Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

. Anaharibu uzi wangu huyu mwamba.
Mkuu amini nakwambia ameuongezea thamani... Amejifunza mengi kimya kimya hata kama hataki ku-admit.

Your a good story teller and writer ...fasihi andishi ina misingi yake, ina madhumuni na mitindo ya uandishi umeifuata sawia.

Kwenye uandishi unaweza kuandika kuwakilisha hisia zako bila kukusudia malipo (kama ulivyofanya) Unaweza kuandika ukikusudia kuhabarisha au malipo nk.
Mtindo ulitumia ni wa mtiririko na rejea

Umeelezea hisia zako, umetoa mafunzo fikirishi.... mfano uliposema maisha ya uuzaji sembe huyapendi na namna ulivyonusurika kutiwa mbaroni kwa kuwa na vipande vya karatasi za plastiki za kufungia sembe ambayo hukuwa unahusika nayo. Umetoa taswira ya watanzania wanavyo jihusisha na wizi na mihadarati SA.

Namna ulivyo drop academic performance chuo due to affairs confrict. Umefunza kuhusu kusimamia unachokiamini na uchungu wa kukipoteza unachokipenda. Whether in one-way or another ukaongezea au kupunguza uhalisia wajambo ndio namna ya kuiteka hadhira kwenye kuwabebesha wahusika uhusika wao.

Umeibua wanazuoni wa fasihi kusema kwa namna mbalimbali nk.

Nakushauri uandike novel based on true story. Though utaibua upelelezi wa jinai nk lakini unaweza kulindwa na haki miliki.. kwa ku declear kutohusika na jambo lolote halisi litakalo fanana na ulichoandika.
Big up sana.
 
P1 sana
 
Nakupata mzee
 
P1 sana Mwamba
 
Inaendelea

Swala la kuambiwa nitapigwa risasi ya kichwa liliniogopesha sana. Kwa South Africa mtu akikuambia atakuuwa usifikiri anatania, anakuua kweli. Nilianza kuona maisha yangu yapo hatarini.

Nilikaa wiki bila kumtafuta Khumbu maana nilianza kumwogopa japo bado nilikuwa nampenda. Nilimpigia simu na kumwelezea kuwa kuna mtu alinipigia simu akaniambia ataniua kwa kunipiga risasi, na nikamweka wazi “nahisi anayetaka kuniua anataka kuniua kwa sababu yako. Naomba unieleze kwa nini nataka kuuliwa kwa ajili yako, ubaya upi nimekufanyia hadi nistahili kuuawa? Au mimi kukupenda wewe ndio kosa ninalostahili kuuawa?” Khumbu akajifanya hajui chochote kuhusu hilo, ila mimi niliamini ni bwana zake ndio wanaotaka kuniua. Nikaendelea kumwelezea huku nikitia huruma kuwa hata sababu ya yeye kutokuja Bloemfontein licha ya mimi kumtumia nauli ni hao jamaa, nikazidi kumwambia “Khumbu you have wrecked my heart, you have broken my heart into million pieces”, Yeye aliendelea kusisitiza hajui chochote kuhusu hilo. Binafsi niliona kabisa nikiuendekeza moyo wangu nitafia South Africa. Ila jamani acheni, moyo ukipenda ni ngumu sana kujinasua.

Swala la yeye kuja Bloemfontein sikutaka tena kumwuliza maana nilijua nitakuwa najisumbua tu japo nilikuwa natamani atamke “Konda msafi kesho napanda basi nakuja". Nilikuwa natamani aje nimchakate kwa mara ya mwisho maana kila nikifumba macho nakuwa kama naliona umbo lake, tako lake linavyoning’inia, halafu nawaza mimi ndio basi tena kuligusa hili tako dah! roho inauma kinyama, natamani Mungu afanye muujiza Khumbu amfanye kuwa mke wangu, tupotee tukaishi sehemu isiyojulikana, hata tuondoke South Africa tuende hata bara la Antactica, nikawe mimi na Khumbu tu.

Baada ya kuona maisha yangu na Khumbu hayapo tena nikaanza kuwakumbuka dada zangu watanzania. Nikaanza kujiambia mimi ni foreigner tu, sina thamani katika nchi ya watu. Khumbu hawezi kuwaacha kaka zake akanichagua mimi foreigner, acha nirudi Tanzania nikatafute dada zangu na mimi nipate kuthaminiwa. Kuna demu mmoja alikuwa anaishi Sinza nilimuimbisha kipindi flani niliporudi Bongo nikaanza kumfikiria. Pia kuna demu mmoja mbongo nilikutana naye Kampala nikaanza kumkumbuka. Bahati nzuri namba zao na email address ya yule wa Uganda nilikuwa nazo. Nikaanza kuwatafuta. Wote nikawapata, mawasiliano yaliyokufa nikayafufua. Yule aliyekuwa anasoma Uganda akaniambia alishamaliza form six, akaenda Marekani na sasa yupo Mwanza kwa wazazi wake. Nikaanza kujitetea kwa nini nilikuwa kimya kipindi chote hicho na kwa nini leo nimeamua kuibuka na kumtafuta. Mimi bhana ukinipa dakika za kunisikiliza ngumu sana kuchomoa. Labda nisiwe na hela. Nikiwa na hela huwa nakuwa na confidence ya ajabu. Nikamsomesha, nikampanga akapangika, nikamwambia acha niangalie utaratibu wa kurudi Bongo tuje tufanye mchakato wa kuoana kisha turudi tuje tuishi South Africa. Demu alifurahi kweli, akawa anaomba aje South Africa hata leo ili tuishi pamoja. Mie nikamwambia avumilie kidogo tu, ninakuja hadi kwao Mwanza. Basi jina likabadirika nikaanza kuitwa mume. Nikipiga simu hadi marafiki zake wanaitwa ili waongee na shemeji yao, hadi mama mtu anapewa simu anisalimie, wanawake bhana!

Kwa hiyo nikawa nawasiliana na huyu demu karibia kila siku, na kidogo kidogo ikawa inanisaidia kutokumuwaza Khumbu ile kwa sana, japo Khumbu sikuweza kumsahau moja kwa moja. Huyu demu wa Sinza naye ikawa ahadi ni zilezile kama nilizomuahidi huyu aliyekuwa anasoma Uganda. Lengo langu lilikuwa wote kuwaweka karibu ili nikifika Bongo nichague yupi anafaa zaidi maana ilikuwa kama miaka sita imepita toka tuonane. Yule wa Uganda alikuwa ananitumia picha kwenye email, pia alikuwa facebook, so kwenye picha bado alikuwa anaonekana ana mvuto lakini sikutaka kudanganyika na picha. Iko hivi huyu wa Uganda nilikutana naye stand ya mabasi nilikuwa nakata ticket ya kutoka Kampala kuja Dar, nakumbuka kulikuwa na kampuni moja inaitwa Akamba ndio nilikata ticket ya hilo basi. Yeye alimsindikiza mdogo wake kuja kukata ticket. Tukiwa pale kwenye ofisi za Akamba ndio nikamuona. Alikuwa na mdogo wake, nilikuja kujua baadae kuwa yule mwingine alikuwa mdogo wake. Ilikuwa ni pisi moja kali sana black beauty flani ya kihaya. Pale sehemu ya kukatia ticketi sikutaka kumsomeshea pale,nilihisi ningevuta hisia za watu maana foleni nzima alikuwa ana-shine out, hivyo ningemfuata pale lazima watu wangekuwa macho kodo, hivyo kwa kuwa nilijua kwa sababu anasafiri nitapata nafasi ya kumuimbisha kwenye basi maana niliwasikia wanaongea Kiswahili nikajua hawa tunasafiri pamoja, so nikapanga ikifika zamu yangu ya kukata ticket nikamwombe mkatisha ticketi anipe siti ya jirani na huyu black beauty. Kweli ilipofika zamu yangu nikamwomba mkatisha ticket anipe siti ya jirani na huyu black beauty, bila hiyana nikapewa hiyo siti.

Siku ya safari ilikuwa kesho yake, naingia kwenye basi, black beauty simuoni bali namkuta yule mwenzake. Basi nikakaa siti moja na huyu mwenzake kinyonge huku najiuliza ile pisi iko wapi? Ikabidi nianzishe maongezi na huyu mwenzake ili nipate nafasi ya kumwulizia huyu mwenzake waliyekuwa naye jana pale kwenye ofisi za Akamba yuko wapi? Mazungumzo yalipokolea ndio nikamwuliza, mwenzake yuko wapi? Akanijibu yule ni dada ake anaitwa Amina, alimsindikiza tu kuja kukakata ticket, yeye kabaki hajasafiri. Basi baada ya kupata hayo maelezo nikamweleza kuwa dada ako nimemzimia kinoma, na hii siti nilimuomba mkatatisha ticket anipe specifically kwa ajili yake. Basi yule mdogo mtu akacheka sana hadi machozi yakamtoka. Stori zikawa tamu kweli, njia nzima full furaha tu. Bill za chakula tunashare. Akanipa namba yake na ya dada ake, akaniahidi ujumbe wangu ataufikisha kwa dada ake kabla hata mimi sijamtafuta. Nilipofika Dar nilimtafuta baada ya kama siku mbili hivi, demu alifurahi sana. Mdogo mtu tayari alikuwa keshamaliza kazi ya kunitambulisha kwa dada ake, mimi ikawa kazi ya kufukia mabonde tu ambayo mdogo mtu alikuwa hajayaona. So, huo ndio ulikuwa mwanzo wa kujuana na hii pisi kali ya kihaya iliyokuwa inasoma Kampala ambayo kwa kiasi kikubwa ilinisaidia kuniondolea mawazo ya Khumbu.

Nikipata nafasi nitaielezea hii pisi ya Sinza jinsi tulivyokutana maana nayo ina historia kubwa sana kwenye maisha yangu, na ina mchango wa kunisaidia kumsahau Khumbu. In fact hii pisi ninimezaa nayo, niliporudi bongo nikaitandika mimba bila kutarajia, sijui ilinitegeshea.

Kitendo cha kuambiwa nitapigwa risasi na kitendo cha Khumbu kula nauli kilisababisha niamue kujitahidi kumsahau Khumbu. Japo moyo ulikuwa ni vigumu kukubaliana na hili lakini akili ilikuwa inaniambia “Konda msafi kwenu watapeleka jina tu ukiendelea kumng’ang’ania Khumbu".

Niliamua kumrudisha ulingoni yule demu niliyemfanyia vitimbi. Haikuwa hata kazi kubwa kumrejesha. Nilimwambia tu nadhani break imeisha, na sasa nipo sawa kiakili hivyo tunaweza kuendelea na mahusiano yetu.

Huyu demu wa Bloemfontein yeye aliamua kuwekeza kwangu. Ila alikuwa na wasiwasi sana kuwa huenda yeye sio changuo langu maana kila mara alikuwa ananiambia anahisi ananibore. Yule demu kusema ukweli alikuwa na sura ya kawaida ila alikuwa na mkia kufuru. Alikuwa na tako kubwa sana. Nilishawahi kumpiga picha ya uchi halafu nikawarushia masela wa Durban wakasema huo mzigo unahitaji kuwekwa kwenye makumbusho. Yule demu alikuwa na tako kubwa, yaani kubwa.

Itaendelea.
 
Ngoja Niishie hapa Kesho niendelee kupekua hadi Nione Mwisho wake
 
P1 sana Kaka, Safi sana
 
Hatimae....ngoja sasa
 
Mkia kufuru [emoji28][emoji28][emoji1787][emoji95][emoji95]kama siafu tu...shusha story mzee[emoji122]
 

Hiyo paragraph ya mwisho hapo nimeweka imagination na nimejikuta napata picha ya huyo mchepuko.

Mkuu nasisitiza usimuache huyo kisebengo, endelea kula tunda, watutsi kwa shape wako vizuri mkuu, Ila hakikisha wife hajui.

Endelea kutekeleza ilani ya chama [emoji1420]
 
Kuna dictionary nilinunua Kampala, hiyo ticket ya Akamba niliichomeka humo. Ni oxford Advanced Learner's 7th Edition. Uganda ilikuwa inauzwa kwa bei ndogo sana ukilinganisha na bei ya Tanzania. You can't believe hiyo ticket mpaka leo ninayo. Nilikuwa naiona ona kila ninapoitumia hii dictionary, sasa leo wakati naandika kipengele cha Amina nikakumbuka, nikajisemea acha niiangalie hii ticket kama bado ipo niiambatanishe kwenye huu uzi. Kama kumbukumbu zangu zipo vizuri nilikutana na Amina tarehe 17 March 2006. Just imagine. Hiyo hapo ticket nimewawekea
 

Attachments

  • Akamba.jpeg
    47.5 KB · Views: 81

Tunataka picha ya khumbu[emoji849]
 
Kuna mdau mmoja alisema kuwa huwa hutimizi ahadi zako, mwanzo nilimpuuza lakini kumbe alikuwa sahihi, anyway sawa mkuu.
 
Kuna mdau mmoja alisema kuwa huwa hutimizi ahadi zako, mwanzo nilimpuuza lakini kumbe alikuwa sahihi, anyway sawa mkuu.
Mkuu umesoma mpaka nilipoishia jana usiku lakini? Isije ikawa unalaumu tu kumbe kuna miendelezo mingi hujaifikia. Anyway niwie radhi mkuu, stori nitaimaliza. Leo nitaweka tena huenda nikaimaliza. Tatizo kuna matukio ambayo hata sikutegemea kama yatakuja kuwa integrated kwenye hii stori ila kadri ninavyoielezea najikuta yana pop up. Kwa mfano tukio la Amina sikutarajia kama lingejitokeza kwenye hii stori lakini unaweza kuona jinsi lilivyoplay part. Nilitaka niliruke maana halikuwepo hata kwenye muainisho wangu lakini nikaona nikiliruka stori itakosa connection yaani ingekosa ushirikiano. So unaweza kuona kwa nini stori inachukua muda kuisha. Hata kipengele cha demu wa Bloemfontein nacho lazima nikielezee kwa undani japo hakikuwa sehemu ya muainisho wangu maana nacho ni kiungo muhimu cha hii stori. Nikikiruka stori itakosa connection. Au niachane na vipengele ambavyo havikuwa sehemu ya muhitasari niimalize kibabe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…