Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Inaendelea

Ilipofika saa 6 za usiku nikawaomba jamaa wanirudishe nyumbani maana wao walikuwa hata hawana dalili za kutaka kuondoka. Wakaniomba wamalizie vinywaji vyao kisha tutaondoka.

Tulifika mjengoni kwenye mida ya saa 8 hivi, mie nikaenda moja kwa moja kulala.

Asubuhi nikamcheki Khumbu kujihakiki kama anakuja kukutana na mimi. Akasema anakuja. Basi nikaingia bafuni kuoga, nikapata kifungua kinywa na safari ya kwenda town kukutana na Khumbu ikaanza. Hayo maeneo waliyokuwa wanakaa jamaa zangu nilikuwa hata sijui wapi pa kupandia daladala, ilibidi niwaombe washikaji wanielekeze. Jamaa wakaniambia nisubirie tutaondoka wote maana hata wao wanaelekea huko huko lakini niliwakatalia, niliwaambia nahitaji kuwahi hivyo acha tu nitumie daladala. Basi wakanielekeza sehemu ya kupandia daladala na wakanipa ufunguo wa akiba wa mjengo in case nitarudi mapema.

Safari ya town ikaanza na nikafika mapema kabla ya saa nne. Nikamcheki Khumbu kwenye simu na kumjulisha tayari nimeshafika na yeye akasema yupo njiani. …Baada ya muda akanipigia akasema tayari yupo workshop. Nikamwelekeza sehemu nilipo, nilikuwa ndani ya shopping mall. Akaniambia nitoke tukutane kwa nje. Basi nikatoka nikaenda sehemu moja hivi nje pale pavement za workshop zinapoanzia. Kuna nguzo flani fupi fupi nene za zege zenye urefu kama mita moja hivi zimepandwa kuzunguka hiyo pavement ya workshop kuzuia magari kuingia workshop kwa kutumia njia isiyo rasmi. Nikawa nimekaa kwenye hizo nguzo. Nikamwelekeza Khumbu sehemu nilipo, akaja. Alikuwa amevaa sketi ya blu ya jean inayoishia juu ya magoti, juu amevaa vest ametupia na kimkoti cha jeans. Miguu yake unaiona kabisa jinsi ilivyosimikwa vizuri. Alipofika pale na yeye akakaa kwenye nguzo halafu akanyoosha miguu. Kitendo cha yeye kukaa kwenye ile nguzo huku akiwa ameinyosha miguu kilinitia kiwewe, mnara ukasoma maana mapaja yakawa yamemwagika, si unajua mwanamke akikaa hata kama hana hips lakini huwa anaonekana ana hips. Sasa khumbu kajaliwa hips naturally halafu piga picha sasa amekaa kwenye nguzo na kunyosha miguu. Kisiketi kikapanda kidogo, mijipaja ikawa imemwagika, hips zimetanuka halafu nikimcheki miguu soft inawaka kama kamwagiwa asali. Nikawa natamani nimrukie. Basi tukasalimiana pale kisha nikamweleza kuwa narudi nyumbani. Akaniuliza “narudi nyumbani kusalimia au moja kwa moja?’ nikamwambia moja kwa moja, akaulizwa kwa nini? Nikamwelezea sababu nyingi kama kumiss nyumbani na nyingine nyingi lakini kubwa kuliko yote nikamwambia yeye ni sababu. Nikamwambia “maisha yangu yote niliyoishi South Africa sijawahi kupenda mwanamke kama ninavyokupenda kwa hiyo naona nikiendelea kuishi hapa nitaendelea kuteseka tu na huenda nikapoteza hata maisha kwa sababu yako” Akaniuliza unaondoka lini? Nikamwambia keshokutwa na tayari ticket ninayo. Naondokea OR Tambo airport. “Leo ni siku yangu ya mwisho kuwepo Durban. Kesho asubuhi naelekea Johannesburg kwa sababu keshokutwa saa nne asubuhi ndio naondoka”. Nilikuwa naongea kwa hisia kali, tone niliyokuwa natumia ilikuwa ya huzuni sana, body language niliyokuwa nayo ilikuwa ya majonzi. Nilipokuwa naongea nikamuona machozi yanamtiririka, akawa anajifuta kwa vidole. Nikamwangalia usoni nikaacha kuendelea kuongea, na yeye akaniangalia kisha akaniuliza “Kwa hiyo mimi ndio sababu unaondoka South Africa?” Nikamwambia usijisikie vibaya, kuna sababu nyingi zinazonifanya niondoke ila na wewe ni sababu mojawapo. Akaniambia “ahirisha safari ili tuwe pamoja” nikamwambia siwezi kuahirisha safari, tayari nimeshakata ticket. Nikamwambia kama unaweza twende zetu tukawe faragha japo kwa hii siku moja niliyo nayo hapa Durban. Akasema kwa leo hawezi ila kwa kesho sawa. Nikamwambia kesho sitakiwi kuwepo hapa, kesho nitakuwa safarini kwenda Johannesburg. Akasema “kama kweli unataka kuwa na mimi naomba uahirishe safari, ondoka siku nyingine”. Nikapiga mahesabu ya haraka haraka, nikaona kuahirisha safari itakuwa jambo la kipumbavu. Naweza kuahirisha safari halafu nikapigwa chenga tena, nikabaki kujuta. Nikamwambia, Khumbu kama hutaki kuwa na mimi kwa siku ya leo basi, siwezi kuahirisha safari. Na yeye akasema kama siwezi kuahirisha safari basi, kwa leo haitawezekana. Basi tukaagana pale nikiwa heart broken. Akaniambia nikifika Johannesburg nimpigie simu, pia nikifika Tanzania nimpigie. Nikainuka kwenye nguzo, nikaanza kuondoka. Nimepiga kama hatua tatu akaniita, “Konda msafi naomba urudi”. Nikasimama, nikageuka kumwangalia, akanifanyia ishara ya kuniita kwa mkono. Na mimi nikamwonyesha ishara kwa mikono kumwuliza anasemaje? Akasema njoo. Nikarudi, akaniambia “usiondoke kesho”. Nikamwangalia kisha nikatikisa kichwa kuashiria siwezi kuahirisha safari. Nikageuka, nikavuka barabara upande wa pili, nikamwangalia kama bado yupo nikamwona bado yupo ananiangalia, nikaendelea kutokomea, nikaondoka maeneo ya workshop.

Itaendelea.
 
Maamuzi ya kiume haya.Safi sana
 
Najaribu kuvaa uhusika of that feelings!! You guys loved each other.......
 
Duh!uliweka msimamo wa nguvu,mbele ya khumbu umekaza?
 
Naona kama stori imeisha. Kipande kilichobaki nitamalizia kesho. Acha nifanye kazi zingine wakuu.
yes mkuu..it is almost over...ila bado kipande kimoja ambacho naamini kesho utakimalizia...kifo cha khumbu...na ikiwezekana basi japo picha yake.
 
Sawa mkuu. Kiufupi South africa imejengeka sana kimiundo mbinu. Sijawahi kufika Ulaya au Marekani lakini nimeishi na watu wa hayo mataifa nilipokuwa Johannesburg. Kuna jamaa mmoja ana asili ya kieritrea ila anaishi Canada na ni raia wa Canada tulikuwa tunafanya kazi wote pale kwenye taasis ya kidini, na pia kuna wamerekani tulikuwa nao pale. In fact kuna raia kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya nimefanya nao kazi na wote hao wanasema South Africa haina tofauti na Ulaya au Marekani. Hakuna kitu utakipata Ulaya au Marekani usikipate South Africa. Huyu jamaa mwenye asili ya Eritrea alikuwa mhuni mmoja hivi. Kila weekend tulikuwa tunaenda downtown Johannesburg club au live band. Katika kupiga piga stori naye nilikuwa namwambia dhamira yangu ya kwenda Marekani lakini yeye akawa ananiambia nikae tu South africa, anasema South africa is the best country, sina haja ya kuondoka, kilichopo Marekani ndio kilichopo hapa. Tena alikuwa anasema UK huenda hata ikazidiwa na SA maana huko majengo yao ni ya kizamani ukilinganisha na majengo ya kisasa ya SA. Huyo jamaa ana ndugu zake wa damu Europe hivyo anaijua vizuri europe.
Kwa upande wa maisha, maisha ya South africa ni marahisi kama una elimu. Kwa foreigner kama upo vizuri kwenye masomo ya science na hesabu ukienda SA unakula shavu fasta la kufundisha shule za secondari. Kule kuna upungufu wa walimu wa masomo ya science na hesabu. Kuna rafiki yangu mkameruni tulikutana naye pale kwenye taasis ya dini alikuwa vizuri kwenye hesabu. Yeye alikuwa na degree ya economics. Alipata kazi ya kufundisha hisabati kwenye shule ya serikali Johannesburg. Alianza kufundisha huku pia akaanza kusoma masters. Sasa hivi yuko Marekani anaishi huko. Kaondoka mwaka Juzi South africa. Alisoma mpaka akapata Phd, huwa namuona facebook akitupia picha akila good time in the US. Nadhani alipata kazi kubwa sana huko US iliyomfanya aondoke SA.
Kwa wabongo wanaozamia SA bila kuwa na elimu yoyote wanaishi maisha ya kuunga unga sana. Wanaofanya kazi halali ni wale wanaoamua kuuza matunda na pipi mitaani. Maisha yao ni magumu tu. Wengine ambao hawataki kufanya kazi halali na wanaotaka mafanikio ya haraka ni hao wanaouza unga, waganga wa kienyeji na wezi. Wauza unga wana hela chafu na wanaishi maisha ya kifahari sana. Waganga wa kienyeji nao wanapiga pesa sana (utapeli). Wezi nao wanapata vihela, wanaendesha magari ila huyo mwizi unaweza ukamkuta leo anaendesha gari la kifahari lakini kesho ukamkuta analala nje, amekosa hata hela ya kuchangia chumba. Wabongo wengine ndio hao mabaharia wapanda meli. Wao ni kutembea na vibegi mgongoni na kwenda kunyatia meli ili wazamie. Hao utawakuta wamejaa Durban na port moja inaitwa Richardsbay. Hao ni wachafu hatari. Wanalala parking, wapo standby kudandia meli, sehemu wanazolala ukienda kukaa lazima utoke na chawa.
 
Siwez kuacha maisha Kama hayo afu et nirudi kupigwa vumbi la bongo huu ujing nisingefany
 
Yaan south Africa inahitaji waalimu wakat sisi uku waalimu hawana ajira, aiseeh Niko na Kaka yangu mwalimu wa biology and chemistry, nipe connection aibuke pande za South
 
Naona kama stori imeisha. Kipande kilichobaki nitamalizia kesho. Acha nifanye kazi zingine wakuu.
Mkuu kifo cha kumbu ndo mwisho lazima tujue kifo cha starling kilisababishwa na nin isiwe Kama picha la kihindi starling anakufa ktk maua[emoji38][emoji38]
 
Yaan south Africa inahitaji waalimu wakat sisi uku waalimu hawana ajira, aiseeh Niko na Kaka yangu mwalimu wa biology and chemistry, nipe connection aibuke pande za South
Sina connection mkuu. Yeye aende kihalali tu kisha akifika kule atapata njia ya kuingia kwenye system ya kishuleshule.
 
Yaan south Africa inahitaji waalimu wakat sisi uku waalimu hawana ajira, aiseeh Niko na Kaka yangu mwalimu wa biology and chemistry, nipe connection aibuke pande za South
Nadhani jamaa anamahanisha miaka iyo aliyokuwa South, sasa ivi sidhani kama wanauitaji wa hao waalimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…