amshapopo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 1,834
- 4,161
Imekuwa ni kawaida kwa desturi zetu za sasa, hususani maeneo ya mijini pindi familia inapohotaji msaidizi wa kazi za ndani ya nyumba, hupelekekea kupiga simu maeneo ya pembezoni mwa miji Ili kupata msaidizi wa kusaidia kazi za ndani.
Wengi wetu tumekuwa tukihitaji wafanyakazi hawa bila kufuata taratibu na Sheria za nchi kuhusiana na umri sahihi na majukumu yapasayo kwa mfanyakazi wa ndani kufanya. Mama wengi wa familia wanakiuka majukumu yao ya familia kwa kisingizio cha kutafuta mfanyakazi.
Tuangalie baadhi ya majukumu yanayokiuka utu na wajibu wa mfanyakazi wa ndani;
Kufanya kazi bila kuzingatia muda sahihi wa Sheria za kazi.
Kushurutishwa, kudhalilishwa na kufokewa na mwajiri.
Kukatishwa masomo kwa kigezo cha kupata ajira mjini.
Kuingiliwa kimwili pasipo ridhaa zao kisa ni wafanyakazi wa ndani.
Kupewa kazi ambazo hakustaili kuzifanya mfano kufua nguo za ndani za baba na mama.
Kutokuwa na mkataba maalumu wa malipo kama wafanyakazi wengine.
Kupewa ujauzito na kufukuzwa na waajiri.
Kudhulumiwa vipato vyao kwa baadhi ya makosa walioyatenda, mfano kupasua vyombo n.k
Baadhi ya suluhisho kudhibiti matendo haya;
Serikali kutunga Sheria itakayo ainisha haki na wajibu wa mfanyakazi wa ndani kama wafanyakazi wengine.
Kupewa mkataba ya kazi na stahiki zao.
Kuwa na chombo maalumu cha kulinda haki zao mfano TUCTA n.k
Sheria kali zitungwe kwa wanaofanyanyia udhalilishaji wa kijinsia.
Wakina baba na mama kutambua majukumu yao ya msingi kwenye familia zao.
Wazazi wa watoto kuepuka tamaa ya kuwatoa watoto wao kufanya kazi za ndani kisa tamaa ya fedha.
Jamii kutambua haki za watoto Hawa.
Asante

Upvote
4