Jinsi mbunge Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti

Hivi mnamkumbuka Mbunge aliyeitwa Kihiyo? Mwaka 1995?

Alikuwa Mbunge wa Temeke kupitia chama cha mapinduzi.

Alishtakiwa kwa kosa la kughushi vyeti, mahakama ikatengua Ubunge wake na uchaguzi ukarudiwa, katika uchaguzi wa marudio alishinda Mh Agustine Lyatonga Mrema.

Kihiyo alihukumiwa kwa kutumia sheria za Tanzania ambazoleo Mama Angela Kairuki kazinukuu.

Je? inamana Kihiyo hakuwa anajua kusoma na kuandika kama amabavyo tumeambiwa ndiyo sifa ya kitaaluma ya mwanasiasa?

Au Kihiyo alikuwa mjinga alieweza kushinda ubunge halafu akashindwa kujitetea mahakamani kuwa anajua kusoma na kuandika?

NB: Huenda sheria zimebadilika sisi hatujui...
 

Mimi nafikiri kosa linahesabika pale ambapo mwanasiasa ( Mbunge , Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Diwani) atakuwa amewasilisha cheti feki kwenye wasifu wake. Hilo automatically linahesabika kama kosa la kughushi. Lakini kama atakuwa amekaa kimya inaonekana sheria inamlinda. Ikiwa atakuwa na vyeti halali basi sifa hizo zitahesabika kama sifa za ziada- added advantages
 
Hivi bwana huyu Mbowe majina yake halisi ni nani? Kuwa kwenye kundi la walio gushi vyeti ilitakiwa iende sambamba na majina yake halisi kama ushahidi.Rejea kwa DAB=PCM.Je, FAM=?
Felia= fojara?, nimesoma tuhuma Zeke za kufeli humu Jf.
 
JiBASHITEGE(0%) Tu.
 
Alishitakiwa kwa sab alighushi ambalo ni kosa la jinai bila kujali elimu hata makonda anastahili kufikishwa mahakamani kama kihiyo alivyofikishwa na mrema na wakili wake lamwai. Badala ya mawakili wasomi kumpeleka mahakamani wanalialia mitandaoni wanaogopa kumfunga paka kengele. Upinzani wa kweli ulikuwa zamani siku hizi ni upinzani wa mitandaoni tu rubbish.
 
Mimi najiuliza ikiwa viongozi hawa wa ki siasa ndiyo wasimamizi wa hawa wanaoitwa watumishi wa umma !! Huku elimu yao ya mashaka (bashite) hapa haki iko wapi ?!

Nchi moja sheria tofauti kwa swala moja?? Kweli hii ni awamu ya tano !!
 
Some people are equal than others. Kuna dada alienda kusomea cheti cha mdogo wake, nursing. Akaja akawa nurse mzuri sana. Hii op ya vyeti feki imempitia. Amepata stroke. Hatembei.
 

umenikumbusha kihiyo alikuwa DIT pale miaka hiyo akadanganya ni msomi kumbe alikuwa ..........
 

unazani Uyo bwana zero angaekuwa anavyo vyeti mpaka leo asingeviweka? hana vyeti na wananchi kazi yetu kupaza sauti jambo ambalo sio zuri linapotokea kama hili la uyu bwana zero lakini cha ajabu mtu tuliyemuweka kuangalia mali za umma kwa miaka mi 5 kaishajiona yeye kama mungu-mtu kutetea hata waovu , hii dhambi itamla hata akimaliza miaka yake mi 5 , watanzania sio wajinga kwamba hatukui bwana zero anatetea na uyu mtu tuliyemuweka atutumikie kwa miaka mi 5 badala yake anataka sisi ndio tumtumikie , wote mnao mtetea bwana zero na uyo tuliyemuweka kututumikia kwa miaka mi 5 wasaliti wa nchi hii
 
That was then, this is now.
 
Kumbe ni mahakama ndio ilitengua ok Sasa wapelekeni mahakamani mnao ona wamefoji vyeti.
 
Sasa vyeti vya nini waliangalia ikiwa sifa kuu ya ubunge ni kujua kusoma na kuandika vyeti vya nini ikiwa vyeti ni sifa moja wapo ya kuwa mbunge mbona wabunge hawajakaguliwa sasa kama kuwa na vyeti feki au halali ndio sifa ya ubunge
Kusoma mpaka degree au masters sio sifa ya ubunge kwa mujibu wa katiba.... Lakini yule alishtakiwa kwa kesi ya kufanya fogery ambayo adhabu yake inakufanya kupoteza sifa za kuwa mbunge.... Kumbuka mbunge anapoteza sifa kama atahukumiwa kifungo chochte kilichozidi miaka mitatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…