mtoto anakua full supported na west.

Miaka ya 1950s alikua Waziri mkuu mossadeq ndie Alienationalize mafuta na alikua na nguvu kipindi hicho sababu shah mtoto bado hajakamata power vizuri, Shah akataka kumtoa zikatokea vurugu na shah mtoto akasepa, Mataifa ya magharibi yakamtoa mossadeq madarakani na ndio shah mtoto akarudi.

Alivyorudi shah mtoto akawapa Magharibi mafuta, Usa alichukua share kama 40% ya mafuta yote ya Iran kwa ruhusa ya huyo kibaraka wako unaemtetea.
 
Back
Top Bottom