Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Samahani mkuu, kuna sehemu ukiulizwa sababu ya kifo cha Khumbu, ukajibu urembo wake ndo uliomponza? Sasa kuna uhusiano gani kati ya kubanwa mbavu na kufariki na kuponzwa na urembo wake?
 
Samahani mkuu, kuna sehemu ukiulizwa sababu ya kifo cha Khumbu, ukajibu urembo wake ndo uliomponza? Sasa kuna uhusiano gani kati ya kubanwa mbavu na kufariki na kuponzwa na urembo wake?
Very good question. Yaani wewe ingekuwa ni mtihani ungepata extra max kwa kusoma between the lines na kugundua kitu ambacho wengi hawakukiona. Kuna scenerio nyingi tu sikuzisimulia kwa sababu ningezisimulia huu uzi ungechukua muda mrefu sana kuisha. So nakuomba upotezee tu kwa sababu uzi tulishaufunga.
 
Nafikiri mkuu konda msafi ingekuwa busara ukamjibu hilo swali kwa njia ambayo ni fupi na ya kueleweka. "Curiosity killed a Cat"
 
Bonge la story. Zaidi ya mahusiano uliyokuwa nayo kuna la kujifunza hapa. Maisha ni safari.
 

Good
 
Ahsante kwa simulizi nzuri.
Naomba nimuongelee Khumbu (the character) kwa namna tofauti kidogo na konda msafi pia (the character). Konda msafi hakufika Durban kwa bahati mbaya, hata kukatisha masomo haikuwa bahati mbaya vile vile ndiyo maana akafanikiwa kumalizia masomo yake.

Kwangu Khumbu ni binadamu ambaye alikuwa wa kipekee sana na konda msafi alibahatika kupewa kazi ya kumlinda na kumuepusha na mabalaa ya hapa duniani. Khumbu (the character) ni binti ambaye alikulia kwenye mazingira magumu na alipitia mambo ambayo yalimuathiri kiasi fulani. Kutokana na hayo 'alijiapiza' kuwa hataki kuja kuishi maisha ya shida na watoto wake waje kuwa na maisha mazuri na wapate vile ambavyo hakuvipata. Kutokana na hilo moyo wake ulikuwa umeshapigwa ganzi na alikuwa na mission moja tu ya kufanikiwa.

Upekee wa Khumbu tunaanza kuuona kwa kukutanishwa na konda msafi, sio kila mja hupata bahati hii. Nafsi ya Khumbu inamtambua konda msafi bila shida na bila kipingamizi wanafahamiana na mengine kuendelea. Ningekuwa na uwezo wa kuelezea tukio hili kiroho ningelielezea kwa kirefu lakini elimu yangu huko haijitoshelezi kumuelewesha mwingine. Hii ni moja ya udhaifu wa kizazi cha sasa, kama ambavyo shuleni hatufundishwi kuhusu fedha na mifumo yake ndivyo pia hatufundishwi kuhusu mambo ya kiroho. Dini ni sehemu ndogo tu ndiyo maana dini zipo nyingi, hakuna ubishi kuwa jamii zetu kwa miaka mingi zilikuwa na taratibu za kuendesha mambo yake kiroho walitambua kama kuna MTU anazaliwa au kama kuna mabalaa yanakuja na nini cha kufanya.

Turudi kwa Khumbu, waswahili wanaweza kusema binti huyu alikuwa na nyota kali na mafanikio ya konda msafi yaliunganishwa na nyota yake. Konda msafi ndiyo mtu pekee aliyekuwa anamfanya Khumbu kujiona naye ni mtu (hasa baada ya bibi kufariki) kwahiyo uwepo wake ulikuwa ni kama kamba aliyofungwa Khumbu ili asipitilize au asijisahau katika matendo yake. Siku zote Khumbu alikuwa ana amani kwasababu anajua chochote kitakachotokea kuna mtu anayejali na kuna kimbilio sehemu.

Changamoto zote zilizotokea kati ya hawa wawili zilikuwa ni za kuwajenga, hasa konda msafi. Kugombana kulisaidia aweze kumaliza chuo hata kuja kupata kazi baadae, kwa maneno mengine kuna vikwazo viliwekwa ili konda msafi abaki kwenye jukumu lake kuu la kuwa 'guardian angel' wa Khumbu. Kama konda msafi angeweza kutambua mapema na angekuwa na misingi mizuru kiroho bila shaka simulizi hii ingekuwa na uelekeo tofauti kidogo hata kama matokeo ya mwisho yangebaki vile vile.

Kama katika maisha yako ukipata bahati ya kukutanishwa na Khumbu basi jitahidi utimize jukumu lako, kama ukibahatika kukutanishwa na konda msafi ushukuru na usiufanye moyo wako kuwa mgumu. Sio lazima Khumbu na konda msafi wawe wapenzi, wanaweza kuwa jinsi moja, wanaweza kuwa wafanyakazi sehemu moja, majirani au watu wa rika tofauti kabisa.

Hongera kwa konda msafi kwa kumfanya Khumbu aishi na kujiona ni mtu anayethaminiwa, kitu alichokikosa sehemu kubwa ya maisha yake. Khumbu alishindwa kukiri kwa kinywa chake namna maisha yake yalivyobadilika kutokana na kukutana na konda msafi lakini hii haikuwa siri, macho yake, moyo wake na tone yake viliongea.
 
R.I.P khumbu!

Though jamaa anagoma kuelezea kifo chake
 
Hatimaye nimeimaliza leo hii story hongera zako mkuu kwa story nzuri ya kusisimua ja yenye Mafunzo mengi.

Japokua najua kuna details nyingi sana hujaziweka ila Bado burudani umeitoa to the maximum kongele zako na Asanteh mkuu.
 
Hatimaye nimeimaliza leo hii story hongera zako mkuu kwa story nzuri ya kusisimua ja yenye Mafunzo mengi.

Japokua najua kuna details nyingi sana hujaziweka ila Bado burudani umeitoa to the maximum kongele zako na Asanteh mkuu.
Hongera mm naisoma ila Kuna episode zinapotea balaa.
 
Hii tabia ya kuleta story kama episodes za HBO sijui mmetoa wapi. Acheni utiaji. Anyway, mwenye link(s) kuanzia sehemu ya 30 acheze kama yeye tafadhali, wengine hatuna brain cells za kupitia kila page.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…