Jinsi kiswahili kinavyomrudisha nyuma Diamond

Hivi watanzania wengi sana wanapenda sana nyimbo za wacongo zinazoimbwa kwa kilingala na wacongo kama koffi olomide,je watanzania hao wanaelewa kilingala ?
 
Nyie ndo mnaowadanganya hao wasanii waimbe kingreza wakati hawawezi!
Naona hata harmonize nae siku hizi anachomeka maneno ya kingereza mengi!

Mkuu mziki ni hisia unapogusa hisia za mteja wako basi umemaliza kila kitu!
Na ili uweze kumkuna vilivyo msikilizaji wako imba kwa lugha yako!

Nakumbuka miaka yetu ile kulikua kuna muziki ule wa south africa ebhanaeeeee wale wajomba walikuwa wanaimba kwa hisia hatari unajikuta kanda nzima unasikiliza vizuri kabisa ila huelewi chochote!

Na nilibahatika kuwaona wakiwa wanaimba laivu walipokuja kupata mafunzo ya kwenda kupigania uhuru huko kwao miaka ya 90+ kwenye kambi yao kule Iringa
 
Haukuwa Wimbo Ilikuwa Style Ndio maana Style Ya ngororo Ya Diamond Isambaa lakini Ojolegba Ya Wizkid Inaeleweka sana Kuliko Kamwambie Ya Diamond
Inaelewekaje wakati kiswahili ni popular kuliko hicho ki-yoruba sijui igbo/Hausa? Acha porojo bana

Gangnam style ni wimbo sio style, kubali kuwa hoja yako imekosa mashiko
 
[emoji870][emoji870][emoji870] Pamoja boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lil kesh,Olamide na Phyno wa Nigeria ngoma zao wanatumia sana Igbo na Yoruba language, lakini ngoma zao nazielewa kinoma na zinavuka border hata wasio elewa lyrics wana-enjoy... tafuta sababu nyingine
 
Kabisa ksma phyno na olamide hawaimbi kingereza kabisa Ni kilugha tu lakini magoma Yao yanatusua.
Diamond sikuhizi ubunifu umepungua nyimbo zake nyingi maneno yanajirudia rudia mfano maneno Kama
kitandani unanimaliza,
Msambwanda
Sotojo
Mtoto fundi
Kungwi
Hayo maneno ukisikiliza nyimbo za hivi karibuni lazima ukutane nayo Ni maka unasikiliza kitu kimoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiingereza wabachoimba wanaijeria wanaelewa wanaijeria wenyewe tu. Nilisikiliza wimbo wa Davido alioimba na Meek Mill aibu niliona mimi.
 
Ni Kweli mkuu, hicho kitu nimekiona kwenye ngoma zake za hivi karibuni.. ubunifu ni Zero kabisa hata Discipline ya kazi saivi Imepungua sana, Kingine Management yake inaogopa kumchana
 
Mleta uzi mziki mzuri sio lugha asee, mziki mzuri ni melody ndio maana unaweza ukasikia wimbo ukajikuta unatikisa kichwa tu pasipo hata kujua maana yake, hao hao wakina Davido n Wiz kid nyimbo zao nyingi tu wamejaza kiYORUBA na ki IGBO na bado tunawasikiliza refer UJUELEGBA by wizkidayo
 
Ajiloge tu aimbe kingereza ndio atapotea zaidi ya sasa
 
Mziki hauna lugha mkuu,Kuna migoma ya kispaniola huwa naiselebuka mpaka chini lakini sijui maana ya nini?
 
Shida utakuwa ujuwi nini maana ya kujulikana.(humaarufu).
 
Ina maana kwa kipindi ambacho walikua sawa kimuziki diamond alikua anatumia lugha gan

Lugha sio kigezo sana cha kufanya muZiki unaoufanya ufike mbali. Music it's all about melody.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu hata yeye anaamua kubalance kwa kushirikisha wa nje waimbe lugha yao kingereza
 
Muziki wenyewe tayari ni lugha ambayo inaeleweka dunia nzima. Music itself is a universal language. Wahindi wametuimbisha sana masongi na tulikuwa hata hatuelewi wanachoimba. Sasa Kuch Kuch Hota Hai nani alikuwa anaelewa?

Una hoja dhaifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…