Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu
Hapa katikati ya mvutano wa nani anaefaa kuwa mwenyekiti wa Chadema. Baada ya upepo kuonekana kwenda upande wa Lissu, wazee wa kazi wakakaa kikao kimya kimya kama walivyofanya wakati wa Lowasa (lkn safari hii kwa namna nyingine) na kuja na njia ambayo itasaidia kumtia Lisu nguvuni, ili yule mgombea wao aweze kupita kiurahisi katika uchaguzi mkuu wa chama.
Katika kuangalia huku na kule ndo ikaonekana kwamba Dr Slaa anaweza kufaa sana katika dili la kusaidia kukamatwa kwa Lisu, lkn ili hilo litokee ni lazima kuwe na sababu ya kumkamatia.
Dkt. Slaa akapewa kazi ya kutengeneza uongo dhidi ya mkuu wa mhimili uliojichimbia (mama Abdu) na kuuweka kwenye media ili waone Lisu ata react vipi kupitia uongo huo.
Baada ya kuona Lisu hakutilia maanani sana swala hilo, wakaja na gia ya kwenda kumkamata Dr Slaa na kumtupa lupango ili kuona kwamba yule anaejifanya kutetewa na Dr Slaa ambae ni Tundu Lisu atalichukuliaje swala la mtetezi wake uchwara kukamatwa.
Kama hiyo haitoshi, Dkt. Slaa akanyimwa dhamana. Lengo la kumnyima dhamana ni kuangalia kama Lisu atalivalia njuga swala hilo, na pengine kuhamasisha watu wake akiwemo yeye mwenyewe kuingia barabarani kumpigania Dr Slaa apewe apewe dhamana, na hivyo kuwa rahisi kwa Lisu na wafuasi wake ambao wangeandamana kukamatwa na kutupwa ndani, kisha kuja kuachiwa mwisho wa mwezi huu baada ya uchaguzi wao wa chama kuisha na mtu wao kupita katika kinyang'anyiro bila upinzani wowote.
Ama kweli Lisu ana machale aisee. Angekurupuka kujifanya anaingia barabarani kumpigania Dr ilikuwa amekwisha.