Jinsi Lissu alivyoushtukia mtego uliopangwa na mamlaka wakishirikiana na Dkt. Slaa

Jinsi Lissu alivyoushtukia mtego uliopangwa na mamlaka wakishirikiana na Dkt. Slaa

Basi watu wa mfumo watakuwa wa hovyo sana. Chama kinaweza kuendeleaje na uchaguzi wakati makamu mwenyekiti wao na ambaye ni mgombea yuko ndani? Kama waliweza kumchagua kuwa makamu mwenyekiti akiwa ubeligiji anajiuguza huoni kama kumfunga Lisu ndio kutachochea ushindi wake hata akiwa hukohuko gerezani? Huoni kama kutachochea vurugu za kiuchaguzi ndani ya CDM kama uchaguzi utaendelea Lisu akiwa mahabusu?

Silaa amekamatwa kutokana na maneno yake jambo ambalo si vibaya kumshikilia atoe ushahidi kwa tuhuma nzito alizozitoa. Sidhani kama Mbowe ni mjinga kiasi hicho au watu wa kitengo kwamba wamekosa akili kwa kiasi hicho.
Unajua ni sababu gani Lisu alionesha kuchukizwa zaidi Maria alipokamatwa huko Kenya, kuliko kuchukizwa na jinsi Dr Slaa alivyokamatwa na kunyimwa dhamana hapa Tz.

Ukibahatika kuijua sababu hata kwa 20% tu, hautakuwa na sababu ya kupinga nlichoandika. Kuna mambo mengi yanaendelea chini kwa chini ambayo wewe muona karibu hauwezi kuyajua.
 
Uliifuatilia press ya Lema kuhusu Lissu atakavyomlipa fadhila Dr.Slaa?Je,Lema ni sehemu ya hiyo idara?
Lema ni mwanasiasa. Hivyo sometimes mtu anaweza kuliongelea jambo kisiasa. Ila kiuhalisia anakuwa hakulenga kile ulichokisikia kutoka kwake.

Subiri uchaguzi wa Chadema uishe halaf utaona jinsi kesi ya Dr Slaa itakavyoyayushwa kimya kimya.
 
Mungu wa kweli na mwema, tunaweka uchaguzi huu mikononi mwako. Tunaamini kuwa kwa uongozi wako, matokeo yatakuwa ya kutangaza utukufu wako na kuimarisha mshikamano wetu.

Katika jina la Yesu Kristo tunaomba na kushukuru. Amina.
Ameen.. Hakika Mungu atatenda jambo ambalo wengi hawakulitegemea.
 
Watu wakubwa ktk nchi hawawekwi lupango kam watu wa kawaida ktk jamii bali sehemu maalumu ya kupata huduma zote ambazo unaweza ukazipata ukiwa nyumbani kwako
Ndomaana inasemekana kuwa ule ni mtego. Kwa sababu kuna tetesi kwamba Dr huwa anapelekwa kwake usiku kulala alaf alfajiri anarudishwa ili kuwahadaa wanaofikiri kwamba amekamatwa kwa sababu zilizotolewa.

Uchaguzi wa Chadema ukiisha, Dr na yeye kesi yake itaisha.
 
Kwa hiyo kwa mantiki yako Mwenyekiti anahusika na mpango? Aisee
Kwani unafikiri mwenyekiti yuko upande gani?

Kiufupi sio tu anahusika, bali yeye ndio mpangaji mkuu wa tukio ambalo walipanga ili yeye aweze kushinda uchaguzi mkuu wa Chadema kuirahisi bila upinzani mkubwa kutoka kwa mpinzani wake Lissu.
 
Mleta mada alivyo mpumbavu unaweza kukuta ameacha kupyambya kabisa eti kwa ajili ya kutunga huu ujinga. Kuna wakati mwingine unapitia nyuzi humu halafu unatafakari kuhusu familia ya mleta mada, hususani mkewe na watoto, kisha unasikitika sana.
Jadili kilichoandikwa mkuu, hayo ya familia hayahusiani na uzi huu.
 
Huenda Lissu ana watu wake katika system wanaompa habari ya kila kinachopangwa juu yake.
Hata mimi nafikiria hivyo mkuu, maana kumsusa chawa anaejifanya kumpigania sio jambo la kawaida.

Kuna kitu nyuma ya pazia.
 
Huu uzi umejikita kwenye umbea na tetesi kuliko facts. Lowasa kuhamia CHADEMA haikuwa ishu za usalama wa taifa, tena hiki ndio kipindi CHADEMA ilipata wabunge wengi kuliko wakati wowote. Hata uchaguzi mkuu, hakuna uhakika kama JPM alishinda ule uchguzi.
Unapotaka kubishana na mtu mwenye akili kubwa kama mimi, basi hakikisha na wewe kichwani una angalau nusu au nusu na robo ya akili kama yangu.

Hebu twende mdogo mdogo.

Lowasa aligombea kipindi ambacho Chadema ilikuwa imeungana na vyama vingi (UKAWA) hivyo ni lazima kura zake ziwe nyingi kuliko alizopata Mbowe 2005, na Slaa 2010. Kwa muungano ule wa vyama karibia vyote vikubwa vya upinzani hata ungekuwa wewe ndio mgombea wao ungesomba kura tu kutoka Chadema, NCCR Mageuzi, CUF nk. Maana wengi walichagua sio kwa sababu Lowasa ni msafi au mchafu. Bali walimchagua kwa sababu vyama vyao na viongozi wao wameamua kumuunga mkono yeye kama mgombea wao wa pamoja wa uraisi.

Na hilo Kikwete ambae ndio mastermind wa mchezo na team yake walilitambua sana kabla hata ya kumtuma aende huko. Ndiomaana hata Lissu juzi amekiri kufanya makosa makubwa ya kumkaribisha Lowasa, kwa sababu walikuja kugundua kwamba jamaa alikuwa amepandikizwa mahususi na mfumo ili kuhakikisha upinzani hauingii ikulu, bali unashinda tu viti vingi vya ubunge na viti maalum basi.

Kwa muungano ule hata Hashim Rungwe angekuwa mgombea wa ukawa angepata kura nyingi kuwahi kutokea katika maisha yake.
 
Ina maana hwdi Leo hujui?

Mwingine yupo selo alitaka kujifanya bosi wa usalama kwamba wanaripoti kwake na wako tayari kuingia mtaani
Inaonekana hajui mambo yanakwendaje nchini 🤣🤣🤣
 
Uzushi.

#FREE DR.SLAA
Uchaguzi wa Chadema ukishaisha Dr Slaa atakuwa free tu mkuu. Maana mbinu ya kumfunga Slaa, na kumnyima dhamana kwa makusudi ili Lissu aingie babarani wamfunge hadi uchaguzi wa chadema upite imeshindikana.
 
Uchaguzi wa Chadema ukishaisha Dr Slaa atakuwa free tu mkuu. Maana mbinu ya kumfunga Slaa, na kumnyima dhamana kwa makusudi ili Lissu aingie babarani wamfunge hadi uchaguzi wa chadema upite imeshindikana.
Nchi isiyofuata sheria inafuata maagizo kutoka juu kosa la Dr.Slaa linadhamana.
 
Nchi isiyofuata sheria inafuata maagizo kutoka juu kosa la Dr.Slaa linadhamana.
Tatizo sio dhamana.. tatizo ni jinsi walivyoitengeneza kesi yenyewe kwa lengo la kumuwekea mtego Lisu. Slaa anajua anachokifanya na Lisu ashakifahamu kile Slaa anachokifanya ndiomaana unaona hajishughulishi nae sana.

Slaa ashapewa advance na kuambiwa avumilie kwa mateso madogo ya kuwekwa jela week 1 au 2 ili kuangalia namna ya kumtia Lisu kwenye 18.

Vijana mmekuwa wepesi kiasi hiki mpaka kufikia hatua ya kumsahau yule Slaa aliepewa ubalozi na huyu anaejifanya mpinzani wa mchongo.

Mmeshasahau alichokuwa anaongea Dr Slaa kuhusu swala la Lissu kupigwa risasi 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom