Kuwa spika ni lazima uwe sponsored na Chama cha siasa ata kama wewe si Mbunge
Sawa.
Kama angekuwa na hoja nzito zenye mashiko kwa wananchi, angepata chama cha kum sponsor au hata kuanzisha faction ndani ya CCM kumpa support.
Bottom line, mtu mwenye kusimamia priciple angekuwa tayari kupigania ukweli mpaka dakika ya mwisho hata kama ilimaanisha ataukosa Uspika na ubunge. Ndugai kajiuzulu bila kupigana mpaka mwisho, ametuonesha hana principle. Pengine hata hizo hoja kazitoa kisiasa zaidi tu.
Basi Ndugai angeacha chama kimfukuze, kisimpe sponsorship, wananchi tujue kwa wazi bila speculation kwamba chama kimemfukuza Spika uanachama kwa sababu katofautiana na msimamo wa serikali.
Halafu tungepima mbivu mbichi, kama Ndugai yuko sawa au chama kiko sawa.
Sasa hivi, Ndugai, kama Ndugai alitishiwa kweli, Ndugai anakuwa katukatili haki yetu ya kujua ukweli.
Hakutuambia kwamba katishiwa, na wala hakudinda mpaka afukuzwe yuone kafukuzwa.
Imabakia watu wanafanya speculations tu.
Kuna mambo mengi yenye matatizo na watetezi wa Ndugai.
1. Kuna speculation kwamba Ndugai kalazimishwa kujiuzulu. Hizi si habari zenye kuthibitishwa vyovyote.
2. Hata kama Ndugai kalasimishwa kujiuzulu, yeye kama Spika kazi yake ni kuisimamia serikali (executive), si kuchukua amri kutoka kwenye serikali. Kwa hivyo kama kajiuzulu kwa amri kutoka juu, alistahili kujiuzulu hata kama hakushinikizwa, kwa sababu hana sifa za USpika za kusimamia anachoona ni sawa.
3. Inawezekana kabisa Ndugai kajiuzulu mwenyewe kwa woga wake, na ujinga wake wa kusema mambo bila mkakati, halafu mnailaumu bure serikali kwamba imemtisha