Shukrani mkuu. Kama nitaamua kufanya hivyo nadhani kuna matukio mengi sana ya kufurahisha, kuburudisha na kushangaza ambayo sijayaweka hapa itabidi niyaweke kwenye kitabu. Kuna jamaa yangu mbongo sasa hivi yuko UK Manchester nilisafiri naye wakati natoka Bongo. Kuna mambo aliyafanya pale Lusaka, maana tulilala hapo, pia siku zake za mwanzo tulipofika Johannesburg kabla hajatimukia England kuna stori nzuri sana ya kusisimua inayomhusu, huwa nacheka sana nikimkumbuka huyo baharia. Kwa hiyo kuna mambo mengi sana ambayo sijayaweka hapa ambayo yataongeza mvuto wa kitabu.Kuna kitabu kizuri kabisa hapa. Please compile hizi, ziboreshe kidogo (e.g. tumia tafsida baadhi ya simukizi ili kisiwe na ukakasi kwa baadhi wasomaji). Naona kipaji ndani yako cha kusimulia.
Usiache kuandika kitabu(actually umeshaandika, kiboreshe tu).
Kabisa, hapa una kitabu kizuri. Mtu akianza mwanzo anatamani kuendelea....good work, good talent. Ni mwandishi mzuri pia na makini....typos kama zipo ni chache sana. Kila la heri.Shukrani mkuu. Kama nitaamua kufanya hivyo nadhani kuna matukio mengi sana ya kufurahisha, kuburudisha na kushangaza ambayo sijayaweka hapa itabidi niyaweke kwenye kitabu. Kuna jamaa yangu mbongo sasa hivi yuko UK Manchester nilisafiri naye wakati natoka Bongo. Kuna mambo aliyafanya pale Lusaka, maana tulilala hapo, pia siku zake za mwanzo tulipofika Johannesburg kabla hajatimukia England kuna stori nzuri sana ya kusisimua inayomhusu, huwa nacheka sana nikimkumbuka huyo baharia. Kwa hiyo kuna mambo mengi sana ambayo sijayaweka hapa ambayo yataongeza mvuto wa kitabu.
Jumatano mkuu. Kuweni na subra tu ndugu zangu.Mkuu mzigo utadrop tena lini?
Bora ukimaliza usiache kuandika kitabuJumatano mkuu. Kuweni na subra tu ndugu zangu.
Ile stori ya yule jamaa toka wiki iliyopita nimemsikia akiielezea redioni. Hiyo stori niliisoma hapa na nilishangaa sana kuisikia akiielezea RFA. Nilichokigundua kwenye hiyo story ni hiki: Yule msimuliaji wa hiyo stori kule redioni sio huyu aliyeileta hapa JF. Inaonekana huyo jamaa wa redioni kaiiba hiyo stori kutokea hapa JF na kuipeleka huko redioni maana nilivyokuwa namsikiliza kama anajing'atang'ata sana kwenye kusimulia kwakwe, yaani ukimsikiliza kwa makini hana ile natural flow ya kusimulia ambayo anatakiwa aionyeshe kama mhusika wa tukio, anasimulia kama vile na yeye amesimuliwa, halafu cha pili hata kiswahili kama vile hayuko fluent ukilinganisha na maisha aliyoishi. Maana mtu kama wazazi wote walikuwa watumishi tunategemea huyo mtu ataongea kiswahili kilichonyooka kwa sababu ameishi mazingira ya kuongea kiswahili muda wote tofauti na mtu aliyekulia kijijini. Kitu kingine hiyo stori mie binafsi naiona kama ni chai. Haina uhalisia kabisa, kuna mambo mengi sana ya kufikirisha kuhusu hiyo stori.Bora ukimaliza usiache kuandika kitabu
kuna Member humu jukwaani anaitwa LWANDA MAGERE alileta Tukio la Jini mwanamke toka Singida Baba yake akampeleka Musoma, alipomaliza kisa hicho akweka cua utajiri wa kikongo, akaanza kuuwa watu apate damu, alituomba twende Telegram tukamchangia huko, cha ajabu leo kasikika Redio Free Afrika saa 4 asubuhi kamwaga Story ileile, sijajua kule kalipwa au ni njia yake ya kupata waumini kwa njia ya Dini.
Naomba usiuze hadithi yake kwa vyombo vya habari bora ibane utoe kitabu na sisi tumalizie hivyo vipengele vi4 vilivyobaki.
Kuna siku watoto wetu wataandika script wacheze filamu sifa itarudi kwako
Ila konda msafi kuna kitu unakosea..ahadi zako nyingi ni zile ambazo sio timilifu..last week uliahidi j5 ungeleta MKEKA wa maana..matokeo yake ukaleta story ya kawaida yenye aya kama 8 tu...hahahahha....leo tena umetujaza kuwa j5 inaisha..(binafsi naamini haitaisha j5 maana ahadi zako hazitimii)...lakini mkuu, mda mwingi upo online JF, hivi ungekuwa unaandika kidogo, una save then unakuja kuandika kidogo mwisho unamaliza unatuma si ingekuwa imeenda mbali hadi now?...Kama kweli ungekuwa na nia ungeshaimaliza maana kama mtu ukiamua kuandika kwa nusu saa tu lazima uandike kitu kirefu...Ile stori ya yule jamaa toka wiki iliyopita nimemsikia akiielezea redioni. Hiyo stori niliisoma hapa na nilishangaa sana kuisikia akiielezea RFA. Nilichokigundua kwenye hiyo story ni hiki: Yule msimuliaji wa hiyo stori kule redioni sio huyu aliyeileta hapa JF. Inaonekana huyo jamaa wa redioni kaiiba hiyo stori kutokea hapa JF na kuipeleka huko redioni maana nilivyokuwa namsikiliza kama anajing'atang'ata sana kwenye kusimulia kwakwe, yaani ukimsikiliza kwa makini hana ile natural flow ya kusimulia ambayo anatakiwa aionyeshe kama mhusika wa tukio, anasimulia kama vile na yeye amesimuliwa, halafu cha pili hata kiswahili kama vile hayuko fluent ukilinganisha na maisha aliyoishi. Maana mtu kama wazazi wote walikuwa watumishi tunategemea huyo mtu ataongea kiswahili kilichonyooka kwa sababu ameishi mazingira ya kuongea kiswahili muda wote tofauti na mtu aliyekulia kijijini. Kitu kingine hiyo stori mie binafsi naiona kama ni chai. Haina uhalisia kabisa, kuna mambo mengi sana ya kufikirisha kuhusu hiyo stori.
Nilihisi utakua umeiacha njiani ingeniuma sana,Matukio yote nayasummarise hapa angalau nitoe lawama maana mnavyonishambulia si kitoto.
Baada ya Khumbu kuja na huo mkoko mpya nikamwuliza ameupataje. Akasema kanunua kwa mkopo. ...Baadae kupitia kwa yule demu wa mshikaji niliyewaambia alihamia, alinipa siri ya huo mkoko mpya wa Khumbu. Aliniambia hiyo ndinga kanununuliwa na Mayor wa Durban. Khumbe hata ile habari ya kuniambia kuwa kapata kazi bank hatutakuwa tunaonana mara kwa mara ilikuwa uongo tu. Alitengeneza mazingira ya mimi kutokuwa namuhitaji kila mara ili Mayor akimuhitaji awe anapatikana. Yaani mimi aniweke kando ili awe huru na Mayor. Hivyo hizo story za kuwa busy na kazi ilikuwa za uongo.
Siku niliyotaka kuingia mikononi mwa police:
Wale jamaa walianza kufungia mzigo humu ndani tulimokuwa tunaishi. Lile gheto la kule mwanzo ulikokuwa unafungiwa mzigo waliacha kulitumia. Hivyo mzigo ukaanza kupimwa humo humo getoni tunapoishi. Binafsi kukaa kwenye nyumba na hayo makitu kilikuwa ni kitu ambacho nilikuwa sikitaki kabisa. Baada ya mambo kuanza kufungiwa humo nikaanza mchakato wa kuhama maana niliona hapa naenda kuhatarisha maisha yangu ya chuo. Nilijua tu kuna siku tutavamiwa humu.
Kufunga hayo madude wanatumia hii mifuko ya plastic tuliyokuwa tunaiita ya rambo. Sasa kwenye kufunga lazima kuwe na vipande vipande vya hiyo miplastic kwenye kukatakata. Na hivyo viplastic ukikutwa navyo hata kama hawajakuta mzigo umekwisha maana wazee wanavijua hivyo vipande vya plastic huwa vinasababishwa na nini.
Sasa hawa jamaa kila wakifunga walikuwa wanavizoa tu hivyo vipande na kuvikusanya na kuviweka kwenye makabati. Walikuwa wanasubiria mpaka yawe mengi ndio wakatupe. Kitendo cha kuishi na hivyo vipande vya plastic kilikuwa kinaninyima amani kabisa, halafu ukiwaangalia hawa masela hata hawajali kabisa. Nilichokuwa nafanya ilikuwa kila asubuhi nikiwa naenda chuo navishindilia kwenye begi naenda kuvitupa mbele ya safari ili angalau tukivamiwa wasikute ushahidi wowote. Maana hawa jamaa zangu walikuwa hawajali kabisa.
Sasa siku moja ilikuwa Jumapili, na sikuwa na mpango wa kwenda kokote. Mule ndani kulikuwa na hivyo vipande vya viplastic. Nikaamua acha nikavitupe ili nishinde home kwa amani. Nikawa nimevishindilia kwenye begi langu la shule. Ila kama Mungu tu ameniambia, Konda msafi be careful. Japo nilikuwa natoka mara moja kwenda kuvitupa, niliamua kuvaa kama vile naenda mbali. Yaani sikutaka kutoka let's say nimevaa bukta na vest kwa sababu najua natoka mara moja na kurudi. Nilivaa nguo kama naenda mjini au chuo. Nikachukua kabisa na kitambulisho changu cha chuo. Nikaweka begi mgongoni, nikatoka ndani, nikashusha ngazi na kuanza kuelekea getini nikiwa na rimoti ya geti. Ile kufungua geti tu nakutoka nje ya geti, mara pah! Kipira cha wazee kimepiga break miguuni kwangu, dah! Roho ikalipuka pah! Nikasema hapa nimekwisha. Wakisema tu fungua hicho kibegi tuone ndani kuna nini nimekwisha. Nikawa naona sasa shule ndio imefikia mwisho. Kipira kimesimama miguuni kwangu. Walikuwa askari weusi. Wakashusha kioo cha gari upande niliokuwepo wakaniambia nisogee karibu. Nikasogea, jamaa walikuwa wawili, kama nilivyosema wote weusi wapo kwenye uniform. Nikawa najitahidi nisionyeshe wasiwasi wowote. Wakaniuliza, unakaa humu ndani? Maana nilikuwa ndio nimetoka tu hapo getini. Nikasema ndio nakaa humu. Wakaniuliza tena, humo kwenye begi kuna nini, nikasema kuna vitabu vya dini, naelekea kanisani kufundisha kipindi cha dini kwa ajili ya watoto. Halafu kile kitambulisho cha chuo nilikuwa nimeking'iniza kifuani. Wakaniuliza wewe ni mwanafunzi, nikasema ndio, nikawapa kile kitambulisho wakakiangalia harafu wakanirudishia. Kisha wakasema tulikuwa tunakusalimia tu, wahi kanisani ukamtumikie Mungu. Wakakanyaga mafuta wakasepa, dah! Aisee! Kwanza nilifikiria sijui nirudi ndani nisiendelee kwenda kuyatupa haya madude. Nikaona acha niendelee na safari ya kwenda kuyatupa maana wasije wakageuka wakaniona tena narudi ndani nikawapa wasiwasi, mbona huyu kasema anaenda kanisani halafu amerudi ndani tena? Basi nikaanza kutembea fasta, hapo naangalia kona yoyote nitakayokutana nayo nipige, nipotee kabisa kwenye hiyo barabara. Kona tu ya kwanza nilipoipata nikaikamata, nikatembea mbele kidogo tu, nikafungua begi na kuyatoa hayo madude fasta na kuyatupa. Nikatembea mbele kabisa huko kuzunguka ili nirudi nyumbani kutokea upande mwingine.
Itaendelea jamani.... nilisema nitasummarise ila nashindwa kusummarise. Huko mbele acha nijifunze kusummarise.
Mkuu Fohadi, kujibu comments na kuandika stori ni vitu viwili tofauti. Kuandika stori inahitaji muda. Mwanzoni nilikuwa naandika mfululizo na kuitupia mara kwa mara kwa sababu nilidhani niingeimaliza fasta tu lakini kadri muda ulivyoenda nikaona hii kitu nikitaka niielezee na ieleweke sio ya kuisha fasta. Ni stori iliyochukua muda wa miaka 6, kuna mambo mengi tu sijayaelezea lakini bado sijaimaliza. Kiufupi inahitaji utulivu sana. Leo mchana kwa sababu nimeshinda nyumbani nilitaka nipunguze mzigo kidogo, nitupie hata episode moja lakini kuna mambo ya kikazi yakaingia kati.Ila konda msafi kuna kitu unakosea..ahadi zako nyingi ni zile ambazo sio timilifu..last week uliahidi j5 ungeleta MKEKA wa maana..matokeo yake ukaleta story ya kawaida yenye aya kama 8 tu...hahahahha....leo tena umetujaza kuwa j5 inaisha..(binafsi naamini haitaisha j5 maana ahadi zako hazitimii)...lakini mkuu, mda mwingi upo online JF, hivi ungekuwa unaandika kidogo, una save then unakuja kuandika kidogo mwisho unamaliza unatuma si ingekuwa imeenda mbali hadi now?...Kama kweli ungekuwa na nia ungeshaimaliza maana kama mtu ukiamua kuandika kwa nusu saa tu lazima uandike kitu kirefu...
NIONAVYO MIMI..
1. Mkuu unafurahi sana unavyoona wana wanaulizia hii story kila muda. Maana kama unapata mda wa kusoma comments kwenye uzi wako na kureply, unakosaje muda wa kuandika story yako? Nahisi mkuu unafurahi kuona notifications zimejaa quotes kuhusu uzi wako.
2. Story yako imeshapoteza mvuto..watu wamesubili na wameshazoea...haina mvuto tena kama ule wa mwanzo na haija vuta tension ya watu tena... wiki hii inayoisha leo umeandika post chache na fupi kweli tofauti na ahadi yako ilivyokuwa mwanzo.
3. Sitaki nataka zako zimefanya mpaka story imekosa mvuto..HOW?, Uliwaambia watu hutaimalizia, wakakubembeleza wee mwisho ukaja na conclusion mara oooh khumbu alifariki...sasa sitaki nataka zako ndo zimeharibu utamu wa story, yaani watu wanasoma huku wanaujua mwisho wa story, ile ladha imeotea.
4. Inshu ya bundle haina logic, JF haili bundle sana na pia hata wasomaji na wana tumia bundle...as long as umeamua kuandika kwa hiarai, andika tu mkuu.
USHAURI:
Mkuu siku nyingine usilete tena story hapa JF maana unapenda sana kutrend. Unachelewesha story isiishe ili kila saa wakutaje taje..trust me, kama usingekuja na zile episodes 32 za kwanza mapema, huu uzi wako usingekuwa hai hadi leo maana watu wasingeweza kuvumilia kiu kwa kitu kisichoeleweka ila ulikuwa mjanja kuteka hisia za wtu.
HITIMISHO: Uwezo wa kuandika story ndefu kwa siku unao, nia ya kuandika unayo, muda wa kuandika unao ila tu sababu za kutoandika/kuchelewesha story HAUNA....Basi tu unapenda trending na kiki kama wasanii
Ni mimi Mtetezi wa wana JF wanaoogopa kukwambia ukweli.
Shukrani mkuu kwa kunielewa.Kumchangia mleta uzi ama kutokumchangia ni suala na maamuzi binafsi. Kama unao uwezo, toa na kama huna/hutaki tulia. Mambo yakuanza kuwaita mods kwa jambo ambalo wengine wameridhia ni kuwakosea heshma. Mods hawahusiki na michango iweje tuwashurutishe kuingilia kati. Halafu mbna sijaona sehemu mtoa mada amesema ni lazima uchange?
konda msafi endelea kwa muda wako. Tuko pamoja
Miendelezo ipo kibao mkuu. Pekua kila page utaipata.Nilihisi utakua umeiacha njiani ingeniuma sana,
ila tunashukuru Mkuu kwa muendelezo huu. Ila hii story imekula siku ya jana na leo kuisoma hivi na bado naendelea kusaka miendelezo zaidi...
[emoji122][emoji122]
Hope J5 utaweka mzigo wote? Tumalizane na hii story Mkuu...Jumatano mkuu. Kuweni na subra tu ndugu zangu.
Ndio huyo huyo sema kuna wengine wanauwez wa kuandika lakn ukiwapeleka kweny kuongea unaweza kushangaa kabisa lakn ndio huyo huyo mzee wa show za kimkakatIle stori ya yule jamaa toka wiki iliyopita nimemsikia akiielezea redioni. Hiyo stori niliisoma hapa na nilishangaa sana kuisikia akiielezea RFA. Nilichokigundua kwenye hiyo story ni hiki: Yule msimuliaji wa hiyo stori kule redioni sio huyu aliyeileta hapa JF. Inaonekana huyo jamaa wa redioni kaiiba hiyo stori kutokea hapa JF na kuipeleka huko redioni maana nilivyokuwa namsikiliza kama anajing'atang'ata sana kwenye kusimulia kwakwe, yaani ukimsikiliza kwa makini hana ile natural flow ya kusimulia ambayo anatakiwa aionyeshe kama mhusika wa tukio, anasimulia kama vile na yeye amesimuliwa, halafu cha pili hata kiswahili kama vile hayuko fluent ukilinganisha na maisha aliyoishi. Maana mtu kama wazazi wote walikuwa watumishi tunategemea huyo mtu ataongea kiswahili kilichonyooka kwa sababu ameishi mazingira ya kuongea kiswahili muda wote tofauti na mtu aliyekulia kijijini. Kitu kingine hiyo stori mie binafsi naiona kama ni chai. Haina uhalisia kabisa, kuna mambo mengi sana ya kufikirisha kuhusu hiyo stori.