Inaendelea
Kama nilivyoeleza hapo awali kuwa siku yangu ya mwisho kule Bloemfontein nililala kwa yule mwanamke wangu. Usiku kucha ilikuwa ni kupigana miti tu na stori, hatukulala kabisa mpaka kunakucha. Tunapiga stori huku tumekumbatiana, mnara ukisoma shughuli inaanza upya. Demu nilikuwa nampa ahadi za uongo za kurudi South Africa. Kiukweli hata kama ningerudi South Africa sikupanga kuendelea kuwa naye, kama ningerudi South Africa ningekomea Durban, Durban ni mji mtamu sana. Pamoja na kwamba nilipata kazi Bloemfontein lakini nilikuwa natamani kama hii kazi ningekuwa nimeipata Durban. Durban kuna maraha sana.
Asubuhi yule demu alinisindikiza hadi kituo cha daladala (taxi). Nikachukua daladala hadi town stand ya mabasi. Nilikuwa naondoka na basi la saa mbili asubuhi.
Nilifika Durban saa 11 Jioni. Jamaa zangu wakaja kunipokea na kunipeleka magetoni. Walikuwa wamehamia sehemu nyingine tofauti na ile ya zamani tulipokuwa tunaishi kipindi ninasoma. Ulikuwa mjengo mmoja mzuri wenye kila kitu ndani. Ukiwa unafanya hizi kazi kuhama hama ni kama jadi. Hata kipindi nimekuja kwenye graduation walikuwa wanakaa sehemu tofauti na ile tuliyokuwa tunakaa kabla sijapata kazi. Kwa hiyo kuhama hama ni kawaida sana kwa hawa jamaa zangu.
Tulipofika mjengoni jamaa wakanionyesha chumba nitakachotumia na mazingira ya mule ndani halafu kabla hawajaondoka kwenda kwenye mishe zao tukapanga baadae watarudi kunichukua twende out nikaiage Durban.
Walipoondoka nikaingia bafuni kuoga, kisha nikaingia jikoni kuandaa chakula. Hawa jamaa kati ya vitu ninavyowapendea chakula ni moja ya priorities yao. Kwenye misosi jamaa hawana longolongo. Kwenye fridge na kwenye makabati kuna kila kitu labda uwe mvivu tu wa kupika. Huwa wanapika kuku mzima wa kienyeji na kumtafuna tu.
Baada ya kumaliza kula nikaanza sasa kupanga jinsi ya kukutana na Khumbu. Nikawa nafikiria kama atakubali kukutana na mimi wapi nitampeleka, nilikuwa nataka nimgonge kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoka South Africa. Nikafikiria kumleta humu ndani isingekuwa jambo la busara sana maana kazi ya hawa jamaa hairuhusu watu kupajua jua sana hapa. Maana naweza kumleta hapa halafu nikawasababishia matatizo. Kumpeleka guest house na kwenyewe nikawa naona kama yatakuwa matumizi mabaya ya hela ukizingatia kuwa hapa nipo safarini na huko bongo sijui kutakuwa na hali gani hivyo natakiwa nitumie hela kwa uangalifu ili inisaidie kwa muda nikiwa bado sijapata kazi. Baada ya kufikiria sana nikachukua maamuzi ya kukutana naye town halafu nitajua cha kufanya nikishakutana naye. Nikachukua simu nikampigia. Hapo ilikuwa kwenye saa moja hivi usiku. Nikamwambia tayari nipo Durban hivyo namuomba kesho asubuhi ajitahidi sana tuonane, akakubali. Tukapanga tukutane kesho mida ya saa nne maeneo ya workshop halafu kutokea hapo tutaamua cha kufanya.
Kwenye saa tatu jamaa wakawa wamerudi, wakaweka mambo yao sawa kisha tukaingia kwenye gari tukaelekea town moja kwa moja kwenye bar moja ilikuwa inamilikiwa na mnaijeria. Jamaa wakaanza kupiga mtungi kama kawaida yao, mie nikawa nakunywa vinywaji laini tu na nyama choma. Ile sehemu ilikuwa imechangamka kweli. Inapigwa kwaito na miziki ya kikongo. Kulikuwa machine flani hivi unaenda kudumbukiza sarafu kama unataka upigwe wimbo unaoupenda. Hapo watu wanaponda starehe tu kama vile hawajui kama kuna kufa. Masista du wakali wimbo mzuri ukipigwa wanainuka kwenda kukata nyonga. Mademu wakali wamezunguka meza wanakunywa pombe huku wakijitikisa kama hawana akili nzuri. Kuna demu mmoja alikuwa anajuana na hawa jamaa zangu akawa anawauliza jamaa mimi ni nani mbona sinywi pombe halafu naonekana mstaarabu? Jamaa wakanitambulisha, wakamwambia huyu ni homeboy amekaa sana hapa Durban, hakuwepo hapa Durban kwa muda kidogo alikuwa zake Bloem. Demu akaanza kusema kama anatania, anawaambia jamaa zangu “nimempenda ndugu yenu” akainuka akawa ananivutavuta ile kilevilevi anataka nicheze naye, mie nikawa namkatalia sitaki kuinuka kwenda kucheza. Demu akawa ananikatikia kwa nyuma huku ananishikashika kama kutaka kunikumbatia hivi. Jamaa wakawa wananiambia huku wakicheka “Konda msafi unarudi bongo unaziacha starehe zote hizi mkuu, unamuacha Khumbu”? Dah!walipomtaja Khumbu moyo ukalipuka pah! moyo ukaanza kuuma, raha zote hizi naziacha jamani. Sijui nighairi safari?!
Itaendelea