Peramiho yetu
JF-Expert Member
- May 25, 2018
- 5,303
- 14,983
Mkuu tumesubir had tumechoka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana niyeye mwenyewe maana jamaa ni rafikiyangu sana tu na sisi ndio tulimpa hiyo connection ya RFA.Ile stori ya yule jamaa toka wiki iliyopita nimemsikia akiielezea redioni. Hiyo stori niliisoma hapa na nilishangaa sana kuisikia akiielezea RFA. Nilichokigundua kwenye hiyo story ni hiki: Yule msimuliaji wa hiyo stori kule redioni sio huyu aliyeileta hapa JF. Inaonekana huyo jamaa wa redioni kaiiba hiyo stori kutokea hapa JF na kuipeleka huko redioni maana nilivyokuwa namsikiliza kama anajing'atang'ata sana kwenye kusimulia kwakwe, yaani ukimsikiliza kwa makini hana ile natural flow ya kusimulia ambayo anatakiwa aionyeshe kama mhusika wa tukio, anasimulia kama vile na yeye amesimuliwa, halafu cha pili hata kiswahili kama vile hayuko fluent ukilinganisha na maisha aliyoishi. Maana mtu kama wazazi wote walikuwa watumishi tunategemea huyo mtu ataongea kiswahili kilichonyooka kwa sababu ameishi mazingira ya kuongea kiswahili muda wote tofauti na mtu aliyekulia kijijini. Kitu kingine hiyo stori mie binafsi naiona kama ni chai. Haina uhalisia kabisa, kuna mambo mengi sana ya kufikirisha kuhusu hiyo stori.
Ngumu kumeza.. 😄Mambo vipi...
Naona wote maskini ,mtoa mada na wachangia mada.
Ndo mana nilimpiga chini konda msafi sababu ni fukara wa kutupwa, mpenda mteremko na ana mawazo ya kimaskini.
Sasa story hata haijafika kati kashaanza omba omba hela za bando.
Ooh mara itatokea jina la kampuni.
Kama bando si watu wamemchangia hao watatu....ana japo 5000.
Kwa nn asinunue bando la mwezi......
Umaskini huu utamuuaaa
Ni kweli ni yeye mwenyewe maana kuna kitu anasisitiza mara kwa mara kuwa ni Mtumishi wa Mungu.Hapana niyeye mwenyewe maana jamaa ni rafikiyangu sana tu na sisi ndio tulimpa hiyo connection ya RFA.
Hii chaiMwaka 2008 niliingia Durban baada ya kuitwa na jamaa zangu waliokuwa huko. Hawa jamaa zangu tuna undugu pia. Kaka yao kaoa shangazi yetu, na pia kaka yetu kaoa dada yao, ni kama tumeoleana, wao wameoa kwetu na sisi tumeoa kwao. Pia hawa jamaa tumesoma shule moja ya msingi japo madarasa tofauti.
Historia fupi kabla sijaingia Durban. Nilifika South Africa toka 2003. Nilifikia Johannesburg. Joburg nilienda kama volunteer kwenye taasisi moja ya kidini ambayo nisingependa kuitaja. Nikiwa naendelea kufanya kazi kwenye hiyo taasisi niliwaomba wanisaidie kumalizia elimu nyangu ya sekondari. Walinikubalia na process zikaanza kufanyika. Ilibidi nirudi Tanzania kwa ajili ya kwenda shule niliyokuwa nasoma ili kupata nyaraka za kuonyesha nimesoma mpaka level gani maana nilitoka bongo nikiwa hata sijamaliza form three. Mambo yalienda vizuri na niliweza kuanza masomo kwenye shule moja inaitwa Mosupatsela High School iliyopo kwenye kitongoji kinaitwa Kagiso. Kagiso ipo karibu na suburb moja inaitwa Krugersdorp. Nilimaliza high school 2007, na 2009 nikafanikiwa kuingia chuo. Mwaka 2008 ndio nikapata mawasiliano na hao ndugu zangu waliopo Durban, Kwa Zulu Natal.
Huko Joburg sio kwamba sikuwa na mahusiano, mahusiano nilikuwa nayo ila nimeamua kuongelea mahusiano ya Durban maana vurugu za Durban naweza kusema kama ni jembe basi mpini ulivunjikia Durban. Kuna mambo kila nikiyakumbuka yanafurahisha na kuhuzunisha. Durban kuna mambo mengi nimeyafanya, mengine siko proud nayo kabisa. Mojawapo ni hili la mshikaji kumleta demu gheto na tukamla wote wawili, demu mwenyewe alilidhia. Hili wala sitaliongelea.
Mwaka 2008 nikawa nimeingia Durban. Nilipanda basi sehemu moja inaitwa Park station mida ya saa tatu usiku. Saa tisa alfajiri nikawa nimetia timu stand ya mabasi Durban. Nikawacheki wenyeji wangu kwenye simu, wakasema nisubiri kupambazuke watanifuata. Asubuhi jamaa zangu wakaja na kipira kunichukua. Break ya kwanza nikapelekwa sehemu moja inaitwa “the workshop”. The workshop ipo downtown Durban, ipo karibu tu na kituo cha mabasi. Kipindi hicho masela wangu walikuwa na goli la viatu vya kike. Tulipofika hapo workshop jamaa wakawa wanafunga tent ili wapange viatu tayari kwa biashara. Baada ya kumaliza kupanga viatu na movements za watu kwenda kazini zishaanza kuwa nyingi jamaa akaniambia sasa ni muda wa kunipeleka magetoni nikapumzike kwanza. Tukaingia kwenye ndinga na safari ya kwenda magetoni ikaanza. Tukiwa tunaelekea magetoni jamaa akapitia KFC ili nipate kitu cha kwenye mabox kwa ajili ya msosi. Jamaa walikuwa wamepanga sehemu moja inaitwa Rossburg. Walikuwa wamechukua flat nzima yaani floor nzima. Kwenye hiyo flat walikuwa wanashare watu watatu. Flat ilikuwa na vyumba vitatu, sebule moja kubwa, jiko na bafu. Pia kulikuwa na kichumba kimoja kwa ajili ya store. Sasa kwenye hicho kichumba nilikuwa nalala mimi na mshikaji mmoja ambaye pia ni homeboy. Nyumba nzima tulikuwa watu watano, yaani Jamaa zangu wawili walioniita (ni mtu na mdogo wake), Mburundi mmoja, jamaa mmoja Mbongo alikuwa akiitwa baba Isa, na mimi sasa. Hawa jamaa wote walikuwa na mademu zao wa kizulu. So siku ya kwanza ikaisha kwa kupumzika.
Siku ya pili jamaa wakaniambia nikiamka nifanye mpango wa chai kisha nipande taxi kwenda workshop wanakofanyia biashara. Kule daladala zinaitwa taxi. Kule taxi zinaitwa “meter taxi”. Ukisema taxi unamaanisha daladala. Nilipoamka, nikafanya utastaarabu wa chai kisha nikapanda taxi kuelekea workshop. Jamaa enzi hizo walikuwa wanaamuka saa 11 alfajiri kwa ajili ya kujiandaa kwenda kufungua goli. Saa 12 asubuhi yatari wapo kazini. (Sasa hivi jamaa hawauzi tena viatu, wanafanya biashara za magari, ni madon wakubwa. Sembe inalipa).
Maisha rasmi ya Durban yakaanza. Nikawa kila siku naamka alfajiri tunaenda kufungua goli la viatu. Biashara ilikuwa nzuri sana hasa siku za Jumamosi na Jumapili. Workshop siku za Jumamosi na Jumapili ilikuwa inajaa watu sana. Of course hata siku zingine watu walikuwa wanajaa lakini siku za weekends ilikuwa funga kazi. Watu wa Durban na vitongoji vyake siku za weekends ndio siku za kwenda kutembea town. Na ndio siku wabongo huzitumia kwenda kupiga mchomoko maana watu huondoka familia nzima na kwenda town kufurahia maisha. Pia shamrashamra za weekend huko huanza Ijumaa. (Mchomoko ni wizi wa kwenda kuvunja majumba na kuingia ndani na kuiba). Kule ukitaka kumjua kama demu ni wako na anakupenda muombe muonane siku za weekends. Demu wa South Africa, hasa Durban huwezi kumpata siku za weekends. Siku zingine zote utampata lakini weekends never ever. Akija siku ya weekend huyo ni wako na anakupenda.
Safari yangu ya mahusiano nikiwa Durban.
Kuna mademu watano ambao nilijihusisha nao kwa ukamilifu. Achana na wale wakuokota na kupiga na kusepa. Ila nitamuongelea huyu mmoja ambaye aliuteka moyo wangu, nikawa kama zezeta. Na hii ndio sababu imenifanya nianzishe huu uzi baada ya kumkumbuka huyu mtoto wa kizulu na drama zake zilizotaka kunitoa uhai.
Picha linaanza kama ifuatavyo:
Kama nilivosema saa 12 asubuhi tayari tupo workshop tunafunga tent kwa ajili ya kupanga viatu. Kazi ya kufunga tent na kupanga viatu ilikuwa inachukua kama masaa mawili hivi au saa moja na nusu hivi. Kwa hiyo kwenye saa mbili hivi tunakuwa tushamaliza kupanga viatu, na kuanza kutafuta chai. Kulikuwa na mbongo (jamaa) mmoja alikuwa anatupitishia chai na chapati. So, mida ya saa mbili hivi atatuletea chai na chapati. Jina lake alikuwa anaitwa Chaduma. Nadhani masela wa Durban kama wamo humu JF watakuwa wamemnyaka huyu mwamba na huenda wakanijua, ila nitajitahidi kuficha codes zote muhimu ili nisitambulike. Sometimes chapati za Chaduma zilikuwa zinakifu hivyo mtu unaamua kwenda kufungua kinywa sehemu nyingine. Dah! Chaduma alikuwa na maneno ya shombo hatari. Usipokula chapati zake atakusema kwa wabongo balaa. Kwa hiyo sometimes unaamua kula chapati za Chaduma kwa kuogopa kwenda kusemwa kwa wabongo kwamba unaringa.
Siku moja nilichoka kula chapati za Chaduma nikaamua kwenda kutafuta chakula sehemu nyingine. Hiyo siku ndio siku niliyokutana na kipenzi changu Khumbu Mkhize.
Nilipomaliza kufunga tent na kupanga viatu, kabla Chaduma hajafika nikaamua kwenda kufuata chai na vitafunio sehemu moja hivi. Hiyo sehemu ni ng’ambo ya pili kutoka workshop, yaani unatoka nje ya workshop, unavuka barabara ndio unaifikia hiyo sehemu. So, wakati nataka kuvuka barabara nikamuona msichana amekaa kwenye kingo ya barabara kajiinamia kama mtu yupo kwenye lindi la mawazo hivi. Basi nikamsogelea, nikamsemesha. Nikamsalimia, kisha nikamwuliza, vipi? Kulikoni asubuhi hii upo hapa? Akaniambia ana njaa. Nikimcheki ni binti mdogo tu, alikuwa na miaka 18 (nilikuja kujua umri wake baadae tulipokuja kuwa wapenzi). Basi nikampa rand 20 akale, nikamwelekeza goli langu (ninapofanyia kazi) ili akimaliza kula aje tufahamiane zaidi.
Nimechoka kuandika nipumzike kidogo, itaendelea.
Kusoma muendelezo bofya
SEHEMU YA PILI
SEHEMU YA TATU
SEHEMU YA NNE
SEHEMU YA TANO
SEHEMU YA SITA
SEHEMU YA SABA
SEHEMU YA NANE
SEHEMU YA TISA
SEHEMU YA KUMI
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
SEHEMU YA KUMI NA TATU
SEHEMU YA KUMI NA NNE
SEHEMU YA KUMI NA TANO
SEHEMU YA KUMI NA SITA
SEHEMU YA KUMI NA SABA
SEHEMU YA KUMI NA NANE
SEHEMU YA KUMI NA TISA
SEHEMU YA ISHIRINI
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
SEHEMU YA THELATHINI
SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI
SEHEMU YA THELATHINI NA TATU
SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
Wewe ni msema ukweli, inaonekana hata shuleni ulikuwa unatumwa na wenzako usimame uwasilishe hoja zao au maoni yao! Hiyo hali umekua nayo naona had ukubwani.Ila konda msafi kuna kitu unakosea..ahadi zako nyingi ni zile ambazo sio timilifu..last week uliahidi j5 ungeleta MKEKA wa maana..matokeo yake ukaleta story ya kawaida yenye aya kama 8 tu...hahahahha....leo tena umetujaza kuwa j5 inaisha..(binafsi naamini haitaisha j5 maana ahadi zako hazitimii)...lakini mkuu, mda mwingi upo online JF, hivi ungekuwa unaandika kidogo, una save then unakuja kuandika kidogo mwisho unamaliza unatuma si ingekuwa imeenda mbali hadi now?...Kama kweli ungekuwa na nia ungeshaimaliza maana kama mtu ukiamua kuandika kwa nusu saa tu lazima uandike kitu kirefu...
NIONAVYO MIMI..
1. Mkuu unafurahi sana unavyoona wana wanaulizia hii story kila muda. Maana kama unapata mda wa kusoma comments kwenye uzi wako na kureply, unakosaje muda wa kuandika story yako? Nahisi mkuu unafurahi kuona notifications zimejaa quotes kuhusu uzi wako.
2. Story yako imeshapoteza mvuto..watu wamesubili na wameshazoea...haina mvuto tena kama ule wa mwanzo na haija vuta tension ya watu tena... wiki hii inayoisha leo umeandika post chache na fupi kweli tofauti na ahadi yako ilivyokuwa mwanzo.
3. Sitaki nataka zako zimefanya mpaka story imekosa mvuto..HOW?, Uliwaambia watu hutaimalizia, wakakubembeleza wee mwisho ukaja na conclusion mara oooh khumbu alifariki...sasa sitaki nataka zako ndo zimeharibu utamu wa story, yaani watu wanasoma huku wanaujua mwisho wa story, ile ladha imeotea.
4. Inshu ya bundle haina logic, JF haili bundle sana na pia hata wasomaji na wana tumia bundle...as long as umeamua kuandika kwa hiarai, andika tu mkuu.
USHAURI:
Mkuu siku nyingine usilete tena story hapa JF maana unapenda sana kutrend. Unachelewesha story isiishe ili kila saa wakutaje taje..trust me, kama usingekuja na zile episodes 32 za kwanza mapema, huu uzi wako usingekuwa hai hadi leo maana watu wasingeweza kuvumilia kiu kwa kitu kisichoeleweka ila ulikuwa mjanja kuteka hisia za wtu.
HITIMISHO: Uwezo wa kuandika story ndefu kwa siku unao, nia ya kuandika unayo, muda wa kuandika unao ila tu sababu za kutoandika/kuchelewesha story HAUNA....Basi tu unapenda trending na kiki kama wasanii
Ni mimi Mtetezi wa wana JF wanaoogopa kukwambia ukweli.
MKUU HAYO YOTE ULIOYAANDIKA NI UKWELI MTUPU....Ila konda msafi kuna kitu unakosea..ahadi zako nyingi ni zile ambazo sio timilifu..last week uliahidi j5 ungeleta MKEKA wa maana..matokeo yake ukaleta story ya kawaida yenye aya kama 8 tu...hahahahha....leo tena umetujaza kuwa j5 inaisha..(binafsi naamini haitaisha j5 maana ahadi zako hazitimii)...lakini mkuu, mda mwingi upo online JF, hivi ungekuwa unaandika kidogo, una save then unakuja kuandika kidogo mwisho unamaliza unatuma si ingekuwa imeenda mbali hadi now?...Kama kweli ungekuwa na nia ungeshaimaliza maana kama mtu ukiamua kuandika kwa nusu saa tu lazima uandike kitu kirefu...
NIONAVYO MIMI..
1. Mkuu unafurahi sana unavyoona wana wanaulizia hii story kila muda. Maana kama unapata mda wa kusoma comments kwenye uzi wako na kureply, unakosaje muda wa kuandika story yako? Nahisi mkuu unafurahi kuona notifications zimejaa quotes kuhusu uzi wako.
2. Story yako imeshapoteza mvuto..watu wamesubili na wameshazoea...haina mvuto tena kama ule wa mwanzo na haija vuta tension ya watu tena... wiki hii inayoisha leo umeandika post chache na fupi kweli tofauti na ahadi yako ilivyokuwa mwanzo.
3. Sitaki nataka zako zimefanya mpaka story imekosa mvuto..HOW?, Uliwaambia watu hutaimalizia, wakakubembeleza wee mwisho ukaja na conclusion mara oooh khumbu alifariki...sasa sitaki nataka zako ndo zimeharibu utamu wa story, yaani watu wanasoma huku wanaujua mwisho wa story, ile ladha imeotea.
4. Inshu ya bundle haina logic, JF haili bundle sana na pia hata wasomaji na wana tumia bundle...as long as umeamua kuandika kwa hiarai, andika tu mkuu.
USHAURI:
Mkuu siku nyingine usilete tena story hapa JF maana unapenda sana kutrend. Unachelewesha story isiishe ili kila saa wakutaje taje..trust me, kama usingekuja na zile episodes 32 za kwanza mapema, huu uzi wako usingekuwa hai hadi leo maana watu wasingeweza kuvumilia kiu kwa kitu kisichoeleweka ila ulikuwa mjanja kuteka hisia za wtu.
HITIMISHO: Uwezo wa kuandika story ndefu kwa siku unao, nia ya kuandika unayo, muda wa kuandika unao ila tu sababu za kutoandika/kuchelewesha story HAUNA....Basi tu unapenda trending na kiki kama wasanii
Ni mimi Mtetezi wa wana JF wanaoogopa kukwambia ukweli.
Acha nikujibu tu. Nimekuona muda mrefu umekazana kuongea upuuzi. Hivi umelazimishwa kusoma huu uzi? Wewe kama huwezi kuchangia kaa kimya. Acha kunilisha maneno. Hakuna sehemu nime-demand mchango ili stori iindelee. Stori itawekwa hapa utasoma bure kama bado uko interested. Hakuna sababu ya kujifanya unajua sana kuongea. Wewe ungekuwa South Africa na huo mdomo wako kama mwanamke ungeshaliwa kichwa kitambo.Wewe ni msema ukweli, inaonekana hata shuleni ulikuwa unatumwa na wenzako usimame uwasilishe hoja zao au maoni yao! Hiyo hali umekua nayo naona had ukubwani.
Jamaa alilewa sifa, gafla akaona ikiwa thread ina visitor 5000 na zaidi nikiwaambia wachangie buku buku nina milion tano, hahaa Basi akaanza kudeka kama ulivyo sema,
Akaona ajivute ili reply za kumuomba zifike elf 5 naona watu wameishapuuza na kuendelea na issue zingine.
Hivyo basi
Lengo la hela limekwama na lengo la kubembelezwa limekwama.
Bora atuhamishie instagram sijui telegram tutachangia elfu kumi huko,
Nimesema yale wanaosema hatuna hela nyuma ya keyboard waendelee kutoa povu
Mkuu mbona kama una shida kichwani? Kwani umeniajiri kuandika hii stori? Mambo mengine unakaa kimya tu kama unaona hayakupendezi.MKUU HAYO YOTE ULIOYAANDIKA NI UKWELI MTUPU....
Kuanzia alipoanza na swala la kutumiwa hela ya bando niliona kabisaa hamna kitu hapa...
Haingiii akilini story uilete mwenyewe alafu watu wakuchangie Vocha...
Sambamba na Hilo Kuna watu walitetea etii...[emoji1787]
Mkuu achana nae huyo unaharibu energy bure tuMkuu mbona kama una shida kichwani? Kwani umeniajiri kuandika hii stori? Mambo mengine unakaa kimya tu kama unaona hayakupendezi.
Kesho kutwa mzee namaliza kazi, ila kuna watu wana mambo ya kibwege kweli. Hata kama unajitahidi kuwavumilia lakini inafikia stage unaamua kuwajibu tu maana wanakuchukulia poa sana. Stori nimeilata mwenyewe kwa hiari yangu, that means nina uwezo wa kuachana nayo kwa hiari yangu pia. Sasa humu kuna watu wanaongea upuuzi mwingi mpaka nimeamua kuwajibu. Sikutaka kujibishana nao ila nimeona wanataka kunipanda kichwani.konda msafi njoo huku tumemmisi khumbu wetu
Huu uzi unatrend si mchezo ngoja niupitie kwanza!
Usitupangie mkuu utaikuta ukiwa ndani ya mtandaoNahisi j5 utakapo toa mwendelezo ntakuwa nje ya mtandao naomba uhairishe utoe mwendelezo ijumaa mkuu konda msafi
Hapana niyeye mwenyewe maana jamaa ni rafikiyangu sana tu na sisi ndio tulimpa hiyo connection ya RFA.
Mkuu,sasa siku nyingine tumia nguvu hii hii kupambana ili upate hela! Ushauri tu!MKUU HAYO YOTE ULIOYAANDIKA NI UKWELI MTUPU....
Kuanzia alipoanza na swala la kutumiwa hela ya bando niliona kabisaa hamna kitu hapa...
Haingiii akilini story uilete mwenyewe alafu watu wakuchangie Vocha...
Sambamba na Hilo Kuna watu walitetea etii...[emoji1787]
Lol sina ucelebrity wowote mie wakuja tuSawa celebrity wa jf