Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Khumbu angetuulia ndugu yetu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Haya tunaendelea, hapa tunaelekea lile tukio lililonifanya nimkimbize Khumbu nikiwa na boxer tu kama nimepandwa na kichaa, of course kila binadamu ana elements za ukichaa maana siku ile sikuamini kama ni mimi.
Nilipoupata ule mpunga kutoka kwa Don wa sembe nikasema afe punda huu mzigo lazima Khumbu apate share, hata kama ataamua kuuchukua wote sawa tu ilimradi roho yangu ipate hitaji lake.
Nikaona njia pekee ni kumuibukia kwao. Maana niliona nikimpigia simu nimwambie kuna hela hapa njoo uchukue atahisi kama namnunua, of course niliamua kumnunua ila niliona kwenda direct ataniona kavu.
Kesho yake sikuingia darasani, asubuhi tu tayari nipo stend kwenye foleni ya kwenda Inanda. By the way kule mnapanda daladala kwa foleni, sio kama huku kupigana vikumbo mwenye nguvu ndio anapanda. Huko ukifika stand unapanga foleni kama upo bank.
Sikutaka kumpigia simu wala kutuma sms. Nilitaka kumfanyia ambush tu. Kuhusu baba watoto wake nilikuwa sijali tena, uwazimu ulikuwa kama umenipanda kichwani. Mara huyu nishafika, bahati nzuri nikamkuta hata nguo za kulalia hajabadilisha. Nikamkuta yeye, bibi yake na mwanae. Akanikaribisha kwa heshima zote japo alikuwa na sura ya kujiuliza, this nigga what is he here for? Halafu Khumbu ana kicheko flani kama cha wadada wa kiswahili, akacheka akaniangalia, kama vile anajiuliza huyu jamaa vipi asubuhi asubuhi yote hii? Haogopi kufumuliwa ubongo? Anyway demu ukishamula tena mara nyingi hata hazihesabiki hana nguvu kubwa ya kukuintimidate. Kwa hiyo nikamwambia young lady I need you. Hapa hata chuo sijaenda kwa sababu yako, kwa hiyo leo lazima kieleweke. Simu hupokei, ukipokea unasema uko busy so nimeamua kukufuata kwenu labda utanielewa. Tuliongea mengi na tukakubaliana. Atakuja jioni. Kwa hiyo niondoke nikaendelee na shughuli zangu jioni atakuja. Basi mie nikawaaga nikaondoka. Siku sikutaka tena kwenda chuo japo kuna vipindi vya mchana ningeweza kuviattend. Nikanyoka moja kwa moja supermarket kwenda kufanya mahemezi ya mgeni. Jioni kwenye saa 10 akanipigia akasema amekaribia hivyo niwepo nyumbani. Nikamjibu aje tu nipo nyumbani. Muda si mrefu akawa amefika.
Alipofika nikanotice hajabeba chochote, hana mkoba wake anaokujaga nao, ana kiwallet kidogo dogo hivi. Nikahisi hapa kuna hatari inaenda kutokea. Roho yangu ikawa inaniambia huyu mtu hajaja kulala wala nini, amekuja kusoma mazingira tu kama kuna maisha au hakuna. Tumekaa kidogo akaniomba nikamnunulie vocha dukani, nikahisi huyu ataondoka, nikienda tu dukani nikirudi sitamkuta. Nikamwambia mie kwa kweli nimekumiss sana, naomba kwanza unipe kimoja halafu mambo mengine yafuate. Halafu nikaamua kuchomekea harakaharaka kama nina hela ili kama ana mpango wa kunikimbia aahirishe, so nikaendelea kumwambia, najua wewe ni mwanamke unahitaji pia hela ya kujikimu hivyo sometimes natakiwa nikuelewe unaposhindwa kuja kunitembelea, japo nilijihisi nimeongea pumba ila nilijipa moyo kwa kufikiria huyu shida yake si ni hela hata kama nikiongea pumba hakuna shida ilimradi nimpa fungu lake. Basi akaniambia, nenda basi ukaoge then nikupe. Kidogo nikaanza kupata matumaini kuwa mzigo napewa, hata kama hatalala haina shida. Nikaingia kwenye kabati nikamtolea rand 400, akazipokea akawa kama kazikunja kunja hivi. So, fasta nikaingia bafuni ili nioge fasta nile mzigo. Nilipokuwa bafuni nikawa nasikia kama movements hivi, nikahisi hapa nakimbiwa, nilichofanya nikaufungua kidogo mlango wa bafu ili kama atataka kukimbia nimdake maana mlango wa kutokea lazima upitie mbele ya bafu. Basi bana nikatupa boxer huko, nikafungua bomba mvua nikaanza kuoga, sekunde chache tu baada ya kuanza kuoga nikaona mtu ananyata kuelekea mlangoni, roho ikanilipuka paa! Basi namipovu yangu nikakurupuka kuwahi mlangoni, nikawa nimechelewa, huyo keshafyatuka kama radi, nikatoka nje kuchungulia nikamuona anaishiria kutoka getini, fasta nikarudi ndani nikavaa boxer nikatoka ili nimfukuze, nikatoka mpaka barabarani kabisa huku natetemeka hata sijielewi, dah! baadae nikajitambua hapa sijavaa chochote, nipo na boxer tu acha nirudi ndani nikatafakari.
Itaendelea...
😂😂😂 Ukikesha tu upo singleAisee..next episode please
Haya malaika wa jf msianze hukumu maana hamkawii..
Ndo na kwnye pepa utaexplain namna matrrako ya khumbu yanafananaKesho nna test cjasom sbb ya khumb dooh ebu ishia hpa mzee
Tuendelee...By the way kwa wale ambao hawajafika Durban mnaweza kuigoogle "the workshop mall" mkaiona.
Nami ndio nimemaliza uzi wote muda huu. Mapenzi ni usenge kweli, yanaweza yakakufanya upoteze kitu muhimu kisa mbunye.Hatimae nmemaliza kusoma uzi wote na comments zake..nipende tu kusema mapenzi ni usenge..jamaaa unanikumbusha kisa cha demu mmoja nilikutana nae bukoba..sito kuja msaahau hadi na kufa miss yu sana M.
#MaendeleoHayanaChama
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
[emoji8][emoji8][emoji8]
@konda msafi ongeza mzgoKabla hatujaendelea na matukio ya Khumbu hebu jaribuni kuigoogle "the workshop mall" ili muweze ku-visualize ile park(garden) niliyoenda kukaa na kuanza kutokwa machozi bila kupenda, huenda hata mkapaona hiyo sehemu niliyokaa ndugu yenu hahahaha!
Haya tuendelee,
Baada ya kujiapiza kuwa huyu anayeutesa moyo wangu lazima nifanye rebound ya kufa mtu ili nimle hata mara moja ya mwisho, na siku akijiroga aingie kwenye 18 zangu nitakachomfanya hatanisahau. Ikawa kama namtaka Khumbu kwa ajili ya kumkomesha na si kwa ajili ya kumpenda. Of course deep down nilikuwa nampenda ila tayari moyo wangu ulikuwa umejawa hisia za kumkomesha.
Hapa nikawa natafakari nini cha kufanya ili nitimize dhamira yangu. Cha kwanza nilichokifikiria ni kumpigia simu jamaa yangu don wa unga anitoe hii sehemu niliyokuwa naishi ili nikakae kwenye mijengo yake maana alikuwa na mijengo kibao ya kufanyia mambo yake. Unajua wauza ngada huwa na machimbo tofauti tofauti. Yaani huwa wanakodisha majumba sehemu tofauti tofauti tena maeneo wayayokaa watu wenye pesa zao mjini kwa ajili ya kufanyia biashara zao. Humu ndimo shughuli ya kufunga mzigo tayari kwa kuupeleka streets hufanyika. Hilo wazo nikaona halifai. Nikafikiria nikija kudakwa kwenye hizo yumba za sembe si na shule itaishia hapo. Of course kufungwa nisingefungwa maana don angenitoa fasta tu ila hii kesi ikifika chuo lazima nitimuliwe, so nikaona idea ya kwenda kuishi huko haifai. Idea ya pili nikawaza labda nipambane nitafute hata part time job maana documents nilizokuwa natumia zilikuwa zinaniruhusu kusoma na kufanya kazi. Nipambane nipate mjengo wa maana wa kuishi peke yangu. Hii idea tena nikaona kama itakuwa ngumu. Kuishi mjengo wa maana peke yako kwa South africa inahitajika hela ndefu sana, so hata kama nikipata kazi sidhani kama itakidhi haya ninayoyapanga. Nikawa kama nimevurugwa vile maana moja haikai, mbili haikai. Anyway nikajiambia acha niyapeleke mambo taratibu mbele ya safari nitapata tu njia ya kutokea na hatimae kumtia Khumbu mikononi.
Itaendelea...