Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uno la kukung'uta siafu. [emoji3][emoji3][unalitaka
Kabisa mkuu. Ningendelea kubaki South africa ningekuwa mbali sana kimaisha. Sasa hivi kila nikreflect back naona nilifanya maamuzi based on emotion. Kuna fursa nyingi sana niliziacha kwa sababu I was irrational. Of course hata huku bongo niliweza kusoma na kupata CPA. I'm a CPA holder from NBAA lakini nadhani ningekuwa South Africa ningekuwa mbali mno.konda msafi kutokana na hii sehemu ya mwisho uliyoweka inaonekana (kutokana na mtazamo wangu) hisia zilikutawala kurudi nyumbani hayakuwa mawazo pevu kwani tayari ulikubalika kwenye hiyo kampuni na huyo director alijaribu kukusaidia kwa mawazo.
Na kitu kingine ulipata marafiki wazuri kama kina Sandile na hao ndugu zako wa Workshop ambao tayari ungeamua kufanya maisha yako huko ya kudumu , Nyumbani ungekua unaenda kusalimia tu na kama nitakua nakosea unisamehe mkuu lakini naweza sema kwasasa unajutia hayo maamuzi ndiyo yaliyopelekea kuandika huu uzi ili watu wajifunze.Ukizingatia na hali ya uchumi huko Tanzania kwa sasa pamoja na janga hili la korona.
Maisha si lazima ufanye nyumbani na kwa takwimu wengi wao ambao hufanikiwa ni wale wanafanya maisha mbali na nyumbani kwao.
Nimejifunza sana hapa kuwa USIKUBALI KUFANYA MAAMUZI YA MAISHA UKIWA NA 'EMOTIONAL THINKING' kuna kipindi nikiwa chuo nilitaka kuharibu maisha kwa mwenendo wa hisia za mapenzi.
Mytake: Ukipata nafasi ya kutoka nje ya mipaka ya nchi hakikisha unapambana huko unawekeza kidogo lakini nyumbani unawekeza vya kutosha kwa ajili ya kusaidia ndugu,jamaa na marafiki na itakusaidia pia hata ukiamua kurudi nyumbani.
Cheers!!
ila konda u are the pain that is sweet yani unazunguuka ila basi ndo addiction imekuwa sasa nimejipromise kukublok hereafter nisisome simulizi yako yoyote tena ikiisha hiiSiku nilipoondoka tulionana na tuliagana. Kuhusu msiba nitaelezea kwa kirefu maana stori bado haijaisha.
Sitaleta simulizi yoyote zaidi ya hii. This is a reflection on my life.ila konda u are the pain that is sweet yani unazunguuka ila bad ndo addiction imekuwa sasa nimejipromise kukublok hereafter nisisome simulizi yako yoyote tena ikiisha hii
Inaendelea
Khumbu alinipeleka nilikofikia kuchukua vitu vyangu kisha akanipeleka stand kuangalia usafiri wa kunirudisha Bloemfontein. Katika mizunguko yote hiyo niliweza kunotice kuwa Khumbu bado alikuwa ananipenda ila ni kama alikuwa na commitment flani hivi zinanamfanya kuwa na wakati mgumu kunisikiliza kila ninachomwambia, maana kuna kipindi alikuwa kama anazama kwenye lindi la mawazo hivi, halafu nikiwa namweleza ni jinsi gani anayafanya maisha yangu kuwa magumu kimahusiano nilikuwa namuona kama mtu anayejutia hivi. Kulikuwa na zile moments ukimya unatawala halafu mkija kuangalia unaona kama kila mtu machozi yanamlengalenga. Aliponifikisha stand, nikashuka na yeye akashuka, tukaagana kwa kukumbatiana, sikuweza kuongea chochote maana kitendo cha kumkumbatia na kuushika mwili wake kilinifanya niingiwe na huzuni sana, nilimsikia tu akitamka maneno mawili “I’m sorry” na akaanza kujitoa mikononi mwangu, nilikuwa nimemkumbatia kuzungusha mikono yangu kiunoni kwake mpaka ikakutana, kwa hiyo akawa anaishika kwa kuiachanisha ili niweze kumuachia. Baada ya kujitoa mikononi mwangu akaingia garini akaondoka. Niliendelea kusimama pale nikimwangalia mpaka alipojichanganya kwenye magari mengine ndio nikaondoka hilo eneo.
Njiani nikiwa kwenye basi nilianza kufikiria vitu vingi sana vya kimaisha. Mojawapo nilianza kufikiria je nieendelee kuishi Bloemfontein nijenge maisha na huyu mwanamke wa Bloemfontein? Je nirudi Durban nikatafute kazi huko ili niweze kuwa karibu na Khumbu? Je nirudi Tanzania nikamthaminishe Amina na yule demu wa Sinza kisha atakayelipa zaidi nije naye South Africa? Baada ya hii graduation je niendelee kuishi South Africa yaani nijichanganye kabisa hapa niachane na mawazo ya kurudi Tanzania yaani hapa Sauzi yawe ndio maisha yangu permanent? Je nirudi Tanzania nikatafute kazi, nikaishi tu nyumbani huenda nikaishi kwa furaha zaidi? Maswali yalikuwa mengi na sikujua lipi niamue.
Baada ya graduation niliendelea na kazi huku nikiwa na huyu mwanamke wa Bloemfontein. Pia niliendelea kuwasiliana na Amina na huyu wa Sinza. Huyu wa Sinza alikuwa na sauti moja amazing. Kipindi naonana naye alikuwa mzuri sana ila kwa kuwa ilikuwa ishapita miaka mingi nilikuwa na wasiwasi kama bado ni mrembo maana wanawake huwa wanabadirika haraka sana, miaka sita kwa wanawake ni miaka mingi sana. Amina alikuwa ananitumia picha na alionekana bado analipa sana tu ila huyu wa Sinza kila nikimwomba anitumie picha alikuwa anadai nije nimuone mwenyewe kwa macho yangu ila kwa maoni yeke yeye ni mrembo wa haja. Huyu wa Sinza kitendo cha kukataa kunitumia picha kilianza kunitia wasiwasi hivyo nikaamua kutuma mtu kwenda kukutana naye ili anipe feedback. Kuna mdogo wangu alikuwa anasoma chuo flani nikampigia simu nikamwomba akamcheki huyu demu. Nikampa namba ya huyo demu na pia nikampigia simu huyo demu nikamwambia shemeji yako nimemwomba aje akusalimie ili mjuane pia apajue unapoishi ili hata kama kuna shida yoyote iwe rahisi kupatikana kwako. Demu akakubali. Dogo akaenda kumcheki na baada ya kumcheki akanipigia simu kunijulisha matokeo. Dogo akaniambia demu ni wa kawaida sana hana maajabu yoyote. Kama ni wa kula na kusepa fresh ila kama unataka kufanya naye maisha na kwa jinsi ninavyokujua unapenda kula vilivyo bora huyo hajafikia viwango vyako. Hiyo ilikuwa tathimini ya dogo. Dah! nikawa najiuliza labda huyu dogo ana jambo lake tu. Mbona demu alikuwa kifaa hivi enzi hizo, iweje awe mbovu tena? Nikasema huyu dogo anazingua, acha niendelee na mchakato wa kuwa naye karibu huyu demu. After all nishatumia gharama za kupiga simu karibia kila siku hivyo hata kama atakuwa halipi acha angalau nikafidie gharama zangu kwa kumla. Hivyo maisha ya kuendelea kuwasiliana na wote hawa wawili yaliendelea hadi niliporudi Tanzania.
Kadri siku zilivyokuwa zinasonga ndivyo nilivyozidi kupata moto wa kurudi nyumbani. Picha za Amina na Sauti ya demu wa Sinza zilikuwa zinanipa matumaini mapya ya kimapenzi. Huyu wa Sinza alikuwa na sauti nzuri hatari, nikiwa naongea naye nilikuwa hadi dushe linasimama. Amina naye hivyo hivyo, picha zilikuwa zinanichangaya sana.
Siku moja usiku mwezi wa 10, 2012 nikakata shauri la kurudi nyumbani. Niliamka usiku wa manane, nikachukua diary yangu nikaandika tarehe ya hiyo siku nikasema hii tarehe ndio tarehe niliyokata shauri na kuamua kurudi Bongo.
Kesho yake asubuhi nilipofika ofisini nikamfuata Boss wa kampuni, ni mmoja wa madirectors, nikamwambia “Leo naacha kazi”. Aliniangalia akiwa kama anashangaa, akasema nirudie tena nilichokisema, nikarudia tena “Leo naacha kazi” nilimuona kama kaduwaa. Alikuwa ana kikombe cha kahawa mkononi akakiweka kwenye mezani kisha akaniuliza vipi unaumwa? Umechanganyikiwa? Nikamjibu siumwi wala sijachanganyikiwa. Nimeamua tu niache kazi, nimeamua kurudi nyumbani. I miss home. Akasema wewe Konda msafi unacheza na maisha. Unarudi Tanzania kufanya nini? Akaanza kunipa ushauri, nakumbuka kuna maneno nayakumbuka mpaka leo aliniambia, alisema “All these achievements I have I never got them in one day I have acquired them in years. If you serve God, God will take care of you” . Akaniomba jioni baada ya kazi nisiondoke ili tupate muda wa kuzungumza zaidi. Jioni baada ya kazi nikaenda ofisini kwake. Jamaa alinishauri mambo mengi sana ya kimaisha. Akawa ananiambia sio jambo la kushangaza kama siku moja ataniona namiliki kampuni yangu hapa South Africa kama nitakuwa na nidhamu ya kazi. Pale kwenye kampuni nilikuwa nadili na suppliers wa materials na payroll. Auditor wa kampuni alikuwa Ernst and Young kwa hiyo queries zote za auditor kuhusu suppliers na payroll nilikuwa nazi-attend. Kila mwisho wa mwezi nilikuwa napelekwa na dereva wa kampuni kwa auditor. Suppliers wakipiga simu kuulizia malipo yao mimi ndio nilikuwa nadili nao au mimi kuwapigia simu kama kuna mzigo una shida au umechelewa kufika. Kuhakikisha materials yamepokelewa na kampuni ilikuwa ni kazi yangu, invoice za suppliers lazima nizihakiki kabla ya malipo. Jamaa akawa ananiambia hatashangaa siku moja akiniona nimeshakuwa Chartered Accountant kama nitavumilia, na akasema ataniunganisha na CAs ili wanipe muongozo jinsi ya kufika hapo. Kiufupi jamaa alianza kunipa elimu ya maisha mpaka nikaghairi maamuzi yangu.
Itaendelea
Sitaleta simulizi yoyote zaidi ya hii. This is a reflection on m
leta vitu mkuu mi nakutisha tu labda nafsi yako itaguswa kuongeza nondoSitaleta simulizi yoyote zaidi ya hii. This is a reflection on my life.
Tupia stry mfululizo mkuuSitaleta simulizi yoyote zaidi ya hii. This is a reflection on my life.
Dada wa Sinza nilikutana naye kati ya 2007 au 2008, tena kesho yake ndio nilikuwa nasafiri kurudi SA. Mawasiliano niliyafufua 2012 so unaweza kuona muda gani ulikuwa umepita, na kama unavyojua wanawake mnavyobadirika kimaumbile fasta, pia wasiwasi uliongezeka alipokataa kutuma picha.Sijapapenda hapo pa kumthaminisha dada wa sinza kupitia dogo[emoji276]
Karibu sana mkuuNimepata wazo la kuzamia south ki ukwel bongo wachaw wengi
Mwana uko dizonga tutakuwa wote Mungu akijaalia maana nataka nije nimehipanga hata 2000$ iwe mfukoniKaribu sana mkuu
Huyo Dada wa Sinza na Amina nao Wana story yao katika uzi mwingine kabla ya huu Kaka. So ukiwasoma ndo utaelewa kwenye huo uzi mwingineHiyo story ya amina ndiyo vile vipande kwenye movie na pelekaga mbele nataka kusikia story ya khumbu tu na maisha ya bondeni kwa ujumla
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]wachawi??? Kmmmke pesa huna weweNimepata wazo la kuzamia south ki ukwel bongo wachaw wengi
Poa mkuu sema angalia iyo hela usije kuwaachia kina khumbu maana wapo wengi sana alafu wanapenda sana helaMwana uko dizonga tutakuwa wote Mungu akijaalia maana nataka nije nimehipanga hata 2000$ iwe mfukoni