Kwanza chemsha ziive kiasi
Baada ya hapo kata kitunguu karoti ikune nyembamba na nyanya isage na ukiwa una isaga kama kwenye brenda weka mafuta kidogo
Kisha anza kwa kuweka mafuta kidogo kisha weka kitunguu kikologe mpaka kilegee kisha weka karoti nayo koroga kisha weka nyanya na uiache iive vzri mpaka uone kama kuna mafuta yana jitenga kiasi ndipo uweke njegere kisha changanya na baada ya hapo weka nazi yako kama una tumia nazi ya azamu utaongeza maji kidogo ili upate mchuzi kama una penda mchunzi
Wali wa nazi kama una tumia nazi ya azam hizi za kisasa basi utachemsha maji kisha utakaanga mchele wako na kuweka maji ya moto baada ya hapo utafunika ukiona maji yanakaribia kuisha basi utaweka nazi yako na kupunguza moto uwe mdogo ili nazi ikolee sana
Lakini pia kama una pika wali wa nazi kupitia hzi za kienyeji uta chuja nazi yako na maji ya uvuguvugu tui la kwanza liweke pembeni kisa tui la pili na latatu uta kadilia maji yasiwe mengi af lile tui la kwanza utakuja kuliweka mwishoni baada ya kuona mchele wako au wali wako una karibia kuiva ili wali ukolee nazi
Karibu