Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Vunga mwana, we endelea kushusha Nondo tu. Hao wazulu na xhosa nasikia michosho sana.

One time natoka zanzibar narudi dar kwenye meli nilikaa na dada wa kizulu tukaongea sana, ila nilichogundua toka kwake ni kuwa wanajua kupenda ila kukushindilia bisu la kifua ukiwazingua ni simple sana.
Yaani hiyo simple Sana wamachame wakasome hao watu ninyoko kukuchoma na pasi mgongoni au kukupiga Bomba Ni Kama kunywa mchuzi yaani [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Baada ya hapo mapenzi yaliendelea. Khumbu alionyesha kunijali. Kama nilivyosema nimedate na wasouth wengine tofauti na Khumbu ila treatment aliyokuwa ananipa huyu mwanamke ni tofauti sana. Kuna siku nikiwa bado nipo Rossburg, maana baada ya kuanza chuo nilihama huko. Nilimuomba aje mjengoni maana tulikuwa hatujaonana karibia wiki hivi. Nilikuwa nimemmiss kinyama. Akasema atakuja lakini hakutokea. Usiku wake nikawa nampigia hapokei, baadae nilipozidi kupiga simu akazima.

Basi nikajua tu hapa yupo na msela mwingine. Ukimpenda mtu wivu hauwezi kukosekana, so nikawa namtumia msg ili akiwasha simu azikute. Simu haikupatikana mpaka kesho asubuhi. Mawazo yalikuwa mengi sana, ile kufikiria tu demu alikuwa analiwa ilikuwa inaniumiza sana. Siku hiyo sikuweza hata kufanya kazi, nilienda kufungua goli lakini baadae nikarudi mjengoni kupumzika. Kule mjengoni alikuwepo demu wa baba Isa, alikuwepo kama wiki hivi. Huyo demu alikuja na sijui baba ake.

So, nilivyofika nikamkuta demu wa baba Isa yupo sebleni anaangalia tv. Kumbuka apartment ilikuwa ya vyumba vitatu. Sebule, jiko na bafu la kushare. Nilipomkuta demu wa baba Isa nikawa nimemjoin hapo sebuleni. Tukawa tupiga story mbili za hapa na pale. Baadae mie nikaamua kuingia chumbani kupambana na stress zangu, hivyo nikamuacha demu wa baba Isa akiendelea kuangalia TV. Nilipoingia chumbani sikuufunga mlango wangu.

Nikiwa nimejilaza nikaanza kusikia makelele hapo sebleni, nikakurupuka kuelekea sebleni kujua nini kinaendelea. Ile kutoka nikakuta yule demu wa baba Isa hayupo ila kuna demu mwingine wa baba Isa yupo jikoni anatukana kwa kizulu huku anatembea tembea, na kugonga mlango wa baba Isa. Harakaharaka nikajua hapa kuna fumanizi. Mademu wote wa baba Isa nilikuwa nawafahamu maana walikuwa wanakuja kila mmoja kwa wakati wake.

Nadhani kuna mmbea aliamua kuchoma utambi siku hiyo. Basi yule demu aliyekuwa anaangalia tv alikuwa kajifungia ndani, halafu mle ndani kulikuwa na baba ake pia, we acha tu. Sasa picha linakuaje hapa. Yule demu mwingine ndio anagonga mlango kwa nguvu akimtaka mwenzie afungue wapambane. Hapo mie nimeduwaa tu sijui hata cha kufanya.

Huyu anayegonga mlango sijui alifikiria nini, mara nashangaa kaingia jikoni sijui kabeba jiwe, sijui alibeba kitu gani mara vuuu kaingia chumbani kwangu na kukipasua kile kidirisha nilichokuwa nawaambia hapo awali. Basi vipande vya glass vikawa nimetawanyika kila sehemu mle chumbani kwangu. Kile kidirisha ndio kikawa kimebomolewa.

Sasa hapa nikawa namuwazia Khumbu, sijui akija atakubali kulala kwenye hiki chumba kisichokuwa na dirisha, maskini mimi Khumbu akigoma kulala humu nitampeleka wapi? Gharama za kulala guest kwa South Africa nitaziweza kweli?
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kumbe Khumbu alipokimbia alipanda taxi mpaka workshop. Kutoka sehemu niliyokuwa naishi hadi workshop ni kama dakika 15 tu kama hakuna foleni. So Khumbu alipofika pale akawa anamweleza mshikaji eti nilikuwa nataka kula mambo wakati yupo kwenye breed, eti nilikuwa nabehave as if nimechanganyikiwa hivyo akaona isiwe kesi bora akimbie. Yote yalikuwa uongo tu na mpaka leo sijawahi kuelewa kwa nini alikimbilia workshop kwenda kuongea huo uongo. Anyway jamaa nikamwomba akifunga goli aje geto anipe ushauri kabla sijachukua maamuzi mabaya zaidi. Jioni jamaa alikuja akanishauri nini cha kufanya.

Kusema kweli kile kitendo kiliathiri sana, hadi performance yangu darasani ilishuka. Mwaka wa kwanza nilipata tuition fee remission kwa sababu ya kiwango cha juu cha ufaulu. Lakini mwaka wa pili ambapo hili tukio lilifanyika nilianza kupata max za kufaulu, nilikuwa na stress hatari. Nilikuwa najitahidi kumsahau Khumbu lakini wapi?

Ilichukua kama miezi kadhaa kabla hatujaanza tena kuwasiliana na Khumbu.

Tukio linalofuata nitaelezea nilipokutana na Khumbu akiwa na msela.
 
Washkaji zako nimewakubali,ni watu wenye upendo inaonekana mliishi vizuri maana sijaona mahali umeandika kua kuna siku mlizinguana,
Respect.
Nilitaka kumuambia hivi pia ...jamaa zake wako real ile mbaya mpaka raha yaani
 
duh huyu khumbu anafananaje kwan maana jamaa ulidata haswaa
 
Huu mzigo inabidi uishe leo, kama zege vile hakilali kitu hapa
 
Khumbu kwa mashtaka yote haya tunakuhukumu kifungo cha maisha
 
Back
Top Bottom