Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Tunaendelea,
Guess what happened baada ya Khumbu kunikimbia?
Nikiwa nimerukwa na akili baada ya kushuhudia hicho kitendo cha kutokwa nduki na demu mara simu yangu ikaita, kucheki nani ananipigia, namkuta msela wangu wa workshop ndio anapiga. Nikawa najiuliza sijui nipokee au nisipokee, maana kwa muda ule nilitakuwa kutosumbuliwa na chochote. Akili ilikuwa kama imeduwaa hivi halafu nipo kwenye maumivu makali. Simu ikazidi kuita non stop. Nikaona acha nipokee nijue jamaa anataka kusemaje. Baada ya kupokea akaanza kucheka, nikawa najiuliza huyu anacheka nini? Nikaona kama anazingua bangi tu, jamaa akaacha kucheka akaniambia "vipi wa kusoma umemfanyaje Khumbu? Nikapigwa na butwaa, mambo ya Khumbu ameyajuaje huyu. Jamaa akaendelea kusema Khumbu huyu hapa anasema amekukuta kama umechanganyikiwa hivi? ....Simu imeisha chaji baadae.
Mkuu mwambie basi khumbu tutamjia tu asijifanye mjanja mpka google tumemkosa
 
Kumbe Khumbu alipokimbia alipanda taxi mpaka workshop. Kutoka sehemu niliyokuwa naishi hadi workshop ni kama dakika 15 tu kama hakuna foleni. So Khumbu alipofika pale akawa anamweleza mshikaji eti nilikuwa nataka kula mambo wakati yupo kwenye breed, eti nilikuwa nabehave as if nimechanganyikiwa hivyo akaona isiwe kesi bora akimbie. Yote yalikuwa uongo tu na mpaka leo sijawahi kuelewa kwa nini alikimbilia workshop kwenda kuongea huo uongo. Anyway jamaa nikamwomba akifunga goli aje geto anipe ushauri kabla sijachukua maamuzi mabaya zaidi. Jioni jamaa alikuja akanishauri nini cha kufanya.

Kusema kweli kile kitendo kiliathiri sana, hadi performance yangu darasani ilishuka. Mwaka wa kwanza nilipata tuition fee remission kwa sababu ya kiwango cha juu cha ufaulu. Lakini mwaka wa pili ambapo hili tukio lilifanyika nilianza kupata max za kufaulu, nilikuwa na stress hatari. Nilikuwa najitahidi kumsahau Khumbu lakini wapi?

Ilichukua kama miezi sita kabla hatujaanza tena kuwasiliana na Khumbu.

Tukio linalofuata nitaelezea nilipokutana na Khumbu akiwa na msela.
Mkuu hapo ndo penyewe sasa
Sema khumbu jamaa yake huenda alianza kumpa pesa nzuri ndo maana akawa anakukwepa ..

Ila mpka sasa khumbu halisi hajapatikana tutampata tu wala usiweke picha
 
Haya tunaendelea, hapa tunaelekea lile tukio lililonifanya nimkimbize Khumbu nikiwa na boxer tu kama nimepandwa na kichaa, of course kila binadamu ana elements za ukichaa maana siku ile sikuamini kama ni mimi.
Nilipoupata ule mpunga kutoka kwa Don wa sembe nikasema afe punda huu mzigo lazima Khumbu apate share, hata kama ataamua kuuchukua wote sawa tu ilimradi roho yangu ipate hitaji lake.
Nikaona njia pekee ni kumuibukia kwao. Maana niliona nikimpigia simu nimwambie kuna hela hapa njoo uchukue atahisi kama namnunua, of course niliamua kumnunua ila niliona kwenda direct ataniona kavu.
Kesho yake sikuingia darasani, asubuhi tu tayari nipo stend kwenye foleni ya kwenda Inanda. By the way kule mnapanda daladala kwa foleni, sio kama huku kupigana vikumbo mwenye nguvu ndio anapanda. Huko ukifika stand unapanga foleni kama upo bank.
Sikutaka kumpigia simu wala kutuma sms. Nilitaka kumfanyia ambush tu. Kuhusu baba watoto wake nilikuwa sijali tena, uwazimu ulikuwa kama umenipanda kichwani. Mara huyu nishafika, bahati nzuri nikamkuta hata nguo za kulalia hajabadilisha. Nikamkuta yeye, bibi yake na mwanae. Akanikaribisha kwa heshima zote japo alikuwa na sura ya kujiuliza, this nigga what is he here for? Halafu Khumbu ana kicheko flani kama cha wadada wa kiswahili, akacheka akaniangalia, kama vile anajiuliza huyu jamaa vipi asubuhi asubuhi yote hii? Haogopi kufumuliwa ubongo? Anyway demu ukishamula tena mara nyingi hata hazihesabiki hana nguvu kubwa ya kukuintimidate. Kwa hiyo nikamwambia young lady I need you. Hapa hata chuo sijaenda kwa sababu yako, kwa hiyo leo lazima kieleweke. Simu hupokei, ukipokea unasema uko busy so nimeamua kukufuata kwenu labda utanielewa. Tuliongea mengi na tukakubaliana. Atakuja jioni. Kwa hiyo niondoke nikaendelee na shughuli zangu jioni atakuja. Basi mie nikawaaga nikaondoka. Siku sikutaka tena kwenda chuo japo kuna vipindi vya mchana ningeweza kuviattend. Nikanyoka moja kwa moja supermarket kwenda kufanya mahemezi ya mgeni. Jioni kwenye saa 10 akanipigia akasema amekaribia hivyo niwepo nyumbani. Nikamjibu aje tu nipo nyumbani. Muda si mrefu akawa amefika.
Alipofika nikanotice hajabeba chochote, hana mkoba wake anaokujaga nao, ana kiwallet kidogo dogo hivi. Nikahisi hapa kuna hatari inaenda kutokea. Roho yangu ikawa inaniambia huyu mtu hajaja kulala wala nini, amekuja kusoma mazingira tu kama kuna maisha au hakuna. Tumekaa kidogo akaniomba nikamnunulie vocha dukani, nikahisi huyu ataondoka, nikienda tu dukani nikirudi sitamkuta. Nikamwambia mie kwa kweli nimekumiss sana, naomba kwanza unipe kimoja halafu mambo mengine yafuate. Halafu nikaamua kuchomekea harakaharaka kama nina hela ili kama ana mpango wa kunikimbia aahirishe, so nikaendelea kumwambia, najua wewe ni mwanamke unahitaji pia hela ya kujikimu hivyo sometimes natakiwa nikuelewe unaposhindwa kuja kunitembelea, japo nilijihisi nimeongea pumba ila nilijipa moyo kwa kufikiria huyu shida yake si ni hela hata kama nikiongea pumba hakuna shida ilimradi nimpa fungu lake. Basi akaniambia, nenda basi ukaoge then nikupe. Kidogo nikaanza kupata matumaini kuwa mzigo napewa, hata kama hatalala haina shida. Nikaingia kwenye kabati nikamtolea rand 400, akazipokea akawa kama kazikunja kunja hivi. So, fasta nikaingia bafuni ili nioge fasta nile mzigo. Nilipokuwa bafuni nikawa nasikia kama movements hivi, nikahisi hapa nakimbiwa, nilichofanya nikaufungua kidogo mlango wa bafu ili kama atataka kukimbia nimdake maana mlango wa kutokea lazima upitie mbele ya bafu. Basi bana nikatupa boxer huko, nikafungua bomba mvua nikaanza kuoga, sekunde chache tu baada ya kuanza kuoga nikaona mtu ananyata kuelekea mlangoni, roho ikanilipuka paa! Basi namipovu yangu nikakurupuka kuwahi mlangoni, nikawa nimechelewa, huyo keshafyatuka kama radi, nikatoka nje kuchungulia nikamuona anaishiria kutoka getini, fasta nikarudi ndani nikavaa boxer nikatoka ili nimfukuze, nikatoka mpaka barabarani kabisa huku natetemeka hata sijielewi, dah! baadae nikajitambua hapa sijavaa chochote, nipo na boxer tu acha nirudi ndani nikatafakari.

Itaendelea...
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] ma-tacore yalikupagawisha mdogo wangu
 
Halafu nimesahau kuelezea kitu pale nilipomuona ananyata kukuelekea mlango ili akimbie. Nilipoona kile kiwilowili chake kinakatiza kuelekea mlangoni roho ikapiga pah! Halafu nikajikuta nimeropoka kwa sauti kubwa "**** you bitch"
Aisee uliharibu zaidi ... Hata hivyo alishageuka kuwa Toxic
 
Tuendelee
Baada ya kumuona Khumbu anaendelea kulia huku akiniomba niifute hiyo namba mbele ya macho yake na nisijaribu kuipiga in case nitakuwa bado nimeikariri niliamua kuifuta, na yeye akashuhudia kuwa nimeifuta. Baada ya kuifuta hiyo namba akaanza kupack vitu vyake kwenye mkoba akiwa hanijibu chochote ninachomwuliza. Baada ya kumaliza kupack vitu vyake, aliambia maneno machache tu "Konda msafi naomba nauli niondoke". Mzee nikagoma kutoa nauli. Basi akafungua mlango akaondoka. Baadae na mimi nikaingia bafuni nikaoga nikaelekea workshop. Hata hamu ya chai sikuwa nayo tena. Nikiwa kwenye taxi naelekea workshop nilijaribu kumpigia simu lakini hakupokea. Roho ilianza kuniuma kwa nini najivurugia mambo mwenyewe, kwa nini nisingeendelea kujifanya mjinga tu ili niendelee kufaidi penzi la Khumbu? Anyway nilianza kuwaza mengi.
Nilipofika kule workshop nikawahadithia jamaa zangu yaliyotokea kati yangu na shemeji yao. Jamaa waliposikia kuwa mzazi mwenzie na Khumbu ni mmiliki wa taxi (daladala) wakaniambia mzee hapo umeingia cha kike. Wamiliki wa taxi ni ma-gangstars, hapo ni chuma mkononi. Ni kati ya industries in South Africa zinazoongoza kwa kuuana kwa risasi. Wamiliki wa taxi kuchapana risasi ni swala la kawaida kabisa. Siku ile ya kwanza Khumbu alishawahi kuniambia babe father wake ni mmiliki wa taxi. Kwa hiyo jamaa wakaconnect dots kuwa mwenye ile namba lazima atakuwa ni baba wa mwanae.
Aisee

Khumbu ni mnoma
 
Oyaaa na I'd ya khumbu tushafungua aiseeh
Dah haya wewe khumbu wa jf tupe hiyo chura tuione
 
Back
Top Bottom