Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Inaendelea

Siku ya mazishi niliamua kutokuhudhuria. Nilimpigia simu nikamwambia aniwie radhi sitaweza kuhudhuria kwenye mazishi, aliniuza kwa nini sitaweza, nikamwambia nina test, akaniuliza test gani hiyo siku ya Jumamosi, nikamjibu chuoni kwetu hadi Jumamosi huwa tunafanya test. Kiunyonge akabidi akubaliane na mimi. Kiukweli sikuwa na test wala nini, niliamua tu kutokuhudhuria mazishi. Sababu iliyonifanya kughairi kwenda msibani, sikutaka kukutana na mzazi mwenzie. Sikutaka jamaa anijue. Nilijua siku ya msiba lazima jamaa anijue hata kama sitatambulishwa maana Khumbu lazima zingetokea moments tungekuwa pamoja, mwenyeji wangu alikuwa ni yeye peke yake hivyo lazima tungekuwa pamoja jambo ambalo jamaa angenijua, hivyo jamaa ingeanza kumpa mashaka kumuona mzazi mwenzie yupo beneti na mimi. Khumbuka nilishaambiwa jamaa bado anamhudumia na anaendelea naye.

Baada ya msiba Khumbu alisafiri, tuliendelea kuwasiliana na aliendelea kunilalamikia kwa nini sikuja siku ya mazishi, na mimi niliendelea kusimamia kuwa test ndio ilikuwa sababu.

Baada ya kama mwezi Khumbu alirudi Durban, aliendelea kukaa pale pale kwenye nyumba ya bibi ake na ndugu zake wengine waliokuja kuishi hapo. Maisha yaliendelea, Khumbu aliendelea kutokupatikana kama ilivyokuwa huko nyuma.

Mwaka wangu wa kwanza chuoni kuna module moja sikuisajili, hivyo kila mwaka nilikuwa nabakiwa na module moja ambayo ilipelekea kumaliza chuo mwaka wa nne badala ya mwaka wa tatu. Iko hivi, kila module ina prerequisite yake. Kwa mfano huwezi kusoma economics ya mwaka wa pili kama kuna module ya economics ya mwaka wa kwanza hujaisoma. Kwa hiyo kila mwaka kuna module moja ilikuwa inabaki nyuma. Nilikuja ku-graduate mwaka wanne semester ya kwanza kwa sababu ya somo moja tu tena module moja iliyokuwa inabaki.

Ule mwaka wa nne niliamua kuanza kutafuta kazi kwa sababu nilikuwa nimebakiza somo moja tu tena module moja kugraduate. Hilo somo lilikuwa rahisi sana kwangu, nilikuwa nalimudu bila hata kuingia darasani. Mungu akabariki nikapata kazi shemu moja inaitwa Bloemfontein, ni jiji ambalo liko katikati ya South Africa, province moja inaitwa Free state. Maisha yakabadirika yakawa matamu. Nikawa naenda chuoni kila kunapokuwa na test tu, darasani nikawa siingii tena. Nikawa na mawasiliano ya karibu na wanafunzi wenzangu kuniupdate chochote ambacho kingehitaji uwepo wangu personally. Hivyo siku za test nikawa napanda basi kwenda Durban. Kama test let’s say ni kesho. Leo jioni napanda basi, alfajiri nishafika tayari na kwenda darasani. Baada ya test napanda tena basi kurudi Bloemfontein.

Huko Bloemfontein kuna watoto wa kisutu wakali balaa. Wana maumbo ya kutoa udenda, nadhani kwa South Africa kabila linaloongoza kwa watoto wazuri ni la kisutu likifuatiwa na waxhosa na wazulu. Kuna mmoja nilianza kumdate kunipunguzia machungu ya Khumbu. Mie sinywi pombe wala kuvuta sigara kwa hiyo starehe yangu ilikuwa watoto wa kike tu, na ukizingatia tayari nimeshapata na kazi inayoniingizia kipato ilikuwa full burudani. Nina wasiwasi kama sijaacha mtoto huko Bloemfontein maana huyo mwanamke nilikuwa napiga karibia kila siku.

Nilipopata kazi nikamjulisha Khumbu. Alifurahi sana, tukapanga mipango ili aje Bloemfointein anitembelee.

Itaendelea
Khumbu kama Khumbu yan
 
Inaendelea,

Baada ya kupata kazi nikaanza harakati za kumleta Khumbu japo pia huko Bloemfontein nilipata mwanamke wa kunitoa upweke. Unajua kuna kipindi mwanaume unaweza kumpenda mwanamke kiasi kwamba hata ukiletewa wanawake wengine wazuri kumzidi huyo unayempenda lakini ukiambiwa umwache huyo uchukue hawa wengine bado unaweza usikubali kumwacha huyo unayempenda. Nadhani Khumbu alikuwa ameniingia sana rohoni kiasi kwamba wanawake wote nilikuwa nawaona hawatoshi. Kuna siku moja nilikuwa shopping mall huko Bloemfontein nikakutana na demu mmoja kisu hatari, nikamfuata na kujaribu kuanzisha mazungumzo naye, demu alikuwa anasukuma kitoroli hivi vya kufanyia shopping, nikawa namfuata nyuma nyuma akiwa anachukua vitu kwenye shelves na mimi huku nikiendelea kuimbisha, demu alikuwa anatoa ushirikiano mzuri tu, nikimwuliza kitu anajibu na yeye ananiuliza namjibu, kifupi alikuwa anaelekea kulainika lakini ingetokea nichague kati yake na Khumbu ningemchagua Khumbu.

Tulipopanga Khumbu aje kunitembelea, nilianza kufikiria huyu demu wa huku nitamkwepaje ili nipate nafasi ya kuwa na Khumbu. Kadri siku zilivyosonga akili yote ikawa inafikiria tu kumleta Khumbu maana kama kazi tayari nimeshapata, nakaa kwenye mjengo wa maana tu, pesa sio tatizo tena japo mshahara sio mkubwa kivile, ila kwa maisha ya kukaa na mwanamke unatosha kabisa.

Turudi nyuma kidogo, nilipoajiriwa Bloemfontein nilianzia kukaa nyumbani kwa mfanyakazi mwenzangu kitongoji kimoja kinaitwa Botshabelo. Nilipopata mshahara wangu wa kwanza ndio nikaenda kutafuta flat yangu. Nilipata flat ambayo alikuwa anaishi demu mmoja mwanafunzi. Tukakubaliana aniuzie kila kitu kilichokuwemo ndani. Nilimlipa kwa awamu kama nne hivi maana alikuwa anamiliki vitu vingi sana si unajua wanawake wanavyopenda kuwa na kila kitu kwenye magheto yao hivyo nisingeweza kuvilipia kwa mshahara wa mwezi mmoja. Nilipomaliza kulipa deni tukaenda kubadirisha jina la mpangaji na kuwekwa jina langu. Kule kuna ma-agent wanaopangisha nyumba, yaani ni kampuni inayojihusisha na kupangisha nyumba, kwa hiyo mpangaji ukikidhi vigezo wanakupangisha na unakuwa responsible kwa chochote kitakachotokea kwenye mjengo. Geto likawa limekamilika tayari kwa kuanza mchakato wa kumleta Khumbu.

Haya tuendelee, Nikatafuta sababu ya kugombana na yule demu ili aniache kwa muda nipate nafasi ya kuwa na Khumbu. Nilianzisha visa visivyokuwa na kichwa wala miguu, kila nikikumbuka roho huwa inanisuta sana. Nilianza tabia ya kununa nuna bila sababu ya msingi, demu akawa anashangaa nilivyobadirika. Kuna siku tulikuwa tunafanya mapenzi, kwa bahati mbaya sijui nilimkwaruza na kucha kwenye k, sijui nilimpiga pipe tu mpaka kupelekea hilo tatizo, hata sielewi, nikiwa nampelekea moto nikaona damu inatoka, ilikuwa style ya kumchumisha tembele. Nilipoona zile damu nikawa kama namgombeza, nikawa namlaumu kwa nini ananipa mzigo akiwa kwenye siku zake. Akawa anajitetea hayupo kwenye siku zake ila anadhani amechunika tu. Basi mie nikakasusa, sitaki tena kuendelea. Kila siku vitimbwi haviishi, baadae akajiongeza akaniambia tuchukue break kwanza, akaniambia anahisi kama ananibore siku hizi. Na mimi nikamwambia sawa let us have a break. Hapo lengo langu likawa limetimia.

Nikaanza mchakato wa kumtumia nauli Khumbu. Nikamwambia nimkatie kabisa ticket hukuhuku. Makampuni ya mabasi kwa South Africa unaweza kumkatia mtu tiketi kama unavyomnunulia mtu kifurushi cha tigo. Basi nikaenda shopping mall flani inaitwa Water front, mle kuna ofisi za wakala wa mabasi. Nikaamua kumfanyia booking tu badala ya kulipia kabisa. Nikamwambia hela nitakutumia ila tayari nimeshakufanyia booking kwenye mabasi ya “SA Road Link” hela nitakutumia kwenye account yako ya benki. Tukawa tumekubaliana hivyo. Kesho yake ndio alitakiwa kusafiri kuja Bloemfontein. Akanitumia namba za account yake, nikaenda kumtumia nauli na hela kidogo ya kutumia njiani.

Nilipomtumia hiyo hela nikawa namsisitiza aende akailipie hiyo ticket, na yeye akawa ananiambia muda si mrefu atatoka nyumbani ana ataelekea town kutoa hiyo hela na kwenda kuilipia ticket. Mie nikawa namwambia hakuna haja ya kwenda benki kutoa hela, yeye aende tu akalipie kwa kutumia card yake ya bank, maana ilikuwa visa debit card. Yeye akasisitiza anaenda kutoa hela, anataka kulipia kwa cash. Sikutaka kumbishia sana, nilimwacha aamue anataka kulipiaje, cha muhimu tu kesho alfajiri awe Bloemfontein. Basi tukaagana hapo, mie nikaenda zangu nyumbani kupumzika nikisubiria anijulishe kashalipia ticket. Hapo ilikuwa mida ya saa nne asubuhi.

Masaa yakazidi kwenda bila kupata feedback yeyote. Ilipofika saa tisa nikampigia kumwuliza kama amepata hiyo ticket. Akaniambia bado hata mjini hajaenda ila nisiwe na wasiwasi. Nikaanza kupata wasiwasi, huyu mwanamke huenda anataka kunichezea mchezo hapa. Huko bank atafika saa ngapi, na bank zinafungwa saa 11 na hataki kwenda kulipia kwa card yake. Nikajisemea acha nisubiri nione. Nikawa nampigia simu karibia kila baada ya nusu saa kumharakisha atoke aende kulipia hiyo ticket. Baadae ndio akaniambia yupo anadrive anaenda bank. Hapo ni kama saa 10:30 jioni, dah! Kwa huo muda nikawa na mashaka kama atakuta benki bado zipo wazi. Kwenye saa 11 hivi nikampigia tena kujua kinachoendelea simu ikawa haipatikani, nikaconclude huyu mwanamke haji, acha nipambane na hali yangu. Nilipata hasira, nikajiona bonge la fala. Nikawa namfikiria huyu dada wa watu niliyemfanyia visa mpaka akaamua kuchukua break. Niliendelea kumtafuta Khumbu kwenye simu na ikaendelea kutokupatikana. Nikawa nafikiria hivi huyu Khumbu ananionaje? Ole wake ajichanganye aje Bloemfotein. Kila nikifikiria napata hasira kinoma. Ilipofika kwenye saa mbili hivi usiku nikaona simu yake inaingia, akaanza kuniomba samahani kwa kushindwa kuja kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake. Hapo mimi namsikiliza tu hata siongei, alipomaliza kuongea nikamwuliza swali moja tu. Lini utakuja? Akasema atanijulisha. Nikajua tu hapa hakuna kitu. Nikiwa na hasira huwa siwezi kujicontrol nilimtukana. Basi nikiwa na stress zangu nikaamua acha nijilazimishe kulala tu maana usingizi sikuwa nao kabisa. Ile nikiwa kwenye lindi la mawazo simu ikaita, kucheki hivi number inasoma “number withheld”, nikaipokea, nikawa nasikia kama watu wapo bar, jamaa aliyepiga akaniambia “I am going to kill you, just one bullet on your head”, kabla sijaongea chochote jamaa akakata simu. Hapo nikaingiwa na hofu. Kwanza nikawa najiuliza, huyu jamaa yupo wapi? Isije ikawa tayari yupo Bloemfontein ananiwinda, namba yangu kaipata wapi? Ila nikajua tu hii itakuwa sababu ya Khumbu. Nikawa najiuliza sijui nimpigie simu Khumbu nimwulize kwa nini anataka kunitoa roho? Wazo jingine likanijia labda kumpigia simu sio jambo sahihi maana huenda yupo na huyo muuaji hivyo kumpigia simu itakuwa kama naharakisha kifo changu. Basi nikaamua acha kwanza nitulie nione nini kitaendelea ila inabidi niwe makini sana.

Itaendelea, nitajitahidi leo niimalize.
Bonge la Uzi mzee, Ngoja niendelee sasa
 
Inaendelea

Swala la kuambiwa nitapigwa risasi ya kichwa liliniogopesha sana. Kwa South Africa mtu akikuambia atakuuwa usifikiri anatania, anakuua kweli. Nilianza kuona maisha yangu yapo hatarini.

Nilikaa wiki bila kumtafuta Khumbu maana nilianza kumwogopa japo bado nilikuwa nampenda. Nilimpigia simu na kumwelezea kuwa kuna mtu alinipigia simu akaniambia ataniua kwa kunipiga risasi, na nikamweka wazi “nahisi anayetaka kuniua anataka kuniua kwa sababu yako. Naomba unieleze kwa nini nataka kuuliwa kwa ajili yako, ubaya upi nimekufanyia hadi nistahili kuuawa? Au mimi kukupenda wewe ndio kosa ninalostahili kuuawa?” Khumbu akajifanya hajui chochote kuhusu hilo, ila mimi niliamini ni bwana zake ndio wanaotaka kuniua. Nikaendelea kumwelezea huku nikitia huruma kuwa hata sababu ya yeye kutokuja Bloemfontein licha ya mimi kumtumia nauli ni hao jamaa, nikazidi kumwambia “Khumbu you have wrecked my heart, you have broken my heart into million pieces”, Yeye aliendelea kusisitiza hajui chochote kuhusu hilo. Binafsi niliona kabisa nikiuendekeza moyo wangu nitafia South Africa. Ila jamani acheni, moyo ukipenda ni ngumu sana kujinasua.

Swala la yeye kuja Bloemfontein sikutaka tena kumwuliza maana nilijua nitakuwa najisumbua tu japo nilikuwa natamani atamke “Konda msafi kesho napanda basi nakuja". Nilikuwa natamani aje nimchakate kwa mara ya mwisho maana kila nikifumba macho nakuwa kama naliona umbo lake, tako lake linavyoning’inia, halafu nawaza mimi ndio basi tena kuligusa hili tako dah! roho inauma kinyama, natamani Mungu afanye muujiza Khumbu amfanye kuwa mke wangu, tupotee tukaishi sehemu isiyojulikana, hata tuondoke South Africa tuende hata bara la Antactica, nikawe mimi na Khumbu tu.

Baada ya kuona maisha yangu na Khumbu hayapo tena nikaanza kuwakumbuka dada zangu watanzania. Nikaanza kujiambia mimi ni foreigner tu, sina thamani katika nchi ya watu. Khumbu hawezi kuwaacha kaka zake akanichagua mimi foreigner, acha nirudi Tanzania nikatafute dada zangu na mimi nipate kuthaminiwa. Kuna demu mmoja alikuwa anaishi Sinza nilimuimbisha kipindi flani niliporudi Bongo nikaanza kumfikiria. Pia kuna demu mmoja mbongo nilikutana naye Kampala nikaanza kumkumbuka. Bahati nzuri namba zao na email address ya yule wa Uganda nilikuwa nazo. Nikaanza kuwatafuta. Wote nikawapata, mawasiliano yaliyokufa nikayafufua. Yule aliyekuwa anasoma Uganda akaniambia alishamaliza form six, akaenda Marekani na sasa yupo Mwanza kwa wazazi wake. Nikaanza kujitetea kwa nini nilikuwa kimya kipindi chote hicho na kwa nini leo nimeamua kuibuka na kumtafuta. Mimi bhana ukinipa dakika za kunisikiliza ngumu sana kuchomoa. Labda nisiwe na hela. Nikiwa na hela huwa nakuwa na confidence ya ajabu. Nikamsomesha, nikampanga akapangika, nikamwambia acha niangalie utaratibu wa kurudi Bongo tuje tufanye mchakato wa kuoana kisha turudi tuje tuishi South Africa. Demu alifurahi kweli, akawa anaomba aje South Africa hata leo ili tuishi pamoja. Mie nikamwambia avumilie kidogo tu, ninakuja hadi kwao Mwanza. Basi jina likabadirika nikaanza kuitwa mume. Nikipiga simu hadi marafiki zake wanaitwa ili waongee na shemeji yao, hadi mama mtu anapewa simu anisalimie, wanawake bhana!

Kwa hiyo nikawa nawasiliana na huyu demu karibia kila siku, na kidogo kidogo ikawa inanisaidia kutokumuwaza Khumbu ile kwa sana, japo Khumbu sikuweza kumsahau moja kwa moja. Huyu demu wa Sinza naye ikawa ahadi ni zilezile kama nilizomuahidi huyu aliyekuwa anasoma Uganda. Lengo langu lilikuwa wote kuwaweka karibu ili nikifika Bongo nichague yupi anafaa zaidi maana ilikuwa kama miaka sita imepita toka tuonane. Yule wa Uganda alikuwa ananitumia picha kwenye email, pia alikuwa facebook, so kwenye picha bado alikuwa anaonekana ana mvuto lakini sikutaka kudanganyika na picha. Iko hivi huyu wa Uganda nilikutana naye stand ya mabasi nilikuwa nakata ticket ya kutoka Kampala kuja Dar, nakumbuka kulikuwa na kampuni moja inaitwa Akamba ndio nilikata ticket ya hilo basi. Yeye alimsindikiza mdogo wake kuja kukata ticket. Tukiwa pale kwenye ofisi za Akamba ndio nikamuona. Alikuwa na mdogo wake, nilikuja kujua baadae kuwa yule mwingine alikuwa mdogo wake. Ilikuwa ni pisi moja kali sana black beauty flani ya kihaya. Pale sehemu ya kukatia ticketi sikutaka kumsomeshea pale,nilihisi ningevuta hisia za watu maana foleni nzima alikuwa ana-shine out, hivyo ningemfuata pale lazima watu wangekuwa macho kodo, hivyo kwa kuwa nilijua kwa sababu anasafiri nitapata nafasi ya kumuimbisha kwenye basi maana niliwasikia wanaongea Kiswahili nikajua hawa tunasafiri pamoja, so nikapanga ikifika zamu yangu ya kukata ticket nikamwombe mkatisha ticketi anipe siti ya jirani na huyu black beauty. Kweli ilipofika zamu yangu nikamwomba mkatisha ticket anipe siti ya jirani na huyu black beauty, bila hiyana nikapewa hiyo siti.

Siku ya safari ilikuwa kesho yake, naingia kwenye basi, black beauty simuoni bali namkuta yule mwenzake. Basi nikakaa siti moja na huyu mwenzake kinyonge huku najiuliza ile pisi iko wapi? Ikabidi nianzishe maongezi na huyu mwenzake ili nipate nafasi ya kumwulizia huyu mwenzake waliyekuwa naye jana pale kwenye ofisi za Akamba yuko wapi? Mazungumzo yalipokolea ndio nikamwuliza, mwenzake yuko wapi? Akanijibu yule ni dada ake anaitwa Amina, alimsindikiza tu kuja kukakata ticket, yeye kabaki hajasafiri. Basi baada ya kupata hayo maelezo nikamweleza kuwa dada ako nimemzimia kinoma, na hii siti nilimuomba mkatatisha ticket anipe specifically kwa ajili yake. Basi yule mdogo mtu akacheka sana hadi machozi yakamtoka. Stori zikawa tamu kweli, njia nzima full furaha tu. Bill za chakula tunashare. Akanipa namba yake na ya dada ake, akaniahidi ujumbe wangu ataufikisha kwa dada ake kabla hata mimi sijamtafuta. Nilipofika Dar nilimtafuta baada ya kama siku mbili hivi, demu alifurahi sana. Mdogo mtu tayari alikuwa keshamaliza kazi ya kunitambulisha kwa dada ake, mimi ikawa kazi ya kufukia mabonde tu ambayo mdogo mtu alikuwa hajayaona. So, huo ndio ulikuwa mwanzo wa kujuana na hii pisi kali ya kihaya iliyokuwa inasoma Kampala ambayo kwa kiasi kikubwa ilinisaidia kuniondolea mawazo ya Khumbu.

Nikipata nafasi nitaielezea hii pisi ya Sinza jinsi tulivyokutana maana nayo ina historia kubwa sana kwenye maisha yangu, na ina mchango wa kunisaidia kumsahau Khumbu. In fact hii pisi ninimezaa nayo, niliporudi bongo nikaitandika mimba bila kutarajia, sijui ilinitegeshea.

Kitendo cha kuambiwa nitapigwa risasi na kitendo cha Khumbu kula nauli kilisababisha niamue kujitahidi kumsahau Khumbu. Japo moyo ulikuwa ni vigumu kukubaliana na hili lakini akili ilikuwa inaniambia “Konda msafi kwenu watapeleka jina tu ukiendelea kumng’ang’ania Khumbu".

Niliamua kumrudisha ulingoni yule demu niliyemfanyia vitimbi. Haikuwa hata kazi kubwa kumrejesha. Nilimwambia tu nadhani break imeisha, na sasa nipo sawa kiakili hivyo tunaweza kuendelea na mahusiano yetu.

Huyu demu wa Bloemfontein yeye aliamua kuwekeza kwangu. Ila alikuwa na wasiwasi sana kuwa huenda yeye sio changuo langu maana kila mara alikuwa ananiambia anahisi ananibore. Yule demu kusema ukweli alikuwa na sura ya kawaida ila alikuwa na mkia kufuru. Alikuwa na tako kubwa sana. Nilishawahi kumpiga picha ya uchi halafu nikawarushia masela wa Durban wakasema huo mzigo unahitaji kuwekwa kwenye makumbusho. Yule demu alikuwa na tako kubwa, yaani kubwa.

Itaendelea.
Tupo pamoja
 
Nilichogundua wengi tuna ham na picha ya Khumbu.Konda msafi kama vipi tuwekee tu hiyo picha kisha story achana nayo
 
Hivi bado yapo haya mabasi?
Kampuni ilikufa siku nyingi.. unajua technoligy ndio imewanondoka kwenye game (M pesa) zamani nakumbuka wakati nasoma Kampala, unaweza kuondoka Ubungo mpo watano tuu kwenye Bus mpaka Nairobi.. Jamaa walikuwa wanasafirisha pesa sana na percal. Ukienda kwenye ofisi zao utadhani ni bank, watu walivyojipanga kutuma na kupokea pesa..
 
We jamaa maliza story ili nianze kuisoma,huwa naanza kuisoma story mwishoni huku nikielekea mwanzoni.mf naanza chapter 10, nakuja 9, nakuja nane.... mpaka moja
 
Kuna dictionary nilinunua Kampala, hiyo ticket ya Akamba niliichomeka humo. Ni oxford Advanced Learner's 7th Edition. Uganda ilikuwa inauzwa kwa bei ndogo sana ukilinganisha na bei ya Tanzania. You can't believe hiyo ticket mpaka leo ninayo. Nilikuwa naiona ona kila ninapoitumia hii dictionary, sasa leo wakati naandika kipengele cha Amina nikakumbuka, nikajisemea acha niiangalie hii ticket kama bado ipo niiambatanishe kwenye huu uzi. Kama kumbukumbu zangu zipo vizuri nilikutana na Amina tarehe 17 March 2006. Just imagine. Hiyo hapo ticket nimewawekea
Hii kampuni yule mama mliki alikufa,ndio chanzo cha hii kampuni kufa, walikuwa na hadi Mafuta ya kupikia.
 
Back
Top Bottom