Zawadi zinazotolewa kupitia kampeni hiyo ni pamoja na televisheni janja, simu za mkononi, pikipiki, muda wa maongezi na fedha taslimu.
Godfrey Lwambano mkazi wa Dar es Salaam, matumizi yake ya kawaida ya Airtel Money yaligeuka kuwa fursa ya kupata zawadi kubwa baada ya kushinda televisheni.
“Natumia Airtel Money mara kwa mara kutuma fedha, hivyo nilipoona mchezo huo nikaamua kujaribu,” alisema.
Bw Lwambano alisema alianza kwa kushinda muda wa maongezi na kiasi kidogo cha fedha kabla ya kupata ushindi mkubwa wa televisheni.
“Mwanzoni nilishinda zawadi ndogo kama muda wa maongezi na baadaye fedha, hivyo nikaamua kuendelea kujaribu kwa sababu haikunigharimu chochote,” alisema.
Alisema hakutarajia kushinda televisheni hadi alipopokea taarifa iliyomjulisha kuhusu ushindi huo.
“Siku moja niliona taarifa kwamba nimeshinda TV, lakini sikuamini kabisa,” alisema.
Bw Lwambano alisema aliamini ushindi huo baada ya Airtel kumpigia simu kupitia namba rasmi ya huduma kwa wateja, 100.
“Nilipopigiwa simu na Airtel kupitia namba 100, nilitambua kwamba ilikuwa ni kweli,” alisema.
Mteja mwingine, Hamida Ramadhan, alishinda simu janja baada ya kushiriki kupitia miamala yake ya kawaida ya Airtel Money.
“Natumia Airtel Money mara kwa mara, hasa ninapotuma fedha au kutoa fedha kupitia wakala,” alisema.
Bi Ramadhan alisema mchezo huo hujitokeza wakati wa kufanya miamala, ukimpa mteja nafasi ya kuzungusha na kuona zawadi anayoweza kushinda.
“Kila ninapofanya muamala, mchezo hujitokeza na mimi huzungusha kuona kama nimeshinda muda wa maongezi, fedha, TV au simu,” alisema.
Alisema hakujua kuwa alikuwa ameshinda simu janja hadi alipopigiwa simu na Airtel kupitia namba 100.
Fursa kwa wateja wapya na waliopo
Mkuu wa Kitengo cha Enterprises and SMEs wa Airtel Money, Janeth Kilasa, alisema kampeni hiyo inawahusisha wateja wapya na waliopo wa Airtel Money.
“Tunaendelea kuwafikia na kuwapongeza washindi wetu kupitia kampeni ya Minyoosho Inaendelea, ambayo inawazawadia wateja kwa kutumia Airtel Money kufanya malipo na kutuma fedha,” alisema.
Bi Kilasa aliwahimiza wateja kutumia programu ya Airtel Money katika kufanya miamala, huku wale ambao hawana programu hiyo wakielekezwa kuipakua kupitia Play Store au App Store.
Alisema kampeni hiyo ni sehemu ya juhudi za Airtel kuhamasisha matumizi ya huduma za fedha kidijitali na kuunga mkono mabadiliko kuelekea malipo ya kidijitali nchini.
“Tunataka kuendelea kushirikiana na Serikali kuhamasisha na kusaidia mabadiliko kuelekea malipo ya kidijitali,” alisema.
Airtel pia inaendelea kuhamasisha matumizi ya Lipa Namba, inayowawezesha wafanyabiashara kupokea malipo kwa njia ya kidijitali.
“Huduma zetu za malipo ya kidijitali, ikiwamo Lipa Namba, zinawawezesha wafanyabiashara kukusanya malipo kwa njia ya kidijitali,” alisema.
Kwa mujibu wa Bi Kilasa, wafanyabiashara wanaweza kupata Lipa Namba bila kulipa ada.
Tahadhari dhidi ya utapeli
Airtel Money imewaonya wateja kuwa makini dhidi ya watu wanaoweza kutumia jina la kampeni hiyo kufanya utapeli.
Bi Kilasa alisema washindi halali watawasiliana na Airtel kupitia namba rasmi 100.
“Airtel itawasiliana na washindi wa kampeni kupitia namba 100 pekee. Mtu akikupigia simu kutoka namba nyingine na kukuomba utume fedha ili upate zawadi, kata simu. Huo ni utapeli,” alisema.
Kilasa aliongeza kuwa Airte washindi wanapatikana kutoka mikoa mbalimbali nchini, huku wale walio nje ya Dar es Salaam wakielekezwa maeneo ya kuchukulia zawadi zao.
Kampeni ya Minyoosho Inaendelea inaendelea wakati matumizi ya fedha kwa njia ya simu yakizidi kuwa sehemu ya shughuli za kila siku, kuanzia kutuma na kupokea fedha hadi kufanya malipo.
Kwa mtazamo huo, Airtel inaunganisha matumizi ya kawaida ya huduma za fedha kidijitali na fursa za zawadi, huku ikihamasisha wateja kuongeza matumizi ya miamala ya Airtel Money.